Vyakula na vinywaji

Page 1

Vyakula na Vinywaji (Mfululizo wa Masuala ya Kisheria)

‫الطعام والشراب‬

Kimeandikwa na: Jumuiya ya Utamaduni na Maarifa ya Kiislamu

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 1

11/25/2014 4:23:10 PM


‫ترجمة‬

‫الطعام والشراب‬

‫تأليف‬ ‫جمعية المعارف اإلسالمية الثقافية‬

‫من اللغة العربية الى اللغة السوا حلية‬

‫‪11/25/2014 4:23:10 PM‬‬

‫‪41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 2‬‬


ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 17 - 095 - 1 Kimeandikwa na: Jumuiya ya Utamaduni na Maarifa ya Kiislamu Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa Kea Kimehaririwa na: Hemedi Lubumba Selemani Kimepitiwa na: Mbaraka A. Tila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Machi, 2015 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 3

11/25/2014 4:23:10 PM


Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 Utangulizi......................................................................................... 2 SEHEMU YA KWANZA............................................................. 4 HUKUMU ZA VYAKULA NA VINYWAJI.............................. 4 Kwa nini uwepo uharamisho?.......................................................... 4 Aina za vyakula na vinywaji:........................................................... 6 Mnyama: ......................................................................................... 6 Wanyama wa nchi kavu: ................................................................. 6 Wanyama pori: ................................................................................ 6 Wanyama wafugwao: . .................................................................... 7 Wanyama wafugwao walio halali kuliwa: ...................................... 8 Wanyama wafugwao walio haramu kuliwa: ................................... 8 Wanyama wafugwao walio makuruhu kuliwa: . ............................. 8 Vitu ambavyo ni haramu kuliwa toka kwa mnyama: ..................... 9 Vitu ambavyo vinaruhusiwa kuliwa toka kwenye mzoga:............ 10 Wadudu: ........................................................................................ 10 Wanyama wa baharini: . ................................................................ 11 Hukumu ya mayai ya samaki: . ..................................................... 12 Ndege: ........................................................................................ 12

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 4

11/25/2014 4:23:10 PM


Vyakula na Vinywaji

Ndege walio halali kuliwa: ........................................................... 13 Ndege walio haramu: .................................................................... 13 Ndege walio makuruhu kuliwa: .................................................... 13 Hukumu ya ndege wengine: ......................................................... 15 Hukumu ya mayai ya ndege: ........................................................ 16 Aliye haramu kwa sababu ya chakula chake: ............................... 17

1. Kinyesi cha binadamu: ....................................................... 17

Miongoni mwa hukumu za mnyama anayekula kinyeshi: . .......... 17 Vipi tutamtoharisha mnyama anayekula kinyesi: ......................... 18

2. Kunyonya maziwa ya nguruwe: ......................................... 18

Kisichokuwa mnyama: ................................................................. 18

1. Vile vinavyoudhuru mwili: ................................................. 19

2. Najisi na kilichonajisika: .................................................... 20

3. Pombe na madawa ya kulevya: . ......................................... 20

4. Juisi ya zabibu iliyochemshwa: .......................................... 21

5. Udongo: .............................................................................. 21

Udongo ambao ni halali kuliwa: ................................................... 22 Hukumu za dharura: . .................................................................... 22 Angalizo muhimu: ........................................................................ 24 v

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 5

11/25/2014 4:23:10 PM


Vyakula na Vinywaji

SEHEMU YA PILI: ................................................................... 25 ADABU ZA KULA..................................................................... 25 Utangulizi: .................................................................................... 25 Faida za kula kidogo: .................................................................... 25 Madhara ya kula sana: .................................................................. 27 Miongoni mwa adabu za meza ya chakula................................ 28 Nawa kabla na baada ya kula: . ..................................................... 28 Soma Bismillahi na omba dua: ..................................................... 29 Tumia muda mrefu: . ..................................................................... 31 Kula punje zilizodondoka: ............................................................ 31 Anza na malizia kwa chumvi: . ..................................................... 32 Mtu ale sehemu iliyo mbele yake: ................................................ 33 Mlishe yule mwenye hamu na chakula chako: ............................. 33 Kutokula kwa mkono wa kushoto: ............................................... 34 Usile hali yakuwa unatembea: ...................................................... 35 Usile chakula cha moto: . .............................................................. 35

vi

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 6

11/25/2014 4:23:10 PM


Vyakula na Vinywaji

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, at-Ta’aam wa ash-Sharaab, kilichoandikwa na Jumuiya ya Utamaduni na Maarifa ya Kiislamu. Sisi tumekiita, Vyakula na Vinywaji (Mfululizo wa Masuala ya Kisheria). Uislamu ni dini na mfumo kamili wa maisha. Kutokana na ukweli huu, Uislamu umeshughulikia kila kipengele kinachohusu maisha ya mwanadamu. Uislamu umeweka sheria na hukumu katika vyakula na vinywaji. Kwanza, umebainisha uhalali na uharamu (yaani, kipi ni halali na kipi ni haramu). Pili, Uislamu umeweka adabu za kula na kunywa. Haya na mengine yote utayaona katika kitabu hiki. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana hususan wakati huu wa sayansi na tekinolojia ambapo wengi wanaathirika na afya zao kutokana na vyakula na vinywaji na ulaji na unywaji wa vitu hivyo. Taasisi yetu ya al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa na manufaa makubwa kwao. Tunamshukuru ndugu yetu Amiri Mussa Kea kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake na kuwa mikononi mwa wasomaji. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera pia. Amin! Mchapishaji Al-Itrah Foundation 1

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 1

11/25/2014 4:23:11 PM


Vyakula na Vinywaji

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI

S

ifa njema zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote, kisha rehema na amani zimfikie bwana wetu Muhammad na Aali zake wema watoharifu. Mwenyezi Mungu anasema: ρ÷ r& πº tGøŠtΒ χ š θä3tƒ βr& ω H Î) …ÿ çμßϑyèôÜtƒ Ο 5 Ïã$sÛ ’ 4 n?tã $·Β§ptèΧ ¥’n<Î) © z Çrρé& $! tΒ ’Îû ‰ ß É`r& ω H ≅è%

⎯ Ç yϑsù 4 ⎯ÏμÎ/ ! « $# Î ötóÏ9 ≅ ¨ Ïδé& $¸)ó¡Ïù ρ÷ r& [ ê ô_Í‘ …çμ¯ΡÎ*sù 9 ƒÍ”∴Åz Ν z óss9 ρ÷ r& %·nθàó¡¨Β $YΒyŠ

