WITO KWA WAUMINI َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ...ين آ َمنُوا “ENYI MLIOAMINI!....”
Kimekusanywa na kuandikwa na: Muhammad A. Bahsan
Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 1
12/8/2014 2:43:33 PM
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 2
12/8/2014 2:43:33 PM
© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation
ISBN No: 978 – 9987 – 17 – 088 – 3
Kimeandikwa na: Muhammad A. Bahsan
Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba Selemani
Kimepitiwa na: Al Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo Na Mubarak A. Nkanatila
Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
Toleo la kwanza: Julai, 2015 Nakala: 1000
Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S. L. P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 3
12/8/2014 2:43:33 PM
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 4
12/8/2014 2:43:33 PM
YALIYOMO Neno la Mchapishaji.................................................................................................. 1 Utangulizi................................................................................................................... 2 WITO WA KWANZA.............................................................................................. 4 Sababu ya Kuteremka................................................................................................ 4 Maelezo .................................................................................................................... 5 WITO WA PILI....................................................................................................... 9 Sababu ya Kuteremka................................................................................................ 9 Maelezo .................................................................................................................... 9 Kubakia Hai kwa Mashahidi.................................................................................... 12 Duniani ni Mahala pa Mtihani................................................................................. 13 Kwa nini Mwenyezi Mungu Awatahini Watu.......................................................... 14 Mtihani wa Mwenyezi Mungu ni kwa Waja Wake Wote......................................... 16 Maudhui ya Mtihani................................................................................................. 17 Sababu za Kufaulu Mtihani..................................................................................... 18 WITO WA TATU................................................................................................... 20 Maelezo .................................................................................................................. 21 Vizuri ni kwa Ajili ya Waumini............................................................................... 21 WITO WA NNE..................................................................................................... 24 Sababu za Kuteremka.............................................................................................. 24 Kisasi ni Uhai........................................................................................................... 24 Mtazamo wa Baadhi ya Watu Katika Kisasi............................................................ 26 Je, Hukumu ya Kisasi Inamdhulumu Mwanamke?................................................. 28 Udugu wa Kiislamu................................................................................................. 29 Uzuri wa Sheria za Kiislamu................................................................................... 29 WITO WA TANO.................................................................................................. 31
v
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 5
12/8/2014 2:43:33 PM
WITO KWA WAUMINI
Maelezo: Swaumu ni Chuo Cha Uchamungu.......................................................... 32 Faida za Kiroho, Kijamii, na Kisiha Zitokanazo na Swaumu:................................ 35 Athari nzuri za Kiafya Zitokanazo na Swaumu:...................................................... 38 Swaumu ya Umma Zilizotangulia:.......................................................................... 38 Utukufu wa Mwezi wa Ramadhani.......................................................................... 40 Kanuni ya Kutotenzwa Nguvu................................................................................. 42 Sababu ya Kuteremka:............................................................................................. 42 Masharti ya Kukubaliwa Du’a................................................................................. 47 Sababu ya Kuteremka:............................................................................................. 47 Maelezo .................................................................................................................. 48 Utafiti
.................................................................................................................. 49
1. Mipaka ya Mwenyezi Mungu.................................................................... 49
2. Ibada Ya Itikafu:......................................................................................... 49
WITO WA SITA..................................................................................................... 50 Maelezo .................................................................................................................. 53 WITO WA SABA................................................................................................... 53 Maelezo .................................................................................................................. 56 WITO WA NANE.................................................................................................. 55 Maelezo .................................................................................................................. 56 Mfano Mwema:........................................................................................................ 56 Utafiti
.................................................................................................................. 57
WITO WA TISA.................................................................................................... 59 Sababu ya Kuteremka.............................................................................................. 59 Maelezo .................................................................................................................. 60 Mazingatio............................................................................................................... 61 Kupambana Dhidi ya Vikwazo vya Utowaji:.......................................................... 61 WITO WA KUMI.................................................................................................. 64 Sababu ya Kuteremka.............................................................................................. 65 vi
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 6
12/8/2014 2:43:33 PM
WITO KWA WAUMINI
Maelezo .................................................................................................................. 65 Madhara ya Riba:..................................................................................................... 67 WITO WA KUMI NA MOJA............................................................................... 69 Maelezo .................................................................................................................. 70 Utafiti
.................................................................................................................. 73
WITO WA KUMI NA MBILI.............................................................................. 76 Mazingatio............................................................................................................... 79 WITO WA KUMI NA TATU................................................................................ 76 Sababu ya Kuteremka.............................................................................................. 80 Maelezo .................................................................................................................. 81 Wito wa Umoja........................................................................................................ 82 Maadui wa Jana Leo ni Marafiki:............................................................................ 82 Umuhimu wa Umoja................................................................................................ 84 Kutetea haki na Kuung'oa Ufisadi:.......................................................................... 85 Umuhimu wa Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya........................................... 85 Je, Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya Kunamnyima Mtu Uhuru?................. 87 WITO WA KUMI NA NNE.................................................................................. 88 Sababu ya Kuteremka.............................................................................................. 88 Maelezo .................................................................................................................. 89 Chuki baada ya Upendo........................................................................................... 90 Tahadhari Kwa Waislamu:....................................................................................... 90 WITOWA KUMI NA TANO................................................................................ 92 Maelezo: Kuharamishwa Riba kwa Awamu............................................................ 92 Uharamu wa Riba Katika Aya Tunayoitafsiri.......................................................... 94 WITO WA KUMI NA SITA................................................................................. 96 Maelezo .................................................................................................................. 98 WITO WA KUMI NA SABA................................................................................ 98 Maelezo .................................................................................................................. 98 vii
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 7
12/8/2014 2:43:33 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA NANE............................................................................. 100 WITO WA KUMI NA TISA............................................................................... 102 Maelezo ................................................................................................................ 104 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 104 Utetezi wa Haki za Wanawake:............................................................................. 105 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 107 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 108 Maelezo ................................................................................................................ 108 Maelezo ................................................................................................................ 112 Ndoa ya Mut'a Katika Uislamu:............................................................................. 112 Ndoa ya Mut'a ni rehema kwa Jamii:..................................................................... 117 Hoja Dhidi ya Ndoa ya Mut'a:............................................................................... 118 Kwa Nini Kukawekwa Masharti Haya?................................................................ 122 WITOWA ISHIRINI........................................................................................... 124 Uchumi Mzuri ni Sababu ya Utulivu wa Jamii:.................................................... 124 Madhambi Madogo Yanapokuwa Makubwa......................................................... 126 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 128 Maelezo………………………………………………………….......................... 129 WITO WA ISHIRINI NA MOJA………………………………....................... 130 Maelezo – Baadhi ya Hukumu za Kifiqhi…………………………...................... 130 WITOWA ISHIRINI NA MBILI....................................................................... 134 Ni Kina Nani Hao Ululul Amri:............................................................................. 134 Utafiti Katika Nadharia Zilizotajwa:...................................................................... 135 Ushahidi wa Hadithi:............................................................................................. 136 WITO WA ISHIRINI NA TATU........................................................................ 138 WITO WA ISHIRINI NA NNE.......................................................................... 140 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 140
viii
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 8
12/8/2014 2:43:33 PM
WITO KWA WAUMINI
Maelezo ................................................................................................................ 141 Vita Vya Jihadi Havina Lengo la Kujitajirisha:..................................................... 141 WITO WA ISHIRINI NA TANO....................................................................... 143 Uadilifu wa Kijamii:.............................................................................................. 143 WITO WA ISHIRINI NA SITA.......................................................................... 145 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 145 Maelezo ................................................................................................................ 145 WITO WA ISHIRINI NA SABA........................................................................ 147 Maelezo ................................................................................................................ 147 WITOWA ISHIRINI NA NANE........................................................................ 149 Maelezo:Ulazima wa Kutekeleza Ahadi:............................................................... 149 WITOWA ISHIRINI NA TISA.......................................................................... 151 Maelezo: Hukumu Nane Katika Aya Moja:........................................................... 152 Kusaidiana Katika Mambo Mema:........................................................................ 154 Hali ya Kati na Kati Katika Ulaji wa Nyama:....................................................... 155 Ni Lini Mwenyezi Mungu Aliikamilisha Dini?..................................................... 156 Baadhi ya Vigezo Vinavyounga Mkono Rai Hii:................................................... 158 WITO WA THELATHINI.................................................................................. 160 Kujisafisha Kimwili na Kiroho:............................................................................. 160 Hekima ya Kutayammamu:................................................................................... 162 Hekima ya Kukoga:............................................................................................... 164 WITO WA THELATHINI NA MOJA............................................................... 166 Maelezo ................................................................................................................ 166 Uadilifu ni Nguzo Muhimu Katika Uislamu:........................................................ 166 WITOWA AROBAINI NA MBILI.................................................................... 169 Maelezo ................................................................................................................ 169 WITO WA THELATHINI NA TATU................................................................ 171 Maelezo ................................................................................................................ 171 ix
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 9
12/8/2014 2:43:33 PM
WITO KWA WAUMINI
Kutawasali Katika Qur’ani:................................................................................... 172 Kutawasali Katika Riwaya:.................................................................................... 174 Angalizo ................................................................................................................ 176 WITOWA THELATHINI NA NNE................................................................... 178 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 178 Maelezo ................................................................................................................ 179 Kuwategemea Wageni:.......................................................................................... 181 WITO WA THELATHINI NA TANO............................................................... 183 Maelezo ................................................................................................................ 183 Ni Akina Nani Hao Walioamini?........................................................................... 185 WITO WA THELATHINI NA SITA.................................................................. 187 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 187 Maelezo ................................................................................................................ 187 Adhana ni Alama Kubwa ya Uislamu:................................................................... 188 Kushuka Wahyi wa Adhana kwa Mtume (s.a.w.w.):.............................................. 189 WITO WA THELATHINI NA SABA................................................................ 191 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 191 Maelezo ................................................................................................................ 193 WITOWA THELATHINI NA NANE................................................................ 196 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 196 Maelezo:Awamu za Kuharamishwa Ulevi:............................................................ 197 Madhara Yatokanayo na Kamari:........................................................................... 200 WITOWA THELATHINI NA TISA.................................................................. 202 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 202 Hukumu za Uwindaji wakati wa Ihramu:.............................................................. 202 WITOWA AROBAINI........................................................................................ 204 Hekima Ya Kuharamishwa Kuwinda:.................................................................... 207 WITOWA AROBAINI NA MOJA..................................................................... 208 x
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 10
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 208 Maelezo: Maswali ya Ziada:.................................................................................. 209 WITO WA AROBAINI NA MBILI................................................................... 212 Maelezo:Kila Mtu na Majukumu Yake:................................................................. 212 Ufahamu Mbaya:................................................................................................... 213 WITO WA AROBAINI NA TATU..................................................................... 215 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 216 Maelezo ................................................................................................................ 216 WITO WA AROBAINI NA NNE....................................................................... 219 Maelezo: Ni Haramu Kukimbia Vita:.................................................................... 219 WITO WA AROBAINI NA TANO.................................................................... 223 Maelezo: Walisema Wamesikia Kumbe Hawakusikia!:........................................ 223 Awamu za Kusikiliza Haki:................................................................................... 225 WITO WA AROBAINI NA SITA....................................................................... 227 Maelezo: WITOKwenye Uhai:.............................................................................. 227 WITO WA AROBAINI NA SABA..................................................................... 232 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 232 Maelezo ................................................................................................................ 233 WITO WA AROBAINI NA NANE.................................................................... 236 Maelezo: Uchamungu na Upambanuzi:................................................................. 236 WITO WA AROBAINI NA TISA....................................................................... 240 Maelezo: ................................................................................................................ 240 WITO WA KHAMSINI...................................................................................... 243 Maelezo ................................................................................................................ 243 Angalizo ................................................................................................................ 245 WITO WA KHAMSINI NA MOJA................................................................... 247 Maelezo ................................................................................................................ 247 Wajibu wa Waislamu kwa Ahlul Kitabi:................................................................ 248 xi
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 11
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
WITOWA KHAMSINI NA MBILI................................................................... 250 Maelezo ................................................................................................................ 250 Abu Dharr na Utetezi wa Wanyonge:.................................................................... 253 Malipo ya Mwenye Kujikusanyia Mali:................................................................ 255 WITO WA KHAMSINI NA TATU.................................................................... 257 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 257 Maelezo ................................................................................................................ 257 Utafiti
................................................................................................................ 258
WITO WA KHAMSINI NA NNE...................................................................... 261 Maelezo ................................................................................................................ 261 WITO WA KHAMSINI NA TANO.................................................................... 265 Maelezo ................................................................................................................ 265 WITO WA KHAMSINI NA SITA...................................................................... 267 WITO WA KHAMSINI NA SABA.................................................................... 270 Maelezo ................................................................................................................ 270 WITO WA KHAMSINI NA NANE................................................................... 273 Maelezo ................................................................................................................ 273 Utafiti: Usalama Na Uhuru Ndani Ya Nyumba:..................................................... 275 WITO WA KHAMSINI NA TISA...................................................................... 277 Maelezo: Utaratibu Maalumu wa Kuingia Kwa Wazazi Wawili:.......................... 277 Hekima Ya Kuomba Ruhusa Ya Kuingia Ndani:................................................... 278 WITO WA SITINI............................................................................................... 280 Maelezo ................................................................................................................ 280 WITO WA SITINI NA MOJA............................................................................ 284 Maelezo ................................................................................................................ 284 Utafiti
................................................................................................................ 288
WITO WA SITINI NA MBILI........................................................................... 290 Maelezo ................................................................................................................ 290 xii
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 12
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
WITOWA SITINI NA TATU.............................................................................. 293 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 294 Maelezo ................................................................................................................ 294 Utafiti
................................................................................................................ 297
WITOWA SITINI NA NNE................................................................................ 302 Maelezo ................................................................................................................ 302 WITOWA SITINI NA TANO............................................................................. 310 Maelezo ................................................................................................................ 310 WITO WA SITINI NA SITA............................................................................... 312 Maelezo ................................................................................................................ 312 WITOWA SITINI NA SABA.............................................................................. 315 Maelezo ................................................................................................................ 315 WITOWA SITINI NA NANE............................................................................. 318 Maelezo ................................................................................................................ 318 Utafiti: Mambo Yanayoporomosha Matendo Mema.............................................. 319 WITOWA SITINI NA TISA............................................................................... 322 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 322 Maelezo ................................................................................................................ 322 Kufuata Mafunzo Ya Uislamu Kikamilifu:............................................................ 323 WITOWA SABINI............................................................................................... 325 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 325 Maelezo ................................................................................................................ 325 Utafiti
................................................................................................................ 329
Kunyanyua Sauti Kwenye Kaburi La Mtume (s.a.w.w.):...................................... 328 WITOWA SABINI NA MOJA........................................................................... 329 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 329 Maelezo ................................................................................................................ 330 Utafiti: Majuto Ni Mjukuu:.................................................................................... 331 xiii
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 13
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
WITOWA SABINI NA MBILI........................................................................... 333 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 333 Maelezo ................................................................................................................ 334 WITOWA SABINI NA TATU............................................................................. 336 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 336 Maelezo ................................................................................................................ 337 Tiba ya Usengenyaji Na Namna Ya Kutubia:........................................................ 340 Maeneo Yanayoruhusiwa Kusengenya:................................................................. 341 WITO WA SABINI NA NNE.............................................................................. 342 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 343 Maelezo ................................................................................................................ 343 Utafiti: Uchamungu Na Upambanuzi:................................................................... 345 WITO WA SABINI NA TANO........................................................................... 347 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 347 Utafiti: Aina Za Kunong'ona:................................................................................. 347 WITO WA SABINI NA SITA............................................................................. 350 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 350 Maelezo: Kuwaheshimu Waliotangulia Katika Kheri:.......................................... 351 Utafiti: Nafasi ya Wanachuoni:.............................................................................. 352 WITO WA SABINI NA SABA............................................................................ 353 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 353 Maelezo:Sadaka Kabla Ya Kunong'ona:................................................................ 354 Utafiti: Mtu Pekee Aliyetoa Sadaka Kabla Ya Kusema Siri na Mtume:................ 355 Hekima Ya Kuwekwa Sadaka na Hatimaye Kufutwa:........................................... 357 WITO WA SABINI NA NANE........................................................................... 358 Maelezo ................................................................................................................ 358 Utafiti: Yanayostahiki Kutendwa:.......................................................................... 360 WITO WA SABINI NA TISA............................................................................. 363 xiv
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 14
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 364 Maelezo: ................................................................................................................ 366 Natija Ya Mahusiano Na Maadui Wa Mwenyezi Mungu:..................................... 366 Utafiti: Vigezo Vyema:........................................................................................... 371 Udugu Katika Uislamu:......................................................................................... 371 WITO WA THEMANINI................................................................................... 374 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 374 Maelezo: ................................................................................................................ 375 Kufidia Gharama Kwa Waislamu Na Makafiri:..................................................... 375 Uadilifu hata kwa Maadui:..................................................................................... 378 WITO WA THEMANINI NA MOJA................................................................ 380 Maelezo ................................................................................................................ 380 WITO WA THEMANINI NA MBILI................................................................ 382 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 382 Maelezo ................................................................................................................ 383 Utafiti: ................................................................................................................ 384 Umuhimu wa Umoja wa Kiislamu:....................................................................... 384 Kauli Bila ya Vitendo:........................................................................................... 385 WITO WA THEMANINI NA TATU................................................................. 386 Maelezo ................................................................................................................ 386 Utafiti: Ushindi wa Karibu:.................................................................................... 388 Dunia ni Mahala pa Biashara Kwa Wachamungu................................................. 389 WITO WA THEMANINI NA NNE................................................................... 391 Maelezo ................................................................................................................ 391 Ni Akina Nani Hao Wanafunzi Wa Nabii Isa (a.s.)?.............................................. 392 WITO WA THEMANINI NA TANO................................................................. 394 Sababu ya Kuteremka............................................................................................ 394 Maelezo: ................................................................................................................ 395 xv
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 15
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
Mkusanyiko Mkubwa wa Kisiasa Kila Wiki:........................................................ 395 Utafiti: ................................................................................................................ 397 Swala ya Mwanzo ya Ijumaa Katika Uislamu:...................................................... 397 Umuhimu wa Swala ya Ijumaa:............................................................................. 388 Hekima ya Swala ya Ijumaa:................................................................................. 399 Adabu ya Swala ya Ijumaa na Khutba Mbili:........................................................ 401 Masharti ya Swala ya Ijumaa:................................................................................ 402 WITO WA THEMANINI NA SITA................................................................... 403 Maelezo ................................................................................................................ 403 Unafiki wa Kiitikadi na wa Kivitendo:.................................................................. 405 WITO WA THEMANINI NA SABA................................................................. 407 Maelezo ................................................................................................................ 407 WITO WA THEMANINI NA NANE................................................................. 411 Maelezo ................................................................................................................ 411 Utafiti: ................................................................................................................ 412 Malezi kwa Familia:.............................................................................................. 412 WITO WA THEMANINI NA TISA................................................................... 415 Maelezo ................................................................................................................ 415 Utafiti: ................................................................................................................ 417 Toba ni Mlango wa Rehema za Mwenyezi Mungu:.............................................. 417 HITIMISHO........................................................................................................ 418
xvi
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 16
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
بسم اهلل الرحمن الرحيم NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu ulichonacho mikononi mwako ni kitabu ambacho kimeandikwa kutokana na aya za Qur’ani Tukufu zinazowaita waumini katika mambo ya kheri. Kimekusanywa na kuandikwa na Sheikh Muhammad A. Bahsan kwa jina la, Wito kwa Waumini. Wito kwa Waumini ni kitabu kilichokusanya baadhi ya aya za Qur’ani Tukufu zenye kuwaita waumini katika mambo ya kheri au katika kutekeleza amri za Allah ‘Azza wa Jalla. Kwa kawaida aya hizi huanzia na maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu yanayosema: “Yaa ayyuha ‘l-ladhiin aamanuu!” (Enyi mlioamini!). Mwandishi wa kitabu hiki ametumia kalamu yake kuelezea maana ya aya hizi na jinsi ya kutekeleza wito huu wa Allah. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo watu wameghafilika kwa ghururi za ulimwengu huu. Hivyo, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha yake ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Sheikh Muhammad A. Bahsan kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kuandika kitabu hiki kwa lugha yake ya asili ya Kiswahili, pia na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin kisha amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation
1
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 1
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
بسم اهلل الرحمن الرحيم UTANGULIZI Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
K
ila sifa njema inamstahikia Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, na Swala na Salamu zimwendee Mtume wetu Mtukufu (s.a.w.w.), ambaye aliletwa kuwa ni rehema kwa walimwengu wote, na pia ziwaendee watu wa nyumbani kwake waliotakaswa na kila aina ya uchafu, na Maswahaba wake walio wema. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametumia wito katika Kitabu Chake Kitukufu kuwaita watu wenye sifa mbali mbali, na miongoni mwa watu aliowaita ni Waumini, wito huu unapatikana katika Aya zilizoteremshwa Madina tu, na hakuna hata moja iliyoteremshwa Makka iliyo na wito wa aina hii, huenda sababu ya Waislamu kuanza kuitwa na Mwenyezi Mungu kwa jina la Waumini ni kule kuunda jamii na dola ya Kiislamu katika mji wa Madina baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuhamia huko pamoja na Maswahaba wake. Wito wa “Enyi mlioamini!” ni dalili ya ahadi ya kusalimu amri, ahadi iliyochukuliwa na kundi la Waislamu kwa Mola wao baada ya kumuamini Yeye, ahadi hii inawalazimisha kukubali na kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu zinazofuatia mara tu baada ya wito huu. Mambo ya msingi yanayopatikana katika Aya za aina hii ni maamrisho, makatazo au maelezo mbali mbali yenye lengo la kuwataka Waumini kujifunza kutokana na matendo ya watu wengine. Kwa hiyo kitabu hiki kilichoko mikononi mwako ewe ndugu Muumini ni baadhi ya maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu Muumba mbingu na ardhi yaliyoelekezwa kwako, imani yako itabakia thabiti na kustahiki kuitwa Muumini ikiwa tu utashikamana vilivyo na amri za Mwenyezi Mungu na kuachana na yale yote yaliyokatazwa na Aya hizi, Aya ambazo tumejaribu kuzikusanya pamoja katika kitabu hiki ili kukurahisishia kujua wajibu wako mbele ya Mola Wako Mlezi. Kwa kiwango kikubwa tumetumia kitabu cha Ayatullahil-Udhma; Samahatu Sheikh Makarimu Shiraziy, kiitwacho ‘Tafsirul Amthal’ katika mukhtasari huu, kwani tafsiri yake hiyo imekusanya mafunzo na hazina kubwa ya kielimu. Lakini kutokana na kuchunga mazingira yetu ya Kitanzania na Kiafrika Mashariki kwa ujumla tumejaribu kuongeza maelezo pale palipohitajika na kuyaacha baadhi. Kwa 2
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 2
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
hivyo yule anayehitaji mafunzo yanayopatikana katika Aya hizi kwa upana zaidi, anaweza kurejea huko na kwengineko. Ewe Mola! Tuoneshe haki kuwa ni haki na utuwezeshe kuifuata, na tuoneshe batili kuwa ni batili na utuwezeshe kuiacha. Muhammad A. Bahsan
3
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 3
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
بسم اهلل الرحمن الرحيم WITO WA KWANZA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اس َمعُوا ْ اع َنا َو ُقولُوا ا ْن ُظ ْر َنا َو ِ ين آ َمنُوا اَل َت ُقولُوا َر ْ َ َ اب أَلِي ٌم َما َي َو ُّد الَّ ِذ َ َولِْل َكا ِف ِر ٌ ين َع َذ اب ِ ين َك َف ُروا ِم ْن أ ْه ِل ال ِك َت ُ ْك ْم ِم ْن َخيْر ِم ْن َرب ُ ين أَ ْن يُ َن َّز َل َعلَي َ َو اَل ْال ُم ْش ِر ِك ص ُّ ِّك ْم َواللهَُّ َي ْخ َت ٍ ْ ضل ْ ِب َر ْح َم ِت ِه َم ْن َي َشا ُء َواللهَُّ ُذو ْال َف يم ظ ع ال َ ِ ِ ِ “Enyi mlioamini! Msiseme Raa’ina bali semeni Undhurnaa na sikilizeni; na makafiri wana adhabu iumizayo. Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu, wala washirikina, mteremshiwe kheri kutoka kwa Mola wenu. Na Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema Zake amtakaye; na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.” (Qur’ani 2:104-105).
SABABU YA KUTEREMKA:
I
mepokewa kutoka kwa ibn Abbas ya kwamba: “Wakati Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akiwasomea Maswahaba Aya za Qur’ani na kuwabainishia hukumu zake, walimtaka Mtume (s.a.w.w.) asifanye haraka ili waweze kuelewa vizuri na kupata muda wa kuweza kumuuliza masuala, Maswahaba walikuwa wakitumia neno:’Raa’inaa’ likiwa na maana, ‘Tupe muda kidogo’ Lakini Mayahudi walilitumia neno hili kwa mujibu wa lugha yao, ambalo lina maana ya kumwambia mtu: ‘Sikia, mbona husikii.’ Kwa hivyo wakaitumia nafasi hiyo kumkejeli na kumbeza Mtume (s.a.w.w.) na wakasema: “Tulikuwa tukimtukana Muhammad kwa siri, lakini sasa tunamtukana kwa uwazi.” Mayahudi hao walikuwa wakilisema neno hili mara kwa mara mbele ya Mtume (s.a.w.w.) na huku wakicheka. Mmoja kati ya Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa akijulikana kwa jina la Sa’d ibn Muadh alilisikia neno hilo, naye alikuwa akiielewa vyema lugha ya Mayahudi, aliwaambia: “Mwenyezi Mungu awalaani, nikimsikia yeyote kati yenu akimwambia Mtume (s.a.w.w.) neno hili nitamkata shingo yake.” Mayahudi wakasema: Je, nyinyi si mnalisema neno hili? Hapo Mwenyezi Mungu akaiteremsha Aya hii kwa lengo la kuwakataza wasiwaigize Mayahudi 4
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 4
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
katika kulitamka neno hili, kwani wao wanakusudia maana nyingine, na wamepata sababu ya kumtukana na kumfanyia kejeli Mtume (s.a.w.w.)1
MAELEZO: Aya inawahutubia Waumini kwa kuwakataza wasiseme: “Raa’inaa” na badala yake waseme: “Undhurnaa.” Kutokana na sababu ya kuteremka kwake tunajifunza ya kwamba, ni wajibu juu ya kila Muumini kutowapa maadui wa Uislamu fursa ya kuweza kuwafanyia kejeli na dharau ya aina yoyote, hata kama ni kwa maneno. Aya inabainisha wazi namna ya kujiepusha na maneno yanayoweza kuwafanya maadui kuyatumia maneno hayo hayo kwa lengo la kudhoofisha morali na hamasa ya Waumini wa kweli katika kuipenda na kuitetea Dini yao, na badala yake wanatakiwa watumie maneno ambayo si rahisi mtu kuweza kubadilisha maana yake ya asili. Ikiwa Uislamu unatilia mkazo juu ya kujiepusha na jambo hili jepesi na dogo, ni wazi kwamba wajibu wa Mwislamu ni mkubwa zaidi katika mambo makubwa na mazito, basi inawapasa kuchukua tahadhari zaidi katika masuala ya kilimwengu ili wasije wakawafungulia maadui milango ya kuushambulia Uislamu pamoja na Waislamu kwa ndimi zao na mikono yao. Waislamu kukatazwa kusema neno hilo, ambalo halikuwa na maana mbaya kwa mujibu wa lugha ya Kiarabu, lakini kwa lugha ya Mayahudi lilikuwa na maana isiyopendeza, kwa hivyo Mayahudi walijipatia fursa ya kumkejeli Mtume (s.a.w.w.) Mwenyezi Mungu aliamua kuchukua hatua za makusudi ili kumlinda Mtume Wake dhidi ya maneno yenye kumuudhi na kumkera. Ikiwa neno hili lina maana ya matusi kwa mujibu wa lugha ya Kiyahudi, kama walivyosema baadhi ya wafasiri, basi Mwenyezi Mungu amewakataza Waislamu wasiwatukane hata wale wenye kuabudu miungu wengine wasiokuwa Mwenyezi Mungu, seuze vipi hawa wamtukane na kumkashifu Mtume Wake! Aya hii inatoa somo kubwa kwa Waislamu, wanatakiwa wafahamu vyema vitimbi na mbinu mbalimbali zinazoelekezwa kwao, kwa hivyo ni juu ya kila Mwislamu asihadaike nao, kwani hao ni watu wenye kuwachukia mno Waislamu, na haya tunayashuhudia wenyewe hadi hivi leo, namna wanavyoendesha ugaidi wa hali ya juu dhidi ya Waislamu, kwa kuikalia ardhi yao kwa mabavu na kufanya mauwaji ya kutisha kwa watu wasio na hati yoyote, kubwa ni kudai haki zao za kimsingi na kutaka kuishi kama wanadamu wengine wanavyoishi. Kwa hivyo kama vile ambavyo Uislamu unatukataza kufuata tabia na mienendo ya Mayahudi, basi pia tunakatazwa 1
Al-Wahid An-Nisaburiy,Asbabu Nnuzul, Uk. 20 5
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 5
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
hata kusema maneno yenye kubeba ujumbe mbaya yanayoanzishwa na wao, maneno yenye lengo la kupotosha itikadi sahihi za Kiislamu. Leo kuna maneno yenye sura nzuri na yanayokubalika katika Uislamu, lakini Mayahudi pamoja na washirika wao wamepotosha maana halisi ya maneno hayo, kwa mfano neno ‘Uhuru’ neno hili ni zuri mno, kiasi kwamba kila mwanadamu ana haki ya kuwa huru, kwani kinyume cha uhuru ni utumwa, Uislamu ulipokuja ulikuta biashara ya utumwa ikiwa imeshamiri miongoni mwa Waarabu, ilichofanya ni kuchukua hatua mbalimbali za kuondosha jambo hilo. Imamu Ali (a.s.) naye anatuambia:
.حرا ّ وقد جعلك اهلل,وال تكن عبد غيرك “Usiwe mtumwa wa mwingine, wakati Mwenyezi Mungu amekuumba hali ya kuwa ni huru.”2
Mayahudi na washirika wake wanalitumia neno ‘Uhuru’ kwa malengo mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa upande wa kisiasa ni baada ya kuona kwamba baadhi ya viongozi ulimwenguni hawaendeshi siasa zao kwa mujibu wa matakwa yao, kwa hivyo wakanyanyua mabango ya kudai kuwepo uhuru wa kisiasa, kwa kuwepo uhuru wa kila mtu kushiriki katika uchaguzi, kuchagua au kuchaguliwa, hapo nchi nyingi zikaingia katika mfumo wa vyama vingi. Lakini pale viliposhinda uchaguzi vile vyama ambavyo vilikuwa na milengo ilio kinyume na wao hawakuwa tayari kuutetea uhuru huo, bali wao ndio wa kwanza kutoa amri ya kubatilisha matokeo na badala yake jeshi kuchukua mamlaka kwa nguvu, haya tumeyashudia kwa macho na masikioyetu katika nchi ya Aljeria, baada ya chama cha Kiislamu (F. I. S.) kushinda uchaguzi wa nchi hiyo mnamo mwaka 1992. Ama kwa upande wa kiuchumi, hasa baada ya Mayahudi kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na badhi ya nchi za Kiarabu, nchi ambazo ni soko kubwa la kuuzia bidhaa za nchi za Magharibi zenye thamani ya hali ya juu, Mayahudi pamoja na washirika wake wamekuja na sera ya soko huria, soko ambalo baadhi ya nchi za Kiarabu wamejiunga nalo, na miongoni mwa masharti yake ni kwa mwanachama kuuza bidhaa zake katika nchi nyingine mwanachama bila ya vikwazo vyovyote vile, kwa hivyo hii imekuwa sababu kubwa ya Mayahudi kuzidi kuimarisha utawala wao wa kimabavu, kwani uchumi wao unapanda siku hadi siku kutokana na kupanuka soko la bidhaaa zao ndani ya baadhi ya nchi za Kiislamu! 2
Imamu Ali (a.s.) Nahjul-Balaghah Jz. 3, Uk. 37 6
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 6
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
Ama neno ‘Uhuru’ kwa upande wa kijamii, sote ni mashuhuda, Waislamu na wasiokuwa Waislamu, tunaona ni kiasi gani jamii yetu inavyoporomoka siku hadi siku kwa kukosa maadili mema, tunaona ni namna gani akina dada wanavyokashifiwa kwa kuvishwa nguo zenye kuwadhalilisha, eti ni kutaka kumpata aliye mrembo zaidi! Hupelekwa huku na kule wakiwa wamevaa mavazi ya ndani tu, ukisema, utaambiwa: “Wako huru kufanya hivyo.” Na baya zaidi ni kwa wale wanaotakiwa kulinda maadili yetu ndio wanaotoa ruhusa ya kufanyika hayo, na zaidi ya hayo, wao ndio wanaokuwa wageni rasmi! Mambo hayo yameathiri hata katika mitaa na hata barabarani, kila kona utawakuta watu waliojisitiri nusu mwili, ustaarabu umekosekana na badala yake uhuru wa bandia umetawala kwa kuwakashifu akina dada hao! Kuna haja kubwa ndugu Mwislamu, kutafakari vyema yale yote yanayotoka kwa wageni, kwani wengi wao si wenye kututakia mema, hao ndio waliotutawala miaka mingi, wakatudhalilisha na kupora rasilimali zetu nyingi kwa lengo la kuimarisha nchi zao. Aya inayofuatia Mwenyezi Mungu amewakusanya wote Mayahudi na washirikina katika sifa moja, nayo ni sifa ya ukafiri, anasema:
ْ ين َك َف ُروا ِم ْن أَ ْهل ََّما َي َو ُّد ال َ َ اب َو اَل ْال ُم ْش ِر ِك َ ين أَ ْن يُ َن َّز َل ت ك ال ذ ِ ِ ِ ِ َُّص ب َر ْح َم ِت ِه َم ْن َي َشا ُء َوالله َُُّ لله َُ ِ ُّ ْر ِم ْن َربِّك ْم َوا َي ْخ َت ٍ َعليْك ْم ِم ْن َخي ْ ضل ْ ُذو ْال َف يم ظ ع ال َ ِ ِ ِ “Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu, wala washirikina, mteremshiwe kheri kutoka kwa Mola wenu. Na Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema Zake amtakaye; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.” (Qur’ani 2: 105).
Kwa vile watu waliopewa Kitabu pamoja na washirikina wamemkataa Mtume (s.a.w.w.), wote wana nafasi sawa, wote wana chuki kubwa dhidi ya Waumini na hawapendi kuona kheri yoyote ikiwashukia Waumini, na kubwa ni kule kuona Ujumbe wa Dini hii ya Uislamu umeshushwa kwa Mtume (s.a.w.w.), kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema Zake amtakaye;” (Qur’ani 2: 105). Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba viumbe, na yeye Ndiye Mtambuzi zaidi wa kujua ni nani ampe dhamana na jukumu la kuufikisha Ujumbe Wake kwa wengine, kwa hivyo alimtuma Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kutekeleza jukumu hilo, na hili 7
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 7
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
ndilo kubwa lililowafanya wamchukie Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Waislamu kwa ujumla. Ibara ya mwisho ya Aya hii inasema: “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.” (Qur’ani 2: 105). Hakuna fadhila kubwa zaidi ya fadhila ya Unabii na Utume, hakuna fadhila kubwa zaidi ya imani juu ya Mtume (s.a.w.w.) na kulingania imani hiyo. Kwa vile wale Waumini wa Dini hii huhisi fakhari katika nafsi zao kwa kuwa wafuasi wa Mtume (s.a.w.w.), lakini maadui huchukizwa mno na jambo hilo. Kwa hivyo ni juu ya kila Muumini kuchukua tahadhari dhidi ya makafiri na kujua namna ya kuishi nao, kwani wao ni watu wenye choyo na husda kwa Waumini, wanasononeka na kuungulika ndani ya nafsi zao pale wanapowaona Waislamu wakineemeka kwa neema mbali mbali kutoka kwa Mola wao Mlezi.
8
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 8
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA PILI
ََّيا أَُّي َها ال ُ ُ َ َ الص اَل ِة إِ َّن اللهََّ َم َع ب الص ب وا ن ي ع ت اس وا ن م آ ين ذ َّ ْر َو َّ ْ َ ِ ِ ِ ِ َ ْات َبل ُ ُ َّلله ٌ يل ا ِ أ ْم َو َ الص ِاب ِر َّ ِ ين َو اَل َت ُقولوا لِ َم ْن ي ُْق َتل ِفي َس ِب َ ُر ف ُ أَ ْح َيا ٌء َو َٰل ِك ْن اَل َت ْشع ِ ون { َولََنبْلُ َونَّ ُك ْم ِب َش ْي ٍء ِم َن ْال َخ ْو َ ْال ْم َوال َو أ َ َْو ْال ُجوع َو َن ْقص ِم َن أ ُ ال ْن ات َو َب ِّش ِر ف ِ س َوالثَّ َم َر ِ ٍ ِ ِ َ ُ َّ ٌ َّللِه َ َ َ ْ َّ َّ َ ين الٰ ِذ َ الص ِاب ِر صي َبة قالوا إِنا ِ َوإِنا إِل ْي ِه َّ َ ين إِذا أ ِ صا َبت ُه ْم ُم َ ُ َ َراجع َ ٌ صلَ َو ِّه ْم َو َر ْح َم ٌة َو ُأو َٰل ِئ َك َ ْه ْم ِ ِ ات ِم ْن َرب ِ ُون أول ِئ َك َعلي َ ُه ُم ْال ُم ْه َت ُد ون “Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na Swala; hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri. Wala msiseme kwamba wale wanaouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wa hai lakini nyinyi hamtambui. Na hakika tutawajaribu kwa chembe ya hofu na njaa na upungufu wa mali na wa nafsi na wa matunda. Na wape bishara wanaosubiri. Ambao ukiwapata msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na Kwake tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola Wao, na rehema, na hao ndio wenye kuongoka. (Qur’ani 2: 153-157).
SABABU YA KUTEREMKA: Ibn Abbas anaelezea sababu ya kuteremka Aya 153, kwa kusema: “Aya hii imeteremka kuhusiana na Waumini waliouwawa katika vita vya Badr, idadi yao ilikuwa kumi na nne: Muhajirina walikuwa sita, na Maanswari walikuwa nane, baada ya kumalizika vita baadhi ya Waislamu waliwaita mashahidi ‘Maiti’ Aya ilikuja kwa lengo la kuwakataza kuwaita hivyo.”3
MAELEZO: Aya mbali mbali katika Qur’ani Tukufu zinaelezea mambo mbali mbali yanayopaswa kutekelezwa na kila Mwislamu, baadhi ya wakati mambo hayo yanakuwa na uzi3
Al-Wahid An-Nisaburiy, Asbaabun-Nuzul, Uk. 12 9
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 9
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
to katika utekelezaji wake, kitu pekee kinachoweza kukabiliana na uzito unaoweza kujitokeza ni ‘Subira na Swala.’ Aya inaanza kwa kusema: “Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na Swala; hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri.” Baadhi ya watu wanadhani ya kwamba maana ya Subira ni kuvumilia mashaka na matatizo, kwa kukubali udhalili na kusalimu amri mbele ya mtu dhalimu, bali subira ni kuendeleza mapambano na kuwa thabiti na imara mbele ya matatizo yanayomkabili mwanadamu. Kutokana na maana hii ya Subira, Wanachuoni wa Akhlaq, wameigawa Subira katika makundi matatu: Kwanza: Kusubiri katika utiifu, ikiwa na maana ya kukabiliana na vikwazo vilivyopo katika kutekeleza wajibu. Pili: Kusubiri dhidi ya Maasi, ina maana kupambana na nafsi mbele ya matamanio na makatazo mbali mbali. Tatu: Kusubiri katika msiba, maana yake ni kuvumilia na kuwa mkakamavu na bila ya kutetereka katika imani, kutokana na matukio mbali mbali yanayomkabili mwanadamu katika maisha yake. Suala la Subira ni suala lililopewa umuhimu zaidi katika Qur’ani, kwani limezungumziwa karibu mara sabini, mara kumi kati ya hizo zinamuhusu Mtume (s.a.w.w.). Historia ya watu wakubwa na watukufu inajieleza ya kwamba, moja kati ya nguzo muhimu za mafanikio yao inatokana na subira yao pamoja na misimamo yao madhubuti. Na watu waliokosa subira walifeli na kuporomoka kwa haraka sana katika harakati zao. Tunaweza kusema ya kwamba nafasi ya subira katika kumuendeleza mwanadamu au jamii katika harakati za kimaendeleo ni kubwa kuliko nguvu, uwezo na hata akili. Qur’ani Tukufu inabainisha uzito wa subira katika maisha ya mwanadamu kwa kusema:
َ َ الصاب ُر َّ .اب ٍ ْر ِح َس ِ َّ إِنَّ َما يُ َوفى... ِ ون أ ْج َر ُهم ِب َغي “Hakika wenye subira watalipwa malipo yao bila ya hesabu.” (Qur’ani 39:10).
