Urejeo

Page 1

RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

UREJEO (al-Raj'ah)

Kimeandikwa na:

Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani

Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim J. Nkusui

7/15/2011

11:43 AM

Page A


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 49 - 2

Kimeandikwa na: Sheikh Abdul -Karim- Bahbahaniy

Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim J. Nkusui

Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab

Toleo la kwanza: Julai, 2009 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

7/15/2011

11:43 AM

Page B


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

11:43 AM

Page C


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

YALIYOMO 2. Maana ya Raja’a............................................................................2 3. Daraja ya itikadi yake....................................................................2 4. Hoja za kuthibi itakadi ya Raja’a..................................................4 5. Wanapinga na athari zao zinasema hayo.....................................10 6. Maswali kuhusu itikadi ya Raja’a................................................11 7. Matokeo.......................................................................................13

11:43 AM

Page D


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Neno la Mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, ar-Raj’ah. Sisi tumekiita, Urejeo. Kitabu hiki ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni wa Kiislamu, Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani. Raj’ah (Urejeo) ni itikadi ambayo kwayo wanavyuoni wa Kiislamu wamehitalifiana: Wako wanaosema ni kurejea kwa baadhi ya wafu wakati wa mwisho wa dunia, wakati ambapo wengine wanasema ni kurejea dola ya haki na uadilifu na kushindwa kwa dhulma, ujeuri na ufisadi. Mwanachuoni wetu huyu ameainisha rai hizi kwa kurejea kwenye aya za Qur’ani na Sunna na kuhitimisha juu ya Raj’ah kuwezekana; kwa maana ya baadhi ya wafu kufufuliwa na kurejea duniani na baadaye kufariki tena, kama ambavyo utaona katika kitabu hiki. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul-Karim J. Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

11:43 AM

Page E


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya AHLUL-BAYT ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanachuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bayt. Wanachuoni waliyokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikra kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bayt na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanachuoni wa kambi ya Ahlul-Bayt katika dhamira hii ni vya aina ya pekee, kwa sababu una nguzo ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na uzalendo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanaharakati wenye fani maalumu mazungumzo ambayo yanaituliza akili na yanapokewa na maumbile salama. F

11:43 AM

Page F


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya nchi zenye chuki dhidi ya uislamu na waislamu. Jumuiya imejiepusha na udadisi uliokatazwa na ni yenye kuhangaikia kuzidadisi akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalum toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tunachokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulio nao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aidhihirishe juu kuliko dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.

JUMUIYA YA KIMATAIFA YA AHLUL-BAYT KITENGO CHA UTAMADUNI

G

11:44 AM

Page G


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

H

7/15/2011

11:44 AM

Page H


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

11:44 AM

Page 1


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah)

1. Maana ya Raja'a: Raja’a: Kama ilivyo katika itikadi ya Shia inamaanisha kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atawarejesha watu miongoni mwa wafu duniani katika sura zao walizokuwa nazo na hawa wako aina mbili: - Aliyebobea imani katika maisha yake ya duniani - Na aliyebobea ukafiri katika maisha yake ya duniani Kisha Mwenyezi Mungu atawalipizia kisasi wenye haki kwa waovu, na waliodhulumiwa kwa madhalimu ,na kwamba hayo yatatokea atakapodhihiri Imamu Mahdi (a.s.) kisha baada ya hapo watarejea katika mauti. Na kuna ambao wamefasiri Raja’a kwamba ni kurejea haki katika nafasi yake na hiyo ni katika utawala wa Mahdi. Na kwamba jambo hili halihusu kufufua wafu na kurejesha watu duniani tena. Rai ya kwanza ndio ilioenea baina ya Shia Ithna-ashariyah kutokana na kuchukua yaliyokuja kutoka kwa Ahlul-Bait hususan tangu zama ya Sheikh Suduq, Mufid, Sayyid Murtadhwa Tusiy, Haadiy Allammah AlMajilisiy, Hurul-Amiliy hadi kwa mafaqihi na maulamaa waliopo sasa.