∩⊇⊆∈∪ Ο Ò ‹Ïm§‘ ‘Ö θàxî  š −/u‘ β ¨ Î*sù Š7 $tã ω Ÿ uρ 8ø$t/ u öxî §äÜôÊ$#

“Sema:Sioni Sioni katika yale niliyofunuliwa wahyikitu mimi kitu “Sema: katika yale niliyofunuliwa wahyi mimi kilichoharkilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe mzoga au amishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe mzoga au damu inayomdamu inayomwagika au nyama ya nguruwe, kwani hivyo ni uchafu, wagika au nyama ya nguruwe, kwani hivyo ni uchafu, au kisicho cha au kisicho cha dini, kilichochinjwa kwa jina la asiyekuwa dini, kilichochinjwa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu, lakini mwenye kushikwa na dharura pasipo mwenye kushikwa na dharura kupenda wala kuruka mipaka, kupenda wala kuruka mipaka,pasipo basi hakika Mola wako ni Mwingi basi hakika Mola wako ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehewa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (6:145) mu.” (6:145) Kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amemhalalishia binadamu Kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amemhalalishia kustarehe na kuburudika kwa kutumia yale aliyomneemesha, ambayo binadamu na maisha, kuburudika kutumia yale ameyaumba kustarehe ili kuendeshea aidha ni kwa ili aende sawiya na nidhamu ya kijamiiambayo kwa ajiliameyaumba ya ulimwemgu Hakika viumbe katika aliyomneemesha, ili huu. kuendeshea maisha, aidha zama zote wamekuwa wakizitumia na kufaidika na neema hizo kwa ni ili aende sawiya na nidhamu ya kijamii kwa ajili ya ulimwemgu kupitia uwindaji wa wanyama, kilimo na unywaji wa maji, na ujumbe huu. Hakika viumbe katika zama zote wamekuwa wakizitumia na wa Mwenyezi Mungu ulimbeba binadamu ukamchukua kwa mkono kufaidika neema hizokatika kwa kupitia uwindaji wanyama, wake na na kumuongoza yale yenye maslahiwakwake, hadi kilimo pale ujumbe wa Mwenyezi Mungu ulipotimia na kukamilika kupitia neema ya Uislamu, pale uliporatibu na kupambanua na kuchanganua vile vitu ambavyo mtu anaruhusiwa kuvila2 au kuvinywa na vile ambavyo haruhusiwi. Na kitabu kilichopo mikononi mwako hueleza kwa muhtasari hukumu ambazo zimewekwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu ili kuweka 11/25/2014

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 2

4:23:11 PM


Vyakula na Vinywaji

na unywaji wa maji, na ujumbe wa Mwenyezi Mungu ulimbeba binadamu ukamchukua kwa mkono wake na kumuongoza katika yale yenye maslahi kwake, hadi pale ujumbe wa Mwenyezi Mungu ulipotimia na kukamilika kupitia neema ya Uislamu, pale uliporatibu na kupambanua na kuchanganua vile vitu ambavyo mtu anaruhusiwa kuvila au kuvinywa na vile ambavyo haruhusiwi. Na kitabu kilichopo mikononi mwako hueleza kwa muhtasari hukumu ambazo zimewekwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu ili kuweka mpangilio juu ya suala la vyakula na vinywaji kwa ajili ya mwanadamu, kwa mfumo na njia nyepesi yenye kwenda sanjari na picha zenye kuweka bayana, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atuwezeshe kupata kheri na kuitendea kazi, kwani Yeye ni Msikivu Mwenye kujibu. Jumuiya ya utamaduni na maarifa ya Kiislamu.

3

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 3

11/25/2014 4:23:11 PM


Vyakula na Vinywaji

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ SEHEMU YA KWANZA HUKUMU ZA VYAKULA NA VINYWAJI Kwa nini uwepo uharamisho?

Y

ampasa mtu Mwislamu aelewe kwamba hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuweka sheria mbalimbali, sunna au taratibu ila kwa ajili ya faida ya viumbe, ni dhahiri shahiri kwamba lolote lile analoliamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hakika huwa lina maslahi kwa mja aliye mukallafu, na lile alikatazalo kwa hakika analikataza ili kumkinga na kumuepusha na hasara. Kwa hakika imepokewa hadithi kutoka kwa Mufadhal bin Umar amesema: Nilisema kumwambia Abu Abdillah (a.s): “Niambie – natoa nafsi yangu fidia kwako – kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha pombe, mzoga, damu na nyama ya nguruwe?”

Akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu hakuwaharamishia waja hayo na kuwahalalishia yasiyokuwa hayo kutokana na kupenda tu kuwaharamishia, na wala sio kwa kuyatamani yale ambayo amewahalalishia wao, lakini Yeye ndiye aliyeviumba viumbe na anajua yale yanayoifaa miili yao na yale yenye maslahi kwao, basi akawahalalishia wao na akawaruhusu kwa fadhila Zake kwa maslahi yao. Na anajua yale yenye kuwadhuru wao basi akawakataza wao 4

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 4

11/25/2014 4:23:11 PM


Vyakula na Vinywaji

na akawaharamishia, kisha akayaruhusu kwa mwenye dharura, na akamhalalishia katika wakati ambao mwili wake hauwezi kuimarika ila kupitia hayo, basi hapo akamruhusu kula kiasi cha haja tu na sio zaidi ya hapo.” Kisha akasema: “Ama mzoga kwa hakika hauzoei yeyote kuula ila ni lazima kiwiliwili chake kitadhoofika, na kukonda mwili wake, na kuisha nguvu zake na kukatika kizazi chake, wala hafi mlaji mzoga ila kifo cha ghafla. Na ama damu kwa hakika kuila husababisha kuwa na maji ya manjano tumboni, hutoa mvuke kinywani, hutoa harufu mbaya mno, humfanya kuwa na tabia mbaya, husababisha ugonjwa wa hofu, moyo mgumu na upungufu wa upole na huruma, hadi hufikia hali ya kuweza hata kumuua mwanawe na wazazi wake wawili, wala haaminiki kwa kipenzi chake, wala haaminiki kwa anayefuatana naye. Na ama nyama ya nguruwe kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu aliibadilisha kaumu katika sura mbalimbali kama vile nguruwe, nyani na dubu, na wale ambao ni miongoni mwa wale waliobadilishwa, kisha akakataza kula vile vinavyofanana na hivyo ili wasivitumie watu wala kudharau adhabu yake. Ama pombe kwa hakika ameiharamisha kwa vitendo vyake na uovu wake, na akasema: Mnywaji pombe ni kama vile mwabudu masanamu na humsababishia ugonjwa wa kutetemeka, na huondoa nuru yake, na huondoa murua wake, na humfanya awe na ujasiri wa kufanya mambo ya haramu na umwagaji wa damu, na kufanya zinaa, na akinywa hasalimiki kumfanyia vibaya maharimu wake hali ya kuwa yeye hajitambui, na pombe haimuongezei mnywaji ila kufanya kila jambo la shari.” Isipokuwa yapo maslahi mengi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na zipo baadhi ya hukumu maslahi yake yamejificha kwetu, pamoja na hivyo tunawajibika kutekeleza maamrisho yake na kuacha makatazo yake kwa kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu ili 5

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 5

11/25/2014 4:23:11 PM


Vyakula na Vinywaji

kwa utekelezaji wetu tutumaini kupata malipo, thawabu na kheri hapa duniani na akhera. Aina za vyakula na vinywaji: Zipo aina mbili za vyakula na vinjwaji ambavyo mtu hula na hunywa, aina hizo ni: Aina ya kwanza: Kutokana na mnyama. Aina ya pili: Vile visivyotokana na mnyama. Tutaeleza muda mfupi ujao aina zote hizo na makundi mengine ya vyakula na tutoe mchanganuo kuhusu vyakula vya halali na vya haramu. Mnyama: Wanyama wapo wa aina tatu: Wanyama wa nchi kavu, wanyama wa baharini, na ndege, na kila moja kati ya aina hizo ina hukumu yake mahsusi. Na tutayaeleza hayo na kuyatolea ufafanuzi katika upande wa kuruhusiwa kula, na hilo tunalieleza kwa urefu na mapana kama ifuatavyo: Wanyama wa nchi kavu: Kwa hakika wanyama wa nchi kavu wapo wa aina mbili: Wale wenye kuishi na binadamu (wafugwao) na wanyama pori (wasiofugwa). Wanyama pori: Na makusudio ya wanyama pori hapa ni wale ambao hawafugwi na binadamu na hawaishi pamoja naye, katika hao ambao Mwenyezi Mungu amewahalalishia watu ni: 6

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 6

11/25/2014 4:23:11 PM


Vyakula na Vinywaji

i.

Paa na swara na mbogo na aina zao zote.

ii. Mbuzi wa milimani na kondoo wa milimani. iii. Ng’ombe pori (nyati), nao ni ng’ombe pori ambao huishi kwa makundi makubwa nchi kavu. iv. Pundamilia ambaye huishi porini, naye hufanana na punda anayeishi na watu, ambaye ana michirizi ya rangi nyeupe na nyeusi. Ama wanyama wa nchi kavu walio haramu nao ni wanyama wakali wenye kushambulia wanyama wengine, yaani kila mnyama mwenye makucha na meno, sawa awe mwenye nguvu au dhaifu, baadhi ya wanyama hao ni: 1.