Na sehemu nyingine, baada ya Mwenyezi Mungu kuielezea subira katika mambo mbali mbali alisema:
ُْإ َّن َذل َك م ْن َع ْزم أ... .المُور ِ ِ ِ ِ
“…hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.” (Qur’ani 31:17). 10
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 10
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
Miongoni mwa umuhimu wa subira ni kwamba, jambo lolote linakuwa halina thamani ikiwa litakosa subira, kwani subira ndio nguzo madhubuti na iliyo muhimu zaidi katika kila jambo la kheri, kama anavyosema Imam Ali a.s:
ّ بالصبر ,كالرأس من الجسد ّ الصبر من اإليمان ّ فإن ّ وعليكم . وال في إيمان الصبر معه,وال خير في جسد ال رأس معه “Ni juu yenu kuwa na subira, kwani subira katika imani ni kama kichwa katika mwili, na hakuna ubora wowote katika mwili usio na kichwa, na wala hakuna ubora wowote katika imani isiyokuwa na subira.”4
Riwaya mbali mbali zinaeleza ya kwamba daraja kubwa ya subira ni kuidhibiti nafsi wakati kunapopatikana sababu mbalimbali zinazompelekea mtu kuweza kumuasi Mwenyezi Mungu. Aya hii inaelezea namna kundi la wanaharakati wa Kiislamu wa mwanzoni mwa Uislamu walivyozungukwa na maadui katika kila upande, Mwenyezi Mungu aliiteremsha Aya hii ili kuwataka wajisaidie katika mapambano yao dhidi ya maadui wao kwa kusubiri na kuswali, lengo la amri hii ni kuifanya nafsi kuwa huru na kumtegemea Mwenyezi Mungu peke yake. Na historia ya Kiislamu inatuonesha ya kwamba jambo hili ndilo lililokuwa chanzo cha kila ushindi walioupata. Jambo jingine la msingi lililotajwa baada ya subira katika Aya hii ni ‘Swala’, imepokewa ya kwamba Imamu Ali (a.s.) pale alipokuwa akipatwa na jambo lililokuwa likimfadhaisha katika nafsi yake alikuwa akiswali, na kisha kuisoma Aya hii: “Takeni msaada kwa subira na Swala.” Ni jukumu la Mwislamu aliyemuamini vyema Mwenyezi Mungu pindi anapoiona nafsi yake iko katika matatizo makubwa na kuhisi udhaifu katika kukabiliana nalo, kutafuta mwega usio tetereka na wenye nguvu zisizo na kifani, miongoni mwa mambo yanayomhakikishia usalama na utulivu wa nafsi yake katika kuzikabili changamoto mbali mbali ni ‘Swala’. Aya hii inataja mambo mawili muhimu ya mtu kuweza kujikwamua kutoka katika misukosuko mbalimbali: Jambo la kwanza ni kumtegemea Mwenyezi Mungu, na dhahiri yake ni ‘Swala,’ na jambo la pili ni kuitegemea nafsi, kama lilivyoelezewa kwa jina la ‘Subira.’ Baada ya kumaliza kutaja Subira na msimamo unaotakiwa kufuatwa na kila Mwislamu, Aya inayofuata inaelezea kubakia hai kwa mashahidi, kwani watu hao ni 4
Imamu Ali (a.s.) Nahjul-Balaghah Jz. 4, Uk. 18 11
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 11
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
mfano bora wa watu walioshikamana na Subira katika kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu: Wala msiseme kwamba wale wanaouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wa hai lakini nyinyi hamtambui.” Ni kawaida kwamba wakati wa harakati zozote hujitokeza baadhi ya watu kujitenga na harakati hizo na badala yake kuwaona wale waliojitolea katika kupigania haki za wengine kuwa ni wachochezi na wavunjaji wa amani, na pale inapobidi kuingia katika mapambano na baadhi yao kufa mashahidi, watu hao huonesha masikitiko juu ya watu hao na kusema ya kwamba wamejitakia wenyewe kufa, watu wa aina hiyo hujisahau ya kwamba jambo lolote takatifu haliwezi kusimama bila ya watu wengine kujitoa muhanga, Mwenyezi Mungu anawarudi na kuwakataza watu hao kuacha kueneza uzushi wao huo, na amebainisha wazi kwamba wale waliojitolea katika kuitetea na kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu na kuuwawa kwamba wao si maiti, watu hao wako hai na wanafurahia neema mbalimbali wanazoruzukiwa na Mola Wao, lakini wale walioko duniani hawahisi uhai wa watu hao. Kubakia Hai kwa Mashahidi: Wanachuoni wa tafsiri ya Qur’ani wana rai mbalimbali kuhusiana na mashahidi kubakia hai, wako wanaosema ya kwamba hayo maisha wanayoishi ni maisha maalumu kwa ajili ya mashahidi, kiasi ambacho hakuna mtu anayeweza kuyaelezea undani wake. Na wengine wanasema ya kwamba uhai uliotajwa katika Aya hii unamaanisha uongofu, na mauti yana maana ya upotevu, kwa hivyo Aya itakuwa imekataza kuwasifu mashahidi kwa sifa ya upotevu, bali wao ni wenye kuongoka. Na wengine wanaona ya kwamba, uhai wa mashahidi ni kule kuwa hai ule ujumbe walioupigania. Maana hizi zilizoelezewa na baadhi ya wanachuoni wa tafsiri hazikubaliki, kwani dhahiri ya Aya inaonesha wazi ya kwamba roho za mashahidi zinaendelea kuwa hai huku zikifurahia na kupata starehe za kila aina kutoka kwa Mola Wao hata baada ya miili yao kumalizika na kuliwa na mchanga, starehe hizo wanazipata katika maisha ya barzakh (kaburi) na wataendelea nazo baada ya kufufuliwa na kuingizwa Peponi. Kuwepo maisha ya barzakh na neema yake au adhabu yake ni jambo lililothibiti katika Qur’ani Tukufu kama Mwenyezi Mungu anavyotuambia:
. َو ِمن َو َرا ِئ ِهم َب ْر َز ٌخ إِلَى َي ْو ِم يُ ْب َعثُون...
“…na mbele yao kuna barzakh (maisha baada ya kufa) mpaka siku watapofufuliwa.”(Qur’ani 23:100).
12
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 12
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
Na dalili nyingine inayothibitisha kuwepo kwa maisha katika kaburi ni Aya inayoelezea uhai wa mashahidi, anasema Mwenyezi Mungu:
ْ ُ ُ َ ال َت ْح َس َب َّن الَّ ِذ َ َو يل اللِهّ أَ ْم َواتاً َب ْل أَ ْح َياء ِعن َد ِ ين ق ِتلوا ِفي َس ِب َ ُر َز ُق ون ْ ِّه ْم ي ِ َرب “Na usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa, bali wako hai mbele ya Mola Wao wanaruzukiwa.” (Qur’ani 3: 169).
Ama kwa upande wa riwaya, anasema Mtume (s.a.w.w.): “Hakika kaburi ni bustani miongoni mwa mabustani ya Pepo au ni shimo miongoni mwa mashimo ya Moto.” Kuwepo kwa dalili hizi na nyinginezo zinazothibitisha kuwepo kwa maisha ya kiroho katika kaburi mara baada ya mtu kufariki dunia, Waumini wanakatazwa kusema au kudhania kwamba wale walioutoa uhai wao kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu kuwa ni watu waliokatikiwa na uhai. Aya hizi ni changamoto kwa kila Mwislamu kuishi katika misingi ya Dini yake, kwa kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kuachana na kila katazo ili ayaanze maisha yake ya akhera kwa salama na amani mara tu atakapowekwa katika kaburi lake, kwani tunapoiangalia kwa makini na kwa mazingatio Aya ya 154 ya Suratul Baqara pia inatupasha habari ya kwamba tabia ya mwanadamu ni kupenda maisha bora na yenye furaha, basi maisha hayo yanapatikana kwa kila yule ambaye ataamua kujiunga katika safu ya mashahidi kwa kuitetea Dini ya Mwenyezi Mungu kwa njia moja au nyingine. Duniani ni mahala pa mtihani: Baada ya Mwenyezi Mungu kuzungumzia masuala ya Subira, Swala na kubakia hai kwa mashahidi, mambo yote haya ni mtihani kwa mwanadamu, katika Aya zifuatazo anazungumzia kuhusu mtihani wake kwa wanadamu wote, Aya inasema: “Na hakika tutawajaribu kwa chembe ya hofu na njaa na upungufu wa mali na wa nafsi na wa matunda. Na wape bishara wanaosubiri.” Suala la kupata mitihani mbalimbali hapa duniani ni jambo la kawaida na la kimaumbile, jambo ambalo hakuna yeyote atakayeepukana nalo. Na kwa vile mshindi hujulikana baada ya kutahiniwa, basi mshindi wa mtihani huu ni yule tu mwenye kujua namna ya kukabiliana na mitihani hiyo na kuwa na msimamo thabiti katika haki na kujipamba kwa pambo la uvumilivu na subira. Ni wale tu wenye subira ndio watakao kuwa washindi wa mitihani hii na si wengineo. 13
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 13
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
Aya inayofuata inatueleza ni akina nani hao wenye kusubiri, inasema: “Ambao ukiwapata msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na Kwake tutarejea.” Kukiri Uungu wa Mwenyezi Mungu asiye na mshirika, inatufunza ya kwamba, tusihuzunike kwa yale yanayotusibu au tunayoyakosa, kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mmiliki wa nafsi zetu na pia ni Mmiliki wa kila kitu tunachokimiliki, akitaka hutupa, na pale anapoona kuna maslahi makubwa zaidi huvichukua vitu hivyo kutoka kwetu, na pia katika majanga na masaibu mbalimbali kuna faida na maslahi kwetu. Kule kujikumbusha mara kwa mara ya kwamba mwisho wa siku ni kurudi kwake Mwenyezi Mungu, kunatufundisha ya kwamba maisha haya ya dunia yana mwisho, na vyote anavyoturuzuku navyo vina mwisho wake, na kitu pekee cha kumfanya mwanadamu kufikia katika kilele cha ubora na ukamilifu ni kujikumbusha mara kwa mara upwekesho wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu,na kujikumbusha ya kwamba mwisho wa siku ni kurudi kwake Mwenyezi Mungu kwa ajili ya malipo, ukumbusho huu uko katika ibara ya Qur’ani isemayo: “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” Ibara hii inajenga roho ya kujiamini, ujasiri, ukakamavu na subira katika nafsi ya mwanadamu. Makusudio sio tu kuitamka ibara hii kwa ulimi, bali kinachotakiwa ni kujenga hisia ya hali ya juu ya ukweli huu, na kuzingatia ule ujumbe uliomo ndani yake, ujumbe ambao ni upwekesho wa Mwenyezi Mungu na kujiandaa kwa ajili ya Siku ya Mwisho. Aya ya mwisho inaelezea takrima kubwa ya Mwenyezi Mungu atakayo wakirimu hao washindi wa mitihani, inasema: “Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola Wao, na rehema, na hao ndio wenye kuongoka.” Hawa watu wenye uoni na ufahamu na kujua namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali na kujua ya kwamba hayo yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, na mwisho wake kila mtu atarudi kwa Mola wake, kwa hakika hao ndio wenye mafanikio makubwa duniani na akhera: “Na hao ndio wenye kuongoka.” Kwa nini Mwenyezi Mungu Awatahini Watu? Inawezekana akili ya mwanadamu ikahoji juu ya sababu ya Mwenyezi Mungu kuwatahini waja Wake, kwani sisi tunapowafanyia watu wengine mitihani, tunalengo la kutaka kujua yale yaliyofichika kwetu, na tunatambua fika kwamba Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yale yaliyodhahiri na yaliyojificha. Jawabu la suala hili ni kwamba, ile dhana ya mtihani kwa wanadamu inatofautiana kabisa na dhana ya mtihani kwa Mwenyezi Mungu, mtihani wa mwanadamu ni kama tulivyoona, ama mtihani wa Mwenyezi Mungu kwa waja Wake ni kuwazindua na kuwafunza. Mtihani wa Mwe14
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 14
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
nyezi Mungu kwa waja Wake ni kama mfano wa mkulima mahiri, ambaye hukabiliana na changamoto mbalimbali, mkulima huyo anachofanya si kuachana na kilimo, bali kuendelea na kazi hiyo kwa kutafuta mbegu bora zinazovumilia hali ya hewa ya aina yoyote ile itakayo jitokeza, na kupalilia kwa wakati, na kutafuta viatilifu dhidi ya wadudu waharibifu, hatua zote hizi anazokabiliana nazo mwisho wake ni kuvuna mavuno mazuri yenye faida. Na mfano mwingine wa mtihani wa Mwenyezi Mungu, ni kama wanajeshi wanapopelekwa manuva (mazoezi ya kijeshi), huko hufanya mazoezi kama kwamba wako vitani, hukabiliwa na njaa, kiu, baridi, joto na mazingira magumu kwa ujumla, haya yote yana lengo la kuwafanya wakakamavu wakati wa vita vitakapotokea. Kwa kweli hii ndio siri kubwa ya mitihani ya Mwenyezi Mungu katika kuwatahini waja wake. Mtihani unalenga kumfanya mwanadamu ajipange upya ikiwa atagundua kasoro zozote zitakazojitokeza, Mwenyezi Mungu anasema:
َُّص َما ِفي ُقلُوب ُك ْم َوالله ََُّولَِي ْب َتلِ َي الله ُ ص ُدور ُ ح م ي ل و م ك ي ف ا م ِّ ُ ْ َ َ َ َ ِ ِ ِ ِ ور ُّ ات ِ َعلِي ٌم ِب َذ ِ الص ُد
“Na ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu na ayasafishe yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo vifuani.” (Qur’ani 3:154).
Na Imamu Ali (a.s.) anasema kuhusiana na sababu ya kuwepo mtihani wa Mwenyezi Mungu:
ولكن لتظهر األفعال,إن كان سبحانه أعلم بهم من أنفسهم... ّ .يستحق الثّواب والعقاب الّتي بها “… licha ya kwamba Mwenyezi Mungu anawajua zaidi kuliko wanavyojijua wenyewe, lakini anataka vidhihirike vitendo ambavyo vinastahiki thawabu na vile vinavyostahiki adhabu.”5
Pia Mwenyezi Mungu anapowatahini waja wake, hukusudia kuwatambulisha wale waovu waliojificha katika kundi la Waumini, ili Waumini wa kweli wawajue hao dhahiri shahiri kama anavyosema: “ 5
Imamu Ali (a.s.) Nahjul-Balaghah Jz.4, Uk.20 15
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 15
12/8/2014 2:43:34 PM
WITO KWA WAUMINI
َ ين َعلَى َما أَنتُ ْم َعلَ ْي ِه َحتَّ َى َي ِم َ ان اللُهّ لَِي َذ َر ْال ُم ْؤ ِم ِن َ َّما َك يز َّ َ ْال َخ ِب ِّب ِ يث ِم َن الطي “Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kutaka kuwaacha waumini juu ya hali mliyo nayo mpaka awapambanue wabaya na wazuri.” (Qur’ani 3:179).
Mtihani wa Mwenyezi Mungu ni kwa Waja Wake Wote: Mfumo wa maisha ya mwanadamu hapa duniani, ni mfumo wa kusongambele katika kujiboresha katika imani yake na utekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu, mfumo huu wa kupiga hatua iliyobora zaidi pia uko kwa viumbe vyote vyenye uhai, ikiwemo miti, kwani thamani ya mti huonekana zaidi pale unapoanza kutoa matunda. Kwa hivyo kanuni hii ya kutahiniwa imelengwa hata kwa Mitume (a.s.) Ama kanuni hii kwa watu wote ni kama tulivyoona katika Aya iliotangulia, ila kwa kuongezea tunapenda kunakili Aya ifuatayo:
َ ُاس أَن ي ُْت َر ُكوا أَن َي ُقولُوا آ َمنَّا َو ُه ْم اَل ي ُْف َتن ون ُ َّأَ َح ِس َب الن “Je, wanadhani watu wataachwa waseme tumeamini nao wasijaribiwe?” (Qur’ani 29:2).
Ama kuhusiana na kutahiniwa Mitume, Mwenyezi Mungu anasema:
َّ ات َفأَ َت َّمه ...ُن ٍ اهي َم َر ُّب ُه ِب َكلِ َم َ َوإِ ِذ ا ْب َتلَى إِب ِ ْر “Na Mola wake alipomjaribu Ibrahim kwa matamko, naye akayatimiza.” (Qur’ani. 2:124).
Na anasema tena kuhusiana na mtihani kwa Nabii Suleiman (a.s.):
َ َفلَ َّما َرآ ُه ُم ْس َت ِق ّرًا ِعن َد ُه َق ْ ال َه َذا ِمن َف ض ِل َربِّي لَِيبْلُ َو ِني أَأَ ْش ُك ُر أَ ْم أَ ْك ُف ُر “Basi alipokiona kimewekwa mbele yake, alisema: Haya ni katika fadhila za Mola Wangu, ili anijaribu, nitashukuru au nitakufuru.” (Qur’ani. 27:40). 16
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 16
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
Maudhui ya Mtihani: Aya imetaja baadhi ya mambo wanayotahiniwa wanadamu, kama vile hofu, njaa, kuanguka kiuchumi, kupoteza ndugu na jamaa na ukosefu wa chakula, lakini mtihani wa Mwenyezi Mungu si katika mambo haya tu, bali kuna mambo mengi ambayo kwayo hutahiniwa wanadamu, kama vile kuwa na mali, kuwa na watoto, Mitume, hukumu za Mwenyezi Mungu, na kila aina ya jambo jema na ovu ni mtihani kwa mwanadamu, kama Mwenyezi Mungu anavyosema:
ْ ُ ُ َّ ْر ِف ْت َن ًة ِ َو َنبْلوكم ِبالش ِّر َوال َخي “… na tutakufanyieni mtihani (kwa mambo ya) shari na ya kheri…” (Qur’ani 21: 35).
Katika mtihani wa Mwenyezi Mungu, watu hugawika sehemu mbili: Sehemu ya kwanza ni wale wenye kufaulu katika mtihani, watu wa aina hii ni wale wenye imani thabiti na ukakamavu wa hali ya juu, wasiomuogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, watu hawa wanaelezwa katika Qur’ani kama ifuatavyo:
ْ اس َق ْد َج َمع َ ين َق ْ ُوا لَ ُك ْم َف َ الَّ ِذ اخ َش ْو ُه ْم ُ َّال لَ ُه ُم الن َ َّاس إِ َّن الن ُ وا َح ْسبُ َنا اللُهّ َو ِن ْع َم ْال َو ِك ْ َُف َزا َد ُه ْم إي َماناً َو َقال يل ِ
“Wale ambao waliambiwa na watu: Hakika watu wamewakusanyikia kwa hivyo waogopeni. Lakini yakawazidishia imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha na bora ya mwenye kutegemewa ni Yeye.” (Qur’ani 3: 173).
Na sehemu ya pili, ni wale wenye kufeli na kupata hasara. Kwa mfano, wakati mambo yanapopamba moto na hofu kutawala, utawaona baadhi ya watu wakirudi nyuma na kubweteka, na hatimaye kukubali kurubuniwa, ili wote wasifikwe na matatizo, na huku wakitoa visingizio mbalimbali visivyo na msingi, kama vile Mwenyezi Mungu anavyoelezea hali ya watu hao kwa kusema:
ُُ ٌ وب ِهم َّم َر َ ُيه ْم َي ُقول َ ار ُع َ َف َت َرى الَّ ِذ ون َن ْخ َشى َض ي ِ ين ِفي قل ِ ون ِف ِ ُس صي َب َنا َدآ ِئ َر ٌة ِ ُأَن ت “Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunaogopa yasitusibu majanga.” (Qur’ani 5: 52). 17
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 17
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
Sababu za Kufaulu Mtihani: Kama ambavyo Aya mbalimbali zilivyoeleza juu ya kila mwanadamu kuingia katika mtihani wa Mwenyezi Mungu. Basi ni mambo gani yanayomfanya mtu kufaulu mtihani huo? Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kupitia Kitabu chake ametaja njia za kufuata ili mtu aweze kufaulu mtihani Wake, miongoni mwa njia hizo ni kama zifuatazo: 1.
Njia muhimu katika kufaulu mtihani wa Mwenyezi Mungu ni kama ilivyoelezwa katika ibara ifuatayo: “Na wabashirie wanaosubiri.” Ibara hii ya Aya inatoa bishara njema kwa wale wenye kusubiri na kuvumilia, na inatoa uhakika ya kwamba subira ni alama kubwa ya kufikia malengo.
2.
Kuwaza na kufikiria mara kwa mara ya kwamba matatizo yanayomkabili mwanadamu ni jambo la kupita na kumalizika, hata kama matatizo hayo ni makubwa kiasi gani, nadharia hii tunaipata katika ibara isemayo:
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” Maneno haya ni mukhtasari wa somo zima la Tawhidi (Upwekesho wa Mwenyezi Mungu) na namna ya kumtegemea Yeye tu katika kila kitu na katika kila zama. Mawalii wa Mwenyezi Mungu daima husema maneno haya wanapokabiliwa na matatizo mbali mbali, ili wasije wakashindwa katika mtihani wanaokabiliana nao, na badala yake hutoka katika mtihani huo kwa salama na amani, huku wakiwa na yakini ya hali ya juu ya kwamba mwisho wa yote ni kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya malipo. 3.
Kutegemea nguvu za Mwenyezi Mungu katika harakati mbalimbali katika kuitetea na kuipigania Dini Yake, na huku nyoyo zikiwa ni zenye matumaini makubwa juu msaada Wake na malipo Yake, ikiwa ni kupata ushindi hapa duniani au malipo mema Siku ya Kiyama au yote mawili, Mwenyezi Mungu anasema:
َ ُح ِس ِن َ َوالَّ ِذ َ ين َج .ين ْ اه ُدوا ِفي َنا لََن ْه ِد َينَّ ُه ْم ُسبُلََنا َوإِ َّن اللهََّ لَ َم َع ْالم “Na wale wanaofanya juhudi kwa ajili Yetu, hakika tutawaongoza kwenye njia Zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wema.” (Qur’ani 29: 69).
18
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 18
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
Na pia kutambua ya kwamba kila lifanyikalo liko katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Siku ya vita vya Karbalaa, Imamu Husein (a.s.), baada ya kuona wafuasi wake pamoja na watoto wake wanauwawa kinyama mmoja baada ya mwingine, alisema:
.علي ما نزل بي أنّه بعين اهلل ّ ه ّون “Haya yanayonisibu ni mepesi kwa vile yanaonekana na Mwenyezi Mungu.”6
4.
Kuwasoma watu waliotangualia, ili kujua ni misimamo gani walioichukua pale walipokabiliana na matatizo ni muhimu sana, kwani mtu mwerevu ni yule anayejifunza kupitia uzoefu wa wengine. Kutokana na kanuni hii Mwenyezi Mungu amehimiza sana katika Kitabu Chake juu ya kusoma habari za watu waliotutangulia, anasema:
َ ص لَ َعلَّ ُه ْم َي َت َف َّك ُر ….ون ُ َف ْاق َ ص َ ص ْال َق ِ ص
“… Basi simulia visa, huenda wakatafakari.” (Qur’ani 7:176).
Tunaporudi katika visa mbali mbali tunawashuhudia Mitume wa Mwenyezi Mungu namna walivyojipamba na vazi la subira pale walipofanyiwa mambo mengi ya maudhi kutoka kwa watu wao, Mwenyezi Mungu anasema:
ُ ُُوا َوأ ْ وذ ْ وا َعلَى َما ُك ِّذب ْ ص َب ُر وا َ َولَ َق ْد ُك ِّذ َب ْت ُر ُس ٌل ِّمن َق ْبلِ َك َف َ ات اللِهّ َولَق ْد َج َ ص ُر َنا َو ُ َحتَّى أََت اءك ِمن نَّ َب ِإ ْ اه ْم َن ِ ال ُم َب ِّد َل لِ َكلِ َم َ ِْال ُم ْر َسل .ين “Na hakika walikadhibishwa Mitume kabla yako, wakavumilia juu ya kukadhibishwa na kuudhiwa, mpaka ikawafikia nusura yetu. Na hakuna wa kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu. Na bila shaka zimekujia baadhi ya habari za Mitume hao.” (Qur’ani 6:34).
6
Muhsin al-Amin, A’yaanu Shia, Jz.1, Uk. 609 19
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 19
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA TATU
ُ ات َما َر َز ْق َن ْ اك ْم َو َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اش ُك ُروا ِ ين آ َمنُوا ُكلُوا ِم ْن َطيِّ َب َّللِه ُ ون إنَّ َما َح َّر َم َعلَي ُْ ُ َّ ْك ُم ْال َم ْي َت َة َو الد َم َولَ ْح َم ِ َ ِ إِ ْن كنت ْم إِيَّاُُه َت ْعبُ ُد ْ ْال ِخ ْ ْر اللهَِّ َف َم ِن َ اض ُط َّر َ ِير َو َما أ ِه َّل ِب ِه ل اغ َو اَل َعا ٍد ب ْر ي غ ي غ ز ن َ َ ِ ِ ِ ٍ ور َر ِحي ٌم ٌ َف اَل إِ ْث َم َعلَ ْي ِه إِ َّن اللهََّ َغ ُف “Enyi mlioamini! Kuleni vizuri tulivyowaruzuku, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa mnamwabudu Yeye tu. Hakika amewaharamishia mzoga tu na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichochinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Basi aliyefikwa na dharura (akala) bila kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani 2: 172-173).
MAELEZO: Qur’ani Tukufu inatumia utaratibu wa kusisitiza na kurudia rudia mara nyingi katika kuyatafutia ufumbuzi mambo maovu yalioenea katika jamii na kuzoeleka kiasi huonekana ni mambo ya kawaida. Aya hizi zinaelezea namna washirikina walivyokuwa wakijiharamishia vyakula mbali mbali pasi na kuwa na dalili yoyote au sababu ya kisayansi inayoonesha ubaya wa vyakula hivyo. Kwa vile suala la kujiharamishia vyakula lilianza katika zama za kijahilia na kuendelea baada ya kudhihiri Uislamu, Mwenyezi Mungu amewataka wale walioamini waachane na kanuni hizo za kijahilia na badala yake washikamane na sheria za Kiislamu alizokuja nazo Mtume (s.a.w.w.), kwa kula vyakula vizuri na vya halali vinavyolingana na maumbile yao ya kibinadamu, na kuachana na vyakula vinavyosababisha madhara katika afya zao, kama Aya inavyosema: “Enyi mlioamini! Kuleni vizuri tulivyowaruzuku, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa mnamwabudu Yeye tu. Ni wazi ikiwa mtu atashikamana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kuachana na makatazo yake huku akijichunga katika vyakula vyake na vinjwaji vyake, hiyo itakuwa ni sababu ya kuweza kupata nguvu na siha njema katika kutekeleza majukumu yake na kumuwezesha kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kumshukuru kutokana na neema mbali mbali anazomruzuku. 20
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 20
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
Aya hii pia inatoa maana pana ya ibada, na kuonesha kwamba mtu anatakiwa amwabudu Mola Wake hata kwenye kujitafutia riziki kwa kuangalia ni kipi kinasatahiki kuliwa na kipi hakifai, kwani Mwenyezi Mungu ametoa sharti kwa watu kula riziki ya halali ikiwa kweli wanamwabudu Yeye tu, ama yule asiyejali katika chumo lake, anajali kupata tu kwa njia yoyote ile, mtu huyo atakuwa bado hajamwabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake, bali atakuwa amemshirikisha na utashi wa nafsi yake, kama anavyosema:
َ أَ َف َرأَي ...ُْت َم ِن اتَّ َخ َذ إِلَ َه ُه َه َواه “Je! Umemuona yule aliyeyafanya yale anayoyataka yeye kuwa ndiye mungu wake…?” (Qur’ani 45:23).
Amri nyingine ilioelekezwa kwa Waumini ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kule kuwaruzuku riziki nzuri na ya halali, hii inamaanisha ya kwamba, wanatakiwa waelewe ya kwamba riziki hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu kwa hivyo ni juu yao kuitumia katika mipaka aliyowawekea, kwa kutofanya israfu na ubadhirifu katika matumizi yake, kama anavyosema:
ْ ُ ُ َ ْ ْ ْ ُُ َ وا إنَّ ُه َ ُس ِر ِف ين ْ ُح ُّب ْالم ِ ال ي ِ وكلوا َواش َربُوا َوال ت ْس ِرف “Na kuleni na kunyweni wala msifanye ufujaji (israf), hakika Yeye hawapendi wafanyao ufujaji (israf).” (Qur’ani 7: 31).
Vizuri ni kwa Ajili ya Waumini: Mwenyezi Mungu amewataka Waumini wale na kujistarehesha kwa vyakula mbalimbali alimradi vyakula hivyo viwe vizuri kiafya na halali na bila ya kufanya israfu na ufujaji katika ulaji, hii ni ishara kwamba pamoja na kuwa wasiokuwa waumini wanajistarehesha kwa vyakula vizuri lakini walengwa hasa ni Waumini, na ni mawazo yasio sahihi kuwaona baadhi ya Waislamu wakijiepusha kabisa kuzitumia neema hizo kwa kudhani kwamba huo ndio uchamungu wa hali ya juu, tukumbuke ya kwamba wakiacha kuzitumia, maadui zao watazitumia na kupata afya njema ya kuweza kuwahujumu Waislamu, Mwenyezi Mungu anasema:
21
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 21
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
الر ْز ِق ِّ ات ِم َن ِ ُق ْل َم ْن َح َّر َم ِزي َن َة اللِهّ الَِّت َي أَ ْخ َر َج لِ ِع َبا ِد ِه َو ْال َّطيِّ َب ْ ُين آ َمن ُّ وا ِفي ْال َح َيا ِة َ ُق ْل ِهي لِلَّ ِذ ص ًة َي ْو َم ْال ِق َيا َم ِة َك َذلِ َك َ ِالد ْن َيا َخال َ ات لِ َق ْو ٍم َيعْلَ ُم ون ِّ نُ َف ِ ص ُل اآل َي “Sema: Ni nani aliyeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu ambalo amewatolea waja Wake, na vilivyo vizuri katika riziki? Sema: Hivyo ni kwa wale walioamini katika maisha ya dunia, ni vyao tu siku ya Kiyama. Namna hii tunazieleza Ishara kwa watu wajuao.” (Qur’ani 7: 32).
Kwa hivyo neema hizi zimekusudiwa Waumini hapa duniani, pamoja na hivyo wasio waumini nao wanazitumia, ama Siku ya Kiyama ni Waumini tu ndio watakaoendelea kuzipata, basi ni kwa nini watokee baadhi ya Waislamu wajizuie kuzitumia neema zilizoandaliwa kwa ajili yao hapa duniani na huko akhera! Aya inayofuatia inawaelezea Waumini baadhi ya vyakula vilivyo haramu, kama Mwenyezi Mungu anavyosema:
َّ الد َم َولَ ْح َم ْال ِخ ْنزير َو َما أُ ِه ُ إنَّ َما َح َّر َم َعلَي َ َّ ْك ُم ْال َم ْي َت َة َو ْر ي غ ل ه ب ل ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ُ َّلله َّلله ْ ْ ا ِ َف َم ِن ور ٌ اغ َو اَل َعا ٍد َف اَل إِث َم َعلَ ْي ِه إِ َّن ا َ َغ ُف َ اضط َّر َغي ٍ ْر َب َر ِحي ٌم “Hakika amewaharamishia mzoga tu na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichochinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Basi aliyefikwa na dharura (akala) bila kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani 2: 173).
Vyakula vya haramu vilivyotajwa katika Aya hii vina madhara katika mwili wa mwanadamu, kama vile nyama ya nguruwe, nyamafu na damu, ama nyama ya mnyama aliyechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu inakuwa na madhara ya kiroho. Kuna aina ya vyakula mbali mbali vilivyoharamishwa katika Qur’ani na katika Hadithi za Mtume (s.a.w.w.), na hivi vilivyotajwa hapa ni vile ambavyo walijihalalishia baada ya kujiharamishia vyakula vizuri kiafya. Licha ya uharamu wa vyakula hivi, si dhambi ikiwa mtu atafikwa na shida ya chakula kiasi cha kumpelekea kula chakula 22
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 22
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
kilicho haramu, kwa sharti ale kiasi cha kuondosha tatizo lake na sio kwa kutaka kujistarehesha nacho, kwa hivyo ruhusa iliyotolewa ni kwa yule tu asiyependa kula chakula hicho katika wakati wa kawaida, bali hulazimika kula kwa kukosa budi, basi pindi alapo ale kiasi tu cha kumuokoa na mauti. Baadhi ya waanachuoni wameonelea ya kwamba, ruhusa ya kula chakula kilichoharamishwa ni kwa msafiri tu aliyeishiwa chakula halali, kwa sharti safari yake iwe ni ya halali, kama vile ruhusa ilivyotolewa kwa msafiri safari ya halali kupunguza Swala, ama msafiri ambaye safari yake si ya halali haruhusiwi kupunguza Swala, kwa hivyo pia hana haki ya kula vyakula vya aina hii wakati wa dharura. Aya inamalizikia kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.� Ni kwamba Mwenyezi Mungu ambaye ameharamisha vyakula hivyo ameruhusu kuliwa wakati wa dharura kwa rehema zake.
23
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 23
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA NNE
ُ ين آ َمنُوا ُك ِت َب َعلَي َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اص ِفي ْال َق ْتلَى ْال ُح ُّر ُ ص َ ْك ُم ْال ِق ُْال ْن َثىٰ ب أ ُْب ْال ُح ِّر و ْال َع ْب ُد ب ْال َع ْبد و أ ال ْن َثىٰ َف َم ْن ُع ِف َي لَ ُه ِم ْن أَ ِخي ِه َ ِ ِ َ ِ ِ َ َ ِ ْر ٌ ان َذٰلِ َك َت ْخ ِف ٌ َش ْي ٌء َفاتِّ َب يف ِم ْن ُ اع ِب ْال َمع ٍ وف َوأ َدا ٌء إِل ْي ِه ِبإِ ْح َس ُ َرب ْ ِّك ْم َو َر ْح َم ٌة َف َم ِن ٌ ى َب ْع َد َذٰلِ َك َفلَ ُه َع َذ اب أَلِي ٌم َولَ ُك ْم ِفي ٰ اع َت َد َ ْصاص َح َيا ٌة َيا أُولِي أ ْ ال ْ َ اب لَ َعلَّ ُك ْم َتتَّ ُق ون ب ل َ ِ ِ َ ال ِق “Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kisasi kwa wenye kuuliwa; muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na anayesamehewa na ndugu yake chochote, basi ni kufuatana kwa wema na kulipa kwa ihsani. Hiyo ni tahafifu itokayo kwa Mola Wenu na rehema. Na atakeyeruka mipaka baada ya hayo, basi ana adhabu iumizayo. Mna uhai katika kisasi, enyi wenye akili, ili msalimike.” (Qur’ani 2:178-179).
SABABU YA KUTEREMKA: Katika makabila ya Kiarabu kulienea suala la kabila moja kulipiza kisasi dhidi ya kabila jingine, na huko kulipiziana kisasi kulikuwa hakuna mipaka, ilikuwa mtu mmoja akiuwawa na mtu wa kabila jingine, watu wa kabila lililouliwa mtu wao walikuwa wakipambana dhidi ya kabila jingine na kuwauwa wengi miongoni mwa wanaume wa kabila la mtu muuwaji, Aya ya Qur’ani iliteremka kwa lengo la kuweka sheria ya kisasi. Sheria hii ya Kiislamu imekuja na kukubaliana na kanuni mbili zilizokuwepo kwa Waarabu: kanuni ya wale waliokuwa wakiona kwamba adhabu anayostahiki muuwaji ni kuchukuliwa kisasi, na baadhi ya watu waliona kwamba njia ya kufuata ni kutolewa fidia tu, kwa hivyo Aya ikaja kuthibitisha kuchukuliwa kisasi ikiwa ndugu wa marehemu hawatakubali kuchukua fidia, na kama watakubali basi watachukua fidia tu.7 7
Shirazy, Tafsirul Amthal,Jz. 1, Uk.501 24
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 24
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
Pia imepokewa ya kwamba Aya hizi ziliteremka kutokana na makabila mawili ya Kiarabu yaliyopigana vita vikali wakati wa Mtume (s.a.w.w.), wakasema: Kutokana na kuuwawa mtumwa wetu tutalipiza kisasi kwa kumuua fulani mtoto wa fulani (ambaye hakuwa mtumwa), na kwa sababu ya kuuwawa mjakazi wetu, tutamuuwa mwanamke fulani mtoto wa fulani (ambaye hakuwa mjakazi), hapo Aya ikateremka na ikisema: “Muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke.”8 Kisasi ni Uhai: Aya inaelezea kwa uwazi utaratibu wa Kiislamu katika maisha ya mwanadamu kwa kutaja hukumu inayoharamisha umwagaji wa damu ya mtu asiye na hatia, bila ya shaka hili ni suala muhimu katika maisha ya kijamii, kwa hivyo ikaja kupinga tabia ya kijahilia ya kuuwana ovyo pasi na sababu ya msingi: “Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kisasi kwa wenye kuuliwa..” Aya hii inatoa msisitizo na kutilia mkazo juu suala la kuchukuliwa kisasi. Aya haikuishia tu kuelezea adhabu inayofanana na kosa la mtu alilomtendea mwenzake, bali pia imebainisha namna kisasi kinavyostahiki kuchukuliwa, kama inavyosema: “Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke.” Pia Aya inabainisha ya kwamba wenye haki ya kukubali kuchukuliwa kisasi dhidi ya aliyetenda kosa la mauwaji ni ndugu wa mtu aliyeuwawa, na si lazima wakubali kisasi, bali wanaweza kuchukua fidia au kusamehe yote mawili. Na kama wataamua kuchukua fidia badala ya kisasi, basi ndugu hao wasimlazimishe kulipa fidia ndani ya muda ambao hawezi kulipa, bali wanatakiwa kuonesha wema juu ya mtu huyo ambaye Qur’ani inamzingatia kuwa ni ndugu yao, na ndugu huyo aliyesamehewa kuchukuliwa kisasi na badala yake kutakiwa kulipa fidia, ni juu yake kuilipa kwa ukamilifu na haraka kwa kadiri ya nafasi yake, kama Aya inavyoendelea kusema: “Na anayesamehewa na ndugu yake chochote, basi ni kufuatana kwa wema na kulipa kwa ihsani.” Baada ya hapo Aya inasisitiza umuhimu wa kushikamana na hukumu za Mwenyezi Mungu na kutoa onyo kali kwa wale wanaokwenda kinyume nazo: “Hiyo ni tahafifu itokayo kwa Mola Wenu na rehema. Na atakeyeruka mipaka baada ya hayo, basi ana adhabu iumizayo.” Kulipiza kisasi au kutoa fidia ni hukumu zinazokubaliwa na kila mwenye akili timamu, kwani kwa upande mmoja hupinga ujahilia wa kale na pia ujahilia mambo leo unaotoa fursa ya kulipiza kisasi kwa kuuwawa maelfu ya watu kwa sababu ya 8
As-Suyutiy, Addurul Manthur,Jz. 1, Uk.172 25
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 25
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
kifo cha mtu mmoja! Na kwa upande mwingine inafungua mlango wa msamaha kwa muuwaji. Na kwa upande mwingine, pande zote mbili hazina haki ya kuchupa mipaka ikiwa ndugu wa marehemu watasamehe kisasi na badala yake kukubali kuchukua fidia, hii ni kinyume kabisa na hali ilivyokuwa katika zama za kijahilia ambapo baadhi ya wakati walikuwa wakimuuwa muuwaji hata baada ya kuchukua fidia. Aya inayofuatia ibara yake ni fupi lakini imekusanya maana pana sana huku ikitoa majibu ya masuala mengi yanayoulizwa kuhusiana na kisasi, inasema: “Mna uhai katika kisasi, enyi wenye akili” Aya hii yenye maneno yapatayo kumi, na kujaa balagha na fasaha, inabainisha malengo ya hukumu ya kuchukuliwa kisasi katika Uislamu, kwani inaeleza wazi kwamba kulipiza kisasi hakumaanishi kufuta uhai wa mtu mwingine, bali ni njia ya kuyalinda na kuyahifadhi maisha ya watu kwa ujumla, lau kama hukumu ya kisasi haitokuwepo katika jamii, itawapelekea wauwaji kuendeleza ubabe wao na kuziweka roho za watu katika hatari, kama tunavyoshuhudia katika nchi zilizofuta hukumu ya kifo, katika nchi hizo kuna ongezeko kubwa na la kasi la ujambazi na ukatili. Na mwishoni mwa Aya kuna ibara isemayo: “ili msalimike.” Mwenyezi Mungu anatoa tahadhari kwa wale wanaokwenda kinyume na hukumu hii ya Kiislamu iliojaa uadilifu, kwani usalama wa raia utakuwa hatarini ikiwa hukumu ya kifo itafutwa kwa wauwaji, na watu wengine hawatosalimika dhidi ya mauwaji. Mtazamo wa Baadhi ya Watu Katika Kisasi: Kuna baadhi ya watu wanaona kwamba hukumu ya kuuwawa muuwaji ni jambo lisilokubalika kiakili, na wamejaribu kuleta hoja mbalimbali dhidi yake, miongoni mwa maneno yao ni kama yafuatayo: 1. Ukatili hauzidi kwa sababu ya kuuliwa mtu mmoja, na kulipiza kisasi (kuuliwa muuwaji) kunapelekea kurudia tendo hili baya. 2. Kisasi kinatokana na roho ya ukatili na moyo usio na huruma, kwa hivyo inabidi kuiondosha hali hii kwa njia ya malezi, ama kwa kulipiza kisasi ni kuikuza hali hii. 3. Mtu mwenye akili timamu hawezi kumuuwa mtu mwingine, wanaofanya kitendo hicho ni wale tu walio na ugonjwa kisaikolojia, na inapasa kutibiwa mtu huyo, ama kuchukuliwa kisasi sio suluhisho la tatizo lake. 4. Kanuni za kijamii zinapaswa kwenda sambamba na maendeleo ya kijamii, na haiwezekani katika zama hizi kufuatwa kanuni zilizokuja tokea karne kumi na nne zilizopita.
