Vikao vya furaha

Page 1

Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page A

VIKAO VYA FURAHA Ni Mfululizo wa Masuala ya Kisheria

Kimeandikwa na: Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu.

Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa Kea.


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

B

7/16/2011

12:39 PM

Page B


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page C

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 -77 - 5

Kimeandikwa na: Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu.

Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa Kea.

Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab

Toleo la kwanza: Januari, 2011, Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page D

YALIYOMO Uislamu na Vikao vya Furaha……………………………………….........2 Aina ya Kikao………………………………………………………..........4 Vidhibiti vya Kisheria Kuhusu Aina ya Kikao……………………............4 Mambo Mahsusi ya Sehemu…………………………………....................4 Kujiepusha Kuchanganyika pamoja Baina ya Wanaume na Wanawake……………………………………………………...................5 Vazi la Kuhudhuria…………………………………………......................6 Mavazi Yenye Kuonesha Maungo………………………...........................6 Vita vya Kitamaduni………………………………………........................6 Nguo za Umashuhuri……………………………………….......................8 Kujishauwa………………………………………………..........................9 CHAKULA CHA HARUSI……………………………………..............9 Kutowaalika Matajiri Pekee…………………………………..................10 Kufanya Ikhlas kwa Mwenyezi Mungu katika Mwaliko……..................11 Kutofanya Ubadhirifu na Ufujaji wa Chakula……………….................. 11 Ufupisho wa Vidhibiti vya Kisheria………………………………..........12 Wimbo ni nini………………………………………………………........12 Nyimbo katika Qur’ani Tukufu na Hadithi Takatifu……………….........14 Usemaji wa Uovu……………………………………………..................15 Mazungumzo ya Upuuzi……………………………………...................15 Ni Aina ya Batili……………………………………………....................16 Ni Shirki Iliyojificha………………………………………......................16 Athari za Nyimbo Ndani ya Moyo wa Binadamu……………….............17 Nyumba inayoimbwa Nyimbo…………………………………..............18 Nyimbo katika Vikao vya Furaha……………………………….............19 Pili: Muziki………………………………………………………...........20


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page E

Vikao vya Furaha Muziki Uliyoharamu…………………………………………….............20 Ngoma za Kimila………………………………………………...............21 Hukmu ya Vyombo vya Muziki………………………………….............22 Uuzaji na Ununuaji wa Vyombo vya Muziki……………………............23 Hukmu ya Kujifunza Muziki…………………………………….............23 Makosa katika Uchanganuaji…………………………………….............24 Tatu: Uchezaji na Upigaji Makofi………………………………............25 Uchezaji………………………………………………………….............25 Hukmu ya Kisheria Kuhusu Uchezaji…………………………...............25 Uchezaji wa Wanandoa…………………………………………..............27 Mwanamke Kucheza Mbele ya Wanaume………………………............27 Kupiga Makofi Vikaoni………………………………………….............28 Ufupisho wa Madhumuni ya Kikao……………………………...............29 Upigaji Picha Vikaoni…………………………………………................31 Hukmu ya Upigaji Picha za Filamu……………………………..............31 Uhudhuriaji Katika Vikao Vinavyopigwa Picha………………................33 Kuangukia katika Mambo ya Haramu…………………………...............33 Mwanaume Kupiga Picha katika Vikao vya Wanawake na Mwanamke kupiga Picha katika Vikao vya Wanaume……………..............................34 Kupiga Picha Uchezaji na Unenguaji……………………………............34 Viathiri vya Sauti katika Filamu………………………………................34 Usafishaji wa Filamu…………………………………………….............35 Usambazaji wa Picha na Filamu………………………………................35

E


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page F

Vikao vya Furaha

Neno la Mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Majalisu ‘l-Afrahi. Sisi tumekiita, Vikao vya Furaha. Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika nyanja zote za maisha yake. Kitabu hiki kinazungumzia taratibu na kanuni za kufutwa katika mikusanyiko ya sherehe, kwani mara nyingi watu hukiuka taratibu hizi na kwenda kinyume na maadili ya Kiislamu. Mwandishi wa kitabu hiki ameainisha taratibu na kanuni zote zinazofaa kufuatwa katika mikusanyiko hii na ambazo hazivunji misingi na maadili ya dini. Vilevile ameainisha mambo yale ambayo hayafai kufanywa katika mikusanyiko hii ambayo huvunja misingi na maadili ya dini. Kwa hakika, katika kitabu hiki mwandishi amewahimiza Waislamu kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu na maadili ya dini ili wasipotee katika upotofu na waifuate njia iliyonyooka. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania. F


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page G

Utanguluzi Sifa njema zote zinamstahiki Mola wa viumbe, kisha rehema na amani zimfikie mbora wa Mitume na mwisho wa Manabii, AbalQasim Mtume wetu Muhammad na Aali zake watukufu masumina. Kwa hakika kati ya vikao vingi vinavyowekwa hupatikana maswali chungu nzima kuhusiana na suala hili, ni vikao vya furaha ambavyo huwekwa kwa matukio mbali mbali ambapo watu hupata burudani kama vile sherehe za ndoa, kuzaliwa watoto n.k. Swali: Kuna hukmu gani kuhusu vikao hivyo? Ni madhumuni gani ambayo hufaa kuangaziwa katika vikao hivyo? Na upi wigo ambao sheria imeweka ili kuhifadhi hilo? Je! Ni matumizi gani ambayo sheria imeruhusu, au imekataza mambo gani ndani ya vikao hivyo au nje ya vikao hivyo? Jibu: Maswali hayo na yale yanayofanana na hayo ni kati ya maswali mengi ambayo tutajaribu kuyatolea majibu katika kitabu hiki, tunamuomba Mola Muweza atie furaha nyoyo za waumini, na tusiwe na huzuni Siku ya Qiyama, siku ambayo haitomfaa mtu mali wala watoto ila mwenye kwenda kwa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa moyo wake umesalimika‌

Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu.


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 1


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 2

Vikao vya Furaha

UISLAMU NA VIKAO VYA FURAHA Uislamu umekuja kuwaongoza na kuwaelekeza watu katika hali iliyo nzuri, na kuwapatia wema na uhakika wa daima, na sio starehe za muda mfupi, kwa hakika Uislamu umeruhusu suala la furaha, bali umehimiza suala la uingizaji furaha nyoyoni mwa waumini, Mwenyezi Mungu (a.j) ameweka malipo makubwa kuhusiana na hilo. Imekuja katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s.) kwamba siku moja alimuuliza mmoja wa masahaba wake hivi: Ni kiwango gani mnafurahishana nyinyi kwa nyinyi? Sahaba akajibu: Ni mara chache sana, Imam (a.s.) akasema:

“Kwa nini hamfanyi hivyo!! Hakika kufurahishana ni miongoni mwa tabia njema, ingiza furaha moyoni mwa ndugu yako, kwani alikuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akicheza na mtu kwa lengo la kumfurahisha.” 1 Na imekuja katika hadithi nyingine kutoka kwake (a.s.) amesema:

“Mwenye kumfurahisha mu’mini kwa hakika amenifurahisha mimi, na mwenye kunifurahisha mimi amemfurahisha Mtume na mwenye kumfurahisha Mtume kwa hakika amemfurahisha Mwenyezi Mungu, na mwenye kumfurahisha Mwenyezi Mungu atamuingiza peponi.”2 1 Al-Kaafi, Juz. 2 uk. 663 Darul-Kutubi Islamiyya Akhundi cha Sheikh Kulain.

2 Fiqhu Ridha uk. 374 kuhusu Imam Ali, Muassasat Ahlul-bayt cha Ibn Baabaway. 2


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 3

Vikao vya Furaha Na imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s.) amesema: “Katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyozungumza na Musa (a.s.) alisema:

“Ninao waja ambao nimewahalalishia pepo yangu pia tutawadumisha humo, Musa (a.s.) akasema: Ni nani hao ambao umewahalalishia pepo yako na kuwadumisha humo? Akasema: Ni yule mwenye kuingiza furaha ndani ya moyo wa mu’mini.”3 Hakuna shaka kwamba kwa kawaida vikao ambavyo waumini huviweka kwa ajili ya furaha zao na hafla zao nzuri vinaruhusiwa, lakini hubakia maelezo kuhusiana na vidhibiti vya ujumla na madhumuni maridhawa, kwa hivyo tutalieleza hilo katika kurasa zifuatazo akipenda Mwenyezi Mungu.