Chui

2.

Simba

3.

Mbwa Mwitu

4.

Bweha

5.

Watu waliogeuzwa kuwa wanyama kama vile nyani, ngedere, kima, tembo na wengineo

6.

Nguruwe wa nchi kavu

7.

Sungura wa kiume na wa kike. Na wanyama wengi miongoni mwa wale ambao hutimia masharti yaliyotangulia.1

Wanyama wafugwao: Nao ni wanyama ambao huishi pamoja na watu, huwatumia kwa kilimo na hula nyama zao, kama vile ng’ombe, mbuzi, kondoo n.k, au 1

Angalizo:Nyoka huingia katika aina ya wadudu, na maelezo yake yatafuata pale tutakapoeleza wale ambao ni haramu kuliwa kwa aina zake zote. 7

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 7

11/25/2014 4:23:11 PM


Vyakula na Vinywaji

wale ambao huishi jirani na binadamu bila ya kuwatumia, kwa mfano paka na mbwa, kwa hivyo hao wana makundi matatu, wapo walio halali kuliwa, walio haramu kuliwa na walio makuruhu kuliwa. Wanyama wafugwao walio halali kuliwa: 1.

Mbuzi na kondoo wa aina zote.

2.

Ng’ombe wa aina zote.

3.

Ngamia wa aina zote.

Wanyama wafugwao walio haramu kuliwa: 1.

Mbwa na vigao vyake.

2.

Paka.

3.

Nguruwe wafugwao au nguruwe wa mashambani (nao ni wale ambao wana rangi ya waridi), na wanyama wengineo.

Wanyama wafugwao walio makuruhu kuliwa: 1.

Farasi.

2.

Nyumbu.

3.

Punda.

Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam Muhammad bin Ali alBaqir (a.s), amesema:

‫انّما نهى رسول اهلل (ص) عن أكل لحوم‬ 8

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 8

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

‫الحمراالنسية بخيبر لئال تفنى ظهورها وكان‬ ‫ذلك نهى كراهة ال نهى تحريم‬ “Hakika Mtume (s.a.w.w.) alikataza kula nyama za punda wanaoishi na binadamu katika Khaybar, ili wasitoweke na watu kukosa kipando, na katazo hilo lilikuwa ni makuruhu, na hakukataza kwa kuharamisha.”

Vitu ambavyo ni haramu kuliwa toka kwa mnyama: Vipo baadhi ya vitu vilivyopo kwa mnyama ni haramu kuliwa hata kama vikiwa vinatokana na mnyama ambaye ni halali nyama yake kuliwa, idadi ya vitu hivyo ni kumi na nne, na tunavitaja kama ifuatavyo: 1.

Damu

2.

Kinyesi

3.

Bandama

4.

Uume

5.

Uke

6.

Kende mbili

7.

Nyongo

8.

Mfuko wa mkojo

9.

Chango za tumboni 9

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 9

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

10. Kifuko mfanyizwamo maji yenye dawa yaingiapo damuni na kufanya kazi zingine mwilini 11. Mfuko wa mtoto 12. Mirija miwili yenye kuanzia shingoni hadi mkiani 13. Kipunje kilichopo kwenye ubongo 14. Mboni wa jicho. Vitu ambavyo vinaruhusiwa kuliwa toka kwenye mzoga: Yapo masharti kadhaa ambayo kwa njia moja au nyingine kwa kawaida anapochinjwa mnyama kisheria huwa ni halali kuliwa, na iwapo havitazingatiwa vigezo husika huwa ni haramu kuliwa aidha huwa ni najisi, na huitwa mzoga. Lakini vipo baadhi ya vitu katika mzoga ulionajisi ambavyo huzingatiwa kuwa ni tohara, miongoni mwa vitu hivyo ni kinyama kidogo cha njano ambacho hutumiwa katika kutengenezea siagi, kwa hakika hiyo ni tahiri na inaruhusiwa kuliwa, na imepokewa riwaya kuhusu hilo kutoka kwa Abu Hamza Thumali kutoka kwa Abu Ja’far Imam Muhammad al-Baqir (a.s.), imekuja katika riwaya hiyo kuwa: “Hakika Qutada alimwambia: Nipe habari kuhusiana na siagi?” Akasema (a.s.): “Hakuna taabu kwayo.” Akasema: “Hakika huenda imeingizwa ndani yake kipande kidogo cha njano?” Akasema (a.s.): “Hakuna ubaya wowote.” Wadudu: Na wadudu ni haramu kula nyama yao isipokuwa nzige tu. Na miongoni mwa wadudu ambao ni haramu kuliwa ni chawa, kiroboto, mende na nyoka. Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kuwa amesema:

10

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 10

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

‫ال تؤكل من الحيّات شيئ‬ “Katika nyoka hakiliwi chochote”

Ama nzige hawaruhusiwi miongoni mwao wale wasioweza kuruka, nao huitwa kwa jina la Duba, nao ni wale nzige ambao wanapotembea hazioti mbawa zao, ama wale wawezao kuruka ni halali kuliwa. Wanyama wa baharini: Kwa hakika vigezo vya kisheria vilivyowekwa katika suala la kuhalalisha na kuharamisha kula nyama za wanyama wanaoishi ndani ya maji, ikiwa ni samaki ni wale tu wenye magamba, na magamba ni yale ambayo huwa juu ya ngozi ya samaki. Kwa hivyo samaki ambaye ana magamba ni halali kuliwa, ama ambaye hana magamba ni haramu kuliwa. Ama wale ambao hawaitwi samaki ni haramu kuliwa nyama yao. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Ja’far Imam Muhammad al-Baqir (a.s) pindi alipoulizwa na mmoja wa masahaba wake: Mwenyezi Mungu akurehemu, hakika sisi tunaletewa samaki hawana magamba, tufanye nini? Akasema (a.s.):

‫كل ما له قشر من السمك وما ليس له قشر فال تأكله‬ “Kula kila samaki aliye na magamba, na usile asiyekuwa na magamba.”

Na imepokewa hadithi nyingine kutoka kwa Abu Abdullah Imam as-Sadiq (a.s) kuwa amesema: “Alikuwa Imam Ali (a.s) katika mji wa Kufa akipanda nyumbu wa Mtume (s.a.w.w.), kisha akipita katika soko la samaki, na afikapo hapo husema: 11

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 11

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

‫ال تأكلوا وال تبيعوا ما لم يكن له قشر من السمك‬ ‘Msile, wala msiuze samaki wasiokuwa na magamba.”

Na katika viumbe vya majini ambavyo si samaki ambavyo vyaruhusiwa kuliwa ni kamba - Ruubiyan kwa jina lingine huitwa (Qariidis). Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Hasan Imam Ali Ridha (a.s) pindi alipoulizwa na mmoja wa masahaba wake: “Nafsi yangu nimeitoa fidia kwako, unasemaje kuhusu kula Arbiyan?” Alisema: “Si vibaya hilo.” Na imekuja katika hadithi nyingine kutoka kwa Abu Hasan wa mwanzo yaani Imam Musa Al-Kadhim (a.s) kuwa amesema:

ّ ‫ال‬ ‫الجري وال السلحفاة وال السرطان‬ ّ ‫يحل أكل‬ “Si halali kula mkunga, kobe wala kaa.”

