Ujumbe wa yesu

Page 1

Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page A

UJUMBE WA YESU Kimeandikwa na: Barbara A. Brown

Kimetarjumiwa na: Dr. M. S. Kanju


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page B

© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Tahrike Tarsile Qur’an, Inc. ISBN: 978-1-879402-09-2 Kimeandikwa na: Barbara A. Brown Kimetarjumiwa na: Dr. M. S. Kanju Email: mokanju2000@yahoo.com Dar es Salaam/Tanzania. Kimehaririwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo Toleo la kwanza: Julai 2007 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Tahrike Tarsile Qur’an, Inc. 80-08 51st Avenue, Elmhurst, New York 11373 Tel: 718 446 6472 Fax: 718 446 4370 www.koranusa.org Email:read@karanusa.org


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page C

YALIYOMO Dibaji ................................................................................................2 Utangulizi..........................................................................................5 Agano lililopotoka.............................................................................6 Ujumbe wa Yesu................................................................................8 Mwanzilishi halisi wa Ukristo...........................................................9 Itikadii za Ukristo............................................................................13 Maelezo ya jumla juu ya itikadi ya Ukristo.....................................42 Maandiko ya Kikristo......................................................................44 Imani Halisi ya kuamini Mungu mmoja imehuishwa.....................64 Ukristo na Uislamu.........................................................................68 Madhehebu katika Ukristo...............................................................77 Hitimisho....................................................................................... 80 Orodha ya vitabu, vitabu vingine vinavyohusiana na ulinganishaji baina ya Uislamu na Ukristo...........................................................84


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page D

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la: “A closer look at Christianity.” Sisi tumekiita “Ujumbe wa Yesu” kilichoandikwa na: Barbara A. Brown Mwandishi wa kijitabu hiki, Barbara A. Brown ambaye alilelewa na kukulia katika Ukristo amefanya uchunguzi wa kina juu ya Dini tatu kubwa duniani; Uyahudi, Ukristo na Uislamu. Matokeo yake ni kijitabu hiki na vingine ambavyo ameviandika kuhusiana na suala hili, na baada ya kuiona haki hakusita kuifuata. Baada ya kuukubali Uislamu kuwa ndio Dini ya haki aligundua dhulma na fitna kubwa inayofanyiwa Dini hii ya Uislamu. Na si wengine bali ni Wayahudi na Wakristo. Zamani, haswa zama za Mtukufu Mtume na za makhalifa; Mayahudi ndio waliokuwa maadui wakubwa wa Uislamu, na Wakristo walikuwa haijambo kidogo. Lakini baadae Wakristo nao wakaungana na Mayahudi kuupiga vita Uislamu. Mayahudi na Wakristo wa zama zetu hizi wameandika (na wanaendelea kuandika) vitabu na vipeperushi vingi, na sasa hivi vimefunguliwa vituo vingi vya Redio na Televisheni kwa lengo la kuukashifu na kuupaka matope Uislamu, ili uonekane ndani ya jamii kuwa ni Dini ya vurugu na isiyo ya kistaarabu. Hii ni dhulma kubwa tunayofanyiwa sisi Waislamu, kwa ajili hiyo hatupaswi kukakaa kimya na kuwa kama wasikilizaji, ni jukumu letu kujibu mashambulizi haya kwa nguvu zetu zote, kwa kutumia hoja za mantiki na kwa uadilifu kama ilivyo Dini yetu. Na sio haki kwa mtu yeyote kutulaumu au kujaribu kutuzuiya tusitekeleze wajibu wetu huu. Mtukufu Mtume wetu (saww) anasema: “Mwenye kuona jambo uovu, na alibadilishe kwa mkono wake, ikiwa hataweza abadilishe kwa ulimi wake, kama hataweza abadilishe kwa moyo wake, na hiyo ni imani dhaifu.”


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page E

Mwandishi wa kitabu hiki ametekeleza wajibu wake kama Mwislamu, ni jukumu letu sisi tulio bakia kuungana naye ili tuitetee Dini yetu dhidi ya maadui hawa wapotoshaji. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo maadui wanatumia kila mbinu ili kuhakikisha kwamba Uislamu unaondoka katika ramani ya ulimwengu. Kutokana na ukweli huo, tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswhili ili iwe ni changamoto kwa wasomaji wetu Waislamu wazungumzaji wa lugha hii. “Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia. Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake (Muhammad) kwa uongofu na dini ya haki ili ipate kushinda dini zote, ijapokuwa washirikina watachukia.” (Qur’an; 61:8-9 & 9:32-33)

Tunamshukuru ndugu yetu, Dr. M. S. Kanju kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Tahrike Tarsile Qur’an, Inc. 80-08 51st Avenue, Elmhurst, New York 11373 Tel: 718 446 6472 Fax: 718 446 4370 www.koranusa.org Email:read@karanusa.org


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 1


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 2

2

DIBAJI Nafsi kuwa katika amani kuhusu Mwenyezi Mungu, hili ndio lengo haswa la kitabu hiki. Wengi wetu tunaridhika kuishi tu bila udadisi na tunayakubali mambo "kama yalivyo"; tunayapuuza yale maswali madogo yanayosumbua na mashaka katika akili zetu, haswa masuala yanayohusiana na dini. Kwa kufanya hivi, ndiyo ni kweli kwamba tunaendelea kuishi, lakini kamwe hatupati utulivu wa akili na amani ndani ya nafsi zetu. Hata hivyo wengine miongoni mwetu, hawaridhiki kuyachukua mambo kama yalivyo, na hivyo kwa bidii na shauku tunafanya jitihada kuyatafutia majibu sahihi maswali yanayojitokeza katika maisha yetu. Tunahoji imani za baba zetu, hatupo tayari kuzikubali na kuzifuata kibubusa. Barabara hii haipitiki kwa urahisi kwa namna yoyote, lakini malipo yake ni yenye faida kubwa. Nimelelewa kama Mkristo, na nikakua katika madhehebu ya kiprotestanti yajulikanayo kama "Imani ya kikristo iliyofanyiwa marekebisho." Licha ya ufuasi wangu mzuri wa dini - ibada za kanisa mara mbili kila Jumapili na siku za mapumziko, mafunzo ya Jumapili, masomo juu ya mafunzo, misingi na imani ya kanisa, shule za Biblia katika msimu wa kiangazi na kambi maalum juu ya Biblia - bado nilijikuta na maswali mengi kuhusiana na misingi halisi ya imani yangu ambayo hakuna yeyote wala taasisi yoyote ya kidini ambayo ingeweza kuyajibu. Kwa kipindi cha miaka thelathini na saba nilitangatanga ndani ya ukungu wa utata kuhusiana na Mwenyezi Mungu na njia sahihi ya kutoa heshima na utii wangu Kwake, mpaka mwaka 1991, nilipoungundua Uislamu.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 3

3

"Kimbunga cha Jangwani" (Desert Storm) katika Mashariki ya kati kilikuwa kimefikia kilele chake; sambamba mwa vitabu juu ya mbinu na silaha za kivita katika duka la vitabu mjini petu kulikuwa na kitabu kidogo kilichoandikwa juu yake "Understanding Islam" (Kuuelewa Uislamu). Nilifunua kurasa zake, nikiwa na hamu ya kutaka kujua juu ya dini hii "ya ajabu" ya Mashariki ya kati kama wenzangu wengi walivyokuwa wakitaka kujua juu ya dini hii. Udadisi wangu mara moja ulibadilika na kuwa wa mshangao, hata hivyo, nilipojifunza kutokana na kurasa za kitabu hiki kwamba Uislamu umetoa majibu kwa maswali yangu yaliyokuwa yakinitatiza kwa miaka yote hii - sikupoteza muda zaidi. Nikawa Muislamu. Baada ya muda mrefu, hatimaye nikawa nimefaulu kupata lile lengo la kuwa na amani katika nafsi yangu kuhusu uhusiano wangu na Mwenyezi Mungu. Kwa vile Mwenyezi Mungu amenipa uwezo wa kujieleza vizuri katika maandishi, ninataka kuwafikia watu wengine ambao wana maswali yote yale yanayowasumbua katika akili zao kuhusiana na dini. Nina matumaini kuwa huenda nikawasaidia kufikia majibu ya maswali hayo. Taarifa ninayowasilisha hapa inaweza kuwashangaza na hata kuwashitua baadhi ya wasomaji, lakini kazi ya kufuatilia ukweli daima huwa sio rahisi, hususan mbele ya imani na kanuni zilizoshikiliwa kwa muda mrefu. Nilianza kazi yangu siku nyingi kidogo kwa kuandika vijitabu vingi vidogo vidogo: 1) Tatu katika moja (Three In One), uchambuzi wa imani ya Kikristo juu ya Utatu Mtakatifu, kilichochapishwa mwanzoni mwa 1993 na Shule Huria ya Chicago (The Open School of Chicago). 2) Kijitabu kiitwacho "A Closer Look at Christianity" (Uchunguzi makini juu ya ukristo) ambacho kinahusiana na uchunguzi juu ya ukristo kwa mujibu wa Biblia, na


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 4

4

3) Kitabu kiitwacho "A Case of Corruption" (Suala la upotofu) ambacho kinahusiana na uvurugaji wa maandiko katika Biblia. Kitabu ulichonacho mikononi kinawasilisha mkusanyiko wa vitabu vyote hapo juu, pamoja na utafiti ulioongezwa kama nilivyoendelea kusoma zaidi kati ya miswada yangu ya awali na ile ya mwisho kwa ajili ya shule huria. Ni matarajio yangu kwamba, katika kurasa zinazofuatia, wasomaji watakuwa na fursa ya kuona mtazamo juu ya ukristo kama ambavyo mimi nilivyouelewa. Barbara A. Brown 23 March 1993


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 5

5

UTANGULIZI Ndani ya dini nyingi ambazo zipo duniani leo; ni tatu zinazodai kuwa zinampwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu - yaani imani ambazo msingi wake ni kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mmoja asiye na mshirika. Uchunguzi wa karibu, katika dini mbili kati ya hizi - Uyahudi na Uislamu - utaonyesha hili kuwa ni kweli: Wote Wayahudi na Wislamu wanamuabudu Mungu mmoja, Muumba wa Mbingu na Ardhi. Dini nyingine, ile ya Ukristo, ina matatizo, hata hivyo, wakati tunapoelezea maana ya imani ya kumuamini Mungu Mmoja asiyekuwa na mshirika tofauti na inavyoaminiwa na Ukristo. Badala ya kumfanya Mwenyezi Mungu Mtukufu awe ndio kiini na msingi mkuu wa imani yao, Wakristo wamegeuza fokasi yao kuwa juu ya Yesu, anayeeleweka kwao kama "Yesu kristo" au "Yesu Aliyepakwa mafuta." Kwa Wayahudi Yesu alikuwa "Kijana mzuri wa kiyahudi;" kwa Waislamu, Yesu alikuwa Mtume na mja wa Mwenyezi Mungu; mmoja wa wajumbe wateule wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa Wakristo, hata hivyo, Yesu ni zaidi ya hayo. Fokasi ya ukristo iko juu ya Yesu Kristo. Dini hii imepata jina lake kutokana na jina la Yesu Kristo. Itikadi na imani zote muhimu za kikristo kitovu chake ni Yesu kristo. Sikukuu kubwa za Kikristo huwa ni kumbukumbu ya matukio katika maisha ya Yesu Kristo. Alama ya imani ya Kikristo, msalaba, ni alama ya Yesu Kristo. Sala na dua za Wakristo huelekezwa kwa Yesu Kristo, kwa vile wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mwenyewe huwa hawezi kuombwa na binadamu wa kawaida.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 6

UJUMBE WA YESU

6

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Kikristo Fritz Ridenour: "Ufunguo wa Ukristo ni kwamba Yesu Kristo ni sababu haswa kwa yote hayo na yeye ndiye anayeushikilia na kuumiliki".1 Wakristo wengi leo wanashindwa kuelewa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu bila ya Yesu kusimama mbele kwa ajili yao. Bwana Ridenour anasema kwamba Ukristo ni: "...Uhusiano na mtu, Yesu Kristo,"2 na Wakristo wengi sana wana imani hii: hawamwelewi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kwa kupitia kwa Yesu Kristo. Wakristo wanasema wanamuabudu Mwenyezi Mungu, lakini Yesu pia yuko pale katika akili zao. Kwa jinsi wanavyomuona - kwa nyongeza ya Mwenyezi Mungu - kama Mungu halisi, Ukristo ni dini yenye miungu wawili, sio mmoja; na dini yenye Mungu zaidi ya mmoja sio dini inayompwekesha Mwenyezi Mungu. Hali hii ilikujaje? Ilikuwaje dini ya Ukristo imbadilishe Mtume wa Mwenyezi Mungu (ambaye ni binadamu) na kumfanya yeye mwenyewe (Yesu kristo) kuwa Mungu?

*** *** AGANO LILILOPOTOKA Ili kuelewa Ujumbe na kazi halisi ya Yesu, lazima turudi nyuma kabla ya muda wake katika Historia ili kuona kwanza kabisa ni kwa nini alitumwa. Akiwa amechoshwa na ibada ya masanamu miongoni mwa watu wake, Nabii Ibrahim aliiacha nchi yake karibu miaka 2000 kabla ya Yesu ili apate uhuru wa kumuabudu Mwenyezi Mungu tu. 1 How to be a Christian in an unchristian world uk. 176 2 Ibid p. 14 3 Islam Revealed, uk. 129


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 7

7

Ilikuwa vigumu kwake kuicha nyuma familia yake, hivyo Mwenyezi Mungu alimbariki kwa kumpa watoto wawili wa kiume. Kisha akamfariji Nabii Ibrahim kwa kumwambia kwamba mtoto wake mdogo, Is’haq atamfanya taifa kubwa (Mwanzo 17:16, 19). Kutokana na Is’haq baadaye likazaliwa taifa la Kiyahudi, "Wateule" wa Mungu. (Baadaye tunaona ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa mtoto mwingine wa Nabii Ibrahim, Ismail). Licha ya heshima na utukufu huu wa kuitwa "watu wateule" wa Mungu, Wayahudi waliendelea kurudi nyuma kwenye ibada ya masanamu, na Mwenyezi Mungu aliendelea kupeleka Mitume mmoja baada ya mwingine ili kuwaonya Wayahudi juu ya kutoridhishwa Kwake na tabia yao. Baada ya maonyo kushindwa kuibadilisha hali hiyo, nchi adui zilizokuwa jirani ziliingia na kuwapiga vibaya Wayahudi. Ingawa Mwenyezi Mungu aliwakubalia muda wa amani na nafuu mara nyingi aliposikia kilio chao cha kutaka Rehema Yake, ghadhabu Zake ziliwaka mno sana mwaka 581 (kabla kuja Yesu) kwa kuendelea kwao kutomtii kiasi kwamba, Aliruhusu Wababiloni kuvamia ufalme wa kiyahudi wa kusini mwa Yuda, ambako Mfalme Nebuchadnezzar na jeshi lake walisonga mbele na kuupiga vibaya mji wa Jerusalem na kuwachukua Wayahudi kama mateka. Upande wa kaskazini wa Ufalme wa Kiyahudi wa Israel ulipatwa na balaa kama hili mwaka 721 kabla ya Yesu katika mikono ya Waassyria. Wakiwa wametawanyika na jumba lao la ibada kuharibiwa vibaya, Wayahudi waliamua kuipa mgongo sheria ya Mwenyezi Mungu. imani ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu mmoja asiye na mshirika ilikuwa ilipotea tena, lakini wakati huu walijiingiza katika mazonge zaidi ya kaida na ibada za matambiko. Ilikuwa katika hali hii ambayo ilikuwepo katika ulimwengu, ambapo Yesu alipokea wito wake kutoka kwa Mwenyezi Mungu.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 8

UJUMBE WA YESU

8

UJUMBE WA YESU. Katika kipindi alipoanza kazi yake ya Utume rasmi akiwa na umri wa miaka kama 30, Yesu alibainisha wazi kwamba kazi yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu ilikuwa ni kurejesha Wayahudi kwenye njia iliyonyooka. "Maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.� (Mathayo;18:11) "Akajibu, akasema, sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." (Mathayo 15:24) Yesu pia aliweka wazi ni nini Mwenyezi Mungu alimtaka afanye: "Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.� (Yohana 12:49) "Msidhani ya kuwa nimekuja kutengua torati au manabii; la, sikuja kutangua bali kutimiliza". (Mathayo 5:17) Uchunguzi makini wa maneno ya Yesu unaonyesha kwamba, kinyume na Wakristo wanavyo fikiri, Yesu hakuwa na nia ya kuanzisha dini mpya; alikuja tu kusisitizia ujumbe ambao Mwenyezi Mungu aliwapa Mitume wote waliotangulia kabla yake: Mwanadamu alitakiwa atii sheria za Mwenyezi Mungu na amuabudu Mwenyezi Mungu tu. Hakuna wakati wowote katika ujumbe wake ambapo Yesu alidai kuwa zaidi ya kitu chochote kuliko mwanaadamu, aliyepewa ufunuo na Mwenyezi Mungu Mtukufu.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 9

UJUMBE WA YESU

9

Hakika, alijitambulisha mwenyewe kuwa ni mwana wa mwanadamu, na akaweka wazi, katika aya nyingi ndani ya Injili, kwamba yeye alikuwa tu ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. "Yesu akamjibu, kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, Ndiye Mungu." (Marko 10:18) "...Na mtu akinipokea Mimi, humpokea si Mimi, bali yeye aliyenituma.” (Marko 9:37) "Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kirsto uliyemtuma.” (Yohana 17:3) "Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa mungu…” (Yohana 8:40) "…, ninapaa kwenda kwa baba yangu naye ni baba yenu, kwa mungu wangu, naye ni mungu wenu.” (Yohana 20:17) Licha ya juhudi zake zote - maneno matamu yakiungwa mkono na miujiza mizuri - Yesu alikataliwa katakata, hususan na watu wake mwenyewe. Miaka mitatu baada ya kuanza ujumbe wake, alikamatwa na kushitakiwa kwa shutuma za uchochezi wa uhaini na kufuru. Mafanikio yalikuwa yamemkwepa - katika mwisho wa maisha yake hapa duniani, aliacha nyuma yake wafuasi kidogo tu wasiozidi 500. Hata hivyo, hali hii yote ilibadilika kwa kuvutia, wakati mhubiri mpya, akidai kuongea kwa jina la Yesu, alipojitokeza miaka michache tu baadaye.

MWANZILISHI HALISI WA UKRISTO Wafuasi wa Yesu waliojiita “Wanazareti” waliendelea kuchochea migogoro pote walipokwenda baada ya Yesu kuaga dunia; walifanya hivyo kwa kurudia maneno yake juu ya kuangamia kwa Wayahudi ikiwa


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 10

10

hawakubadilisha nyendo na tabia zao mara moja. Mmoja wa Wanazareti, aliyeitwa Stephano, mwishowe alielekeza mahubiri yake mbali zaidi kwa kutoa mahubiri ya kuhamasisha wakati alipoyaleta mbele ya Mahakimu wa kiyahudi waliokuwa wakijulikana kama Sanhedrin. Wakifoka kwa hasira kwa sababu ya maneno yake ya "kufuru," mahakimu waliruka na kumkamata, kisha wakamburuza Stefano nje ya mji, ambako alipigwa mawe mpaka kufa. Kisa hiki kinapatikana katika "Matendo ya Mitume," sura ya 7, katika Biblia. Mauaji ya Stephano yalishuhudiwa na kijana mdogo wa kiyahudi aliyeitwa Sauli. Alizaliwa katika mji wa Tarsus, si muda mrefu sana baada ya Yesu mwenyewe. Sauli alikuwa amejiunga na moja ya madhehebu ya kiyahudi ya Mafarisayo ("Pharisees"); haya “makunguru ya kisheria” (“legal eagles”) walikuwa mashabiki katika kuwafukuzia Wanazareti; kufuatia kuuliwa kwa Stefano, Paulo mwenyewe alianza kuchukua jukumu kali katika jitihada hii. Utendaji wake katika cheo hiki ulikuwa mzuri mno kiasi kwamba alifanywa kuwa ni wakala mkuu wa harakati hizi katika mji wa Jerusalem, na alipewa hati muhimu ili kuendeleza usafishaji huu katika miji ya jirani. Takriban miaka 5 tangu kupaa kwa Yesu kwenda mbinguni, mshabiki huyu mwenye umri wa miaka 25 alikuwa njiani kuelekea Damascus kwenda kulichukuwa kundi la Wanazareti kwa ajili ya kuwarudisha Jerusalem wakati alipata maono ambayo kwayo alidai kujitokeza kwa Yesu, akiuliza kwa nini Sauli alikuwa anamtesa yeye. Visa mbali mbali vimetolewa kwa yaliyotokea kwa Sauli siku ile - kwa vile kuzimia kutokana na jua kali, ndoto za jinamizi, na hata kifafa-lakini hakuna lenye yakini isipokuwa kwamba yoyote ambayo yalitokea yalimbadilisha mtesaji mshabiki kuwa mhubiri mwenye shauku. Sauli alibadilisha jina lake kuwa Paulo na akaenda katika jangwa la Arabuni ili kutafakari ni jinsi gani angetekeleza amri aliyoamini kuwa ime-


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 11

11

toka kwa Yesu ya kwenda kuhubiri. Nini hasa angelifanya, ilikuwa ni mtanzuko kwake, hata hivyo, kwa vile wayahudi walikuwa wamemkataa Yesu na ujumbe wake, Paulo hakuona uwezekano wa kuwashawishi kwa mahubiri na ama kuwapata. Aliamua kwamba ni vizuri zaidi kuwaacha kabisa na badala yake kuwalenga mataifa (wasiokuwa Wayahudi). Ili kulifanya hili, hata hivyo, busara na akili nyingi vilitakiwa kutumika. Warumi na Wagiriki ambao ndio wanaofanya mataifa ya ulimwengu wa Paulo, walikuwa ni wapagani ambao waliabudu wingi wa miungu ya kiume na ya kike. Mahekalu na masanamu ya miungu wao vimeenea katika nchi, na sheria ya Kirumi iliwataka watu wote, isipokuwa Wayahudi, lazima kusujudia na kutoa heshima kwa miungu hii ya kisanamu. Paulo alielewa kwamba watu waliokuwa na imani ya kipagani iliyowakolea kiasi hicho wasingeweza kukubali wazo la kwamba neema ya Mungu na uokovu vingeletwa na mtu tu aliyefikiriwa kuwa muongofu na mwanadamu muadilifu. Ili kupata mafanikio ya haraka katika kazi yake, Paulo alielewa wazi kwamba angelazimika "kugeuza" mambo kidogo, akizingatia utamaduni wa wa mataifa. Paulo Maier, katika kitabu chake "Wakristo wa Mwanzo" (“First Christians�), anatuambia kwamba ilipita miaka kumi na tatu tangu wakati Paulo "alipopokea wito wake" na wakati ambao alianza kuhubiri. Katika hiyo miaka kumi na tatu, akili ya ubunifu ya Paulo muda mwingi ilifikiria; hatimaye aliporudi Damascus, akiwa amejipatia silaha muhimu kwa kutambua kwamba mataifa wangedai mungu aliye dhahiri ndani ya dini yao mpya, na alikuwa tayari kuwapatia hili. Paulo afanikiwa sana katika juhudi za ujumbe wake uliofuatia, pamoja na kuwajengea urahisi wa mapokezi kwa ajili ya mataifa. Japokuwa dini ya ukristo inachukua jina lake kutoka kwa Yesu kristo, Paulo mkazi wa Tarsus