2. DARAJA LA KUITAKIDI KWAKE Ni dhahiri kwamba itikadi ya kiislamu ina misingi na nguzo zilizoafikiwa na humo kuna matawi na michipuo ambayo humo kunaweza kutokea ikhitilafu katika pande kati ya pande zake. Na raja’a sio katika ile misingi ambayo haifai kuwa na ikhitilafu humo. Sheikh Muhammad Al-Huseiniy al-Kashif al-Ghitwaa amefanya vizuri ambapo ameandika, anasema: “Kuamini raja’a sio lazima katika madhehebu ya Shia na wala kutoiamini hakudhuru ingawa ni dharura kwao. Lakini Ushia haufungamanishwi nayo kwa kuwepo wala kwa kutokuwepo, nayo si kingine bali ni kama baadhi ya masharti ya Kiyama, mfano kuteremka Isa (a.s.) kutoka mbinguni, kudhihiri Dajjaal, kutokea kwa Sufiyan, na mfano wake miongoni mwa 2

11:44 AM

Page 2


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) mambo yaliyoenea kwa Waislamu. 1 Na raja’a kwa maana hii inahesabika kuwa ni sehemu kati ya sehemu zinazokamilisha fikra ya Mahdi katika Uislam, ndio maana unaona zinashirikiana katika madhumuni mamoja, nayo ni kunusurika uadilifu na kuanguka batili katika hatua ya mwisho ya historia, ambapo inaashiria kwamba mfumo wa kidunia unapita katika mwendo wa haki. Na kama dini za mbinguni zimeamini kurejea kwa baadhi ya Manabii, na Waislaam wote Shia na Sunni wameafikiana katika itikati yao kwa hilo juu ya asili ya fikra ya Mahdi. Hivyo hakuna kizuizi kuamini raja’a kama upande wa kutilia mkazo juu ya asili hiyo na mwendelezo wa ufafanuzi wake, na ni wigo wa ubainifu wenye kuisherehesha. Hivyo dhana ya raja’a inakuja kukamilisha, kupanua, kufafanua na maelezo ya ziada ya fikra ya asili ya Mahdi ambayo wameiamini Waislamu wote, kwani ikiwa asili wameiafiki waislamu wote basi mkazo juu ya asili hii na kuifafanua kwa kina zaidi kupitia fikra ya maelezo ya ziada kuna ambayo unayoyaunga mkono katika Kitabu na Sunna. Hivyo inahesabika kuwa ni fadhila inayostahiki heshima na utukufu. Lakini pamoja na hivyo ni kama alivyosema as-Sayyid Muhsin al-Amiliy: “Jambo la kunukuu ikisihi kunukuu kwake inalazimu kuliitakidi, vingine hailazimu....”2 Kutokana na mwelekeo huu wa mwisho tunakuta kwamba baadhi ya Maulamaa wa Shia Ithana-ashariyah wao wenyewe ni kati ya ambao haijawafikia hoja ya Hadith ya raja’a yenye kukubalika kwao kiasi cha kupata yakini katika maana hii mashuhuri, wamefasiri kwa namna ambayo hailazimu kurejea katika uhai baada ya mauti kwa baadhi ya kundi la watu, bali inasimama katika maana ya kurejea dola ya haki na uadilifu na kushindwa kwa dhulma, ujeuri na ufisadi.3 1 Aswilu-Shia wa Usuuliha Uk: 35 chapa ya Muasasatul- Ilimiy, Beirut 2 Naqidhul-Washiah Uk: 376 “ “ “ 3 Tazama Majmaul-Bayaan Juz: 7 Uk: 366 (Tafsir ya aya 83 Suratu Namli) 3

11:44 AM

Page 3


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah)