Hukumu ya mayai ya samaki: Kwa hakika mayai ni moja ya aina ya chakula, lakini je, mayai yote ya samaki ni halali au zipo aina zingine za mayai ni halali na nyingine ni haramu? Kwa hakika mayai ya samaki hufuata asili yake, yakiwa mayai ya samaki ambayo yamechukuliwa kutoka kwa samaki aliye halali kuliwa, basi mayai yake ni halali, na samaki ambaye ni haramu kuliwa nyama yake vile vile mayai yake huwa ni haramu, na kigezo hapa ni asili ya samaki ambao mayai yao yamechukuliwa. Ndege: Yapo maandiko yanayohusu uhalali wa baadhi ya ndege na baadhi ya ndege ni makuruhu kuliwa, na yapo maandiko kuhusu baadhi 12

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 12

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

ya wengine ambao ni haramu kuliwa, na tunaeleza hapa kwa urefu kama ifuatavyo: Ndege walio halali kuliwa: Yapo makundi kadhaa ya ndege ambao ni halali kuliwa nao ni: 1.

Njiwa wa aina zote.

2.

Kuku wa aina zote, kama vile wa kienyeji, wa kizungu na kanga.

3.

Bata.

4.

Tetere.

5.

Membe.

6.

Korongo.

7.

Ndege wadogo wa aina zote kwa mfano kasuku, Zarzuur {ndege kama mwamba mweusi} na kisosi.

8.

Tandawala (shingo yake ni ndefu zaidi ya kuku).

9.

Kwale wa Ulaya.

10. Kabju (Anafanana na sikipi). 11. Mbuni. Ndege walio haramu: Yapo maandiko yaliyopokewa ambayo yanaharamisha baadhi ya makundi ya ndege, nayo ni: 13

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 13

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

1.

Kipanga.

2.

Mwewe.

3.

Baashiqu (ndege mkubwa tena mwenye nguvu kama shakevale).

4.

Popo.

5.

Bazi.

6.

Bundi.

7.

Tausi

8.

Kunguru wa aina zote.

9.

Furukombe.

10. Shahiin. 11. Kila ndege mwenye makucha. Imekuja katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Abu Hasan Imam Ali Ridha (a.s) kuwa amesema:

ّ ‫الطاووس ال‬ ‫يحل أكله وال بيضه‬ “Si halali kula Tausi wa mayai yake”

Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam Musa Al-kadhim (a.s) kuwa amesema:

14

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 14

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

ّ ‫ال‬ ‫يحل أكل شيئ من الغربان‬ “Sio halali kula chochote kinachotokana na kunguru.”

1. Ndege walio makuruhu kuliwa: Ni makuruhu kula aina za ndege wafuatazo, miongoni mwa aina hizo ni: 1.

Hudihud.

2.

Mbayuwayu.

3.

Mlamba (Mkiapanda), ni ndege ana kichwa kikubwa pamoja na mdomo mkubwa, tumboni ana rangi nyeupe.

4.

Sawaam, ni ndege ana shingo ndefu, huishi juu ya mitende.

5.

Shuqraaq, ni ndege mwenye michirizi ya rangi ya kijani, nyekungu na nyeupe, hula nyoka.

2. Hukumu ya ndege wengine: Kwanza: Ndege ambao hawakutajwa hapo kabla, tunaweza kuchanganua walio halali na walio haramu miongoni mwao kwa kuzingatia mambo mawili nayo ni: Ambao huzikunjua na kisha kuzituliza mbawa zao wakati wa kuruka. Na ambao huzichezesha na kuacha kuzichezesha mbawa zao wakati wa kuruka. Hivyo tunapomchunguza ndege katika urukaji wake tunamkuta yupo yule ambaye ukunjuaji wa mbawa zake na kuzituliza ni zaidi kuliko kuzichezesha, yaani aghlabu hukunjua mbawa zake na bila kuzichezesha, ndege kama huyo ni haramu. Ama yule ambaye aghlabu huchezesha mbawa zake bila kuzikunjua na kuzituliza, huyo ni halali kuliwa. Na ama ambaye 15

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 15

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

utulizaji wa mbawa zake hulingana sawa na uchezeshaji wake, basi ndege kama huyo ni bora zaidi tuchunguze jambo la pili ambalo tutalieza hilo muda si mrefu, na kama ikishindikana mchanganuo wa kadhia hiyo, basi hapo huwekewa shaka uhalali wake. Pili: Ndege huwa halali ikiwa ana mfuko kooni ambao hukusanya punje za nafaka anazokula, au ana sehemu ndogo ambayo inakusanya vijiwe vidogo ambavyo huvimeza ili kusagia chakula chake, au ana mwiba ambao upo mguuni mwake. Hivyo wasiokuwa na chochote kati ya hayo ni haramu kuliwa. Ikiwa zinasigana alama mbili, kama vile tutakapomkuta ndege ambaye utulizaji wa mbawa zake ni zaidi kuliko uchezeshaji wa mbawa zake, lakini anayo alama ya pili kwamba ana mfuko kooni mwake wa kukusanya punje za nafaka au sehemu ndogo ya kukusanya vijiwe vidogo anavyokula kwa ajili ya kusaga chakula au mwiba uliyopo mguuni mwake, au tukamkuta ndege utingishaji wa mbawa zake ni zaidi kuliko utulizaji wa mbawa zake, lakini hana moja ya vitu vitatu (mfuko wa chukula, mfuko wa kihifadhi vimawe vidogo ili kusaga chakula wala mwiba mguuni kwake), basi linalozingatiwa katika alama ni ya kwanza tu, na hivyo yule ambaye utulizaji wa mbawa zake ni zaidi kuliko utingishaji wake ni haramu kuliwa nyama yake hata kama ana moja ya vitu vitatu vilivyotajwa hapo kabla, na ambaye utingishaji wa mbawa zake ni zaidi kuliko utulizaji wake basi huyo ni halali hata kama hana chochote kati ya hivyo vitatu. 3. Hukumu ya mayai ya ndege: Mayai ya ndege hufuata hukumu ya ndege husika, ikiwa ndege ni halali kuliwa basi vivyo hivyo ni halali mayai yake kuliwa, na lau ikiwa ni haramu kuliwa kadhalika mayai yake huwa ni haramu, ama lau jambo likawa na utata kuhusiana na mayai kwamba hayajulikani 16

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 16

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

chanzo chake, je, ni miongoni mwa ndege walio halali au haramu?! Kwa hivyo kigezo kinachotumika hapa ni kuliangalia yai lenyewe, ikiwa pande mbili za ndani ya yai zinalingana sawa kwa kushikana mzunguko basi yai hilo ni haramu, ama ikiwa pande zake mbili sio zenye kushikana, basi yai hilo ni halali. 4. Aliye haramu kwa sababu ya chakula chake: Hakika wanyama wana chakula chao cha kawaida ambacho hula wakiwa baharini na nchi kavu, hula punje za nafaka mbali mbali, mboga mboga na nyama, wala hakuna tabu yoyote kuhusiana na chakula cha wanyama hawa, isipokuwa tu iwapo chakula hicho ni katika mambo mawili, iwapo mnyama atakula kimoja kati ya hayo mawili, basi kula nyama yake huwa ni haramu hata kama ni yule ambaye kwa asili nyama yake ni halali kuliwa, na mambo mawili hayo ni: 5. Kinyesi cha binadamu: Lau mnyama atakula kinyesi cha binadamu kwa kiwango ambacho mazoea husadiki kwamba kinyesi hicho ndicho chakula chake, kisheria nyama yake huwa ni haramu kuliwa, sawa iwe inatokana na mnyama wa nchi kavu au wa baharini au ndege, na mnyama ambaye hula kinyesi cha binadamu huitwa (Jalal), kwa hivyo ni haramu kula nyama yake, maziwa yake na mayai yake. 6. Miongoni mwa hukumu za mnyama anayekula kinyeshi: Hakika Jalal ni mnyama anayekula kinyesi cha binadamu, na si kinyesi chochote kile au najisi mbali mbali zinginezo. Lau kama atakuwa anakula kinyesi cha binadamu siku moja na siku zingine anakula vyakula vingine, na wala haendelei siku kadhaa kula kinyesi 17