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 12

UJUMBE WA YESU

12

lazima achukuliwe kama muanzilishi wake wa kweli, kwa vile yeye ndiye aliyebuni na kutunga itikadi zake zote, na akasimamisha Makanisa yake ulimwenguni pote katika zama zake. Wakristo hawalikatai hili pia: "Hakuna mtu yeyote katika historia ya ukristo aliyejitokeza mno, mwenye athari kubwa na umaarufu kama Sauli mkazi wa Tarsus‌"3

Katika kitabu "The 100: A Ranking of the most Influential Persons In History: (uorodheshaji wa watu 100 wenye mvuto mkubwa katika historia ya ulimwengu). Michael Hart anasema: "Hakuna mtu mwingine aliyefanya kazi kubwa kiasi hiki (mbali ya Paulo) katika kueneza Ukristo.�4

Hata hivyo, kuna tatizo moja kubwa katika kadhia hii: mafundisho ya Paulo, mwanzilishi halisi wa ukristo, hayawezi kupatikana mahali popote katika mafundisho ya Yesu wala katika mafundisho ya Mitume waliotangulia kabla yake. Si hivyo tu, bali Paulo alikuwa na mawasiliano machache na wanafunzi wa kweli wa Yesu ambao vilevile wangeweza kumuongoza na kumuweka sawa; hawakukubaliana na mafundisho ya upotoshaji ya Paulo, na alilielewa hili kama iwezekanavyo. Hatimaye, hata hivyo, Ukristo mpya wa Paulo ulifanikiwa kwa sababu, kutokana na haiba yake, bila kutaja ukweli kwamba yeye na wafuasi wake waliwapita wanafunzi wa kweli wa Yesu katika hadhi muhimu kama vile sifa ya kijamii, utajiri na elimu, alipata wafuasi wengi miongoni mwa mataifa na wakristo wa kiyahudi, kiasi kwamba wanafunzi wa Yesu hawakuweza kusimama. Hebu ngoja tufanya uchunguzi wa makini juu ya uzushi wote ambao Paulo aliuingiza katika dini "yake" ya Ukristo. 4 The 100: A Ranking of the Most Influential Persons In History, uk. 62.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 13

13

ITIKADI ZA UKRISTO 1) MWANA WA MTU AU MWANA WA MUNGU? Tukiliweka kwa urahisi, itikadi ya Uungu inasema kwamba Yesu ni mwana wa Mungu - Neno la Mungu lililofanywa mwili. Ingawa Yesu mwenyewe, kama tulivyotaja hapo nyuma, kamwe hakudai kuwa yeye ni Mungu; Paulo alimpa sifa hii kwa sababu moja: ili kupata wafuasi miongoni mwa mataifa. Mataifa walikuwa ni wapagani ambao walizoea kuabudu miungu wengi wenye historia ndefu iliyojaa hekaya za ajabu na ngano nyuma yao. Miungu wengi wa kipagani wa wakati ule - Mithras, Adonis, Attis na Osiris, tukitaja baadhi tu - wote walikuwa ni watoto wa mungu mkuu anayetawala, na kila mmoja wa watoto hawa wa mungu alikufa kwa ajali mbaya katika utoto wake, ili kuja baadaye kuokoa maisha ya watu wao. Paulo alilizingatia hili, akawapatia wapagani jambo lililofanana na hilo katika Ukristo: akauhusisha Uungu kwa Yesu, akisema kwamba alikuwa mwana wa Mungu (Mkuu) na kwamba, yeye pia alikufa kwa ajili ya dhambi zao. Kwa kufanya hivyo, Paulo aliyapatanisha mafundisho ya Yesu na imani za kipagani ili kuufanya Ukristo ukubalike zaidi kwa watu wa mataifa. Ilivyo hasa, Paulo hakutaja asili ya upagani katika itikadi hii makhususi. Ni yule tu anayechunguza kwa kina katika historia ya zama zile - watu na utamaduni wao - ataweza kuuona ukweli huu, Paulo alithibitisha itikadi hii kwa namna nyingine. Hususan, alihisi kwamba kuna sababu tano zinazomfanya Yesu awe Mungu.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 14

14

1) Yesu alizaliwa na mwanamke bikira bila ya "msaada" wa baba wa kibinadamu. Kulijibu hili, tunaweza kuangalia mfano wa Adam, mwanadamu wa kwanza. Alizaliwa bila ya baba wala mama, lakini hatumfikirii kuwa yeye ni Mungu. 2) Yesu alifanya miujiza. Kuliangalia hili tunaweza kuangalia mfano wa Nabii Musa na Nabii Elisha; wote walifanya miujiza mikubwa ya kustaajabisha, lakini hakuna yeyote kati ya hawa anayefikiriwa kuwa ni Mungu. Ukweli kwamba Yesu alifanya miujiza sio uthibitisho kwamba Yesu alikuwa Mungu kama alivyokuwa akionesha kwa upesi wakati mambo kama haya yakitokea, na kwamba uwezo wa kufanya matendo haya ya kushangaza umetoka kwa Mwenyezi Mungu- sio kwake. Miujiza yake ilifanyika kwa kusudio lile lile kama la Mitume waliotangulia kabla yake: nalo ni kuuthibitisha ukweli wa ujumbe na utume wake kwa watu waliokuwa wagumu kuamini. 3) Yesu alikuwa na tabia "isiyo na kifani." Kujibu hili, mtu anaweza kuonyesha idadi ya mifano katika injili - kama vile kumwita Petro "Shetani" katika Mathayo 16:23, na kuwaita wengine "nyoka na kizazi cha nyoka wenye sumu" katika Mathayo 23:33 baada ya kuonesha nukta ya kusema mapema katika Mathayo 5:22, kwamba kutumia majina yenye kuumiza ni kosa – hiyo huleta mashaka kuhusu sifa hii, kwa kadri ambavyo Yesu wa Injili alivyotambulishwa. 4) Yesu alifufuka kutoka katika wafu. Ni kweli, "kuyashinda mauti" ni tendo kubwa, lakini vipi kuhusu Nabii Eliya ambaye hakufa kabisa, bali alichukuliwa moja moja kwenda mbinguni katika gari la kukokotwa na farasi liwakalo moto (Wafalme wa pili 2:11)? Ni tendo kubwa kabisa, lakini bado hachukuliwi kuwa ni Mungu. Na mwisho, Wakristo wanasema kwamba:


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 15

UJUMBE WA YESU

15

5) Yesu alitabiriwa katika agano la kale. Wakristo hufanya haraka kusoma Isaya 53 kama utabiri wa kuja kwa Yesu na ujumbe wake kwa wanadamu. Tatizo hapa, hata hivyo, ni kwamba hakuna jina lililotajwa katika sura hii. Bila kutaja jina makhususi, nani anayejua kwa uhakika ni NANI hasa anayezungumziwa katika sura hii. Neno "Mwana wa Mungu" Neno "Mwana wa Mungu" haikuwa ni kitu kipya, hata hivyo, lilitumika katika Agano la Kale kumaanisha Daudi (Zaburi 2:7) na mtoto wake Suleimani (Solomon) (mambo ya Nyakati wa Kwanza 22:100), na kumtaja Adam (Luka 3:38) katika Agano Jipya. Katika hotuba yake maarufu kule Mlimani, ambayo imeelezewa kwa urefu katika Mathayo 5, Yesu anawaambia wasikilizaji wake: "Heri yao wapatanishi, kwa maana wataitwa wana wa Mungu." (Mathayo 5:9) Katika hali zote, neno "Mwana wa Mungu" halikumaanishwa kutumika kihalisi, bali kumaanisha upendo na mapenzi ya Mungu kwa watu waongofu. "Mwana wa Mungu" ina maana ukaribu maalumu KWA Mwenyezi Mungu-sio kuwa (ukaribu maalumu) WA Mwenyezi Mungu. Pamoja na hayo, kila mtu ni mwana wa Mungu, kwa vile Yeye ni Muumba wa maisha yote. Neno "Masiya - Masihi" Neno jingine linalotumiwa na Wakristo kuunga mkono nadharia kwamba Yesu ni Mungu ni neno Masihi (Angalia Yohana 1:41). Neno Masihi ni neno la kiebrania lenye maana "Mtu wa Mungu aliyepakwa mafuta,� na neno "Kristo" ni tafsiri tu ya kigiriki ya neno hili la Kiebrania. Masihi au kristo, Kiebrania au Kigiriki – maneno yote yana maana moja: "Mtu wa Mungu aliyepakwa mafuta."


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 16

16

Neno hili, hata hivyo, halikutumika kwa Yesu peke yake, limetumika kwa watu wengine kabla yake. Katika Zaburi 2:2, limetumika kwa Nabii Daudi, na katika (Isaya 45:1) limetumika kwa Cyrus (Koreshi). Wayahudi waliwafikiria Wafalme wao kama "Masihi," kwa maana kwamba Mungu kiistiari aliwapaka mafuta. Dhana nzima ya Masihi ilikuwa ni ya Wayahudi, iliyotumika kwa mkombozi wa taifa ambaye waliamini kwamba, kwa msaada wa Mungu angewaokoa kutokana na uonevu na ukandamizaji wa watu wa Mataifa. Halikuleta pamoja nalo sifa ya kimungu. Neno "Mwokozi" Neno la mwisho linalotumiwa na Wakristo ni "mwokozi." Katika hali hii, pia, Yesu hakuwa wa kwanza kwake kutumika neno hili. Wakati Shamu (Syria) ilipofanya vita dhidi ya ufalme wa Israel, Jehoahaz mfalme wa wakati ule, aliomba msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu; katika Wafalme wa pili 13:5, Mungu alimwambia: "Bwana akawapa Israel mwokozi, nao wakatoka mikononi mwa Washami‌;� (2 Wafalme 13:5) Wakati Yehoashi, mwana wa mfalme, alipochukua ufalme, alifanya kama Mungu alivyoahidi; katika 2 Wafalme 13:25, Yehoashi akawa mwokozi wa watu wake kwa sababu aliwashinda Wasyria (Washamu) na akairejesha miji ya kaskazini ya ufalme wa Israel. Neno "Mwokozi" halileti sifa ya kimungu pamjoa nalo pia. Utumiaji wa Tafsiri Potofu Mbali na majina, njia nyingine inayotumiwa na wakristo wanapojaribu kuthibitisha uungu wa Yesu ni kutafasiri kwa upotofu vifungu mbalimbali katika Biblia. Kuna vifungu viwili wanavyopenda sana kuvinukuu kwa kusudio hili:


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 17

UJUMBE WA YESU

17

1) Aya ya kwanza ni Yohana 10:30 ambapo Yesu anasema: "Mimi na Baba yangu ni kitu kimoja." Utumiaji wa kiakili wa aya hii unaonyesha kwamba, linamaanisha tu kwamba Yesu anazungumza KATIKA Jina la Mungu-sio kwamba yeye NI Mungu. Yesu na Mungu ni kitu kimoja kwa malengo - sio kwa asili. Wakristo itawasaidia kwa kuangalia zaidi katika Yohana 17, kwa mfano, Yesu anaomba katika sura hii, na maneno yake hayaachi shaka yoyote kwenye ukweli kwamba yeye ni mtumishi tu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuthibitisha wazo hili la umoja wa lengo, na si la kiasili, tunaangalia kwenye aya mbalimbali zipatikanazo katika katika sura ya 17 ya Yohana, ya kwanza yake ikiwa ni Yohana 17:8. Hapa Yesu anasema: "Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa; nao wameupokea; wanajua kwamba kweli nimetoka kwako; na wanaamini kwamba wewe ulinituma." Katika Yohana 17:11 kuna uthibitisho mwingine unaoonyesha umoja wa lengo, kwani Yesu anasema: "‌Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja." Mada ya umoja wa lengo inarudiwa tena katika Yohana 17:21-23. Kwa kifupi Yohana 10:30 SIO maelezo kutoka kwa Yesu kuthibitisha uungu wake, bali kwa umoja pamoja na Mungu katika lengo, kama inavyoonekana katika aya zilizotajwa hapo awali katika Yohana 17. 2) Aya nyingine ambayo Wakristo wanapenda kuitumia ni Yohana 14:9. Ndani yake Yesu anamwambia Filipo:


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 18

UJUMBE WA YESU

18

"Aliyeniona mimi amemuona Baba". Ni vizuri kwa Wakristo wanaotumia aya hii kuthibitisha uungu waYesu wakaangalia Yohana 5:37, ambapo Yesu anasema: "Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Nanyi hamjapata kamwe kusikia sauti Yake, wala kuuona uso wake." Kama Mkristo atakuwa hakuridhika na aya hiyo hapo juu basi anaweza kuangalia Agano la Kale katika kitabu cha Kutoka 33:20, ambako Mungu anamwambia Musa: "…Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi." Ili kuielewa vizuri aya hii ya Yohana 14:9, ni vizuri tuiangalie katika maana ya kiistiari: Kwa vile Yesu alikuwa analeta neno la Mungu, kumuona na kumsikiliza yeye ilikuwa ni sawa na kuwepo Mwenyezi Mungu papo hapo. Yesu alikuwa anatenda mambo kwa amri ya Mwenyezi Mungu - si kwamba yeye mwenyewe alikuwa Mungu. Hii inaonekana kwa uwazi zaidi katika Yohana 8:19, ambapo Yesu anasema: "Kama mngenijua mimi, hata Baba pia mngemjua". Kama ilivyo, zipo aya nyingine zaidi ambazo mkristo atazigeukia katika jitihada zake za kumpa Yesu Uungu, lakini zote si chochote ila ni tafsiri potofu kwa upande wake - hamu ya kusoma au ya kuona kitu pale ambacho kwa hakika hakipo pale. Tunatakiwa kuangalia tu katika Yohana 17:3 kuona kwamba Yesu alikuwa haleti ujumbe wowote mpya; hapa anasema: “…na uzima wa milele ndio huu, wa wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 19

UJUMBE WA YESU

19

Hapa anatuambia kwamba ni lazima tumuamini Mungu mmoja tu na ambaye ni wa kweli na kwamba yeye, Yesu ni mjumbe tu aliyetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. "Baba saa imefika! Mtukuze mwanao ili naye akutukuze. Maana ulimpa Mwanao mamlaka juu ya watu wote ili awape uzima wa milele wote hao uliompa. Na uzima wa milele ndio huu, kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma--". Katika dua hii ya Yesu inadhihirisha wazi kwamba yeye hakuwa Mungu bali alikuwa ni mja na Mtume wa Mungu. Je Yesu Aliwahi Kujitangaza Kuwa Yeye ni Mungu? Wakristo ni wepesi wa kuonyesha rejea nyingi katika injili ya Yohana ambapo Yesu anajiita "Mwana wa Mungu." Kwa upande mwingine, wanapuuzia rejea nyingi katika injili hiyo hiyo ya Yohana ambapo Yesu anajiita "Mwana wa Binadamu." Hii inaonyesha wazi kwenye ukweli kwa mara nyingine tena kwamba neno "Mwana wa Mungu" halikumaanishwa kuchukuliwa katika maana halisi. Yesu alikuwa na ukaribu maalum kwa Mwenyezi Mungu - alikuwa mwana wa Mungu katika maana ambayo sisi wote ni wana wa Mungu. Katika Mathayo 16:13, Yesu anawauliza wanafunzi wake kuwa wanafikiri yeye ni nani? Wakristo wanalipenda zaidi jibu la Petro ambalo lipo katika Mathayo 16:16 ambapo Petro anasema "Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aliyehai." La kuvutia zaidi, katika maelezo ya tukio hilo hilo ambalo linalopatikana katika Marko 8:16, Petro anasema tu "Wewe ni Kristo." Maneno machache tu yalioongezwa kwenye Mathayo kinyume na yale ya Marko, lakini yanabadilisha maana yote ya maneno! Yakuvutia zaidi, hata hivyo, ni nukta ambayo wakristo wengi tena wanaipuuza, ambayo inayopatikana aya chache zinazofuatia chini ya Mathayo 16. Katika aya ya 20 – na pia katika Marko 8:30 - Yesu anawaambia wanafunzi wake kwamba wasimwambie mtu yeyote yule kuwa yeye ni


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 20

20

Kristo. Kwa nini hakutaka watu wengine walijue hili? Je Paulo Alifanikisha Kitu Gani? Kwa kusema kwamba Yesu alikuwa Mungu, Paulo aliwasihi watu kwa maneno ambayo walikuwa nayo moyoni kabisa, na alipata mafanikio. Shauku yake na haiba kubwa, pamoja na kuwa tayari kuafikiana na ujumbe halisi wa Yesu na imani za kipagani zilimfanya kumpachika Yesu uwana wa Mungu - imani yenye mashaka kwa vyovyote, kwa vile uwana (wa Mungu) unaelezea mtu ambaye aliyeumbwa, ambapo Uungu unaelezea muumba wa milele katika asili. Baadaye viongozi wa kanisa walifikiria kuondoa utata huu kiulaini kwa kusema kwamba Yesu alikuwa Mungu aliyevaa mwili wa kibinadamu - na wa milele ambaye "alichangua" kuwa mwanadamu katika tumbo la Bibi Mariamu. Kwa maneno mengine, Yesu alikuwa na asili (maumbile) mbili – ya kimungu na kibinadamu- ambazo ziliungana na kuwa mtu mmoja. Ambapo huenda walimaanisha vizuri, kutoa maelezo kama haya kulizidisha tu utata zaidi. Mtazamo wa Uislamu Kama ilivyo katika Biblia, Qur’an pia inasema, Yesu alizaliwa bila ya msaada wa baba wa kibinadamu. Hii hata hivyo haina maana kwamba Yesu alikuwa Mungu; inaonyesha tu kwamba Mungu aliyeweka kanuni za maumbile (Laws of Nature) mwanzoni kabisa, ana uwezo vilevile wa kuzisimamisha kwa utashi wake. Kama kwa hakika Yesu angekuwa ni Mwana wa Mungu, “…angekuwa ni mshirika katika uungu na asili ya Mungu mwenyewe, na kwa hali hii, Mungu angekuwa moja kwa moja aliyezalishwa, akiwa mwenye kuzaliwa, akiwa aliyezaliwa, aliishi kama binadamu na kufa.5 5 What Every one Should Know About Islam and Muslim, uk. 176, 177


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 21

21

Dhana hii ni ya kipuuzi mno kuweza kufikiriwa. Uislamu unasimama kwa imara juu ya msingi wa kwamba Yesu alikuwa ni Mtume wa kibinadamu tu, aliyeongozwa na Mwenyezi Mungu. "…Hakuwa Isa mwana wa Mariamu isipokuwa ni Mtume tu… “(Qur’an; 4:171) Kusema kwamba yeye alikuwa Mungu ni upakazaji wa ushirikina ambao ni kinyume na dhana ya umoja wa Mwenyezi Mungu. "…Hakika Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu, kwani kutukuka ni Kwake ameepukana na kuwa na mtoto…” (Qur’an; 4:171) Itikadi ambayo ina mizizi yake kwenye upagani na pia huenda kinyume na dhana ya Mungu Mmoja tu haina sehemu katika didi ambayo inadai kuwa yenye imani ya Mungu Mmoja. 2) Watatu Katika Mmoja (Trinity)? Tukiliweka kwa urahisi, Itikadi ya Utatu inasema kwamba Mungu ameundwa na vitu vitatu: Mungu Baba, Mungu Mwana - Yesu, na Mungu Roho Mtakatifu. Pamoja na kumuamini Yesu, Itikadi ya Utatu Mtakatifu ni moja ya misingi mikubwa kabisa ya Ukristo na ambao kwamba juu yake imejengewa itikadi nyingine za Ukristo".6 Dhana ya Imani ya Mungu Mmoja Kamusi iitwayo "Webster's New World Dictionary" imelitafsiri neno "Monotheism" kama “imani au itikadi kwamba kuna Mungu Mmoja tu."7 Dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu zote zinadai kushirikiana dhana hii. Imani hii ilisisitizwa na Nabii Musa katika kifungu ndani ya Biblia kijulikanacho kama "Shema," au imani ya Kiyahudi: 6 This Is The Catholic Church, uk. 4


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 22

22

"Sikieni, enyi Israel: Bwana Mungu wetu ni Mungu Mmoja tu" (kumb. ya torati 6:4) Takriban miaka 1500 baadae, ilirudiwa neno kwa neno na Yesu wakati aliposema: “…amri ya kwanza ni hii, Sikia, Israili, Bwana Mungu wetu ni Bwana Mmoja.” (Marko 12:29) Alipokuja Nabii Muhammad (saww) takriban miaka 600 baada ya Yesu, alileta ujumbe huo huo tena wakati aliposema: "Na Mola wenu ni Mungu mmoja hakuna Mungu mwingine isipokuwa Yeye tu…” (Qur’an; 2:163) Hata hivyo Ukristo umetoka kwenye dhana ya umoja (upweke) wa Mwenyezi Mungu, katika utata wao na fumbo la itikadi ya Utatu. Vipi Mwenyezi Mungu anaweza kuwa Mmoja wakati unamjumuisha Yesu na Roho mtakatifu? Ushawishi wa Paulo Na Hadhira Yake Ya Mataifa Ingawa hii ni itikadi moja ambayo haikupendekezwa rasmi na Paulo, hapana shaka yoyote kwamba alikuwa na itikadi kama hii akilini: Hata hivyo, kama angelimfanya Yesu kuwa mwana wa Mungu, inakubalika akilini kwamba baba wa kimungu alikuwa anahitajika: marekebisho pia yalihitajika ili kuthibitisha kuwepo kwa Roho Mtakatifu, ambaye Paulo aliamini kuwa ni chombo kilichotumika kuleta ufunuo wa Mungu kwa wanadamu. Kwa asili, Paulo aliwataja wahusika wakuu, lakini kanisa halikuvitambua rasmi mpaka karne ya nne ambapo kanisa liliweka vitu vyote pamoja. Kama hali ilivyokuwa kwa imani nyingine zilizopendekezwa kwa ajili ya Ukristo na Paulo, Utatu wa waungu pia ulikuwa na mizizi yake kwenye imani za upagani. Madhehebu ya watu wa Nimrod, yalianza mwanzo