3. HOJA ZA KUTHIBITI ITIKADI YA RAJA’A Hakika kazi ya kuthibitisha hoja na kutoa ushahidi juu ya hilo kuna hatua zifuatazo: a). Hatua ya kuthibitisha uwezekano wa raja’a na kutoshindikana kwake. Na bora ya yanayothibitisha uwezekano wake kwa kutazama hali halisi ni kwamba raja’a ni aina ya marejeo na haitofautiani nayo kwa chochote isipokuwa raja’a ni marejeo madogo yatakayotokea katika mwisho wa zama kwa baadhi ya watu, nao ni viongozi wa imani na ukafiri, na Mi’ad ni raja’a ya Akera itakayohusisha wanandamu wote, na kila ushahidi unaotolewa juu ya uwezekano wa miadi unafaa kuwa hoja juu ya uwezekano wa raja’a - hivyo hatua hii - ni hatua ya kiakili (kifikra) ya utafiti uliosheheni hoja za miadi vilevile, na unajitosheleza kutokana na ushahidi huo. b) Hatua za kuthibitisha kutogongana fikra ya raja’a na upande kati ya pande za itikadi ya kiislaam ambapo wakati mwingine fikra yenyewe inawezekana kulingana na hali halisi isipokuwa kuiamini kwake kunagongana au kunadhoofisha upande fulani kati ya pande za itikadi ya Kiislam. Je, raja’a inajitosheleza juu ya uthibitisho huu? Jawabu juu ya hilo: Hakika fikra ya raja’a inajumuisha uthibitisho huo kwa pande mbili: Fikra ya raja’a sio tu haigongani na upande kati ya pande za itikadi ya kiislaam bali inaipa kina, nishati na nguvu kubwa misingi mitano, hivyo ni udhihirisho unaodhihirisha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu usio na mpaka, uadilifu wa mfumo wa Unabii na kazi ya Uimamu na uhalisia wa marejeo ya Siku ya Kiyama. Hakika fikra hii ina utekelezaji katika umma na unabii uliotangulia Uislamu, na Qur’ani inasimulia utekelezaji huu kwa njia inayotia mkazo ambapo inaonyesha wazi kwamba fikra ya raja’a sio tu haigongani na 4

11:44 AM

Page 4


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) itikadi ya kiislam bali ni kati ya haja na mahitaji yake, hiyo ni kwa sababu Qur’ani tukufu haielezi yanayopingana na tawhidi na kuyatilia nguvu humo. Anayechunguza Qur’ani tukufu ataona kuwa haitosheki na kuashiria kwa ishara moja ya kupita kwa kupatikana mas’ala ya raja’a na kutokea kwake katika umma zilizotangulia Uislamu bali inarudiarudia ishara hii kwa namna ambayo inamaanisha kwamba inataka kutilia mkazo juu yake, ambapo inaonyesha kuwa fikra ya raja’a manufaa yake yanarejea kwenye tawhidi. Katika Suratul-Baqara tunasoma kauli Yake (s.w.t.): “Je, hukuona wale ambao walitoka majumbani kwao kwa maelfu kwa kuogopa mauti Mwenyezi Mungu akawaambia, kufeni, kisha akawahuisha, hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kwa watu lakini watu wengi hawashukuru.”4 Wafasiri wamepokea na kati yao ni Ibnu Jarir at-Twabariy riwaya nyingi kutoka kwa Ibnu Abbas, Wahab bin Munabbihi, Mujahidi, Sadiy na Atwai kwamba watu kutoka katika Bani Israil walikimbia kutoka kwa Twau’n na wakaingia katika kijiji chao Mwenyezi Mungu akawafisha na akapitia kwao Nabii anayeitwa Hezekieli akasimama kwa kutafakari katika jambo lao na miili yao ilishamalizika; Mwenyezi Mungu akamfunulia, je, unataka nikuonyeshe kupitia kwao vipi nitawafufua? Basi akawafufua kwa ajilli yake. Na Suyutwi amepokea mfano wa hayo.5 Pia tunasoma kauli Yake (s.w.t.): “Na mliposema: ‘Ewe Musa hatutakuamini hadi tumuone Mungu waziwazi,’ basi adhabu ikawachukua hali ya kuwa mnaaangalia kisha tukawafufua baada ya kufa kwenu huenda mkashukuru.”6 4 Suratul-Baqara: 243 5 Tafsir Twabariy Juz: 2, Uk: 586- 588, Durul Manthur Juz: 2, Uk: 741 chapa ya Darul-Fikir 6 Suratul-Baqara: 55 - 56