26
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 26
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
5. Ni jambo zuri zaidi kwa muuwaji kufanyishwa kazi kwa nguvu, kwa kufanya hivyo jamii itafaidika na nguvu zake na kuepukana na shari zake. 6. Haya ndiyo baadhi ya maneno yanayosemwa na wapingaji wa hukumu ya kisasi kwa muuwaji. Sheikh Makarim Shiraziy amewajibu wale wenye fikra hizi kwa kusema: “Lau kama tutaangalia kwa makini katika Aya zinazozungumzia kisasi, basi ndani yake tutapata majibu ya kila hoja yao, kwa mfano Aya hii: “Mna uhai katika kisasi, enyi wenye akili, ili msalimike.” Inabainisha wazi ya kwamba maisha ya kijamii hayawezi kuwa na amani na utulivu bila ya kung’olewa sababu zenye kuidhuru na kutaka kuiangamiza jamii hiyo, ni wazi ya kwamba ulipizaji kisasi ni katika njia zinazotoa dhamana ya kuhifadhi maisha ya wanajamii, ulipizaji kisasi ni katika mambo ya maumbile ya mwanadamu. Hata mfumo wa tiba na kilimo umesimamia juu ya msingi huu wa kiakili, ni mfumo wa kuondoa kiungo chenye madhara na hatarishi; tunawashuhudia madaktari wakikata baadhi ya viungo vilivyo na matatizo ikiwa viungo hivyo vinasababisha madhara kwa viungo vingine, na mimea hung’olewa au kukatwa baadhi ya matawi yaliyoharibika ili mimea mingine yenye faida ipate kumea vizuri. “Wale wanaoona kulipizwa kisasi kwa muuwaji ni ukatili, wanaangalia suala hili kwa mtazamo binafsi, lau kama wengeliangalia kwa ajili ya manufaa ya kijamii bila ya shaka wangelibadilisha msimamo wao huo, kwani kuwaondosha watu hawa katika jamii ni sawa na kukikata kiungo kilichoharibika au kukata tawi lenye kuleta madhara katika mti, na wala hakuna mtu yeyote anayepinga kukatwa kiungo hicho au tawi hilo. Ama jawabu la hoja yao ya pili ni kwamba, hukumu ya kisasi haina mafungamano na ukatili, kwani lengo la ukatili ni kuzima moto wa ghadhabu unaotokana na masuala binafsi, ama kisasi kinalenga kuzuia kuendelea mauwaji katika jamii na kuwahifadhi watu wasio na makosa. “Ama hoja yao ya tatu inayosema ya kwamba: “Muuwaji huwa ana matatizo ya kisaikolojia, na ni muhali mtu mwenye akili timamu kuweza kumuuwa mtu mwingine. Jawabu letu ni kwamba, maneno yao haya ni sahihi katika baadhi ya matukio ya mauwaji, na Uislamu hautoi hukumu ya kisasi kwa mtu mwenye matatizo ya kiakili, lakini haikubaliki kwamba kila anayeuwa huwa ana matatizo ya kiakili, bila ya shaka hoja yao hii ni kichocheo cha ufisadi na kuwahimiza wauwaji waendelee na maovu yao. “Lau kama hoja yao hii ingekuwa sahihi kwa huko kumtetea kwao muuwaji ili asiuwawe, kwa madai eti ni mgonjwa wa akili, pia ingekuwa sahihi kwa wale wanaowakosea watu wengine, kwani mtu mwenye akili timamu katu hamkosei au kumdhulumu mtu mwingine, kwa hivyo itapasa kufutwa kwa adhabu zote za makosa, na wakosaji hao kulazimika kupelekwa hospitali ili wakatibiwe
27
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 27
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
ugonjwa wa kisaikolojia badala ya kupelekwa jela. “Ama hoja yao ya nne ya kudai kwamba sheria ya kisasi imepitwa na wakati kutokana na ulimwengu kupiga hatua za kimaendeleo;hoja hii inapingana na hali halisi ya ukatili ilivyo katika zama hizi, kwani mauwaji ya leo ni ya kinyama na ya kutisha na ya fedheha. Lau kama kweli jamii imeendelea kweli kweli, basi ingeshikamana na kuwasamehe wakosaji badala ya unyama huu wanaoufanya kila kukicha, suala la kusamehewa muuwaji ni jambo linalokubalika katika Uislamu. “Kubatilishwa kwa hukumu ya kisasi ni sababu kubwa ya kuongezeka kwa maovu na ukatili katika jamii. Ama kuwahifadhi wauwaji katika majela hakutoi hakikisho la kuilinda jamii na kuwazuia wasiendelee na unyama wao, hasa katika zama hizi ambapo baadhi ya jela ni bora kuliko nyumba wanazotoka wauwaji. Kuongezeka kwa idadi kubwa ya mauwaji katika nchi zilizofuta hukumu ya kifo ni dalili tosha ya kuthibitisha umuhimu wa kuwepo adhabu hii, leo wauwaji wanaendelea kuyapoteza maisha ya watu pasi na kuwa na khofu yoyote ile.”9
Je, Hukumu ya Kisasi inamdhulumu Mwanamke? Baadhi ya watu huenda wakadhani ya kwamba sheria ya Kiislamu imempunguzia mwanamke haki kutokana na kuweka hukumu ya mwanamume kutouliwa pindi atakapomuuwa mwanamke. Kwa kweli mafundisho ya Kiislamu hayako hivyo, ukweli wa mambo ni kwamba inafaa mwanamume kuchukuliwa kisasi ikiwa atamuuwa mwanamke kwa sharti ndugu wa marehemu wakubali kutoa nusu ya fidia ya huyo mwanamume atakayeuwawa kwa kosa la kumuuwa mwanamke. Makusudio ya ibara isemayo kwamba: ‘Hakuna kisasi kwa mwanamume pindi anapomuuwa mwanamke’. Maana yake ni kwamba ni kuchukuliwa kisasi bila ya sharti, ama akitolewa nusu ya fidia yake, hapo itajuzu naye kuuwawa. Ni wazi kwamba kulipiwa nusu ya fidia kwa mwanamume aliyeuwawa baada ya kumuuwa mwanamke si kumpunguzia mwanamke hadhi yake, bali hukumu hii ina lengo la kuiwezesha kiuchumi familia ya huyo muuwaji baada na yeye kuuwawa. Kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba, wanaume wanabeba majukumu ya kiuchumi na matumizi mbali mbali ya familia zao, na bila shaka kuna tofauti kubwa ya kiuchumi inayopatikana kwa kuondoka (kufariki) mwanamume na kuondoka mwanamke katika familia, lau kama Uislamu haukuangalia tofauti hii familia ya mwanamume aliyeuwawa itasibiwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi, kwa hivyo kulipwa kwa hiyo nusu ya fidia itajaza pengo litakaloachwa na msimamizi wa familia na kuifanya isitetereke kiuchumi. Uislamu hauruhusu kuiona familia ikiwa katika hali mbaya 9
Shirazy, Tafsirul Amthal, Jz. 1, Uk. 507 28
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 28
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
kiuchumi na kukosa haki zao za kila siku kwa sababu ya kaulimbiu ya ‘Usawa’. Ni kweli baadhi ya wanawake wanahali nzuri zaidi kiuchumi kuliko waume zao, lakini ni kwamba sheria za Kiislamu siku zote zinaangalia hali ya kawaida ya mambo na wala haiangalia baadhi ya hali zinazojitokeza mara chache na kwa nadra, kwa hivyo hukumu hii itabakia palepale kwa kulinganishwa kila mwanamume kwa kila mwanamke. Udugu wa Kiislamu: Kitu cha kuzingatia katika Aya hizi tunazokwenda nazo ni kwamba, kuna ibara inayomaanisha kuwepo kwa udugu kati ya muuwaji na jamaa wa mtu aliyeuliwa, yote hayo ni kuonesha namna Uislamu unavyosisitiza juu ya suala la udugu kati ya Waislamu, msisitizo huu umekuja ili kutoa fursa kwa jamaa wa mtu aliyeuwawa mtu wao kumsamehe muuwaji. Bila ya shaka msamaha huo unatakiwa utolewe kwa mtu ambaye ameuwa mtu katika hali na mazingira maalumu na kuonesha majuto makubwa baada ya kufanya kosa hilo, ama watu majangili wanaojifakharisha kutokana na ukatili wao na kutoonesha ishara yoyote ya majuto, watu wa aina hiyo hawastahiki kuitwa ndugu, kwa hivyo hawastahiki kupewa msamaha wowote ule, bali watastahiki kuuwawa kama vile walivyouwa. Uzuri wa Sheria za Kiislamu: Bila ya shaka ndugu msomaji umeona utaratibu wa hukumu ya kisasi katika Uislamu, ama katika sheria zilizotungwa na wanadamu, ni zenye kuwadhulumu wanafamilia waliouliwa mtu wao. Katika kanuni za kibinadamu mara panapotokezea mauwaji, serikali ndio inayokuwa mshitaki, na ndugu wa marehemu hawana nafasi yoyote zaidi ya kushiriki katika usikilizaji wa kesi kama wakipenda. Mara nyingi muuwaji kwa mujibu wa kanuni hizo, hufungwa maisha au miaka kadhaa, na baadhi ya nchi hutoa adhabu ya kifo, na kama kutakua na faini yoyote, basi faini hiyo itaingia katika mfuko wa serikali, bila ya kuzingatia nafasi ya mwenye kuuwawa katika familia yake, huwenda akawa ni baba mwenye kutegemewa katika kuindesha familia yake, na kuondoka kwake kukawa na pengo kubwa, kiasi cha kuifanya familia iyumbe kiuchumi. Katika Uislamu, mustakabali wa muuwaji uko mikononi mwa ndugu wa marehemu, wataamua kuchukua kisasi au kupokea fidia au kumsamehe. Na haya yote yanapaswa kuangaliwa mazingira ya mauwaji na mtu aliyetekeleza mauwaji. Kwa hivyo haki ya watu itaweza kupatikana tu ikiwa hukumu hii ya Kiislamu itakuwa 29
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 29
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
ndio yenye kufuatwa katika mahakama mbalimbali. Ama kudai ya kwamba mauwaji ni miongoni mwa kesi za jinai, na serikali ndio mshitaki, kwa kweli kufanya hivyo ni kuwakosesha wafiwa haki zao za kuamua cha kufanya kwa mtu aliyepoteza maisha ya ndugu yao.
30
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 30
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA TANO
ين آ َمنُوا ُك ِت َب َعلَي ُ الص َيا ُم َك َما ُك ِت َب َعلَى الَّ ِذ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ َ ين ْك ُم ِّ ان ِم ْن ُك ْم َم ِر ً ات َف َم ْن َك َ ِم ْن َق ْبلِ ُك ْم لَ َعلَّ ُك ْم َتتَّ ُق َ يضا ون أَيَّا ًما َم ْع ُدو َد ٍ أَ ْو َعلَىٰ َس َفر َف ِع َّد ٌة ِم ْن أَ َّام أُ َخ َر َو َعلَى الَّ ِذ َ ُط ُيقو َن ُه ِف ْد َي ٌة ي ين ي ِ ٍ ٍ َ َ صو ُموا ْرا َف ُه َو َخي ٌ ين َف َم ْن َت َط َّو َع َخي ً ْر لَ ُه َوأ ْن َت ُ ط َعا ُم ِم ْس ِك ٍ ْر َر َم َ ض َ ْر لَ ُك ْم إِ ْن ُك ْنتُ ْم َتعْلَ ُم َ ان الَّ ِذي أُ ْن ِز َل ِفي ِه ون َشه ُ َخي ٌ ْ ُْ َ ْال ُق ْر ُ ان َف َم ْن َش ِه َد اس َو َبيِّ َن ٍ ات ِم َن ال ُه َدىٰ َوالف ْرق ِ آن ُه ًدى لِلنَّ ِ ِم ْن ُك ُم َّ ان َم ِر ً ص ْم ُه َو َم ْن َك َ يضا أَ ْو َعلَىٰ َس َف ٍر َف ِع َّد ٌة ِم ْن ْر َف ْل َي ُ الشه َ أَيَّام أُ َخ َر يُري ُد اللهَُّ ب ُك ُم ْ ُس َر َو اَ ُس َر َولِتُ ْك ِملُوا ي ل ي ال ُري ُد ِب ُك ُم ْالع ْ ْ ِ ِ ِ ٍ َّ للهَّ ُ ُ ُ ْ َ َ َ ون َوإذاَ ْال ِع َّد َة َولِتُ َ َ َ َ َ ر ك ش ت م ك ل ع ل و م اك د ه ا م ى ٰ ل ع ا وا ِّر ب ك ُ ُ َ ْ ْ َ َ َ ِ يب أُ ََ َ الداع إ َ َ َّ َ َ ْ ُ ان ع د ا ذ ة و ع د يب ج َ َ َسألك ِع َبا ِدي َعنِّي َفإِنِّي َق ِر ٌ ِ ِ ُ ِ ِ َف ْل َي ْس َت ِجيبُوا لِي َو ْلي ْ ُؤ ِمنُوا ِبي لَ َعلَّ ُه ْم َي ْر ُش ُد َ ون أ ِح َّل َ لَ ُك ْم لَيْلَ َة اس لَه َّ ُن َعلِ َم الص َي ام َّ اس لَ ُك ْم َوأَ ْنتُ ْم لَِب ٌ الر َف ُث إِلَىٰ ِن َسا ِئ ُك ْم ُه َّن لَِب ٌ ِّ ِ اب َعلَي ُ اللهَُّ أَنَّ ُك ْم ُك ْنتُ ْم َت ْخ َتانُ َ ْك ْم َو َع َفا َع ْن ُك ْم َفالآْ َن ون أَ ْن ُف َس ُك ْم َف َت َ وه َّن َوا ْب َت ُغوا َما َك َت َب اللهَُّ لَ ُك ْم َو ُكلُوا َو ْ اش ُر ُ اش َربُوا َحتَّىٰ َي َت َبي َ َّن َب ِ ْط أْ َ ْط أْ َ لَ ُك ُم ْال َخي ُ ال ْب َي ُ ال ْس َو ِد ِم َن ْال َف ْج ِر ثُ َّم أَِت ُّموا ض ِم َن ْال َخي ِ ْ َّ اش ُر ُ وه َّن َوأَ ْنتُ ْم َعا ِك ُف َ اج ِد ِّ ْل َو اَل تُ َب ِ الص َيا َم إِلَى اللي ِ ون ِفي ال َم َس ِ ُوها َك َ ٰذلِ َك يُ َبي ُ للهَُّ ِت ْل َك ُح ُدو ُد اللهَِّ َف اَل َت ْق َرب َ اس لَ َعلَّ ُه ْم ِّن ا آ َيا ِت ِه لِلنَّ ِ َيتَّ ُق َ ون 31
12/8/2014 2:43:35 PM
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 31
WITO KWA WAUMINI
“Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu, ili mpate kuwa na takua. Siku maalum za kuhisabika. Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi, au yuko safarini, basi atimize idadi katika siku nyingine. Na wale wanaoiweza kwa shida, watoe fidia kwa kumlisha maskini. Na atakayefanya kheri kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na kufunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua. Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo Qur’ani, kuwa mwongozo kwa watu na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini katika mwezi huu na aufunge; na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anawatakia wepesi wala hawatakii uzito, na mkamilishe idadi hiyo, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amewaongoza, na ili mpate kushukuru. Na waja Wangu watakapokuuliza habari Yangu, Mimi niko karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi nawaniitikie Mimi na waniamini Mimi ili wapate kuongoka. Mmehalalishwa usiku wa saumu kuwaingilia wake zenu. Wao ni vazi lenu na nyinyi ni vazi lao. Mwenyezi Mungu anajua kuwa mlikuwa mkizihini nafsi zenu, kwa hivyo amewatakabalia toba yenu na amewasamehe. Basi sasa ingilianeni nao na takeni aliyowaandikia Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainikie weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Na wala msiingiliane nao na hali mko katika itikafu misikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikaribie. Namna hii Mwenyezi Mungu anabainisha ishara Zake kwa watu ili wapate kuwa na takua.” (Qur’ani 2:183-187).
MAELEZO: Swaumu ni Chuo cha Uchamungu: Aya hizi zinaelezea moja kati ya ibada muhimu za Dini ya Kiislamu, nayo ni ibada ya Swaumu, tena kwa kutumia ibara inayoeleweka uzito wake, Aya imeanza kusema: “Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu.” Pia Aya inakumbusha lengo na hekima ya ibada hii kwa kusema: “ili mpate kuwa na takua.” Ni ibara yenye maneno kidogo sana, lakini ni yenye maana nzito. Swaumu ni ibada inayomjenga mwanadamu kuwa na roho ya uchamungu katika vipengele mbali mbali vya maisha yake, hasa wakati wa msimu wa kiangazi kwani mfungaji hulazimika kuacha kujistarehesha kwa chakula na vinywaji na badala yake hujipamba na vazi la subira, ndio maana Aya Tukufu imeieleza ibada hii kwa taratibu mbali mbali ili kuiandaa nafsi ya mwanadamu kuipokea na kuikubali ibada hii kwa moyo mkunjufu. 32
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 32
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwanza kabisa Aya imeanza kwa njia ya wito kwa kusema: “Enyi mlioamini!” Huu ni wito unaofungua sitara ya moyo wa mwanadamu na kunyanyua hisia zake za ndani, kuna utamu na ladha maalumu kwa mwenye kuitwa kwa wito huo, kama anavyosema Imamu Sadiq (a.s):
أزالت تعب العبادة-ّلذة ما في النّداء – أي يا أيّها الذين آمنوا والعناء “Utamu uliomo katika wito - Enyi mlioamini!- huondosha tabu ya ibada na uchovu.”10
Kisha Aya inaeleza ya kwamba vile vile Saumu imefaradhishwa kwa umma mbali mbali ziliotangulia. Baada ya hapo Aya inaelezea hekima ya Saumu na faida anazozipata mfungaji, yote hayo ni kuifanya ibada hii iwe ndani ya moyo na yenye kupendwa. Aya inayofuatia pia nayo inakhafifisha shida inayopatikana ndani ya Saumu, inasema: “Siku maalum za kuhisabika.” Wajibu huu si wa muda mrefu, bali ni wa siku chache tu katika mwaka. Aya inaendelea kusema: “Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi, au yuko safarini, basi atimize idadi katika siku nyingine.” Mgonjwa pamoja na msafiri wamesamehewa kufunga wakati wa mwezi wa Ramadhani na kutakiwa kuja kuilipa katika miezi mingine baada ya kuondoka udhuru wao. Ama wazee wenye umri mkubwa ambao wakifunga husibiwa na mashaka makubwa pamoja na wagonjwa ambao hawatarajii kupona, Aya imewasamehe kufunga na badala yake wanatakiwa watowe fidia, inasema: “Na wale wanaoiweza kwa shida, watoe fidia kwa kumlisha maskini.” Kisha Aya inaendelea kusema:” Na atakayefanya kheri kwa kujitolea, basi ni bora kwake.” Ikimaanisha ya kwamba, yule atakayejitolea chakula zaidi ya wajibu aliowekewa, basi ni bora zaidi kwake, kwani kufanya hivyo pia kutamzidishia malipo kwa Mwenyezi Mungu. Na mwisho Aya inabainisha uhalisia wa Saumu kwa kusema: “Na kufunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua.” Baadhi ya wafasiri wametolea dalili ibara hii ya Aya kwamba, mwanzoni Saumu ilikuwa ni wajibu wa kuchagua kati ya kutoa fidia au kufunga, kisha hukumu hii ilifutwa na kuwa ni wajibu usio na mbadala, lakini dhahiri ya Aya inaonesha msisitizo mwingine wa hekima ya kufunga. Ibada hii ya Saumu ni kama ibada nyingine, haimzidishii Mwenyezi Mungu utukufu wake, bali faida yote inarudi kwa wanaadamu wanaotekeleza maamrisho Yake, ni wazi katika Saumu amesema: “Na kufunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua.” Ibara kama hii tunaishuhudia katika suala la wajibu wa Swala ya Ijumaa, Mwenyezi Mungu anasema: 10
Ar-Rawandiy, Fiqhul Qur’ani Jz. 1, Uk. 72 33
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 33
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
َ َ ْر لَّ ُك ْم إِن ُكنتُ ْم َتعْلَم .ُون ٌ ذلِ ُك ْم َخي... “…Hiyo ni bora kwenu ikiwa mnajua.” (Qur’ani 62: 9).
Na katika Aya nyingine anasema:
َ اهي َم إ ْذ َق ْ ال لِ َق ْو ِم ِه ْر لَ ُك ْم إِ ْن ٌ اعبُ ُدوا اللهََّ َواتَّ ُقو ُه َذٰلِ ُك ْم َخي َ َوإِب ِ ِ ْر َ ُك ْنتُ ْم َتعْلَ ُم ون “Na Ibrahim pale alipowaambia watu wake: Mwabuduni Mwenyezi Mungu na mcheni Yeye. Hayo ni kheri kwenu ikiwa mnajua.” (Qur’ani 29: 16).
Hii ni dalili tosha kwamba, ibara inayosema: “Na kufunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua.” inamuelekea kila mtu anayefunga na si kwa kundi maalumu, kama walivyopita baadhi ya wafasiri wa Ki-Ahlus Sunna. Aya inayofuata katika uchambuzi huu inaelezea wakati wa kufunga na baadhi ya hukumu zake, inasema: “Mwezi wa Ramadhani.” Huu ndio mwezi ambao Waislamu wamefaradhishwa kufunga. Ni mwezi ambao ndani yake imeteremshwa Qur’ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Baada ya kueleza wakati wa kufunga inaeleza hukumu za Saumu kwa msafiri na mgonjwa, inasema: “Basi atakayekuwa mjini katika mwezi huu na aufunge; na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika siku nyingine” Huenda ikawa sababu kubwa ya kurudiwa tena kwa mara ya pili hukumu ya msafiri na mgojwa katika Aya hii ni kule baadhi ya watu kuona karaha kutokufunga katika masiku ya mwezi wa Ramadhani, hata kama ni wagonjwa au wasafiri. Kutokana na Qur’ani kuikariri hukumu hii ina lengo la kuwafahamisha Waislamu ya kwamba, miongoni mwa kusihi kwa Saumu ni mtu kuwa katika afya njema na kutokuwa msafiri, hukumu hii ni hukumu itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na vile vile mtu kula mchana wa mwezi wa Ramadhani akiwa ni mgonjwa au msafiri pia ni hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa hivyo haifai kwenda kinyume na hukumu zake, bali inampasa kila Mwislamu kufuata hukumu zote za Mwenyezi Mungu. Wafasiri wengi wa Ki-Ahlus Sunna katika tafsiri ya sehemu hii ya Aya: “Na kufunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua.” wamepita ya kwamba, mgonjwa na msafiri ni bora kwao kufunga kuliko kutokufunga. Na wengine wanasema ya kwamba: Kufunga ni bora kuliko kutoa fidia. Kwa kweli tafsiri hizi haziendani sambamba na 34
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 34
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
amri ya Mwenyezi Mungu ya kuwataka wasafiri na wagonjwa kuja kulipa Saumu yao baada ya kuondoka nyudhuru zao, au kuwataka wazee na wagonjwa wasiotarajiwa kupona kutoa fidia, kisha wakati huo huo awaambie kufunga ni bora kuliko kula au kutoa fidia! Kinachojitokeza katika Aya ni kwamba msafiri na mgonjwa ambaye ataendelea kudhurika kwa sababu ya Saumu haruhusiwi kufunga na badala yake aje ailipe, na pindi akifunga katika hali hiyo Saumu yake haitosihi kwa kukosekana sharti la Saumu; kwani miongoni mwa masharti ya Saumu ni mtu kutokuwa msafiri au mgonjwa. Mwisho wa Aya hii inatuelezea hekima nyingine ya kufaradhishwa Saumu, inasema: Mwenyezi Mungu anawatakia wepesi wala hawatakii uzito.” Baadhi ya watu wanaona kwamba, Swaumu ni miongoni mwa mashaka na ni kuingiliwa katika uhuru wake wa kujistarehesha kwa starehe za kimwili na kiroho. (Jawabu la hoja hii litakuja katika maudhui ya Hekima ya Saumu). Pia ibara ya Aya hii inaashiria ya kwamba amri za Mwenyezi Mungu zinatofautiana na amri za mtawala dhalimu, kwani katika ibada ya Saumu Mwenyezi Mungu amemsamehe mgonjwa, msafiri na kila mtu asiyeweza kufunga. Aya inaendelea kusema: “na mkamilishe idadi hiyo” Inamaanisha ya kwamba mtu aliye mzima wa afya analazimika afunge mwezi mzima, kwani jambo hilo ni muhimu sana katika kuulea mwili wake na nafsi yake, kwa mantiki hii pia mgonjwa na msafiri nao pia wanatakiwa walipe zile siku ambazo hawakufunga, vilevile mwanamke aliyekuwa na hedhi au nifasi wakati wa mwezi wa Ramadhani, akiwa katika hali hiyo haruhusiwi kuswali wala kufunga, lakini atalazimika kulipa Saumu, ama Swala hatozilipa. Yote hayo ni kwa ajili ya kutimiza idadi ya siku za mwezi wa Ramadhani, ili kila Mwislamu afaidike na neema mbali mbali zilizomo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ibara ya mwisho kabisa katika Aya hii inasema: “na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amewaongoza, na ili mpate kushukuru.” Mumtukuze kutokana na kukuonesheni njia ya uongofu, na mumshukuru kutokana na neema alizokuneemesheni. Faida za Kiroho, Kijamii, na Kisiha Zitokanazo na Swaumu: Swaumu ina nyanja mbali mbali za faida, faida hizo ni za kimwili na za kiroho, na faida iliyo muhimu zaidi ni katika nyanja za tabia na malezi bora. Saumu humfanya mtu kuwa mpole, mwenye huruma, kuwa na maamuzi thabiti na kuyadhibiti matamanio yake. Kwani mfungaji hujizuia kula na kunywa licha ya kuwa na njaa pamoja na kiu, na vile vile hujizuia kufanya mapenzi, huku ni kuthibitisha kivitendo kwamba yeye si kama mnyama ambaye siku zote pupa yake iko kwenye kujaza tumbo lake, 35
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 35
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
na ni dalili ya kwamba yeye anauwezo wa kuidhibiti nafsi yake dhidi ya matamanio na vishawishi vya aina mbali mbali. Upatikanaji wa faida za kiroho katika Swaumu ndio hekima kubwa ya kufaradhishwa ibada hii tukufu. Mtu ambaye hatekelezi ibada hii na kuishi katika mazingira ya upatikanaji wa chakula na vinjwaji kwa urahisi, kiasi cha kumuwezesha kunyoosha mkono tu pindi anapohisi njaa au kiu kwa kujichagulia aina nzuri ya chakula, mtu huyo ni kama mti ulioko pembezoni mwa mto unaofyonza maji ya kutosha wakati wowote, lakini mti huo unapokosa maji kwa siku chache tu huanza kunyauka na kugeuga rangi ya njano. Ama mti unaoota katika jangwa lililo kavu, na kusibiwa na upepo mkali kila kukicha, na wakati mwingine kupigwa na jua lenye kuunguza, na baadhi ya wakati kusibiwa na baridi kali, na siku zote kukabiliana na changamoto mbali mbali, basi huo ndio mti madhubuti na mkakamavu. Na Swaumu nayo ina athari nzuri katika nafsi ya mwanadamu kama ilivyo kwa mti wa aina hii, hivi vizuizi vya muda mfupi humfanya mwanadamu kuwa na nguvu za kiroho na azma ya kuacha kutenda maovu, pia katika nafsi yake kunakuwa na nuru na usafi wa moyo, baada ya kujaa matamanio ya kishetani. Kwa mukhtasari wa maneno ni kwamba: Swaumu humtoa mtu katika ulimwengu wa kihayawani na kumuingiza katika ulimwengu wa Kimalaika, na dalili ya haya ni ibara inayosema: “ili mpate kuwa na takua.” Na pia kutokana na Hadithi inayosema:
الصوم جنّة من النّار ّ Swaumu ni kinga dhidi ya Moto.11
Na kutoka kwa Imam Ali (a.s.) amesema: Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa kuhusiana na njia ya kupambana na shetani, alisema:
ّ والحب في اهلل تكسر ظهره ّ الصوم يس ّود وجهه ّ ّ والصدقة الصالح يقطع دابره واإلستغفار يقطع ّ والمواضبة على العمل .وتينه “Funga inaufanya uso wake (shetani) kuwa mweusi na sadaka huuvunja mgongo wake, na kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kudumu katika amali njema hukata mizizi yake, na kuomba msamaha kunakata mshipa wake.” 11
Al-Kuleyniy, Usulul Kafiy Jz. 2, Uk. 19 36
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 36
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
Na katika kueleza hekima ya ibada Imamu Ali (a.s.) anasema:
والصيام إبتالء إلخالص الخلق ّ “Na Swaumu ni mtihani wa kupimwa ikhlasi za viumbe.”12
Na imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:
ّ الريّان ال يدخل فيها ّ .الصائمون ّ إن للجنّة باباَ يدعى ّ إال “Hakika Pepo ina mlango unaoitwa Arrayan, hawatopita katika mlango huo isipokuwa wafungaji.”13
Katika kuisherehesha Hadithi hii, Sheikh Swadduq anasema: Mlango huo umeitwa Arrayan kwa sababu ya mashaka wanayoyapata wafungaji, kwani mashaka ya funga mara nyingi yanakuwa katika kiu, na wakati wafungaji watakapopita katika mlango huo watakunywa maji na kuondoa kiu na kuwafanya wasipatwe na kiu milele.” Ama faida za kijamii zitokanazo na Saumu ziko wazi kwa kila mtu, kwani Saumu inatupa mafunzo ya usawa baina ya wanajamii, wenyenacho wanahisi yale mashaka wanayoyapata wasionacho miongoni mwa mafukara, kutokana na yale wanayoyahisi katika Swaumu, kama vile njaa na kiu, kwa hivyo inakuwa ni rahisi kwa matajiri kujua hali wanayokumbana nayo masikini katika maisha yao, kwa hivyo inakuwa ni rahisi kwao kuweza kuwasaidia. Inawezekana matajiri wakahisi mashaka na uzito walionao mafakiri kwa njia ya mawaidha, lakini ikiwa matajiri hao watahisi kivitendo kwa kupitia ibada ya funga,watakuwa wepesi zaidi kuathirika na kupata hisia za matatizo yanayowakabili masikini pamoja na mafukara kwa muda mrefu katika maisha yao. Kutokana na hisia hizi wanazozihisi wafungaji katika jamii, Imam Sadiq (a.s.) anaelezea hekima ya kufaradhishwa ibada ya Swaumu baada ya kuulizwa suala linalohusiana na jambo hilo, alisema:
ّ وذلك,الغني والفقير إن الصيام ليستوي به ّ إنّما فرض اهلل ّ ّ و,مس الجوع فيرحم الفقير الغنى إن ّ الغنى لم يكن ليجد ّ ّ كلّما أراد شيئا قدر عليه فأراد اهلل تعالى أن يستوي بين خلقه 12 13
Imamu Ali (a.s), Nahjul Balaghah Jz. 4,Uk.55 Al-Hindiy,Kanzul-Ummal Jz. 8,Hadith Na.23648 37
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 37
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
ّ مس الجوع واأللم ّ ليرق على الضعيف وأن يذيق ّ الغنى ليجد ّ .ويرحم الجائع “Hakika Mwenyezi Mungu amefaradhisha Funga, ili tajiri alingane na masikini, kwani tajiri hawi ni mwenye kuhisi njaa na kuweza kumsaidia fakiri, kwa vile tajiri kila anapotaka kitu hukipata kwa urahisi, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akataka kuwaweka waja wake katika hali ya usawa, ili tajiri ahisi njaa na kuonja maumivu, ili iwe sababu kwake kuweza kumsaidia mnyonge na kumhurumia mwenye njaa.”14
Unaonaje lau kama nchi tajiri zikaamua kufunga baadhi ya siku katika mwaka na kuonja machungu ya njaa, je unadhani ya kwamba kungebakia mtu mwenye kushinda na njaa katika ulimwengu? Athari nzuri za Kiafya Zitokanazo na Swaumu: Kuna faida kubwa za kiafya zilizogunduliwa na wataalamu wa tiba wa zamani na wasasa kutokana na umuhimu wa mtu kujizuia kula chakula. Tafiti mbalimbali za kiafya haziachi kulizungumzia suala hili, kwani sababu za magonjwa mbali mbali husababishwa na kupupia kula vyakula vya aina mbali mbali, chakula kilichozidi katika mwili hujikusanya na kusababisha ongezeko la mafuta mwilini, na mafuta hayo pamoja na sukari huingia katika damu, ongezeko hili la vitu katika mwili huwa ni sababu ya uzalikanaji wa bektiria kwa wingi na kusababisha magonjwa kadha wakadha, katika hali hii njia pekee ya kuepukana na matatizo hayo ni kujizuia kula, ili tumbo lisiwe ni kama jaa la vitu visivyohitajika. Swaumu ndio kitu pekee kinacholiteketeza jaa lililokusanyika tumboni, kwa hakika Swaumu ni kitoharisho kamili cha kiwiliwili cha mwanadamu, pamoja na hayo ni huifanya sehemu ya usagaji wa chakula kuwa katika hali ya mapumziko mazuri na usafi wa hali ya juu, mapunziko haya ni muhimu mno, hupatikana kupitia njia hii ya Swaumu, baada ya kufanya kazi nzito kwa muda mrefu katika mwaka. Ili kulifikia lengo hili la kiafya ni jambo muhimu kwa mfungaji asifanye israfu na ulaji chakula kupita kiasi wakati wa kufutari, na pia wakati wa kula daku, kama mafunzo ya Uislamu yanavyotwambia, kinyume chake ni kwamba matokeo yatakuwa ni kinyume kabisa na yalivyokusudiwa. Mtaalamu mmoja wa Kirusi ajulikanae kama Alex Sufurin anasema: “Funga ni njia yenye tija katika kutibu maradhi ya ukosefu wa damu na udhaifu wa machango, 14
Rishahriy, Mizanul Hikma Jz. 2,Uk.168 38
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 38
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
na pia magonjwa ya muda mfupi na yale ya muda mrefu, mivimbe ya ndani na ya nje, kifua kikuu, ugonjwa wa ngozi, maradhi ya macho, ugonjwa wa sukari, ugonjwa wa mapafu, ini na maradhi mengine mbali mbali.”15 Tiba itokanayo na Saumu si tu katika magonjwa haya yaliyotajwa, bali pia inatibu magojwa yote yanayomkumba mwanadamu, kama vile saratani na tauni. Imepokewa kutoka kwa Mtume s.a.w. akisema:
تصحوا صوموا ّ Fungeni ili mpate siha.16
Na amesema tena:
ّ كل داء والحميّة رأس ّ المعدة بيت .كل دواء “Tumbo ni nyumba ya kila ugonjwa na kujizuia kula ni dawa iliyo bora zaidi.”17
Swaumu ya Umma Zilizotangulia: Katika maandiko ya Biblia yanaonesha wazi kwamba ibada ya Swaumu ilikuwepo kwa Mayahudi na Manasara, na pia inaonesha ya kwamba baadhi ya umma walikuwa wakifunga pindi wanapofikwa na misiba na majanga mbalimbali, imeandikwa katika kamusi ya Biblia ya kwamba: Swaumu kwa ujumla na kwa wakati wote ilikuwepo wakati wa huzuni, na ilikuwa ni jambo lililokuwa likitendwa na watu wa imani na madhehebu mbali mbali.18 Inadhihiri wazi kwamba Musa (a.s.) alikuwa akifunga siku arobaini, kama ilivyoandikwa: “Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano BWANA alilofanya nanyi ndipo nikakaa kule mlimani siku arobaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji”19 Na Mayahudi walikuwa wakifunga kwa ajili ya kutubia na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Mara nyingi Mayahudi walikuwa wakifunga pale walipokuwa Shiraziy,Tafsirul-Amthal Jz. 1, Uk. 524, amenukuu kutoka kitabu ‘Aswumu Twariqun Haditha Li-ilajil-Amradh. Al-Majlisiy, Biharul Anwar Jz. 96, Uk. 255 17 Kitabu kilichotangulia Jz. 59, Uk. 291 18 Kamusi ya Biblia, Uk. 427 19 Kumbukumbu la Torati, 9:9 15 16
39
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 39
12/8/2014 2:43:35 PM
WITO KWA WAUMINI
wakipata fursa, ili kuonesha udhaifu wao na unyenyekevu wao kwa Mwenyezi Mungu, na kukiri makosa yao kwa njia ya Swaumu na toba, ili wapate kuridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.20 “Swaumu kubwa pamoja na kafara ilikuwepo katika siku maalumu katika siku za mwaka miongoni mwa makundi ya Kiyahudi, na bila ya shaka kulikuwepo siku maalumu za kufunga kwa lengo la kukumbuka uvunjwaji wa mji wa Jerusalem na miji mingine”21 Vile vle Nabii Issa (a.s.) alifunga siku arobaini kama ilivyonakiliwa katika kitabu cha Injili: “Kisha Yesu alipopandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.”22 Pia inadhihirika ya kwamba wanafunzi wa Nabii Issa (a.s.) nao walikuwa wakifunga, kama maandishi yanavyosema: “Nao wakamwambia, wanafunzi wa Yohana hufunga mara nyingi na kuomba dua, na kadhalika wanafunzi wa Mafarisayo, lakini wanafunzi wako hula na kunywa! Lakini Yesu akawaambia, Je! Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa harusini? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana harusi, ndipo watakapofunga siku zile.”23 Katika kamusi ya Biblia kuna maandishi yafuatayo: “Maisha ya wanafunzi wa Yesu na waumini yalikuwa yamezungukwa na kujiepusha mbali na starehe na kujipatisha tabu ya Saumu.”24 Hata baada ya kuchafuliwa maandiko ya vitabu vya dini vya kizamani, bado tunakuta ushahidi kutokana na yale yaliyoelezwa katika Qur’ani ya kwamba, pia wale waliokuwa kabla yetu nao walifaradhishiwa ibada ya Saumu.