3 . Bihar Anwar juz. 13 uk. 356 kuhusu Imam Muhammad Baqir, Muassasat Ahlul-bayt cha Majlisi. 3


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 4

Vikao vya Furaha

SEHEMU YA KWANZA: AINA YA KIKAO Maelezo: Kwa hakika vikao ambavyo huwekwa kwa lengo la kufurahishana kama vile suala la ndoa, kuzaliwa watoto na mengineyo….. Ni miongoni mwa masuala ambayo mara nyingi watu huyafanya katika mikusanyiko yao hali kadhalika katika sherehe zao, na ikiwa hawatozingatia vidhibiti vya kisheria ambavyo ni lazima vichungwe na kuzingatiwa katika sherehe hizo, kwa hakika watakabiliwa na hatari ya kuangukia katika maasi, pia kukasirikiwa na Mola Manani, na maana ya vidhibiti ni kufurahika katika silka iliyo salama, nayo huchukua jukumu la kupunguza hatari hizi, ili furaha iwe halisi yenye kuendelea duniani na akhera. Ni lazima vichunguzwe vidhibiti hivyo kuhusu aina ya kikao na yale yanayofungama nayo, aidha huduma inayotolewa hapo kama vile chakula, vinywaji…

VIDHIBITI VYA KISHERIA KUHUSIANA NA KIKAO Miongoni mwa vidhibiti vilivyo muhimu sana ambavyo hapana budi vizingatiwe kuhusiana na mazingira ya kikao cha furaha ni:

VIGEZO MAHSUSI VYA SEHEMU Sehemu na mahala panapofanyika kikao huenda pakawa na vigezo maalum, sehemu ambayo hutumiwa katika mambo ya furaha za haramu, hususan pakiwa mashuhuri na panajulikana kuwa ni mahala pa mambo maovu, machafu, ufasiki na ufisadi. Ayatullah Khamenei anasema: “Na huenda ikawa aina ya sherehe za ngoma, muziki au maneno mabaya yasemwayo hapo, au ubaya wa sehemu na mambo 4


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 5

Vikao vya Furaha mengine ambayo yanahusiana na muziki chini ya anwani ya muziki wenye kuvutia wa kipuuzi ulio haramu, au chini ya anwani nyingine ya haramu, kama ikiwa kutokana na mambo hayo yenye kusababisha kupatikana maovu.”4 Inapasa mazingira ya sehemu husika yasipatikane aina yoyote ile ya maasi, na hilo husaidia katika kuhifadhi vidhibiti vya kisheria.

KUJIEPUSHA KUCHANGANYIKA PAMOJA BAINA YA WANAUME NA WANAWAKE Hakika kuchanganyika pamoja baina ya wanaume na wanawake kwa ujumla ni mazingira ambayo huchochea zaidi kutokea mmomonyoko mkubwa wa maadili na upotokaji wa nafsi, na ambayo kwa njia moja au nyingine yatamwathiri mtu katika hali mbili; kitabia na kinafsi, katika hali ambayo huikuta nafsi yake katika hali fulani akiwa amepoteza nguvu zote za nafsi za kujizuia na maovu, nguvu ambazo humkinga yeye kutokana na vishawishi vya shetani na nafsi yenye kuamrisha maovu. Na kuanzia hapa ni juu jetu tujihadhari kuandaa mazingira na tangulizi ambazo kwa njia moja au nyingine zitatuingiza katika haramu, kwa namna ambayo kikao kitakavyokuwa pamoja na kuzuia muingiliano wa kuchanganyika baina ya wanaume na wanawake katika vikao husika, miongoni mwa yale ambayo hutoa mwanya wa kuangaliana au kusikiliza haramu na mengineyo. Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam Ali (a.s.) amesema: “Macho ni mitego ya shetani.”5 4 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 21; Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 5Miizanul-Hikma, Juz. 4, uk. 3288 Darul-Hadithi cha Muhammad Rey Shahri. 5


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 6

Vikao vya Furaha Kikao cha wanawake kinatakiwa kiwe mbali na kikao cha wanaume, umbali ambao sauti zao haziwafikii wanaume. VAZI LA KUHUDHURIA: Wahudhuriaji wa kikao cha furaha kama vile cha harusi n.k wanatakiwa kuzingatia vigezo vya kisheria vinavyohusiana na muonekano wa nje, ikiwa pamoja na kuvaa mavazi ambayo Mwenyezi Mungu (a.j) amewahalalishia waja Wake, aidha kujiepusha na mavazi ambayo yameharamishwa, na yale ambayo hayamfai mu’mini. Tutayaeleza hayo lua kwa ufupi, ambapo tutaona jinsi gani sheria inavyokataza baadhi ya mavazi, kama vile: Mavazi Yenye Kuonesha Maungo: Ni mavazi ambayo huonesha viungo vya mwili kutokana na kubana kwake, au hueleza yale yaliyo ndani yake, au kudhihirisha kiungo miongoni mwa vile ambavyo ni haramu mwanamke kuvidhihirisha mbele ya mwanaume ajinabi, iwapo mwanamke atakuwa katika hali ambayo ataonekana na mwanaume haifai kwake kuvaa nguo ambazo kutokana na rangi yake au mtindo wake au namna ya uvaaji wake zitaleta mvuto wa uangaliaji wa mwanaume ajinabi na kusababisha fitna na uovu.6 Ama ikiwa mwanamke ana imani na uhakika kwamba haonekani na macho ya wanaume ajinabi kutokana na yale ambayo huenda yakaleta au kusababisha maovu si vibaya kwayo.7 2) Vita Vya Kitamaduni: Kuna baadhi ya mavazi ambayo yanalingana na tamaduni za kimagharibi na ufisadi, nayo ni matokeo ya propaganda na usambaza6 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 100 Daru-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 7 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 99 Daru-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 6


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 7

Vikao vya Furaha ji ambayo huenda hayo yakamsukuma mu’mini kuvaa mfano wa mavazi hayo akiwaiga watu wa Magharibi, na uenezaji wa tamaduni zao na shakhsia zao kupitia waimbaji na wengineo. Swali: Je! Inaruhusiwa mwislamu kufuata aina yao ya kujipamba au kuwaiga wao katika mavazi au unyoaji wa nywele? Jibu: Hakika kuwahifadhi wavulana na wasichana kuhusiana na muonekano wao katika kujipamba hata katika sherehe maalum kama vile kuzaliwa watoto, harusi na mambo mbali mbali ya furaha, hicho ni kikwazo ambacho huwazuia wao kutokana na tamaduni za kimagharibi zenye kuhujumu umma wetu kwa kuenea kwake, hususan zama hizi ambazo maadui hufanya kila waliwezalo ili kuteka nyara fikra za wavulana na wasichana, aidha huchochea akilini mwao kupitia vyombo vya habari vyenye kuonesha picha, au kwa njia ya sauti, hali kadhalika kutumia vyombo vya kisasa vya mawasiliano kama vile tovuti, baruapepe… na hakuna shaka kwamba uenezaji wa tamaduni wa kimaada na uovu utakuwa na taathira mbaya na kubwa katika jamii, katika dhamira na mustakabali wake, hata jamii ibadilike kidogo kidogo ili apate hasara mwenye kuhudhuria na awe rehani mikononi mwa nguvu kubwa hizo, bali hufuata na huangamiza tija yake, ni dhahiri hilo ni uhalisia wa hadithi Qudusi iliyopokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s.) amesema:

“Hakika Mwenyezi Mungu alimfunulia mmoja wa manabii wake, waambie waumini: Msivae mavazi ya maadui zangu, msile chakula katika migahawa ya maadui zangu, wala msipite njia za maadui zangu