5

11:44 AM

Page 5


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) Na humo wamepokea wafasiri – kati yao ni Twabariy – kwamba walikufa wote pamoja baada ya kauli yao hiyo na Musa hakuacha kumuomba Mola Wake Mtukufu na kumbembeleza hadi akawarejeshea roho zao.7 Pia tunasoma kauli Yake (s.w.t.): “Au kama yule ambaye alipita katika mji uliokwisha kuwa magofu tu, akasema: ‘Vipi Mwenyezi Mungu atahuisha mji huu baada ya kufa kwake,’ Mwenyezi Mungu akamfisha miaka mia moja kisha akamhuisha, akamuuliza umekaa muda gani? Akasema, ‘siku moja au baadhi ya siku.’ Akasema: ‘Bali umekaa miaka mia, tazama chakula chako na kinywaji chako hakikuharibika, na tazama punda wako ili tukufanye kuwa ni hoja kwa watu, tazama mifupa vipi tutaihuisha na kuivika nyama. Ilipombainikia akasema: ‘Natambua kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.”8 Wafasiri wametaja – kati yao ni Twabariy – idadi ya riwaya zinazomaanisha kwamba Uzair au Armiya alipita katika Baitul-Maqdis baada ya kuharibiwa na Nabukhudh Naswir, Mwenyezi Mungu akamuonyesha uwezo wake juu ya hilo kwa kumpigia mfano katika nafsi yake kwa namna ambayo Aya imeeleza.9 Na kuna Aya zingine zinathibitisha kutokea raja’a baada ya mauti, akitaka Mwenyezi Mungu hayo kwa mwanadamu na wanyama, kati ya hizo ni: 1. “Tukasema: Mpigeni na baadhi yake vivyo hivyo Mwenyezi Mungu huhuisha wafu na kukuonyesha hoja zake huenda mtazingatia.”10 2. “Na aliposema Ibrahim, ‘Mola Wangu! nionyeshe namna gani unahuisha wafu.’ Akamwambia: Kwani huamini? Akasema, ‘hasha! Lakini ili moyo wangu utulie.’ Akasema chukua ndege 7 Tafsir Twabar Juz: 1 Uk: 290 - 293 8 Suratul-Baqara: 259 9 Tafsir Twabariy juz: 3 Uk: 28 - 47 10 Suratul–Baqara: 73 6

11:44 AM

Page 6


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) wanne watawanye (nyama zao) kisha weka katika kila mlima kipande kisha waite watakujia mbio na tambua kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.”11 3. “Aliposema Mwenyezi Mungu: Ewe Isa, hakika mimi nitakufisha na kukunyanyua kwangu na kukutoharisha kutokana na waliokufuru hadi Siku ya Kiyama, kisha kwangu ndio marejeo yenu nitahukumu baina yenu katika yale mliyokuwa mnahitalifiana.”12 4. “Sikuwaambia ila uliyoniamrisha kwamba mwabuduni Mwenyezi Mungu Mola wangu na Mola wenu na nilikuwa shahidi nilipokuwa nao na uliponifisha wewe ulikuwa ni mwangalizi juu yao na Wewe ni mwenye kushuhudia kila kitu.”13 Na katika mkusanyiko huu tunaona mkazo wa Qur’ani tukufu juu ya maana hii kupitia mkazo wa kutokea mara baada ya nyingine na katika nyakati tofauti katika kueleza matukio yaliyotokea katika umma zilizopita, jambo ambalo ni lazima nyuma yake kuna lengo linalokusudiwa na Qur’ani tukufu kupatikana, na lazima lengo hilo liwe ni kati ya ambayo manufaa yake yanarejea kwenye kadhia ya tawhidi na itikadi kwa namna ya kuzatiti na kutilia mkazo. Ni hatua ya kuthibitisha kutokea raja’a katika mustakabali wa umma wa kiislam kwa sababu uwezekano wa kitu ni jambo moja na kutokea ni jambo jingine. Je, katika Qur’ani tukufu na Sunna za Mtume (s.a.w.w.) hazionyeshi juu ya kwamba umma wa kiislamu utashuhudia kutokea raja’a katika mustakabali wake? Waumini wanajibu swali hili kwa ndio, kwa namna ya kukinaisha kwa kutegemea idadi ya aya za Qur’ani na Hadith za Nabii tukufu. Nazo ni: 11 Suratul–Baqara: 260 12 Suratu Al–Imran: 55 13 Suratul–Maida: 117 7