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 23

23

Babylon, yalikuwa bado hai na salama wakati wa zama za Paulo: Nimrod kijana maridadi ambaye alimuoa mama yake, alikuwa akichukuliwa kama Mungu na watu wake; waliamini kwamba Baal, mungu wa jua, alikuwa ni baba yake. Baada ya kufa katika umri wake mdogo, mama yake Nimrod akawa mkuu wa madhehebu hii ya kipagani na akaanzisha wazo kwamba mwanaye alikuwa anaendelea kuishi katika maumbile ya kiroho. Kwa hiyo kwa mara ya kwanza utatu ukazaliwa: Baal, Mungu Baba, Mama wa Nimrod, na Nimrod - Mungu Mwana. Inawezekana kabisa kwamba ni kutokana na hekaya hii kwamba Paulo aliapata wazo la Utatu wa waungu kwa ajili ya Ukristo. Utatu Katika Biblia Kuna rejea mbili tu katika Biblia juu ya utatu wa waungu, na zote zinatatanisha kwa vyovyote. 1) Rejea ya kwanza inapatikana katika Mathayo 28:19. Hapa, Yesu anawaambia wanafunzi wake "Nendeni, mkafundishe na kuhuburi mataifa yote, mkiwabatatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu." Hata hivyo kuna matatizo fulani katika aya hii: a) Wakati ambapo inataja watu watatu ambao baadae wamewekwa kwenye utatu wa Ukristo, haitaji chochote kuhusu watu watatu kuwa sehemu ya mungu mmoja: b) Kwa Kuangalia kwenye maelezo mengine ya tukio hili hili - "Tume Kuu"- katika Marko 16:15, Yesu anasema: "Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Injili kwa watu wote." Je maneno ya ziada tunayoyaona katika rejea ya Mathayo yametoka wapi? c) Ubatizo katika zama za mwanzo wa kanisa ulifanywa kwa jina la Yesu tu, kama ilivyothibitishwa na Paulo katika nyaraka zake mbalimbali.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 24

24

2) Rejea ya pili inapatikana katika 1Yohana 5:7, ambako tunasoma: "Kwa kuwa wapo watatu wenye kumbukumbu za mbinguni, Baba, Neno, na Roho Mtakatifu: na watatu hawa ni "Mmoja." Ambapo rejea hii ni ya wazi zaidi juu ya utatu, wasomi wa Biblia katika karne ya 19 walikubali ukweli kwamba maneno "Baba, Neno na Roho Mtakatifu" ni maneno ya uzushi yaliyoongezwa - na maandiko ambayo hayapatikani katika nakala za Biblia za zamani zipatikanazo mpaka sasana maneno haya baadae hayapatikani katika Biblia za siku hizi. Mbali na aya hizi mbili- moja ambayo ni yenye utata, ya pili yenye kukiri ongezeko kwenye maandiko ya Biblia - HAKUNA rejea nyingine YA AINA YOYOTE katika Biblia inayozungumzia Utatu. Kwa kifupi wazo la utatu katika ukristo - Mungu Baba, Yesu Mwana na Roho Mtakatifu kama Mungu Mkuu anayeongoza wanaadamu - halikuwahi kutolewa hata siku moja na Yesu au Mtume yeyote mwingine aliyetangulia kabla yake. Misingi ya itikadi kama hii tayari ilikuwepo katika imani ya kipagani, hata hivyo, bila kutaja ukweli kwamba, wakati wa kipndi chake cha uhubiri, Paulo alitanguliza vitu vilivyohitajika ili kuunda utatu katika Ukristo. Kilichobakia tu kwa ajili ya wasomi wa Kanisa wa baadae ni kuweka kitu chote pamoja (yaani, utatu), kupitisha kitu haswa kabisa ambacho kilikuwa ni itikadi iliyotengenezwa na mwanadamu kama msingi wa itikadi ya Ukristo Ukristo wa Mwanzo Tertullian, mwanasheria na kiongozi wa kanisa katika mji wa Carthage, alikuwa ni wa kwanza kutumia neno "utatu " katika karne ya tatu wakati alipoweka mbele nadharia kwamba, Mwana na Roho Mtakatifu wanashirikiana katika uungu, lakini wote ni kitu kimoja cha kimaada pamoja na baba. Mabishano makali juu ya mada hii ya utatu yaliendelea kwa miaka mingi miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa kanisa: Baadhi waliafikiana


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 25

UJUMBE WA YESU

25

na Tertullian kwamba Utatu ulikuwa na watu watatu walio wazi au asili tatu, ambapo wengine walidai hiyo kuwa na utatu tu wa ufunuo - kwamba Yesu alikuwa ni mtu ambaye aliongozwa na roho wa baba ambaye alikuwa anaishi ndani yake. Mfalme Constantine alijikuta ametumbukia katika mabishano mnamo mwaka 318 B.K., wakati mabishano juu ya utatu yalipokuwa makali sana baina ya viongozi wawili wakubwa wa kanisa kutoka Alexandria: Arius afisa wa ngazi ya juu wa kanisa, anayemfuatia askofu, na Alexander, askofu wake. Baraza la Nisea (NICEA) Bila kuwa na hakika ya sheria za Kanisa lakini kuwa na uhakika katika elimu kwamba kanisa lililoungana lilikuwa muhimu kwa ajili ya mamlaka yenye nguvu; Mfalme Constantine, alijaribu kuwapatanisha hawa viongozi wawili wa kanisa.Wakati Askofu wake aliposhindwa kutatua tatizo hili, Constantine aliitisha mkutano wa baraza la Wasomi wakubwa katika masuala ya dini kwa mara ya kwanza katika historia ya kanisa uliokutana mwaka 325 B.K katika mji wa Nicea. Maaskofu 300 walihudhuria; baada ya kufanya kazi kwa wiki sita, Itikadi ya ya utatu iliundwa rasmi. Mungu wa Wakristo kuanzia siku hiyo alitambulika kuwa ana nafsi tatu - au asili tatu - katika muundo wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Itikadi hii iliyofikiwa baada ya mjadala mkali na Baraza la Nicea ilieleza hivi: ".... tunamwabudu Mungu mmoja katika utatu mtakatifu, na utatu katika umoja --- kwa vile kuna nafsi moja ya baba, nyingine ya mwana na nyingine ya roho mtakatifu ---- sio miungu watatu, isipokuwa ni Mungu mmoja - nafsi zote tatu hulingana kimilele na kulingana sawa--- kwa hiyo yeyote anayetaka kuokoka (kuokolewa) ni lazima afikirie


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 26

26

hivi kuhusu utatu mtakatifu…"8

Hata hivyo, suala hili lilikuwa mbali na utatuzi, licha ya matumaini makubwa kama hayo kwa upande wa Costantine. Arius na askofu mpya wa Alexanderia ayeitwa Athanasius walianza mabishano juu ya suala hili hata baada ya kutiwa saini Itikadi ya Nicea; “Arianism" (yaani, imani ya Arius) ilikuja kuwa ni neno la kurudia rudia kuanzia wakati ule na kuendelea kwa yeyote ambaye alikuwa kinyume na itikadi ya utatu Imeandikwa Katika Jiwe Mnamo mwaka 451 B.K. katika Baraza la Chalcedon, itikadi ya Nicea/ Constantinopole (inayoamini Utatu) iliwekwa kama mamlaka. Mdahalo juu ya utatu haukuvumiliwa tena; kuzungumza dhidi ya utatu ilionekana sasa kama kufuru, na hivyo adhabu yake ilikuwa ni kipigo kikali kwa kukatwa viungo au kifo. Wakristo sasa wakawageukia Wakristo wenzao, wakilemaza na kuchinja maelfu ya kwa sababu ya tofauti ya mawazo. Ingawa adhabu za kikatili za wakati ule sasa hivi hazipo, utatanishi na mabishano juu ya utatu unaendelea mpaka leo. Hata hivyo, kwa ujasiri, wakristo walio wengi bado wanashikilia kwa nguvu mafundisho haya ya msingi wa imani yao. Mantiki au bila mantiki Itikadi ya utatu inaweza kuwa msingi wa mafunzo ya Ukristo, lakini haina kabisa msingi wa Maandiko – asili yake yote ni kitu kilichotengenezwa na mwanadamu. Huu ni mfano mwingine tena wa jinsi gani imani za kipagani zilivyoingizwa kwenye mfumo wa imani ya Ukristo ili kuufanya ukubalike zaidi kwa wapagani. 8 Excerpts from The Athanasian Creed


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 27

UJUMBE WA YESU

27

Wakristo walio wengi, wanapotakiwa kuielezea itikadi hii (ya utatu), hawawezi kutoa jibu lolote isipokuwa kusema: "Ninaamini hivyo kwa sababu niliambiwa kufanya hivyo." Kwa kukwepa huielezea kama ni "fumbo”- ambapo Biblia inasema katika Wakorinto wa kwanza 14:33 kwamba: “…Mungu sio mwanzilishi wa utatanishi…” Hata mwanzilishi mwenyewe wa itikadi hii alipata ugumu wa kuielewa: Inasemekana kwamba Athanasius, askofu aliyetunga itikadi ya utatu, alikiri kwamba kila alivyoendelea kuandika juu ya mada hiyo, ndivyo alivyokosa uwezo wa kuelezea fikra zake kwa uwazi kuhusu itikadi hiyo. Mtazamo wa Uislamu Wakati ambapo ukristo unaweza kupata ugumu wa kufafanua asili ya "Mungu," tatizo hilo halipo katika Uislamu: "Wamekufuru wale wasemao - Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa utatu, hali hakuna Mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja (tu peke yake)…” (Qur’an; 5:73) Mwandishi Mmarekani wa Kiislamu Suzanne Haneef ameliweka jambo hili kwa maneno machache na kwa uwazi kabisa pale anaposema: "…Mungu sio kama nanasi au chungwa linaloweza kugawanywa katika sehemu tatu zinazounda kitu kimoja kizima; kama Mungu ni nafsi tatu au ana sehemu tatu, basi kwa vyovyote vile hawezi kuwa Mmoja, wa pekee, Mungu asiyeonekana ambaye ni Yeye…”9 Tukiliangalia suala hili kwa upande mwingine: utatu una maana Mungu ana vijisehemu vitatu vilivyo tofauti tofauti - Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ikiwa Mungu ni baba na vile vile mwana, basi atakuwa mwenyewe yu baba kwa sababu Yeye ni mtoto wa Yeye mwenyewe. 9 What Everyone Should Know About Islam and Muslims, uk. 183-4.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 28

28

Hii sio mantiki kabisa Ukristo unadai kuwa ni dini yenye kuamini Mungu Mmoja. Kwa kuanzisha utatu wa waungu, hata hivyo, hakuna shaka katika fikra za Mwislamu kwamba ukristo umeshapoteza kabisa dhana ya kumwabudu Mungu Mmoja. Wameondoka kwenye ibada na imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja kwenda kwenye ushirikina kwa sababu hawamuabudu Mungu Mmoja tena - wanaabudu watatu. Hii ni shutuma ambayo haichukuliwi kwa wepesi na Wakirsto. Wao, badala yake wanawashutumu Waislamu kwa kutokuelewa utatu, wakidai kwamba Qur’an huiweka kama Allah ni baba, Yesu ni mwana, na Mariamu ni mama yake. Ambapo utukuzaji wa Mariamu umekuwa ni ubunifu wa Kanisa la Kikatoliki tangu 431 B.k. wakati alipopewa cheo cha “mama wa Mungu” na baraza la Efesazi (Ephesus), uchunguzi wa karibu kwenye aya za Qur’an Tukufu ambazo hutajwa zaidi na Wakristo kwa kuunga mkono shutuma zao huonesha kwamba uteuzi wa Mariamu katika Qur’an Tukufu kama “mshirika” wa utatu kwa ufupi sio kweli kabisa. Ambapo Qur’an inaishutumu vikali imani ya utatu (4:171), (5:73) na ibada ya Yesu na Mama yake, Mariamu (5:116), hakuna sehemu yoyote katika Qur’an ambapo inavikubali vitu hivi vitatu haswa vya utatu wa Ukristo. Msimamo wa Qur’an ni kwamba NANI au NINI kinachounda itikadi hii si suala lenyewe; suala ni kwamba dhana yenyewe haswa ya utatu ni tusi dhidi ya Upweke (umoja) wa Mwenyezi Mungu. Hakuna nafasi yoyote katika imani ya Mungu Mmoja kwa ajili ya mungu mwingine wa kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu, na katika hilo Qur’an inasimama imara: "Na Mola wenu ni Mungu Mmoja: hakuna mungu mwingine isipokuwa Yeye, Mwingi wa Rehema, Mwingi wa kurehemu." (Qur’an; 2:163)


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 29

UJUMBE WA YESU

29

"…Na Mimi ni Mola wenu kwa hiyo niabuduni.” (Qur’an; 21:92) 3) Kifo Kimoja kusamehe Wote! Tukiweka kwa urahisi, itikadi ya kafara inaeleza kwamba Yesu aliteswa na kufa msalabani ili kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye minyororo ya dhambi. Dhana ya Dhambi ya Asili Inawezekana Paulo alikuwa mfanyabiashara, lakini alikuwa mtu mjanja sana, hii inaweza kuonekana kwa jinsi alivyounda mfumo wenye utatanishi wa imani kwa ajili ya uokovu katika Ukristo. Hii inaonekana vizuri zaidi katika Itikadi ya Mateso na kifo cha Yesu Imani ambayo imani nyingine zote - ile ya uungu wa Yesu, Utatu na kuokoka kwa imani – hutegemea kabisa juu ya msingi huo. Mbele ya Paulo, wanadamu wote ni waovu, sifa isiyoaminika ambayo wote wameirithi kutoka kwa Adam na dhambi yake katika kula tunda la mti uliokatazwa katika Bustani ya Eden. Hii "dhambi ya asili" imewatia doa wanadamu wote tokea wakati wa Adam; kwa sababu ya doa hili la dhambi, mwanadamu hawezi kujihudumia kama mkombozi wake mwenyewe. Yesu ndiye angeweza kumhudumia katika wadhifa huu kwa vile yeye hakuzaliwa kutokana na mbegu ya mwanadamu. Japokuwa kimantiki hii ni dhulma kwa wowte; Mwenyezi Mungu na mwanadamu, ukristo kwa moyo wote umeichukua na kuihalalisha itikadi hii ya dhambi ya asili ili kuithibitisha dhana yao ya ujumbe wa Yesu, yaani kafara kwa ajili ya dhambi za mwanadamu. Kwa kuifanya itikadi hii ya dhambi ya asili itumike, yaelekea Paulo alisahau maneno ya Mungu katika Ezekiel; 18:20 -22: "…Mtoto hatabeba dhambi za baba, wala baba hatabeba dhambi za mtoto..."


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 30

UJUMBE WA YESU

30

Muhanga wa Mwisho Kwa mujibu wa Paulo, mwokozi wa mwanadamu alikuja katika sura ya Yesu: Mungu alimtuma mwanaye wa pekee duniani ili aje apate mateso na hatimaye afe msalabani ili damu itakayomwagika iwe kafara ya dhambi za wanaadamu. Yesu ndiye aliyekuwa mhanga wa kafara. Paulo alikumbusha kafara zilizokuwa zikitolewa na Wayahudi kwa Mungu katika agano la Kale na akahisi kwamba kafara hizi zilitolewa ili kupata msamaha wa Mungu kutokana na madhambi ya watu. Wakati baadhi ya kafara hizi zilizotolewa na Wayahudi zilifanywa kwa ajili ya maondoleo ya dhambi, Mitume waliokuja baadaye walikataza jambo hili. Katika Hosea; 6:6, kwa mfano, tunasoma: "Kwa kuwa Ninataka upendo thabiti na sio kafara." Mungu alitaka upendo - ambao husababisha kumwamini Yeye na utii wa sheria yake - kuliko damu. Hata Yesu mwenyewe aliusisitiza ujumbe huu tena, katika Mathayo; 9:13, ambapo tunasoma: "Nendeni na mkajifunze maana ya maneno haya: Ninataka rehema sio kafara." Paulo aliyaweka yote haya pembeni, akasema kwamba Yesu, kiumbe mkamilifu, alikuwa "Kafara wa mwisho" alipoyatoa maisha yake msalabani. Nadharia ya Paulo ni kwamba Mungu hawezi kuchukuliwa kuwa ni Muadilifu mpaka amuadhibu mwenye dhambi. Toba peke yake haiwezi kuwa kigezo "muhimu" kwa ajili ya (kusamehewa) madhambi yaliyofanywa. Anasema kuwa kuteswa na kufa msalabani kwa Yesu, ni muhimu sana


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 31

31

kwa sababu heshima, uadilifu, utukufu na uongofu wa Mungu haviwezi kutosheleza kwa toba "peke yake." Kwa Mkristo, Yesu alipatanisha baina ya wanadamu na Mwenyezi Mungu kupitia kifo chake. Mwandishi wa Kikristo Anis Shorrosh alilichunguza jambo hili kwa umakini sana miaka mingi iliyopita, na akahitimisha kwamba hakuna ukweli juu ya kuteswa na kufa katika kukiri imani na toba; nani atakayechukua mzigo wa dhambi zetu? 10 Kutokana na suala zima kwamba Mwenyezi Mungu alimtaka Yesu ayatoe maisha yake kwa ajili ya dhambi za wanadamu, Paulo alichukua dhana ya Mwenyezi Mungu ambaye anayewapenda na kuwajali viumbe wake, na akamfanya kuwa ni katili na aliye mbali sana ambapo kitu kingine chochote kisichokuwa damu ya Yesu hakiwezi kumfikia wala kumridhisha. Mungu wa Upendo Wazo lililoasisiwa kwanza na Paulo -- na ambalo hujitokeza tena na tena katika Ukristo, hususan kuhusiana naYesu -- ni lile la Upendo na Mungu. Kwa mujibu wa wakristo, upendo wa Mungu unahusika katika kusulubiwa na kufa kwa Yesu - wanasema, alama ya upendo wa Mungu ni msalaba. Kwa mujibu wa namna yao ya kufikiri, Mungu alitupenda mno hata akamtuma mwanae wa pekee ili apate mateso na hatimaye afe ili amwokoe mwanadamu kutoka kwenye minyororo ya dhambi. Je, Mungu Anaweza Kufa? Tukiendelea na dhana yenye kutatanisha kwamba Mungu wa Wakristo atasamehe tu rundo la dhambi ndogo kwa njia ya dhambi kubwa – ile ya kuua - kuna suala la kuvutia mno la uungu hapa lenye utata. Mungu ni wa milele, alikuwepo tangu na tangu na atakuwepo milele na milele: Hakuumbwa. 10 Ibid uk. 135


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 32

32

Hawezi kufa Kama Yesu ni mtoto wa Mungu, kama wakristo wanavyodai, hii ingemfanya na yeye kuwa Mungu pia, ingewezekanaje yeye, kama Mungu, afe msalabani kama wanavyodai? Ikiwa "mwili wake wa ubinadamu" ndio ulikufa, hii italeta maana kwamba alikufa kama mtu mwingine yeyote. Na kwa hali hii, itikadi yote ya kuwa Yesu aliteswa na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanaadamu, itakuwa haina msingi wowote -- damu ya mtu haiwezi kuwa fidia ya dhambi za mtu mwingine. Ushawishi wa Upagani Paulo hakuyaelewa madhumuni ya kafara zilizokuwa zikitolewa na Wayahudi katika Agano la Kale; zilitolewa kuonesha shukrani kwa Mwenyezi Mungu kutokana na neema nyingi ambazo Mwenyezi Mungu aliwajaalia - na sio kwa ajili ya kuhakikishiwa msamaha wa Mwenyezi Mungu kutokana na madhambi yao. Karibu dini zote za kipagani zinaamini kwamba kafara wanazozitoa kwa miungu yao ni kwa ajili ya kutaka msamaha wa madhambi yao. Mimea, wanyama na hata watu waliuawa ili kuhakikisha kupatikana kwa "upendeleo wa kimungu." Sio hivyo tu, bali karibu dini zote za kipagani huchukua pamoja nao aina fulani za tambiko ambazo kwazo wafuasi wake hula vyakula vya wakfu hasa mikate na pombe. Wapagani waliamini kwamba, kwa kula vyakula hivi vya wakfu, wao pia walikuwa wanashiriki katika sifa na nguvu za mungu wao – basi roho ya mungu itaishi ndani yao. Paulo alichukua dhana hii ya kipagani akaiingiza katika Ukristo, akaiita kuwa ni "Sakramenti ya chakula cha Bwana au Ekaristi"; kwa sababu inachukuliwa kuwa ni sehemu kubwa ya itikadi ya kuteswa na kufa kwa Yesu, ibada hii ya Ekaristi imekuwa ni moja wa Sakramenti muhimu


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 33

33

kabisa katika Ukristo kwa sababu humuonesha Yesu akitoa mwili na damu yake kama fidia ya dhambi za mwanadamu. Itikadi ya kuteswa na kufa kwa Yesu haikuleta matatizo mengi kwa Paulo kuwageuza mataifa kuwa Wakirsto; hata hivyo kwa vile imani ya Mungu kufa akiwa kijana na baadaye kuwa hai ilikuwepo katika imani zao za kipagani. Ikiwa miungu wao akina Adonis au Mithran waliwahi kufanya kitu cha aina hii kabla ya kuingia katika dini ya Ukristo, kwanini Yesu asilifanye hilo sasa? Paulo Alifanikiwa nini? Watu wa mataifa kwa mara nyingine tena walitulizwa: walikuwa na waokozi wao katika dini zao za zamani, na mara hii tena, Paulo kwa uzuri sana aliwapa mwokozi mmoja katika imani yao mpya. Aliwaambia kwamba walichokuwa wanatakiwa kukifanya tu ili kuwa na yakini kwamba Mwenyezi Mungu atawasamehe madhambi yao ni kuamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zao; hilo tu ndilo lililokuwapo kwa ajili hiyo. Katika sheria ya Kiyahudi, vitu vya upatanisho huwa na Rehema ya Mungu, toba na jitihada za dhati katika kufanya mambo ya kheri; kafara ya damu haikuwa na la kufanya lolote katika hili. Katika jitihada zake za kuwapata watu wa mataifa, hata hivyo, Paulo alilitafsiri upya Agano la kale na akawapa Wakristo wapya mwokozi wao - mtu ambaye huyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine. Wakristo wa leo hawana ukaribu na upagani kama ilivyokuwa katika wakati wa Paulo. Itikadi yake ya kuteswa na kufa kwa Yesu imekuwa ni tatizo kubwa kwa Wakristo wa leo kwa kawaida kuilezea vya kutosha, baada ya kuona kwamba suala lote hutatanisha ambapo nguvu za kimantiki na teolojia zinapokuja kucheza katika akili zao.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 34

UJUMBE WA YESU

34

Mtazamo wa Uislamu Uislamu unaichukulia itikadi hii ya Wakristo kama ifuatavyo: Dhana ya Dhambi ya Asili, itikadi ya ukristo juu ya dhambi ya asili haina nafasi yoyote katika Uislamu, kwani Waislamu wanaamini kwamba mwanadamu huzaliwa akiwa safi bila dhambi yoyote. Ndani ya Qur’ani, Mwenyezi Mungu anasema: "Uelekeze uso wako katika dini iliyokuwa sawa sawa ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumba watu. Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe wa Mwenyezi Mungu, hiyo ndio dini iliyo haki…” (Qur’an; 30: 30) Aya hii inatueleza kwamba Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu katika umbile zuri kabisa, katika hali asili ya usafi; yaani, kuwa na hali ya asili ya kuelekea na kujisalimisha kwenye utashi na amri za Mwenyezi Mungu.11 Dhambi sio ya kurithiwa: ni kitu ambacho mwanadamu mwenyewe anajiletea wakati ambapo anafanya vitu ambavyo hatakiwi avifanye; au hafanyi vitu ambavyo anastahiki kufanya. Kusema kwamba kila mmoja wetu huja duniani anapozaliwa akiwa amebebeshwa mzigo wa madhambi yaliyofanywa na babu wa nyuma kabisa, si chochote bali ni kukana sifa za Mwenyezi Mungu ya Uadilifu na Rehema. Ingawa Mwenyezi Mungu amemjaalia mwanadamu stadi za kuweza kuchagua katika maisha yake, mwanaadamu ni kiumbe mwenye ukomo na ukomo wa asili na uwezo. Athari za mazingira - yenye mema na maovu hutengeneza matokeo ya hulka zetu, sio kitu ambacho kilifanywa wakati uliopita na ndugu wa zamani sana. Kile ambacho tutajifanyia sisi wenyewe mwishowe ndicho kitakachochukuliwa katika hesabu na Mwenyezi Mungu katika Siku ya Hukumu; wakati wa maisha haya, Anatupa kila fursa ya kutosha. Ni sisi, wenyewe tu, ambao ni wasanifu wa kudra zetu 11 Islam in Focus; uk. 32