Utukufu wa Mwezi wa Ramadhani: Mwezi wa Ramadhani ndio mwezi peke yake ulioteuliwa kufungwa kwa vile unatofautiana na miezi mingine. Qur’ani Tukufu imeelezea tofauti hii kwa kusema ya kwamba ni mwezi ambao ndani yake iliteremshwa Qur’ani, kwani Qur’ani ndio kiKamusi ya Biblia, Uk. 428 Kitabu kilichotangulia 22 Matayo,4:1-2 23 Luka, 5:33-35 24 Kamusi ya Bibilia,Uk.428 20 21
40
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 40
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
pambanuzi kati ya mtu mwema na mtu mbaya, na pia inatoa bishara ya furaha kwa kila mtu mwema. Katika Riwaya mbali mbali za Kiislamu zinaonesha ya kwamba vitabu kama vile Taurati, Injili, Zaburi, Assuhufi pamoja na Qur’ani vimeshushwa katika mwezi wa Ramadhani. Kwa hivyo mwezi huu ni mwezi wa mafunzo na malezi bora, na haya hayawezi kupatikana bila ya mafunzo sahihi, kwa hivyo ibada ya Saumu inapasa iende sanjari na mwamko sahihi na wa hali ya juu kwa mfungaji ili afikie lengo la kukitakasa kiwiliwili chake pamoja na roho yake dhidi ya dhambi. Ijumaa ya mwishoni mwa mwezi wa Shaabani Mtume (s.a.w.w.) aliwatolea hotuba Waislamu kwa lengo la kujitayarisha kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuelezea fadhila zake, alisema: “Enyi watu hakika umekukabilieni mwezi wa Mwenyezi Mungu, mwezi ulio na baraka, rehema na maghfira, mwezi ambao ni bora zaidi kuliko miezi mingine kwa Mwenyezi Mungu, na mchana wa siku zake ni mchana uliyobora zaidi, na usiku wa siku zake ni bora ya usiku, na saa zake ni bora ya masaa, huo ni mwezi ambao nyinyi mumeitwa katika ugeni wa Mwenyezi Mungu, na mumejaaliwa kuwa ni miongoni mwa watu watukufu kwa Mwenyezi Mungu, pumzi zenu ni tasbihi na usingizi wenu katika mwezi huo ni ibada, na vitendo vyenu katika mwezi huo ni vyenye kukubaliwa, na dua zenu katika mwezi huo ni zenye kukubaliwa, basi muombeni Mwenyezi Mungu Mlezi wenu kwa nia khalisi na kwa nyoyo safi ili akuwezesheni kuufunga mwezi huu na kukisoma Kitabu chake, kwani mtu muovu zaidi ni yule atakayenyimwa msamaha wa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu. Na njaa zenu na kiu zenu katika mwezi huu, ziwakumbusheni njaa na kiu ya Siku ya Kiyama, na toeni sadaka kwa kuwapa masikini wenu pamoja na mafukara wenu, na waheshimuni wakubwa zenu na warehemuni wadogo zenu, na waungeni jamaa zenu, na zihifadhini ndimi zenu, na inamisheni macho yenu kwa kutoyaangalia yale yaliyo haramu kwenu kuyaangalia na jizuieni kuyasikiliza yale ambayo si halali kwa masikio yenu kuyasikiliza, na wafanyieni upole mayatima wa watu wengine, kwa kufanya hivyo mayatima wenu nao watakuja kufanyiwa upole…. “25
25
Al-Hurrul Amiliy, Wasailu Shia Jz. 10, Uk. 312 41
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 41
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
Kanuni ya Kutotenzwa Nguvu: Katika uchambuzi wa Aya hizi tunakuta kanuni ambayo inaashiria ya kwamba Mwenyezi Mungu anawatakia watu wepesi na hawatakii uzito, kanuni hii imekuja baada ya kuelezwa maudhui yanayohusiana na ibada ya Funga na faida zake na hukumu ya msafiri na mgonjwa katika mwezi wa Ramadhani, lakini kanuni hii inatumika katika kila hukumu miongoni mwa hukumu za Kiislamu. – Kanuni hii inasema: Hukumu za Kiislamu hazisimami kwa lengo la kuwapatisha mashaka wanadamu, na kama hukumu itakuwa inamletea tabu na mashaka mwanadamu basi hukumu hiyo hatoitekeleza kwa muda ule mpaka hapo atakapokuwa katika hali yake ya kawaida, kutokana na kanuni hii ndio maana mtu anayedhuriwa na maji wakati wa kutia udhu anaruhusiwa kutayammam kwa kutumia mchanga, na yule asiyeweza kuswali kwa kusimama anaruhusiwa kuswali kwa kukaa. Na katika sehemu nyingine Mwenyezi Mungu amesema:
ُ اك ْم َو َما َج َع َل َعلَي ُ اج َت َب ِّ ْك ْم ِفي ين ِم ْن َح َر ٍج ْ ُه َو ِ الد
“Yeye ndiye aliye kuchagueni, na hakuwafanyieni uzito katika dini…” (Qur’ani al-Hajj: 78).
Na Mtume s.aw.w. anasema:
ّ بعثت على .السهله ّ السمحة ّ الشريعة “Nimeletwa kwa sheria ilio nyepesi na rahisi.” 26
Mwenyezi Mungu anaendelea kuwafunza waja Wake Waumini mambo ya kufanya katika maisha yao, na hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kama Aya inavyosema: “Na waja Wangu watakapokuuliza habari Yangu, Mimi niko karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba.”
SABABU YA KUTEREMKA: Mtu mmoja alimuuliza Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na Mwenyezi Mungu: “Je, Yuko karibu ili tumnong’oneze kwa sauti ya chini, au yuko mbali tumwite kwa sauti kubwa?” Hapo ikateremka Aya hii. Baada ya Aya zilizopita kuelezea hukumu 26
Al-Burujurdiy, Al-Qawaidul Fiqihiyya, Jz. 1, Uk. 252 42
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 42
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
mbalimbali za Kiislamu, ama Aya hii inaelezea maudhui ya dua, ikizingatiwa ya kwamba ni njia ya mafungamano makubwa kati ya mja na Mola Wake. Aya hii kuwepo katikati ya Aya zinazoelezea ibada ya funga, inatoa taswira ya kwamba dua ni roho ya kila ibada. Waja Wangu watakuuliza kuhusiana Nami, basi waambie ya kwamba Mimi niko karibu mno kuliko wanavyodhani wao, bali niko karibu kuliko hata mishipa yao ya shingo. Mwenyezi Mungu ameeleza wazi ya kwamba Yeye ni Mwenye kuitikia na kukubali maombi ya waombaji pindi wanapomuomba, lakini kwa sharti kwanza hao waombaji wakubali kutekeleza matakwa yake na kumuamini Yeye kikwelikweli: “Basi nawaniitikie Mimi na waniamini Mimi ili wapate kuongoka.” Jambo la kuzingatia hapa ni kuona ya kwamba Mwenyezi Mungu ameashiria Nafsi Yake takatifu mara saba na pia kuwaashiria waja Wake mara saba, huku ni kuonesha namna alivyo na ukuruba,usuhuba na mafungamano ya hali ya juu na waja Wake. Imepokewa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s.) akisema:
فأكثر من ال ّدعاء فإنّه,ال ّدعاء ير ّد القضاء بعد ما أبرم إبراما ّ كل رحمة ونجاح ّ مفتاح ّ كل حاجة وال ينال ما عند اهلل عز ّ ّ وجل وإنّه ليس باب يكثر قرعه إال أن يوشك أن,إال بال ّدعاء .يفتح لصاحبه “Dua inazuia jambo lililopangwa kutokea, baada ya kupitishwa, basi kithirisheni kuomba dua, kwani ni ufunguo wa kila rehema na mafanikio ya kila shida, na wala hayapatikani yale yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu pasi na kuomba dua, na hakuna mlango unaogongwa sana na kufunguliwa huyo mwenye kuugonga kama ilivyo kwa kuomba dua.” 27
Bila ya shaka yoyote, Mwenyezi Mungu yuko karibu sana na waja, na ni vipi isiwe hivyo kwani Yeye huingia kati ya mtu na moyo wake. (Qur’ani 8:24). Ni wazi kwamba tangu kuanza harakati za kulingania Uislamu tokea enzi ya Nabii Adamu (a.s.) mpaka hivi sasa, maadui wa haki waliweza kukabiliana na harakati hizo kwa nguvu zao zote, na huku kukiwa na uhaba wa silaha kwa walinganiaji pamoja na wafuasi wao, njia pekee waliyoielekea ni kumuomba nusra Mwenyezi Mungu baada ya kujitayarisha kwa hicho kichache walichokuwa nacho, kwa kufanya hivyo, 27
Ash-Shahrudiy, Mustadrak Safinatul Bihar Jz. 3, Uk. 284 43
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 43
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
Mwenyezi Mungu aliweza kuwapa ushindi uliowashangaza maadui, siri kubwa ya ushindi huo ni dua, Mtume (s.a.w.w.) anasema:
.ال ّدعاء سالح المؤمن “Dua ni silaha ya Muumini.” 28
Masharti Ya Kukubaliwa Kwa Dua: Kila ibada inataratibu zake na namna ya kuitekeleza ili kufikia lengo, kwa upande wa ibada hii ya dua, kuna masharti yafuatayo: 1.
Ni juu ya muombaji kabla ya kuanza kuomba, aisafishe nafsi yake na kuutakasa moyo wake, na pia atubie kutokana na madhambi, huku akiwa ni mwenye kujipamba na tabia za Mawalii wa Mwenyezi Mungu, imepokewa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s.) akisema:
,إيّاكم أن يسأل أحدكم ربّه شيئا من حوائج ال ّدنيا واآلخرة بي ّ حتّى يبدأ بالثّناء على اهلل والمدحة له ّ ّوالصالة على الن ّ وآله واإلعتراف بالذنب ث ّم المسألة “Tahadharini! Mmoja wenu asimuombe Mola Wake jambo miongoni mwa haja za dunia na Akhera, mpaka pale atakapoanza kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumsifu, na kumswalia Mtume pamoja na jamaa zake, na kuungama madhambi yake, baada ya hapo ndipo aombe.”29
2.
Muombaji aharakishe kuitoharisha mali yake dhidi ya dhulma na unyang’anyi, na wala isiwe matumizi yake yanatokana na chumo la haramu. Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:
ّ من .أحب ان يستجاب دعاؤه فليطب مطعمه ومكسبه “Ambaye anapenda dua yake ikubaliwe, basi akifanye kizuri chakula chake (ale chakula halali) na chumo lake.”30 Al-Haythamiy, Majma’u Zawa’id, Jz. 1, Uk. 147 Al-Majlisiy, Biharul Anwar, Jz. 90, Uk. 314 30 Kitabu kilichotangulia, Uk.372 28 29
44
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 44
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
3.
Maombi yake yasiachane na uwajibikaji wenye kuendelea wa sheria za Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu haikubali dua ya mwenye kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu, kama Mtume (s.a.w.w.) anavyosema:
ّ ّ أوليسل,ولتنهن عن المنك ّ ّ طن اهلل شراركم لتأمرن بالمعروف .على خياركم فيدعوا خياركم فال يستجاب لهم “Mtaamrisha mema na kukataza mabaya, msipofanya hivyo, Mwenyezi Mungu atakusalitishieni (atakutawalisheni) waovu wenu juu ya wema wenu, kisha wema wenu waombe dua, na wasikubaliwe.”31
Kutokana na kuacha kuchunga na kutekeleza yaliyo wajibu, kunatoa fursa kwa mafisadi na madikteta kushika hatamu za uongozi katika jamii. Leo waziri mkuu wa Uingereza ametamka kwa kinywa kipana kwamba wale viongozi wanaotaka msaada kutoka kwake, wawe tayari kuwapa uhuru wale wanaotaka kufunga ndoa za watu wa jinsia moja, kutokana na viongozi waovu walioko katika mataifa mbalimbali bila ya shaka yoyote wataridhia hayo na kuyatekeleza! Hii ndio natija ya Waumini kupuuzia mafunzo sahihi na adhimu ya Dini yao! 4.
Kutekeleza ahadi zote za Mwenyezi Mungu alizozichukua Muumini kwa kutenda mema na kujiepusha na maovu, kwani asiyetekeleza ahadi zake mbele ya Mwenyezi Mungu asitarajie kukubaliwa dua yake. Kuna mtu mmoja alimwendea Imamu (a.s.) na huku akilalamika ya kwamba dua yake haikubaliwi, Imamu Ali (a.s.) alisema: “Hakika nyoyo zenu zimeyafanyia khiyana mambo nane: Kwanza: Nyinyi mmemtambua Mwenyezi Mungu, lakini hamkutekeleza wajibu wake kama alivyokuamrisheni, kwa hivyo utambuzi wenu huo haukuwasaidia chochote! Pili: Nyinyi mmemuamini Mtume Wake, kisha mmekhalifu mwenendo wake, na mmeamini sheria zake, iko wapi faida ya imani yenu? Tatu: Nyinyi mmekisoma Kitabu chake alichokuteremshieni (Qur’ani), lakini hamkukifanyia kazi, na mlisema: “Tumesikia na tumetii.” Kisha mkakikhalifu.
31
Al-Haythamiy, Majma’u Zawa’id, Jz.7,Uk. 266 45
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 45
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
Nne: Nyinyi mlisema ya kwamba mnauogopa Moto, na hali nyinyi kila wakati mnaukabili kwa maasi yenu, basi iko wapi hiyo khofu yenu? Tano: Nyinyi mlisema ya kwamba mnaipenda Pepo, na nyinyi kila wakati mnatenda yale yanayokuwekeni mbali nayo, basi yako wapi hayo mapenzi yenu? Sita: Nyinyi mmekula neema za Mwenyezi Mungu, lakini hamzishukuru! Saba: Hakika Mwenyezi Mungu amekuamrisheni kumfanyia uadui shetani, basi mmemfanyia uadui kwa kauli, na mmemfuata basi na kuwa na khofu. Nane: Nyinyi mmeziweka aibu za watu mbele ya macho yenu na aibu zenu mmeziweka nyuma ya migongo yenu, mnawalaumu wale ambao nyinyi ndio mnaostahiki zaidi kulaumiwa, ni dua gani itakayokubaliwa kwa mwenye mambo haya, na wakati mmeifunga milango yake na njia zake?! Basi mcheni Mwenyezi Mungu na vifanyeni vizuri vitendo vyenu, na kuweni watu wema pale mnapokuwa katika faragha, na amrisheni mema na katazeni maovu, hapo Mwenyezi Mungu atawakubalia dua zenu.32 Maneno haya ya Imamu Ali (a.s.) yanatueleza ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu kuwakubalia waja Wake maombi yao ni ahadi iliyo na masharti, na pindi mja atakapojilazimisha na kuyatekeleza masharti haya aliyoyataja, basi awe na yakini ya kukubaliwa dua yake. 5.
Baada ya mtu kuomba dua asibweteke, bali afanye kila juhudi kwa kuchukua hatua zote zinazopelekea kufikia matakwa yake. Imamu Ali (a.s.) anasema:
.كالرامي بال وتر ّ ال ّداعي بال عمل “Mwenye kuomba dua, pasi na kufanya harakati, ni kama mtupaji mshale bila ya kuwa na upinde.”33
Katika uombaji dua na kutarajia majibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kunapasa kutegemea hali ya kimaumbile na mazingira yanayomzunguka mwanadamu, kwa maneno mengine, inampasa muombaji kujitayarisha, kwa kuhakikisha ya kwamba masharti haya anayatimiza. Aya ya mwisho miongoni mwa Aya hizi inasema: 32 33
Al-Majlisiy,Biharul Anwar,Jz.90,Uk. 376 Imamu Ali (a.s.),Nahjul Balaghah,Jz. 4,Uk. 79 46
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 46
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
َ َأُ ِح َّل لَ ُك ْم لَيْل اس لَ ُك ْم َوأَ ْنتُ ْم ي الص ة َّ ام ٌ الر َف ُث إِلَىٰ ِن َسا ِئ ُك ْم ُه َّن لَِب ِّ َ ِ َ َُّلله َ ُ ُ ُ ُ َ ُ َّ اس لَه َ ُُن َعلِ َم ا أنَّك ْم ك ْنتُ ْم َت ْخ َتان اب َعليْك ْم ٌ لَِب َ ون أ ْنف َسك ْم َف َت ُ اش ُر وه َّن َوا ْب َت ُغوا َما َك َت َب اللهَُّ لَ ُك ْم َو ُكلُوا ِ َو َع َفا َع ْن ُك ْم َفالآْ َن َب َ ْْط أ َ ْْط أ ُ َّن لَ ُك ُم ْال َخي ْ َو ُ ال ْب َي َ اش َربُوا َحتَّىٰ َي َت َبي ال ْس َو ِد ِم َن ِ ض ِم َن ْال َخي َّ ُ اش ُر َ وه َّن َوأَ ْنتُ ْم َعا ِك ُف ون ِّ ْال َف ْج ِر ثُ َّم أَِت ُّموا ِ ْل َو اَل تُ َب ِ الص َيا َم إِلَى اللي ْ ُ ُوها َك َذٰلِ َك يُ َبي َ اج ِد ِت ْل َك ُح ُدو ُد اللهَِّ َف اَل َت ْق َرب ِّن اللهَُّ آ َيا ِت ِه ِ ِفي ال َم َس َ اس لَ َعلَّ ُه ْم َيتَّ ُق ون ِ َّلِلن “Mmehalalishwa usiku wa saumu kuwaingilia wake zenu. Wao ni vazi lenu na nyinyi ni vazi lao. Mwenyezi Mungu anajua kuwa mlikuwa mkizihini nafsi zenu, kwa hivyo amewatakabalia toba yenu na amewasamehe. Basi sasa ingilianeni nao na takeni aliyowaandikia Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainikie weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Na wala msiingiliane nao na hali mko katika itikafu misikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikaribie. Namna hii Mwenyezi Mungu anabainisha ishara Zake kwa watu ili wapate kuwa na takua.” Surat Al Baqarah 2:187
SABABU YA KUTEREMKA: Imepokewa ya kwamba, ilikuwa ni haramu katika mwezi wa Ramadhani kwa mfungaji kula chakula ikiwa atalala, na pia ilikuwa ni haramu kukutana kimwili kwa wanandoa. Kulikuwa na mtu mmoja miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa akiitwa Mat’am ibn Jubeir, mtu huyo alikuwa mzee aliye dhaifu huku akiwa amefunga, siku moja watu wake walichelewa kutayarisha chakula, basi akachukuliwa na usingizi kabla ya kufutari, aliposhituka, aliwaambia watu wake wa nyumbani: Ni haramu kwangu kula katika usiku huu. Siku ya pili alishiriki katika uchimbaji wa handaki, alizimia, Mtume (s.a.w.w.) alimuhurumia sana. Na ilikuwa baadhi ya vijana walikuwa wakikutana na wake zao katika usiku wa mwezi wa Ramadhani kwa siri, hapo Mwenyezi Mungu aliiteremsha Aya hii ili kuhalalisha kukutana kimwili katika usiku wa mwezi wa Ramadhani, pia kutoa ruhusa ya kula mpaka kufikia alfajiri, hata kama mtu atalala kabla ya kufutari.34 34
Tabarasiy, Majma’ul Bayan, Jz.2, Uk.21 47
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 47
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO: Huenda hukumu ya kuzuiliwa kukutana kimwili kwa wanandoa wakati wa usiku wa mwezi wa Ramadhani pamoja na mchana wake, pia kula kwa mwenye kulala usiku, ilikuwa ni mtihani kwa Waislamu wa mwanzo na kuwaandaa katika kuzipokea hukumu za ibada ya Funga pale zitakapokuwa thabiti. Aya hii Tukufu imebeba hukumu nne zinazohusiana na ibada ya Funga pamoja na Itikafu. Kwa kuanzia inasema: “Mmehalalishwa usiku wa saumu kuwaingilia wake zenu..” Kisha Aya inaeleza sababu ya ruhusa hii kwa kusema: “Wao ni vazi lenu na nyinyi ni vazi lao.” Kazi kubwa za nguo ni kuuhifadhi mwili dhidi ya joto na baridi na kusitiri siri za mwili, na zaidi ya hayo ni kwamba nguo ni pambo kwa mwanadamu, na huku wanandoa kushabihishwa na nguo ni kwa sababu kwamba wao wanabeba mambo haya. Nafasi hizi walizonazo wanandoa ni kielelezo cha wazi juu ya mafungamano ya kiroho yaliyopo kati yao, na kuwa katika daraja moja katika jambo hili. Baada ya hapo Aya inaeleza sababu ya kuwekwa hukumu hii: “Mwenyezi Mungu anajua kuwa mlikuwa mkizihini nafsi zenu, kwa hivyo amewatakabalia toba yenu na amewasamehe. Basi sasa ingilianeni nao na takeni aliyowaandikia Mwenyezi Mungu.” Bila ya shaka ruhusa hii iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, ili kuwalinda waja wake dhidi ya kuingia katika madhambi, haina maana kufanya hivyo (kujamiiana) ni wajibu, bali ni ruhusa kwa anayependa kufanya hivyo, baada ya jambo hili kuwa ni lenye kuzuiliwa, ili watu waendelee katika kutafuta kizazi. KishaAya inabainisha hukumu ya pili kwa kusema: “Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainikie weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku.” Kwa hivyo mfungaji anaruhusa ya kula na kunywa mpaka pale itakapochomoza alfajiri. Hukumu ya tatu inabainishwa na Aya kama ifuatavyo: “Kisha timizeni Saumu mpaka usiku.” Ibara hii ya Aya inaashiria uharamu wa kula, kunywa na kujamiiana kwa mfungaji wakati wa mchana wa mwezi wa Ramadhani, na ruhusa ya kufanya hayo imetolewa kuanzia wakati unapoingia usiku mpaka inapochomoza alfajiri. Ama hukumu ya nne ni ile isemayo: “Na wala msiingiliane nao na hali mko katika itikafu misikitini.” Hukumu hii inahusiana na yule aliyeamua kukaa msikitini kwa ajili ya ibada ya Itikafu, Itikafu ambayo muda wake haupunguwi siku tatu, kwa hivyo mwenye kukaa itikafu mfungaji si haki kwake kujamiiana na mke wake wakati wa mchana na usiku. Kwa kumalizia Aya inataja wajibu wa Mwislamu juu ya hukumu zote zilizotangulia kutajwa: “Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikaribie.”
48
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 48
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwani kuikaribia mipaka ya Mwenyezi Mungu ni kuleta wasiwasi katika nafsi ya mwenye kufanya hivyo, na kushawishika kutenda yale yaliyoharamu, kwa minajili hiyo, ndio Mwenyezi Mungu akachukua jukumu la kuwafahamisha waja Wake yale yaliyo na maslahi nao: “Namna hii Mwenyezi Mungu anabainisha ishara Zake kwa watu ili wapate kuwa na takua.’
UTAFITI: 1.
Mipaka Ya Mwenyezi Mungu:
Baada ya Aya kueleza baadhi ya hukumu za ibada ya Funga na Itikafu, imeweka bayana ya kwamba hukumu hizi ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, mipaka inayobainisha kati ya halali na haramu, kati ya kile kinachoruhusiwa kufanywa na kile kilichozuiwa, na kwa uzuri na ufasaha, Aya haikusema msiivuke mipaka hii, bali imesema: “…basi msiikaribie.” Kwa hivyo Uislamu umekataza kukaa katika sehemu ambazo humsababishia mtu kushawishika kufanya maovu, kama vile sehemu zinazouzwa ulevi au kuchanganyika kati ya wanaume na wanawake wanaoweza kuowana. Makatazo hayo yamepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) chini ya anuani ya ‘Kulinda Mipaka.’ Mtume (s.a.w.w.) amesema:
ّ . فمن يرتع حول الحمى يوشك أن يقع فيه,إن حمى اهلل محارمه “Hakika mipaka ya Mwenyezi Mungu ni yale aliyoyaharamisha, basi mwenye kukaribia katika mipaka, hukaribia kutumbukia humo (katika uharamu).”35
Kwa hivyo wale wanaomcha Mwenyezi Mungu kikwelikweli, si tu kwamba hujiepusha na kufanya mambo maovu, bali hujiepusha na kila jambo linalosababisha kutenda uovu. 2.
Ibada Ya Itikafu:
Itikafu ni hali ya mtu kuamua kukaa msikitini kwa muda usiopungua siku tatu kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu. Ibada hii ina athari nzuri katika kuilea nafsi wa Mwislamu kwani ni miongoni mwa ibada zinazomuweka mja karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. Licha ya ibada hii kuwa ni Sunna, lakini kuna hali ambayo inakuwa ni wajibu kujizuilia dhidi ya mambo fulani, miongoni mwa hayo ni kukutana kimwili kati ya mke na mume wakati wa mchana na usiku. Maelezo zaidi yanayohusiana na ibada hii yameelezwa katika vitabu vya fiqhi. 35
Al-Hurrul Amil, Wasailu Shia, Jz. 18, Uk. 122 49
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 49
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ات ِّ ين آ َمنُوا ا ْد ُخلُوا ِفي ِ الس ْل ِم َك َّاف ًة َو اَل َتتَّ ِبعُوا ُخ ُط َو َ َّ ٌ ان إِنَّ ُه لَ ُك ْم َع ُد ٌّو ُم ِب ين َفإِ ْن َزلَْلتُ ْم ِم ْن َب ْع ِد َما َجا َء ْت ُك ُم ِ الشيْط ْ َ ات ٌ اعلَ ُموا أَ َّن اللهََّ َعز ُ َ ْ ِّ يز َح ِكي ٌم ف ن ي ب ال َ ِ “Enyi mlioamini! Ingieni katika usalama nyote, wala msifuate nyayo za Shetani. Kwa hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi. Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu, basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” (Qur’ani 2:208-209).
MAELEZO: Aya inawataka Waumini kuingia katika suluhu na amani kwa kuwaambia: “Enyi mlioamini! Ingieni katika usalama nyote.” Neno ‘Silm’ katika lugha ya Kiarabu lina maana ya suluhu,amani na utulivu, na baadhi wamepita wakionesha ya kwamba lina maana ya utiifu. Kwa hivyo Aya hii inawaita Waumini wote katika suluhu, amani na kusalimu amri zote za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Aya hii pia inatufahamisha ya kwamba amani ya kweli na utulivu haviwezi kupatikana isipokuwa katika kivuli cha Uislamu, na mifumo ya kilimwengu iliyopo hivi leo katu haina uwezo wa kuuzima moto wa vita katika ardhi hii, kwani mfumo wa kimaada na wenye kushikamana nao ndio chanzo cha mizozo na matatizo, inawezekena hapa tukasema ya kwamba wito wa Aya hii kwa Waumini wote bila ya kuangalia matabaka yao, lugha zao, rangi zao utaifa wao, utajiri wao, wa kutakiwa kuingia katika suluhu na amani ni dalili tosha ya uwezekano wa kuundwa dola moja ya Kiislamu iliyo na uwezo wa kuongoza ulimwengu mzima. Na leo ni jambo lililo wazi kwamba tofauti ya lugha, utaifa, rangi na mengineyo yamekuwa ni sababu ya ubaguzi kati ya watu, kwa hivyo kuna haja kubwa ya kuwepo kitu kitakachounganisha nyoyo za watu, kitu hicho si chochote isipokuwa imani thabiti juu ya Mwenyezi Mungu, hilo ndilo jambo peke yake litakalowaweka watu pamoja na kuwakinga na mitafaruku, na pia kufuata maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu ni jambo linalowaunganisha wananchi na kuwa ni jamii iliyoshikana na taifa madhubuti, 50
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 50
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
kwa mfano ulio wazi ni suala zima la ibada ya Hijja, ibada hii huwakutanisha Waislamu wa mataifa mbalimbali wenye kutofautiana lugha, rangi na mengineyo, wote kwa pamoja hukutana katika ibada moja ya kiroho huku wakisafiana nia na kila mmoja kumuombea mwenzake kheri na mafanikio katika maisha na malipo bora ya akhera. Tukilinganisha na namna ya siasa ya kilimwengu ilivyo hivi sasa tunaona kwamba watu wanakosa moyo wa mapenzi, wanakosa kuhurumiana kati yao, wanakosa amani na utulivu ndani ya nchi zao, wanakhofia usalama wa mali zao na watoto wao, hii ni tofauti kubwa kati ya jamii iliyoshikamana na imani na yakini juu ya Mwenyezi Mungu na ile iliyoko mbali na haya. Pia Aya hii inatuashiria ya kwamba baadhi ya Mayahudi walikuwa wakiingia katika Uislamu huku wakiwa bado wanafuata baadhi ya mila za dini yao ya zamani, kwa hivyo Mwenyezi Mungu aliwataka waachane na mila hizo, na badala yake wafuate mafunzo ya Uislamu kwa ukamilifu na wanyenyekee na kusalimu amri kwa kila hukumu iliyomo katika Uislamu. Baada ya hapo Aya inatukataza kufuata nyayo za shetani: “Wala msifuate nyayo za Shetani. Kwa hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.” Sehemu hii ya Aya inatuashiria ya kwamba mara nyingi upotofu na wasiwasi wa shetani huanza kidogo kidogo tena kwa hatua baada ya hatua, ndio maana Qur’ani ikaitambua hali hiyo kama ni ‘hatua za shetani’. Ukweli wa maana hii unaonesha wazi kwamba kuwa mbali na suluhu, amani na utulivu, natija yake ni mtu kusalimu amri mbele ya maadui wa Uislamu na kumpelekea kuwafanyia watu uadui na kumwaga damu zao, haya yote huanzia kutoka katika hatua moja na kuingia katika hatua nyingine na mwishowe mtu huyo huwa sugu na mzoefu wa kufikia katika kiwango cha kutisha na cha hatari, kama ilivyo katika methali isemayo: ‘Mwanzo wa vita ni maneno’. Hata baadhi ya wakati cheche ya vita na maangamizi huanza na maudhi madogomadogo, lakini cheche hiyo hukua na kuzidi na hatimaye huiangamiza jamii kutokana na vita na mapambano ya silaha, kwa hivyo Mwenyezi Mungu ameliona hilo, ndio maana akawaita Waumini wajiepushe na kila aina ya maudhi ili isije ikawa ni chachu na sababu ya kuwaka moto ambao hautazimika kwa urahisi. Aina hii ya ibara: “Wala msifuate nyayo za Shetani. Kwa hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.” Imekuja mara tano katika Qur’ani Tukufu ikiwa na lengo na madhumuni mbali mbali. Baadhi ya wafasiri wanasema ya kwamba: Abdullah bin Salaam pamoja na wafuasi wake waliokuwa katika dini ya Kiyahudi, baada ya kusilimu walimuomba Mtume (s.a.w.w.) awaruhusu kusoma Taurati katika Swala zao na kutenda baadhi
51
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 51
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
ya hukumu zilizomo humo, ndipo Aya hii ikateremka na kuwakataza kufuata nyayo za shetani. Kutokana na sababu hii ya uteremkaji wa Aya hii ni ishara ya wazi ya kwamba shetani hupenya katika fikra ya mwanadamu na moyo wake hatua baada ya hatua na kumshawishi kuanza kufanya maasi madogo na mepesi ili iwe ni sababu na utangulizi wa kufanya maasi makubwa. Na pale Mwenyezi Mungu aliposema ya kwamba: “Kwa hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.” ni ishara ya kwamba uadui wa shetani kwa mwanadamu si jambo lililojificha, kwani uadui huo umeanza tangu kuumbwa kwa Nabii Adam (a.s.) na aliapa kuwapoteza wanadamu wote ila wale waliotakaswa kwani wao ndio peke yao ambao hawatafikwa na vitimbi vya shetani. Basi ni vipi Mwislamu anaghafilika na vitimbi vya shetani! Aya inayofuatia inawaonya Waumini wote kwa kusema: “Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu, basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” Inawawekea bayana waumini kwa kuwaambia ikiwa watateleza kwa kufuata vitimbi na wasiwasi wa shetani kwa kukhalifu utaratibu wa suluhu na amani ya kweli, hiyo haitowafanya kukimbia hukumu ya uadilifu ya Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka njia na utaratibu wa kufuata ni katika mambo yaliyoko wazi, kwa hivyo hakuna udhuru kwa yule anayekengeuka njia ya haki na ya kweli, na hasara kubwa itakuwa ni kwa kila anayekwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu, na tambueni ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza na hakuna yeyote anayeweza kuikimbia hukumu ya uadilifu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
52
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 52
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABA
َ ُ ْ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ْل أَ ْن َي ْأ ِت َي َي ْو ٌم اَل ِ ين آ َمنُوا أ ْن ِف ُقوا ِم َّما َر َزق َناك ْم ِم ْن َقب َّ ون ُه ُم َ الظالِ ُم َ اع ٌة َو ْال َكا ِف ُر ون َ َب ْي ٌع ِفي ِه َو اَل ُخلَّ ٌة َو اَل َش َف “Enyi mlioamini! Toeni katika vile tulivyowapa. Kabla haijafika siku ambayo hapatakuwa na biashara wala urafiki wala shufaa. Na makafiri ndio madhalimu.” (Qur’ani 2:254).
MAELEZO: Miongoni mwa mambo ya wajibu kwa Waumini ni kuunda jamii yenye mapenzi na mafungamano kati yao na kuwafanya kuwa wamoja, miongoni mwa mambo yanayosaidia katika kulifikia jambo hilo ni kwa wale walio na uwezo kuwasaidia wasiokuwa na uwezo. Pale Mwenyezi Mungu aliposema: “Toeni katika vile tulivyowapa” Ni kwamba maneno haya yana maana pana sana, kwani inahusisha utoaji ulio wajibu na ule usio wa wajibu (mustahabbu), pia inahusisha utoaji wa kimaana kama vile elimu na mfano wake, lakini kutokana na msisitizo na ukali wa maneno inaonesha wazi kuwa utoaji uliokusudiwa katika Aya hii ni utoaji wa wajibu kama vile Zaka, Khumsi n.k. Utoaji wa mali iliyo wajibu ndio jambo linaloimarisha benki ya Kiislamu na kuifanya serikali kuwa na uwezo wa kuwahudumikia raia wake kwa ufanisi. Katika suala la utoaji Uislamu unamtaka kila mwenye uwezo wa kufanya hivyo kutoa kiasi cha mali yake na sio mali yote, ndio Mwenyezi Mungu akatumia neno ‘Mimmaa’ ikimaanisha sehemu ya mali. Sheikh Tabrasiy katika tafsiri yake Majmaul Bayan anasema ya kwamba: “Aya hii inajumuisha utoaji wa wajibu na ule usio na wajibu, na vitisho vilivyomo katika Aya sio vitisho bali ni habari tu zinazoelezea hali itakavyokuwa Siku ya Kiyama.”36 Lakini kutokana na mazingatio tunayoyapata katika Aya, inaonesha yakwamba kutokutoa mali kwa mwenye uwezo wa kufanya hivyo ni moja kati ya aina za ukafiri na dhulma, na hali hii haitokei isipokuwa kwa kutokutoa mali ya wajibu. Aya inaendelea kueleza ya kwamba ni juu ya Waumini kuharakisha kutoa pale tu wanapokuwa na uwezo, kwani maisha ya akhera ni pahala pa kuvuna kile kilichopandwa hapa 36
Shiraziy,Tafsirul Amthal, Jz. 2, Uk. 240 53
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 53
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
duniani, kwani huko hakutakuwa na fursa ya kuweza kufanya biashara yoyote itakayomuwezasha mtu kumpatia faida, na kutoa kwa kumpa mwingine kwa lengo la kujiepusha na adhabu na kupata furaha ya milele, na wala huu urafiki usiokuwa na mafungamano ya imani hautokuwa na faida yoyote huko akhera, kwani hata hao marafiki nao watasumbuka na kuhangaika huku na kule kutokana na natija ya matendo yao, na wala hawatakuwa na uwezo wa kuweza kuwatetea na kuwatakia shufaa (maombezi) watu wengine, kwani kwa kujizuia kwao kutoa mali iliyo wajibu kuitoa ndiko kutakakowapelekea kukosa maombezi ya wale watakaopewa ruhusa ya kuwaombea wengine. Na makafiri ndio madhalimu wakubwa kwa kule kujizuilia kwao kutoa, vitendo vyao hivi vya kibakhili ni sababu kubwa ya kuzidhulumu nafsi zao na pia kuwadhulumu wengine. Qur’ani Tukufu kwa kupitia Aya hii inataka kutubainishia mambo yafuatayo: Kwanza: Makafiri wanazidhulumu nafsi zao kwa kuacha kutoa mali iliyowajibu kwao na pia kuacha hukumu nyingine za Kiislamu, kutokana na upingaji wao huu wanazinyima nafsi zao furaha kubwa isio na kifani ya Siku ya Kiyama, matendo yao haya ndio yanayotia uzito migongo yao Siku ya Kiyama, kwa hivyo ni wao wenyewe waliojidhulumu na sio Mwenyezi Mungu. Pili: Makafiri pia wanawadhulumu wanajamii wenzao, kwani ukafiri ndio chanzo cha ugumu wa moyo, choyo na uhasidi na pia ndio sababu kubwa ya kushikamana na kupenda vitu na kuiabudu dunia, natija ya mambo haya hupelekea dhulma kwa watu. Jambo la kuzingatia katika Aya hii ni kwamba, ukafiri uliokusudiwa ni kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kukhalifu amri Zake baada ya kuja amri ya kuwataka Waumini kutoa miongoni mwa mali zao, maana hii ya ukafiri ilivyotumika katika Aya hii imetumika sehemu nyingi katika Qur’ani na katika maandiko mengine ya Kiislamu.
54
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 54
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA NANE
َ ْص َد َقا ِت ُك ْم ب ْال َم ِّن َو أ ُْطل ََّيا أَُّي َها ال ُ َا ُ َ ال َذىٰ َكالَّ ِذي وا ب ت ل وا ن م آ ين ذ َ َ ِ ِ ِ ْلآ ُ ْ َ ُ ْ اس َو اَل ي ُؤ ِم ُن ِباللهَِّ َوال َي ْو ِم ا ِخ ِر َف َم َثل ُه ِ َّيُ ْن ِفق َمال ُه ِر َئا َء الن ْ َ َك َم َث ِل ٌ ان َعلَ ْي ِه تُ َر ص ْل ًدا اَل َ صا َب ُه َو ِاب ٌل َف َت َر َك ُه َ َاب َفأ ٍ صف َو َ ون َعلَىٰ َش ْي ٍء ِم َّما َك َسبُوا َواللهَُّ اَل َي ْه ِدي ْال َق ْو َم ْال َكا ِف ِر َ َي ْق ِد ُر ين َ ون أَ ْم َوالَ ُه ُم ا ْب ِت َغا َء َم ْر َ ين يُ ْن ِف ُق َ َو َم َث ُل الَّ ِذ ات اللهَِّ َو َت ْث ِب ًيتا ِم ْن ِ ض َأَ ْن ُف ِسه ْم َك َم َثل َجنَّ ٍة ب َر ْب َو ٍة أ َصا َب َها َواب ٌل َفآ َت ْت أُ ُكل َ ْن ي ف ع ض ا ه ْ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ َ َ ُ ٌّ ٌ َُّلله ُ َ َ ُص ْب َها َو ِابل َفطل َوا ِب َما َت ْع َمل ير أ َي َو ُّد أ َح ُدك ْم ٌص ِ ون َب ِ َفإِ ْن لَ ْم ي َ ْون لَ ُه َجنَّ ٌة ِم ْن َن ِخيل َوأَ ْع َناب َت ْجري ِم ْن َت ْح ِت َها أ َ أَ ْن َت ُك ار ُ ال ْن َه ٍ ِ ٍ ٌ صا َب ُه ْال ِك َب ُر َولَ ُه ُذ ِّري ُ َّة ض َع َفا ُء َ َات َوأ ِ لَ ُه ِفي َها ِم ْن ُك ِّل الثَّ َم َر ُ اح َت َر َق ْت َك َذٰلِ َك يُ َبي ات ٌ ار ِفي ِه َن ٌص ْ ار َف َ صا َب َها إِ ْع َ ََفأ ِ ِّن اللهَُّ لَ ُك ُم الآْ َي َ لَ َعلَّ ُك ْم َت َت َف َّك ُر ون “Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na udhia; kama yule anayetoa mali yake kwa kuwaonyesha watu; wala hamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha likafikiwa na mvua kubwa na ikaliacha tupu. Hawana uwezo wa chochote katika walivyovichuma; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri. Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na uimara wa nafsi zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu, ikafikiwa na mvua kubwa ikatoa mazao yake maradufu; na isipofikiwa na mvua kubwa, basi manyunyu (huitoshea). Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayotenda. Je, mmoja wenu anapenda kuwa na kitalu cha mitende na mizabibu ambacho mito hupita chini yake, naye humo hupata mazao ya kila namna, na uzee ukamfikia kisha ana watoto walio dhaifu; mara kifikiwe na kimbunga chenye moto kiungue? Hivi ndivyo anavyowabainishia Mwenyezi Mungu ishara ili mpate kufikiri.” (Qur’ani 2: 264-266). 55
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 55
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO: Katika Aya hizi mbili Mwenyezi Mungu anawakataza Waumini wasiziharibu sadaka zao kwa masimango na maudhi, pindi wanapotoa mali zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani kufanya hivyo kunaziporomosha thawabu za amali zao hizo. Baada ya makatazo haya Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa wale wanaotoa mali zao na baada yake kufuatiwa na masimbulizi, masimango na maudhi kuwa wao ni kama jabali ambalo juu yake kuna udongo na kukawa na mbegu iliyo bora na ikapigwa na jua pamoja na kupata hewa vizuri, kisha jabali hilo likanyeshewa na mvua kubwa na udongo huo pamoja na mbegu kuporomoka chini na jabali kubakia tupu, kwani mizizi ya mbegu hiyo haina uwezo wa kuvumilia vishindo vya mvua kubwa ikizingatiwa ya kwamba mizizi ya mbegu hiyo haikuwa na uwezo wa kulitoboa jabali na kupenya ndani yake, hii ni kutokana na mbegu hiyo kutooteshwa mahala panapostahiki, dhahiri yake ni nzuri lakini ndani yake ni ugumu kiasi cha kutowezekana mizizi kupenya ndani ya jabali ili kuiwezesha mbegu kukua na mmea kuchomoza. Hivi ndivyo ambavyo Qur’ani inavyomshabihisha yule ambaye hutoa mali yake kwa kujionesha au kumsimanga yule aliyempa, kile alichokitoa ni kama ule udongo uliopo juu ya jabali gumu, udongo huo hauna manufaa kwani kwa kuwepo hapo ulipo ni kikwazo kikubwa cha kuifanya mbegu kuweza kumea na kukua, bali kwa uoni wa nje kumuhadaa mkulima, na mwisho wake ni kusombwa na maji na upepo na kumsababishia hasara kubwa mkulima baada ya kupoteza juhudi nyingi. Mwishoni mwa Aya Mwenyezi Mungu anasema ya kwamba hawaongoi makafiri, hii ni dalili ya kwamba Mwenyezi Mungu huwaondoshea uongofu na taufiki, kwa vile wao hujionesha kwa watu na pindi watoapo huwasimanga baada ya kutoa mali zao, na wamejichagulia wenyewe njia ya ukafiri, kwa hivyo mtu wa aina hii hastahiki kupata uongofu wa Mwenyezi Mungu, ndio Mwenyezi Mungu akawaweka katika kundi moja wale wanaotoa mali zao kwa kujionesha au kuleta masimango pamoja na makafiri. Mfano Mwema: Baada ya Mwenyezi Mungu kueleza mfano wa watu wanafiki ambao wanakuwa na tabia ya kutoa mali zao kwa kujionesha na kutoa masimango pamoja na maudhi ya aina mbali mbali, Aya inayofuatia inatuelezea watu wanaotoa mali zao kwa misingi ya imani na ikhlasi, inasema: “Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kuitafuta radhi…” Aya hii inatupa taswira ya shamba lililomea na kustawi vizuri lililopo katika ardhi iliyochachuka na yenye rutuba, huku shamba hilo likineemeka kwa 56
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 56
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
upepo, mwanga wa jua pamoja na mvua zenye kuleta manufaa, na hata kama haikunyesha mvua kubwa basi hunyesha mvua ndogo ndogo ili kulifanya shamba libakie katika hali ya kawaida na kutosibiwa na ukame, natija inayopatikana katika shamba la aina hii ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na shamba jingine. Licha ya shamba hilo kuwa na rutuba kiasi ya kutosheka na manyunyu, ni kwamba hupata mvua za kiasi, na licha ya kufaidika kwa hewa na upepo mwanana na mionzi ya jua ya kiasi, kuwepo kwake pahala pa muinuko ni kinga kubwa dhidi ya mafuriko. Aya hii tukufu inataka kutuambia ya kwamba: Hakika wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kuwa na imani thabiti na yakini ya hali ya juu katika nyoyo zao, watu hao ni kama lile shamba lenye rutuba na kumea vizuri na lenye kuleta manufaa kwa mkulima na kwa watu wengine. Mwishoni mwa Aya Mwenyezi Mungu anasema:” Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kuitafuta radhi.” Yeye Mwenyezi Mungu anajua na kuona ikiwa mtu ametoa kwa misingi ya imani na mapenzi au kwa ajili ya kujionesha na kwa sababu ya masimango na maudhi kwa aliowapa. UTAFITI: 1.