7


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 8

Vikao vya Furaha mtakuwa ni maadui zangu kama vile walivyo wao maadui zangu.”8 3) Nguo za Umashuhuri: Ni yale mavazi ambayo yanamfanya mtu awe dhihirisho la maneno ya watu, kumfanyia istihizai, kebehi na kumzungumzia yeye, na hakika zipo hadithi chungu nzima zinazoharamisha aina hiyo ya mavazi. Imekuja katika hadithi kwamba siku moja Ubadu bin Bakr Baswri aliingia kwa Imam Swadiq (a.s.) akiwa amevaa nguo nzito za umashuhuri, Imam (a.s.) akasema: “Ewe Ubadu ni nguo gani hizo?! Akasema: Ewe Abu Abdullah unazitia kasoro hizi? Imam (a.s.) akasema: Ndio, Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Mwenye kuvaa nguo za umashuhuri duniani Mwenyezi Mungu atamvalisha nguo za udhalili siku ya Kiyama.”9 Vivyo hivyo ni haramu kwa mwanaume kuvaa mavazi ya kike na mwanamke kuvaa mavazi ya kiume. Zimepokewa hadithi chungu tele zenye kukemea aina hiyo ya mavazi, na pia mwenye kuvaa mavazi hayo. Imekuja katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s.) amesema: Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Mwenyezi Mungu amemlaani mhalalishaji, aliyehalalishiwa, mwenye kumtawalisha kiongozi asiyestahili, mwenye kudai nasaba 8. Wasail Shiia juz. 3 uk. 279 Daru Ihyau Turaathi Beirut cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 9 Biharul-Anwar, Juz. 76 uk. 316 kuhusu Imam Muhammad Baqir, Muassasat AlWafai chapa ya pili iliyosahihishwa cha Majlisi. 8


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 9

Vikao vya Furaha hali ya kuwa hajui, wanaume wenye kujifananisha na wanawake na wanawake wenye kujifananisha na wanaume.”10 Na imekuja katika hadithi nyingine kutoka kwa Imam Ali (a.s.) amesema: “Watoeni hao majumbani mwenu, kwani wao ni kitu kichafu mno.”11 4) Kujishaua Kujishaua ni hali ya wanawake kujipitisha pitisha mbele ya wanaume ajinabi, nalo ni miongoni mwa mambo ambayo yameelezwa na Qur’ani tukufu kwa namna ambayo Mwenyezi Mungu (a.j) katika aya zake anasema kinaga ubaga:

“Na kaeni majumbani mwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani…” (33:33) na kigezo cha kisheria katika yale ambayo mwanamke hujipodoa kwa lengo la kuwa mrembo kwamba; “Pindi ikisadikika katika mazoea ya watu kwamba rangi ni pambo, basi haifai mwanamke kuidhihirisha mbele ya mwanaume ajinabi.”12 Na inawezekana mwanamke kujishauwa ikiwa hatokuwepo mwanaume ajinabi anaye mwangalia.

CHAKULA CHA HARUSI Miongoni mwa mambo ya kisheria ya sunna yaliyokokotezwa ni suala la uandaaji wa chakula siku ya harusi au usiku wake, kwani hiyo ni sunna nzuri iliyo mashuhuri. Imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume 10. Wasail Shi’ah, Juz. 17 uk. 284 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan cha Al-Hurru Amily. 11. Wasail Shi’ah, Juz. 17 uk. 285 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 12. Ajwibatul-Itiftaat Maktaba ya Ayatullah Khamenei iliyoko Qum katika Tovuti nambari 922. 9


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 10

Vikao vya Furaha (s.a.w.w.) amesema:

“Hakiandaliwi chakula cha sherehe ila katika mambo matano; Harusi, Kuzaliwa mtoto, Kuhitimu, Ununuzi wa nyumba na Kurejea Hijja.”13 Na inapaswa katika uandaaji wa chakula yazingatiwe baadhi ya mambo ambayo yametiliwa mkazo na hadithi kwayo, kwa ufupi ni kama yafuatayo: Kutowaalika Matajiri Pekee: Wapo baadhi ya watu mwaliko wao huwahusisha matajiri na wale wenye hadhi kubwa tu, na wala hawawaaliki mafakiri, chakula cha aina hiyo ambacho mafakiri hawapewi nafasi ya kushiriki na kuhudhuria, bali huachwa nje na kufungiwa milango, na milango hiyo hufunguliwa matajiri pekee, bila shaka hiyo ni aina inayochochea utabaka unaochukiwa, aidha huweka vizuizi na vikwazo baina ya waumini. Sherehe za chakula mfano wa sherehe hizo huwa ni sherehe duni na za hali ya chini kabisa, wala hazina thamani wala hadhi, pia hazipendwi na Mwenyezi Mungu (a.j). Kwa hakika imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Sherehe mbaya zaidi ni zile ambazo hualikwa matajiri tu na huachwa kualikwa mafakiri.”14 13 Tahrirul-Wasiilat, Juz 2, uk. 238 Darul-Kutubi ilmiyya Ismailiyaan Qum cha Ruhullah Musawy Khomeini. 14 Tahrirul-Wasiilat, Juz 2, uk. 238 Darul-Kutubi ilmiyya Ismailiyaan Qum cha Ruhullah Musawy Khomeini. 10


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 11

Vikao vya Furaha Mwaliko Uwe wa Ikhlaas kwa Mwenyezi Mungu Imekuja katika hadithi nyingine kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Mwenye kulisha watu chakula ili aonekane au apate sifa, Mwenyezi Mungu atamlisha moto wa Jahannam mfanowe, na atafanya chakula hicho kuwa ni moto tumboni mwake hadi ahukumiwe baina ya watu.”15 Kutofanya Ubadhirifu na Ufujaji wa Chakula Wapo baadhi ya watu huandaa chakula kingi ambacho huzidi maradufu ya mahitaji ya watu, na sherehe inapomalizika hukimwaga katika shimo la taka, tendo hilo ni ubadhirifu na ufujaji katika utumiaji wa mali, kuhusu hilo Mwenyezi Mungu (a.j) anasema:

“Na umpe jamaa haki yake, na masikini na msafiri wala usitawanye (mali yako) kwa ubadhirifu. Hakika watumiao kwa ubadhirifu ni ndugu za mashetani na shetani ndiye mwenye kumkufuru Mola wake.” 17:26-27 Na katika aya nyingine anasema: 15 Wasail Shi’ah, Juz. 42, uk. 312 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 11


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 12

Vikao vya Furaha “Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo, wala hawafanyi ubakhili na wanakuwa waadilifu baina ya hayo.” 25:67 Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam Swadiq (a.s.) alipokuwa akitoa maelezo kuhusu aya hiyo: “….. basi akachukua gao la changarawe akashika mkononi mwake, hapo akasema: Huku ni kufanya ubakhili ambao Mwenyezi Mungu ameutaja katika kitabu chake, kisha akachukua gao lingine akamwaga lote, hapo akasema: Huu ndiyo ubadhirifu, kisha akachukua gao lingine akamwaga baadhi na akabakisha baadhi akasema: Huu ndiyo uadilifu.”16 Pindi mtu anapofanya sherehe lengo lake huwa ni kumridhisha Mwenyezi Mungu (a.j) na kupata malipo kutoka kwake, ila matendo hayo na yale yanayofanana na hayo huenda yakakosa baraka na kuwa ndiyo kikwazo na kizuizi cha kupata radhi za Mola Manani. MUHTASARI WA VIDHIBITI VYA KISHERIA Tunafupisha vizidhibiti vya kisheria kuhusiana na aina ya kikao kama ifuatavyo: Kuelewa vipengele vya kikao (yaani isiwe ni sehemu ya upuuzi na sherehe za haramu). Kutochanganyika pamoja baina ya wanaume na wanawake. Kutovaa mavazi yafuatayo: Mavazi ya Umashuhuri. Yanayoingia katika vita vya kitamaduni. Hariri kwa wanaume. Mavazi yanayoonesha maungo ya wanawake. Wanawake kuchunga kudhihirisha shauwo mbele ya mwanaume ajinabi. Ni suna kuandaa chakula cha harusi, nayo ni sunna iliyopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 16. Miizanul-Hikma juz. 2 uk. 1295 Darul-Hadith chapa ya kwanza cha Muhammad Rey Shahri. 12


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 13

Vikao vya Furaha

SEHEMU YA PILI: MADHUMUNI YA KIKAO. Kikao kina aina zake, vigezo vyake na vidhibiti vyake mahsusi, kwa hakika madhumuni ya kikao yana hadhi kubwa kulingana na vidhibiti vya kisheria, katika sehemu hii tutalieleza hilo kwa urefu na mapana tukishikamana na rai ya sheria takatifu humo. Na suala la madhumuni ya kikao huhusisha anwani kadhaa wa kadha, tunaeleza madhumuni hayo kama ifuatavyo:

KWANZA: WIMBO Wimbo ni nini? “Wimbo ni sauti ya mtu ikiwa yatoka kwa kurindima yenye kurandana pia huburudisha, ambayo huambatana na vikao vya upuuzi na maasi.�17 Na makusudio ya kurandana ni kule kupanda na kushuka kwa mfumo maalum wenye kufuatana, ama kuburudisha ni hali ya kukonga nyoyo. Swali: Ipi hukmu ya kisheria kuhusu uimbaji? Jibu: Kuimba ni haramu kabisa, haifai kuimba wala kusikiliza nyimbo za haramu, iwe kwa mwanaume au mwanamke, iwe moja kwa moja au kwa njia ya kasseti, iwe inaambatana na vyombo vya muziki au hapana.18 17 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 22 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 18 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 25 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 13


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 14

Vikao vya Furaha Na huenda baadhi ya watu wakadhani kwamba ni haramu kusikiliza nyimbo akiwa na wengine, si vibaya pale anapokuwa faraghani peke yake, au pale asipoathirika na madhumuni yake, kwa hakika hilo ni kosa kwani Mwenyezi Mungu (a.j) ameharamisha nyimbo kwa hali zote isipokuwa katika hali moja ya nyimbo za wanawake kumhusu Bi harusi. Na ufupisho wa hilo ni kwamba: Ni haramu kusikiliza nyimbo sawa iwe mtu anasikiliza nyumbani kwake peke yake au akiwa pamoja na wengine, sawa zitamuathiri au hapana.19 Hata kama ikiwa kikao cha furaha ambacho hutajwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) au Ahlul-Bayt (a.s.), na kwamba utamkwaji wa maneno yenye kuwasifu wao hakuhalalishi utumiaji wa maneno ya haramu ambayo hulingana na vikao vya upuuzi na maasi, bali “Muziki au nyimbo ni haramu hata kama ikiwa ni dua, Qur’ani, Adhana, nyimbo za maombolezo n.k.”20 Hakika nyimbo au muziki ni miongoni mwa mambo yaliyoharamishwa kisheria, vivyo hivyo kufanya biashara kwayo ni haramu pia. Ayatullah Imam Khamenei anasema: “Hakika kuuza, kununua na kugawa kasseti, aidha vile vinavyofanana navyo, ikiwa vitafungamana na muziki na nyimbo za kipuuzi pia ni haramu haifai kuzisikiliza.”21 MUZIKI KATIKA QUR’ANI TUKUFU NA HADITHI TAKATIFU Ni dhahiri kwamba muziki ni miongoni mwa mambo ya haramu, kwa mantiki hiyo Mwenyezi Mungu (a.j) ametutahadharisha kujihusisha na jambo 19 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 23 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 20 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 27 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 21 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 24 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 14


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 15

Vikao vya Furaha hilo, pia akatuamrisha tujiepushe nalo, jambo hilo limeelezwa ndani ya Qur’ani tukufu na hadithi mbali mbali kwa sifa tofauti, miongoni mwa sifa hizo ni: USEMI WA UONGO: Mwenyezi Mungu (a.j) anasema:

“Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu na jiepusheni na usemi wa uongo.” 22:30 Na imekuja katika hadithi hivi: Nilimuuliza Abu Abdillah, Imam Swadiq (a.s.) kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu (a.j): “Na jiepusheni na usemi wa uongo” akasema: “Usemi wa uongo ni muziki.”21 MANENO YA UPUUZI: Imekuja katika hadithi iliyopokewa na Muhammad bin Muslim kutoka kwa Abu Ja’far Imam Muhammad Baqir (a.s.) amesema: Nilimsikia akisema: Muziki ni miongoni mwa mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameahidi adhabu kwayo, hapo akasoma aya hii:

“Na katika watu yupo anayenunua maneno ya upuuzi ili kupoteza katika njia ya Mwenyezi Mungu pasipo na elimu, na kuifanyia mzaha, hao watapata adhabu ifedheheshayo.”22 (31:6) 22. Wasail Shiia juz. 17 uk. 303 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 23. Wasail Shiia juz. 17 uk. 304 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 15


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 16

Vikao vya Furaha NI AINA ZA UOVU: Imekuja katika hadithi iliyopokewa na Yunus amesema: Nilimuuliza Imam Ali Ridha (a.s.) kuhusu nyimbo nikasema: Hakika Abbas amesema kwamba: Wewe unaruhusu nyimbo (muziki), Imam (a.s.) akasema: “Amedanganya muovu, mimi sikumwambia hivyo, aliniuliza kuhusu muziki, nikamwambia: Mtu mmoja alikwenda kwa Abu Ja’far (a.s.) akamuuliza kuhusu muziki? Akasema: “Ewe fulani ikiwa Mwenyezi Mungu akitenga haki na batili, muziki utauweka upande gani? Akasema: upande wa batili, akasema: Hakika wewe mwenyewe umeshahukumu.”24 NI SHIRKI ILIYOJIFICHA Kwa hakika kutenda maasi au uovu wowote ule kitabia huzingatiwa ni kuabudu upuuzi na kupanda kipando cha Shetani, vivyo hivyo suala la muziki. Imekuja katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Abu Ja’far Imam Baqir (a.s.) amesema:

“Mwenye kumtegea sikio mzungumzaji kwa hakika amemwabudu yeye, ikiwa mzungumzaji anatekeleza yale yaliyotoka kwa Mwenyezi Mungu (a.j) kwa hakika atakuwa amemwabudu Mwenyezi Mungu, na ikiwa mzungumzaji anatekeleza yale yatokayo kwa shetani kwa hakika atakuwa amemwabudu shetani.”25 24 Wasail Shi’ah, Juz. 17, uk. 306 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 25 Wasail Shi’ah, Juz. 17, uk. 317 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 16


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 17

Vikao vya Furaha

ATHARI ZA MUZIKI KATIKA MOYO WA BINADAMU Kwa hakika kila tendo ambalo Mwenyezi Mungu (a.j) amewaharamishia waja Wake lina athari mbaya, na miongoni mwa maovu na madhara ambayo yameelezwa kuhusiana na muziki ni: i. Huotesha Unafiki Ndani ya Moyo wa Binadamu: Imekuja katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s.) amesema:

“Muziki husababisha unafiki na hufuatiwa na ufakiri.”26 ii. Husababisha Moyo kuwa Mgumu: Suala la muziki ni miongoni mwa mambo ambayo husababisha ukaukaji wa machozi, kutokuwa na woga na kukosa unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu (a.j). Imekuja katika usia wa Mtume (s.a.w.w.) kwa Imam Ali (a.s.) amesema:

“Ewe Ali mambo matatu hufanya moyo kuwa mgumu; kusikiliza upuuzi, uwindaji na kwenda kwenye mlango wa Sultani.”27 26 Wasail Shi’ah, Juz. 17, uk. 309 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 27 Wasail Shi’ah, Juz. 17, uk. 314 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 17


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 18

Vikao vya Furaha Ni dhahiri shahiri kwamba yule ambaye huiepusha nafsi yake na maasi huwa na haya kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu (a.j) na kumpenda Yeye, kwa hakika atapata malipo ambayo Mwenyezi Mungu amewaahidi wachamungu akhera. Imekuja katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Ali Ridha (a.s.) amesema:

“Yeyote atakayeiepusha nafsi yake na muziki, kwa hakika peponi kuna mti ambao Mwenyezi Mungu atauamrisha upepo hutingishe mti huo, basi atasikia sauti ambayo hajawahi kuisikia mfanowe, na asiyejiepusha nao hatoisikia sauti hiyo.”28

NYUMBA INAYOPIGWA MUZIKI Ni dhahiri shahiri kwamba nyumba ambayo maasi hufanywa humo hukosa rehema za Mwenyezi Mungu, vivyo hivyo Malaika hawaingii nyumba hiyo. Lau tungelichunguza hadithi mbali mbali hata kwa mtazamo mdogo tungezikuta zinaeleza kwamba nyumba ambayo hupigwa humo muziki huelezwa kwa sifa mbaya chungu nzima, na hapa tunataja baadhi ya hadithi hizo nazo ni: Imepokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s.) amesema:

“Nyumba ipigwao muziki haisalimiki na majanga, hayakubaliwi humo maombi na wala haingii Malaika.”29 28 Wasail Shi’ah, Juz. 17, uk. 317 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 29. Wasail Shi’ah juz. 17 uk. 303 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 18


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 19

Vikao vya Furaha Aidha imepokewa hadithi kutoka kwake pindi alipoulizwa kuhusu muziki akasema:

“Msiingie nyumba ambayo Mwenyezi Mungu (a.j) huwapuuza watu wake.”30 Vile vile amesema:

“Nyimbo ni kikao ambacho Mwenyezi Mungu hawaangalii watu wake.” Na kuhusu hilo Mwenyezi Mungu (a.j) anasema:

“Na katika watu yupo anayenunua maneno ya upuuzi ili kupoteza katika njia ya Mwenyezi Mungu…”31 (31:6)

NYIMBO KATIKA VIKAO VYA FURAHA Hakika uharamu wa nyimbo katika vikao vya furaha hutofautiana baina ya wanaume na wanawake, hakuna tofauti ya hukmu ya uharamu wa kuimba kwa wanaume iwe katika sherehe ya harusi na sehemu zingine, ama wanawake: “Si vibaya kuimba wakiwa wao wenyewe (bila kuwepo wanaume) hususan katika vikao na sherehe za harusi, wala haizuiwi kutumia wao vyombo vya muziki katika hali ya uimbaji kwa namna iliyozoeleka hasa hasa katika vikao hivyo, ama katika vikao visivyo kuwa hivyo haifai kabisa.”32 30. Wasail Shiia juz. 17 uk. 306 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily. 31. Wasail Shiia juz. 17 uk. 307 Muassasat Ahlul-bayt chapa ya pili mwaka 1414 H cha Muhammad bin Hasan Al-Hurru Amily 32 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 22 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 19


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 20

Vikao vya Furaha Lakini hapana budi yachungwe na kuzingatiwa mambo kadhaa nayo ni: i. Iwe ni sherehe ya harusi, yaani tukio la bi harusi la kuelekea kwa mumewe, ama katika mazingira yasiyokuwa hayo hairuhusiwi kuimba kabisa. ii. Uimbaji uwe mahsusi tu kwa wanawake. iii. Sauti zao zisisikike na wanaume. vi.Uimbaji usisababishe kutendwa maovu mengine kama vile uchezaji ambao utaleta msisimko na kuamsha hisia za matamanio. Na wala haifai kusikiliza nyimbo na miziki ya upuuzi kwa njia ya kasseti, cd n.k zilizorekodiwa hata zikiwa ni za sherehe za harusi.33 PILI: MUZIKI Muziki upo wa aina nyingi, upo muziki uliyo halali na pia upo uliyo haramu, na hapa tutaeleza aina hizo mbili ili tuchanganue muziki uliyo halali na uliyo haramu, pia hukmu ya utumiaji wa vyombo vya muziki.

MUZIKI ULIYO HARAMU Zipo aina nyingi za miziki inayojulikana. Swali: Ni kidhibiti gani na wigo upi uliyopo baina ya muziki uliyo halalishwa na uliyo haramishwa? 33 Kutoka katika Tovuti ya ofisi ya Ayatullah Khamenei sehemu mpya ya maswali na majibu mlango wa utamaduni na fani suala la kusikiliza miziki kwa njia ya kanda (kassetti). 20


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 21

Vikao vya Furaha Jibu: Swali hilo limejibiwa na mheshimiwa kiongozi Ayatullah Khamenei amesema: Vile vitu ambavyo mazoea ya watu huvihesabu kuwa ni muziki wa kipuuzi wenye kuburudisha, pia huambatana na vikao vya kipuuzi na batili, huo ni muziki uliyoharamishwa hakuna tofauti kati ya muziki wa kitaalamu na usiokuwa wa kitaalamu, na uchanganuzi wa muziki husika hilo hutegemea mtazamo unaoeleweka wa mtu mzima, na muziki ambao hauko hivyo si vibaya katika uhalisia wake na dhati yake.34 Kwa kigezo hicho cha ujumla lau tutasikia mrindimo wa sauti ni juu yetu kuchanganua je! Mrindimo huo unalingana na vikao vya upuuzi na batili? Na baada ya kupata jibu hapo tutakuwa tumechanganua kitu hicho kuwa ni mrindimo ambao tuujuao, iwapo unalingana na vikao vyao basi huo ni haramu, ama ukiwa haulingani na vikao vyao basi huo ni halali. Na lau mtu mzima atashindwa kutambua au kuchanganua kwamba mrindimo huo unalingana na vikao vya uovu au hapana kutokana na kutojua namna ya vikao vyao na nyimbo zao, itambidi yeye kurejea katika uelewa wa watu na kwa hivyo atawauliza watu kuhusu hilo, kwani uelewa wa watu huchanganua muziki wa upuuzi na mwingineo, na kutokana na sifa na vigezo vya muziki uburudishao wa kipuuzi ni kwamba: “Humtoa mtu katika hali yake ya kawaida kwa sababu hufungamana nao vitu mahsusi miongoni mwa yale ambayo hulingana na vikao vya upuuzi na vya maasi…”35

NGOMA ZA JADI Ipo itikadi iliyoenea kwa watu wengi kwamba ngoma za kimila zinaruhusiwa kisheria, na ukweli ni kuwa hukmu ya ngoma za jadi au kimila ni kama vile hukmu ya muziki mwingine kwa ujumla, na huwa chini ya 34 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 20 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 35 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2 uk. 20 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 21


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 22

Vikao vya Furaha kanuni ya msingi iliyokwisha tangulia hapo kabla; “Yale ambayo watu huelewa na huyahesabu kuwa ni ngoma au muziki wa upuuzi, aidha unalingana na vikao vya upuuzi na maasi, basi hilo ni haramu bila kutofautisha… baina ya ufuataji wa kijadi na mwingineo.”36

HUKMU ZA VYOMBO VYA MUZIKI Zipo aina mbili za vyombo vya muziki nazo ni: 1. Vyombo vilivyo mahsusi kwa matumizi ya haramu, yaani hutumiwa tu katika muziki wa haramu. 2. Vyombo vinavyotumiwa katika mambo ya halali na haramu. Aina mbili hizo ni miongoni mwa vyombo ambavyo vina hukmu mahsusi. Ama vyombo vilivyo mahsusi kwa muziki kama vile kinanda, kukitumia chombo hicho ni haramu, vivyo hivyo chombo kiitwacho gita, kwa hivyo kigezo katika uhalali au kuhalalisha yale ambayo huchezwa kwavyo, ni kuwa kwake hayalingani na mambo ya sauti ambayo huimbwa katika vikao vya upuuzi na batili. Ufupisho wa kadhia hii ni kwamba; “Kutumia vyombo vya ngoma na muziki kwa namna ya upuuzi wenye kuburudisha ambao hulingana na vikao vya upuuzi na kuburudisha ni haramu kabisa.”37

36Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 27 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 37 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 32 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 22


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 23

Vikao vya Furaha

KUUZA NA KUNUNUA VYOMBO VYA MUZIKI Baada ya kuchanganua aina za vyombo vya muziki vya halali na vya haramu, kwa hakika ni vizuri kueleza hukmu ya kuuza na kununua vyombo hivyo. Vyombo maalum kwa mambo ya haramu, ama vyombo mahsusi kwa mambo ya haramu ni dhahiri shahiri kwamba haifai kuviuza na kuvinunua, kwa namna ambavyo havitumiwi ila katika mambo ya haramu. Ama vyombo ambavyo vinatumiwa katika mambo ya halali na haramu, si vibaya kuvinunua na kuviuza kwa ajili ya ngoma au muziki usiokuwa wa kipuuzi kwa malengo ya halali, aidha si vibaya kuusikiliza,38 lakini ni sharti kwamba usiwe “Uuzaji kwa makusudio ya matumizi ya haramu.”39

HUKMU YA KUJIFUNZA MUZIKI Inafahamika kwamba muziki upo wa halali na wa haramu, na inafaa kwa mtu mzima kujifunza muziki kwa ajili ya muziki usiokuwa wa haramu, kama vile kuimba kasida za kimapinduzi au za kidini, au kufanya vipindi vya kitamaduni vyenye faida, kuelimisha na yanayofanana na hayo miongoni mwa yale ambayo yanakuwa na lengo linalokubalika kiakili, kwa sharti kwamba kusisababishe maovu mengine.40 Ayatullah Khamenei anasema: “Si vibaya kujifunza fani ya uimbaji na kuifundisha katika dhati yake na uhalisia wake.”41 38 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 28 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 39 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 33 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 40 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 25 Darul-Nabai linashri chapa ya tano cha Ayatullah Ali Khamenei. 41 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 26 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 23