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 35

35

wenyewe. Hii ni kwa sababu Waislamu wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu alimsamehe Adam kosa lake la kutotii kwake amri ya Mwenyezi Mungu. "Kisha Iblis aliwatekelezesha wote wawili humo na akawatoa katika hali waliyokuwa nayo. Tukasema: Shukeni hali ya kuwa nyinyi kwa nyinyi ni maadui, nanyi katika ardhi mna makao na starehe kwa muda. Basi Adam akapokea maneno kwa Mola wake, na akamkubalia toba yake, hakika Yeye ndiye apokeaye toba, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani; 2:36-37) Mwenyezi Mungu alimsamehe Adam, na hatimaye aliondoa doa lolote la dhambi ambayo Wakristo wanadai kuwa imerithiwa na wanadamu kuanzia wakati wa Admu na kuendelea. 2) Kifo Cha Yesu Kuhusiana na suala la kifo cha Yesu msalabani - ingawa ni wazi kwamba Yesu - kama walivyofanya mitume kabla yake - alipatwa na masaibu makubwa kwa sababu ya kujaribu kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu ambao hawakuonyesha moyo. Na alikuwa anajua vizuri kwamba hili lingemtokea, haendi mbali sana kiasi cha kusema kwamba atauliwa - hususan kwa ajili ya madhumuni aliyohusishwa na Paulo baadae, yale ya kumuokoa mtu kutokana na dhambi. Katika Bustani ya Gethsemane, Yesu aliomba kwa unyenyekevu na shauku kwa Mwenyezi Mungu kuwa "kikombe hiki kiniepuke" (Mathayo 26:39), ambako “kikombe hiki” kinamaanisha kukamatwa na kufa kwake. Hivi kweli tuamini kwamba mja mnyenyekevu wa Mwenyezi Mungu angeomba kwa ajili rehema na asiipate? Wazo zima la kuteswa na kufa kwa Yesu msalabani ili awe kafara ya dhambi za wanadamu huja kama dhana isiyo mantiki, nje kabisa ya kawaida tukichukulia wazo la Mungu Mwenye uadilifu. Je, inawezekana kwa


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 36

36

Mwenyezi Mungu Mwenye uadilifu awe hataki kumsamehe Adam - na mwanadamu baada yake - kwa ajili ya dhambi zake mpaka Yesu aje? Je, inawezekana kwa Mungu Mwenye uadilifu angetaka na kuruhusu kudhalilishwa na kuuwawa kwa mmoja wa mitume wake aliyekuwa mnyenyekevu na mtiifu mno sana kwake? Je, inawezekana kwa Mungu Mwenye uadilifu angemlazimisha mtu kufidia dhambi za mtu mwingine? Katika Uislamu, hii haiwezekani. Kama mtu akiangalia hili kutoka kwenye mtazamo wa upendo wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waja Wake, hoja hizo hizo kwa ajili ya Mungu Mwenye uadilifu vile vile huenea: Je, hivi Mungu Mwenye upendo angewaadhibu wanadamu wote mpaka hapo Yesu atakapokuja? Je, Mungu mwenye upendo angedai udhalili unaoogopesha na kifo cha mmojawapo wa watumishi Wake wapendwa mno na mnyenyekevu? Mtu anaweza tu kushangaa ni upendo wa aina gani ungelazimisha gharama kubwa kama hiyo na ya kutisha? Uislamu unasimama imara juu ya nadharia ya uwajibikaji binafsi: kila mtu huwajibika na matendo yake mwenyewe. Haiingii akilini kwamba Mungu Mwenye uadilifu angemshikilia mtu mmoja kuwajibika kwa ajili ya dhambi za mtu mwingine: "...Wala nafsi yoyote haichumi (ubaya) ila ni juu yake, wala mbebaji hatabeba mzigo wa mwingine…” (Qur’an; 6:164) Hakuna mtu anayeweza; wala atakayeadhibiwa, kwa dhambi za mtu mwingine. Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba kila mmoja wetu atalipwa au kuadhibiwa kutokana na aliyoyafanya yeye mwenyewe katika maisha yake: “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote, ila iliwezalo. Ni juu yake (kheri) iliyochuma, na ni juu yake (shari) iliyochuma…” (Qur’ani; 2:286)


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 37

37

3) Ama Kuhusiana na Kafara "Na kila ummah tumewafanyia mahala pa kuchinjia mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyoruzukiwa…Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia uchamungu wenu…” (Qur’ani; 22:34, 37) Kwa hayo, Uislamu hauamini kwamba Yesu aliuliwa. Tunasoma katika Qur’ani Tukufu: "Na kusema kwa hakika tumemuua masihi Isa mwana wa Mariamu, mtume wa Mwenyezi Mungu, wala hawakumuuwa wala hawakumsulubu…Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua Kwake…” (Qur’ani; 4:157-158) Kwa kifupi, itikadi ya ukristo kuwa Yesu aliteswa na kuuliwa ili awe kafara ya dhambi za wanadamu haina nafasi yeyote katika Uislamu. Waislamu wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu anataka sana toba ya kweli tu kwa upande wa wanadamu: "Na ombeni msamaha kwa Mola wenu, kisha tubuni Kwake. Hakika Mola wangu ni mwenye kurehemu, Mwenye kuwapenda." (Qur’ani; 11:90) Wokovu unatoka kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake "Basi ama aliyetubia na akaamini na akafanya vitendo vizuri, ni hakika atakuwa miongoni mwa wenye kufaulu.” (Qur’ani; 28:67) Kama tunamwamini Mwenyezi Mungu, na tukijisalimisha Kwake kabisa na kuufuata Mwongozo Wake, tunaweza kuwa na uhakika wa Huruma na Rehema Yake juu yetu. Kama inavyoonekana kwenye aya hapo juu, kama toba kwa upande wetu ni ya kweli, Mwenyezi Mungu anaweza na hutusamehe dhambi zetu. Hakuna haja ya mwombezi, kwani kila mmoja wetu ana njia ya moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu kwa wakati wote.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 38

UJUMBE WA YESU

38

Kwa kifupi hakuna haja ya mwokozi: Mwenyezi Mungu peke yake anaweza kusimamia yote.12 4) Kuokoka kwa Imani Peke Yake Tukiweka kwa urahisi, itikadi ya wokovu katika Ukristo inasema kwamba mwanadamu anaweza kuokoka kwa kuamini tu katika wazo kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Kuwatuliza Watu wa Mataifa Kulikuwa bado kuna suala juu ya nini kinachotokea baada ya kifo. Mitume wote walifundisha juu ya raha za peponi na shida za motoni, Yesu pia alilifundisha hili. Waumini wapya wa Paulo walihofu sana juu ya hili pia. Walitaka kujua ni namna gani wangeweza kuwa na uhakika wa kuingia peponi pindi mwisho wa dunia utakapofika. Sheria ya Kiyahudi ilifundisha kwamba wokovu hupatikana kwa utii wa sheria hiyo. Hata hivyo watu wa mataifa, hawakulifurahia wazo hili. Walimlalamikia Paulo kwamba Sheria hii ilikuwa ngumu sana kwao. Paulo alilishughulikia hili katika njia ya kipekee kwa kusema kwamba utii kwenye Sheria haukuwa wa lazima tena: â€œâ€ŚNi dhahiri kwamba sheria haiwezi kumfanya mtu akubalike mbele ya Mungu- - - hakuna uhusiano kati ya sheria na imani --- kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria- - -." (Wagalatia 3: 11-13) Wakati ambapo sheria ilikuwa inamweleza mwanadamu yapi ni mazuri na yapi ni maovu, Paulo alisema kwamba kuja kwa Yesu kulibatilisha utii kwenye sheria kama njia ya wokovu: "Maana mtu hufanywa akubalike mbele ya Mungu kwa imani si kwa kutimiza matakwa ya sheria." (Waroma 3:28) 12 What Everyone Should Know About Islam and Muslims, uk. 183-184.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 39

UJUMBE WA YESU

39

Licha ya ukweli kwamba Yesu mwenyewe alisema kuwa hakuja kuivunja sheria bali kuikamilisha (Mathayo 5:17), Paulo aliyadharau kabisa mafundisho haya ya Yesu, kwa kusema kwamba kumuamini Yesu peke yake kulikuwa kunatosha kwa ajili ya wokovu. Kwa mujibu wa Paulo, kuja kwa Yesu na kuyatoa maisha yake kama kafara ya dhambi za wanadamu, kulikuwa ndio mwisho wa haja ya kufuata sheria ya Mungu ili kupata wokovu. Imani peke yake tu katika “nguvu ya wokovu” wa Yesu ndiyo iliyokuwa ya muhimu sasa. Uokovu haukutegemea tena juu ya namna mtu alivyoyaendesha maisha yake au matendo mema ambayo mtu aliyafanya, bali juu ya imani ambayo mtu aliyokuwa nayo. Laana ya Sheria Paulo alikuwa na sababu nyingine kwa kuchukua msimamo ambao alioufanya juu ya Sheria ya Mwenyezi Mungu. Katika kumbukumbu la Torati 21:23, Mungu anamwambia Musa kwamba mtu "aliyetundikwa katika mti"… kwa maneno mengine aliyesulubiwa msalabani "amelaaniwa na Mungu". Ili kulinda hoja hii, Paulo aliamua tu kwamba Sheria ililaaniwa. "Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na sheria, wako chini ya laana. - Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana maandiko yasema "Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa". (Wagalatia 3:10-13) Kwa sababu Paulo aliiona sheria ya Mungu kuwa ni laana, hivyo maneno ya Mungu katika kumbukumbu la Torati 21:23 hayakuwa na maana tena. Alipotosha maneno ya aya hii kwa kusema, wakati ambapo Yesu alikuwa amehusihwa kwenye laana kwa sababu aliuliwa kwa kusulubiwa msalabani, kwa kutokuwa kwake na hatia, aliibeba laana hii kwa sababu ya dhambi za wengine na kulikuwa hakuna dosari ya kulaaniwa kwa namna hiyo kulikohusishwa naye. Alilofanya Paulo hasa ni kulipa utukufu jambo ambalo awali lilikuwa linaonekana ni la aibu sana ili aweze tu (Paulo)


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 40

UJUMBE WA YESU

40

kuthibitisha muundo wake huu wa wokovu aliouanzisha. Kwa mujibu wa Anis Shorrosh anasema: "Msalaba, alama ya aibu, umekuja kupitia kwa Yesu kuwa ni alama ya changamoto. Msalaba, alama ya kifo, ilikuja kupitia kwa Yesu, kuwa alama ya uhai".13

Utekelezaji hakika wa Itikadi hii Kwa sababu ya upinzani mkali kutoka kwa wanafunzi wa Yesu, Paulo alilazimika kwenda pole pole katika utekelezaji wa jambo hili. Alianza na kitu kimoja ambacho watu wa mataifa walikipinga sana: yaani kutahiri. Kwa mujibu wa Paulo, Ibrahimu alikuwa mwongofu hata kabla ya kutahiriwa, sasa kwa nini kuhangaika nako tena? Hata hivyo Paulo alichopuuza, ilikuwa ni ukweli kwamba Mungu alikuwa ameweka agano na Ibrahim mamia ya miaka, likiwa limepigwa muhuri kwa Amri za Mungu pamoja na kutahiriwa kwa Ibrahim na watoto wake wote wa kiume baada ya hapo na kuendelea. Katika kitabu cha Mwanzo 17:14, Mungu aliliweka wazi kabisa jambo hili: “Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu". Mtu anaweza tu tena kushangaa vipi Paulo kwa wazi kabisa kuyafuta maneno haya. Ubatizo ulichukua nafasi ya kutahiri, kumwagiwa maji sasa kumefanywa kuwa ndio alama ya agano baina ya Mungu na Mkristo. Watu wa mataifa kwa mambo yalivyokuwa walifurahia sana. Kilichofuata ni mabadiliko juu ya vyakula, na masuala mengine yalifuatia 13 Islam Revealed, uk. 137


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 41

UJUMBE WA YESU

41

moja baada ya jingine. Ndani ya muda mfupi, Sheria ya Mwenyezi Mungu ikawa si chochote bali ni matayarisho ya nguvu ya wokovu wa Yesu kwa Wakristo - kitu ambacho hakikuwasumbua kwayo tena. Ambapo matendo mema kwa mujibu wa Paulo, kwa kawaida “yatakuja� kwa Mkirsto, lazima aelewe kwamba matendo mema peke yake hayataweza kuhakikisha uwokovu; imani tu peke yake katika nguvu ya wokovu wa Yesu utafanya hivyo. Paulo Alifanikiwa Nini? Paulo aliwapatia wakristo wapya itikadi hii ya wokovu kwa kutegemea juu ya imani peke yake kwa sababu moja: Kupata wafuasi miongoni mwa watu wa mataifa. Watu wa mataifa walikuwa wamewachunguza Wayahudi na ibada walizokuwa wakifanya katika kanuni zao za ibada, na walikuwa wanasita kuukubali ukristo kwa sababu ya hamu kubwa ya kupita kando kabisa ya kanuni na sheria zote zilizomo katika sheria ya Torati ya Musa. Itikidi hii ya mwisho, yaani wokovu kwa imani katika Yesu peke yake, kwa kusema kweli ilikuwa ya siasa kali, ambayo bado ni moja iliyofanikisha ujumbe wa Paulo, kwa sababu iliwapa haswa kile ambacho walikitaka, na walikusanyika kwake katika makundi. Yesu asingelikuwa na mpangilio wa kufundisha ujumbe wake nje ya Wayahudi, wala kuanzisha dini mpya, lakini Ukristo ulizaliwa na kuwa kundi liloenea duniani kote, shukrani ziyaendee mafundisho ya Paulo. Mtazamo wa Uislamu Mungu alimtuma Yesu kwa Wayahudi kwa sababu waliitupa ibada ya Mwenyezi Mungu kwenye usuli kwa upendeleo wa maelezo na ufafanuzi wa Sheria. Vitabu 63 vya Talmud - ambavyo ni tafsiri na uchambuzi wa sheria ya kiyahudi - ni uthibitisho juu ya jambo hili. Kwa Myahudi, wokovu ulipatikana kwa kutii Sheria ya Mungu.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 42

UJUMBE WA YESU

42

Yesu alitumwa katika jitihada za kuwaelewesha Wayahudi kwamba vitendo vizuri peke yake sio mwisho wa mambo -- bali mtu lazima awe na imani katika Mungu pia. Yesu alisisitiza mara kwa mara kwamba "ibada tupu na unafiki wa mapenzi” si jambo lililotakiwa na Mungu katika njia ya ibada; badala yake, Wayahudi walitakiwa kufuata maandiko ya mwanzo “pamoja na uaminifu, uchamungu wa ndani na dhamira ya kweli ya Mungu.”14 Hili ndilo ambalo Yesu alilifundisha kwa juhudi zote, lakini kwa bahati mbaya hili silo ambalo Wakirsto wanaloliamini. Ujumbe ule wa Yesu "…Amri kuu kuliko zote ni, sikieni, Enyi Israel; Bwana Mungu wetu ni Mungu Mmoja". …unaopatikana katika Marko 12:29, si chochote ila ni maandishi tu katika karatasi. Paulo alimpachika Yesu uungu, kisha akabuni mpango uliochanganuliwa wa uwokovu kwa Yesu ambao kwamba huhusisha imani peke yake. Utii kwa Mungu umetupwa kando, ukaitwa kuwa ni "Laana." Qur’ani imeliweka jambo hili wazi kabisa kwa sema kwamba masharti ya uokovu ni mawili: imani katika Mungu Mmoja, na utii kwenye Amri Zake. "Kwa wale ambao wameamini na wakafanya vitendo vizuri Mwenyezi Mungu amewaahidi msamaha na malipo makubwa". (Qur’ani; 5:9)

MAELEZO YA JUMLA JUU YA ITIKADI YA UKRISTO Kwa matumizi ya itikadi hizi nne -- yaani ile ya uungu wa Yesu, utatu, kuteswa na kufa msalabani kwa Yesu na wokovu kwa imani--Paulo alipata ufanisi mkubwa sana katika ujumbe wake. Wayahudi inawezekana walimuweka Yesu kando, lakini watu wa mataifa walimzunguuka Paulo, kwa 14 What Everyone Should Know About Islam and Muslims, uk. 180.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 43

43

vile aliwapa kile ambacho walikitaka katika dini yao mpya. Istilahi kwa wafuasi wa mwanzo wa Yesu ambayo ni - Wanazareti--ilifutwa kwa kupendelea jina jipya lenye kufaa zaidi: Wakristo, au wafuasi wa Yesu Kristo. Dini hii mpya ya Ukristo “…ilikuwa imefumwa kwa wingi sana na mambo ya mithiolojia (ubunifu) yaliyochukuliwa kwa wingi kutoka kwenye vyanzo vya kipagani…” pamoja na kuwa na theolojia “…ambayo ilizalishwa kama haja ilivyohitajia kulingana na akili za wakati…” 15 Wayadi walimuweka kando Yesu; hata hivyo, kwa njia nyingine, dini ya ukristo kama ilivyotungwa na Paulo vile vile imemuweka Yesu kando. Pamoja na atakachosema Mkristo, mtu ataona hakuna ushahidi ambako Yesu mwenyewe ameweka mbele itikadi zozote zilizotangulia kutajwa ndani ya Injili. Kwa vile Yesu alikuwa hana mpango wa kuanzisha dini mpya, ni wazi kabisa kwamba yeye pia hakuunda itikadi yoyote kwa hili. Itikadi zote za Ukristo ni kazi ya Paulo, iliyotegemezwa juu ya matamanio yake ili apate upendeleo -- na wafuasi wapya--miongoni mwa wasio Wayahudi wa wakati wake. Kwa kuingiza imani za kipagani kwenye mafundisho ya Yesu, Paulo alipata mafanikio mkubwa kabisa katika ujumbe wake, lakini kwa gharama ya kuchana kila kitu ambacho imani ya kweli ya Mungu Mmoja husimamia. Kwa kufanya hivyo, Paulo alifuta mafundisho yote ya Yesu na akampa mwanadamu seti ya imani ambayo imetaabisha akili yake ya kuhoji tangu hapo. Ni hapa--kwamba ukweli halisi na jukumu la Yesu, kinyume na mtazamo wa Ukristo kwa hili--ambako tunaona tofauti za kimsingi kati ya Uislamu na Ukristo. Inavutia kuona kwamba Ukristo “…itikadi zile ambazo Qur’ani inazithibitisha zinaweza kuthibitishwa kwa urahisi kabisa, kuwa ni sehemu ya mafundisho ya wanafunzi wa mwanzo kabisa wa Bwana Yesu, ambapo kwamba itikadi zile ambazo Qur’an inazikataa zinathibitisha kuwa 15 Ibid, uk. 182


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 44

UJUMBE WA YESU

44

ni nyongeza zilizoongezwa baadae na Kanisa, zilizosukumwa na filosofia na ibada za kipagani za Kigiriki na za Kiroma.� 16

MAANDIKO YA KIKRISTO Wakati ambapo itikadi ina nafasi ya muhimu katika Ukriosto, ukweli wa msingi wa imani hupatikana katika vitabu 66 vijulikanavyo kama Bibilia. Bibilia ni mwongozo kwa Mkristo; ndani yake kuna mwongozo wa Mungu kwa mwanadamu, umejengwa katika Yesu, umefunuliwa. Dini iliyofunuliwa ni sahihi tu kama ufunuo ambao kwayo imesimamia. Katika suala la Ukristo, msingi wote huu muhimu ni dhaifu kabisa kwa sababu ya kuharibiwa katika maandiko yake na mwanadamu. Ufunuo upo pale sawa sawa, lakini tatizo liko kwa kile kilichotokea kati ya kipindi ufunuo wa kimungu ulipotolewa na kipindi ambacho ufunuo huu ulikuja kuandikwa. Uchunguzi Juu ya Agano La Kale Wayahudi walishuhudia nyumba yao ya ibada ya Jerusalem ikiharibiwa kabisa mnamo mwaka 581 B.K., pamoja na tukio hili zilitoweka pia nakala za asili za Torati. Ingawa wandishi--mashuhuri zaidi Ezra--hatimaye alirudisha kile kilichopotea, waandishi hawa walizifanyia kazi nakala na kutoa nakala nyingine zaidi kutoka humo. Mabadiliko yaliyofanywa ni ukweli ambao ni wanachuoni wachache tu wa Bibilia watakataa: mabadiliko katika muundo, mabadiliko katika nahau, nyongeza kwenye hifadhi mbali mbali (za maandiko) ili kuvipamba visa, na hata kufuta kabisa vitu ambavyo mwaandishi hakufurahishwa navyo. Kwa kifupi, kazi za waandishi hawa ziliathiriwa sana na wakati walioshi, pamoja na hisia zao binafsi na imani. 16 Jesus in the Qur'an, uk. 14.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 45

UJUMBE WA YESU

45

Mifano kadhaa ya mabadiliko ya maandishi ni kama ifuatavyo: 1) Kuna tafsiri mbili zinazotofautiana juu ya uumbaji zinazopatikana katika kitabu cha mwanzo: Katika sura ya kwanza, imeandikwa kwamba uumbaji ulichukua siku sita; hata hivyo kwa mujibu wa sura ya pili Mungu aliifanya yote haya katika siku moja (2:4). Tukiendelea na fikra hii ni ukweli kwamba ilisemwa Adamu alikuwa ni kitu cha mwisho ambacho kiliumbwa katika tafsiri ya kwanza (1:27), ambapo kwamba aliumbwa wa kwanza, kabla ya kitu kingine chochote katika tafsiri ya pili (2:4-9). Pamoja na tafsiri mbili hizi zilizotofautiana juu ya uumbaji, katika Mwanzo 1 na 2, tuweza kuona tafsiri mbili tofauti ya Mafuriko katika Mwanzo 6, 7 na 8: tunasoma tafsiri mbili tofauti kuhusu idadi ya wanyama ambao Nuh anawachukuwa kwenye Safina, tafsiri mbili tofauti za sababu ya mafuriko, na tafsiri mbili tofauti za muda gani mafuriko yalichukuwa. 2) Katika kitabu cha Mwanzo 22:2, Mungu anatoa amri ifuatayo kwa Nabii Ibrahimu: "Mchukue sasa mwanao, Is-haq mwanao wa pekee‌" Maneno "mwanao wa pekee" yanaweza kuchukuliwa kama si chochote bali ni maneno yaliyotomwa kwa vile Ibrahim alikwa na watoto WAWILI wa kiume wakati ule--Ishaq na kaka yake mkubwa Ismail--sio mmoja tu. 3) Na kama Nabii Musa anachukuliwa kama mwaandishi wa kitabu cha kumbukumbu la Torati, inawezekanaje kwamba angeweza kuandika habari juu ya kifo chake mwenyewe kama inavyoonekana katika kumbukumbu la Torati kifungu cha 34? Pia kuna suala juu ya jinsi Mungu anavyoonyeshwa katika Agano la kale kuwa ni katili na asiyekuwa na huruma hata kidogo: 1) Katika kitabu cha Hesabu 21:5-6, wakati Mungu alipeleka nyoka wenye