11:44 AM

Page 7


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) 1. Kauli Yake (s.w.t.): “Na siku tutakapokusanya kutoka kila umma kundi katika wanaokadhibisha Aya zetu nao watagawanywa mafungu mafungu.”14 Aya hii inazungumzia juu ya ufufuo utakaokuwa kwa ajili ya baadhi ya watu, na mfano wa ufufuo huu haiwezekani ukawa ni ufufuo wa Siku ya Kiyama kwa sababu ufufuo humo utakuwa ni wa jumla hivyo nini maana ya umahususi wa baadhi ya watu? Hususan Qur’ani inataja Kiyama baada ya aya tatu kutoka Aya hii kwa kusema: “Na siku litakapopulizwa parapanda na kufadhaika waliopo mbinguni na ardhini isipokuwa anayemtaka Mwenyezi Mungu, na wote watamjia wakiwa dhalili.” Hivyo alama za Siku ya Kiyama ziko wazi katika Aya hii bila ya ile nyingine, na kama Aya iliyotangulia ni ya Siku ya Kiyama basi ingekuwa ni kukariri bila ya sababu. 2. Kauli Yake (s.w.t.): ‘’Vipi mnamkufuru Mwenyezi Mungu na mlikuwa wafu akawahuisha kisha akawafisha kisha Kwake mtarejea.” 15 Na kwa upande wa hoja ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anataja uhai wa aina mbili kwa mwanadamu na baada yake ni kurejea Kwake, uhai wa kwanza ni uhai wa duniani, na uhai wa pili “Kisha atawahuisha” utakuwa baina ya uhai wa kwanza na baina ya kurejea kwake (s.w.t.) na haiwezekani kuwa ni Kiyama isipokuwa ni raja’a. 3. Kauli Yake (s.w.t.): “Mola Wetu umetufisha mara mbili na umetuhuisha mara mbili hivyo tumekiri dhambi zetu je, ipo njia ya kutoka.” 16 Upande wa hoja ni kwamba kufisha haiwi ila kwa aliyekuwa hai na kauli yao “umetufisha mara mbili” yaani kutokea kufisha mara mbili baada ya uhai wa kwanza unaofahamika na wala hakuna maana nyingine ya 14 Suratul-Namli: 83 15 Surutaul–Baqara: 28 16 Suratul–Muumini: 11 8

11:44 AM

Page 8


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) kufisha kwa mara ya pili isipokuwa kwa kupatikana uhai wa pili kisha wakafa baada ya hapo na kukusanyika uhai mara mbili na vifo viwili kama ilivyo katika Aya. Wapinzani wanapokea juu ya chanzo cha raja’a katika Aya hii taawili mbili ambazo hazisimami kwa hali yoyote ile. Baadhi yao wanasema: “Hakika maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu amewaumba wakiwa wafu kabla ya uhai! Na hii ni batili haiafikiani na lugha ya kiarabu, ambaye Mwenyezi Mungu amemuumba mfu haisemwi kuwa amemfisha. Na wengine wanasema: Mauti ya pili yatakuwa baada ya uhai wao katika makaburi kwa ajili ya kuulizwa na hii ni batili vile vile. Hivyo mwanadamu amejuta kwa yale yaliyompita na aya inaweka wazi majuto ya hawa juu ya yaliyowapita katika maisha mawili, hivyo huu si uhai wa kuulizwa”17 Huu ni muhtasari wa hoja za Qur’ani juu ya raja’a na kuna idadi kubwa ya Hadith kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) na Ahlul-Bait wake maasumina (a.s.), zimepokewa katika kuthibitisha raja’a, wamezitaja watu wa hadith wa Shia na wafasiri wao katika utunzi wao katika vitabu vya hadith na tafsiri hususan katika maudhui haya.18 17 Tazama al-Masa’ailu Saruwiyah cha Sheikh: Mufid Uk: 33 18 Baadhi ya watukufu wamevihesabu wakakuta ni zaidi ya vitabu arobaini kuhusu maudhui haya, na haya ni baadhi ya majina ya vitabu hivyo:- Kitabu cha Raja’a cha Abu Hamza al – Batwaiy Najashiy amemtaja Ithibati raja’a cha Ibnu Shadhan Kitabu Raja’a cha sheikh Suduq kitabu cha Raja’a cha Ayaash mwenye tafsiri (Ayaash) Ithibati raja’a cha Allammah al Hilly Al-Iqaadh cha Hurru al Amiliy nacho ni kitabu cha ufafanuzi kimesheheni zaidi ya 64 na hadith 600 rejea kuhusu hayo chapa ya markazi Risaalah. 9