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 24

Vikao vya Furaha

KUKOSEA KATIKA UAINISHAJI Huenda baadhi ya watu wakakosea katika kuainisha baadhi ya aina za kasida, na mukallafu akaweka shaka, je! hii inaingia katika anwani ya nyimbo za haramu au katika anwani ya kasida ya kimapinduzi? Na hilo linatokea pale ambapo mwimbaji au msomaji kasida anapokuwa si miongoni mwa washika dini, pamoja na kuwa kasida ina ujumbe mzuri wenye kuhamasisha mapambano na ukombozi. Je! Kuna hukmu gani mfano wa hali hiyo? Jibu: Hakika kigezo cha uhalali na uharamu ni kile tulichokieleza hapo kabla, ni kutokana na kulingana na jambo la upuuzi na batili, kuburudisha na yasiyokuwa hayo, na kwa hivyo ikiwa kwa mtazamo wa msikilizaji si nyimbo, kiburudisho wala upuuzi, sio vibaya kuusikiliza huo na wala hakuna muingiliano katika nia ya mwimbaji wala madhumuni ya yale yanayoimbwa.42 Na huenda wakawa baadhi ya wale wenye nia nzuri ambao huimba kasida za kimapinduzi au zinazosifia zenye madhumuni mazuri, lakini sauti na mrindimo (mdundo) unaotumiwa unafanana na vikao vya kuburudisha na vya upuuzi, mfano wa hali hiyo usikilizaji wake unakuwa ni haramu pamoja na kuwa nia yake ni nzuri na madhumuni yake ni mazuri, kwa sababu kigezo ni namna na mrindimo, kama ilivyokwishatangulia hapo kabla katika jibu la Ayatullah Khamenei.

42 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 29 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 24


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 25

Vikao vya Furaha

TATU: UCHEZAJI NA UPIGAJI MAKOFI UCHEZAJI MUZIKI Kwa hakika uchezaji muziki ni miongoni mwa ada na desturi ambazo hupatikana katika vikao vya furaha na visivyokuwa hivyo, tangu hapo zama za kale, na bado yaendelea hadi hivi sasa. Swali: Ni upi mtazamo wa kisheria juu ya tendo hilo? Na ipi hukmu ya kisheria kwalo? Jibu: Zipo aina nyingi za uchezaji wa muziki, na baadhi ya aina za kimila huzingatiwa ni miongoni mwa mambo yaliyorithiwa na hufuatwa katika mji huu au ule, kwa hivyo hakuna haja ya upambanuzi wa aina za uchezaji muziki na kuweka hukmu ya kisheria kwa kila moja, kipo kipimo kimoja cha kuhalalisha uchezaji muziki au kuuharamisha, kipimo hicho tunaweza tukakiambatanisha nacho na aina yoyote ile ya uchezaji ili tujue hukmu yake, nalo litabainika kama ifuatavyo:

HUKMU YA KISHERIA YA UCHEZAJI MUZIKI Hakika kipimo cha ujumla kwa aina zote za uchezaji muziki ni kwamba “Ikiwa uchezaji huo utaamsha hisia na kuchochea matamanio au ukawa pamoja na utumiaji wa vyombo vya upuuzi kwa aina ya upuuzi, au ikiwa ni katika yale ambayo husababisha ufisadi kwayo, bila shaka uchezaji huo ni haramu.� Ama ikiwa hautasababisha ufisadi na uovu kwalo na wala haukuwa pamoja na muziki wa upuuzi na wala hauchochei matamanio, basi hilo si vibaya kwake, na hilo linadhihirika kama ifuatavyo:

25


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 26

Vikao vya Furaha Hakika aina za uchezaji wa kuchanganyikana ambao huenda ukatokea katika sherehe na huhusisha baina ya mwanaume na mwanamke, pia husababisha kupatikana matamanio na maovu, hakuna shaka huwa ni haramu. Inaruhusiwa wanawake kucheza bila ya kuchanganyika na wanaume, na iwapo haitasababisha na kuchochea matamanio au maovu mengine humo. Uchezaji wa kimila “Ukiwa wa aina ya kuchochea matamanio au ukawa pamoja na utumiaji wa vyombo vya muziki kwa aina ya upuuzi au ukawa ni miongoni mwa yale yasababishayo uovu au mambo machafu kwa hakika hilo ni haramu, na kama si hivyo hakuna shaka kwalo.�43 Nchini Lebanoni upo uchezaji wa kitaifa wa wanaume uitwao: Al-ddabaka, wanaume huweka mistari hucheza ubavu kwa ubavu ukiambatana na muziki au bila ya kuambatana na muziki. Swali la kwanza: Je! linaruhusiwa hilo? Sawa unaambatana na muziki au la? Swali la pili: Je! linafaa hilo pamoja na upigaji makofi au bila kupiga makofi, na akiwepo mwenye kusoma maulidi ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na kughani? Swali la tatu: Likiruhusiwa hilo, je! inasihi kucheza mbele ya wanawake? Jibu: Hukmu ya Al-ddabaka (uchezaji wa kitaifa uliyo maarufu nchini Lebanoni) kuhusu hukmu ya uchezaji huo ni kwamba; ukiwa kwa aina ya kuchochea matamanio au ukiambatana na vyombo vya upuuzi kwa aina ya upuuzi, au ukawa ni miongoni mwa yale ambayo husababisha uovu, bila shaka hilo ni haramu, na kama si hivyo basi sio vibaya kwalo.44 Harakati za Falkaluriyya ambazo huenda zikatokea katika harusi kwa kutumia upanga na ngao ambapo huenda sanjari na harakati za kibunifu 43 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 37 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Ayatullah Ali Khamenei. 44 Katika Tovuti ya Ayatullah Ali Khamenei. 26


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 27

Vikao vya Furaha “Ikiwa kwa sura ya mchezo wa riadha wa kujifurahisha na hakukuwa na hofu kwayo juu ya nafsi, basi hakuna tatizo kwa dhati na uhalisia wake kwayo, na ama kutumia vyombo vya muziki kwa aina ya upuuzi wenye kuburudisha haifai hata kidogo.”45

UCHEZAJI WA MKE NA MUME Swali: Mwanamke akimchezea mumewe au mume atakapomchea mkewe ni haramu? Jibu la swali hilo ni kwamba: “Ikiwa uchezaji wa mke kwa mumewe au wa mume kwa mkewe ni pasi na kutenda haramu hilo halina tatizo.”46 Na kutenda haramu kwa mfano ni ule uchezaji ambao hutokana na nyimbo ya haramu…

MWANAMKE KUCHEZA MBELE YA WANAUME Tumekwishaeleza hukmu ya mke kucheza mbele ya mumewe. Swali: Ipi hukmu ya mwanamke kucheza mbele ya wanaume ajinabi? Jibu: Ayatullah Imam Ali Khamenei anasema: “Hakika mwanamke kucheza mbele ya wanaume ajinabi ni haramu kabisa kabisa.”47 Na pindi alipoulizwa hukmu ya wanawake kucheza mbele ya wanaume katika vikao vya harusi za vijijini na ambavyo hutumiwa vyombo vya muziki kwavyo, na upi wajibu wa mukallafu kuelekea hilo? 45 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 36 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Imam Ali Khamenei. 46 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 35 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Imam Ali Khamenei. 47 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 35 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Imam Ali Khamenei. 27


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 28

Vikao vya Furaha Mheshimiwa alijibu kama ifuatavyo: “Hakika wanawake kucheza mbele ya wanaume ajinabi, pia uchezaji wowote ule ambao husababisha maovu na kuchochea matamanio ni haramu, aidha utumiaji wa vyombo vya muziki na kuusikiliza ukiwa wa aina ya upuuzi wenye kuburudisha ni haramu pia, ama jukumu la mtu mzima katika hali hizo ni kukataza uovu.”48

UPIGAJI MAKOFI VIKAONI Kupiga makofi katika vikao vya furaha ni ada na desturi iliyozoeleka na kujikita katika jamii, nayo ni kupiga viganja viwili vya mikono katika hali ya kuonesha furaha, na huambatana na ada ya usomaji wa kasida au nyimbo. Swali: Sheria ya kiislamu inasemaje kuhusu hilo? Jibu: Hakika upigaji makofi kwa uhalisia wake sio miongoni mwa mambo yaliyoharamishwa na sheria; “Sio vibaya kupiga makofi kwa aina iliyozoeleka.”49 Na miongoni mwa mambo ambayo hupatikana katika sherehe za kuzaliwa watoto na mambo mengineyo ya furaha, wanawake hupiga makofi hadi wanaume wakasikia sauti, swali: Je! hilo linaruhusiwa? Jibu: Ayatullah Imam Ali Khamenei anasema: “Linaruhusiwa hilo hata kama ikiwa atasikia mwanaume ajinabi, ikiwa upigaji makofi hautakuwa ni miongoni mwa yale ambayo husababisha uovu, mambo machafu na ufisadi.”50 48 Ajwibatul-Istiftaat juz. 2 uk. 36 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Imam Ali Khamenei. 49. Ajwibatul-Istiftaat juz. 2 uk. 38 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Imam Ali Khamenei. . 50 Ajwibatul-Istiftaat juz. 2 uk. 38 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Imam Ali Khamenei. 28