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 17

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

cha binadamu, bila shaka kutokana na hali hiyo halithibiti kwake jina la mnyama anayekula kinyesi (Jalal). 7. Vipi tutamtoharisha mnyama anayekula kinyesi: Inawezekana kumtakasa mnyama aliyezoea kula kinyesi cha binadamu na hatimaye hali hiyo kutoweka kabisa, kwa kweli ataondokana na hali hiyo kwa njia ya kumtenga, na utengaji huo unahusu kumzuia kipindi cha muda maalumu mnyama husika kula kinyesi cha binadamu, na kwa mujibu wa ihtiyat ya wajibu ngamia atengwe siku 40, ng’ombe siku 20 na siku 30 kwa mujibu wa ihtiyat ya istihbabu, na mbuzi na kondoo siku 10, na bata siku 5 na kuku siku 3, na samaki kutwa moja na usiku wake, ama wanyama wengine ni wajibu kuwazuia kutokana na jambo hilo kwa kiwango kinachosadikika kwa mazoea ya watu kuwa imetoweka sifa hiyo. 8. Kunyonya maziwa ya nguruwe: Miongoni mwa mambo ambayo huwafanya wanyama walio halali kuwa haramu ni suala la mbuzi, au ndama au punda kunyonya maziwa ya nguruwe, na maziwa hayo ya nguruwe yatie nguvu mwili wake na hatimaye ikue nyama yake na kuimarika mifupa yake kupitia maziwa hayo, basi ikitokea hali hiyo huwa haramu mnyama aliyenyonya maziwa hayo, aidha inakuwa haramu nyama yake, nyama ya mtoto wake na maziwa yao wote wawili. 9. Kisichokuwa mnyama: Baada ya kueleza kwa urefu lile linalofungamana na hukumu za wanyama walio halali kuliwa na wasio halali, yatupasa sisi kueleza yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu amehalalisha na ambayo ameharamisha miongoni mwa vitu vingine visivyokuwa wanyama, 18

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 18

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

miongoni mwa mimea na visivyokuwa na uhai, navyo vimegawanyika sehemu tano: 10, Vile vinavyoudhuru mwili: Ni haramu kula vitu ambavyo hudhuru mwili wa binadamu na pia husababisha madhara makubwa, ambavyo hupelekea mtu kuangamia, kama vile lau mjamzito atameza dawa yenye kuangusha ujauzito wake, au itapoteza fahamu zake, kama vile lau atameza dawa ambayo itasababisha kupoteza hisia ya kusikia au kuangalia, basi kufanya mambo hayo na yanayofanana na hayo ni haramu. Na kigezo cha madhara hapa ni yale ambayo huhesabiwa na watu wenye akili kuwa ni madhara yatokanayo na sababu hiyo, na kwamba madhara hayo husababishwa na vitu hivyo, kwa mantiki hiyo kila lile ambalo huzingatiwa hivyo na wenye akili basi hilo ni haramu. Na huenda baadhi ya watu wakauliza kuhusiana na ukatwaji wa baadhi ya viungo, kama vile mkono, mguu, jicho au mfuko wa chakula, jambo ambalo hufanywa na watu wengi, hasa wale wenye kupatwa na ugonjwa wa saratani, wanaweza kujiuliza ni ipi hukumu yake? Je, sio miongoni mwa yale ambayo huleta madhara mbele ya watu wenye akili? Jibu: Kwa hakika suala hilo ni lenye tofauti, kwani ukataji wa viungo hapo huwa ndio tiba ya mchakato wa kuponya maradhi hatari ambayo iwapo ukatwaji huo hautafanywa basi hali hiyo itasababisha kuangamia, hivyo kwa mantiki hiyo tendo la ukatwaji hapo linaepusha madhara makubwa. Kwa hakika kufanya matendo hayo ya upasuaji katika hali kama hiyo ni jambo lisilo na mushkeli wowote, hususan baada ya maamuzi ya madaktari bingwa, waaminifu na mahiri na wenye uzoefu mkubwa kwa ajili ya dharura hizo.

19

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 19

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

11. Najisi na kilichonajisika: Ni haramu kula vitu najisi, kama vile damu, mkojo n.k sawa viwe kimiminika au kisichokuwa kimiminika, vivyo hivyo ni haramu kula vitu vilivyonajisika, sawa viwe vimiminika kama vile maji ambayo damu imedondokea humo au vitu vilivyo vigumu kama vile samli ambayo najisi imeangukia juu yake. 12. Pombe na madawa ya kulevya: Pombe ni miongoni mwa vitu vya haramu, na itikadi ya uharamu wake ni miongoni mwa mambo ambayo yameelezwa wazi wazi na dini ya Kiislamu, vile vile pombe ni mama wa machafu. Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa amesema:

ّ ‫ان الخمر أ ّم الخبائث ورأس‬ ّ ‫شر يأتي على‬ ّ ‫كل‬ ‫شاربها ساعة يسلب لبه فال يعرف ربّه وال يترك‬ ّ ‫اال ركبها وال يترك حرمة‬ ّ ‫معصية‬ ‫اال انتهكها‬ ّ ‫اال قطعها وال فاحشة‬ ّ ‫وال رحما ماسة‬ ‫اال أتاها‬ “Hakika pombe ni mama wa machafu, na kichwa cha kila shari, itafika wakati mnywaji pombe atatokwa na akili na hapo asimjue Mola Wake, wala haoni maasi ila atayafanya, wala haoni haramu ila ataitenda, wala undugu wa karibu mno ila ataukata, wala uovu ila ataufanya.”

Na imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema:

20

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 20

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

‫ غارسها وحارسها وعاصرها‬:‫لعن فيها عشرة‬ ‫وشاربها وساقيها وحاملها والمحمول اليه‬ ‫وبائعها ومشتريها وآكل ثمنها‬ “Katika pombe wamelaaniwa watu kumi; Mlimaji wake, mlinzi wake, mkamuaji wake, mnywaji pombe, mshwaji wake, mbebaji wa pombe, mpelekewa, muuzaji pombe, mnunuzi na mwenye kula thamani yake.”

Na kila kilevi hukumu yake ni hukumu ya pombe, sawa kiwe ni kimiminika au sio kimiminika (madawa ya kulevya), na kila kinacholewesha kidogo au sana hukumu yake ni haramu. 13. Juisi ya zabibu iliyochemshwa: Ni haramu kunywa juisi ya zabibu pindi inapochemka, sawa uchemkaji huo uwe unatokana na moto au jua au jambo lingine, kwa hakika inapoanza tu kuchemka papo hapo unaanza uharamu wake, wala katika hukumu hiyo haiunganishwi juisi ya zabibu isiyochemshwa na juisi nyingine, kwa hivyo juisi ya balungi na juisi ya tende haziwi haramu kwa kuchemka, isipokuwa tu itakapothibiti kwamba hizo mbili ni vileo, basi hapo nazo zitakuwa haramu. 14. Udongo: Miongoni mwa mambo ya haramu ni kula udongo, nao ni udongo uliyochanganyika na maji (yaani tope), na ni haramu hata ukikauka na kuwa dongo, ama udongo uliyo mkavu ikiwa ulaji wake hausababishi madhara basi unaruhusiwa kuliwa.