Ibara inayosema: “Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na udhia.” Ni dalili ya kuwepo uwezekano wa baadhi ya matendo mema kuporomoka na kuharibika, kama ilivyo katika Aya 217 ya Suratul Baqarah na Aya ya 2 ya Suratul Hujuraat.
2.
Kushabihishwa amali iliyofanywa kwa kujionesha na jabali lililofunikwa na udongo laini, ni tashbihi inayotuonesha ya kwamba mwenye kufanya amali kwa kujionesha undani wake ni mgumu, kwa hivyo hujaribu kujionesha ya kwamba yeye ni mtu mwema na mzuri, na kwamba ni mtu anayependa mambo mema na ya kheri, ni mtu anayewependelea wenzake mambo mazuri, lakini ni kwamba matendo ya mtu wa aina hiyo hayakufungamana na ukhalisia wa moyo wake na roho yake, ndio mara baada ya matukio fulani, kwa haraka hudhihirika undani wake.
3.
Ibara inayosema: “Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na uimara wa nafsi zao.” Inatoa motisha na msukumo wa kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani mtoaji hupata radhi ya Mwenyezi Mungu na moyo wake huzidi imani na kupata utulivu wa hali ya juu katika nafsi yake. Aya hii tukufu inaonesha wazi ya kwamba watoaji wa kweli ni wale tu wanaotoa kwa ajili ya kupata radhi na kutarajia malipo yasiyo na mfano 57
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 57
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na wakiwa na lengo la kuzilea nafsi zao katika mafunzo mazuri ya kiadabu, na kuzitakasa nafsi zao kutokana na ugonjwa wa wasiwasi unaowasibu wale wanaotoa kwa kujionesha. 4.
Ibara ya mwisho iliyoko katika Aya ya pili, isemayo “Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayotenda,” inatoa tahadhari na kuwaonya wale wanaotenda matendo mema wasije wakafanya amali zao kwa ajili ya kuwaonesha wengine, au kumshirikisha asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kwani kufanya hivyo ni kuziharibu na kuzichafua amali zao njema, na watambue kwamba wako katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu, na anajua vyema ni amali gani iliofanywa kwa ajili yake.
Baadaa ya utafiti huo,Mwenyezi Mungu anawapigia Waumini mfano mwingine wa mtu anayetoa mali yake kwa ajili ya kujionesha kwa kusema:” Je, mmoja wenu anapenda kuwa na kitalu cha mitende na mizabibu ambacho mito hupita chini yake, naye humo hupata mazao ya kila namna, na uzee ukamfikia kisha ana watoto walio dhaifu; mara kifikiwe na kimbunga chenye moto kiungue? Hivi ndivyo anavyowabainishia Mwenyezi Mungu ishara ili mpate kufikiri.” Aya inatubainishia ni namna gani mwanadamu Siku ya Kiyama atakavyokuwa na haja ya kuwa na amali njema katika daftari lake la amali, na wakati huo utakuwa ni wakati wa amali njema kutokuwa na baraka yoyote ikiwa alizifanya kwa ajili ya kujionesha au kufuatiliwa na masimango au maudhi ya aina mbalimbali, mfano wa amali za aina hii ni kama mtu mwenye shamba lenye mimea ya aina mbalimbali iliyonawiri vizuri, mimea hiyo ikawa inapata maji ya kutosha bila ya kutegemea maji ya kumwagiliwa, mara shamba hilo likasibiwa na ukame wa hali ya juu na kulikausha shamba hilo lote na yule mkulima akawa ni mwenye watoto wadogo ambao alikuwa akilitegemea shamba hilo kwa kujikimu yeye pamoja na watoto wake. Kwa hivyo yule ambaye alikuwa akihangaika kwa kufanya amali mbalimbali, akaziporomosha amali zake njema kwa kujionesha au kwa kuwaudhi watu kutokana na masimango yake juu ya watu hao, hali yake ni kama hali ya mkulima anayepoteza nguvu zake nyingi na wakati wake, na unapofika wakati wa mavuno asiambulie kitu chochote na huku akiwa na watoto wasio na uwezo wa kujisimamia maisha yao. Mwisho wa Aya Mwenyezi Mungu anamalizia kwa kusema: “Hivi ndivyo anavyowabainishia Mwenyezi Mungu ishara ili mpate kufikiri.” Mwenyezi Mungu anawataka waja Wake wafikiri na kuzingatia juu ya kila jambo wanalolifanya, kwani masimango na kuwaudhi watu baada ya mtu kutoa mali yake kwa kuwapa wanaostahiki si kitu kinachokubalika na kila mtu mwenye akili timamu. 58
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 58
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA TISA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ات َما َك َسبْتُ ْم َو ِم َّما أَ ْخ َر ْج َنا ِ ين آ َمنُوا أَ ْن ِف ُقوا ِم ْن َطيِّ َب َ ْلَ ُك ْم ِم َن أ َ ض َو اَل َت َي َّم ُموا ْال َخ ِب َ يث ِم ْن ُه تُ ْن ِف ُق آخ ِذي ِه ر ال ْ ِ ون َولَ ْستُ ْم ِب ِ َ َ الشي َّ اعلَ ُموا أ َّن اللهََّ َغ ِن ٌّي َح ِمي ٌد ُ إِ اَّل أَ ْن تُ ْغ ِم ُ ْط ْ ضوا ِفي ِه َو ان ْ َي ِع ُد ُك ُم ْال َف ْق َر َو َي ْأ ُم ُر ُك ْم ِب ْال َف ْح َشا ِء َواللهَُّ َي ِع ُد ُك ْم َم ْغ ِف َر ًة ِم ْن ُه َو َف ض اًل اس ٌع َعلِي ٌم ِ َواللهَُّ َو “Enyi mlioamini! Toeni katika vizuri mlivyovichuma na katika vile tulivyowatolea ardhini; wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kuvifumbia macho. Basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Mwenye kusifiwa. Shetani anawatisha na ufukara na anawaamrisha ubakhili; na Mwenyezi Mungu anawaahidi msamaha utokao Kwake na fadhila na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu, Mjuzi.” (Qur’ani 2:267-268).
SABABU YA KUTEREMKA: Imam Sadiq (a.s.) amesema: “Aya hii iliteremka kwa watu waliokuwa wakichuma chumo la riba katika zama za kijahilia, na riba hiyo wakiitolea sadaka, ndipo Mwenyezi Mungu aliwakataza jambo hilo, na kuwaamrisha watoe sadaka kwa mali iliyo nzuri na ya halali.”37 Na kutoka kwa Imamu Ali (a.s.) anasema: “Aya hii imeteremka kwa sababu ya watu waliokuwa wakitoa sadaka tende zilizoharibika”38 Hadithi hizi mbili hazina upinganaji wowote, na huenda Aya ikawa imeteremka kutokana na sababu zote mbili, kwani Hadithi ya kwanza itokayo kwa Imamu Sadiq (a.s.) inaangalia usafi na utohara wa ndani (kiroho) na Hadithi ya pili inaangalia usafi na utohara wa nje. Lakini jambo la kuzingatia hapa, ni kwamba watu waliokuwa wakichuma kwa njia ya riba katika zama za kijahilia waliachana na uchumi huo baada ya kuteremka Aya ya 275 ya Suratul Baqarah, na wala hawakukatazwa kuitumia mali yao walioichuma katika mfumo wa riba wakati wa zama hizo, lakini ni jambo la wazi ya kwamba mali ya aina hiyo licha ya kuwa ilikuwa ni halali, lakini ilikuwa 37 38
Tabarasiy, Majma’ul Bayan, Jz. 2, Uk.191 Shiraziy, Tafsirul Amthaj, Jz.2, uk.308 59
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 59
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
inatofautiana na mali nyingine isiyotokana na chumo la haramu, uhakika wa mali hiyo ilikuwa inashabihiana na mali iliyopatikana kwa njia isiopendeza (Makruhu).
MAELEZO: Aya zilizotangulia zimetueleza faida za utoaji, sifa anazotakiwa kuwa nazo mwenye kutoa na mambo ambayo hubatilisha thawabu za utoaji. Ama Aya hii inatubainishia aina ya mali inayostahiki kutolewa kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu. Mwanzoni mwa Aya Mwenyezi Mungu anawaamrisha Waumini watoe vile vilivyo vizuri miongoni mwa mali zao, na uzuri unaokusudiwa ni uzuri wa kimaana, kwa maana kinachotolewa kiwe ni kitu cha halali, na uzuri mwingine uwe ni wa kimaada, ikimaanisha kitu kizuri ambacho yule mwenye kupewa atafaidika nacho, pia ibara inayosema: “Hali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kuvifumbia macho.� Inamaanisha ya kwamba, hata nyinyi mlio na uwezo hamko tayari kuchukua sadaka isio nzuri ila ikiwa mtafumba macho yenu, hii ni dalili ya kwamba mali itakayotolewa haitakiwi iwe ni nzuri katika sura yake ya nje tu, bali pia inatakiwa iwe na uzuri wa ndani, kwa kuwa halali, kwani Muumini wa kweli hakubali kupokea kitu kilicho na uzuri wa nje tu. Pale Mwenyezi Mungu anapowakataza Waumini wasikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali ya kuwa wao wenyewe wasingevipokea ila baada ya wao kufumba macho, hii ni ishara ya kwamba watu walio wengi wamezoea kutoa vile ambavyo havina thamani na wala hawana haja navyo, utoaji wa vitu vya aina hii si wenye kuilea malezi mazuri nafsi ya mtoaji, na wala haukidhi shida ya muhitaji, bali ni njia ya kumfanya kuzidi kuwa mnyonge na dhalili, kutokana na tabia hii mbaya ndio Mwenyezi Mungu akaikemea kwa kusema: Vipi mnatoa mali ambayo nyinyi wenyewe kama mtafikwa na shida hamko tayari kuipokea isipokuwa pale mtakapokuwa hamna budi kuipokea? Je mnawaona ndugu zenu Waislamu hawana hadhi yoyote? Au hiyo njia ya Mwenyezi Mungu mnayoitolea hizo mali zenu haina thamani kwenu? Aya tukufu inatukhabarisha ya kwamba utoaji wa mali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu uko wa aina mbili: Kwanza, ni kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Pili, ni kutoa kuwapa wanaohitaji, basi ikiwa mtu atatoa kitu kisicho na thamani, kufanya hivyo itakuwa ni kumdhalilisha Mwenyezi Mungu na pia kuwadhalilisha waja Wake wahitaji ambao huenda wakawa ni watu walio na imani ya hali ya juu, na huko kupewa vitu visivyo na thamani huwasababishia maumivu ya kisaikolojia katika nafsi zao. Mwishoni mwa Aya Mwenyezi Mungu anawataka Waumini watambue ya kwamba Mwenyezi Mungu hana haja na mali zao, kwani Yeye ni Mkwasi na Mwenye kujitosheleza
60
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 60
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
kwa kila kitu na Yeye ni Mmiliki wa neema zote na ndiye anayewaruzuku waja Wake, kwa hivyo ni wajibu wa kila mja kumshukuru na kumsifu kwa kila sifa njema, anasema: “Basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Mwenye kusifiwa.”
MAZINGATIO: Bila ya shaka kutoa kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu ni sababu kubwa ya kujikurubisha kwake, ni kawaida pale watu wanapotaka kujikurubisha kwa watawala na wale wenye mamlaka fulani, huwapa zawadi zilizo bora zaidi na zenye thamani ya hali ya juu sana, licha ya kuwa watawala hao ni wanadamu kama wao, basi iweje mtu anapotoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ambaye ndiye Muumba Wake, atoe kitu kilicho duni sana?! Tunachokishuhudia katika vitabu vya fiqhi, ni watu kuhimizwa kutoa mali iliyo nzuri pindi wanapotaka kutoa Zaka, na pia wanapotaka kuchinja mnyama wakati wa ibada ya Hijja anatakiwa mnyama huyo asiwe na kasoro wala aibu, mambo haya yote ni katika mtiririko huu wa mtu kutoa kile kilicho halali na kizuri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kutokana na maelezo haya, inatupasa kuyatekeleza mafunzo haya, kwa kujilazimisha kutoa vile vilivyo bora na vizuri, na pia kuwaelimisha wengine juu ya hili. Kupambana Dhidi ya Vikwazo vya Utowaji: Aya ya pili katika kipengele hiki, inatueleza kikwazo kikubwa kinachowazuia watu kutoa mali zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kikwazo hicho ni wasiwasi wa shetani unaomhofisha mwanadamu dhidi ya kusibiwa na ufakiri ikiwa atatoa mali yake kuwasaidia wengine, na hasa ikiwa atatoa sadaka kwa mali nyingi na iliyo nzuri. Aya inasema: “Shetani anawatisha na ufukara na anawaamrisha ubakhili.” Aya inabainisha ya kwamba shetani huwashawishi na kuwadanganya wale wanaotaka kutoa vile wanavyovipenda miongoni mwa mali zao ya kwamba: Msisahau mustakbali wenu pamoja na watoto wenu, na iwapo mtatoa, basi mtakuwa mmepunguza sehemu fulani ya mali zenu, na natija yake ni kusibiwa na ufakiri. Zaidi ya hayo ni kwamba shetani huyo huwataka watu hao kujitumbukiza katika uovu na maasi. Nadharia ya mwanzo ya kishetani katika utoaji wa mali ni kwamba, jambo hili linapelekea upungufu wa mali na kusababisha ufakiri. Nadharia hii ni nadharia iliyo dhaifu sana kwani utoaji wa mali kwa kuwasaidia wasiojiweza ni dhamana kubwa ya kubakia jamii iliyoshikamana na kuwepo uadilifu wa kijamii na kupunguza matabaka kati ya watu, na pia ni sababu ya kupiga hatua za kimaendeleo. Na ni wazi kwamba maendeleo ya jamii, ni watu kuishi katika hali nzuri ya kiuchumi, baada ya 61
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 61
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
kumuamini Mwenyezi Mungu na kufuata mafunzo ya Dini Yake, hii ndio nadharia halisi ya kimaendeleo kwa mujibu wa mafunzo ya Uislamu. Hapa Qur’ani Tukufu inawaelimisha watu ya kwamba, utoaji wa mali ni kuwapa wahitaji misingi ya kimaisha, na hao watoaji hunufaika kimwili na kiroho. Kimwili, huwa wamejiwekea ulinzi na usalama wa mali zao, kwani pale atakapotokea mtu, au kukawa na sababu yoyote itakayopelekea kupotea kwa mali hiyo, wanajamii watakuwa tayari kujitolea kwa hali na mali kuilinda mali hiyo. Ama kiroho, ni kwa mtoaji kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kumuongezea baraka katika mali yake. Leo katika dunia yetu hii tunashuhudia tofauti kubwa ya kipato kati ya watu na kusababisha matabaka ya watu, hii inatokana na udhalimu unaofanywa na wenye nacho kwa kujikusanyia mali bila ya kuwasaidia wahitaji. Imepokewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s.)
َ فاللذان, و شيئين من الشيطان,إن في اإلنفاق شيئين من اهلل ّ غفران:من اهلل هما و فالّلذان من,والسعة في المال ّ الذنوب ّ .الشيطان هما الفقر واألمر بالفحشاء “Katika kutoa mali kuna mambo mawili yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu, na pia kuna mambo mawili yanayotoka kwa shetani. Ama yale yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu ni kusamehewa madhambi na kuzidishiwa mali, na yale yanayotoka kwa shetani ni ufakiri na kuamrisha uovu.”39
Na Imamu Ali (a.s.) naye amesema:
إذا أملقتم فتاجروا اهلل بالصدقة “Pindi mnapochelea kusibiwa na ufakiri, basi fanyeni biashara na Mwenyezi Mungu kwa kutoa sadaka.”
Mwishoni mwa maudhui ya Aya hizi Mwenyezi Mungu anamalizia kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu, Mjuzi.” Anatuashiria ya kwamba Yeye anauwezo wa hali ya juu sana na maarifa yasiyo na mpaka, ya kwamba anauwezo wa kuyalipa yale aliyowaahidi watu wema. Bila ya shaka Muumini wa kweli anakuwa na utulivu wa nafsi pindi asikiapo ahadi kama hii kutoka kwa Mola Wake, kwani ahadi Yake si kama ahadi 39
Kitabu kilichotangulia, Jz. 2, Uk. 314 62
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 62
12/8/2014 2:43:36 PM
WITO KWA WAUMINI
ya shetani, ahadi ambayo mara zote inakuwa ni dhaifu na yenye hadaa, inayompelekea mtu kujitumbukiza katika maasi na ufisadi. Hakika shetani ni kiumbe dhaifu na asiyejua mambo yatakayotokea baadaye, kutokana na sifa zake mbaya, ndio ikawa ahadi zake ni za uongo na kuwahimiza watu kufanya uovu wa aina mbalimbali.
63
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 63
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ الر َبا إِ ْن ُك ْنتُ ْم ِّ ين آ َمنُوا اتَّ ُقوا اللهََّ َو َذ ُروا َما َب ِق َي ِم َن َ ُم ْؤ ِم ِن ين َفإِ ْن لَ ْم َت ْف َعلُوا َف ْأ َذنُوا ِب َح ْر ٍب ِم َن اللهَِّ َو َر ُسولِ ِه َوإِ ْن َ ون َوإِ ْن َك َ ون َو اَل تُ ْظلَ ُم َ وس أَ ْم َوالِ ُك ْم اَل َت ْظلِ ُم ان ُ تُبْتُ ْم َفلَ ُك ْم ُر ُء ْر لَ ُك ْم إِ ْن ُك ْنتُ ْم ٌ ص َّد ُقوا َخي َ ْس َر ٍة َوأَ ْن َت َ ُذو ُع ْس َر ٍة َف َن ِظ َر ٌة إِلَىٰ َمي ْ ُّ ُ َّ ُ ََّ لله َ ون َواتَّ ُقوا َي ْو ًما تُ ْر َجع َ َتعْلَ ُم س َما ٍ ُون ِفي ِه إِلى ا ِ ث َّم تُ َوفىٰ كل َنف ْ َك َس َب ْت َو ُه ْم اَل ي َ ُظلَ ُم ون “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi msipofanya (hivyo) jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe. Na akiwa (mdaiwa) anashida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa munajua. Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilichokichuma. Nao hawatadhulumiwa. (Qur’ani 2:278:281)
SABABU YA KUTEREMKA: Baada ya kuteremka Aya inayokataza kula riba, Khalid ibn Walid alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na akasema: “ Baba yangu alikuwa akifanya muamala wa riba pamoja na watu wa Bani Thaqiif, na baba yangu alifariki kabla ya kurejeshewa pesa zake, na aliniusia nichukue faida ambazo alikuwa hajalipwa, je inafaa mimi kufanya hivyo?” Baada ya suala lake hili, ndipo Aya hii ikateremka ikiwakataza watu kufanya hivyo. Na katika Riwaya nyingine ni kwamba baada ya kuteremka Aya hii, Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Tambueni ya kwamba kila riba iliyokuwepo wakati wa ujahilia ni haramu, na riba ya kwanza kuiharamisha ni ya Abbas ibn Abdul Muttalib.”40 Katika Riwaya hii tunamshuhudia Mtume (s.a.w.w.) akianza kuikataza riba kwa watu wake wa karibu kinasaba, mfano ni ami yake; Abbas bin Abdul Muttalib, ambaye alijikusanyia utajiri mkubwa uliotokana na chumo litokanalo na riba. Pia 40
Kitabu kilichotangulia, Uk. 345 64
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 64
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
imepokewa kutoka katika Riwaya mbalimbali ya kwamba, baada ya kuteremshwa Aya hii, Mtume (s.a.w.w.) alimuamrisha amiri wa mji wa Makka kuwapiga vita watu wa familia ya Mughira ikiwa wataendelea na biashara yao ya riba.
MAELEZO: Katika Aya ya kwanza Mwenyezi Mungu anawataka Waumini kushikamana na uchaji Mungu, na baada ya hapo anawataka waachane na faida zenye riba zitokanazo na mikopo waliowakopesha watu wengine. Jambo la kuzingatia hapa, ni kwamba Aya imeanza na suala la kumuamini Mwenyezi Mungu na kuishia kukataza riba, hii inamaanisha ya kwamba mfumo wa kiuchumi wa riba haukubaliani na imani khalisi juu ya Mwenyezi Mungu. Aya inayofuata Mwenyezi Mungu anasema: “Na kama hamtafanya, basi jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Katika Aya iliyopita tunaona namna Mwenyezi Mungu alivyotumia utaratibu wa kutoa nasaha na mawaidha kwa walaji riba, ama katika Aya hii ya pili mambo si hivyo, hapa Mwenyezi Mungu ametumia lahaja nzito na maneno makali kwa kuwaonya na kuwatahadharisha walaji riba ikiwa wataendelea na biashara yao hiyo na kuishi kwa kutegemea jasho la watu wengine na kutoshikamana na mafunzo thabiti ya Qur’ani, ikiwa hali itaendelea kuwa hivyo, basi ni jukumu la Mtume (s.a.w.w.) kutumia nguvu kwa ajili ya kuiondosha dhulma hiyo, kwani kuendelea kwao kula riba ni sawa na kutangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.). Bila ya shaka vita dhidi ya watu hawa ni jambo lililo thibiti kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, kama Mwenyi Mungu alivyosema:
َ َ َّ ُ َ َ َّ َِّْر الله ِ فقا ِتلوا ال ِتي َت ْب ِغي َحتى َت ِفي َء إِلى أم “…Basi lipigeni lile linaloonea mpaka lirudi katika amri ya Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani 49:9).
Kutokana na mafunzo haya ya Qur’ani, Imam Sadiq (a.s.) aliposikia ya kwamba kuna mtu anaishi kwa mfumo wa riba na kutoa maneno ya kejeli juu ya uharamu wake, alimtishia kumuuwa. Kwa mujibu wa Riwaya hii ni kwamba, mtu anayepinga ya kwamba riba ni haramu, na kuendeleza biashara hiyo anastahiki kupigwa vita, kwa hivyo ni jukumu la serikali ya Kiislamu kusimama kidete katika kupambana na watu wa aina hiyo, kwani kitendo chao cha kula riba ni sawa na kutangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.), kwa hivyo wale walioshika nafasi
65
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 65
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
za uongozi wa dola ya Kiislamu ni juu lao kupambana na wahalifu hao. Iwapo mtu amewaidhika na kukubali kufuata kanuni za Mwenyezi Mungu na kutubia kutokana na kula riba, basi itampasa kuchukua rasilimali yake tu, pasi na kuchukua nyongeza yoyote ya riba, kama Aya inavyosema: “Na mkiwa mmetubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu; msidhulumu wala msidhulumiwe.” Bila ya shaka yoyote hii ndio kanuni yenye uadilifu wa hali ya juu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwani inawazuia watu wasidhulumu na wakati huo huo wasidhulumiwe na wengine. Ibara inayosema: “Msidhulumu wala msidhulumiwe.” Licha ya kuja katika maudhui ya walaji riba, lakini kwa uhakika ni kaulimbiu ya Uislamu yenye upana wa hali ya juu, ikimaanisha ya kwamba, kama ilivyo wajibu kwa Waislamu kujiepusha na dhulma ya kuwadhulumu wengine, pia ni wajibu kutofanya kitu kitakachowapelekea kujidhulumu wenyewe. Ni ukweli usiofichika, lau kama wapokeaji wa mali ya dhulma wangepungua, basi na pia wale wanaodhulumu nao pia wangepungua. Na lau kama Waislamu wangelikuwa na matayarisho mazuri ya kutetea haki zao, asingetokea yeyote wa kuweza kuwanyang’anya haki zao na kuwadhulumu. Basi kabla ya kumwambia mtu dhalimu: “Usidhulumu.” Ni juu yetu kumuambia mtu aliyedhulumiwa: “Usikubali kupokea kitu cha dhulma.” Aya inayofuata inasema: “Na kama ana dhiki, basi angoje mpaka awe na uwezo.” Katika kukamilisha haki ya mdai, ambayo ni rasilimali yake bila ya kuchukua ziada yoyote, Aya inatubainishia utaratibu wa kuufuata katika kuipata hiyo haki yake, ikiwa yule mdaiwa hana uwezo wa kulipa deni analodaiwa, jambo linalotakiwa kwa mdeni ni kuvuta subira na kumpa wakati zaidi mdaiwa mpaka hapo atakapopata uwezo wa kulipa. Tumeona ni namna gani hali ilivyokuwa katika zama za ujahilia na hata katika zama hizi za kijahilia mamboleo ni kwamba mdaiwa analipa riba zaidi kila anapochelewa kulipa deni lake, lakini Uislamu ukaja na hukumu inayozingatia ubinadamu na uadilifu, kwani licha ya kukataza riba, imewataka wadai kuwapa muda zaidi wadaiwa wao kuwatafutia rasilimali zao ikiwa hali zao za kiuchumi si nzuri. Kwa kweli Aya hii imekuja kubainisha kanuni ya Kiislamu yenye uadilifu wa hali ya juu, ya kwamba, si haki kwa mdai kuhodhi nyumba ya mdaiwa au rehani nyingine kwa lengo la kufidia deni lake, ikiwa atashindwa kustahamili, basi asichukue zaidi ya kile anachokidai, kanuni ya kiadilifu imekuja kuwatetea watu mafakiri na wa tabaka la chini katika jamii. Ibara ya mwisho katika Aya hii inayosema: “Na kama deni mkizifanya sadaka, basi ni bora kwenu ikiwa mnajua “Mwenyezi Mungu anawashauri wadai kuwasamehe
66
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 66
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
wadaiwa wao ikiwa wataonekana kushindwa kabisa kulipa deni wanalowadai, na hicho walichowakopesha wasikidai tena na watie nia ya kuwa ni sadaka. Kwa hakika suala hili ni suala lenye hadhi ya hali ya juu katika masuala ya haki za binadamu, na ni kupiga hatua kubwa sana kwa Muumini ya kujiweka karibu zaidi na Mola Wake, na ni jambo bora zaidi kuliko kung’ang’ania kumdai mtu asiye na uwezo, au kuuza baadhi ya vitu vyake muhimu katika maisha yake kwa ajili ya kulipia deni lake. Aya ya mwisho, inasema: “Na iogopeni siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi ilipwe iliyoyachuma; nao hawatadhulumiwa.” Hapa Mwenyezi Mungu anawataka wanadamu wote, na hasa Waumini kushikamana na maamrisho Yake na kuachana na yale yote aliyoyakataza, kwani kuendelea kufanya maovu kutamsababishia mwanadamu kuishi maisha mabaya mara baada ya kuiaga dunia, na miongoni mwa makosa makubwa ni kula riba, kama ilivyoelezwa katika Aya zilizotangulia. Kwa hivyo haitotosha tu kwa mwanadamu kusema kwamba ameamini mambo yote yanayopaswa kuaminiwa bila ya kuchukua tahadhari katika kila jambo analolitenda kabla hajafikiwa na siku ambayo matendo ya kila mwanadamu yatawekwa dhahiri shahiri na kila mmoja kulipwa kwa mujibu wa amali zake bila ya kupunguziwa au kuzidishiwa.
Madhara ya Riba: 1.
Riba inapelekea kukosekana kwa uwiano wa kiuchumi katika jamii, huwafanya watu wachache kujikusanyia na kujirundukia mali, na huku ikiwaacha walio wengi katika dimbwi la hasara, ukandamizwaji na ufukara wa kupindukia. Katika zama zetu hizi, tunashuhudia ya kwamba nchi tajiri zinaitumia riba kama nyenzo ya kuzitawala kifikra na kitamaduni nchi masikini, kwani kutokana na mzigo wa madeni yatokanayo na ongezeko la riba, viongozi wa nchi hizo wanakubali kuitikia wito na kutii kila amri itikayo kwa viongozi wa nchi tajiri.
2. Riba ni miongoni mwa ubadilishanaji wa kibiashara usio halali, kwa hivyo hudhoofisha mafungamano ya kimapenzi kati ya watu na badala yake hupanda mbegu ya hasadi na chuki katika nyoyo, kwa vile mtu anayeishi kwa chumo la riba hana analoliangalia isipokuwa kupata faida kutokana na mali alioikopesha, na wala hashughulishwi na madhara pamoja na hasara atakayoipata mkopaji, katika hali kama hii, mkopaji hamuoni mdai wake ila ni mtu aliye na lengo la kuyaangamiza maisha yake kwa kupitia mali yake. 67
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 67
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
3.
Ni jambo lililowazi, kwamba, mtu anayekubali kukopa na kulipa deni lake pamoja na ziada (riba), amechukua uamuzi huo mwenyewe kutokana na shida yake. Lakini mtu huyo katu hatosahau dhulma ya aina hii, na huenda akafikia hali ya kuchukua maamuzi mazito ya kutaka kuyamaliza maisha yake, au kuanza kupeleka kila aina ya matusi na laana mbali mbali kwa mdai wake na hatimaye kufikia uamuzi wa kutaka kumuua, kwani huona ni namna gani maisha yake yalivyodhibitiwa na mlaji riba.
Hakika mahusiano mabaya kati ya nchi zilizo na uchumi unaozingatia riba na zile nchi zinazokopa na kutakiwa kulipa riba ni jambo linaloeleweka. Nchi inayoikopesha nchi nyingine kwa njia ya riba, inachokingojea ni chuki na bughudha kutoka kwa wananchi wa hiyo nchi masikini iliyokopeshwa licha ya kwamba pale inapokopa hufanya hivyo kutokana na kukosa budi ila kukubali kulipa ziada baada ya kukopa. Kutokana na natija hizi, ndio ikatupelekea kusema ya kwamba, riba inajenga athari mbaya sana za kisaikolojia katika nafsi za wakopaji, na kusababisha chuki na hasira katika nyoyo zao, kukosekana maelewano, mshikamano na kusaidiana kati ya wanajamii. 4.
Katika Hadithi Tukufu iliyopokewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s.) inayoeleza sababu ya kuharamamishwa riba inamaana pana sana licha ya ufupi wa ibara yake, anasema:
ّ عز ّ حرم اهلل الربا لكي ال يمتنع النّاس عن ّ وجل ّ إنّما اصطناع المعروف “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha riba, ili watu wasijizuie kufanya mambo mema.”41
41
Swadduq, Ilalu Shara’, Jz.2, Uk.482 68
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 68
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA MOJA
َيا أَُّي َها الَّ ين آ َمنُوا إ َذا َت َدا َي ْنتُ ْم ب َديْن إلَىٰ أَ َج ٍل ُم َس ًّمى َف ْ َ اكتُبُو ُه ذ ِ ِ ٍْ ِ ِ َ ْ َو ْل َي ْكتُ ْب َب ْي َن ُك ْم َكا ِت ٌب ِبال َع ْد ِل َو اَل َيأ َب َكا ِت ٌب أ ْن َي ْكتُ َب َك َما َعلَّ َم ُه اللهَُّ َف ْل َي ْكتُ ْب َو ْليُ ْملِ ِل الَّ ِذي َعلَ ْي ِه ْال َح ُّق َو ْل َيتَّ ِق اللهََّ َربَّ ُه َو اَل َيب َ ان الَّ ِذي َعلَ ْي ِه ْال َح ُّق َس ِفيهًا أَ ْو َ س ِم ْن ُه َشي ًْئا َفإِ ْن َك َ ض ِع ًيفا ْخ ْ اس َت ْش ِه ُدوا أَ ْو اَل َي ْس َت ِط ُ يع أَ ْن يُ ِم َّل ُه َو َف ْليُ ْملِ ْل َولُِّي ُه ِب ْال َع ْد ِل َو ْ َشهي َديْن ِم ْن ر َجالِ ُك ْم َفإ ْن لَ ْم َي ُكو َنا َر ُجلَيْن َف َر ُج ٌل َوا ْم َرأَ َ ان ت ِ ِ ِ ِ ِ ِ َ َّ ِّ ُّ اه َما َفتُ َذك َر إِ ْح َد ُ ضل إِ ْح َد ُ ِم َّم ْن َت ْر َ اه َما ض ْو َن ِم َن الش َه َدا ِء أ ْن َت ِ أُْ ال ْخ َرىٰ َو اَل َي ْأ َب ُّ الش َه َدا ُء إِ َذا َما ُد ُعوا َو اَل َت ْسأَ ُموا أَ ْن َت ْكتُبُو ُه يرا أَ يرا إلَىٰ أَ َجلِ ِه َ ٰذلِ ُك ْم أَ ْق َس ُط ِع ْن َد اللهَِّ َوأَ ْق َو ُم لِ َّ َ لش َها َد ِة ب ك و ً ص ِغ ً ْ َ ِ ِ َوأَ ْد َنىٰ أَ اَّل َت ْر َتابُوا إِ اَّل أَ ْن َت ُك َ يرو َن َها َب ْي َن ُك ْم اض َر ًة تُ ِد ُ ون ِت َج َ ار ًة َح ِ ْس َعلَي ُ ُوها َوأَ ْش ِه ُدوا إِ َذا َت َبا َيعْتُ ْم َو اَل ي َ اح أَ اَّل َت ْكتُب َ ار ْك ْم ُج َن ٌ ُض َّ َفلَي َ َكا ِت ٌب َو اَل َشهي ٌد َوإ ْن َت ْف َعلُوا َفإنَّ ُه ُف ُس ٌ وق ِب ُك ْم َواتَّ ُقوا اللهََّ َويُ َعلِّ ُم ُك ُم ِ ِ ِ اللهَُّ َواللهَُّ ِب ُك ِّل َش ْي ٍء َعلِي ٌم َوإِ ْن ُك ْنتُ ْم َعلَىٰ َس َف ٍر َولَ ْم َت ِج ُدوا َكا ِتبًا ْض ُك ْم َبع ً ُوض ٌة َفإِ ْن أَ ِم َن َبع ُ ْضا َف ْليُ َؤ ِّد الَّ ِذي ْ َف ِر َه ٌ ان َم ْقب َ اؤتُ ِم َن أَ َما َن َت ُه َو ْل َيتَّق اللهََّ َربَّ ُه َو اَل َت ْكتُ ُموا َّ الش َها َد َة َو َم ْن َي ْكتُ ْم َها َفإِنَّ ُه آ ِث ٌم ِ ُ َق ْلبُ ُه َواللهَُّ ِب َما َت ْع َمل َ ون َعلِي ٌم “Enyi mlioamini! Mnapokopeshana deni kwa muda uliowekwa, basi liandikeni; na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu. Wala mwandishi asikatae kuandika kama vile alivyomfunza Mwenyezi Mungu; basi na aandike. Na aandikishe yule 69
12/8/2014 2:43:37 PM
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 69
WITO KWA WAUMINI
ambaye iko juu yake haki; na amwogope Mwenyezi Mungu Mola Wake; wala asipunguze chochote katika deni. Na kama yule ambaye juu yake iko haki ni mpumbavu au mnyonge au yeye hawezi kuandikisha mwenyewe, basi na aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu. Na muwashuhudishe mashahidi wawili katika watu wenu waume, kama hakuna wanaume wawili, basi ni mwanamume mmoja na wanawake wawili, katika wale mnaowaridhia kuwa mashahidi, ili kama mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwingine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msichoke kuliandika deni likiwa dogo au kubwa, mpaka muda wake. Hayo ndiyo uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu na imara sana kwa ushahidi na ni karibu zaidi kutofanya shaka. Ila ikiwa ni biashara ya mkono kwa mkono mnayopeana baina yenu, basi si vibaya kwenu msipoandika. Na wekeni mashahidi mnapouziana, wala asitiwe tabu mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo, basi hakika hilo ni ufasiki kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anawaelimisha; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi kwa kila kitu. Na kama mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, basi ni rahani itakayokabidhiwa. Na kama mmoja wenu akimwamini mwingine, basi aliyeaminiwa atekeleze uaminifu wake na amche Mungu, Mola Wake. Wala msifiche ushahidi. Na atakayeuficha, basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi kwa mnayoyatenda.” (Qur’ani 2:282-283).
MAELEZO: Baada ya Qur’ani Tukufu kukemea kwa ukali ulaji riba, kujilimbikizia mali na ubahili, katika Aya hii inatoa maelezo ya namna ya utaratibu wa kuihifadhi mali ya biashara ili isipotee na badala yake ikuzwe na kuongezeka kwa wingi kwa njia iliyo halali, na bila ya kusababisha mizozo na mivutano kati ya watu. Aya hii iliyo refu kuliko Aya nyingine katika Qur’ani Tukufu imebainisha vipengele kumi na tisa vinavyoelezea utaratibu wa kuhifadhi mali, vipengele hivyo ni kama vifuatavyo: 1. Ikiwa mtu atakopa au ataingia katika mkataba wa kibiashara na mtu mwingine, katika hali ambayo mtu mmojawapo atakuwa na deni, basi itawajibika juu yao waandikiane ili pasije pakatokea mzozo na kutokuelewana baadaye, kama sehemu ya Aya inavyosema: “Enyi mlioamini! Mnapokopeshana deni kwa muda uliowekwa, basi liandikeni.” Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu ametumia neno ‘Deni’ na wala hakutumia neno ‘Mkopo’ kwani neno ‘Mkopo’ kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu linamaana kubadilishana vitu viwili vilivyofanana kama vile pesa au bidhaa, vitu ambavyo mkopaji huvikopa na kuvitumia, kisha huvirejesha kwa mwenyewe vitu hivyo vikiwa na thamani ya vile alivyokopa. 70
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 70
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
ma deni ni neno lililo na upana zaidi, kwani linakusanya kila muamala wa A kibiashara, kama vile muswalaha, upangishaji, kuuza, kununua na mfano wa haya, katika hali inayoufanya upande mmoja kuwa ni mdaiwa wa upande mwingine. Kwa hivyo Aya hii inahusisha aina zote za miamala na mikataba ya kibiashara, ikiwa tu upande mmoja utakuwa na deni, ikiwemo mkopo. 2.