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 46

46

sumu kali kwa Wayahudi ambapo wetu wengi waliumwa na kufa kwa sababu tu walilalamika juu ya chakula chao. 2) Katika kumbukumbu la Torati 7:2, wakati Mungu anawaambia Wayahudi kwamba wawaue watu wote watakaowakamata kama mateka katika vita -- wasionyeshe huruma hata kidogo. 3) Katika Samuel; II, 24:1-7, wakati Wayahudi 70,000 walipokufa kutokana na tauni iliyoletwa na Mungu kwa sababu ya kutoridhishwa Kwake na sensa iliyofanywa na Daudi. Pamoja na nyongeza kwenye maelezo ya Mungu yasiyofaa, kuna mifano mingi ya kashifa na ya kutweza ya mitume mbalimbali wa Mungu: 1) Mabinti wa Luti walimnywesha pombe baba yao ili waweze kufanya naye mapenzi katika kitabu cha Mwanzo 19:30-38. 2) Inasemekana kwamba Daudi alikuwa mzinifu katika Samwel II, 11:4-5. 3) Inasemekana Suleimani alikuwa muabudu masanamu katika Wafalme II 11:9-10. Ndiyo, ni muhimu kwa sisi kujua kwamba Mitume hawa wa mwanzo walikuwa ni wanadamu katika nyanja zote, lakini kusema mambo ya kutweza kama hayo, kama mifano iliyooneshwa hapo juu, ni kwenda mbali ZAIDI. Hii sio mwisho. Katika vitabu vya Samueli, Wafalme na Mambo ya Nyakati hurudia maelezo mengi ya matukio hayo hayo ambayo yalitokea katika historia ya mwanzo ya Kiyahudi, lakini pia ndani yake kuna idadi kubwa ya migongano kati yao katika kushughulikia kwao matukio yaliyotajwa. Kitabu cha Isaya, kitabu kinachopendelewa sana cha "utabiri" kwa Wakristo, kinazo sifa za mifano inayoonekana zaidi ya uharibifu katika Agano la Kale, ile ya kuiba wazi wazi maandishi: tazama Isaya 37, ambapo takribani ni nakala halisi ya juhudi ya mwanzo iliyofanywa na mwandishi


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 47

UJUMBE WA YESU

47

wa Bibilia ambayo inayopatikana katika Wafalme II, 19. Hii ni mifano michache tu katika mingi ambayo inayoweza kupatikana ndani ya kurasa za Agano la Kale kuthibitisha tuhuma kwamba maandiko yameharibiwa. Itakuwa vigumu kufikiria vinginevyo, tukichukulia mifano mingi mno inayothibitisha tuhuma hizi, tukiachilia ukweli kwamba hakuna miswada ya asili ya Agano la Kale ambayo inapatikana leo. Uchunguzi Juu Ya Agano Jipya Ambapo Agano la kale lina umuhimu mkubwa sana kwa Wayahudi, kwa Wakristo halina nafasi muhimu kiasi hicho, ambapo wao wanaliona kama mkusanyiko wa ushuhuda wa utabiri wa ujio wa Yesu. Amri na mafundisho yake hayana usahihi halisi kwao tena. Mapenzi yao yamehifadhiwa kwenye Agano Jipya. Vitabu hivi 27 hujumuisha kwa kawaida maandiko ya Paulo; vitabu hivi-pamoja na Injili nne—ambazo hakuziandika yeye, hata hivyo huunga mkono fikra ambazo alizianzisha. Kwa hali ilivyo, ni “kazi” ya moja kwa moja ya Paulo. Baada ya kufanya uchunguzi katika vitabu vyote viwili, Biblia na Qur’ani, Dr. Maurice Bucaille anasema kwamba: "… kuzisoma injili kikamilifu kuna uwezekano wa kuwasumbua Wakristo sana.” 17 Ametoa maelezo haya kwa sababu, kwa mujibu wa utafiti wake, migongano, mikorogano, ukinzani na mabadiliko ya maandiko “…vinaongezea kwenye ukweli kwamba vitabu vya Injili vina sura na vifungu ambavyo ni matokeo ya mawazo ya mwanadamu tu. 18 17 The Bible, The Qur’an and Science, uk. 44 18 Ibid, uk. 109


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 48

UJUMBE WA YESU

48

Mifano mbalimbali juu ya migongano katika vitabu vya Injili ni: 1) Injili ya Mathayo ina mtiririko wa kizazi cha Yesu (Mathayo 1:7) ambao unamuonyesha kutoka kwa Ibrahimu hadi kwa Suleiman, mtoto wa Daud, ambapo mtiririko wa kizazi hiki katika Injili ya Luka (3:31) unamuonyesha Yesu kutoka kwa Adam kupitia kwa Nathan, mtoto mwingine kabisa wa Daud. Na hata uchunguzi wa juu juu utaonesha majina ambayo yamo katika maelezo ya Mathayo hayawiani na yale ambayo yako katika Luka, na vivyo hivyo. Nukta ya kuzingatia hapa ni kwamba kujumuisha aina YOYOTE ya mtiririko wa kizazi cha kiume cha Yesu kwa kupitia kwa Yosefu ni jambo lisiloingia akilini, kwa vile Yesu hakuwa na baba wa kibailojia. Ukoo sahihi unaweza kuwa ni ule unaopitia kwa mama yake, Mariam - sio kwa Yosefu (Yusuf). 2) Injili ya Yohana inakhitilafiana na Injili nyingine tatu takribani katika KILA sura ya maisha ya Yesu na ujumbe wake kama vile sehemu alipozaliwa na kukua, ubatizo wake, na hata sehemu na muda wa ujumbe wake. Inasemekana kwa kweli kwamba 92% ya maelezo katika injili ya Yohana hayamo kabisa katika zile injili nyingine tatu.19 Moja ya tofauti inayovutia zaidi kati ya injili ya Yohana na zile nyingine tatu ni kwamba Yohana hasemi lolote juu ya Komunio Takatifu (chakula cha Bwana yaani mkate na divai). Katika maelezo ya Yohana juu ya Karamu (chakula) ya Mwisho, inayopatikana katika vifungu vya 13-17, Yesu anaosha miguu ya wanafunzi wake na kisha anatoa hotuba ndefu (ambapo sasa inachukuliwa kama yenye kutatanisha) kuhusu Mfariji atakaye kuja baada yake. Hakuna utajo hata kidogo katika sura hizi juu ya komunio takatifu ya mkate na divai ambayo ni tegemeo kuu katika Ukristo leo. 3) Si Mathayo wala Yohana wanazungumza juu ya kupaa kwa Yesu. 19 All Scripture Is Inspired of God and Beneficial, uk. 195


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 49

UJUMBE WA YESU

49

Ambapo Luka anaongea juu ya hili katika Injili yake na pia katika kitabu chake kingine alichoandika kiitwacho Matendo ya Mitume, wakati na mahali hutofautiana katika maelezo yote. Marko pia anazungumzia juu ya kupaa kwa Yesu, lakini sasa wanachuoni wa Biblia wanakubali kwamba taarifa yote juu ya tukio hili kama ilivyoandikwa katika injili ya Marko "sio sahihi" (angalia sehemu ya mbele juu ya tafsir ya Bibilia). Katika namna ya "mafundisho yasiyowiana", tunaangalia katika itikadi ya Ukristo ya kafara (yaani kwamba Yesu aliteswa na kuuawa ili awe kafara ya dhambi za wanadamu), ambayo imejengwa juu ya kanuni ya kwamba Yesu alikuwa kiumbe mkamilifu katika kila hali. Mtu anaweza kushangaa tu, katika mwanga ule, Wakristo wanazithibitisha nukuu mbalimbali katika injili kwa Yesu kwamba sio mtu kamilifu kiasi hicho, baadhi yake ni hizi zifuatazo: 1) Katika Mathayo 16:23, Yesu anamwita Petro "Shetani" na "mtego wa hatari". Wakati Petro anapojaribu kumkinga. 2) Katika marko 11, Yesu anaulaani mti wa mzaituni kwa sababu tu haukuwa na matunda nje ya msimu wake wakati alipokuwa na njaa. 3) Katika Yohana 2:1- 4, Yesu anaonyesha kukosa adabu kabisa kwa mama yake. Katika Mathayo 28:19, Yesu anawaambia wanafunzi wake waende wakawabatize watu kwa jina la Baba na Mwana na Roho Matakatifu. Kwamba maneno haya tisa huwezekana kabisa ni nyongeza kwenye maandiko huweza kuoneka kwa kusoma kwa urahisi barua za Paulo: husema kwazo kwamba ubatizo katika kanisa la mwanzo ulifanywa katika jina la Yesu peke yake. Inavutia kuona kwamba katika Marko, 16:15 Yesu anasema: "Enendeni ulimwenguni kote, mkahubiri injili kwa watu wote."


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 50

50

Marko anazungumzia tukio hilo hilo katika 16:15 kama Mathayo katika 28:19; ni wapi haswa yametoka maneno yale ya ziada ambayo tunayaona katika maelezo ya Mathayo? Yesu Katika Injili Kama ilivyotajwa mwanzo, Agano Jipya -- hususan Injili -- lina nafasi maalumu kwa Wakristo. Wanavichukulia vitabu hivi vinne kama mwongozo, na kwa sababu nzuri: Injili iliandikwa NA Wakristo KWA ajili ya Wakristo. Katika injili nne, Yesu wa kihistoria amewekwa pembeni kwa faida ya Yesu “aliyefanywa” Mkristo. Waandishi wa injili wenyewe bado hawajulikani. Ingawa hakuna uhakika ni nani aliyeziandika, wanazuoni wengi wa Biblia wanakubaliana kwamba Mathayo na Marko hawakuwa waandishi wa injili ambazo zina majina yao. Injili kwa mujibu wa Luka inadhaniwa kuwa iliandikwa na rafiki wa Paulo mtu wa mataifa ambaye hakuwahi hata kumuona Yesu; ni sehemu ya kwanza ya maandiko yake juu ya Ukristo wa Mwanzo ambayo vile vile inajumuisha kitabu cha Matendo ya Mitume. ambapo wakristo wengi wanasema kwamba injili ya Yohana iliandikwa na mwanafunzi wa Yesu aliyekuwa na jina kama hili, wanazuoni wa Biblia sasa wanalihoji hili katika mwanga wa ukweli kwamba kitabu hiki kiliandikwa mwaka 100 Baada ya kristo, na Yohana, mwanafunzi wa Yesu, alikufa shahidi mwaka 70 Baada ya kristo -- miaka 30 kabla. Katika kuikubali nadharia hii kwamba watu wengine tofauti na wanafunzi wa Yesu waliandika vitabu vinne vya injili, lazima pia ikubalike kwamba waandishi hawa inawezekana kwamba hawakuwa mashahidi wa macho -au hata kwa ushahidi wa kusikia kwa mengi -- kama si kwa wote -- ya matukio waliyoyaandika. Hata kama mtu atapenda kung’ang’ania kwenye wazo kwamba wanafunzi wa Yesu walisaidia kuziandika injili, tunaelewa kwamba hawakushuhudia matukio yaliyotokea pindi Yesu alipochukuliwa


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 51

51

na maaskari kutoka katika Bustani ya Gethsemane kwa sababu tunasoma: "...kisha wanafunzi wote walimuacha wakakimbia …", katika injili zote mbili Mathayo 26:56 na katika Marko 14:50. Kwa kifupi, mengi tunayoyaona katika injili yameegemezwa juu ushahidi wa kusikia -- nia sio maandishi ya watu ambao kwa hakika walishuhudia matukio yaliyotajwa. Nukta nyingine ya kuchukuliwa maanani kuhusu Injili ni kwamba hakuna hata moja iliyoandikwa wakati wa Yesu, kwa vile hakuna kumbukumbu iliyohifadhiwa kuhusu kazi zake katika wakati wa uhai wake. Kwa hakika, karibu miaka arobaini ilipita kati ya kipindi wakati Yesu alipoondoka duniani na kitabu cha kwanza cha injili kilipodhihiri. Mwishowe wakati injili ya Marko ilipotoka, Paulo alikuwa ameshaanza kuhubiri kwa takriban miaka ishirini; na alikuwa tayari ameshaandika waraka wake kwa Warumi, ambao humo aliweka itikadi zake zote kwa ajili ya Ukristo. Katika mwanga huu, tunaweza kuona kwamba mafundisho ya Paulo, bila shaka yaliwavutia waandishi wa injili kwa kiwango kikubwa. Injili zote ziliandikwa kati ya miaka 70 B.K. na 100 B.K., ya Marko ikija ya kwanza; ikifuatiwa na ya Mathayo, Luka na Yohana. Injili tatu za mwanzo kwa ujumla zinafanana; kwa hakika, uchunguzi wa juu juu utaonyesha kwamba waandishi wa injili zote za Mathayo na Luka waliazima kwa wingi mno kutoka kwa Marko walipokuwa wanaandika injili zao. Hii ndio sababu injili hizi tatu zinaonekana kuelezea “vidokezo” vya Injili. Injili ya Yohana inatofautiana sana na injili zingine tatu hata hivyo, na ni moja ambayo bado inachochea migongano kwa sababu tu mwandishi wake alijihusisha zaidi na umuhimu wa Yesu kwa ajili ya imani ya Ukristo kuliko yale yaliyosemwa na kufanywa na Yesu. Kwa hiyo, tunaweza kwa hoja kuhitimisha, kwamba kwa sababu ya hali ya muda, kuandika kutokana na ushahidi wa kusikia, na ushawishi wa Paulo, picha ya Yesu ambayo inawasilishwa kwetu katika injili si ya yule Yesu wa kihistoria; badala yake, waandishi hawa waliandika juu ya Yesu aliyetokana na hadithi za kale, kwa kutumia mtazamo wa kithiolojia ambao


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 52

52

uliufanya “Ukristo” wa ukweli wa kile kilichotokea. Waandishi walijifunga kwenye imani za Ukristo, na waliandika wakiwa na mtazamo huu akilini. Matokeo yake ni kwamba injili hizi nne zina ngano zaidi kuliko ukweli. Ujumbe wa kimungu wa Yesu, wote umepotea chini ya rundo la yale ambayo watu waliyatarajia na waliyotaka Yesu aseme na kufanya badala ya lile kwa hakika lililotokea. Nakala za Nakala Nakala zote za mwanzo za Biblia zilikuwa ni nakala tu. Nakala zote hizi ziliandikwa kwa mkono (Nakala ya kwanza kuchapwa ya Bibilia haikutoka mpaka katika karne ya kumi na tatu -- Biblia iliyoitwa "Gutenburg"); miswada ya asili ilitupiliwa mbali mapema kwa kuzipendelea nakala mpya na vile vile kwa sababu imechakaa kwa kutumika. Nakala hizi mpya baadaye, zilitumika kutengenezea nakala nyingi zaidi. Hata hivyo, kila nakala iliyotengezwa, ilimaanisha kuwepo kwa nafasi zaidi ya kufanya mabadiliko -- ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi - kuingizwa katika maandishi. Kama ilivyokuwa kwa Agano la Kale, maandisahi ya Agano Jipya pia yaliathirika kutokana na uhariri wa kimawazo, mabadiliko yasiyokusudiwa, na hila za kimakusudi za maandishi kwa upande wa waandishi. Ni lazima ionyeshwe kwamba hakukuwa na namna yoyote ya kurudi nyuma na kuangalia usahihi wa kazi za waandishi, kwa vile hakuna miswada ya asili ya ama Agano la Kale au Agano Jipya ambayo inapatikana. Nakala za zamani sana zilizopo za Agano la Kale ni za nyuma za karne ya 7 au 8 B.K., wakati ambapo maandishi yaliyosanifiwa yalitolewa kutokana na miswada yote mbalimbali -- yenyewe ni nakala za nakala -- ambazo zilipatikana wakati ule. Kwa upande wa Agano Jipya halina miswada ya asili inayopatikana, ama -- tuna nakala tu, ya mwanzo yake ambayo ni ya karne ya nne, wakati ambapo “sheria za Kanisa”, au maandishi rasimi ziliwekwa


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 53

53

na Kanisa. Ukosefu huu wa maandishi ya asili ulifuta fursa ya mtu yeyote kuchunguza usahihi wake. Mabadiliko ambayo yamepenya kwenye maandiko ya Bibilia yamebakia kwenye maandiko ya Bibilia. Suala la Kutokamilika Makanisa ya mwanzo ya Kikristo hayakuwa na seti rasmi ya maandiko Matakatifu. Baadhi ya Makanisa yalikuwa na seti moja ya vitabu, wakati mengine yalikuwa na seti tofauti. Wakati bado baadhi yao yaliridhika na kuwa na seti moja tu ya Injili, yakiendelea kuamini kwamba zote ziliongelea habari moja tu. Pia kulikuwa na vitabu katika mzunguko ambavyo mtu hawezi kuvipata katika Biblia nyingi za leo -- katika vitabu kumi na tano vya Agano la Kale, na katika vitabu kumi na sita vya Agano Jipya. Kutokana na ukosefu wa mpangilio katika Kanisa kuhusiana na maandiko yake matakatifu, Maaskofu walikutana pamoja ili kuweka sera rasmi ya Kanisa juu ya suala la utatu katika Mkutano wa Nicea mwaka 325 B.K.; na vile vile walijichukulia wenyewe kuweka rasmi “Sheria za Kanisa za maandishi� kwa ajili ya Kanisa. Walikusanya kila kitu pamoja ambavyo vilikuwa wakati ule katika mzunguko na wakafanya uamuzi wa mwisho juu ya vitakavyotumika katika Maandiko matakatifu ya Ukristo. Mwishowe, vitabu 66 vilichaguliwa--39 kwa Agano la Kale, na 27 kwa ajili ya Agano Jipya. Vitabu saba katika kumi na tano vya ziada vya Agano la Kale viliwekwa na Kanisa Katoliki, lakini hata hivi viliachwa na Waprotestanti wakati wa harakati za mageuzi ya karne ya 16. Hata hivyo, HAKUNA HATA KIMOJA katika vitabu kumi na sita vya ziada vya Agano Jipya, ambavyo vimefanywa sehemu rasmi ya Sheria za Kanisa za Maandishi. Vile ambavyo huitwa "Apocrypha" - - neno la kigiriki lenye maana ya "iliyofichika" -- vitabu hivi vya ziada ambavyo hapo awali vilikuwa sehemu ya Biblia vilitupiliwa mbali na viongozi wa Kanisa kwa sababu vilikuwa "vikitofautiana" na itikadi zinazokubaliwa na Kanisa: "Waandishi


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 54

54

wa vitabu hivi vya kiaprocrypha bila shaka walikuwa wachamungu na wafanya kazi waaminifu--na bado wakati ukisoma waliyoyaandika, mara moja utagundua kwamba maneno yao ni -- mbali sana na hadhi na uwezo wa utukufu wa Maandiko..� 20 La kushangaza zaidi, rejea kwenye baadhi ya vitabu hivi vilivyofichika zinaweza pia kupatikana katika Biblia rasmi ya leo kama vile "kitabu cha vita vya Yehova", kilichotajwa katika Hesabu 21:14, na "kitabu cha Jashar", kilichotajwa katika Joshua 10:13. Hivyo, Biblia ya leo, mbali na kuwa muathiriwa wa uharibifu wa maandishi, haiwezi pia kuchukuliwa kama iliyokamilika. Inawezekanaje Maneno ya Mungu yakaondolewa na kutupiliwa mbali kwa sababu ya haja ya mwanadamu? Tatizo la Tarjuma Wataliano wana msemo unaovutia ambao unasema kwamba "Watarjuma ni waongo." Hii sio shutuma ya uovu kiasi hicho kwa vile ni uchunguzi mkali. Kuchukua kitu fulani kilichoandikwa katika lugha fulani na kujaribu kukiingiza katika lugha nyingine ni tatizo, kwa sababu mtu mara nyingi hukutana na maneno katika lugha moja ambayo hayana ulinganifu katika lugha nyingine. Mbadala lazima ufanyike, na hatimaye maana ya misemo hubadilika. Agano la kale mwanzo kabisa liliandikwa kwa Kiebrania, lakini lilitafsiriwa katika karne ya tatu K.B. katika lugha ya Kigiriki kwa ajili ya Wayahudi waliokuwa wanaishi nje ya Palestina (na walikuwa wakiongea Kigiriki - badala ya Kiebrania katika misingi ya kawaida). Iliitwa "Septuagint", tafsiri hii ilikuwa inatumika sana hata na Wakristo wa mwanzo. Agano Jipya liliandikwa katika lugha ya Kigiriki; hata hivyo, kwa vile 20 Is the Bible Reliable? Uk. 30


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 55

55

Yesu mwenyewe aliongea lugha ya kiaramaiki, hii ina maana kwamba maneno yake baadae yalitafsiriwa na uwezekano wa makosa ulikuja kuonekana. Tafsiri ya kigiriki iliyokuwa ikiitwa Septuagint iliunganishwa na maandiko ya Agano Jipya yaliyokuwa katika lugha ya kigiriki katika karne ya nne. Maandiko haya yaliyounda Biblia kamili sasa hivi yanaeleweka kama "Codexsinaiticus" na "Codex Vaticanus" na hizi ndio nakala za maandiko ya zamani kabisa zilizopo leo. Hakuna maandiko ya mwanzo kabla ya haya yaliyonusurika. Katika karne ya nne, Biblia ilitafsiriwa kwenda katika lugha ya Kilatini na Mt. Jerome. Na hii ilibakia kuwa lugha ya Biblia hadi karne ya kumi na sita ambapo watu wa Mageuzi kama John Wycliffe, William Tyndale na Martin Luther walipoifasiri Biblia katika lugha mbalimbali za watu - jambo ambalo lilikuwa haliruhusiwi kabisa na ambalo lilimgharimu Tyndale maisha yake. Walifanya hivi kwa nia ya kuifikisha Biblia mikononi mwa watu, ambao mpaka sasa walikuwa hawajaruhusiwa kuyaona maandiko yao wenyewe. Tafsiri nyingine zilijitokeza ndani ya muda mfupi; karibu na mwisho wa karne ya kumi na sita, tafsiri nyingi na za aina mbalimbali za Biblia ambazo wakati ule zilikuwa kwenye mzunguko zilikuwa sababu ya mabishano mengi, kiasi kwamba Mfalme James 1 wa Uingereza aliteuwa kamati ya wanachuo 54 kutengeneza tafsri “yenye kuaminika�. Watu walichunguza tarjuma zote ambazo zilijulikana kwa wakati ule, na katika mwaka wa 1611, walitoa tafsri ya King James -- ambayo imekuwa ya kawaida kwa Wakristo kwa muda wa mamia ya miaka iliyofuata. Tatizo la zama hizi: Tafsri mpya Wakati ambapo madhara yaliyoambatana na tafsiri yalifikia mwisho mwaka 1611, kwa kupatikana tafsir ya King James ya Biblia, tatizo la masahihisho - - "kuiboresha" au kuifanya Biblia kuwa ya "kisasa" -kumeikabili leo hii.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 56