11:44 AM

Page 9


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) Muhtasari huu ni kati ya hoja zilizotolewa juu ya kutokea raja’a katika zama za mwisho na vyovyote itavyowezekana unyenyekevu wa kielimu kuhusu jambo hilo kwa kiasi cha chini kabisa kinaifanya raja’a kuwa ni fikra yenye kukubalika, hivyo basi kuna uwanja mpana kwa mpinzani na ni juu yake kuleta dalili, pia yawezekana asilete dalili; lakini haikubaliki katika mantiki kudharau fikra za wengine na itikadi zao ambazo wameziamini kutokana na hoja na dalili.

WANAPINGA NA TURATHI ZAO ZINAKUBALI Ambaye anasoma maneno ya wapinzani wa Ahlul-Bait (a.s.) katika mas’ala ya raja’a anapata picha kwamba wao wako mbali sana na yanayopatikana katika turathi zao na mtazamo wao wa kifikra, lakini anayesoma turathi hizi anaona humo kunapatikana kiasi kikubwa cha riwaya na habari hizi ambazo zinaonyesha kuwepo itikadi hizi kwao zenye msingi na madhumuni ya fikra ya raja’a. Imethibiti katika vitabu vya historia ya kiislam kwamba habari ya kufariki Nabii (s.a.w.w.) ilipoenea kwa Waislamu Umar bin al-Khatab alisimama na kusema – kutokana na miji fulani fulani ya kirumi - “Hakika Nabii hatokufa hadi tuifungue na lau akifa tutamsubiri kama Bani Israil walivyomsubiri Musa.” Na alikuwa anasema: ‘Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu hajafa lakini ameenda kwa Mola wake kama alivyokwenda Musa bin Imran hivyo akaghibu kwa kaumu yake siku arobaini kisha akarejea baada ya kusemekana amekufa, Wallahi Mtume wa Mwenyezi Mungu atarejea na atakata mikono na miguu ya watu waliodai kuwa amefariki.’’19 Na wala sio Abdullah bin Saba’a mtu wa kuzua ambaye inanasibishwa kwake kila tuhuma katika historia ya kiislamu. Ibnu Abi Duniya aliyefariki 281 A.H ametunga kitabu kwa anuani: “ an a’asha baadal-mauti” kitabu hiki kimechapishwa kwa kuhakikiwa na 19 Siratu Nabawiyah ya Ibnu Hishaam Juz: 4, Uk: 305, Twabaqaatul Kubra ya Ibnu Sa’ad Juz: 2, Uk; 266 10

11:44 AM

Page 10


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) Darul-Kutubil-Islamiyah ya Beirut mwaka 1987. Na Abu Nuaym al-Isfahaaniy ametunga kitabu maalum cha Dala’ailunNubuwah na Suyutiy katika “Al-Khaswaisul-Kubra” mlango maalum katika miujiza ya Nabii (s.a.w.w.) katika kuhuisha wafu, na Suyutiy ametaja karama katika kuhuisha wafu kwa asiyekuwa Nabii. 20 Na wamepokea kwamba Zaid bin Harith, Rabi’u bin Kharash na mwanaume katika Answar walizungumza baada ya kufa.21