21

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 21

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

15. Udongo ambao ni halali kuliwa: Udongo ambao ni halali kuliwa una mambo kadhaa, nayo ni: i.

Udongo huo uwe ni ule uliochukuliwa kutoka katika kaburi la Imam Husein (a.s.) kwa lengo la kujitibu, wala haifai kwa lengo lingine lisilokuwa hilo, na inaruhusiwa kula kiasi kidogo ukubwa wa punje ya ulezi ya kati na kati, wala hairuhusiwi kula zaidi ya hivyo, na hairuhusiwi kula udongo kutoka katika kaburi la sharifu mwingine yeyote yule, kwani hukumu hiyo inahusu tu kaburi la Imam Husein (a.s).

ii. Udongo ambao huliwa na binadamu kwa dharura ya ugonjwa kama vile udongo uitwao udongo wa Armani, lakini hairuhusiwi kula udongo huu ila iwapo tu ni dawa pekee yenye kutibu maradhi husika, ama iwapo inawezekana mgonjwa kujitibia kwa dawa zingine basi hairuhusiwi wakati huo kutumia udongo. 16. Hukumu za dharura: Kwa hakika hukumu mbali mbali za kisheria zilizotangulia hapo kabla ni hukumu ambazo humlazimu mtu katika hali ya mwanzo ya kawaida, isipokuwa zipo hali zingine ambazo huondoa uharamu kwa muda fulani, hali ambazo humfanya mtu atumie chakula au kinywaji kilichoharamishwa, katika hali hizo na zinazofanana na hizo mukalafu ana hukumu mahsusi, hukumu hizo ni: i.

Anaruhusiwa mtu kutumia jambo lolote lile la haramu ambalo maelezo yake yametangulia hapo kabla katika suala la vyakula na vinjwaji lau ikiwa itahusiana na matibabu, na kwa hivyo ikahitajika kula aina za vyakula hivyo vya 22

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 22

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

haramu, kwa mfano msafiri akiwa jangwani akashikwa na njaa kali sana na hakupata chochote cha kula isipokuwa mzoga na akakaribia kuangamia, basi katika hali hiyo itamlazimu kula kiasi ambacho kitamfanya kubakia hai. ii. Anaruhusiwa hayo pale anapopatwa na ugonjwa, na kwamba tiba yake inategemea kula kitu cha haramu, kwa mfano kula nyama ya Nungunungu, na mtu akachelea nafsi yake kupatwa na kifo kwa sababu ya ugonjwa, katika hali hiyo inamlazimu yeye afanye haraka kula kile ambacho kitamuokoa yeye kutokana na kuangamia. iii. Inaruhusiwa lau atakhofia nafsi yake kutokana na udhaifu mkubwa ambao sio wa kawaida, na mfano wa hilo ni kwamba mwanadamu ambaye amezuiwa njia au amefungiwa katika mahala ambapo hakuna isipokuwa vyakula vyenye najisi, na akaendelea kubakia hivyo bila chakula hadi akachelea nafsi yake udhoofu mkubwa ambao kwa kawaida mtu hawezi kustahamili, basi katika hali hiyo ni wajibu kwake kula kile kilicho najisi ili asifikwe na hali ya kupatwa na ugonjwa hatari. iv. Hofu juu ya nafsi yenye heshima; kama vile lau mjamzito yupo katika sehemu ambayo hakuna chakula isipokuwa mzoga, na lau kama hatokula sehemu ya mzoga basi kitakufa kichanga kilichomo tumboni mwake, basi katika hali hiyo hukumu yake ni kula sehemu ya mzoga huo kiasi cha kuhifadhi uhai wa kichanga ambacho kimo tumboni mwake. v.

Katika hali ya kulazimishwa; nayo ni pale atakapolazimishwa na mtu kwa kushikiwa mtutu wa 23

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 23

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

bunduki au silaha nyingine ili ale chakula ambacho hakiruhusiwi kuliwa, kwa mfano nyama ya nguruwe, amepewa hiari ya kuchagua kati ya mambo haya; ima ale au auawe au ajeruhiwe, basi hapo ni wajibu kwake kula nyama hiyo ili aiokoe nafsi yake na hatari. 17. Angalizo muhimu: i.

Katika mazingira ya dharura inawajibika kutosheka kwa kadiri ya chini zaidi ya mahitaji ya dharura iliyolazimu kutenda mambo ambayo kiasili ni haramu, yaani iwe ni kwa kadiri ya dharura, hivyo akiwa ni mwenye njaa haruhusiwi kula chakula cha haramu hadi kushiba, bali lililo la wajibu katika hali hiyo ni kula kiwango cha kuzuia njaa.

ii. Katika mazingira ya dharura tuliyoyataja hapo kabla ni wajibu kwa mukallafu kuyatenda hayo, wala haifai kuiepusha nafsi yake na hayo, kama vile mtu asema: Kufa ni bora kuliko kula nyama ya mzoga, au kufa kwa kiu ni bora kuliko kunywa kitu kilicho najisi n.k.

24

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 24

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

SEHEMU YA PILI ADABU ZA KULA Utangulizi:

K

wa hakika sheria takatifu imeweka adabu nyingi za kula chakula, kama ilivyokwishatangulia hapo kabla kwamba hukumu za Mwenyezi Mungu zipo kwa ajili ya maslahi na kuepusha madhara, kwani adabu ambazo Mwenyezi Mungu ameziweka kuhusiana na mtu anapokuwa katika meza ya chakula na namna ya kula na kunywa zina faida nyingi, miongoni mwa faida hizo ni zile ambazo zimegunduliwa na elimu na tiba za kisasa, na kati ya hukumu hizo bado maslahi na faida zake hazijajulikana hadi hivi sasa, ila hakika itikadi yetu ni kwamba mambo ambayo ameamrisha Mwenyezi Mungu hapana budi yapo kwa maslahi ya waja, nayo ni imani ya utekelezaji wa kiibada, na kwamba binadamu anastahiki juu yake kupata malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na tutazungumza muda mfupi ujao baadhi ya adabu ambazo zimepokewa na hadithi tukufu au nukuu mbali mbali kutokana na taratibu na nyendo za maisha ya Bwana Mtume (s.a.w.w.) pamoja na maisha ya Ahlul-Bayt wake (a.s), huenda Mwenyezi Mungu Mtukufu akatuwezesha kutenda amali njema kwa miongozo yao kwani Yeye ni Mwezeshaji wa kila jambo. Faida za kula kidogo: Kwa hakika hali ya mtu kula chakula kidogo hutoa nafasi kubwa kwa mtu katika kuhifadhi afya yake ya kimwili, vile vile huwa na 25

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 25

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

faida nyingi mno katika nafsi ya mtu, na kutokana na umuhimu wake ni vyema kuzitupia macho hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.), ambazo zinahimiza kula chakula kidogo, pia zinataja faida zake. Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kuwa amesema:

‫للصحة‬ ‫قلّة الغذاء أكرم للنفس وأدوم‬ ّ “Kula chakula kidogo ni bora zaidi kwa nafsi na hudumisha afya.”

Na imepokewa hadithi kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kuwa amesema:

ّ ‫من‬ ‫قل طعامه قلّت آالمه‬ “Mwenye kula kidogo basi hupungua maumivu yake.”

Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam Musa Al-Kadhim (a.s.) kwamba amesema:

ّ ‫لو‬ ‫ان النّاس قصدوا في الطعم العتدلت أبدانهم‬ “Lau watu wangelikadiria kula basi miili yao ingekuwa ya wastani.”

Na huenda hilo likawa hivyo kwani kula sana na kukithirisha kula aina mbali mbali za vyakula huchafua mfuko wa chakula ambao huzingatiwa kuwa ni miongoni mwa viungo muhimu na nyeti mno, na husababisha madhara mbali mbali ndani ya mwili, vivyo hivyo kuuhifadhi mfuko huo wa chakula ni kati ya yale ambayo huleta raha kwa mwanadamu, na maradhi ya kisasa yatosha kuonesha umuhimu 26

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 26

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

wa kutokula sana, ambapo tunashuhudia katika zama hizi matokeo mabaya ya kula sana, na miongoni mwa matokeo hayo ni maradhi ya unene ambayo watu huyaita kwa jina la maradhi ya kisasa, kwani watu wengi wanasumbuliwa na matatizo ya unene na maradhi ya moyo na mengineyo yatokanayo na ulafi wa chakula. Madhara ya kula sana: Hakika kula sana sio miongoni mwa mambo yenye kusifiwa kisheria, na zimepokewa hadithi chungu nzima zenye kutilia mkazo juu ya ukaraha wa jambo hilo. Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kuwa amesema:

‫شر العيوب‬ ّ ‫كثرة األكل من الشره والشره‬ “Kula sana ni miongoni mwa ulafi, na ulafi ni aibu mbaya zaidi.”