Ili kila upande uwe na uhakika wa kusihi kwa mkataba na kutomfanya mmoja wapo kuja kumgeuka mwenzake, itawajibika kuwepo mtu wa tatu ambaye atasimamia shughuli za uandishi wa mkataba, kama Aya inavyosema: “na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu.” Dhahiri ya Aya inaonesha ulazima na wajibu wa kuandikwa mkataba, lakini katika Aya inayofuata inaweka bayana ya kwamba iwapo watu watakuwa wameaminiana na kuwa na uhakika wa kutokupoteza haki zao, basi si lazima kuandikiana.
3.
Ni juu ya mwandishi wa mkataba, awe mtu mkweli na mwadilifu, na asimame upande wenye haki ikiwa kutatokea kutokuelewana: “na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu.”
4.
Mwislamu ambaye anauwezo wa kuandika mkataba, inampasa asikatae kuandika pindi atakapohitajika kufanya hivyo, bali ni juu yake kutoa msaada wake juu ya jambo hili: “Wala mwandishi asikatae kuandika.”
5.
Upande mmoja kati ya pande mbili ndio ulio na haki ya kueleza namna ya kuandikwa huo mkataba, mwenye haki hiyo ni upande wa mdaiwa, kama Aya inavyoeleza: “Na aandikishe yule ambaye iko juu yake haki.” Jambo lililo muhimu katika mkataba wa deni ni ushahidi na uthibitishao wa mdaiwa, na ushahidi utapatikana bila ya mzozo ikiwa yeye mwenyewe ataeleza namna ya kuandikwa na kuweka sahihi yake.
6.
Wakati mdaiwa anapoelezea namna ya kuandikwa mkataba kwa mwandishi ni wajibu wake kueleza kila ambalo analiona lina umuhimu kuweko katika mkataba ili mali yake isije ikapotea, huku akimuweka Mwenyezi Mungu mbele ya macho yake, aelewe ya kwamba Mwenyezi Mungu anashuhudia kila kitu: “Na amwogope Mwenyezi Mungu Mola Wake; wala asipunguze chochote katika deni.”
7.
Iwapo mdaiwa ana upungufu fulani wa akili au si mwenye kusimamia mali yake vizuri, au akiwa ni bubu au kiziwi, basi msimamizi wake (walii) ndiye atakayekuwa na wajibu wa kueleza namna ya kuandika mkataba mbele ya 71
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 71
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
mwandishi: “Na kama yule ambaye juu yake iko haki ni mpumbavu au mnyonge au yeye hawezi kuandikisha mwenyewe, basi na aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu.” 8.
Ni juu ya walii wakati wa kueleza namna ya kuandikwa mkataba akubali juu ya kudaiwa mtu anayemsimamia, afanye hivyo kwa uadilifu kwa kulinda haki ya mtu anayemwakilisha na kujiepusha na aina yoyote ya dhulma: “Basi na aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu.”
9.
Licha ya kuandikwa mkataba, ni juu ya pande hizo mbili kuweka mashahidi wawili watakaoulinda mkataba huo pindi ikitokea kutoelewana: “Na muwashuhudishe mashahidi wawili.”
10. Ni wajibu mashahidi wawe ni Waislamu wawili wanaume waliobaleghe, haya tunayashuhudia katika ibara isemayo: “Katika watu wenu waume.” Inamaanisha watu walio katika Dini yenu. 11. Inafaa kuweka shahidi mmoja mwanamume na mashahidi wawili wanawake: “Kama hakuna wanaume wawili, basi ni mwanamume mmoja na wanawake wawili.” 12. Ni wajibu kuchagua mashahidi waadilifu na wanaokubalika kila upande: “Katika wale mnaowaridhia kuwa mashahidi.” Bila ya shaka hakuna anayeridhika na mtu asiye mkweli na mwaminifu. 13. Ikiwa mashahidi wote ni wanaume wawili, anatakiwa kila mmoja atoe ushahidi wake peke yake, ama akiwa ni mwanamme mmoja na wanawake wawili, ni juu ya wanawake hao wawili kutoa ushahidi wao wakiwa pamoja, ili mmoja amkumbushe mwenzake pindi atakaposahau au kukosea. 14. Ama sababu ya kuzingatiwa ushahidi wa wanawake wawili kulingana na ushahidi wa mwanamme mmoja ni kwa sababu ya maumbile ya mwanamke ambayo huathirika zaidi na vichocheo au vitisho, kwa hivyo kuwepo kwao pamoja ni kizuizi kikubwa cha kutokea mambo haya: “ili kama mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwingine. “ 15. Ni wajibu kwa mashahidi kuhudhuria tena bila ya kuchelewa, pale watakapohitajika kwenda kutoa ushahidi: “Na mashahidi wasikatae waitwapo.” 16. Ni wajibu kuandikwa deni likiwa kubwa au dogo, kwani Uislamu hautaki patokee mizozo ya aina yoyote hata katika biashara ndogo ndogo, ambayo huenda ikiwa ni sababu ya kupatikana mizozo mikubwa kati ya Waumini: 72
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 72
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
“Wala msichoke kuliandika deni likiwa dogo au kubwa, mpaka muda wake.” 17. Ikiwa biashara ya aina yoyote itafanywa kwa njia ya mkono kwa mkono (kulipa taslim), hakuna umuhimu wowote wa kuandikiana: “Ila ikiwa ni biashara ya mkono kwa mkono mnayopeana baina yenu, basi si vibaya kwenu msipoandika.” Ibara hii pia inatoa umuhimu wa kuandikiana kwenye biashara isiyo ya mkopo, ya mkono kwa mkono, ili kuondosha mizozo inayotarajiwa kutokea baadaye, ila hakuna kosa lolote ikiwa wataacha kuandikiana. 18. Muamala wa kibiashara usiokuwa na mkopo kinachohitajiwa ni kuwepo mashahidi wakati wa kutekeleza muamala huo: “Na wekeni mashahidi mnapouziana.” 19. Inapasa kwa mwandishi na mashahidi kulindwa ili wasisibiwe na madhara yoyote kwa sababu ya kutekeleza kazi na wajibu wao kwa uadilifu na haki: “Wala asitiwe tabu mwandishi wala shahidi.” Aya inamalizia kusema ya kwamba ikiwa mashahidi na waandishi watafanyiwa njia yoyote ya maonevu kwa sababu ya ukweli wao, basi jambo hilo ni kosa kubwa linalomtoa mja katika imani thabiti ya kumwamini Mwenyezi Mungu, hasa ikizingatiwa kwamba Aya hii imeanza kwa kuwaita na kuwahutubia Waumini: “Na mkifanya hivyo, basi hakika hilo ni ufasiki kwenu.” Aya inahitimisha kwa kuwataka Waumini kumcha Mwenyezi Mungu kwa kushikamana na maamrisho Yake na kuachana na kila alilolikataza, kwani Yeye anaelewa vyema taratibu na kanuni wanazozihitaji waja Wake, na pia anaelewa kila kilicho na maslahi kwao na kile chenye madhara: “Na mcheni Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anawaelimisha; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi kwa kila kitu.”
UTAFITI: 1.
Hukumu na kanuni madhubuti zilizobainishwa katika Aya hii iliyo ndefu kuliko zote, inabainisha kwa uwazi namna Dini ya Kiislamu ilivyoupa kipaumbele uchumi kwa Waislamu, hasa ikizingatiwa ya kwamba Kitabu hiki (Qur’ani) kiliteremshwa katika jamii iliyokuwa nyuma kielimu, kwani hata suala la kujua kuandika na kusoma lilikuwa ni nadra kujulikana, na hata Mtume mwenyewe hakuwa ni mwenye kupata mafunzo hayo, lakini jambo 73
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 73
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
limekuwa ni dalili ya wazi juu ya ukweli wa Qur’ani na utukufu wake kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine limeonesha juu ya uchumi kwa Waislamu. li ibn Ibrahim, katika Tafsiri yake (Tafsirul Qummiy) anasema: “Imepokewa A ya kwamba, katika Suratul Baqara kuna hukumu mia tano za Kiislamu, na katika Aya hii kuna hukumu kumi na tano.”42 Bila ya shaka umeshajionea mwenyewe ndugu msomaji ya kwamba tumebainisha hukumu kumi na tisa, bali ikiwa mtu atazama zaidi anaweza kubaini zaidi ya hizo, kama alivyobainisha Fadhil Miqdad katika kitabu chake Kanzul-Irfan hukumu ishirini na moja, kwa hivyo huku kutajwa hukumu kumi tano, ukweli wa mambo ni zaidi ya hizo, ila kilichofanywa ni baadhi ya hukumu kuingizwa ndani ya hukumu nyingine. 2.
Ibara isemayo: “Na mcheni Mwenyezi Mungu” Na ibara isemayo: “Na Mwenyezi Mungu anawaelimisha,” licha ya ibara hizi mbili kila moja kutajwa kivyake vyake kwa ibara moja kuunganishwa na ibara nyingine, lakini kwa kuweka karibu ibara hizi ni dalili ya kuwepo mafungamano ya hali ya juu kati yao, maana ya ibara hizi ni kwamba uchaji Mungu na unyenyekevu ni vitu visivyoweza kufikiwa pasi na mja kuwa na maarifa kamili ya Dini yake.
Aya ya pili katika maudhui haya, inakamilisha utafiti wa Aya iliyotangulia, nayo imekusanya vipengele vya sheria vifuatavyo: 1.
Ikiwa pande mbili zinataka kuingia katika mkataba wa biashara ambayo upande mmoja hautolipa wakati wa kuuziana, bali utanunua kwa mkopo, ikiwa hakutakuwa na mtu wa kuandika, kwa mfano wakiwa katika safari, wakati huu yule anayetaka kukopa itampasa aweke rahani ili mkopeshaji awe na matumaini ya kurejeshewa haki yake: “Na kama mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, basi ni rahani itakayokabidhiwa.” uelezwa hukumu ya kuwekwa kitu rahani katika safari, haimaanishi ya K kwamba katika mazingira yasiokuwa ya safari haifai mtu kuweka rahani pindi atakapohitaji kukopa, kwani imepokewa ya kwamba, Mtume (s.a.w.w.) aliweka rahani nguo yake ya kivita kwa Myahudi wakati alipohitaji mkopo wa fedha wakati akiwepo katika mji wa Madina.
42
Tafsirul Qummiy, Jz.1, Uk.94 74
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 74
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
2.
Ni wajibu rahani ibakie kwa mkopeshaji mpaka pale atakapolipwa haki yake au atakapokuwa na matumaini ya kulipwa: “basi ni rahani itakayokabidhiwa.”
3.
Hukumu zote hizi zilizotajwa, kama vile kuandikwa mkataba, kushuhudisha, kuwekwa rahani na nyinginezo, zinatakiwa zitekelezwe pindi panapokosekana uaminifu kati ya pande mbili, ama ikiwa kutakuwa na kuaminiana itakuwa hakuna haja ya hukumu hizo, na ni juu ya mdaiwa kuheshimu kuaminiwa kwake kwa kulipa deni la watu katika wakati waliokubaliana, na wala asisahau suala zima la uchaji Mungu: “basi aliyeaminiwa atekeleze uaminifu wake na amche Mungu, Mola Wake.”
4.
Wale ambao watakuwa na habari juu ya haki za wengine, itawapasa waitikie wito pindi watakapoitwa kwenda kutoa ushahidi na wala wasiufiche ukweli, kwani kuficha ushahidi ni katika madhambi makubwa: “Wala msifiche ushahidi. Na atakayeuficha, basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini.” Suala la kwenda kutoa ushahidi juu ya kitu fulani litakuwa ni jambo la wajibu kwa mtu ikiwa njia nyingine zitashindikana kuthibitisha haki za wengine. Aya inamalizia kwa kusisitiza kuchunga amana na haki za wengine: “Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi kwa mnayoyatenda.”
75
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 75
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA MBILI
َ ين آ َمنُوا إِ ْن تُ ِطيعُوا َف ِر ًيقا ِم َن الَّ ِذ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اب َ ين أُوتُوا ْال ِك َت ُ ون َوأَ ْنتُ ْم تُ ْتلَىٰ َعلَي ُ َي ُر ُّد َ ين َو َكي َ ْف َت ْك ُف ُر َ وك ْم َب ْع َد إِي َما ِن ُك ْم َكا ِف ِر ْك ْم ُ ات اللهَِّ َو ِف ُ آ َي اط ٍ ص َر ِ ٰص ْم ِباللهَِّ َف َق ْد ُه ِد َي إِلَى ِ يك ْم َر ُسولُ ُه َو َم ْن َي ْع َت َ يم ٍ ُم ْست ِق “Enyi mlioamini! Mtakapotii kikundi katika watu wa Kitabu watawarudisha kuwa makafiri baada ya kuamini kwenu. Na vipi mnakufuru na nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu na Mtume wake mnaye? Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu basi ameongozwa katika njia iliyonyooka.” (Qur’ani 3:100-101)
Kama tulivyoeleza mwanzo ya kwamba lengo kubwa la kitabu chetu hiki ni kukusanya Aya zote zinazotoa wito kwa Waumini na hukumu nyingine zilizomo katika Aya zinazofuatia, katika Aya hizi mbili zilizoko mbele yetu nazo ni katika mtiririko wa Aya hizo, lakini lengo halisi la Aya hizi hatutaweza kulifikia kwa usahihi mpaka tuzijumuishe Aya mbili zilizo kuja kabla ya hizi, Aya hizo ni hizi zifuatazo:
ْ َ َ ُْ َ اب لِ َم َت ْك ُف ُر ات اللهَِّ َواللهَُّ َش ِهي ٌد َعلَىٰ َما ِ ون ِبآ َي ِ قل َيا أ ْهل ال ِك َت ْ ون ُق ْل َيا أَ ْه َل َ َ ْ ُّ َ َ َُت ْع َمل يل اللهَِّ َم ْن آ َم َن ب س ن ع ون د ص ت م ل اب ت ك ال ُ َ َ ِ ِ َ ِ ِ ِ َ َُت ْب ُغو َن َها ِع َو ًجا َوأَ ْنتُ ْم ُش َه َدا ُء َو َما اللهَُّ ِب َغا ِف ٍل َع َّما َت ْع َمل ون “Sema: Enyi watu wa Kitabu! Kwa nini mnazikanusha ishara za Mwenyezi Mungu na hali Mwenyezi Mungu ni shahidi juu ya muyatendayo? Sema: Enyi watu wa Kitabu! Kwa nini mnawazuilia njia ya Mwenyezi Mungu walioamini, mkaitafutia kosa na nyinyi mnashuhudia? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na muyatendayo.” (Surat Aal Imraan 3:98-99)
Aya hizi nne zinasababu moja iliyosababisha kuteremshwa kwake, sababu hiyo ni kama ifuatayo:
76
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 76
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
Ni kwamba Sha-as ibn Qaysi ambaye alikuwa ni mzee na mtu mzima wa Kiyahudi, mzee huyo alikuwa amebobea katika ukafiri na alikuwa na chuki na hasadi kubwa dhidi ya Waislamu, siku moja alipita katika kikundi cha Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) wa kabila la Awsi na Khazraji, Maswahaba hao walikuwa wamekusanyika na kuzungumza mambo mbali mbali kati yao, Sha-as bin Qaysi hakufurahishwa na hali ile ya watu hao kukaa pamoja na wenye kushikamana na kupendana kati yao, baada ya kuishi katika vita na uhasama wa miaka mingi katika zama za ujahilia, Sha-as alisema: “Watu wa Bani Qaytati wamekusanyika katika mji huu, kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa kukusanyika kwao pamoja, sisi hatutakuwa ni wenye kubakia katika mji huu.” Kutokana na khofu yake hiyo alimwamrisha kijana wa Kiyahudi aliyekuwa pamoja naye, kwa kumwambia: “Nenda ukakae pamoja nao, na kisha uwakumbushe siku ya ‘Biath’ (Siku iliyotokea vita vikali kati ya Awsi na Khazraj na walioshinda ni Awsi, na kiongozi wa Awsi wakati huo alikuwa akiitwa Hadhir bin Samaak al Ash-haliy, na kiongozi wa Khazraji alikuwa akiitwa Amru Annu-uman al Bayadhiy na wote waliuwawa siku hiyo), yule kijana alifanya kama alivyoagizwa na Sha-as, baada ya Awsi na Khazraj kusikia habari hiyo walianza kugombana na kila kundi likijifakharisha juu ya kundi jingine, kulitokea watu wawili kutoka kila upande wakishambuliana kwa maneno makali na kila mmoja akimtishia mwenzake maisha, hali ilikuwa mbaya kiasi ya kupelekea kuibuka tena upya moto wa vita kati ya makabila hayo mawili. Ilipomfikia Mtume (s.a.w.w.) habari ya tukio hilo, alitoka pamoja na Maswahaba wake Muhajirina na wakawaendea, na aliwaambia: “Enyi Waislamu! Muogopeni Mwenyezi Mungu, mnaitikia wito wa kijahilia na ilhali mimi niko pamoja nanyi, baada ya Mwenyezi Mungu kukuongoweni kwenye Uislamu na akakutukuzeni kwao, na akakuondosheni mambo ya kijahilia kwa kupitia Uislamu, na kukuokoeni kutokana na ukafiri, na akaziunganisha nyoyo zenu?” Kutokana na maneno hayo ya Mtume (s.a.w.w.), watu walitambua ya kwamba yaliyotokea yalitokana na ushawishi wa shetani na vitimbi vya maadui wao, hapo walilia na ikawa watu wa Awsi na Khazraj wanakumbatiana wao kwa wao. Baada ya hapo waliondoka pamoja na Mtume (s.a.w.w.) hali ya kuwa ni wasikivu wa maneno yake na watiifu wa amri zake, Mwenyezi Mungu aliwaepushia vitimbi vya adui huyo wa Mwenyezi Mungu (Sha’s ibn Qaysi). Kutokana na tukio hilo ndipo Mwenyezi Mungu alipoteremsha Aya hizi nne, mbili zinahusiana na tukio la Sha-as bin Qaysi na vitimbi vyake, na mbili zinatoa tahadhari kwa Waumini wote dhidi ya kuwatii wasiokuwa wao.43 43
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 2, Uk. 613 77
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 77
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
Tukirejea katika Aya ya 100 na 101 ambazo ndizo tulizozilenga zaidi katika maudhui ya kitabu hiki, ni kwamba baada ya kuona sababu ya kuteremshwa Aya hizi, tunajifunza ya kwamba lau kama Waislamu wa kabila la Awsi na Khazraj wangeendelea na mzozo wao ambao ulifikia pahala pa kutishiana maisha na kurudi katika kufanya mambo waliyokuwa wakiyafanya katika zama za kijahilia, basi natija yake ni kurudi katika ukafiri. Kwa hivyo huu ni wito kwa kila Muumini kuacha kufuata na kutii amri ambazo zitapelekea kumuasi Mwenyezi Mungu, na baadi ya dhambi hizo zinapelekea katika ukafiri, kama mtu kuamrishwa kuua mtu asiyestahiki kuuliwa kisheria, au jambo litakalopelekea watu kuuwana, kwani hili ni miongoni mwa makosa makubwa mno, Mwenyezi Mungu anasema:
َُّض َب الله ِ َو َم ْن َي ْقتُ ْل ُم ْؤ ِم ًنا ُم َت َع ِّم ًدا َف َج َزا ُؤ ُه َج َهنَّ ُم َخالِ ًدا ِفي َها َو َغ َعلَ ْي ِه َولَ َع َن ُه َوأَ َع َّد لَ ُه َع َذابًا َع ِظي ًما “Na mwenye kumuua muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo; na Mwenyezi Mungu amemughadhibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa.” (Qur’ani 4:93).
Katika ulimwengu wetu huu wa leo ni mara ngapi tunasikia viongozi walio Waislamu wakiwaamrisha askari wao kuwauwa raia wake kwa sababu zisizo na msingi au uzito wowote katika mizani ya kiubinadamu, wanapika mambo fulani fulani ili raia wasifahamiane na hatimaye raia hao wanaingia katika mizozo na mauwaji ya wenyewe kwa wenyewe ili hao watawala wazidi kubakia madarakani kwa kujinufaisha na jasho la wengine. Kwa mujibu wa Aya hii ni wazi kwamba Muumini anapomtii mtu mkorofi na mwingine asiye na Dini ni kurejea katika ukafiri wa kikweli kweli na kujiengua kikamilifu kutoka katika Uislamu, kwani imani ya kweli haizai isipokuwa mapenzi na mshikamano na maelewano, kama ilivyo kwa ukafiri hauzai isipokuwa ukatili, mauwaji na kufarikiana. Aya ya mwisho inauliza kwa mshangao mkubwa, “Na vipi mnakufuru na nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake mnaye?” Yaani ni vipi nyinyi mnafuata njia na mifumo ya kikafiri katika maisha yenu na ilhali bado Mtume (s.a.w.w.) yupamoja nanyi na Aya za Mwenyezi Mungu zinasomwa na mnazisikia na mionzi ya nuru ya Wahyi inapenya katika nyoyo zenu?! 78
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 78
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa kweli ni jambo linalostaajabisha na kuacha mshangao wa hali ya juu kwa watu hawa wanaoishi katika nuru na mwanga kuweza kufanya mambo yatakayowapelekea kurudi katika ukafiri, na bila shaka wao watakuwa wahusika wakubwa wa kutumbukia katika shimo la upotevu, kwani watakuwa wamepotea baada ya kubainishiwa uongofu ulio wazi kwa kusomewa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuwa na Mtume (s.a.w.w.) miongoni mwao, kwa hivyo pasi na shaka adhabu yao itakuwa ni kali mno na yenye kuumiza. Mwisho wa Aya Mwenyezi Mungu anawaeleza Waislamu njia ya kuifuata ili wasalimike na ushawishi na wasiwasi wa maadui na hatima yake kuelekea katika njia ya sawa na iliyonyooka, jambo hilo ni kushikamana na Mwenyezi Mungu kwa kufuata mafunzo yake na kuachana na kila alilolikataza, kwa hivyo analieleza jambo hili kwa uwazi kwa kusema: “Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu basi ameongozwa katika njia iliyonyooka.”
MAZINGATIO: Kitu cha kuzingatia katika Aya hizi, ni kwamba katika Aya mbili za mwanzo (Aya 98 na 99) Mwenyezi Mungu anawahutubia Mayahudi kwa kupitia Mtume Wake (s.a.w.w.), kwani Mwenyezi Mungu amemtaka Mtume Wake ayafikishe mafunzo haya kwa Mayahudi kwa kutumia ulimi wake, kwani Mwenyezi Mungu amemwambia Mtume Wake aseme na kuwaita watu waliopewa kitabu (Mayahudi na Manasara): “Sema: Enyi Watu wa Kitabu!” Lakini wakati alipoelekeza wito wake kwa Waumini, kama ilivyo katika Aya mbili za Mwisho, Mwenyezi Mungu aliwahutubia moja kwa moja, bila ya kumtuma Mtume Wake awaambie kwa kusema: Enyi Waumini, hii ni dalili ya wazi jinsi Mwenyezi Mungu anavyowapa kipaumbele waja Wake waliomuamini, kwani wao si kama waja wengine, kwa hivyo wanastahiki kuwa na mwito wao maalumu, nao ni kuwaita moja kwa moja pasi na kuwa na mwingine kati yake Yeye (Mwenyezi Mungu) na waja Wake Waumini.
79
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 79
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA TATU
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين آ َمنُوا اتَّ ُقوا اللهََّ َح َّق تُ َقا ِت ِه َو اَل َت ُموتُ َّن إِ اَّل َوأَ ْنتُ ْم َ ُم ْسلِ ُم ْ ون َو ْل اللهَِّ َج ِميعًا َو اَل َت َف َّر ُقوا َو ْاذ ُك ُروا ِ اع َت ِ ص ُموا ِب َحب ُُ َ ف َبي ُ ِن ْع َم َت اللهَِّ َعلَي َ َّْك ْم إِ ْذ ُك ْنتُ ْم أَ ْع َدا ًء َفأَل ص َب ْحتُ ْم ْ َوب ُك ْم َفأ ِ ْن قل َِّب ِن ْع َم ِت ِه إ ْخ َوا ًنا َو ُك ْنتُ ْم َعلَىٰ َش َفا ُح ْف َر ٍة ِم َن الن ار َفأَ ْن َق َذ ُك ْم ِم ْن َها ِ ِ ُ ُ َك َ ٰذلِ َك يُ َبي َ ون َو ْل َت ُك ْن ِم ْن ُك ْم أ َّم ٌة َي ْد ُع َ ِّن اللهَُّ لَ ُك ْم آ َيا ِت ِه لَ َعلَّ ُك ْم َت ْه َت ُد ون ْ إلَى َ َ ْر َو َي ْأ ُم ُر وف َو َي ْن َه ْو َن َع ِن ْال ُم ْن َك ِر َو ُأو َٰل ِئ َك ي خ ال ُ ون ِب ْال َمع ِ ْر ِ ِ َّ ْ ُ ُ َ ُ ْ ْ ين َت َف َّرقوا َو َ ون َو اَل َتكونُوا َكال ِذ َ ُه ُم ال ُمفلِ ُح اخ َتلفوا ِم ْن َب ْع ِد َما ُ َجا َء ُه ُم ْال َبيِّ َن ٌ ول ِئ َك لَ ُه ْم َع َذ اب َع ِظي ٌم ٰ َ ُات َوأ “Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu ipasavyo kumcha; wala msife isipokuwa mmekuwa Waislamu. Na Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarikiane; na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu mlipokuwa maadui, naye akaziunganisha nyoyo zenu; hivyo kwa neema yake mkawa ndugu; na mlikuwa ukingoni mwa shina la moto naye akawaokoa nalo. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyozibainisha Aya Zake ili mpate kuongoka. Na liwepo miongoni mwenu kundi lenye kulingania kwenye kheri, na kuamrisha mema na kukataza maovu. Na hao ndio wenye kufaulu. Wala msiwe kama wale waliofarakana wakahitalifiana baada ya kuwajia wao dalili zilizo wazi; na hao ndio wenye adhabu kubwa.” (Qur’ani 3:102-105)
SABABU YA KUTEREMKA Makabila mawili makubwa ya Awsi na Khazraji yaliyokuwa yakiishi katika mji wa Madina, waliishi katika hali ya vita vya umwagaji damu mkubwa na mizozo kwa muda unaokaribia miaka mia moja, vita vikali vilikuwa vikitokea mara kwa mara kati yao, ambavyo vilichukua roho za watu wengi kwa kila upande na pia kusababisha hasara kubwa ya mali, uhalifu wa aina hiyo ulitokea wakati wa zama za kijahilia na kabla ya kudhihiri mwanga wa uongofu katika mji wao, lakini hali hiyo ilibadilika 80
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 80
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
na kupotea mara tu baada ya kuchomoza nuru ya Uislamu kwa kupitia mafunzo ya Mtume (s.a.w.w.) na kwa hekima zake. Na katika Aya zilizopita tumejionea ni namna gani moto wa ikhtilafu na mizozo ulivyokuwa ukitaka kujirudia kuwaka tena kutokana na vitimbi na mikakati ya maadui dhidi yao. Aya hizi zinaelezea aina nyingine ya mizozo iliyojitokeza baada ya wao kuingia katika Uislamu, mizozo hiyo ilisababishwa na baadhi ya watu miongoni mwao, watu hao bado walikuwa na mabaki ya hali ya majivuno na kujifakharisha juu ya wengine. Inasemekana ya kwamba: Watu wawili kutoka katika makabila ya Awsi na Khazraji walijifakharisha, watu hao ni Tha-ala bin Ghanam na As-ad bin Zurara, alisema Tha-ala: “Watu hawa wanatokana na kabila letu: Khuzayma bin Thabit aliye na shahada mbili, Handhala ambaye alioshwa na Malaika, Aasim bin Thabit bin Aflah yeye ni muhami wa Dini na Sa-ad bin Muadh ambaye Mwenyezi Mungu aliridhika na hukumu yake kwa watu wa Bani Quraydha.” As-ad naye alisema: “Sisi tuna watu wanne waliokuwa na ujuzi wa kuzitolea hukumu Aya zilizomo katika Qur’ani: Ubayya ibn Ka’b, Muadh ibn Jabal, Zayd ibn Thabit na Abu Zayd, na pia tunaye Saad ibn Ubadah khatibu wa Maansari na raisi wao.” Mazungumzo yao hayo ya kujifakharisha yaliishia kwa kugombana na kusababisha mzozo mkubwa na kila mmoja wao aliwaita watu wa kabila lake huku wakiwa na silaha, habari ilpomfikia Mtume (s.a.w.w.) alipanda punda wake na akawaendea, na ndipo hapo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hizi, na baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuwasomea walipatana na kufikia suluhu.44
MAELEZO: Aya ya mwanzo kati ya Aya hizi inawataka Waumini kushikamana na uchaji Mungu, kwani ndio utangulizi wa udugu na umoja kati yao. Ukweli wa mambo ni kwamba ulinganiaji usiokuwa na misingi ya uchaji Mungu na misingi sahihi ya imani na itikadi, faida yake ni ndogo mno ikiwa utakuwa na faida. Kwa hivyo Aya hii inatoa suluhisho kamili la kuondosha mizozo na migongano katika jamii, suluhisho ni imani na uchaji Mungu, hii ndio sababu Qur’ani Tukufu ikawaelekea Waumini kwa kuwaambia: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu ipasavyo kumcha.” Jambo la msingi tunalopaswa kulielewa katika ibara isemayo: “ipasavyo kumcha.” ni kufikia daraja ya hali ya juu ya uchaji Mungu, nayo ni kuacha kila kilichokatazwa na kufanya yale yaliyoamrishwa kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume s.a.w. katika kuisherehesha ibara hii, alisema: 44
Kitabu kilichotangulia, Uk. 617 81
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 81
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
.أن يطاع فال يعصى ويذكر فال ينسى ويشكر فال يكفر “Ni kumtii Mwenyezi Mungu bila ya kuasiwa, na kukumbukwa pasi na kusahauliwa, na kushukuriwa pasi na kukufuriwa.”45
Wito wa Umoja: Baada ya Aya ya kwanza kuusia juu ya kushikamana na uchaji Mungu kwa dhati kabisa, Aya ya pili inawataka Waumini wazingatie juu ya suala la umoja, na kusimama kidete dhidi ya kila jambo litakalopelekea mzozo kati yao na mgawanyiko, Mwenyezi Mungu amesema kwenye Aya hii: “Na Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarikiane.” Suala la kujiuliza hapa ni hili, Ni ipi hiyo kamba ya Mwenyezi Mungu? Wafasiri wamekuja na jawabu mbali mbali kuhusiana na suala hili, baadhi yao wamesema ya kwamba ni Qur’ani, na baadhi yao wamesema ya kwamba ni Uislamu, na baadhi yao wamesema ya kwamba ni Maimamu Watoharifu watokanao na kizazi cha Bwana Mtume (s.a.w.w.). Maana hizi zote zimeelezwa katika Riwaya zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Ahlul Bayti wake (a.s.),licha ya kuwa na maana mbali mbali, lakini maana hizi hazina pingamizi yoyote, kwani maana halisi ya kamba ya Mwenyezi Mungu ni kuchukua mafunzo kutoka katika Qur’ani Tukufu na viongozi waongofu, kwani mafunzo yao ndio yanayowatoa watu katika upotevu na kuwafikisha katika uongofu. Maadui wa Jana Leo ni Marafiki: Baada ya Aya kuwaelezea Waumini juu ya suala la kushikamana na Mola Wao, ibara inayofuata inawakumbusha neema kubwa ya umoja na udugu walioufikia baada ya kuishi katika maisha ya chuki na uhasama kwa muda mrefu, kwa hivyo Aya inawataka wajikumbushe hali hiyo mbaya waliokuwa wakiiishi na kisha walinganishe na hali yao ya hivi sasa iliojengeka katika misingi ya umoja, udugu na mapenzi: “Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu mlipokuwa maadui, naye akaziunganisha nyoyo zenu; hivyo kwa neema yake mkawa ndugu.” Katika Aya hii kuna kitu kikubwa cha kuzingatia, nacho ni kukaririwa mara mbili neno ‘Neema’ hii ni kuashiria umuhimu mkubwa wa Waumini kuwa kitu kimoja, 45
Suyitiy, Jz. 2, Uk. 59 82
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 82
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
na neema hii haipatikani isipokuwa katika mafunzo ya Uislamu na kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Jambo jingine la kuzingatia ni kwamba Mwenyezi Mungu amejinasibisha Yeye mwenyewe kwamba Ndiye aliyeziunganisha nyoyo za hao waliokuwa mahasimu kwa kipindi kirefu. Kutokana na hali hii, Qur’ani inathibitisha kutokea kwa muujiza mkubwa wa kijamii katika historia ya Kiislamu, kwani tunapoiangalia jamii ya watu wa Makka na Madina ilivyokuwa na maisha ya kijahilia waliyokuwa wakiishi, maisha yaliyogubikwa na uadui, chuki, hasadi iliyokuwa imeota mizizi katika nyoyo zao, mizozo na kila aina ya dhulma, ilitosha jambo moja dogo sana kuwa ni sababu ya kutokea mauwaji ya kinyama. Dhulma za aina hii pia zilichangiwa na ujinga uliokuwa umekithiri na kuwazunguka kila upande, watu wa aina hii ni vigumu kusahau kitu kidogo, seuze mambo makubwa ya umwagaji damu waliyoyafanya. Kutokana na hali yao ya kijamii kubadilika, kwani hatimaye walikuwa wamoja kama ndugu wa damu na kusameheana kwa yote yaliyopita, hapa ndipo unapodhihirika muujiza huo ulioletwa na Uislamu, kwani mabadiliko hayo yaliyotokea ilikuwa si rahisi kuweza kutokea lau kama si kwa kutumika njia ya kiroho na imani thabiti juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hali ya watu hao ilikuwa ni mbaya kupita kiasi, mpaka Qur’ani Tukufu ikieleza hali yao hiyo kwamba wameifikisha jamii yao pembezoni mwa shimo na wakati wowote watatumbukia ndani yake: “Na mlikuwa ukingoni mwa shina la moto naye akawaokoa nalo.” Kwa mujibu wa ibara hii Mwenyezi Mungu anawataka wakumbuke ile hali yao mbaya ya maisha yao ya kijamii ilivyokuwa, ni kwamba walifikia pahala pa kujiweka katika kuitafuna na kuimaliza jamii yao kutokana na tabia zao chafu, na ilikuwa ni wakati wowote wakitarajiwa kulifikia hilo janga la maangamizi, lakini Mwenyezi Mungu aliwaokoa kutokana na janga hilo, na badala yake akawapa utulivu baada ya kuishi katika hofu, na badala ya kuanguka aliwanyanyua na kuwakirimu, na mwisho aliwaongoa na kuwapelekea imani na amani na kuwafanya kuwa ndugu walioshikana. Katika kutilia mkazo zaidi umuhimu wa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu, na kuwa na mazingatio juu ya matukio yaliyopita na yaliyopo,Mwenyezi Mungu anamalizia Aya kwa kusema: “Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyozibainisha Aya Zake ili mpate kuongoka.” Kwa hiyo lengo la msingi ni kuokolewa nyinyi dhidi ya kila aina ya maangamizi na kuongozwa katika njia ya amani na salama, na kwa vile katika haya kuna manufaa kwenu, basi ni juu yenu kuyashika vizuri haya yote mliobainishiwa.
83
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 83
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
Umuhimu wa Umoja: Licha ya mengi yaliyosemwa kuhusiana na faida kubwa ya kimaendeleo na ya kijamii inayopatikana katika taifa kwa sababu ya kuungana kwao na kushikamana kwa pamoja, yamkinika kusema ya kwamba faida ya suala hili (umoja) bado hazijaeleweka kama itakikanavyo. Leo ulimwengu unashuhudia mabwawa mengi yaliyojengwa katika sehemu mbali mbali, mabwawa haya yamekuwa ni tegemeo kubwa la viwanda vikubwa vikubwa kutokana na nguvu za umeme zinazozalishwa humo, maji yaliyohifadhiwa humo yalikuwa yakipotea bure katika zama zilizopita, ama leo ni vyanzo muhimu vya nishati, kama yanavyotumika maji hayo katika umwagiliaji mashamba. Ikiwa tutakaa na kufikiri, tutagundua ya kwamba mkusanyiko huo mkubwa wa maji haukufanyika isipokuwa ni kwa matone madogo madogo ya maji ya mvua. Kutokana na mfano huu kila mtu sasa ataweza kudiriki ni umuhimu gani wa watu kuungana na kuwa kitu kimoja. Hadithi nyingi zimepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu watoharifu zikielezea umuhimu wa udugu na umoja katika Uislamu. Miongoni mwa hadithi hizo ni kama zifuatazo: Anasema Mtume s.a.w.w:
ّ .إن المؤمن للمؤمن كالبنيان يش ّد بعضه بعضا “Muumini kwa Muumini mwenzake ni kama jengo, linashikana lenyewe kwa lenyewe.”46
.المؤمن كالنّفس الواحدة “Waumini ni kama nafsi moja.”
مثل المؤمنين في توا ّدهم وتراحمهم كمثل الجسد الواحد إذا .بالسهر والح ّمى ّ اشتكى بعضه تداعى سائره “Mfano wa Waumini katika kupendana kwao na kuoneana kwao huruma, ni kama kiwiliwili kimoja, ikiwa kiungo kimoja kitasumbuliwa na ugonjwa, basi viungo vyote vitaumwa na kukesha.”47 46 47
Bukhariy, Sahihul Bukhariy, Jz. 1, Uk. 123 Muslim, Sahihu Muslim, Jz. 8, Uk. 20 84
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 84
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
Kutetea haki na Kuung’oa Ufisadi: Baada ya maelezo marefu ya Aya zilizopita, bado Mwenyezi Mungu anawaita waja Wake walioamini katika kutekeleza kazi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya: “Na liwepo miongoni mwenu kundi lenye kulingania kwenye kheri, na kuamrisha mema na kukataza maovu.” Kwa hakika suala la kuamrisha mema na kukataza mabaya ni kinga kubwa ya kuikinga jamii dhidi ya masaibu mbali mbali. Kukosekana kwa kazi hii kunatoa nafasi ya kuzorotesha umoja katika jamii kidogokidogo, ni kama vile mchwa wanavyolitafuna gogo kwa ndani, kwa hivyo hakuna budi kuendelea kazi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya, ili umoja wa Kiislamu uzidi kuimarika vizuri. Pia Aya hii imesisitiza hukumu hizi mbili zilizo wajibu kwa Waumini, kutaka yawe ni mambo yanayotendwa mara kwa mara, kwani mambo haya ndio rahani ya kufanikiwa kwa umma wa Kiislamu: “Na hao ndio wenye kufaulu.” Pia Mtume (s.a.w.w.) amepiga mfano mzuri wa mafanikio inayoyapata jamii kwa kuwepo baadhi ya watu katika jamii kufanya kazi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya, anasema: “Mfano wa mtu ambaye anatekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu na yule anayekwenda kinyume chake ni kama mfano wa wasafiri wa jahazi katika bahari, ikawa kuna tabaka mbili; juu na chini, na wote wakabanwa na kiu kali, wale walioko chini wakawaambia wale walioko juu: Sisi tunataka kuitoboa jahazi ili tupate maji tunywe, ikiwa wale wa juu watawazuia mikono yao wataokoka wote, na kama wakiwaachia wataghariki wote.”48 Riwaya hii pia inaonesha ya kwamba suala la kuamrisha mema na kukataza mabaya ni suala lililo wajibu kwa mujibu wa akili hata kama kusingekuwa na maandiko yanayowajibisha kufanya hivyo. Umuhimu wa Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya Kuna Aya katika Qur’ani na Riwaya nyingi zinazoelezea umuhimu wa kazi hii iliyo wajibu katika jamii, na pia maandiko yameashiria mwisho mbaya kwa jamii inayoacha kazi hii, mingoni mwa maandiko hayo ni kama yafuatayo: Kutoka kwa Imam Baqir (a.s.) amesema: 48
Tirmidhiy, Sunan Tirmidhiy Jz. 3, Uk. 318 85
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 85
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
ّ بها,إن األمر بالمعروف والنّهي عن المنكر فريضة عظيمة ّ , وتر ّد المظالم,وتحل المكاسب , وتأمن المذاهب,تقام الفرائض . ويستقيم األمر, وينتضف من األعداء,وتعمر األرض “Kuamrisha mema na kukataza mabaya ni wajibu mkubwa, kutokana na kutekelezwa wajibu huu, ndio sababu ya kutekelezwa wajibu mwingine, na huyasalimisha madhehebu, na huufanya uchumi uwe wa halali, na ni sababu ya kurejeshwa vitu vilivyochukuliwa kwa dhulma, na huimarisha nchi, na ni usalama dhidi ya maadui na huufanya Uislamu usimame.”49
Mtume (s.a.w.w.) naye amesema:
فهو خليفة اهلل في,من أمر بالمعروف ونهي عن المنكر .أرضه وخليفة رسول اهلل وخليفة كتابه “Mwenye kuamrisha mema na kukataza mabaya atakuwa ni khalifa wa Mwenyezi Mungu katika ardhi yake, na khalifa wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na khalifa wa Kitabu chake.”50
Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alikuwa katika mimbari, mara akaendewa na mtu na kumuuliza: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani mtu aliye bora zaidi kwa watu? Mtume (s.a.w.w.) alisema:
.آمرهم بالمعروف وأنهاهم عن المنكر وأتقهم هلل وأرضاهم “Ni yule anayewaamrisha mema na kuwakataza mabaya, na mchaji wao zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.”51
Na katika Hadithi nyingine, Mtume (s.a.w.w.) amesema:
ّ ّ أو ليسل,لتأمرون بالمعروف وتنهون عن المنكر طن عليكم ّ سلطانا ظالما ال يجل كبيركم وال يرحم صغيركم وتدعوا Hurrul Amil, Wasailu Shia, Jz. 11, Uk. 395 Tha’labiy, Tafsiru Tha’labiy, Jz. 3, Uk. 123 51 Tabarasiy, Majma’ul Bayan, Jz. 2, Uk. 359 49 50
86
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 86
12/8/2014 2:43:37 PM
WITO KWA WAUMINI
خياركم فال يستجاب لهم وتستنصرون فال تنصرون .وتستغيثون فال تغاثون وتستغفرون فال تغفرون “Mtaamrisha mema na kukataza mabaya, au Mwenyezi Mungu atakutawalishieni mtawala dhalimu, asiyewaheshimu wakubwa wenu (wazee) na asiyewarehemu wadogo zenu, wale walio wema kati yenu wataomba na hawatokubaliwa, na mtaomba nusra na hamtonusuriwa, mtaomba msaada na hamtosaidiwa na mtaomba msamaha lakini hamtasamehewa.”52
Kutokana na msisitizo huu kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Ahlu Bayt wake juu ya kuamrisha mema na kukataza mabaya, ni ishara ya wazi kwamba kazi hii ndio roho ya jamii, na ni kazi inayotoa dhamana kubwa ya kubakia jamii katika hali ya usalama na kulinda heshima yake, na kutotekelezwa kazi hii ni sababu kubwa ya kuzorota hukumu za Mwenyezi Mungu na kuporomoka maadili ya watu. Je, Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya Kunamnyima Mtu Uhuru? Katika kulijibu suala hili, hakuna budi kusema ya kwamba mfumo wowote wa maisha wenye manufaa kwa jamii, ni kwa kila mwanajamii kuwa na uhuru wa kuwa na namna yake ya kuishi, lakini pamoja na hayo katika jamii hiyo haikosi kuwa na baadhi ya kanuni zinazowazuia watu kufanya kila walitakalo hata kama mambo hayo yana madhara madogo, utaratibu huu ndio uliofuatwa na wanadamu tangu zama za kale na hadi sasa, kwani hata zile nchi zinazodai kuwa na uhuru mkubwa wa haki za binadamu haziruhusu kufanyika kwa kila jambo.