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 29

Vikao vya Furaha Na upigaji makofi sio njia bora zaidi na kielelezo cha furaha, bali jambo lililo bora zaidi ya upigaji makofi “Mazingira ya vikao vya kidini yanakshiwe na manukato mazuri kwa kumswalia Bwana Mtume (s.a.w.w.) na kumtukuza Mwenyezi Mungu (a.j) kwa kutoa takbiira hususan katika vile vikao ambavyo vyafanyika misikitini, kumbi za maombolezo na sehemu za swala, ili sehemu hizo zipate hadhi kutokana na thawabu za kumswalia Bwana Mtume (s.a.w.w.) na kumtukuza Mwenyezi Mungu (a.j).�50

UFUPISHO WA MADHUMUNI YA VIKAO Muhtasari wa yale ambayo yanayohusiana na madhumuni ya kikao ni kama yafuatavyo:

VIGEZO VYA NYIMBO: Inaruhusiwa kwa wanawake kuimba katika kikao cha harusi, lakini yawapasa kuzingatia mambo mengi nayo ni: Iwe katika kikao cha harusi, yaani ile hali ya bi harusi kwenda kwa mumewe. Uimbaji uwe mahsusi baina yao wanawake tu. Sauti zao zisisikike na wanaume. Uimbaji usisababishe maovu mengi kama vile uchezaji pamoja na kuvaa nguo nyepesi au zilizobana, mambo ambayo huchochea matamanio.

51 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 38 Darul-Nabai linashri chapa ya kwanza cha Imam Ali Khamenei. 29


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 30

Vikao vya Furaha Ama kuhusu wanaume hairuhusiwi kwao kabisa kuimba sio katika harusi tu bali hata nje ya hali hiyo.

VIGEZO VYA MUZIKI Muziki wa haramu ni ule ambao unaburudisha na wa kipuuzi na maasi. Ni haramu kutumia vyombo vya muziki vilivyo mahsusi kwa mambo ya haramu, na inaruhuisiwa kutumia vyombo vinavyohusika katika malengo ya halali. Hakuna tofauti kati ya muziki wa kimila na usiokuwa huo, iwapo utalingana na vikao vya upuuzi basi huo ni haramu na kama si hivyo huo ni halali.

VIGEZO VYA UCHEZAJI WA MUZIKI NA NGOMA Uchezaji wa muziki au ngoma ni haramu kwa aina ambayo huchochea matamanio au ikiwa utaambatana na utumiaji wa vyombo vya upuuzi kwa namna ya upuuzi, au ikiwa ni miongoni mwa yale ambayo huleta uovu na mambo machafu. Inaruhusiwa wanawake kucheza bila ya kuwepo wanaume, ikiwa hautapatikana uovu na uchocheaji wenye kuamsha hisia na matamanio. Uchezaji wa kimila ukiwa kwa namna ambayo utachochea matamanio, au ukiwa waambatana na utumiaji wa vyombo vya upuuzi kwa namna ya upuuzi, au ukawa ni kati ya yale ambayo huleta uovu, muziki huo ni haramu, na kama si hivyo sio vibaya hilo. Hakika suala la upigaji makofi kwa uhalisia wake sio haramu wala sio miongoni mwa mambo yaliyoharamishwa kisheria, na lililo bora zaidi ya upigaji makofi ni kunukisha manukato mazuri mazingira ya kikao cha kidi30


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 31

Vikao vya Furaha ni kwa kumswalia Bwana Mtume (s.a.w.w.) na kumtukuza Mwenyezi Mungu, yaani kutoa takbiira hususan katika vikao ambavyo hufanywa misikitini, sehemu za maombolezo na sehemu za swala ili papate hadhi kwa thawabu za kumsalia bwana Mtume (s.a.w.w.) na kumtukuza Mwenyezi Mungu (a.j).

SEHEMU YA TATU: UPIGAJI PICHA NA UCHUKUAJI WA PICHA ZA VIDEO Kupiga Picha Vikaoni Upigaji Picha: Hakika upigaji picha huenea na kuzagaa kila kukicha baina ya watu, kwani huhifadhika kwawo maadhimisho ya vikao vyao na wapendwa wao huhifadhi na kuweka kumbukumbu picha zinazohusu hatua za maisha yao, na baadhi yao hupiga picha kama fani ambayo huvutiwa na kuliwazika kwazo, na hakika upigaji picha umeteka maisha ya binadamu hadi hali kufikia kuwa hakuna nyumba inayokosa kamera, na hilo linahusiana na uchunguzi kutokana na kigezo cha kisheria cha upigaji picha kama vile fani maalum au kazi za kawaida ambazo watu huzifanya, bali ni chombo cha kujipatia kipato na kazi ambayo watu wengi kupitia chombo hicho hujipatia chakula chao cha kila siku. Swali: Ipi hukmu ya kisheria kuhusu suala la upigaji picha?

HUKMU YA UPIGAJI PICHA Jibu: Hakuna shaka kwamba hukmu ya asili ya upigaji picha – na kuwa mbali na mambo mengine ambayo yawezekana kuunganishwa kwalo – jambo hilo linaruhusiwa, na wala sio baya, inaruhusiwa kupiga picha vitu 31


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 32

Vikao vya Furaha visivyo na uhai, mimea, wanyama, binadamu n.k Lakini vipo vigezo ambavyo hapana budi kuzingatiwa ili hukmu ya upigaji picha ibakie katika ulalali wake na jambo hilo lisigeuke na kuwa haramu, na miongoni mwa vigezo hivyo ni:

KURUHUSIWA KUTUMIA Hakika upigaji picha iwapo unahusiana na utumiaji wa mali ya mwingine hapo inahitaji kupata ruhusa au idhini kutoka kwa wahusika, kama vile kuingia nyumbani kwa mtu au kupiga picha sehemu ya ndani kwake, au matumizi yoyote yale kwa mfano uhamishaji wa kitu kutoka mahala fulani hadi mahala pengine n.k.52 Na huenda ukafahamu ruhusa kutokana na kanuni na vigezo vilivyowekwa katika sehemu za umma, na kuhusu hilo Ayatullah Imam Khamenei anasema: “Si vibaya kupiga picha katika sehemu takatifu ikiwa haitokwenda kinyume na kanuni na vigezo vilivyowekwa huko.”53

KUTOUDHI Hairuhusiwi kumpiga picha mtu bila ruhusa yake, ikiwa litasababisha hilo kumuudhi yeye.54 52 Ajwibatul-Istiftaat, uk. 27 cha Ayatullah Khamenei, imenakiliwa kutoka katika kitabu “Ahkam Akkasi” kilichoandikwa na: Kamati ya Uhuishaji wa kuamrisha mema na kukataza maovu iliyopo Qum Iran. 53 Ajwibatul-Istiftaat, uk. 27 cha Ayatullah Khamenei, imenakiliwa kutoka katika kitabu “Ahkam Akkasi” kilichoandikwa na: Kamati ya Uhuishaji wa kuamrisha mema na kukataza maovu iliyopo Qum Iran. 54 Ajwibatul-Istiftaat, uk. 27 cha Ayatullah Khamenei, imenakiliwa kutoka katika kitabu “Ahkam Akkasi” kilichoandikwa na: Kamati ya Uhuishaji wa kuamrisha mema na kukataza maovu iliyopo Qum Iran. 32


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 33

Vikao vya Furaha

MWANAUME KUMPIGA PICHA MWANAMKE Inaruhusiwa mwanaume kumpiga picha mwanamke ikiwa upigaji picha huo hautasababisha utazamaji wa haramu kwake.