Na huenda kukithirisha kula kukasababisha athari mbaya kwa mtu kwa sababu ya umuhimu wa mfuko wa chakula, na hatimaye ikasadifu kwake hadithi iliyo mashuhuri iliyopokewa kutoka kwa Amiirul-Mu’miniina Ali (a.s.) kuwa alisema:

‫كم من أكلة تمنع أكالت‬ “Ni vyakula vingapi vimezuia vyakula vingine.”

Hayo ni madhara ya kimwili, lakini pia yapo madhara ya kiroho ambayo husababishwa na ulafi na kuvimbiwa, hali ambayo huathiri moyo na mwelekeo wake, ndio maana ulinganio wa Maimamu (a.s.) kwetu sisi ulikuwa tusile isipokuwa tunapohisi njaa. Imekuja katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: 27

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 27

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

‫كل وأنت تشتهي وأمسك وأنت تشتهي‬ “Kula hali ya kuwa una hamu na chakula, na acha kula ilihali ­unakitamani.”

Miongoni mwa adabu za meza ya chakula Nawa kabla na baada ya kula: Kunawa kabla ya kula na baada ya kula ni katika adabu za Kiislamu, hakika sheria ya Kiislamu imelipa umuhimu makhsusi suala la usafi, na suala la kula ni miongoni mwa mambo ambayo tumeamrishwa kuwa na adabu nalo, miongoni mwa adabu zake ni kuosha mikono miwili kabla ya kuanza kula na baada ya kula. Imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema:

‫الوضوء قبل الطعام وبعده ينفي الفقر‬ “Kunawa kabla na baada ya kula kunaepusha ufukara.”

Na imekuja katika hadithi nyingine kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema:

‫اذا توضأت بعد الطعام فامسح عينيك بفضل ما‬ ‫الرمد‬ ّ ‫في يديك فانّه أمان من‬ “Utakaponawa baada ya kula chakula basi paka macho yako mawili kwa majimaji yaliyobakia mkononi mwako, kwani kufanya hivyo ni usalama kutokana na ugonjwa wa macho.” 28

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 28

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

Na miongoni mwa adabu za kula ni mtu akinawa kabla ya kula asitumie taulo (kitambaa) ili kukausha mikono yake kabla ya kula. Hakika imepokewa hadithi kutoka kwa Sufyan Al-Jamal amesema: “Tulikuwa kwa Abu Abdillah (a.s.), kikaletwa chakula, basi msaidizi akaleta chombo cha kunawia, na akampa kitambaa (taulo), basi hilo lilimchukiza mno, kisha akasema: ‘Tumenawa kwa sababu ya hilo.”’ Si vibaya mtu kukausha mikono yake baada ya kunawa baada ya kula, imekuja katika riwaya kutoka kwa Nazar amesema: “Nilimuona Abu Hasan (a.s.) anaponawa kabla ya kula hagusi kitambaa (taulo), lakini akinawa baada ya kula hujifuta kwa kitambaa (taulo). Soma Bismillahi na omba dua: Miongoni mwa adabu zilizo mashuhuri ni kusoma Bismillah na kuomba dua, imepokewa hadithi kutoka kwa Amirul-Mu’miniina Ali bin Abi Talib (a.s.) kuwa amesema:

‫اذكروا اهلل عز وجل عند الطعام وال تلغوا فيه‬ ‫فانّه نعمة من نعم اهلل يجب عليكم فيها شكره‬ ‫وحمده أحسنوا صحبة النّعم قبل فراقها فانّها‬ ‫تزول وتشهد على صاحبها بما عمل فيها‬ “Mtajeni Mwenyezi Mungu wakati wa kula wala msifanye upuuzi katika hilo, kwani hiyo ni neema miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu, ni wajibu juu yenu kwayo kumshukuru Yeye na kumtukuza Yeye, amilianeni vizuri na neema kabla ya kutoweka kwake, kwani hutoweka na itamshuhudia sahiba wake kwa yale ambayo ameitendea.” 29

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 29

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

Na katika riwaya nyingine imepokewa kutoka kwa Imam asSadiq (a.s.) kuwa amesema: Hakika Mtume (s.a.w.w.) amesema:

ّ ‫اذا وضعت المائدة‬ ‫حفها أربعة أمالك فاذا قال‬ ‫ اخرج يا‬:‫(بسم اهلل) قالت المالئكة للشيطان‬:‫العبد‬ :‫ واذا فرغوا فقالوا‬.‫فاسق فال سلطان لك عليهم‬ ‫ قوم أنعم اهلل عليهم‬:‫الحمد هلل قالت المالئكة‬ ‫ بسم اهلل قالت‬:‫ واذا لم يقل‬.‫فأ ّدوا الشكر لربّهم‬ ‫ واذا‬.‫ ادن يا فاسق فكل معهم‬:‫المالئكة للشيطان‬ :‫رفعت المائدة ولم يحمدوا اهلل قالت المالئكة‬ .‫قوم أنعم اهلل عليهم فنسوا ربّهم‬ “Litakapoletwa sinia la chakula huzungukwa na malaika wanne pembezoni mwake, na atakaposema mja: “Bismillah” malaika watasema kumwambia shetani: ‘Toka ewe muovu wala huna uwezo na mamlaka juu yao.’ Na atakapomaliza na kusema: “Al-hamdulillah”, Malaika watasema: ‘Watu wameneemeshwa na Mwenyezi Mungu basi wakatekeleza shukurani kwa Mola Wao.’ Na ikiwa hatasema: “Bismillah”, Malaika watasema kumwambia shetani: ‘Karibia ewe muovu kula pamoja nao.’ Na litakapoondolewa sinia la chakula bila kumuhimidi Mwenyezi Mungu, Malaika watasema: ‘Watu wameneemeshwa na Mwenyezi Mungu lakini wamemsahau Mola Wao.”’

Na imepokewa kwamba inatakiwa kusoma Bismillah kwa kila aina ya chakula kilichopo mezani, na ikiwa mtu atakuwa amesahau 30

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 30

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

kufanya hivyo basi afanye lile ambalo Imam as-Sadiq (a.s.) ameusia, imepokewa hadithi kutoka kwake (a.s) kuwa amesema:

ّ ‫أن من نسي أن يسمي على‬ ّ ‫ بسم‬:‫كل لون فليقل‬ ‫اهلل على أ ّوله وآخره‬ “Mwenye kusahau kusema Bismillah katika kila aina ya chakula basi aseme: Bismillah katika mwanzo wake na mwisho wake.”

Tumia muda mrefu: Miongoni mwa adabu za kula ni mtu atumie muda mrefu akiwa anakula, na asifanye haraka kumaliza chakula, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hatomuuliza kuhusu wakati ambao mtu anautumia kujipatia mlo, na imepokewa hadithi kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kuwa amesema:

‫أطيلوا الجلوس على الموائد فانها ساعة ال‬ ‫تحسب من أعماركم‬ “Refusheni muda wa kukaa katika meza ya chakula, kwani huo ni muda ambao hauhesabiwi katika umri wenu.”