52
Tha’labiy, Tafsiru Tha’labiy, Jz. 3, Uk. 123 87
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 87
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA NNE
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين آ َمنُوا اَل َتتَّ ِخ ُذوا ِب َطا َن ًة ِم ْن ُدو ِن ُك ْم اَل َي ْألُو َن ُك ْم َ َخ َب اًال َو ُّدوا َما َع ِن ُّت ْم َق ْد َب َد ِت ْال َب ْغ اه ِه ْم َو َما تُ ْخ ِفي ِ ضا ُء ِم ْن أَ ْف َو َ ُات إِ ْن ُك ْنتُ ْم َت ْع ِقل ون َها أَ ْنتُ ْم ُ ص ُد ُ ِ ور ُه ْم أَ ْك َب ُر َق ْد َبيَّنَّا لَ ُك ُم الآْ َي ُأ ُ ون ب ْال ِك َتاب ُكلِّ ِه َوإ َذا لَ ُق ُ ُحبُّو َن ُ ُ َا َا ُ َ ْ َ وك ْم ن م ؤ ت و م ك ي ل و م ه ن ُّو ب ح ت ء ول ُ ْ ْ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ َ ْْك ُم أ ُ ضوا َعلَي ُّ َقالُوا آ َمنَّا َوإِ َذا َخلَ ْوا َع ْظ ُق ْل ُموتُوا ِ ال َنا ِم َل ِم َن ْال َغي َ ْظ ُك ْم إ َّن اللهََّ َعلِي ٌم ب ُ ور إِ ْن َت ْم َس ْس ُك ْم َح َس َن ٌة َت ُس ْؤ ُه ْم د الص ات ذ ُّ ِ ِ ِ ِ ِ ِب َغي ُ صب ُ ص ِب ُروا َو َتتَّ ُقوا اَل َي ض ُّر ُك ْم ْ ْك ْم َسيِّ َئ ٌة َي ْف َر ُحوا ِب َها َوإِ ْن َت ِ َُوإِ ْن ت ٌ ون ُم ِح َ َُك ْي ُد ُه ْم َشي ًْئا إِ َّن اللهََّ ِب َما َي ْع َمل يط
“Enyi ambao mmeamini! Msiwafanye wasiri wenu wasiokuwa katika nyinyi. Hawazembei kuwaharibia. Wanapendelea yanayowapa mashaka. Imedhihiri chuki katika vinywa vyao, Na wayafichayo vifuani mwao ni makubwa. Tumewabainishia ishara ikiwa nyinyi ni wenye akili. Hivyo basi! Nyinyi ndio hao muwapendao hali wao hawawapendi, nanyi mwaviamini vitabu vyote. Na wakikutana nanyi husema: Tumeamini, na wanapokuwa faraghani huwaumia vidole kwa hasira. Sema: Kufeni na hasira zenu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa yaliyo vifuani. Ukiwagusa wema unawasononesha, na kama likiwapata baya wanalifurahia. Na kama mkisubiri na mkaogopa, basi hila zao hazitawadhuru kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyazunguka wayatendayo.” (Qur’ani 3:118-120)
SABABU YA KUTEREMKA Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas ya kwamba, Aya hizi ziliteremka pale baadhi ya Waislamu walipowaambia Mayahudi siri za Waaislamu, baada ya kupewa siri hizo, wale Mayahudi waliokuwa wakidhihirisha mapenzi kwa Waislamu walianza kazi ya kuwapeleleza na kufuatilia mienendo ya Waislamu, hapo ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hizi kwa lengo la kuwaonya Waislamu dhidi ya kuwafanya Mayahudi marafiki wa kuwapa siri zao, kwani ni watu wanaotarajiwa kufanya kila 88
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 88
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
wawezalo ili kuwadhuru Waislamu, kwa kuwapa siri kunaweza kurahisisha kufikia lengo lao hilo, kwa vile wao siku zote wanapenda kuwaona Waislamu wanaishi katika tabu na mashaka na kuwa mbali na mafunzo ya Dini yao.53
MAELEZO: Aya zinaashiria jambo muhimu sana katika maisha ya kijamii ya Waumini na wale wasiokuwa waumini, jambo hilo ni kukatazwa Waumini wasiwafanye wale wanaotofautiana nao kiimani kuwa ni wandani wao kwa kuwapa siri za mikakati yao walioipanga ihusianayo na Dini yao na maisha yao kwa ujumla, amesema Mwenyezi Mungu: “Enyi ambao mmeamini! Msiwafanye wasiri wenu wasiokuwa katika nyinyi.” Hii inamaanisha ya kwamba haifai kuwafanya makafiri marafiki, kama ilivyokuwa haifai kuwafanya wandani na kuwapa siri, kwasababu si watu wenye dhamana ya kutowatendea ubaya Waumini pindi wanapopata uwezo wa kufanya hivyo: “Hawazembei kuwaharibia.” Urafiki, ujirani na uhusiano wa damu uliopo kati ya Waumini na wasiokuwa waumini si sababu zinazowazuia makafiri kuwafanyia uadui Waumini na kuwatakia wafikwe na kila aina ya balaa, daima utawaona wanawachunguza na kuwapeleleza Waumini katika vitendo vyao na maneno yao, baada ya kusikia maneno kutoka kwa Waumini hapo ndipo zinapodhihiri chuki walizozificha vifuani mwao dhidi ya Waumini:” Imedhihiri chuki katika vinywa vyao.” Ukweli huu tunaushuhudia katika maneno ya Imam Ali (a.s.) pale aliposema:
ّ ما أضمر أحد شيئا إال ظهر في فلتات لسانه وصفحات وجهه “Mtu yeyote hatoficha kitu (moyoni mwake), isipokuwa atakidhihirisha kitu hicho katika ncha za ulimi wake na paji la uso wake.”54
Kwa kupitia Aya hizi, Mwenyezi Mungu amebainisha moja kati ya njia za kujulikana undani wa nafsi za maadui wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu anaendelea kuwaelezea ubaya wao: “Na wayafichayo vifuani mwao ni makubwa.” Yaani hayo yanayotokea vinywani mwao ni kama cheche zinazoruka kutoka katika moto mkubwa uliofichika ndani ya vifua vyao. Mwenyezi Mungu anazidi kusema: “Tumewabainishia ishara ikiwa nyinyi ni wenye akili.” Inamaanisha ya kwamba, suala la kuelezwa njia ya kuwatambua maadui hao, ni jambo lililo na umuhimu mkubwa ikiwa mtalizingatia jambo hili, ni Yeye Mwenyezi Mungu aliyekuwafikisheni kujua yale yanayofichwa 53 54
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 2, Uk. 660 Al-Majlisiy, Biharul Anwar, Jz. 105, Uk. 54 89
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 89
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
katika nyoyo za maadui dhidi ya usalama wenu, maisha yenu na mikakati yenu ya kimaendeleo.
Chuki Baada ya Upendo Baadhi ya Waislamu wanadhani ya kwamba wanaweza kuvuna upendo na mapenzi kutoka kwa maadui zao ikiwa wataonesha mapenzi juu yao, kwa kweli fikra hii ni batili na isiyo sahihi, anasema Mwenyezi Mungu:” Hivyo basi! Nyinyi ndio hao muwapendao hali wao hawawapendi, nanyi mwaviamini vitabu vyote.” Mwenyezi Mungu Mtukufu anawahutubia Waumini wenye tabia ya kuwapenda maadui wa Uislamu kwa kuwaambia: Nyinyi mnawapenda watu waliotofautiana nanyi katika Dini, kwa sababu tu ni ndugu zenu na majirani zenu, na mnawadhihirishia mapenzi ya hali ya juu na wakati wao hawakupendeni, na pia nyinyi mnaviamini vitabu vyao vyote walivyoteremshiwa na pia mnakiamini Kitabu kilichoteremshwa kwenu bila ya kuwepo tofauti yoyote kwenye imani yenu juu ya vitabu hivyo, lakini wao hawakiamini Kitabu chenu na wala hawaamini ya kwamba kimeteremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika kundi hili la baadhi ya ahlulkitabi (Mayahudi na Manaswara) wanafanya unafiki na kukudanganyeni, pale wanapokutana nanyi husema ya kwamba wao ni waumini, na wanapoondoka huuma vidole vyao kutokana na chuki ya hali ya juu wanayokuchukieni. Chuki ya aina hii waliyonayo haikuwadhuru Waislamu, bali iliwarejea wenyewe, ndio maana Mwenyezi Mungu akamuamrisha Mtume Wake awaambie: “Kufeni na hasira zenu!” Huu ndio undani wa makafiri ulivyo, undani ambao nyinyi Waumini mmeghafilika nao, lakini Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika nao: “Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa yaliyo vifuani.” Mwenyezi Mungu anataja alama nyingine ya uadui iliojificha katika vifua vya makafiri kwa kusema: “Ukiwaguseni wema unawasononesha, na kama likiwapata baya wanalifurahia.” Lakini je! Uadui wa aina hii unawadhuru Waumini?Jawabu la suala hili tunalipata katika mwendelezo wa Aya hii, Mwenyezi Mungu anasema:” Na kama mkisubiri na mkaogopa, basi hila zao hazitawadhuru kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyazunguka wayatendayo.” Tahadhari Kwa Waislamu: Katika Aya hizi Mwenyezi Mungu ametoa tahadhari kwa Waislamu dhidi ya makafiri kwa kuwapa siri za mipango yao, tahadhari hii inawahusu Waislamu wote wa 90
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 90
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
zama zote popote walipo. Lakini kwa masikitiko makubwa ni kwamba leo tunawashuhudia viongozi wengi walio Waislamu wakighafilika na tahadhari hii itokayo kwa Mwenyezi Mungu, natija yake ni kuyafanya mataifa yao kutumbukia katika udhalili na unyonge wa hali ya juu, na kukosa uhuru wa kujiamulia mustakabali wao. Leo tunashuhudia kwa macho yetu maadui wakiwazunguka Waislamu kila upande wa maisha yao, huku Waislamu hao wakionyesha mapenzi ya hali ya juu kwa maadui hao, wakati mwingine hutangaza wazi wazi kuwaunga kwao mkono katika baadhi ya mambo, lakini baadhi ya mambo wanayoyadhihirisha huonesha misimamo ya wazi ya uadui wao kwa Waislamu, pamoja na hivyo Waislamu hughafilika kwa kudanganywa pale maadui hao wanapoonesha mapenzi na urafiki kwa Waislamu, na jambo la kusikitisha zaidi ni Waislamu hao kuwa na ukuruba zaidi na maadui kuliko na Waislamu wenzao wanaoshirikiana nao katika imani na akida, wakati maadui hawawatakii Waislamu isipokuwa maangamizi na matatizo katika maisha yao. Kwa mfano wa wazi ni suala la Palestina, maisha ya kinyonge na udhalili wanayoishi wananchi wa nchi hiyo hayatokani na uwezo mkubwa wa nguvu za kijeshi wa serikali ya walowezi wa kiyahudi, bali ni kwa sababu ya mughafala mkubwa uliowakumba viongozi wa nchi za Kiislamu, na leo imefikia hadi baadhi ya nchi hizo kuwa na uhusiano wa kibalozi na adui huyo asiyesikia la yoyote pale anapotaka kutekeleza uadui wake au anapotaka kuendelea kuiteka ardhi kwa kujenga makaazi mapya ya walowezi. Lau kama umma wa Kiislamu utarudi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuchota mafunzo yaliyomo humo, bila ya shaka wazayuni hao wanaweza kugharikishwa na kuangamizwa kwa mate tu ya Waislamu, kama alivyoyasema hayo kiongozi na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; Imam Khomein r.a.
91
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 91
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA TANO
ْ َالر َبا أ َ ض َع ًافا ُم َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اع َف ًة َواتَّ ُقوا ِّ ين آ َمنُوا اَل َت ْأ ُكلُوا َ ض َ ار الَِّتي أُ ِع َّد ْت لِْل َكا ِف ِر َ اللهََّ لَ َعلَّ ُك ْم تُ ْفلِ ُح ين َوأَ ِطيعُوا َ َّون َواتَّ ُقوا الن ُ ون َو َسار ُعوا إلَىٰ َم ْغ ِف َر ٍة ِم ْن َرب َ الر ُس ََّالله ُول لَ َعلَّ ُك ْم ت َ ِّك ْم م ح ر و ْ َّ ُ َ َ ِ ُ ِ َ ْات َو أ ْ َّ ُ الس َما َو ُ ال ْر ُ َو َجنَّ ٍة َع ْر َ ض أ ِع َّد ْت لِل ُمت ِق ين َّ ض َها “Enyi mlioamini! Msile riba ziada juu ya ziada. Na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu. Na uogopeni moto ambao umeandaliwa makafiri. Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemiwa. Na harakisheni kuomba maghufira kwa Mola Wenu na pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi imeandaliwa wenye takua.” (Qur’ani 3:130-133)
MAELEZO Kuharamishwa Riba kwa Awamu Mwenyezi Mungu ametumia utaratibu wa kukataza baadhi ya mambo hatua kwa hatua, hasa yale mambo yaliyokuwa yameota mizizi katika jamii, hiyo ilikuwa ni hali ya kuandaa mazingira mazuri ya kuweza kukubalika makatazo ya mambo hayo, kisha ndipo inapokuja hukumu ya mwisho inayokataza mambo hayo, utaratibu huu ulikuwa ukitumika katika mambo yaliyokuwa yamezoeleka sana kwa kiasi cha kuwa ni jambo zito kwa mtu kuachana nayo mara moja. Miongoni mwa mambo yaliyokuwa yameenea sana katika jamii ya Waarabu, hasa Waarabu wa Makka ni uchumi wao kuambatana na riba, uchumi wa aina hii uliwasababishia matatizo na ufakiri watu wengi, kutokana na jambo hilo kuota mizizi katika jamii hiyo, Mwenyezi Mungu aliiharamisha riba katika hatua nne: Hatua ya Kwanza: Mwenyezi Mungu ametumia njia ya nasaha, na kuonesha ya kwamba ni katika tabia zisizo nzuri kwa mtu kula riba, amesema:
ََو َما آ َتيْتُم ِّمن ِّرباً لَِّي ْربُ َو ِفي أ َّ اس َف اَل َي ْربُو ِعن َد اللهَِّ َو َما الن ال و م ْ َ ِ ِ ُ ْ ُ ْ ون َو ْج َه اللهَِّ َفأ ْولَِئ َك ُه ُم ال ُم َ ض ِعف َ آ َتيْتُم ِّمن َز َكا ٍة تُ ِري ُد ون 92
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 92
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
“Na ile riba mtoayo ili izidi katika mali ya watu, basi mbele ya Mwenyezi Mungu haizidi, lakini (mali) mnayoitoa kwa ajili ya zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio wazidishao (mali zao).” (Qur’ani 30:39).
Aya hii inabainisha udhaifu wa fikra waliyonayo watu wengi ya kwamba, riba inazidisha mali yao, na kumbe jambo linalozidisha mali ni kutoa Zaka na Sadaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hatua ya Pili: Mwenyezi Mungu anaashiria ya kwamba mila na desturi mbaya walizokuwa nazo mayahudi ni ulaji wa riba, Mwenyezi Mungu anasema:
ْ الر َبا َو َق ْد نُه ...ُوا َع ْن ُه ِّ َوأَ ْخ ِذ ِه ُم “Na kuchukua kwao riba, nao wamekatazwa…” (Qur’ani 4: 161).
Hatua ya Tatu: Hatua hii tunaishuhudia katika Aya hii tunayokwenda nayo, ambayo nayo inaelezea uharamu wa kula riba kwa uwazi kabisa, lakini si kwa lugha iliyo kali zaidi ikilinganishwa na hatua ya mwisho iliyochukuliwa katika kuharamishwa riba. Hatua ya nne: Baada ya hatua tatu zilizotumika katika kuonesha uharamu wa riba, hatua ya mwisho ilikuja kuiharamisha riba katika vipengele vyote tena kwa kutumia kauli kali na ya vitisho, kiasi kuonekana kwamba kula riba ni sawa na kutangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.), Mwenyezi Mungu anasema:
َ إِ َّن الَّ ِذ الص اَل َة َوآ َت ُوا َّ ات َوأَ َقا ُموا َّ ين آ َمنُوا َو َع ِملُوا ِ الصالِ َح َف َعل ٌ الز َكا َة لَ ُه ْم أَ ْج ُر ُه ْم ِع ْن َد َربِّه ْم َو اَل َخ ْو َّ ْه ْم َو اَل ُه ْم ي ِ ِ َ ون َيا أَُّي َها الَّ ِذ َ َُي ْح َزن الر َبا ِّ ين آ َمنُوا اتَّ ُقوا اللهََّ َو َذ ُروا َما َب ِق َي ِم َن َ إِ ْن ُك ْنتُ ْم ُم ْؤ ِم ِن ين َفإِ ْن لَ ْم َت ْف َعلُوا َف ْأ َذنُوا ِب َح ْر ٍب ِم َن اللهَِّ َو َر ُسولِ ِه َ ون َو اَل تُ ْظلَ ُم َ وس أَ ْم َوالِ ُك ْم اَل َت ْظلِ ُم ون ُ َوإِ ْن تُبْتُ ْم َفلَ ُك ْم ُر ُء “Hakika wale walioamini wakatenda mema na wakasimamisha Swala na wakatoa Zaka, wao watapata ujira wao kwa Mola Wao, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. Enyi mlioamini! Mcheni Mungu na acheni yaliyobaki katika riba, ikiwa mmeamini. Na kama hamtafanya, basi jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu 93
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 93
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
na Mtume wake. Na mkiwa mmetubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu; msidhulumu wala msidhulumiwe.” (Qur’ani 2: 277-279).
Uharamu wa Riba Katika Aya Tunayoitafsiri Aya hii tunayoitafsiri hapa inaelezea uharamu wa riba ulio mbaya zaidi, kwani aina hii ya riba hufanywa kwa mkopaji kuongezewa kiwango cha riba kila anapochelewa kulipa deni analodaiwa, na hali huendelea hivyo mpaka atakapolipa deni, na kama atashindwa basi mali aliyoiweka rahani humtoka na kuchukuliwa na mkopeshaji (mlaji riba). Kutokana na dhulma hii ndio Mwenyezi Mungu akaikemea kwa kusema: “Enyi mlioamini! Msile riba ziada juu ya ziada.” Mfumo huu wa riba ndio unaotumiwa hivi leo na walaji riba wakubwa pasi na kuwa na huruma kwa wanadamu wenzao. Bila ya shaka vitendo vya aina hii huwakusanyia walaji riba mrundiko wa mali bila ya kutoa jasho, kwa hivyo ni jambo gumu sana kwa mtu kuliwacha isipokuwa kwa mtu kumcha Mwenyezi Mungu, ndio maana Mwenyezi Mungu katika kuikataza riba akamalizia kwa kusema: “…Na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu.” Lakini, je Inatosha kutakiwa kumcha Mwenyezi Mungu na kuelezwa ya kwamba huko ndiko kufaulu na kufanikiwa kimaisha? Au kulikuwa hakuna budi kutishiwa kwa adhabu ya Siku ya Kiyama kwa wanaokhalifu amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu. Kutokana na jambo hilo kukita na kuota mizizi katika nafsi za watu, katika Aya ya pili Mwenyezi Mungu anasema: “Na uogopeni moto ambao umeandaliwa makafiri.” Neno ‘Makafiri’ katika Aya hii linabainisha ya kwamba, ulaji riba hauwafikiani kabisa na misingi ya imani, kwa hivyo walaji riba nao wanasubiri kupata adhabu sawa na adhabu watakayoadhibiwa makafiri Siku ya Kiyama. Na pia tunafaidika katika ibara isemayo ya kwamba Moto umeandaliwa hasa kwa ajili ya makafiri, basi huko waasi na wenye madhambi kuadhibiwa kwa moto ni kwasababu ya kujifananisha kwao na makafiri na kuwa wasaidizi wao katika kumuasi Mwenyezi Mungu. Baada ya Mwenyezi Mungu kutoa vitisho kwa waasi, pia anatoa bishara na habari njema na kuwahamasisha watu katika kumtii Yeye pamoja na Mjumbe Wake (s.a.w.w.), anasema: “Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemiwa.” Amri nyingine iliyoelekezwa kwa Waumini ni kutakiwa kukimbilia katika kutafuta msamaha wa Mola Wao ili Naye awalipe Pepo iliyo na upana wa mbingu na ardhi, anasema: “Na harakisheni kuomba maghufira kwa Mola Wenu na pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi imeandaliwa wenye takua.” 94
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 94
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
Baada ya Mwenyezi Mungu kutoa onyo kali kwa wale wanaopinga amri Zake, katika Aya hii anatoa bishara njema kwa wale watakaoitikia na kutekeleza maamrisho Yake, kwa hivyo anawataka warejee Kwake kwa kutubia makosa yao na washindane mashindano ya kiroho kwa lengo la kukimbilia rehema na radhi za Mola Wao na neema Zake zisizo na kikomo. Neno ‘Saari’uu’ linamaanisha mashindano ya mbio kati ya watu wawili au zaidi, kila mmoja akiwa na lengo la kufika mwanzo pahala maalumu palipokusudiwa. Hapa Qur’ani Tukufu inaeleza hali ya nafsi ya mwanadamu ya kwamba pindi mtu anapokuwa peke yake hatumii nguvu nyingi au uwezo wake wote katika kazi fulani, lakini anapokuwa na wenzake, kazi hiyo huifanya kwa njia ya kimashindano yaliyo na zawadi kubwa kwa kila mtu atakayeshinda. Lengo la kwanza la mashindano yaliyotajwa katika Aya hii ni kufikia kwenye maghfira, ni dalili ya wazi ya kwamba mtu hawezi kufikia katika daraja za kiroho ambazo humkurubisha kwa Mwenyezi Mungu bila ya kuitakasa na kuitoharisha nafsi yake kwanza. – Ama lengo la pili ni kupata Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, kama Aya hii na nyinginezo zilivyobainisha.
95
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 95
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA SITA
ُ ين َك َف ُروا َي ُر ُّد َ ين آ َمنُوا إِ ْن تُ ِطيعُوا الَّ ِذ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ٰ َوك ْم َعل ى َ اص ِر َ اس ِر ين ُ ين َب ِل اللهَُّ َم ْو اَل ُك ْم َو ُه َو َخي ِ َّْر الن ِ أَ ْع َق ِاب ُك ْم َف َت ْن َقلِبُوا َخ “Enyi ambao mmeamini! Mkiwatii ambao wamekufuru watawarudisha nyuma mtageuka kuwa ni wenye kuhasirika. Bali Mwenyezi Mungu ndiye kiongozi wenu Naye ndiye bora wa wasaidizi.” (Qur’ani 3:149-150)
MAELEZO Aya hizi kama zilivyo Aya nyingine zinatoa tahadhari kwa Waumini juu ya kuwasikiliza na kuwatii makafiri. Aya hizi ziliteremka baada ya vita vya Uhud, ni kwamba mara baada ya kumalizika kwa vita maadui wa Uislamu walikuwa wakieneza chokochoko na kasumba miongoni mwa baadhi ya Waislamu ili kuwatenganisha na wenzao, wakati mwingine walikuwa wakitumia njia ya kuwanasihi Waislamu katika kufikia lengo lao, na wakati mwingine kutumia vitisho hasa baada ya masaibu yaliyowakumba Waislamu, walijaribu kuitumia nafasi hiyo kutokana na baadhi ya Waislamu kuonesha misimamo dhaifu katika imani zao. Na wala si jambo lililombali ya kwamba Mayahudi walikuwa msitari wa mbele wakishirikiana na wanafiki katika mpango wao huo, kama vile walivyoshiriki kueneza uongo wakati wa vita ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliuwawa vitani, lengo la kuzua uwongo huo lilikuwa ni kuwadhoofisha wapiganaji wa Kiislamu. Aya ya mwanzo inasema: “Enyi ambao mmeamini! Mkiwatii ambao wamekufuru watawarudisha nyuma mtageuka kuwa ni wenye kuhasirika.” Aya inatoa tahadhari kwa Waislamu dhidi ya kuwatii makafiri, na kubainisha wazi kwamba kuwatii makafiri natija yake ni kurudi katika maisha ya kijahilia baada ya safari ndefu ya mafunzo ya kiroho na kimaada yaliyoletwa na Dini ya Kiislamu. Hakika kuwatii makafiri kwa kusikiliza maneno yao na kukubali propaganda zao ni kurudia katika ukafiri na ufisadi na kuporomoka kwa maadili. Katika hali kama hii itakuwa wamebeba dhambi nzito na kuwalazimu kupata kila baya wanalostahili kulipata makafiri. Ni hasara gani iliyo kubwa zaidi ambayo mtu anayoweza kuipata, 96
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 96
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
kama kuubadilisha Uislamu wake kwa ukafiri, na nuru kwa giza na uongofu kwa upotofu, na furaha kwa majonzi?! Aya ya pili Mwenyezi Mungu anawathibitishia Waislamu ya kwamba, wanaye Mlezi na Msaidizi aliye bora zaidi: “Bali Mwenyezi Mungu ndiye kiongozi wenu Naye ndiye bora wa wasaidizi.� Hakika Yeye Mwenyezi Mungu ni Mlinzi asiyeshindika, bali uwezo Wake haulingani na yeyote yule, kila mwenye nguvu asiyekuwa Yeye mwisho wake hushindwa.
97
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 97
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA SABA
َ ين آ َمنُوا اَل َت ُكونُوا َكالَّ ِذ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين َك َف ُروا َو َقالُوا لإِِ ْخ َوا ِن ِه ْم َ ْض َربُوا ِفي أ َ إِ َذا ض أَ ْو َكانُوا ُغ ًّزى لَ ْو َكانُوا ِع ْن َد َنا َما ر ال ْ ِ ُُ ُُ َ َ ََُّ لله ُح ِيي ْ وب ِه ْم َواللهَُّ ي ِ َماتُوا َو َما ق ِتلوا لَِي ْج َعل ا ذٰلِك َح ْس َر ًة ِفي قل ُْ ُ َويُ ِم َ ُيت َواللهَُّ ِب َما َت ْع َمل يل اللهَِّ أَ ْو ٌص ِ ون َب ِ ير َولَِئ ْن ق ِتلتُ ْم ِفي َس ِب َ ْر ِم َّما َي ْج َمع ُون َولَِئ ْن ُم ُّت ْم أَ ْو ٌ ُم ُّت ْم لَ َم ْغ ِف َر ٌة ِم َن اللهَِّ َو َر ْح َم ٌة َخي َ ُق ِت ْلتُ ْم لإَ ِلَى اللهَِّ تُ ْح َش ُر ون “Enyi mlioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakawasema ndugu zao, waliposafiri katika nchi au walipokuwa vitani: lau wangelikuwa kwetu wasingekufa na wasingeliuawa; ili Mwenyezi Mungu ayafanye hayo kuwa majuto katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu anahuisha na kufisha na Mwenyezi Mungu anaona mnayoyatenda. Na kama mkiuawa katika njia ya Mwenyezi Mungu au mkifa, basi maghufira na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko yale wanayoyakusanya. Na kama mkifa au mkiuawa, nyote mtakusanywa kwa Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani 3:156-158)
MAELEZO Tukio la vita vya Uhud lilitawala vichwa vya Waislamu wengi kutokana na mambo mawili: Jambo la kwanza: Lilikuwa likizingatiwa kama ni kioo kizuri cha kuweza kutazama udhaifu uliojitokeza kwa Waislamu na kuweza kuuondoa, kutokana na hali hii ndio maana Qur’ani Tukufu ikajishughulisha sana na tukio la vita vya Uhud na kulipa umuhimu wa kipekee, kwani tutashuhudia ni namna gani tutakavyopata faida kutokana na Aya hizi. Jambo la Pili: Tukio la vita vya Uhud liliandaa mazingira kwa wanafiki kuweza kueneza uzushi na propaganda zao zisizo na mashiko, katika kubainisha ubatili wa propaganda za wanafiki na vitimbi vyao ndipo Mwenyezi Mungu akashusha Aya hizi. Kwa kuanzia, Aya hizi zinawaelekea Waumini ili wawe tayari kupambana dhidi ya 98
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 98
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
njama za wanafiki zinazolenga katika kuubomoa Uislamu, na pia kuwatahadharisha nao: “Enyi mlioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakawasema ndugu zao, waliposafiri katika nchi au walipokuwa vitani: lau wangelikuwa kwetu wasingekufa na wasingeliuawa;” Licha ya maneno haya kuyasema katika pazia la shauku na mapenzi kwa jamaa zao, lakini hawakuwa na lengo hilo, bali walikusudia kupandikiza sumu katika nafsi za Waislamu na kudhoofisha ukakamavu wao na kuzitikisa imani zao, kwa hivyo inawapasa Waumini wasiathirike na maneno yao hayo ya hadaa. Enyi Waumini! Iwapo mtafuata maneno hayo yasiyo na faida, basi yatadhoofisha nafsi zenu na kujizuia kwenda katika viwanja vya mapambano dhidi ya maadui wenu, na kwa kufanya hivyo mtakuwa mmewahakikishia wanafiki ushindi mnono usio na gharama yoyote kwao, lakini jambo mnalostahiki kufanya ni kwenda katika vita vya jihadi mkiwa na imani ya hali ya juu ya kupata ushindi au shahada na muwe na azma kubwa ya kufanya hivyo bila ya kusitasita, mkifanya hivi mtakuwa mmewatia hasara na majonzi makubwa “Ili Mwenyezi Mungu ayafanye hayo kuwa majuto katika nyoyo zao.” Kisha Qur’ani Tukufu inazijibu hoja dhaifu za wanafiki kama ifuatavyo: Kwanza: Uhai na mauti ni vitu vilivyo katika mamlaka ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo mtu kwenda katika uwanja wa mapambano hakubadilishi kitu, na Mwenyezi Mungu anajua matendo ya waja Wake wote: “Na Mwenyezi Mungu anahuisha na kufisha na Mwenyezi Mungu anaona mnayoyatenda.” Pili: Kisha hata hapo mtakapokufa au kuuwawa – kwa mtazamo wa wanafiki– ni kwamba nyinyi hamtopata hasara yoyote, kwani rehema za Mwenyezi Mungu na msamaha Wake ni bora zaidi kuliko hivyo mnavyovikusanya au wanavyovikusanya wanafiki: “Na kama mkiuawa katika njia ya Mwenyezi Mungu au mkifa, basi maghufira na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko yale wanayoyakusanya.” Kwa hakika haistahiki kulinganishwa utajiri wa mali inayomalizika na malipo makubwa yanayowangoja wale wanaopigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni malipo ambayo hayana mwisho wala kikomo. Tatu: Hata kama mtu atauawa au kufariki ni kwamba mauti si mwisho wa uhai hata kumfanya mtu awe na khofu kiasi chote hicho,bali ni hali ya kumtoa Muumini kwenye uhai na kumpeleka katika uhai mwingine ulio nzuri na bora zaidi, ni kwenda katika uhai wa milele usio na mwisho: “Na kama mkifa au mkiuawa, nyote mtakusanywa kwa Mwenyezi Mungu.”
99
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 99
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA NANE
ََّيا أَُّي َها ال ََّصاب ُروا َو َراب ُطوا َواتَّ ُقوا الله ُ َ و وا ر ب اص وا ن م آ ين ذ ُ ْ َ َ َ ِ ِ ِ ِ َ لَ َعلَّ ُك ْم تُ ْفلِ ُح ون “Enyi ambao mmeamini! Fanyeni subira na mvumilie na muwe imara na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu.” (Qur’ani 3:200).
Katika mfululizo wa Aya hizi tulizozichagua, hii ndio Aya yenye maneno mafupi zaidi, lakini ni miongoni mwa Aya zilizo na ujumbe mzito na mafunzo makubwa katika maisha ya mwanadamu. Aya hii inawataka Waumini kuzingatia na kutekeleza amri nne zilizotajwa, amri hizo ni kama zifuatazo: Kwanza: “Fanyeni subira” hii ndio amri ya kwanza katika mtiririko wa amri nne, amri hii inatoa dhamana ya heshima na ushindi kwa Waislamu, kwani subira inamfanya mtu kuthibiti katika jambo na kuwa na msimamo madhubuti. Subira ni msingi wa kila mafanikio ya kilimwengu na sababu ya ushindi wa kiroho, kwa hivyo jambo hili linastahiki maelezo ya kina kutokana na faida muhimu katika kuhakikisha ushindi na mafanikio ya mtu binafsi au jamiii. Imam Ali (a.s.) anasimulia umuhimu wa subira kwa kusema:
ّ ...كالرأس من الجسد ّ الصبر من اإليمان ّ إن “Hakika subira ni katika imani, (umuhimu wake) ni kama kichwa katika mwili...”55
Pili: “…na mvumilie.” inamaanisha kuwa na subira, msimamo na ukakamavu mbele ya subira ya watu wengine na msimamo wao na ukakamavu wao. Kwa hivyo kwanza Qur’ani Tukufu inawausia Waumini kujipamba na subira pamoja ushupavu katika kila aina ya Jihadi, kama vile Jihadi ya nafsi, na kuwa na msimamo madhubuti katika kukabiliana na matatizo ya kimaisha. Qur’ani inawausia Waumini kujipamba na vazi la subira, ukakamavu na msimamo wakati wanapokabiliana na maadui. Hata tunajifunza ya kwamba ikiwa umma hautaweza kupata ushindi katika Jihadi ya nafsi, basi ni jambo lisilowezekana kamwe 55
Imamu Ali (a.s.), Nahjul Balaghah, Jz. 4, Uk. 18 100
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 100
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
kuweza kuwashinda maadui, hii ndio sababu kubwa iliyopelekea umma kushindwa na maadui katika uwanja wa mapambano, kwa hivyo ni juu ya Waislamu kuwa na subira kubwa zaidi na msimamo ulio thabiti zaidi kila pale wanapowaona maadui zao wameshikamana na mambo hayo zaidi. Tatu: “…na muwe imara” Ibara hii inawataka Waumini kuwa macho wakati wowote katika kufuatilia harakati za maadui wao na kujiandaa vilivyo kwa kujibu mapigo ikiwa watashambuliwa au kuvamiwa katika nchi yao. Pia wawe macho kwa kujiandaa na kupambana dhidi ya shetani pamoja na matamanio, ili yasije yakawatumbukiza katika maasi na mughafala, kutokana na haya imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s.) katika kueleza maana ya kuwa macho, anasema: Ni kungojea Swala nyingine baada ya kuswali, kwani mwenye kuchunga nyakati za Swala nafsi yake inakuwa macho wakati wote juu ya ibada hii tukufu, mtu wa aina hii anakuwa kama mwanajeshi aliyemacho na mwangalifu aliyejiweka tayari kupambana na uadui wakati wowote utokeapo. Nne: “…na mcheni Mwenyezi Mungu.” Hii ni amri ya mwisho wanayoamrishwa Waumini katika Aya hii, amri hii ni kama mwamvuli unaohifadhi amri zilizopita, na ni muhali hizo amri zilizotajwa mwanzo kuweza kusimama kikamilifu bila ya kuwepo ucha Mungu usio na chembe ya ria, ubinafsi au sababu nyingine. Mwisho kabisa, Aya ina maelezo ya natija ya utekelezaji wa mambo haya manne, inasema: “…ili mpate kufaulu.” Mafanikio na ushindi uliotajwa utamstahikia kila mwenye kushikamana na amri zilizomo katika Aya hii, kinyume chake mtu asitarajie lolote isipokuwa udhalili, unyonge na kushindwa.