56

Kiwango cha madhara ya muundo huu mpya unaweza kuonekana kama ifuatavyo: katika mwaka 1952, makala yenye kichwa cha habari "Ukweli kuhusu Biblia" ilijitokeza katika gazeti la "Look". Makala haya yalisema kwamba kulikuwa na makosa zaidi ya 20,000 (elfu ishirini) katika Agano Jipya peke yake. Mashahidi wa Yehova walilizungumzia suala hili katika toleo la Septemba, 1957 la gazeti lao la "Awake" ambapo walitoa maelezo ya kipekee katika mchakato huo: "…Wafasiri walifanya makosa katika kufasiri (Biblia) ambayo yamesahihishwa na wanazuoni wa zama hizi…" 21. Na ajabu ilioje waliyonayo wanachuoni hawa katika kufanya hivyo!! Katika karne ya kumi na tisa, Wakristo waliamua kuiboresha lugha ilivyotumika katika King James Version. Jitihada yao ilizaa tafsri mpya ya Biblia iitwayo "American Standard Version” iliyotolewa mwaka 1901. Wakristo walioifanyia kazi tafsir hii, hata hivyo, sio tu kwamba waliiboresha lugha, bali pia walifanya mabadiliko katika maandiko yenyewe: 1) Kukiri kwenye utomaji wa maneno -- ukweli kwamba maneno kama hayo yalikuwa hayaonekani kwenye miswada ya zamani ya kigiriki ya Biblia ambayo ilikuwa bado ipo -- neno “Baba, Mwana na Roho Mtakatifu”, yanayoonekana katika Yohana 1; 5:8 ya tafsir ya King James yalibadilishwa na wanachuoni kwa kusoma “Roho, maji na damu.” 2) Aya nzima inayopatikana katika Mathayo 17:21 ambayo inashughulikia maendeleo ya kiroho kwa njia ya sala na kufunga yaliondolewa kwenye American Standard Version, na neno "Kufunga" liliondolewa katika aya kama hiyo inayopatikana katika Marko 9:29. Maelezo juu ya hili yanayopatikana katika tanbihi husomeka “mamlaka nyingi, baadhi zikiwa ni za zamani, zinaingiza aya 21". 3) Katika kuukubali ukweli mwingine juu ya utomaji wa maneno, Yohana 7:53 na Yohana 8:1-11 umefungiwa mabano pamoja na maelezo mengine tena kwamba “haya hayapatikani katika miswada ya zamani mno". 21 Awake! Uk. 26


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 57

UJUMBE WA YESU

57

Baada ya miaka kadhaa, viongozi wa kanisa walikutana tena na wakaamua kuboresha tafsri ya Biblia ya American Standard. Matokeo ya jitihada zao yalikuwa ni kupatikana kwa Revised Standard Version (Masahihisho ya Tafsri ya Kawaida) katika mwaka wa 1952. Katika utangulizi wa Toleo hili tunasoma yafuatayo: "...Toleo la King James (King James Version) lina makosa makubwa mno – kasoro hizi ni nyingi mno na nzito sana kiasi kwamba huhitaji masahihisho…”

Katika tafsir ya Biblia ya The Revised Standard, tunakuta kwamba aya katika injili ya Marko zinazozungumzia juu ya kupaa kwa Yesu (Marko 16: 9-20) zimeondolewa kwa sababu ilisemwa tena kwamba Aya hizi makhususi hazipatikani katika miswada ya “zamani mno”. Katika mwaka 1989, tafsir mpya ya ‘The Revised Standard Version’ ilichapishwa-- “boresho” la Revised Standard Edition ya 1952-- na aya zinazozungumzia juu ya kupaa kwa Yesu katika Marko Sura ya 16 hujitokeza tena hapa. Katika Marko 16 zilirejeshwa. Kwa vile Wakristo wengi hawakufurahia "kudhoofishwa" kwa moja ya imani zao za kimsingi kulikofanywa na Wahariri wa "The Revised Standard Version", aya hizi zirejeshwe tena katika tafsir hii. Kwa kuhitimisha: kwa kunakili miaka nenda, tarjuma na “tafsir” mpya mbali mbali, kile kinachojulikana kama Biblia sasa ni zaidi mno maandiko ya binadamu kuliko ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Kulipeleka Suala Hili Kwa Wakristo Huko nyuma katika karne ya nne, Mt. Augustino mweyewe aliona matatizo katika maandiko ya Biblia. Akizungumzia juu ya suala hili katika barua yake na. 82. Alisema kwamba upungufu wa uelewaji ulikuwa haswa ndio sababu; ilikuwa haikubaliki kwake kwamba uingiliaji wa binadamu kwenye maandiko ya Biblia ungekuwa katika kiini cha suala.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 58

58

Utafiti mkali uliofanywa wa maandiko, kinyume na watu wengi wanavyofikiria, ni wa hivi karibuni tu. Biblia ilikubalika "kama ilivyo" kwa mamia ya miaka. Ilichukuliwa kuwa ni dhambi kubwa kuonyesha hata ukosoaji mdogo sana kwayo -- na Kanisa kwa mafanikio lilinyamazisha majaribio yoyote kwayo. Mwelekeo wa kwanza katika kipengele hiki ulikuja katika mwaka wa 1678 wakati Richard Simon alipochapisha kitabu chake kiitwacho Critical History of the Old Testament (Historia inayojaribu kuonyesha na kukosoa makosa yaliyomo katika Agano la kale). Kitabu hiki kilisasbabisha kashifa, lakini vile vile kilisababisha kufungua njia kwa wengine kujitolea kwenye karne ya 18 na 19 kwa utafiti mkali wa Agano la Kale. Kukubaliana na ushahidfi wote ambao uliletwa mbele, Halmashauri ya ya Pili ya Vatican (1962- 1965) ilitoa maelezo yenye kuvutia juu ya suala hili kwa sema kwamba "…Vitabu vya Agano la Kale--vina maelezo (ndani yake) ambayo sio sahihi na yasiyo faa…” 22 wanachuoni wengine wamekuja mbele na maelezo ambayo yako kinyume kabisa na msimamo wa Vatican: …katika kitabu chake The Call Of The Minaret, (mwito wa mnara) Dr. Kenneth Cragg anasema kwamba kuna “ufupisho na uhariri” katika Agano Jipya; Injili imekuja “kupitia akili ya Kanisa nyuma ya waandishi” na kwamba kwayo “yanawasilisha uzoefu na historia”.23 limepatwa na mashambulizi. Ingawa Halmashauri ya pili ya Vatican inashikilia kwamba Injili "kihistoria ni sahihi” na kwamba "kwa uaminifu kabisa huwasilisha” yale ambayo “kwa hakika Yesu aliyofanya na kufundisha watu wakati wa maisha yake miongoni mwa watu", 24 Wanazuoni wengine wamekuwa na maelezo ambayo ni kinyume kabisa na msimamo wa Vatican.

22 The Bible, The Qur’an And Science. Uk. 41 23 Ibid uk. 57 24 Is the Bible God”s Word? uk. 1,2.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 59

UJUMBE WA YESU

59

Katika kitabu chake "The Call of the Minaret" (Wito kutoka katika mnara wa msikiti, Adhana), Dr. Kenneth Cragg anasema kwamba kuna "mambo yaliyoongezwa na kupunguzwa" katika Agano Jipya Injili na ni kazi ya akili ya viongozi wa kanisa ikiongozwa na waandishi, na kwamba katika kazi zao wanatumia uzoefu na historia."25 Padre Kannengiesser, Profesa katika taasisi ya kikatoliki katika mji wa Paris, alionya katika kitabu chake "Faith in Resurrection", (Imani juu ya ufufuo), kwamba mtu “asiuchukulie neno kwa neno” ukweli uliotaarifiwa kwenye Injili… onyo ambalo pia lilitolewa na Padre Rognet wa Paris katika kitabu chake "Initiation to the Gospels". Carl Andrey, profesa wa falsafa na masomo ya dini katika Chuo kikuu cha Ball State kilichopo Indiana anasema kwamba vitabu vinne vya Injili: "… viliandikwa na watu wenye shauku wa harakati za mwanzo za kikristo” na kwamba… “wanatupatia upande mmoja tu wa habari na kwa kiwango kikubwa ni matokeo ya dhana za waandishi hao" 26 Mwishowe, tuna maelezo ya Dr. W. Graham Scroggie wa "Prestigious Moody Bible Institute" ambaye anasema: "Ndiyo, Biblia ni ya binadamu … vitabu hivyo vimetokana na akili za watu, vimeandikwa kwa lugha ya binadamu, viliandikwa na kalamu za binadamu, na vinabeba katika mtindo wake tabia za kibinadamu. 27 Huu ni msimamo wa wanazuoni wa Biblia; nini, hata hivyo, mkristo wa “kawaida" angesema juu ya jambo hili? 25 Jesus and the Four Gospels, uk. 6,7. 26 Is the Bible God’s Word? uk. 1 27 Personal Communication, Del Kingsriter Of Centre for Ministry to Muslim, March 3,1993


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 60

60

Wengi hata hawajui nukta hii kwa sababu waandishi wa dibaji na tafsir ya Biblia ya leo hutumia mbinu za kimaandishi ambazo zimebuniwa makhususi kujiepusha na maswali ambayo Mkristo angekuwa nayo kuhusu ukinzani ndani ya Biblia. Miongoni mwa mambo mengine, waandishi hawa: 1) Huwasilisha kama ukweli yale ambayo bado huonekana kama yasiyo na uhakika, na 2) Hufunika matatizo kwenye maandiko pamoja na utetezi--chombo cha maandishi cha kujihami, hiyo husaidia kuvuta nadhari ya msomaji kwenye kitu mbali na maandiko yanayohusika. Umbali ambao wafasir hawa wanakwenda ni ushahidi wa kutosha juu ya wasiwasi unao wakabili kuhusiana na makosa ya Kibiblia. Kama wakibanwa juu ya jambo la kuelezea makosa kwenye Biblia, athari ya mfano haswa wa Mkristo ni ile ya uhasama. Niliwasilisha mswada wa utafiti wangu juu ya uharibifu wa Biblia kwa mhubiri wa Kikristo ambaye alirudi kwangu baada ya muda mfupi, akinilaumu kwa “kuishambulia” Biblia. Aliendelea kusema kwamba “…Biblia imeshambuliwa kwa karne nyingi, lakini bado ipo. Imekuwa imara kutokana na uchambuzi wa ndani na nje.”28 Nastaajabu vipi mtu anaweza kung’ang’ania kwenye mwelekeo kama huo mbele ya mifano mingi iliyothibitishwa; na ningevutiwa kuona kipi kinachojiri kwa ajili ya “uchambuzi” pamoja naye. Pengine huenda sambamba na msitari wa kile kinachoonekana katika “kazi bora ya maandiko” ya uteteaji wa Mkiristo yenye anwani: “Is the Bible Reliable?” (Je, Bibilia inaaminika?). Katika kitabu hiki, mwandishi Bjug Horstal anasema kwamba Mungu "aliwashawishi" waandishi wa Maandiko Matakatifu "- - kuandika kasoro na dosari zilizoambatana (zinazotokana) na lugha,” na kwamba yatupasa “...tuliache jambo hili kwa Mungu ili achukue mitindo 28 Is the Bible Reliable? Uk. 86, 87


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 61

61

mingi na hata udhaifu wa kibinadamu kama anavyotaka mwenyewe - - -"29 Mashahidi wa Yehova wameandika kitabu kizima kiitwacho: “Bible: God's Word or Man's?” (Biblia: Ni neno la Mungu au la Mwanaadamu?), ambacho kinazungumzia kasoro na dosari zilizomo ndani ya Biblia. Katika kitabu hiki, wamelizungumzia suala hili kwa mtindo mwingine wa pekee kwa kusema kwamba, wakati ambapo kuna baadhi ya "kasoro na dosari za wazi" katika Biblia ambazo "ni vigumu kuzipatanisha", hatupaswi kufikiria kwamba dosari na kasoro hizi kuwa ni kugongana na kupingana kwa aya za Biblia; mara nyingi ni “…kwa sababu ya ukosefu wa taarifa na habari kamili”.30 Nilibahatika kupata nakala ya tafsiri ya Biblia ya Mashahidi wa Yehova "The New World Translation of the Holy Scriptures". Nilimuuliza mjumbe mmoja wa ngazi za juu wa jopo la Wafasiri wa mjini kwetu kuwa ana maelezo gani juu ya aya ya Mathayo 17:21, ambayo inasomeka: “21----” Hakuna aya; kuna namba tu, mstari mrefu na nafasi ya wazi". Mjumbe yule alibabaika sana alipoangalia sehemu hiyo. Akaahidi kuwa angekuja kuniona; sijamsikia tena akizungmzia juu ya suala hili. Kwa kifupi, Wakristo hawako tayari kuukubali ukweli kwamba Maandiko yao Matakatifu yamepotolewa kwa madai kwamba, ikiwa msingi utayumba na kutokuwa na uhakika, je tutasimama juu ya nini katika siku za mateso?"31 Sio hayo tu, bali kuna “suala dogo” ambalo kwamba linahusiana na ubadilishaji wa maandiko Matakatifu katika maandiko Matakatifu yenyewe. “- - - ikiwa mtu yeyote ataongeza (au kufuta) neno lolote katika kitabu hiki, Mungu atamuongezea balaa zilizoandikwa katika kitabu hiki". 29 Personal communication, Del Kingsriter of Center for Ministry to Muslims, March 3, 1993.

30 Is the Bible reliable? uk. 86-87. 31 Is the Bible reliable? Uk.84.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 62

62

(Ufunuo 22:18, 19) Ushahidi uko hapo, kwa hali yoyote, wazi na rahisi kwa watu wote kuuona; ambapo Mungu huenda alimsukuma mtu kwa ilham (aina fulani ya ufunuo) ambaye ameandika vitabu vya Biblia, hakuna shaka kwamba mwanadamu amecheza mchezo (ameingilia na kubadilisha mambo mengi). Na kwa mara nyingine tena, swali muhimu sana lazima aulizwe Mkristo: Inawezekanaje kwa neno la Mungu kubadilishwa, kuondolewa na hata kutupiliwa mbali kwa matakwa ya mwanadamu?? Msimamo wa Uislamu Suala zima la wanadamu kubadilisha maneno (ufunuo) wa Mwenyezi Mungu ndio ilikuwa sababu ya Mtume Muhammad (saww) kuteremshiwa Qur’ani: Ufunuo wa mwisho kwa Mjumbe wa Mwisho wa Mwenyezi Mungu. Qur’ani katika aya zake kadhaa inazungumzia juu ya kubadilishwa, kupunguzwa na hata kuondolewa kwa baadhi ya mambo katika Maandiko Matakatifu yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu kabla ya Qur’ani. Baadhi ya aya ni kama vile. "…Walioruka mipaka (ya Mwenyezi Mungu) walibadilisha maneno kutoka katika yale waliyoteremshiwa". (Qur’ani; 2:59) "Kundi moja miongoni mwao lilisikia Maneno ya Mwenyezi Mungu kisha likayabadili baada ya kuwa limeyaelewa (maneno hayo)". (Qur’ani; 2:75) "Kuna sehemu (kundi) miongoni mwao ambao wanapotosha (wanakibadilisha) Kitabu (cha Mwenyezi Mungu) kwa ndimi zao pindi wanaposoma ili ufikiri kuwa ni sehemu ya kitabu (cha Mwenyezi Mungu). Lakini sio sehemu ya kitabu; na wanasema: Hayo yametoka kwa Mwenyezi Mungu lakini sio --". (Qur’ani; 3:78)


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 63

63

Aya hizi zinaonyesha ukweli mwingine kwamba, japokuwa Waislamu wametakiwa kuamini ufunuo ulioteremshwa kabla ya Qur’ani, imani juu ya vitabu hivi - - Taurati, Zaburi na Injili--inamaanisha imani juu ya ufunuo ASILIA ulioteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu; hakika sio yale tunayoyakuta katika Biblia zetu za leo, wala hata katika maandiko ya Mayahudi na Wakiristo ambayo yalikuwepo katika zama za Nabii Muhammad (s.a.w.w.). Imani ya Waislamu ni kwamba Qur’ani ililetwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili kuyasahihisha na kuondoa mambo yote yaliyoongezwa na kuyarejesha yale yaliyoondolewa kwa makusudi na wanadamu katika ufunuo wake wa awali. Mwenyezi Mungu aliweka wazi kwamba huu, Ufunuo wake wa Mwisho, hautapatwa na masaibu na balaa la kupotolewa (kubadilishwa) kama vitabu vilivyotangulia: "Bila shaka, Tumeiteremsha Qur’ani, na bila shaka sisi ndio tutakaoilinda kutokana na kupotolewa". (Qur’ani; 15:9) Juu ya hili, Qur’ani inasimama imara. Imebakia katika hali yake ya asili kama ilivyokuwa wakati ilipoteremshwa kwa Mtume Muhammad (saww). Na bado kuna miswada ya asili mjini Madina, Arabia, ni nakala ya Qur’ani iliyoandikwa katika karne ya saba; hii ni miongoni mwa nakala za mwanzo kabisa zinazoeleweka tulizonazo leo hii, na iliandikwa kwa mkono juu ya ngozi ya mnyama jamii ya swala miaka michache baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad (saww). Nakala nyingine iliyoandikwa katika karne ya saba iliyoandikwa katika zama za Khalifa wa tatu, Uthman, ipo katika jumba la makumbusho la Topkapi, Istanbul, Uturuki. Ikiwa mtu atachukua Qur’ani iliyo katika lugha ya kiarabu kisha akajaribu kulinganisha na nakala hizi zilizoandikwa katika karne ya saba hatakuta tofauti (khitilafu) yoyote. Qur’ani iliyo katika lugha ya kiarabu haijabadilishwa, kupunguzwa wala kuongezwa lolote licha ya kupita miaka zaidi ya 1400. Kutokana na hili, hakuna uthibitisho bora kuliko huu kwa ajili ya amri ya ki-Qur’ani kwam-


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 64

UJUMBE WA YESU

64

ba Mungu ametekeleza ahadi Yake kuulinda ufunuo Wake huu wa Mwisho. Ama kuhusu wanadamu kuyabadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu, Qur’ani inasema: "Na wasomee na uwafundishe yale yaliyoteremshwa kwako katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, hakuna atakayeweza kuyabadili Maneno yake na hamtapata msaidizi mwingine yeyote badala Yake (Mwenyezi Mungu)". (Qur’ani; 18:27)

IMANI HALISI YA KUAMINI MUNGU MMOJA IMEHUISHWA Wakati Mayahudi walipoendelea kumkataa Yesu pamoja na ukweli kwamba alikuwa ni mmoja wao, na pamoja na uwezo wa kazi yake, aliwaambia kwamba agano ambalo Mungu amefanya pamoja nao litafutwa kwa kukabiliwa na ukaidi na ukichwa ngumu wao: "Kwa hiyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na litapewa taifa jingine lenye kuzaa matunda". (Mathayo 21:43) Wafuasi wa Yesu kwa shauku waling’ang’ania juu ya hili wenyewe wakijiona ni "Watu wateule" wapya wa Mungu. Ukristo unaendelea Kupotea Kutoka katika Njia Iliyonyooka. Hata hivyo mpaka kufikia karne ya nne, Ukristo ulikuwa umejiimarisha vizuri kama dini, itikadi zake zilipangwa vizuri hasa kwa vile ilikuwa ndio Sheria ya Maandiko kwa wafuasi wake. Kama tulivyoona hapo awali, mafundisho sahihi ya Yesu yalikuwa yamesahauliwa na badala yake yakafuatwa mafundisho ya Paulo wa Tarsus. Imani na mila za kipagani ziliingizwa katika Ukristo na Paulo, ili apate


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 65

65

wafuasi miongoni mwa watu wa mataifa waliokuwa wapagani wa zama zake, imani na misingi yote ya Kikristo imetokana na upagani. Kwa kadri wapagani walivyokuwa wakiingia katika Ukristo kwa wingi zaidi, ndivyo imani zaidi za kipagani zilivyokuwa zikiingia zaidi katika Ukristo. Sikukuu za kipagani zilihamishiwa katika Ukristo: Siku ya kuzaliwa mungu wa wapagani (sanamu) aliyeitwa Mithras ambayo ilikuwa tarehe 25 Desemba (mwezi wa 12). Ilifanywa kuwa ndiyo siku ya kuzaliwa Yesu, ambapo pia vitendo vya ibada hii ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu vilichukuliwa kutoka kwenye vitendo vya sherehe za Warumi za kusherehekea kuzaliwa Saturn. Sherehe hizi zilifahamika kwa jina na Saturnalia. Sikukuu ya wafu (wa kipagani) ilifanywa kuwa ni siku ya watakatifu wote; siku iliyotengwa kwa ajili ya kusherehekea kufufuka kwa mungu wa kisanamu aliyeitwa Attis, ilifanywa kuwa ndio siku ya kufufuka kwa Yesu, ambayo pia vitendo vingi vya sherehe hii vilichukuliwa pia kutoka kwenye upagani kwa madhumuni yale yale. Sabato ya Wayahudi, iliyopangwa na Mungu kuwa iwe siku ya saba ya wiki katika sheria ya Musa, ilibadilishwa na Ukristo na kufanywa kuwa ni siku ya kwanza (yaani badala ya Jumamosi kuwa siku ya saba ilifanywa kuwa ni siku ya kwanza). Jumapili ikafanywa kuwa ndio siku aliyofufuka Yesu, lakini lazima ikumbukwe kwamba Jumapili ilikuwa ni siku ambayo Mungu wa kisanamu, Mithras, "aliliteka jua". Dhana ya ukristo juu ya masuala ya ngono (sexuality) na ndoa iliathiriwa sana na mila za kipagani zilizokuwa katika dini na falsafa za kipagani za "Neoplatonism", Stoicism na Gnosticism (utawa). Dini zote hizi ziliamini kuwa kujamiiana (ngono) hata ndani ya ndoa ni jambo ovu sana, na kwamba kutooa na kutoelewa ni sifa kubwa na nzuri sana ambazo kila mtu inambidi ajitahidi kuzipata. Ukristo kwa moyo mkunjufu uliyachukua mawazo haya na hivyo kumuweka mwanadamu na familia kwa ujumla katika hali isiyokuwa ya asili yake na ambayo ni tofauti na maumbile yake na ambayo kamwe Mungu hakuamrisha hivyo.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 66