MASWALI KUHUSU ITIKADI YA RAJA’A Fikra ya raja’a inakabiliwa na maswali mengi yanayohitaji majibu ya wazi nayo ni: Je, hakika itikadi ya raja’a inasababisha kuchochea maasi kwa kutaraji toba baada ya kurejea? Jawabu: Hakika swali hili litakuja ikiwa raja’a itajumuisha watu wote au kama kuna kuainisha majina ya watu watakaorejea ambapo mambo sio hivyo, raja’a ni mahususi kwa viongozi wa ukafiri na viongozi wa imani na hakuna anayeweza kuwaainisha hawa kwa majina yao, mambo yote yako kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na haya yanatosha kutochochea maasi. Hakika itikadi ya raja’a inamaanisha tanasasukh (roho kuhamia katika kiumbe kingine) ambayo ni batili kwa dharura ya Uislam? 20 Sheikh Abdul Husein Al-Aminiy amefanya utafiti mpana katika juzuu ya kumi na moja katika Al-Ghadir uk. 103–195 humo amepokea riwaya za kisuni zikionyesha kuwa kuna ghuluu na nyingi kati ya hizo zinabeba maana ya raja’a 21 Tahadhibut-Tahadhib Juz. 3, Uk. 410 na nyinginezo nyingi 11

11:44 AM

Page 11


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) Jawabu: Tanasukh (roho kuhamia katika kiumbe kingine) ni jambo moja na raja’a ni jambo jingine linalotofautiana nalo kabisa, tanasukh inamaanisha roho za wafu kurejea katika viwiliwili vingine vinavyotakiwa kuishi, wakati raja’a ina maana ya kurejea roho za badhi ya watu, kurejea katika viwiliwili vyake kwa lengo la yale yatakayotokea Siku ya Marejeo na katika Isa kuhuisha wafu ni yaliyotokea kati ya raja’a katika umma zilizotangulia. Na imepokewa kwa tawatur kutoka kwa Maimamu (a.s.) ubatili wa tanasukh (roho kuhamia katika kiumbe kingine) na maulamaa wa Shia wametilia mkazo zamani na sasa juu ya hilo na kwamba inasababisha kufuru, na Abu Hasan al-Ashiariy ametofautisha katika kitabu chake “Maqaalatul-Islaamiyiina” baina ya kauli ya Shia katika raja’a na baina ya kauli za wazandiki wanaokanusha Kiyama.22 Hakika itikadi ya raja’a inasababisha kudhihiri uyahudi katika Ushia na hayo ni aliyoyasema Ahmadi Amini katika kitabu chake “Fajrul-Islaam” Jawabu: Hakika kudhihiri mafunzo ya dini zilizotangulia katika dini ya kiislamu ni jambo linalokubalika katika itikadi ya kiislamu, kwa sababu Uislamu umefuta utendaji wa dini zote zilizotangulia, ama upande wa kiitikadi ni jambo lililothibiti kwamba dini zote zimeshirikiana, na Uislamu ndio kauli ya sawa na kamilifu zaidi kuliko zote. Kupatikana itikadi ya dini iliyotangulia katika itikadi ya kiislam sio dosari katika Uislamu, hii ni ikiwa raja’a ni katika rai za kiyahudi kama anavyoadai mwandishi huyu. Itikadi ya tawhidi, unabii, ufufuo, hisabu, Pepo na Moto ni kati ya itikadi zinazoshirikiana baina ya dini zote, bali itakuwa ni jambo la aibu kuiga itikadi batili aliyoingiza myahudi au mnasara au wengineo miongoni mwa dini. Raja’a sio katika aina hii kwani Qur’ani imezungumza katika aya nyingi na imetupa mifano mbalimbali. Vipi kauli ya raja’a itakusanyika na kauli yake (s.w.t.) “Na haiwi kwa mji 22 Tazama: Maqaalatul–Islamiyiina juz: uk: 114 12