Kula punje zilizodondoka: Miongoni mwa adabu za kula chakula ni kuokota punje za chakula zilizodondoka. Imepokewa hadithi kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: 31

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 31

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

‫من وجد كسرة أو تمرة فأكلها لم تفارق جوفه‬ ‫حتى يغفر اهلل له‬ “Mwenye kupata kipande au tende na akala basi haitotoka tumboni mwake hadi Mwenyezi Mungu amsamehe.”

Na miongoni mwa thawabu ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amemwahidi mwenye kutenda amali hii ambayo mtu anaweza akaiona kuwa ni ndogo, imepokewa ya hadithi kutoka kwa Imam Ali Ridhaa (a.s.) kuwa amepokea kutoka kwa jadi zake kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema:

‫ما سقط من المائدة مهور الحور العين‬ “Ambacho kina dondoka katika meza ya chakula ni mahari ya ­Hurulaini.”

Kwa hivyo mwenye kupenda kulipa mahari ya Hurulaini kabla hajaingia peponi ni juu yake kufuata Sunnah ya Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.), na kufanya kitendo hiki kidogo chenye malipo makubwa. Anza na malizia kwa chumvi: Vile vile miongoni mwa adabu za kula ni mtu aanze kwa kuramba kidogo chumvi, vivyo hivyo amalizie kwa kuramba chumvi. Imepokewa hadithi kwamba Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Imam Ali (a.s.):

‫يا علي افتح بالملح واختتم به فانّه شفاء من‬ 32

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 32

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

‫سبعين داء منها الجنون والجذام والبرص ووجع‬ ‫الحلق ووجع األضرس ووجع البطن‬ “Ewe Ali anza kula kwa kuramba kidogo chumvi na malizia kwa kufanya hivyo, kwani hiyo ni tiba ya magonjwa sabini, miongoni mwa magonjwa hayo ni uwendawazimu, ukoma, upofu, maumivu ya koo, maumivu ya meno na maumivu ya tumbo.”

Mtu ale sehemu iliyo mbele yake: Ni ada kwamba mtu ale sehemu iliyo mbele yake, yaani upande wa mbele ya chakula, vivyo hivyo huzingatiwa katika mazoea ya watu kwamba kula sehemu iliyo mbele ya wengine ni katika ada na desturi mbaya, hali kadhalika sheria imetufundisha na kutuelekeza tuwe na adabu hiyo. Imekuja katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema:

‫اذا وضعت المائدة بين يدي الرجل فليأكل م ّما‬ ‫يليه وال يتناول م ّما بين يدي جليسه‬ “Chakula kikiwekwa mbele ya mtu basi ale sehemu iliyo mbele yake, wala asile sehemu ya mwingine aliyekaa naye.”

Mlishe yule mwenye hamu na chakula chako: Miongoni mwa adabu muhimu ni mtu ajifunze kuwafariji wengine kupitia mambo ya dunia yake, hivyo awafariji masikini kwa chakula chake pindi anaposimama na kumwangalia yeye akila. Imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: 33

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 33

11/25/2014 4:23:12 PM


Vyakula na Vinywaji

‫من أكل وذوا عينين ينظر اليه ولم يواسه ابتلي‬ ‫بداء ال دواء له‬ “Mwenye kula na anaangaliwa na mwenye macho mawili na wala hakumfariji, basi atapatwa na ugonjwa usiokuwa na dawa.”

Bali hakika Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) wametufundisha tutosheke na tujali haja za wengine hata za mnyama pindi anaposimama mbele yetu wakati tunakula. Imepokewa hadithi kwamba: Nilimuona Hasan bin Ali (a.s.) akila na mbele yake kuna mbwa, kila alipokuwa akila tonge moja basi alimtupia pia mbwa mfanowe, nikasema kumwambia yeye: Ewe mtoto wa Mtume (s.a.w.w.) unamhurumia huyu mbwa kwa chakula chako? Akasema:

‫دعه انّي ألستحيي من اهلل تعالى أن يكون ذوا‬ ‫روح ينظر في وجهي وأنا آكل ث ّم ال أطعمه‬ “Achana nalo, hakika mimi ninaona haya kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwepo kiumbe mwenye roho ananiangalia usoni nami nakula, kisha nisimpatie chakula.”

Kutokula kwa mkono wa kushoto: Miongoni mwa adabu za Kiislamu ambazo zimesisitizwa na hadithi mbali mbali ni kwamba mtu asile au kunywa kwa mkono wa kushoto, bali ale chakula kwa mkono wake wa kulia. Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kuwa amesema :“Ni makuruhu kula na kunywa kwa mkono wa kushoto.”

34

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 34

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

Usile hali yakuwa unatembea: Na kula wakati wa kutembea ni miongoni mwa mambo ambayo hayapendezi katika jamii, hususan kwa mtu muumini, bali tendo hilo ni kati ya yale ambayo huangusha hadhi ya mtu na heshima yake mbele ya macho ya watu. Zipo hadithi mbali mbali zenye kukataza jambo hilo, imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Abdullah Imam as-Sadiq (a.s.) kuwa amesema:

ّ ‫ال تأكل وأنت تمشي‬ ‫تضطر الى ذلك‬ ‫اال أن‬ ّ “Usile hali ya kuwa wewe unatembea isipokuwa ukilazimika kufanya hivyo.”

Usile chakula cha moto: Hakika sheria takatifu imetufundisha sisi kungojea mpaka chakula kipoe. Imepokewa hadithi kutoka kwa Amirul-Mu’miniina Ali bin Abi Talib (a.s.) kuwa amesema:

ّ ‫أقروا الحار حتى يبرد‬ ‫فان رسول اهلل ص قرب‬ ‫ أقروه حتى يبرد ما كان‬:‫اليه طعام حار فقال‬ ‫اهلل ليطعمنا النار والبركة في البارد‬ “Acheni chakula cha moto hadi kipoe, hakika Mtume (s.a.w.w.) siku moja aliletewa chakula cha moto akasema: Kiacheni hadi kipoe, Mwenyezi Mungu si mwenye kutulisha sisi chakula cha moto na hali chakula cha baridi ndicho chenye baraka.”

Vili vile miongoni mwa adabu zilizoelezwa na sheria ni mtu asipulize chakula cha moto ili kukipoza, anatakiwa akiache hadi 35

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 35

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

kipoe chenyewe. Imepokewa hadithi kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kuwa amesema:

‫ونهى أن ينفخ في طعام أو شراب‬ “Na amekataza (Mtume) kupuliza chakula au kinywaji.”

36

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 36

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

MWISHO ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1.

i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili

ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini

2.

Uharamisho wa Riba

3.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza

4.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili

5.

Hekaya za Bahlul

6.

Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)

7.

Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)

8.

Hijab vazi Bora

9.

Ukweli wa Shia Ithnaashari

10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 37

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 37

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 38

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 38

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 39

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 39

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 100. Idi Al-Ghadir 40

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 40

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunna za Nabii Muhammad (saww) 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Mwanamke Na Sharia 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 41

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 41

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1

42

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 42

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 43

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 43

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi

44

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 44

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 227. Yafaayo kijamii 228. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 229. Mkakati wa Kupambanana Ufakiri 230. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 45

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 45

11/25/2014 4:23:13 PM


Vyakula na Vinywaji

231. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 232. Imam Mahdi Na Bishara Ya Matumaini 233. Jihadi 234. Majanga Na Jukumu La Jamii 235. Muhadhara wa Maulamaa 236. Mashairi ya Kijamii 237. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 238. Mwanamke Katika Harakati za Mageuzi 239. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 240. Yusuf Mkweli 241. Hotuba Za Kiislamu Juu ya Haki Za Binadamu 242. Ugaidi wa Kifikra katika Medani ya Kidini

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Ya Muhammadi (s.a.w.w) Na Aba’ Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n’amavuko by’ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

46

41_14_Vyakula Na Vinywaji_25_Nov_2014.indd 46

11/25/2014 4:23:13 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.