KUHUDHURIA VIKAO VINAVYOPIGWA PICHA Hakuna shaka kwamba upigaji picha uwe wa picha za kawaida au wa picha za filamu ni miongoni mwa mambo yanayoruhusiwa, ni matendo ya halali ambayo inawezekana mtu kwa njia moja au nyingine akafanya ghushi,55 na mara nyingi uchukuaji wa picha za harusi, au sherehe za kuzaliwa na nyinginezo huhifadhi na kuweka kumbukumbu za sherehe hizo, na upigaji huo wa picha unaruhusiwa ikiwa halitoingizwa jambo miongoni mwa mambo ya haramu ambayo tutayatolea ishara ndani ya anwani zifuatazo:

KUANGUKIA KATIKA MAMBO YA HARAMU Zipo baadhi ya hafla na sherehe ambazo huwafanya watu wasitekeleze hukmu za kisheria, hufanywa humo maasi na dhambi nyingi, kama vile kusikiliza nyimbo na muziki wa haramu, uchezaji na kuchanganyika pamoja baina ya wanaume na wanawake. Swali: Je! Inaruhusiwa kuhudhuria mfano wa hafla hizo kwa lengo la kupiga picha? Jibu: hairuhusiwi, iwapo upigaji picha utalazimu kuwaangalia wahusika kwa uangaliaji wa matamanio, au kutendwa maovu mengineyo, au kueneza uovu na ufisadi, kama vile haifai kusikiliza nyimbo au muziki uliyo haramu.55 55 Tahrirul-Wasiila, Juz. 2, uk. 659 cha Imam Ruhullah Musawy Khomeini. 56 Ajwibatul-Istiftaat, Juz. 2, uk. 39 swali la 107 Darul-Islamiyya cha Ayatullah Khamenei. 33


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 34

Vikao vya Furaha

MWANAUME KUPIGA PICHA KATIKA VIKAO VA WANAWAKE NA MWANAMKE KUPIGA PICHA KATIKA VIKAO VYA WANAUME Kiasili inaruhusiwa mwanaume kupiga picha katika vikao vya wanawake, vivyo hivyo mwanamke kupiga picha katika vikao vya wanaume, lakini hilo litakuwa haramu iwapo itasababisha kutendwa tendo la haramu kama vile uangaliaji wa matamanio au ikapelekea kutendwa uovu mwingine.57 Lau itajaaliwa kwamba bi harusi ametaka apigwe picha inaruhusiwa mmoja wa mahrimu wake miongoni mwa wanaume kama vile kaka, baba mdogo au mjomba kumpiga picha.

UPIGAJI PICHA ZA UCHEZAJI Hairuhisiwi kuchukua picha za video za uchezaji wa wanawake ikiwa uchezaji huo utakuwa ni aina iliyoharamishwa.58

SAUTI ZENYE KUATHIRI KATIKA FILAMU Baada ya uchukuaji wa picha za filamu na huenda mchukuaji picha hizo akaweka sauti zenye kuathiri kwazo, kama vile muziki au nyimbo na mengineyo. Swali: Ipi hukmu ya hayo? Jibu: Si vibaya kisheria kuutumia muziki usio kuwa wa haramu, vivyo hivyo viathiri vingine ambavyo vinaruhusiwa kusikiliza, ama utumiaji wa haramu kwayo kwa mfano utumiaji wa muziki unaolingana na vikao vya 57 Tahrirul-Wasiila, Juz. 2, uk. 659 cha Imam Ruhullah Musawy Khomeini na Ajwibatul-Istiftaat Juz. 2, uk. 39 swali la 107 Darul-Islamiyya cha Ayatullah Khamenei. 58 Ajwibatul-Istiftaat, uk. 31 cha Ayatullah Khamenei, imenakiliwa kutoka katika kitabu “Ahkam Akkasi” kilichoandikwa na: Kamati ya Uhuishaji wa kuamrisha mema na kukataza maovu iliyopo Qum Iran. 34


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 35

Vikao vya Furaha upuuzi katika hafla za ndoa hilo ni haramu.59

USAFISHAJI WA FILAMU Picha za filamu usafishaji wake huhitaji baada ya kupita muda fulani, aghlabu wasafishaji wa picha huwa wanaume. Swali: Ipi hukmu ya filamu ambazo zinahusiana na picha za wanawake wasio kuwa na hijabu mbele ya mwanaume ajinabi? Jibu: Si vibaya ikiwa mtu huyo hamjui mwenye picha hizo, kwa mantiki hiyo inaruhusiwa kuusafisha mkanda huo,60 aidha inaruhusiwa kizisafisha kwa sharti kwamba asikusudie kupata ladha, pia asifikwe na matamanio na kutenda uovu. Na ama ikiwa anamjua mwenye picha basi haifai kuziangalia picha hizo.

USAMBAZAJI WA PICHA NA FILAMU Haifai kuzitoa nakala na kuzisambaza picha za watu bila ruhusa yao ikiwa utawasababishia kupata maudhi kwazo.61 Haifai kuzisafisha zaidi, kuzitoa nakala na kuzigawa picha za maovu na zile zenye kuchochea matamanio.62 59 Tahrirul-Wasiila juz. 2 uk. 659 cha Imam Ruhullah Musawy Khomeini na Ajwibatul-Istiftaat juz. 2 uk. 39 swali la 107 Darul-Islamiyya cha Ayatullah Ali Khamenei. 60 Ajwibatul-Istiftaat, juz. 2 uk. 39 swali la 105 Darul-Islamiyya cha Ayatullah Ali Khamenei. 61 Ajwibatul-Istiftaat, uk. 39 cha Ayatullah Khamenei, imenakiliwa kutoka katika kitabu “Ahkam Akkasi” kilichoandikwa na: Kamati ya Uhuishaji wa kuamrisha mema na kukataza maovu iliyopo Qum Iran. 62 Ajwibatul-Istiftaa, uk. 41 cha Ayatullah Khamenei, imenakiliwa kutoka katika kitabu “Ahkam Akkasi” kilichoandikwa na: Kamati ya Uhuishaji wa kuamrisha mema na kukataza maovu iliyopo Qum Iran. 35


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 36

Vikao vya Furaha Haifai kuzidhihirisha na kuzionesha picha ambazo hazina hijabu kwa wasio kuwa mahrimu hata wakiwa ni miongoni mwa wanandugu.63

63 Ajwibatul-Istiftaat, uk. 54 cha Ayatullah Khamenei, imenakiliwa kutoka katika kitabu “Ahkam Akkasi� kilichoandikwa na: Kamati ya Uhuishaji wa kuamrisha mema na kukataza maovu iliyopo Qum Iran. 36


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:39 PM

Page 37

Vikao vya Furaha

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 37


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:40 PM

Page 38

Vikao vya Furaha 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 38


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:40 PM

Page 39

Vikao vya Furaha 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86.

Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali 39


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:40 PM

Vikao vya Furaha 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne

113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 40

Page 40


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:40 PM

Vikao vya Furaha 114.

Iduwa ya Kumayili

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha

139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 41

Page 41


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:40 PM

Page 42

Vikao vya Furaha 140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No1

153

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2

154.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3

155.

Abu Huraira

156.

Kati ya Alama kuu za dini Swala ya Jamaa. na Adabu za Msikiti na Taratibu zake.

157.

Uadilifu katika Uislamu

42


Vikao Vya Furaha by Lubumba Final Dr.Kanju.qxd

7/16/2011

12:40 PM

Page 43

Vikao vya Furaha

BACK COVER Kwa hakika kati ya vikao vingi vinavyowekwa hupatikana maswali chungu nzima kuhusiana na suala hili, ni vikao vya furaha ambavyo huwekwa kwa matukio mbalimbali ambapo watu hupata burudani kama vile sherehe za ndoa, kuzaliwa watoto, n.k Swali: Kuna hukmu gani kuhusu vikao hivyo? Ni madhumuni gani ambayo hufaa kuangaziwa katika vikao hivyo? Na upi wigo ambao sheria imeweka ili kuhifadhi hilo? Je! Ni matumizi gani ambayo sheria imeruhusu, au imekataza mambo gani ndani ya vikao hivyo au nje ya vikao hivyo? Jibu: Maswali hayo na yale yanayofanana na hayo ni kati ya maswali mengi ambayo tutajaribu kuyatolea majibu katika kitabu hiki. Tunamuomba Mola Muweza atie furaha nyoyo za waumini, na tusiwe na huzuni Siku ya Qiyama, siku ambayo haitomfaa mtu mali wala watoto ila mwenye kwenda kwa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa moyo wake umesalimika. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

43


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.