66

Vitendo vya ibada na imani za kipagani zilizoingizwa katika ukristo zilikuwa zinawakera na kuwapa taklifu kubwa wamishenari wa kikristo wa mwanzo, hasa kwa vile mila na tamaduni hizi zilikuwa zimeimarika mno ambapo kwamba ilikuwa haiwezekani kuziondoa kwa namna yoyote ile. Katika mwaka 598 B.K., Papa Gregory, the Great (mkuu), aliwasaidia mapadri kwa kuwaambia kwamba wanatakiwa kuwaruhusu watu kufuata mila na imani zao za zamani, isipokuwa tu hili linatakiwa "likusudiwe" katika "kumsifu" Mungu. Kwa hiyo watu waliendelea na imani zao katika uchawi, kurogana, mizuka, n.k. kwa vile mapadri waliwaambia kuwa udanganyifu huu ulikuwa ni "kudhihirika" kwa shetani. Watakatifu na "warithi wa watakatifu" walihimizwa zaidi, kwa vile wao waliaminiwa kuwa na nguvu za kumfukuza shetani. Ukristo, ukiwa umeelemewa na idadi kubwa ya imani na desturi za kipagani pamoja na kumtambua Yesu -- badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ndio kiini cha imani yao; ilikuwa ni fujo tu, ya wazi isiyo na lolote. Haja ya Mtume Mwingine Wayahudi walipotea katika vitabu vyao vya sheria; Wakristo walipotea kutokana na kumfanya kwao Yesu kuwa ni Mungu. Mwenyezi Mungu aliamua kumpa mwanadamu nafasi moja ya mwisho ili kuirejesha na kuihuisha imani halisi ya kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja tu asiyekuwa na mshirika. Nabii Ibrahim, kama ilivyodokezwa katika sura ya kwanza alikuwa na watoto wawili wa kiume Is’haq na Ismail ambaye ndiye aliyekuwa mkubwa kwa Is’haq. Mungu alipoweka agano lake na Ibrahim kuhusiana na Is’haq, alikuwa pia na maneno ya kuzungumzia juu ya Ismail: “Na kuhusiana na Ismail, Nimekusikia: Tazama Nimembariki, (nitamzidisha) nitauzidisha uzao wake; atazaa Maseyyid kumi na wawili na Nitamfanya kuwa taifa kubwa". (Mwanzo 17:20). Agano Lililofanywa kwa Ismail Limetimia


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 67

67

Ismail na mama yake walikaa Uarabuni ambapo waliishi na kuendelea, kwa kadri miaka ilivyokwenda, ndivyo walivyozidi kuwa taifa kubwa lililokuwa limebashiriwa na Mwenyezi Mungu. Katika mwaka 610 B.K. ahadi ya Mungu ya kukibariki kizazi chake (Ismail) ilitimia, wakati mmoja wa kizazi chake, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 40 aliyeitwa Muhammad (saww) alipoitwa na Mwenyezi Mungu ili kuleta ujumbe wake kwa wanadamu wote. Agano ambalo Mungu aliweka na Ibrahim sasa lilikuwa limekamilika, na uimarishaji wa imani halisi ya kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja asiyekuwa na mshirika -- Uislamu, au kujisalimisha na kujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu Mmoja -- ulikuwa katika njia yake ya kubadilika kutoka kwenye ndoto kuwa kweli. Kwa hakika baraka alizopewa Ismail zilikuwa kubwa kabisa kwani Mtume Muhammad alishuhudia katika kipindi cha maisha yake Uislamu thabiti kabisa ukisimama na kuimarika, na aliuleta ujumbe wa Mwenyezi Mungu katika mfumo ambao umeuwezesha kubakia bila kuharibiwa wala kubadilishwa hadi leo hii. Misingi ya Uislamu ni misingi ya kweli ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja asiyekuwa na mshirika: Ibada ya Mwenyezi Mungu na Mungu peke yake, na utii wa sheria yake. Kwa mara nyingine imani ya kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja ilirejeshwa na kuimarishwa.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 68

68

UKRISTO NA UISLAMU Wakristo wanaonekana kuwa na vitendo vya kushangaza, hususan wakati inapokuja kwenye suala la dini nyingine. Takriban bila tofauti yoyote, Mkristo anaamini kwamba Ukristo ni dini pekee ya kweli. Dini ya Uyahudi ilikuja zamani kabla ya Ukristo, lakini kwa Mkristo, ilikuwa ni matayarisho tu kwa ajili ya imani ya Ukristo. Kwa namna yake ya kufikiri, Mungu aliwafanya Wayahudi kuwa ni watu wake wateule. Kwa hadhi hii waliyopewa Wayahudi, ilimaanisha kwamba ni wao tu (Wayahudi) waliotengwa na Mungu kwa ajili ya kuteremshia ufunuo na kupata Mitume wa Mungu kutoka miongoni mwao. Kwa hiyo Wakristo wanahisi kwamba wanaweza kuwaamini tu mitume Waisraeli, na kwamba wengine wote ni walaghai. Uislamu unawaletea Wakristo suala jingine kwa ajili ya mjadala. Mara tu baada ya kuanza kuenea kwa kasi ya Uislam muda mfupi baada ya kuondoka duniani Mtukufu Mtume Muhammad (saww), Wakristo walianza kueneza habari kwamba mtu mmoja kutoka Uarabuni kwa hakika alikuwa na ujasiri wa kwenda na kuzunguka maeneo mbalimbali akidai kwamba yeye ni Mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Licha ya Uislam kusisitiza kwamba ingekuwa kinyume na busara na uadilifu wa Mwenyezi Mungu kuteremsha Mitume kutoka katika taifa moja tu, lakini bado wakristo hawakutaka kusikia. Mtume Muhammad hakuwa Myahudi, kwa hiyo mbele ya macho yao, alikuwa ni Mtume wa uongo aliyekuja na ushuhuda wa uongo kutoka kwa mungu wa uongo. Awali, mashambulizi ya Wakristo dhidi ya Uislam yalikuwa ni manung'uniko madogo madogo. Baada ya Khalifa wa Ukoo wa Fatimid aliyeitwa Hakim kuyavunja makaburi ya Wakristo Jerusalem katika mwaka 1010, manung'uniko yalibadilika na kuwa ngurumo za simba. Wazungu Ulaya


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 69

69

walianza kuishi kwa hofu kubwa ya kuvamiwa na Waislamu, na hii ilikuwa ni sababu ndogo iliyoamsha chuki iliyokuwa imerundikana kwa muda mrefu. Papa Urban II alipoitisha vita vitakatifu "Crusades" mnamo mwaka 1095 ili kuikomboa Ardhi Takatifu kutoka kwa "makafiri", kampeni ya chuki dhidi ya Uislam ilianza kwa kasi ya roketi, ambapo ilifikia kilele chake katika karne ya kumi na mbili. Katika mashambulizi yao ya maneno dhidi ya Uislam; mambo mengi maovu ya aibu na ya uongo yalipakwa rangi ya ukweli na wale waliodaiwa kuwa ni "wasomi na wanazuoni" wa wakati ule na yakasambazwa kwa wingi kwa karibu watu wote. Mtume Muhammad (saww) alichukuliwa kuwa ni adui wa Kristo, Mtume wa uongo, mwenye kujifaharisha na kujisifia sana, mtawala wa kimabavu, mwenye tamaa nyingi za kimwili, na mengine mengi. Qur’ani ilidaiwa kuwa ni mkusanyiko wa hotuba, maneno ya kipuuzi na yasiyokuwa na maana na kwanza ni "kitabu kinachotia uvivu" kusoma kutokana na kilivyoandikwa mpangilio mbaya na mvurugiko usioweza kueleweka. Mbele ya macho ya Wakristo wa Medievo (yaani walioishi kati ya mwaka 1100 - 1500 B.K), Qur’ani haingewezekana kwa namna yoyote ile kuwa ni Maneno ya Mwenyezi Mungu kwa sababu Muhammad alikuwa ni Mtume wa uongo. Kwa hiyo walidai kuwa Mtume (saww) aligushi (aliandika mwenyewe). Kisha akadai kuwa imetoka kwa Mwenyezi Mungu. Waliendelea kudai kwamba hakuna ufunuo wowote ulioteremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa yalikuwa ni maneno ya kuweweseka ambayo Mtukufu Mtume Muhammad (saww) alikuwa anayasema alipokuwa anabanwa na kifafa, ambayo yeye (Mtume saww) alidai kuwa ni ufunuo. Dini ya Uislam ilionekana kuwa si chochote isipokuwa ni upotofu na kwamba ni mafundisho yenye makosa, mafundisho yaliyochukuliwa kutoka katika Ukristo. Uislamu ulichukuliwa kuwa ni dini ya upanga, na katika jitihada zao za kulichafua jina la Uislam, wakaupachika jina la


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 70

70

"Mohammedanism" (yaani dini iliyoanzishwa na kuletwa na Muhammad (saww) badala ya Mwenyezi Mungu.) Waislamu pia hawakunusurika na ghadhabu hii ya Wakristo wa Medievo (Wakristo walioishi miaka ya 1100 - 1500 B.K) ambao waliwaita (Waislamu) makafiri, wapagani, mabedui wa jangwani na wafuasi wa Muhammad (Muhammedans). Kwa sababu ya kutotaka kwao kuukubali Uislamu, Wakristo wakawa maadui dhahiri wa Uislamu na Waislamu. Katika mashambulizi yao ya maneno, viongozi wa kanisa walitumia mbinu mbalimbali katika hila zao za kuudhuru Uislam; kama vile kuelemea upande mmoja katika hoja zao, upotoshaji, kutafsiri vibaya kwa makusudi, kubuni mambo ya uongo ili kuwashambulia n.k. Wakati haujabadili hali ya mambo, kwa bahati mbaya; zama za vita vitakatifu dhidi ya Uislamu "Crusades" zimepita siku nyingi, lakini wakristo bado hawawezi kuukubali Uislamu. Wakristo wa zama hizi, wanatumia mbinu mpya ili kukabiliana na kile wanachokiona kuwa ni "hatari" ya Uislamu. Jitihada za Wamishenari Matumizi ya nguvu dhidi ya Waislamu ambayo kilele chake ilikuwa ni vita vitakatifu dhidi ya Uislamu (crusades) yaliungana na jitihada za wamishenari kwa upande wa wakristo katika jitihada zao za "Kuwarejesha makafiri kwa Bwana". Jitihada hizi za wamishenari, hata hivyo zilipata mafanikio kidogo sana licha ya muda wote na fedha zilizotumika kwa mamia na mamia ya miaka ambapo jitihada hii imekuwa ikiendelea. Jitihada za mwanzo katika kujaribu kuwabadili Waislamu kuwa Wakristo zilikuwa malumbano/ mabishano kama yale yaliyotumika kwao, Waislamu walikataa kuyasikiliza malumbano hayo. Uzoefu umewaonyesha Wakristo kwamba matusi hayasaidii kitu, kwa hiyo jitihada za wamishenari wa Kikristo wa zama hizi zimechukua mwelekeo mpya kabisa. Wamejiwekea sera mpya ya "kuwahubiria Waislamu kwa upendo."


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 71

71

Nchini Marekani kuna taasisi moja inayoitwa "Center of Ministry to Muslims" (CMM), kituo cha Mahubiri kwa ajili ya Waislamu, taasisi hii imeandaa mpango maalumu (kifedha na kielimu), unaokusudia kufikisha ujumbe wa Ukristo kwa Waislamu. Malumbano (mabishano) hayatumiwi lakini bado njia zinazotumiwa sio za uadilifu kama vile upotoshaji, tafsiri potofu na hata ubunifu wa habari za uongo hutumika. Ukweli juu ya Ukristo umefunikwa kwa utando wenye sukari, na taasisi hii (CMM) unawalenga Waislamu ambao wako peke yao katika nchi hii, bila msaada wa maadili ya familia na marafiki wa kiislamu. Moja ya jitihada zinazovutia kwa upande wa watuishi katika CMM ni gazeti lao la "Noor ul Haq" au "Nuru ya ukweli". Gazeti hili linachapishwa kwa Kiingereza na Kiarabu muundo (format) wake una sura ya kuwa gazeti la Kiislamu, lakini ilivyo ni gazeti la kikristo linalokusudiwa kuwafikia Waislamu. Linatumia misamiati ya Kiislamu na aya za Qur’ani, lakini uangalifu ni muhimu sana hapa kwa vile aya hizi za Qur’ani zinapotoshwa na kutafsiriwa tofauti na zilivyotafsiriwa na Mtume (saww), ili kuwamezesha Waislamu mafundisho ya kikristo. Kwa Muislamu mwenye elimu ndogo ya dini, ni rahisi kupotoshwa na mafundisho haya. CMM ni tasisi ndogo sana ikilinganishwa na "Zwemer Institute For Muslim Studies" (Tasisi ya Zwemer kwa ajili ya mafunzo ya Uislamu). Taasisi hii yenye kituo chake California, ambayo imechukua jina lake kutoka kwa mmishenari raia wa Netherlands ambaye alitumia takriban miaka hamsini katika kipindi cha mwanzo cha karne hii kuwahubiria Waislamu katika Mashariki ya Kati, huwafundisha Wakristo mbinu za kuwahubiria Waislamu. Wanafunzi katika taasisi hii wanajifunza Kiarabu, Historia ya Uislamu, Utamaduni wa kiislamu na imani ya Uislam na utekelezaji wake. Watu hawa wamejizatiti kwelikweli, na sio wajinga wa Uislamu kwa namna yoyote ile. Wamefundishwa na wamekubali kuuchukia Uislamu lakini sio kwamba hawajui Uislamu. Hii ni jitihada kubwa kabisa. Wahubiri wanafunzi na wamishenari wanaoandikishwa katika taasisi hii huchukua aina zote za mafunzo juu ya


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 72

72

Uislamu. Kuna zaidi ya haya. Pia kuna semina fupi zinazotolewa kwa vikundi vya kanisa vinavyopendelea (kufanya hivyo), na taasisi ina kituo cha uchapaji ambacho huchapisha majarida, vitine (pamfleti), vitabu na hata filamu na kanda za video. Ni taasisi nzuri sana kwa Wakristo, lakini ni hatari sana kwa Waislamu. Wamishenari wa Kikristo wanaotoka katika taasisi hii hawajaribu hata kidogo kuonyesha kuwa Uislamu "ni rundo la kasoro na dosari". Wanajaribu kuonyesha kuwa Uislamu una "vipande vya ukweli ambavyo havikuunganishwa", na kutoka hapa, wanajaribu kumshawishi Mwislamu kwamba vipande hivi vya ukweli vimeunganishwa na kuwa kitu kizima katika Ukristo. Mashambulizi ya maneno sasa hivi yameachwa na baadala yake wanajaribu kujenga mashaka katika nyoyo za Waislamu juu ya imani yao. Wakristo wana matumaini kwamba mashaka haya baadaye yatasababisha kutoridhika, ambako kutasababisha kuhama kutoka kwenye Uislamu kwenda kwenye Ukristo. Wamishenari wa Kikristo wanaangalia kwa furaha kabisa migogoro iliyomo ndani ya ulimwengu wa Kiislamu leo hii. Taasisi ya Zwemer inawaambia watu wake kwamba: "Kuhamahama na ukimbizi (unaosababishwa na migogoro) pamoja na kuvurugika kwa maisha ya kawaida kumesaidia kuvuruga utamaduni wa zamani na umeleta uwazi mpya miongoni mwa Waislamu katika kusikia habari njema za Yesu kristo. Imani ya zamani kwamba Uislamu una nguvu isiyoweza kushindwa sasa hivi haina nguvu tena".32 Tarakimu zinazotolewa na Taasisi ya Zwemer kwamba ni ya Wakristo wapya bila chembe ya shaka yoyote zimekuzwa. Hii ni kwa sababu ikitajwa idadi ya ndogo ya Wakristo wapya itakuwa vigumu kupata wanafunzi na fedha za kutosha kwa hiyo wanalazimika kutoa tarakimu kubwa ili ionekane kuwa "mti" wa Ukristo unazaa matunda. 32Muslim Awareness Seminar Notebook, uk. 5.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 73

73

Kwa kadri Uislamu unavyoendelea kukua, mashirika kama CMM na Taasisi ya Zwemer ndivyo yanavyopata nguvu na kujizatiti zaidi. Huu sio wakati kwa Mwislamu kukaa na kulipuuza hili. Siku moja litakuja mpaka mlangoni pake, lazima ajiandae, lazima awe na imani thabiti, na ni lazima amjue jamaa yake (ukristo) ili asitetereke katika imani yake. Kampeni Dhidi ya Chuki Ingawa mashirika kama "CMM na The Zwemer Institute" yanatangaza "kuwafikia na kuwahubiria Waislamu kwa upendo", nyuma ya migongo yao kuna mbinu nyingine (ambayo haitangazwi) ambayo hutumiwa mara nyingi katika kuudhibiti Uislamu. Ni mbinu iliyoanza zama za vita vitakatifu dhidi ya Uislamu (Crusades) na mbinu hiyo kamwe haijafa kifo halisi. Mbinu hii inayotumika katika hila zao za kuudhuru Uislamu imepewa jina la "Vita vitakatifu vya kiakili dhidi ya Uislamu''. Mashambulizi haya ya mdomo dhidi ya Uislamu ni maendelezo ya kazi iliyoanza miaka zaidi ya 900 iliyopita ambapo Papa Urban II alihamasisha vita vitakatifu dhidi ya "makafiri" wa Mashariki ya kati alipokuwa akihutubia umati wa watu katika mji wa Clemont. Ushahidi kwamba kampeni hii ya chuki dhidi ya Uislamu bado inafukuta unaweza kuonekana katika maduka ya vitabu - hususan maduka ya Wakristo - na katika maktaba za umma (public libraries). Wale wanaojiita "Wataalamu bingwa wa historia, utamaduni wa Mashariki ya Kati na dini" (Orientalists/Mustashirik) katika karne ya kumi na tisa na ishirini, wameandika mambo mengi ya kuchukiza juu ya Ulimwengu wa Kiislamu: Mifano mizuri ni kama vile "Story of Civilization" (Simulizi juu ya ustaarabu) kilichoandikwa na Durant. "The Decline and Fall of the Roman Empire" (Kudidimia na Kuanguka kwa Dola ya Urumi) kilichoandikwa na Gibbons. "Inside Asia" (Ndani ya Asia) kilichoandikwa na Gunther. "The Outline of History" (Dondoo za Historia) kilichoandikwa H. G. Welles -- ambavyo vyote vinahesabiwa kuwa ni vitabu "vyenye ubora wa kiwango cha juu kabisa" katika ulimwengu wa historia. Uelemeaji


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 74

74

upande mmoja katika uchambuzi wa hoja na uadui umetapakaa katika maeneo yote na katika kila kona. Mtu anaweza kushangaa na kujiuliza vipi watu hawa wajizatiti kulisoma eneo fulani la ulimwengu, eneo ambalo wana chuki kubwa sana dhidi yake. Hata kitabu cha hivi karibuni cha Albert Hourani ambacho kimesifiwa sana kiitwacho "A History of the Arab Peoples" (Historia ya Waarabu) kimejaa uelemeaji upande mmoja katika uchambuzi wa hoja na uadui dhidi ya Uislamu. Cha ajabu ni kwamba hawa wanaodaiwa kuwa wanapiga vita chuki dhidi ya Uislamu ni Wakristo wenye imani kali. Angalia kwa mfano kitabu "Islam Revealed" (Uislamu wawekwa wazi) kilichoandikwa na Mkristo wa Kiarabu mwaka 1988. Nyuma ya kitabu hiki mwandishi anaahidi kuwapa wasomaji wake "Mtazamo wa kufungua macho juu ya imani hatari za kila mtu katika watu watano katika ardhi. Mwandishi wa kimarekani Robert Morey, "anayedaiwa kuwa ni mwanazuoni (msomi) wa kimataifa" katika fani ya ulinganishaji wa dini mbalimbali - zaidi ya hili ni Mkristo mwenye msimamo mkali kidini - hivi karibuni ameandika kitabu kiitwacho "Islam Unveiled: The True Desert Storm" (Uislamu wafichuliwa: Kimbunga (Dhoruba) halisi cha Jangwani) alichokiandika mwaka 1991. Ndani yake anadai "Kuthibitisha" kwamba vitendo vyote vya ibada na imani za Uislamu zimetokana na Ukafiri (upagani) uliokuwepo kabla ya Uislamu. Dr. Morey pia huandaa kipindi cha redio (Radio show) ambacho ni maalum kwa ajili ya kuushambulia Uislamu. Hivi karibuni, katika kipindi hiki alisema: "- - - kama Muhammad angekuwa hai leo hii, bila shaka angechunguzwa kama mharibifu wa akili za watu, muuaji wa halaiki (ya watu,) na mdhalilishaji (mnyanyasaji) wa watoto". Taarifa kama hizi ni mfano tu wa marundo na marundo ya taarifa zinazokusudiwa kujenga chuki zinazotolewa kila siku dhidi ya Uislamu na ambazo zinastahili kudharauliwa. Taarifa hizi zinakusudiwa kuimarisha na kueneza zaidi propaganda mbalimbali za chuki dhidi ya Uislam zinazoaminiwa na Wakristo walio wengi, na pia kuzidisha kutoaminiana na


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 75

UJUMBE WA YESU

75

uadui. Inawezekana vipi watu wakahubiriana kirafiki na kwa upendo na ilhali akili za watu zinashindiliwa takataka kama hizi? Kwa kadri Uislamu unavyoendelea kukua na kuenea, ndivyo mashambulizi haya yatakavyozidi kuongezeka. Wakristo wanahofu, na hii ndiyo mbinu waliyoamua kuitumia katika kukabiliana na hofu hiyo. Ni mbinu ambayo imekuwa ikitumika kwa mamia ya miaka, na ni mbinu ambayo wametokea kuipenda sana. Badala ya kufungua milango ya mazungumzo juu ya tofauti za imani zao, wanafanya haraka kutumia jazba, hasira, na kujenga uadui. Mbinu na Hila Nyingine Wanazozitumia Kuudhuru Uislamu Mbali na vitabu, vitine (mapamfleti), vipindi vya redio, n.k. ambazo zimekusudiwa moja kwa moja kuudhuru Uislamu, kuna mashambulizi zaidi ya hila yanayofanywa na Wakristo kupitia kwenye maandishi ya habari za kubuni na zisizo za kubuni (fiction and non-fiction), pamoja na televisheni na mikanda ya video ambapo huuonyesha Uislam na Waislamu kuwa ni kundi chokozi la ugaidi na wagaidi. Vitabu ni pamoja na "The Source" (chanzo) kilichoandikwa na James Mitchner na kingine cha hivi karibuni "The sum of All fears" (Jumla ya hofu zote) kilichoandikwa na Tom Clancy. Pia kuna vitabu vingine vinavyopotosha kama vile: "Jihad", "The Holy Sword" (Upanga mtakatifu) na "Sacred Rage" (Hasira Takatifu). Kitabu kingine kinachoonyesha uadui mkubwa ni "Holy of Holies" (mtakatifu wa watakatifu); ambacho kinaelezea jinsi Wafaransa kwa msaada wa Warusi na Waisraeli, wanavyoharibu Msikiti Mkuu (Msikiti mtakatifu) wakati wa hijja. Na bila kusahau kitabu cha kikafiri cha Salman Rushdie, "The Satanic Verses". Mwandishi wa kitabu hiki, Salman Rushdie, amekuwa akieleza mara kwa mara kwamba nia yake haikuwa kuutukana Uislamu isipokuwa majina ya watu na majina ya sehemu (mahali) aliyoyatumia katika kitabu chake yamegongana mno na majina ya