11:44 AM

Page 12


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) tuliouangamiza ya kwamba wao hawatarejea.”23 Aya hii inakiri kutorejea madhalimu, je tutasema kurejea baadhi yake hiyo itakuwa ni kupinga Aya tukufu? Jawabu: Hakika kauli ya raja’a haipingi Aya hii, kwani aya hii inazungumzia juu ya aina mahususi ya madhalimu nao ni ambao wameangamizwa duniani na wamepata adhabu ya mbinguni humo. Ama madhalimu ambao wameondoka duniani bila ya adhabu wala kuchukuliwa hatua aya haijasema chochote kwao, na huenda kunyamaza kwake kunamaanisha aina hii ya kuafiki fikra ya kurejea kwao au kurejea baadhi yao kati ya wale aliowateua Mwenyezi Mungu katika raja’a kati yao.

MATOKEO Raja’a sio jambo lisilowezekana kwa dhati yake na wala haipingi msingi wa tawhidi bali ni udhihirisho wa uwezo wa Mwenyezi Mungu usio na kikomo, hii ni kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine hakika mfano wa msingi wa raja’a umetokea kivitendo na Qur’ani imeshazungumza juu yake - kama ambavyo wajuzi wa Uislam wameamini kurejea baadhi ya wafu duniani baada ya kufariki kwao – na katika upande wa watatu zinapatikana habari nyingi kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s.) baada ya kuwezekana kutoa hoja kwa aya nyingi za Qur’ani juu ya kuthibiti kwake, hiyo ni kama baadhi ya masharti ya Kiyama na kama aina ya marejeo ambayo makafiri hawayakubali, kisha sio katika misingi ambayo juu yake hujengewa dini au madhehebu.

23 Suratul – Anbiyai: 95 13

11:44 AM

Page 13


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah)

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na Nne Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda 14

11:44 AM

Page 14


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah) 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60.

Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) 15

11:44 AM

Page 15


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

Urejeo (al-Ra'ah) 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92.

Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Shahidi kwa ajili ya Ubinadamu Utokezo (al - Badau) Kuanzia ndoa hadi kuwa wazazi Myahudi wa Kimataifa Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 16

7/15/2011

11:44 AM

Page 16


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

Urejeo (al-Ra'ah) 93.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

94.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

95.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

96.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

97.

Hadithi ya Thaqalain

98.

Fatima al-Zahra

99.

Tabaruku

100.

Sunan an-Nabii

101.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

102.

Idil Ghadiri

103.

Mahdi katika sunna

104.

Kusalia Nabii (s.a.w)

105.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

106.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

107.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

108.

Ujumbe - Sehemu ya Nne

109.

Shiya N’abasahaba

110.

Iduwa ya Kumayili

111.

Maarifa ya Kiislamu.

112.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

113.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

114.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

115.

Ukweli uliopotea sehemu ya Nne

116.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

17

7/15/2011

11:44 AM

Page 17


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

7/15/2011

Urejeo (al-Ra'ah)

BACK COVER Raj'ah (Urejeo) sio jambo lisilowezekana kwa dhati yake na wala haipingi msingi wa Tawhidi, bali ni udhihirisho wa uwezo wa Mwenyezi Mungu usio na kikomo - hii ni kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine, hakika mfano wa msingi wa Raj’ah umetokea kivitendo na Qur’ani imeshazungumza juu yake - kama ambavyo wajuzi wa Uislamu wameamini kurejea baadhi ya wafu duniani baada ya kufariki kwao. Haya ni maneno ya mwaandishi wa kitabu hiki ambaye amejaribu kufafanua maana ya Urejeo (Raj’ah) na matokeo yake kwa kutumia mifano kutoka aya za Qur’ani na Sunnah. Ili kumuelewa zaidi, fuatana naye kwenye uandishi wake huu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

18

11:44 AM

Page 18


RAJA’A - PROOFRREAD BY R.S.K.SHEMAHIMBO - 05 - 02 - 2009 Final D.Kanju.qxd

Urejeo (al-Ra'ah)

19

7/15/2011

11:44 AM

Page 19


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.