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 76

76

watu watukufu na sehemu tukufu za kiislamu kiasi kwamba inakuwa vigumu kuamini maneno yake. Mashambulizi yanayofanywa dhidi ya Uislamu kupitia kwenye televisheni yanasikitisha. Katika kipindi cha kiangazi cha mwaka 1991, kulikuwa na mfululizo wa midahalo iliyofanywa baina ya Waislamu wawili na Wakristo wawili kuhusiana na tofauti za dini zao. Midahalo sita ilionyeshwa kwenye televisheni kwa wiki (majuma) kadhaa juu ya injili. Na Waislamu walifanya kazi nzuri sana ya kuwakilisha imani yao, hata mbele ya maadui dhahiri kutoka pande zote, ikiwa ni pamoja na msimamizi wa mdahalo, wazungumzaji wawili wa upande wa imani ya Kikristo, na hata wasikilizaji wa Wakristo walio wengi. Hata hivyo, waandaaji wa kipindi hiki cha televisheni walifanikiwa kupata walichokitaka, kwanza “walihariri� kanda za matangazo ili kuwaonyesha Waislamu katika mwanga mbaya. Na pili, walitoa kijitabu kuhusiana na mdahalo kwa ajili ya watazamaji wa majumbani ambacho walikipa jina "The facts on Islam" (Ukweli juu ua Uislamu). Jina lenye kufaa zaidi kwa kijitabu hiki lingekuwa "Mambo ya uongo na Fitna dhidi ya Uislamu" (Fallacies of Islam), kwa vile mtu atakuta ndani yake ukweli kidogo sana, bali kimejaa upotoshaji na uongo dhahiri dhidi ya Uislamu. Kwa upande wa filamu kuna "Black Sunday" (Jumapili Nyeusi) ambapo "Magaidi" wa kipalestina wanapanga njama za kuwaangamiza wale wote wanaohudhuria "Superbowl" (mashindano ya mwaka ya mpira wa miguu). Nyingine ni "Not Without My Daughter" (Si Bila Binti wangu ), filamu ambayo ianonyesha picha ya kutisha juu ya mahusiano ndani ya familia za Kiislamu. Mambo ya kukaririwa yanakuzwa na kuendelezwa na vitu kama hivi; almradi mambo kama haya yanaendelea, Uislamu utapata wakati mgumu kwa kuonekana katika mwanga mbaya wa kila kitu. Sisi kama Waislamu, lazima tuwe imara pindi tunaposhambuliwa katika


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 77

UJUMBE WA YESU

77

imani yetu - - ikiwa ni kwa "mbinu ya upendo" au uadui dhahiri. Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia katika Qur’ani tukufu. "Mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu, na mtasikia udhia mwingi kwa wale waliopewa kitabu kabla yenu, na kwa wale walioshirikisha. Na kama mkisubiri na kujilinda na aliyoyakataza Mwenyezi Mungu (mtakuwa mmefanya jambo) zuri; kwani mambo haya ni mambo makubwa ya mtu kuazimia kuyafanya". (Qur’ani 3:186)

MADHEHEBU KATIKA UKRISTO Ukristo umekua kwenye nguvu kubwa katika ulimwengu wa leo. Hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba unatoa madai ya kuwa na idadi kubwa ya wafuasi katika ulimwengu, Ukristo wenyewe ni vurugu ya madhehebu mbali mbali, kila moja likiwa tofauti na lingine katika namna fulani. Japo Uislamu pia umegawanyika katika makundi mawili ya Sunni na Shia, lakini mgawanyiko huu ni wa kisiasa (sic), sio wa kidini. Katika Ukristo mgawanyiko ni wa kidini. Japo wote wanamuamini Mungu, lakini tusimsahau Yesu - - - mambo yanakhitilafiana kuanzia hapa. Ingawa idadi kamili haieleweki, ninafahamu takribani madhehebu hamsini ndani ya Ukristo, tukianzia na wa - Amish, ambao wameamua kujitenga na ulimwengu na mambo yote yanayorahisisha maisha (ya kisasa) kama vile umeme na magari, na kumalizia na Unitarians ambao wanaonekana mbele ya wakristo walio wengi kuwa sio wakristo kwa sababu hawaamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu wala hawaamini utatu Mtakatifu. Waromani Katoliki, ambao ni dhehebu la kikristo kubwa kuliko yote ulimwenguni leo, wanawatukuza watakatifu (saints) na mama wa Yesu; “Hostia” (yaani mkate) wakati wa huduma yao ya kumunio inasemekana kwamba huwa ni mwili halisi wa Yesu, divai huwa ni damu halisi inapobarikiwa na padri.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 78

78

Kwa sababu ya kutoridhishwa kwao na imani ya utawa (celibacy), kanisa la Orthodox lilijitenga kutoka Roma katika zama za kati (middle ages) na sasa hivi kanisa hili lina wafuasi wengi katika Ulaya ya Mashariki. Wanaendelea na mapambo katika makanisa yao kama yale ya kanisa katoliki lakini wana sikukuu tofauti na wanaapa kiapo cha utii kwa "Baba Mtakatifu" mwingine asiyekuwa yule wa Roman Katoliki. Mnamo mwaka 1517, kanisa la kiprotestanti lilianzishwa, kwa sababu ya kutokubaliana na baadhi ya mambo (vitendo) ndani ya kanisa katoliki. Baadhi ya mambo hayo ni: 1) Wakatoliki wanapamba na kuyanakshi makanisa yao. Waprotestanti wanayafanya kuwa rahisi. 2) Maandiko Matakatifu ya Wakatoliki yanajumuisha vitabu vya "Apocrypha" (vitabu vilivyofichikana). Waprotestanti hawakubali kitabu chochote katika vitabu hivi. 3) Wakatoliki wana vinyago katika makanisa yao, majumba yao, katika magari yao. Pia wanavichimbia vinyago hivi mbele ya bustani za nyumba wanazotaka kuziuza, na wana misalaba iliyopambwa kwa umbo la Yesu akiwa amesulubiwa. Waprotestanti wanashutumu jambo hili kuwa ni "ibada ya masanamu" kwa hiyo wengi hawana hata msalaba mtupu (usiokuwa na sanamu ya Yesu) ndani ya makanisa yao. Ndani ya tawi hili la Ukristo la Kiprotestanti kuna madhehebu mbali mbali na imani husika. Walutherani wanafuata mafundisho ya Martin Luther. Watu katika makanisa ya kimageuzi hawakumuona kwamba yeye ni makini vya kutosha, hata hivyo walifuata mafundisho ya John Calvin. Wa-Baptisti, ambao wanaamini kuwa watu wazima - - sio watoto - - ndio wanaotakiwa kubatizwa, waliteswa sana na makanisa yote mawili -Wakatoliki na Waprotestanti katika Zama za Kati (Middle Ages) lakini sasa


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 79

UJUMBE WA YESU

79

hivi wamekuwa miongoni mwa madhehebu makubwa ya Ukristo. Kamwe Wakatoliki hawakuwa wapole kuhusiana na harakati za Waprotestanti, na lilikuwa ni uchunguzi kwa ajili ya uhuru wa kidini lililowahamisha Wazungu kutoka miji yao na kwenda katika nchi za ugenini. Wa-Puritan walipohamia Amerika, katika karne ya kumi na saba, kundi zima la madhehebu ya kikristo lilianza kuwepo katika miaka michache iliyofuatia. Wa-Shaker walikuwa na imani kali juu ya imani ya kutokuoa (ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu). Madhehebu hii leo imeshakufa (kutokana na ubovu wa imani na misingi yake). Wapentekoste wanadai "kuzungumza kwa ndimi" (kuzungumza kwa Roho mtakatifu). Huduma zao za kanisa inasemekana zinavutia sana. Pia wanaamini kwamba Biblia ndani yake haina makosa hata kidogo - - - yaani haina kasoro au dosari japo ile ndogo kabisa. Kutokana na nyadhifa zao tumekuja kuwajua watu "maarufu" kama akina Jimmy Swaggert, Jim na Tammy Fay Bakker. Mashahidi wa Yehova wanatumia muda wao mwingi kutafakari kitabu cha Ufunuo, wakiiota siku ambayo kila mtu na kila kitu kitakhiliki (kitaangamia) isipokuwa wao. Wa-Mormon walikuwa na mtume wao, Joseph Smith, ambaye aliwaletea kitabu cha maandiko ambacho wanaamini kuwa ni kitakatifu kama Biblia. Sera yao ya "ndoa za mbinguni" (yaani wake wengi bila mpaka) ilipelekea mwisho wa kuendelea kufanywa kuwa taifa (state) katika nchi hii. Wanasayansi wa kikristo pia wana kitabu chao cha Maandiko mbali na Biblia; Mary Baker Eddy, mtume wao (wa kike) aliwaambia wafuasi wake kuwa imani na sayansi hushinda vyote - - - hata matamanio ya ngono. Madhehebu mengi tofauti tofauti yakiwa na vitendo vingi tofauti tofauti, yote yameungana na kukubaliana kwamba imani yao ya Ukristo ndiyo


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 80

UJUMBE WA YESU

80

"imani pekee ya kweli". Kiapo hiki cha kishahidi kwenye dini imekuwa ndio sababu ya matukio mengi ya ukatili na utumiaji wa nguvu usioelezeka dhidi ya wale wenye imani tofauti na hii. Matukio haya ni kama vile vita vitakatifu dhidi ya Uislamu (crusades). Upelelezi na hata Maangamizi ya moto ya Nazi (Nazi Holocaust). Kutovumiliana ni kitu chenye kutisha sana na hasa kinapotokana na teolojia zisizo na mantiki. Ama kwa Waislamu Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaambia kwamba: "Shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu wala msifarakiane". (3:103) Ni lazima tuwe: "Subirini na muwashinde makafiri, na kuweni imara (nyoyo zenu) na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu". (Qur’ani 3:200) Kwa sababu: "Yeyote anayejinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu, na akafanya mambo mazuri, kwa hakika ameshika kishiko imara kisichokuwa na kukatika: na mwisho wa yote ni kwa Mwenyezi Mungu". (Qur’ani 31:22)

HITIMISHO Wakati ambapo Ukristo zaidi kabisa ni wa Yesu, kwa uwazi zaidi HAUTOKANI na Yesu. Haufanani kabisa na ujumbe ulioletwa na Mjumbe huyu wa Mungu. Badala yake, umekuwa ni vurugu za teolojia isiyoeleweka iliyojenga haiba ya mwanadamu ambaye baadae aligeuzwa kuwa mungu. Katika kitabu chake "Basic Christianity” mwandishi John Stott analeta mbele fikra yenye kuvutia: "Kimsingi Ukristo ni Kristo. Nafsi na kazi ya Yesu ni jiwe la msingi ambapo juu yake imejengwa imani ya


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 81

81

UJUMBE WA YESU

Ukristo. Kama siye aliyesema kuwa ni yeye (ikiwa sio yeye aliyejitangaza kuwa ni Yesu kristo). Na kama hakufanya yale aliyosema aliyokuja kufanya, jengo zima la Ukristo litaporomoka na kuanguka chini‌"33

Mtume Muhammad, baada ya miaka ya mapambano dhidi ya Wayahudi wa Madina juu ya masuala ya dini, alisema teolojia ni upuuzi wa kitoto- - adui wa dini. Uislamu, kama matokeo, ni dini rahisi ambayo haikuzikwa katika vichaka vya ububusa visivyokubaliana na akili na mantiki. Hakuna kundi la watu wanaoshughulika na masuala ya dini peke yake (clergy), hakuna madaraja ya dini, wala hakuna Sakramenti. Teolojia haina nafasi katika Uislamu, kwa vile Uislam ni njia kamili ya maisha, na sio rundo la maneno tu. Licha ya kwamba Uyahudi ulikwenda mrama katika sharhe (fafanuzi) za vitabu vyao vya sheria lakini bado wanayo imani ya msingi na kuu kabisa kuwa Mungu ni mmoja. Uislamu una maana kujinyenyekesha chini ya taa na milki ya Mwenyezi Mungu, imani ya kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu asiyekuwa na mshirika, ikiwa ndio imani kuu na ya msingi kabisa. Ukristo kwa upande mwingine unasema kwamba Bwana wake ni Yesu kristo. Kwa mujibu wa Fritz Ridenour: "------Tunajinyenyekesha yake".34

chini

ya

mamlaka

Hebu tuangalie tena katika Mathayo 4: 10, ambapo Yesu anasema: "Msimsujudie yeyote isipokuwa Bwana Mungu wenu. Na mwabuduni Yeye tu". 33 Basic Christianity, uk. 20. 34 How To Be A Christian In An Unchristian World, uk. 126.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 82

82

Dhahiri shahiri, hapa Yesu anatuambia kwamba ni Mungu peke yake ndiye tunayetakiwa kumwabudu. Dini sio suala la kubahatisha na hotuba bali ni ukweli (fact) na muongozo. Dini ya kweli inajali na kuzingatia utii wa sheria, na utii huu ndio kipimo cha uchamungu wa muumini. Ndugu zetu wa Kikristo wanatakiwa kuzingatia masuala haya katika nyoyo zao. Sio tu kwamba hawafuati miongozo ya dini zao isipokuwa Jumapili, bali pia wamepoteza uhusiano kabisa kutoka kwenye mafundisho ya mtu ambaye jina lake linaunda msingi wa imani yao. Na badala yake wamebugia imani na mila za kipagani ambazo wanajaribu kuzivisha joho la imani juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mmoja asiyekuwa na Mshirika (Monotheism). Marafiki zetu wa kikristo wana kazi kubwa zaidi ya kutafiti. Waislam hawana budi kukumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu katika Qur’ani: "Wayahudi na Wakristo hawatakuwa radhi nanyi mpaka mtakapofuata dini yao". (Qur’ani; 2:120) Pia ni lazima tukumbuke maneno ya mwisho yaliyotolewa na Mwenyezi Mungu kwa Mtume Muhammad (SAWW): "Leo nimekukamilishieni dini yenu (na) kukutimilizieni neema yangu juu yenu na Nimekuchagulieni Uislamu ndio iwe dini yenu". (Qur’ani; 5:3). Baada ya kusema na kufanya yote, ni lazima tuyazingatie maneno muhimu yafuatayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Tunaubainisha na kuuthibitisha ukweli dhidi ya Uongo (Batili) mara Batili ikaondoka. Na adhabu inakungojeeni kwa haya mnayoyasema". (Qur’ani; 21:18)


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 83

83


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 84

UJUMBE WA YESU

84

ORODHA YA VITABU VITABU VINGINE VINAVYOHUSIANA NA ULINGANISHAJI BAINA YA UISLAMU NA UKRISTO Ahmad, Khurshid. Islam and the West. Lahore, Pakistan: Islamic Publications, Ltd., 1986. Ajijole, A.D.A. Myth of the Cross. Chicago: Kazi Publications, 1979. Al-Johani, Dr. Maneh Hammad. The Truth About Jesus. Riyadh, Saudi Arabia: World Assembly of Muslim Youth, 1987. All Scripture Is Inspired of God and Beneficial. Watch Tower Bible and Tract Society. Brooklyn (NY): WTBTS, 1990. Andry, Carl Franklin, Ph. D. Jesus and the Four Gospels. Muncie. IN: Print press, 1978. Badawi, Dr. Jamal. Jesus in the Qur’anii and the Bible: An Outline. Halifax, Nova Sotia: Islamic Information Foundation. Muhammad In the Bible. Halifax, Nova Scotia: Islamic Information Foundation. Bainton, Roland H. Early Christianity. Princeton (NJ): Van Nostrand Co., Inc. "Bits N Pieces". The American Religion: The Emergence of the Post Christian Nation: NY: Simon & Schuster, 1992. Brown, Aisha. Three In One: The Doctrine of the Trinity. Chicago (IL): The Open School,1992. Bucaille, Maurice. The Bible, the Qur’anii and Science. Delhi, India


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 85

UJUMBE WA YESU

85

Cresent Publishing, 1978. Chirri, Imam Mohamad Jawad. Inquiries About Islam. Detroit (MI): Harlo Press, 1986. Davies, A. Powell. The Meaning of the Dead Sea Scrolls: NY: New American Library, Inc.,1956. Deedat, Ahmed. Is the Bible God's Word? Durban, South Africa: Islamic Propagation Centre. Dibble, R.F. Mohammed. NY: Garden City Publishing Co. Inc., 1926. Durant, Will. The Age of Faith. NY Simon and Schuster, 1950. Evans, Rod L. and Irwin M. Berent. Fundamentalism: Hazards and Heartbreaks. LaSalle (IL): Open Court Publishing Co., 1988. Grun, Bernard. The Timetables of History. NY Simon & Schuster, 1991. Frazer, Sir James George. The Golden Bough. Ny: Macmillan Comapany, 1940. Haneef, Suzanne. What Everyone Should Know About Islam and Muslims. Des Plaines (IL): Library of Islam, 1985. Harstad, Bjug A. Is the Bible Reliable? Parkland (WA), 1929. Hart, Michael H. The 100: A Ranking of the Most Influential Persons in History. NY: Hart Publishing Co., Inc., 1978. Holy Bible. Authorized King James Version. Grand Rapids (MI): Zondervan Corp., 1977. Holy Bible. American Standard Version. NY: Thomas Nelson & Sons, 1901.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 86

UJUMBE WA YESU

86

Holy Qur’anii. Trans. by A Yusuf Ali. Madinah (Saudia Arabia): King Fahd Holy Qur’anii Printing Complex, 1989. Jammelah, Maryam. Islam Versus the West. Lahore, Pakistan: M.Y. Khan and Sons, 1984. Jansen, G.H. Militant Islam. NY: Harper & Row, 1979. Johnson, George. Christmas Ornaments, Lights and Decorations. Paducah (KY) : Collector Books, 1990. Kingsriter, Del. Sharing Your Faith With Muslim. Minneapolis(MN): Center For Ministry to Muslims. Journey To Understanding. Minneapolis (MN): Center For Ministry to Muslims. Levy, Leonard W. Treason Against God: A History of the Offense of Blasphemy. NY: Schocken Books 1981. Light of Truth, The Canada Maritime Muslim Students' Association. Lippman, Thomas W. Understanding Islam. NY: Penguin Books, 1990. McCurry, Don M. Muslim Awareness Seminar Notebook. Pasadena, CA: Joy Printing, 1981. Maier, Paulo L. First Christians: Pentecost and the Spread of Christianity. NY: Harper & Row1976. Manchester, William. A World Lit Only By Fire. Buston (MA): Little, Brown and Co., 1992. Mankind's Search for God. Watch Tower Bible and Tract Society. Brooklyn (NY): WTBTS 1990. Marty, Martin E. A Short History of Christianity. Cleveland (NY): William


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

Page 87

UJUMBE WA YESU

87

Collins & World Publishing Co. Inc., 1975. Mears, Henretta C. What the Bible Is All About. Minneapolis, MN: The Billy Graham Evangelistic Association, 1966. "Media Response Publications Edition". Jan. - March, 1992. Mohammad, Ch. Nazar. Commandments By God in The Qur’anii. NY: The Message Publications 1991. Morey, Dr. Robert A. Islam Unveiled: The True Desert Storm. Shermans Dale, P.A. The Scholars Press, 1991. Mufassir, Sulaiman. Jesus in the Qur’anii. Plainfield (NY): Muslim Students' Association, 1977. Murstein, Bernard I. Love, Sex and Marriage through the Ages. NY: Springer Publishing Co., 1974. Neufeldt, Victoria ed. Webster's New World Dictionary. Ny: Simon and Schuster, 1988. New Testament For America. Taken from the Holy Bible, New International Version. South Holland, IL: The Bible League, 1984. New York Public Library Desk Reference, The NY: Webster's New World, 1989. Reach Out In Friendship. Center For Ministry to Muslims Minneapolis (MN): CMM. Ridenour, Fritz How to Be A Christian In An Unchristian World. Glengale, CA: G/L Publications, 1971. Rosten, Leo. Religions of American. NY: Simon and Schuster 1975. Rusell, D.S. Between The Testaments. Philadelphia: Fortness Press, 1960.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 88

88

Shorrosh, Dr. Anis. Islam Revealed. Nashvile: Thomas Nelson Publishers, 1988. Stott, John. Basic Christianity. Downers' Grove, IL: Inter - Varsity press. The Bible: God's Word or Man's? Watch Tower Bible and Tract Society. Brooklyn (YN): WTBTS, 1989. Thiessen, John Caldwell. A survey of World Missions. Chicago: Inter Varsity Press, 1955. This Is the Catholic Church. Knights of Columbus. New Haven (CO): K of C, 1955.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

11:51 AM

UJUMBE WA YESU

Page 89

89

BACK COVER UJUMBE WA YESU Nafsi kuwa katika amani kuhusu Mwenyezi Mungu, hili ndio lengo haswa la kitabu hiki. Wengi wetu tunaridhika kuishi tu bila udadisi na tunayakubali mambo "kama yalivyo"; tunayapuuza yale maswali madogo yanayosumbua, na mashaka katika akili zetu, haswa masuala yanayohusiana na dini. Kwa kufanya hivi, ndiyo ni kweli kwamba tunaendelea kuishi, lakini kamwe hatupati utulivu wa akili na amani ndani ya nafsi zetu. Hata hivyo wengine miongoni mwetu, hawaridhiki kuyachukua mambo kama yalivyo, na hivyo kwa bidii na shauku hufanya jitihada kuyatafutia majibu sahihi maswali yanayojitokeza katika maisha yao. Tunahoji imani za baba zetu, hatupo tayari kuzikubali na kuzifuata kibubusa. Barabara hii haipitiki kwa urahisi kwa namna yoyote, lakini malipo yake ni yenye faida kubwa. Ndani ya dini nyingi ambazo zipo duniani leo ni tatu tu zinazodai kwamba zinampwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu-yaani imani ambayo msingi wake ni kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mmoja asiye na mshirika. Uchunguzi wa karibu, katika dini mbili kati ya hizi - Uyahudi na Uislamuutaonyesha hili kuwa ni kweli: Wote Wayahudi na Waislamu wanamuabudu Mungu mmoja, Muumba wa Mbingu na Ardhi, ingawa kwa mtazamo tofauti.


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 90

90

Wakati tunapoelezea maana ya imani ya kumuamini Mungu Mmoja asiyekuwa na mshirika, kwa Ukristo ni tofauti, wao hawaamini hivyo. Badala ya kumfanya Mwenyezi Mungu Mtukufu awe ndio kiini na msingi mkuu wa imani yao, Wakristo wamegeuza mtazamo wao kuwa juu ya Yesu, anayeeleweka kwao kama "Yesu kristo" au "Yesu Aliyepakwa mafuta." Kwa Wayahudi Yesu alikuwa "Kijana mzuri wa kiyahudi;" kwa Waislamu, Yesu alikuwa Mtume na mja wa Mwenyezi Mungu; mmoja wa wajumbe wateule wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa Wakristo, hata hivyo, Yesu ni zaidi ya hayo. Mwandishi wa kijitabu hiki, Barbara A. Brown ambaye alilelewa na kukulia katika Ukristo amefanya uchunguzi wa kina juu ya dini hizi tatu na matokeo yake ni kjitabu hiki na vingine ambavyo ameviandika kuhusiana na suala hili, na baada ya kuiona haki hakusita kuifuata. Mchapishaji: Tahrike Tarsile Qur’anii, Inc. 80-08 51st Avenue, Elmhurst, New York 11373 Tel: 718 446 6472 Fax: 718 446 4370 www.koranusa.org


Ujumbe Yesu 1 edited M. Ramadhani.qxd

7/16/2011

UJUMBE WA YESU

11:51 AM

Page 91

91


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.