101
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 101
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KUMI NA TISA
َيا أَُّي َها الَّ ِذ َ ين آ َمنُوا اَل َي ِح ُّل لَ ُك ْم أَ ْن َت ِرثُوا النِّ َسا َء َك ْر ًها َو اَل ْضلُ وه َّن لَِت ْ َتع ُ ْض َما آ َتيْتُ ُم ُ ُ وه َّن إِ اَّل أَ ْن َي ْأ ِت َ َ اح َش ٍة ع ب ب ُوا ب ه ذ َ ين ِب َف ِ ِ ِ وف َفإِ ْن َك ِر ْهتُ ُم ُ اش ُر ُ ى أَ ْن وه َّن َف َع َس ٰ وه َّن ِب ْال َمع ُ ْر ِ ُم َبيِّ َن ٍة َو َع ِ اس ِت ْب َد َ ال ْرا َك ِث ً َت ْك َر ُهوا َشي ًْئا َو َي ْج َع َل اللهَُّ ِفي ِه َخي ً يرا َوإِ ْن أَ َر ْدتُ ُم ْ َز ْوج َم َ ان َز ْوج َوآ َتيْتُ ْم إِ ْح َد ُ َ ارا َف اَل َت ْأ ُخ ُذوا ِم ْن ُه ك اه َّن ِق ْن َط ً ٍ ٍ ْ ْ َ َ ُ ُ ْ ْ َ َ ُ ُ ً ً َ َ َ َ ُ ُ َشي ًْئا أتأخذو َنه بُ ْهتانا َوإِث ًما ُم ِبينا َوكيْف تأخذو َنه َوق ْد أف َ ضىٰ ْض ُك ْم إلَىٰ َبعْض َوأَ َخ ْذ َن ِم ْن ُك ْم ِم َيث ًاقا َغلِ ً يظا َو اَل َت ْن ِك ُحوا ٍ َبع ُ ِ َما َن َك َح آ َبا ُؤ ُك ْم ِم َن النِّ َسا ِء إِ اَّل َما َق ْد َسلَ َ ف إِنَّ ُه َك َ اح َش ًة ان َف ِ يل ُح ِّر َم ْت َعلَي ُ َو َم ْق ًتا َو َسا َء َسب اً ْك ْم أُ َّم َهاتُ ُك ْم َو َب َناتُ ُك ْم َوأَ َخ َواتُ ُك ْم ِ ُ أُْ أْ َ ات الخ َو َب َن ُ َو َع َّماتُ ُك ْم َو َخ اَالتُ ُك ْم َو َب َن ُ ات ال ْخ ِت َوأ َّم َهاتُ ُك ُم ِ ُ ُ اَّ ُ الر َ الل ِتي أَ ْر َ اع ِة َوأ َّم َهات ِن َسا ِئك ْم ض ْع َن ُك ْم َوأَ َخ َواتُ ُك ْم ِم َن َّ ض َ َو َر َبا ِئب ُ الل ِتي ِفي ُح ُجور ُك ْم ِم ْن ِن َسا ِئ ُك ُم اَّ ُك ُم اَّ الل ِتي َد َخ ْلتُ ْم ِب ِه َّن ِ اح َعلَي ُ ْك ْم َو َح اَل ِئ ُل أَ ْب َنا ِئ ُك ُم َفإِ ْن لَ ْم َت ُكونُوا َد َخ ْلتُ ْم ِب ِه َّن َف اَل ُج َن َ ْن أُْ ص اَلب ُك ْم َوأَ ين ِم ْن أَ الَّ ْ ْن إِ اَّل َما َق ْد َسلَ َ َ َ ْ َ َ ف ي ت خ ال ي ب ُوا ع م ج ت ن ذ ْ ْ َ َ ِ ِ ِ ْ اَّ ص َن ُ إِ َّن اللهََّ َك َ ات ِم َن النِّ َسا ِء إِل َما ان َغ ُف ً ورا َر ِحي ًما َوال ُم ْح َ اب اللهَِّ َعلَي ُ ْك ْم َوأُ ِح َّل لَ ُك ْم َما َو َرا َء َذٰلِ ُك ْم َملَ َك ْت أَ ْي َمانُ ُك ْم ِك َت َ ْر ُم َسا ِف ِح َ ص ِن َ اس َت ْم َتعْتُ ْم ين َف َما ْ ين َغي َ أَ ْن َت ْب َت ُغوا ِبأَ ْم َوالِ ُك ْم ُم ْح ِ اح َعلَي ُ ِب ِه ِم ْنه َّ ُن َفآتُ ُ ور ُه َّن َف ِر َ ْك ْم ِفي َما يض ًة َو اَل ُج َن َ وه َّن أُ ُج َ 102
12/8/2014 2:43:38 PM
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 102
WITO KWA WAUMINI
َ اضيْتُ ْم ِب ِه ِم ْن َب ْع ِد ْال َف ِر َ َت َر َ يض ِة إِ َّن اللهََّ َك ان َعلِي ًما َح ِكي ًما َو َم ْن ات َف ِم ْن َ لَ ْم َي ْس َت ِط ْع ِم ْن ُك ْم َط ْو اًل أَ ْن َي ْن ِك َح ْال ُم ْح ِ ات ْال ُم ْؤ ِم َن ِ ص َن ات َواللهَُّ أَ ْعلَ ُم ِبإِي َما ِن ُك ْم ِ َما َملَ َك ْت أَ ْي َمانُ ُك ْم ِم ْن َف َت َيا ِت ُك ُم ْال ُم ْؤ ِم َن ُ ُ َبع ُ ُوه َّن ِبإِ ْذ ِن أَ ْهلِ ِه َّن َوآت ُ ْض َفا ْن ِك ُح ور ُه َّن َ وه َّن أُ ُج ٍ ْضك ْم ِم ْن َبع َات أ ْب َ ات َو اَل ُمتَّ ِخ ْ َ َ َ ان َفإِ َذا د خ ذ ح ف ا س م ْر ي غ ات ن ص ح م وف ْر ع م ال ُ ْ ُ ُ ٍ ٍ َ َ َ َ َ ِ ِ ِ ٍ ِ ُأ َ ْ َ َ ُص َ َ َ َ َ ْ َّ َ ات ي ل ع ف ة ش اح ف ب ْن ي ت أ ن إ ف ن ص ح ْ ْ ْه َّن ِن ٍ َ َ ف َما َعلى ال ُم ْح ِ ص َن ِ ِ ِ ِ ِ َ ْ ُ َ َ َ ْ ْر ٌ ص ِب ُروا َخي ْ اب ٰذلِك لِ َم ْن َخ ِش َي ال َع َن َت ِم ْنك ْم َوأ ْن َت ِ ِم َن ال َعذ َ ِّن لَ ُك ْم َو َي ْه ِد َي ُك ْم ُس َن َن الَّ ِذ َ ُري ُد اللهَُّ لِيُ َبي ين ٌ لَ ُك ْم َواللهَُّ َغ ُف ِ ور َر ِحي ٌم ي َُّْك ْم َواللهَُّ َعلِي ٌم َح ِكي ٌم َوالله ُ وب َعلَي ُري ُد أَ ْن ي َ ُِم ْن َق ْبلِ ُك ْم َو َيت ِ ُ وب َعلَي َّ ُون َ ين َيتَّ ِبع َ ُري ُد الَّ ِذ ات أَ ْن َت ِميلُوا َمي اًْل ي و م ْك َ َُيت ْ َ ِ الش َه َو ِ َ ُخ ِّف َ ُري ُد اللهَُّ أَ ْن ي ُ ف َع ْن ُك ْم َو ُخلِ َق الإْ ِ ْن َس َ ان ض ِع ًيفا ِ َع ِظي ًماي Enyi ambao mmeamini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu; wala msiwataabishe kwa kutaka kuwanyang’anya baadhi ya mlivyowapa, ila watakapofanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema; na kama mkiwachukia basi huenda mkachukia kitu na Mwenyezi Mungu amejaalia kheri nyingi ndani yake. Na mtakapotaka kubadilisha mke mahali pa mke, na mkawa mumempa mmoja wao rundo la mali, basi msichukue katika mlichowapa. Je, mnakichukua kwa dhulma na kwa makosa yaliyo wazi? Mtachukuaje na hali mmeingiliana na hali wao wamechukua kwenu agano madhubuti?Wala msiwaoe walioolewa na baba zenu, ila waliokwishapita. Hakika hilo ni ovu na chukizo na njia mbaya. Mmeharamishiwa mama zenu na binti zenu na dada zenu na shangazi zenu na khalat zenu na binti wa kaka na binti wa dada na mama zenu waliowanyonyesha na dada zenu wa kunyonya na mama wa wake zenu na binti zenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia-hapana vibaya juu yenu ikiwa hamkuwaingilia-na wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kukusanya kati ya dada wawili, ila waliokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu. Na wanawake wenye waume; isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni Sharia ya Mwenyezi Mungu kwenu. Na mmehalalishiwa wasiokuwa hao, kwamba Muwatafute kwa mali zenu kwa kuoa bila ya kufanya 103
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 103
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
zina. Ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu. Wala si vibaya kwenu katika yale mliyoridhiana baada ya (kutoa) kile kilichowalazimu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima. Na asiyeweza miongoni mwenu kupata mali ya kuoa wanawake waungwana waumini, basi (na aoe) katika wajakazi wenu waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kuume; na Mwenyezi Mungu anajua sana imani yenu. Baadhi yenu mnatokana na baadhi; basi waoeni kwa idhini ya watu wao na muwape mahari yao kama ada wawe ni wenye kujistahi si waasherati wala wenye kujifanyia mahawara. Watakapoolewa kisha wakafanya uchafu, basi itakuwa adhabu juu yao ni nusu ya adhabu iliyowekwa kwa waungwana. Hayo ni kwa mwenye kuchelea mashaka katika nyinyi. Na mkisubiri ni bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu. Mwenyezi Mungu anataka kuwabainishia na kuwaongoza mwendo wa waliokuwa kabla yenu na awatakabalie toba. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima. Na Mwenyezi Mungu anataka kuwatakabalia toba, na wale ambao hufuata matamanio wanataka mkengeuke mkengeuko mkubwa. Mwenyezi Mungu anataka kuwahafifishia. Na mtu ameumbwa hali yakuwa ni dhaifu. (Qur’ani 4:19-28)
MAELEZO Aya hizi kumi kwa ujumla wake zimetaja maamrisho na makatazo mbali mbali kwa kila Muumini wa kweli. Katika kuzifafanua Aya hizi tutazifafanua kidogo kidogo kwa mujibu wa ujumbe uliomo katika kila Aya au kwa mujibu wa sababu za kuteremshwa kwake. Tunanza na Aya ya kwanza, Mwenyezi Mungu anasema: “Enyi ambao mmeamini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu; wala msiwataabishe kwa kutaka kuwanyang’anya baadhi ya mlivyowapa, ila watakapofanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema; na kama mkiwachukia basi huenda mkachukia kitu na Mwenyezi Mungu amejaalia kheri nyingi ndani yake.”
SABABU YA KUTEREMKA Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s.) ya kwamba: “Aya hii iliterermka kwa mtu aliyekuwa akimfungia mke wake, kwa sababu ya kutokuwa na haja naye (kama mke), alikuwa akisubiri tu afariki dunia ili apate kumrithi (kuchukuwa mali yake kwa dhulma).” Na imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas ya kwamba: “Aya hii iliteremka kwa wale watu waliokuwa wakiowa kwa mahari mengi, kisha wakiwafungia wake zao kwa
104
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 104
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
sababu ya kutokuwa na haja nao, na wala hawakuwa tayari kuwataliki kutokana na mahari makubwa waliyowapa, na badala yake walikuwa wakiwaudhi ili wanawake hao wasamehe mahari waliyoahidiwa.”56 Utetezi wa Haki za Wanawake: Aya hii inaeleza baadhi ya tabia za kijahilia zilizokuwa zikimdhalilisha mwanamke, na kuwatahadharisha Waumini wasije wakazirudia tabia za aina hiyo. Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kupitia Aya hii anawakataza Waumini mambo yafuatayo: Kwanza: Wasiwaweke mahabusu wanawake kwa lengo la kutaka kuja kurithi mali zao. Katika zama za kijahilia kulikuwa na mtindo wa watu kuoa wanawake wenye uwezo wa kimali na utukufu wa kikabila, lakini wanawake hao hawakuwa na uzuri wa kuwavutia hao waume waliowaowa, wanaume hao walikuwa hawawapi haki zao wanazostahiki kama wake na wala walikuwa hawawapi talaka, bali walikuwa wakiwafungia majumbani na kuwafanyia kila aina ya maudhi, na huku wakisubiri siku zao za kufariki dunia ili wapate kurithi mali, katika kukatazwa mwenendo huo mbaya Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hii na kusema: “Enyi ambao mmeamini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu.” Pili: Wasiwadhikishe kwa lengo la kuwapokonya vile walivyowapa. Ada nyingine ya kidhalimu dhidi ya wanawake iliyokuwepo wakati wa zama za kijahilia ilikuwa ni kwa wanaume kutumia kila aina ya maudhi dhidi ya wake zao ili wadai talaka na hapo waume hao huitumia nafasi hiyo kwa kudai kurejeshewa mahari waliyowapa, tabia hii ilikuwa ikifanywa pale ambapo mwanamme alimuoa mwanamke kwa mahari makubwa, Mwenyezi Mungu aliiharamisha tabia hii kwa kusema: “Wala msiwataabishe kwa kutaka kuwanyang’anya baadhi ya mlivyowapa.” Lakini katika Aya hii kuna hali iliyoruhusiwa kwa mume kumbana mke wake ili aachane na kudai mahari yake au arejeshewe ikiwa ameshalipa iwapo mke atafanya uovu wa zinaa ulio wazi kabisa, kwani kufanya hivyo ni kumukhini mume wake, Mwenyezi Mungu anasema: “…ila watakapofanya uchafu ulio wazi.” Hukumu hii ni miongoni mwa adhabu za kuadhibiwa mwanamke kutokana na khiyana aliyomtendea mume wake. Tatu: Kukaa nao (wake) kwa wema, hii ni amri nyingine itokayo kwa Mwenyezi Mungu inayowaamrisha Waumini kuamiliana na wake zao muamala wa kibinadamu unaolingana na hadhi yake kama mwanamke na kama mke: “Na kaeni nao kwa wema.” Mwenyezi Mungu anamalizia kwa kusema: “….. Na kama mkiwachukia basi huenda mkachukia kitu na Mwenyezi Mungu amejaalia kheri nyingi ndani yake.” Yaani hata kama hamkuridhika na wake zenu kwa asilimia mia moja, basi 56
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 3, Uk. 159 105
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 105
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
msifanye haraka ya kukimbilia talaka na kutengana, bali inawapasa kuwa na subira na kutafuta njia za kuifanya hali itengemae, kwani huwenda nyinyi ndio mliowakosea, na Mwenyezi Mungu huenda akataka kukuleteeni kheri kubwa na baraka nyingi baada ya machukivu yenu kwa wake zenu, kwa hivyo haiwapasi kuacha kuwafanyia wema na ihsani ikiwa hali haijavuka mipaka na kufikia kiwango cha kutostahmilika. Tukiendelea na hukumu zilizomo katika Aya hizi kumi, sasa na tuangalie Aya nyingine mbili zisemazo: “Na mtakapotaka kubadilisha mke mahali pa mke, na mkawa mumempa mmoja wao rundo la mali, basi msichukue katika mlichowapa. Je, mnakichukua kwa dhulma na kwa makosa yaliyo wazi? Mtachukuaje na hali mmeingiliana na hali wao wamechukua kwenu agano madhubuti?”
SABABU YA KUTEREMKA Kabla ya Uislamu kulikuwa na tabia ya mtu anapotaka kumuacha mke wake na kuoa mke mwingine, humtuhumu mke wa kwanza kwa kumsingizia kufanya khiyana katika ndoa (zina), ili asimlipe mahari yake au kumfanyia vitendo vya kinyama mpaka mwanammke alazimike kumrejeshea mahari mume wake, yule mume baada ya kurejeshewa mahari aliyotoa huyatumia kulipia mahari kwa ajili ya ndoa ya mke mwingine anayetaka kumuoa, kutokana na udhalimu na ufedhuli wa aina hii, Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hizi ili kuharamisha na kuwakataza Waumini wasije wakajitumbukiza katika dhulma ya aina hii.57Aya inabainisha wazi kwamba suala la kumnyima mwanamke mahari yake ni kosa kubwa, na hizi hila za kijanja walizokuwa wakizifanya ili wanawake wanyang’anywe haki zao za msingi katika ndoa ni dhulma nyingine na iliyo kubwa zaidi. Aya ya pili kati ya Aya hizi, Mwenyezi Mungu anauliza katika hali ya kupinga dhulma hii, akiwa na lengo la kuamsha hisia za kibinadamu kwa wanaume wanaotenda uovu wa aina hii:” Mtachukuaje na hali mmeingiliana na hali wao wamechukua kwenu agano madhubuti?” Yaani ni vipi nyinyi imekupaseni kufanya hivyo na ilhali mmeishi na mke huyo wa kwanza kwa muda mrefu mkishirikiana katika maisha na kila mmoja wenu amejistarehesha kwa mwenziwe kama vile kwamba mlikuwa roho moja katika viwiliwili viwili, baada ya mafungamano na mapenzi ya hali ya juu yaliyokuwepo kati yenu, je, ni haki kwenu enyi wanaume kuwafanyia wake zenu dhulma ya aina hii?! 57
Kitabu kilichotangulia, Uk.162 106
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 106
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa hakika kumtendea uovu wa aina hii mtu ambaye alikuwa ni mwenza katika maisha ni dhulma kubwa ya mtu kuidhulumu nafsi yake, kwani walichukua ahadi nzito wakati wa akdi ya ndoa ya kwamba watawatendea wake zao wema na kuwapa kila haki wanayostahiki iliyoko ndani ya uwezo wao, basi ni vipi wanakwenda kinyume na yale waliyoyaahidi?! Kisha inapasa tuelewe ya kwamba licha ya Aya kuelezea dhulma aliyokuwa akifanyiwa mke wa kwanza pale mume anapotaka kuoa mwingine badala yake, lakini ni kwamba haihusiani na kadhia hii tu, bali inahusisha kila talaka inayoamuliwa na mume katika hali ambayo mke anampenda mume wake na anachukizwa na talaka, katika hali kama hii ni wajibu kwa mume kumpa mke mahari yake yote ikiwa anadaiwa na asimdai kitu katika mahari aliyokwishampa, ni sawa ikiwa anataka kuoa mke mwingine au la. Kwa mujibu wa hali hii ni kwamba ibara ya Aya isemayo: “Na mtakapotaka kubadilisha mke mahali pa mke,” Ilikuwa inaangalia hali ilivyokuwa katika zama za kijahilia, na wala hukumu yake haihusishi sharti la kutaka kuoa mke mwingine, bali hata kama mtu hataki kuoa mke mwingine si haki kwake kumdhulumu mke wake mahari yake. Hukumu nyingine katika Aya hizi tunaikuta katika Aya ifuatayo: “Wala msiwaoe walioolewa na baba zenu, ila waliokwishapita. Hakika hilo ni ovu na chukizo na njia mbaya.”
SABABU YA KUTEREMKA Pia miongoni mwa ada zilizokuwepo wakati wa zama za kijahilia, ilikuwa mtu anapofariki na kuacha watoto pamoja na mke ambaye ni mama wa kambo wa wale watoto, watoto walikuwa wakimrithi mama yao wa kambo kama walivyokuwa wakirithi mali, yaani alikuwa akiolewa na mmoja kati ya watoto wa marehemu, au kuamiliana naye kama wanavyoamiliana na mali nyingine za kawaida. Kitendo kama hiki kiliwahi kujitokeza tena baada ya kudhihiri Uislamu kwa mtu mmoja miongoni mwa Waislamu, ni pale mmoja wa Maanswari ajulikanaye kwa jina la Abu Qaysi alipofariki na kuacha mke pamoja na watoto wa mke mwingine (mama wa kambo), mmoja kati ya wale watoto alipendekeza kutaka kumuoa mama yake wa kambo, yule mama alimwambia yule mtoto: Mimi nakuona kama vile mwanangu, na wewe ni katika watu waliobora kwa jamaa zako, lakini niache niende kwa Mtume (s.a.w.w.) ili nimsikilize ushauri wake, alipofika kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumuelezea yaliyojiri, Mtume (s.a.w.w.) alimwambia: “Rudi nyumbani kwako.” Mara ikateremka Aya hii ikikemea kwa ukali ndoa na tabia ya aina hiyo.58 58
Kitabu kilichotangulia, Uk. 166 107
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 107
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO Aya hii kama tulivyoeleza sababu ya kushushwa kwake, inakataza mwenendo mbaya miongoni mwa mienendo ya kijahilia, na kuwataka Waumini wajiepushe nayo, inasema: “Wala msiwaoe walioolewa na baba zenu,” Kwa vile hukumu hii haibatilishi zile ndoa zilizofungwa kabla ya Uislamu, Mwenyezi Mungu amesema katika Aya hii: “...ila waliokwisha pita.” Katika kusisitiza uharamu wa ndoa ya aina hii, Mwenyezi Mungu ametumia ibara tatu zilizo kali sana, amesema: “Hakika hilo ni ovu., na kisha akasema: “…na chukizo” yaani ni kitendo kisichokubalika kwa mujibu wa mtu mwenye akili timamu. Na mwisho akamalizia kwa kusema: “…na njia mbaya.” Ni jambo lililo wazi kwamba mtoto kumuoa mama yake wa kambo inashabihiyana na kumuoa mama yake mzazi, kwani mama wa kambo ni mama wa pili wa mtoto, na kwa upande mwingine ni kuuvunja murua wa baba na heshima yake. Uharamu mwingine ulioharamishiwa Waumini ni kuwaoa maharimu wao, Aya inasema: “Mmeharamishiwa mama zenu na binti zenu na dada zenu na shangazi zenu na khalat zenu na binti wa kaka na binti wa dada na mama zenu waliowanyonyesha na dada zenu wa kunyonya na mama wa wake zenu na binti zenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia-hapana vibaya juu yenu ikiwa hamkuwaingilia-na wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kukusanya kati ya dada wawili, ila waliokwishapita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.” Katika aya hii Mwenyezi Mungu amebainisha wanawake ambao ni haramu kwa Muumini mwanamme kuwaowa, uharamu huu unapatikana kutokana na sababu tatu: Sababu ya Kwanza: Nasaba Sababu ya Pili: Unyonyeshaji Sababu ya tatu: Ndoa. Aya imeeleza wanawake wa aina saba walioharamu kuwaowa kwa sababu ya mahusiano ya kinasaba, inasema: “Mmeharamishiwa mama zenu na binti zenu na dada zenu na shangazi zenu na khalat zenu na binti wa kaka na binti wa dada,” Kitu kinachopaswa kuzingatiwa katika hukumu hii ni kwamba maana ya ‘mama’ haimaanishi yule mama wa moja kwa moja (mama mzazi), bali pia wanaingia bibi mzaa baba na bibi mzaa mama na kupanda juu), na vile vile neno ‘binti’halimaanishi mtoto wa kike wa kumzaa tu, bali pia wanaingia watoto wa kike wa mtoto wa kike 108
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 108
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
na wa mtoto wa kiume na watoto wao na kushuka chini. Hali ndio hivi hivi kwa makundi mengine matano yaliyobakia. Uharamu wa ndoa wa aina hii ni uovu usiokubalika na maumbile ya kibinadamu, kwani hata wale wasiofuata Uislamu au watu wasio na dini yoyote wanachukizwa na ndoa hii. Zaidi ya hayo ni kwamba utafiti wa kisayansi unaonesha ya kwamba ndoa za watu wa karibu kinasaba ni sababu kubwa ya maambukizi ya magonjwa yaliojificha na yale ya kuambukiza, kiasi ambacho baadhi ya wataalamu hawashauri hata kuowana kati ya jamaa wa karibu walio halali kuowana, kama vile mtu kumuoa binti ya shangazi yake. Sababu ya pili inayopelekea uharamu wa watu kuowana inatokana na unyonyeshaji, Mwenyezi Mungu anasema: “…na mama zenu waliowanyonyesha na dada zenu wa kunyonya,” Hapa Qur’ani Tukufu imeashiria uharamu wa kuwaowa watu wa aina mbili kwa sababu ya unyonyeshaji ambao ni mama aliyemnyonyesha mtoto wa kiume na dada aliyenyonya ziwa moja pamoja na mtoto wa kiume, lakini hukumu hii haiwahusu watu hao wa aina mbili tu, bali inawajumuisha wa juu na wa chini kama ilivyo katika nasaba, kwani imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:
الرضاعة ما يحرم من النّسب ّ يحرم من “Inaharamishwa (kuowana) kwa sababu ya kunyonya yale yaliyoharamishwa kwa sababu ya nasaba.”59
Maelezo ya kina yanayopelekea uharamu kwa watu walionyonya ziwa moja kuowana yamefafanuliwa kwa kina zaidi katika vitabu vya fiqhi. – Miongoni mwa hekima ya kuharamishwa kuowana kati ya mtoto na mama aliyemnyonyesha mtoto huyo ni kwamba, ukuwaji wa mwili wa mtoto kutokana na maziwa aliyoyanyonya kutoka kwa mwanamke fulani kwa muda maalumu, yule mtoto huwa ni kama mtoto aliyezaliwa na mwanamke huyo, kwa kule kukua kutokana na maziwa yatokayo katika kifua chake, kwa hivyo ndugu wa kunyonya ni kama ndugu wa nasaba. Mwisho, Mwenyezi Mungu anataja sababu ya mwisho ya watu kuharamishiwa kuowana, sababu hii inasababishwa na ndoa iliyokwisha kufungwa, maharimu hao wametajwa katika mtiririko ufuatao: Kwanza: “…na mama wa wake zenu,” Yaani mara tu mtu anapofunga ndoa na mwanamke itakuwa ni haramu kwake kumuowa mama wa mke wake (mama 59
Shafiy, Kitabul Ummi, Jz. 5, Uk. 27 109
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 109
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
mkwe) na pia mama wa mama mkwe (bibi wa mke) na kupanda juu, ikiwa ataamua kumuacha mke wake. Hukumu hii haina sharti la kukutana kimwili kati ya wanandoa ili ithibiti uharamu wa kuolewa mama mkwe kama ilivyo katika kipengele kijacho, uharamu wa ndoa ya aina hii unaanza mara tu baada ya kukamilika kufungwa ndoa. Pili: “…na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia.” Yaani kwa kufunga ndoa tu na mwanamke hakupelekei uharamu wa kumuoa binti yake kama mke mwingine baada ya kumtaliki mama yake, bali itakuwa ni haramu kwake milele kumuoa binti wa mke wake ikiwa huyo mume atamwingilia mke wake (mama wa binti) baada ya akdi ya ndoa. Kwa kuwekwa sharti la kuingiliwa mke ili iwe haramu kwa mume kumuoa binti wa mke wake ni kwa sababu baada ya kuingiliwa anakuwa mama wa mke, ambapo tayari imeshaelezwa hukumu ya uharamu wake katika kipengele cha kwanza, kama kilivyosema: “…na mama wa wake zenu,”. Jambo la kuzingatia ni kwamba sharti la uharamu wa kuwaoa watoto wa kambo walio katika uangalizi wa baba zao wa kambo, halimaanishi ya kwamba ikiwa hawako katika uangalizi wao itafaa kuwaoa hata kama mama zao wameingiliwa baada ya ndoa, sharti hili limekuja kutokana na uhalisia wa mambo kwamba mara nyingi mwanamke mjane anapoolewa huenda na watoto wake wachanga kwa mume mpya, na wale watoto hupata huduma zao za msingi kutoka kwa baba yao wa kambo, kutokana na haya huwa kama vile watoto wake wa kuwazaa. Kwa hivyo uharamu wa kuwaowa mabinti wa kambo utabakia hata kama mabinti hao hawakulelewa na baba yao wa kambo, sharti kubwa la uharamu ni mume kukutana kimapenzi na mama yao. Tatu: “(Pia mmeharamishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu.” Huku kutajwa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu,ni kwa ajili ya kubatilishwa tabia iliyokuwepo wakati wa ujahilia, tabia hiyo ilikuwa ni kwa mtu kumuasili mtoto na kumpa haki zote alizokuwa akimpa mtoto wake wa kumzaa, walikuwa hawawaoi watalaka wa watoto wao wa kuasili kama vile walivyokuwa hawawaoi watalaka wa watoto wao wa kuwazaa. Kwa hivyo Uislamu ulikuja kufuta hukumu za mtoto wa kuasili walizojiwekea na hukumu hizo kutokuwa na nafasi yoyote katika Dini ya Kiislamu. Nne: “Na kuwaoa pamoja dada wawili” Yaani ni haramu kwa mtu kuwakusanya madada wawili kwa wakati mmoja katika ndoa, ama kuwaoa madada wawili katika zama tofauti, kwa kumuoa wa kwanza kisha akamuacha na baadaye kuoa mwingine ni jambo linalofaa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Tabia ya kuwaoa madada wawili wakati mmoja ilikuwepo katika zama za kijahilia kama isemavyo: “isipo kuwa yale yaliyokwisha pita.” Kwa hivyo ni kwamba dhambi za kosa hili hazitowapata wale
110
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 110
12/8/2014 2:43:38 PM
WITO KWA WAUMINI
waliofanya ndoa ya aina hii kabla ya kushuka Aya hii, ila walilotakiwa kulifanya ni kuchagua mmoja na kumtaliki mwingine. Siri kubwa ya kuharamishwa ndoa hii, ni kutokana na mapenzi ya hali ya juu yanayokuwepo kati ya madada wawili, kwa hivyo ikiwa watakuwa katika hali ya ushindani wa kila mmoja kutaka kupendwa zaidi na mume wao itakuwa haiwezekani tena kupendana tena wao kwa wao, na siku zote watakuwa katika hali ya ugomvi na uhasama ambao unaweza kupelekea kudhuriana wao kwa wao. Aya bado zinazidi kueleza wanawake walio haramu kuolewa na Waumini, Mwenyezi Mungu anasema: “Na wanawake wenye waume; isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni Sharia ya Mwenyezi Mungu kwenu. Na mmehalalishiwa wasiokuwa hao, kwamba Muwatafute kwa mali zenu kwa kuoa bila ya kufanya zina. Ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu. Wala si vibaya kwenu katika yale mliyoridhiana baada ya (kutoa) kile kilichowalazimu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.�
111
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 111
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO Aya hii ni mtiririko wa utafiti wa Aya zilizopita zinazoelezea wanawake walio haramu kwa mwanaume kuwaoa, katika Aya hii inataja uharamu wa kuwaoa wanawake walio na waume. Katika Aya hii Mwenyezi Mungu ametumia neno ‘Muhswanaat’ likimaanisha maana ya ngome, ni wazi kwamba mwanamke mwenye mume huwa ameihifadhi nafsi yake dhidi ya kufanya uchafu wa zina. Hukumu hii pia inawahusisha wanawake wasio waislamu, kwa hivyo mwanammke akiwa katika dini yoyote na ilhali ana mume ni haramu kwa Muislamu kumuowa. Lakini kama itakuwa mwanamke mwenye mume asie Muislamu akatekwa katika vita itafaa kwa Muislamu kumuowa baada ya kumalizika siku za eda yake, kwani Uislamu unazingatia kuvunjika kwa ndoa ile siku anayoingia katika jumla ya mateka wa kivita katika mikono ya Waislamu, au mateka huyo wa kike anaweza kuamiliwa kama mwanamke mjakazi na hapo pia inajuzu kwa bwana wake kustarehe naye kimapenzi, Mwenyezi Mungu amesema: “…isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume.” Pia Uislamu huzingatia kukatika mafungamano ya kindoa iwapo mwanamke atasilimu na mume wake kubakia katika dini yake ya kikafiri, katika hali kama hii mwanamke huyo atakaa eda, na baada ya kumalizika siku zake za eda anaweza kuolewa na mume aliye Mwislamu. Katika kusisitiza hukumu hizi Mwenyezi Mungu anasema: “Ni Sharia ya Mwenyezi Mungu kwenu.” Kwa hivyo ni uasi ulioje kwa mtu kwenda kinyume na maagizo haya yatokayo kwa Mola Muumba, au mtu kutaka kuibadilisha sheria hii na kuweka ya kwake. Baada ya kueleza wanawake walio haramu kuwaoa, anahitimisha kwa kubainisha kwamba wanawake wasio na sifa hizi zilizotajwa katika Aya hizi inafaa kwa mtu kuwaoa kwa mujibu wa mafunzo ya Dini ya Kiislamu, huku mtu akizingatia usafi wa maadili na heshima katika ndoa na kujiepusha na vitendo viovu vya zinaa, Mwenyezi Mungu anasema: “Na mmehalalishiwa wasiokuwa hao, kwamba muwatafute kwa mali zenu kwa kuoa bila ya kufanya zina.” Ndoa ya Mut’a Katika Uislamu: Mwenyezi Mungu anasema: “Ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu.” Aya hii ni miongoni mwa dalili zinazothibitisha uhalali wa ndoa ya Mut’a, pia Aya inabainisha ya kwamba suala la ndoa ya Mut’a lilikuwa ni jambo lisilo na pingamizi yoyote kati ya Waislamu kabla ya kuteremka Aya hii, ndio maana Aya ikaja kuwausia na kuwasisitiza Waislamu juu ya kuwapa 112
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 112
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
mahari hao wanawake wanaowaoa kwa ndoa ya Mut’a. Kutokana na utafiti wa jambo hili kuwa na umuhimu mkubwa katika maisha ya kijamii, tutaangazia juu ya nukta zifuatazo: 1.
Ishara zilizomo katika Aya hii zinaonesha wazi juu ya uhalali wa ndoa hii.
2.
Ndoa ya Mut’a ilikuwepo katika zama za Mtume (s.a.w.w.) na wala haikuharamishwa.
3.
Jamii inahitaji ndoa ya aina hii.
4.
Majibu yanayotokana na baadhi ya hoja.
Ama kuhusiana na nukta ya kwanza, inatupasa tuangalie mambo yafuatayo: Kwanza: Neno ‘Mut’a’ ambalo linatokana na neno ‘Istamta’tum’ linamaanisha ndoa ya muda. Kwa ibara nyingine tunasema ya kwamba ndoa ya muda ni jambo lililothibiti kisheria, kwani neno ‘Mut’a’ kama lilivyokuja katika Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Maswahaba linamaanisha ndoa ya muda. Pili: Ikiwa neno ‘Mut’a’ litakuwa halina maana ya ndoa ya muda, basi itabidi litafsiriwe kwa misingi ya kilugha, na maana yake kilugha ni ‘Kunufaika’ kwa hivyo maana ya Aya itakuwa ni: “Mtakaponufaika na wake wenu wa ndoa ya kudumu, basi wapeni mahari yao.” Nijambo linaloeleweka ya kwamba hakuna sharti la kunufaika katika kutoa mahari kwa wanawake wa ndoa ya kudumu, bali ni wajibu kupewa mahari yake yote au nusu yake mara baada ya kufungwa ndoa. Tatu: Maswahaba wakubwa wakubwa na matabiina, kwa mfano, ibn Abbas, Ubayya ibn Ka’b, Jabir ibn Abdillahi al-Aswariy, Imran ibn Huswayn, Mujahid, Qutada, Saddiy, na wafasiri wengi wa madhehebu ya kisunni pamoja na ya kishia, wote hao wameifahamu Aya hii kwamba inaelezea juu ya ndoa ya Mut’a, kiasi ya kwamba Fakhru Raziy, licha ya shaka zake nyingi kuhusiana na mambo wanayoyaitakidi Mashia, baada ya kufanya utafiti wa kina amesema hivi: “Jambo ambalo linastahiki kulitegemea katika mlango huu, ni kusema ya kwamba Aya hii imefutwa, pamoja na hayo, lau kama Aya hii inatoa dalili juu ya uhalali wa ndoa ya Mut’a, basi jambo hilo halidhurishi lengo letu. Hili pia ndilo jawabu kutokana na kushikamana kwao na kisomo cha Ubayya na ibn Abbas, kwani kwa hakika visomo vyao kwa kuzingatiwa kusihi kwao, havimaanishi isipokuwa ni kuonesha ya kwamba ndoa ya Mut’a ilikuwa ni halali, na sisi hatuna shaka juu ya hili, bali tunasema ni kwamba sheria hii imefutwa.”60 60
Raziy, Tafsirul Kabir, Jz. 10, Uk. 53 113
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 113
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
Nne: Maimamu Watoharifu watokanao na nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) wote kwa pamoja wamewafikiana juu ya uhalali wa ndoa hii kwa mujibu wa Aya hii, wao ndio watambuzi zaidi wa Qur’ani baada ya Mtume (s.a.w.w.). – Jambo la kuzingatia katika maudhui haya ni kwamba tofauti iliyopo kati ya Waislamu ni juu ya kubakia uhalali wa ndoa hii, na mzozo haupo juu ya kufanyika ndoa hii wakati wa Mtume (s.a.w.w.), kwani maulamaa wote wanakiri kwamba ndoa hii ilifanyika katika zama za Mtume (s.a.w.w.) katika sehemu tofauti. Maneno ya Khalifa Umar ibn Khattab ni dalili tosha juu ya uhalali wa ndoa hii, pale aliposema: “Mut’a mbili zilikuwepo wakati wa zama za Mtume na mimi naziharamisha na nitamuadhibu mwenye kufanya Mut’a mbili hizo, nazo ni Mut’a ya wanawake na Mut’a ya Hijja.” 61 Maneno haya aliyoyasema Umar wakati wa ukhalifa wake ni dalili ya wazi ya kuwepo jambo hili katika zama za uhai wa Mtume (s.a.w.w.). Lakini wale wanaoiharamisha ndoa hii wanadai ya kwamba baadaye ilifutwa na kuharamishwa. Jambo la kuzingatia ni kwamba Riwaya wanazozitegemea katika kuharamishwa ndoa hii ni riwaya zenye mazonge, kwani baadhi yake zinadai ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) ndiye aliyeiharamisha, hivyo ikiwa tutakubaliana na hili, itamaanisha ya kwamba Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) inaweza kufuta hukumu iliyothibiti katika Qur’ani, na wengine wanasema ya kwamba ndoa hii imefutwa na Aya ya talaka, pale Mwenyezi Mungu aliposema: “Ewe Nabii! Mnapowaacha wanawake basi waacheni katika wakati wa eda zao…” Aya hii haina mafungamano yoyote na suala la ndoa ya Mut’a, kwani Aya hii inazungumzia suala la talaka katika hali ambayo ndoa ya Mut’a haina talaka, kwani mtengano kwa waliofunga ndoa ya Mut’a unatokea pale tu muda waliokubaliana kumalizika. Jambo lisilo na shaka wala khitilafu baina ya wanachuoni ni kwamba ndoa ya Mut’a ilikuwepo katika zama za uhai wa Mtume (s.a.w.w.), na hakuna dalili yenye nguvu ya kuthibitisha kuharamishwa kwake, kwa hivyo jambo la msingi kwa mujibu wa elimu ya usuli ni kubakia hukumu yake ya asili, maneno ya Umar ni ushahidi wa wazi wa kutokuharamishwa wakati wa zama za Mtume (s.a.w.w.) Ni suala lililo wazi ya kwamba hakuna yoyote aliye na mamlaka ya kufuta hukumu yoyote katika hukumu za Kiislamu isipokuwa Mtume (s.a.w.w.) tena ni pale atakapoamrishwa na Mola Wake. Mlango wa kufuta hukumu za Kiislamu ulishafungwa tokea alipofariki Mtume (s.a.w.w.), na lau kama ungekuwa wazi, basi kila mmoja angethubutu kufuta hukumu za Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa jitihada yake na matakwa yake, na kusingelibakia hukumu yoyote ya kisheria katika Uislamu. 61
Sahih Muslim Juz. 4, uk. 131 chapa ya Mashkul, Musnad Ahmad Juz. 6, Uk. 405 na Fat’hu Baari Juz. 9, uk.149. na wengine wengi. 114
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 114
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
Jambo la kuzingatia ni kwamba watu hawakuwa tayari kumsikiliza Umar na kuacha mambo yaliyothibiti katika Uislamu, miongoni mwa watu hao ni mtoto wa Umar, maarufu kwa jina la Ibn Umar. Siku moja aliulizwa na mtu mmoja kutoka katika mji wa Sham kuhusiana na Hajj Tamattu’i, Ibn Umar alisema: “Ni jambo jema na lililo zuri.” Yule mtu akasema: “Lakini baba yako alikuwa akiikataza.” Ibnu Umar akasema: Ole wako! Ikiwa baba yangu aliikataza na Mtume (s.a.w.w.) aliifanya na kuiamrisha, je! Nichukue kauli ya baba yangu au amri ya Mtume (s.a.w.w.), hebu niondokee!”62Mfano wa Riwaya kama hii imepokewa katika kitabu cha Sunan Tirmidhiy inayohusiana na Mut’a kutoka kwa huyo huyo mtoto wa Umar; Abdullahi bin Umar. Na katika kitabu Al-Muhadharaat cha Raghib, ni kwamba mtu mmoja alikuwa akifanya Mut’a, akaulizwa: “Ni kwa nani umechukua uhalali wake?” Akajibu: “Ni kutoka kwa Umar.” Watu walimuuliza: “Ni vipi, na wakati Umar alikuwa akiikataza?” Akawajibu: “Ni kutokana na kauli yake pale aliposema: Mut’a mbili zilikuwepo wakati wa zama za Mtume na mimi naziharamisha na nitamuadhibu mwenye kufanya Mut’a mbili hizo, nazo ni Mut’a ya wanawake na Mut’a ya Hijja. Kwa hivyo mimi nakubaliana na maneno yake juu uhalali wake wakati wa zama za Mtume (s.a.w.w.) na sikubaliani na kuikataza kwake kwa sababu tu yakufuata matamanio ya nafsi yake.”63Kwa hakika wale wanaodai ya kwamba ndoa ya Mut’a imeharamishwa wanakumbana na mishikeli mingi, miongoni mwao ni kama ifuatavyo: Kwanza: Kwa mujibu wa vitabu vinavyotegemewa na Massuni, kuna riwaya za wazi kabisa zinazoeleza ya kwamba ndoa ya Mut’a haikuharamishwa wakati wa zama za Mtume (s.a.w.w.), bali iliharamishwa katika zama za ukhalifa wa Umar, kwa hivyo wale wanaodai kuharamishwa ni juu yao wazijibu Riwaya zinazofikia ishirini alizozikusanya Allamatul Amin katika kitabu chake cha Al-Ghadir, katika juzuu ya sita, miongoni mwa Riwaya hizo ni kama ifuatavyo: Imepokewa katika kitabu cha Sahihi Muslim kutoka kwa Jabir bin Abdillahi al-Answariy, ni kwamba alikuwa akisema:
كنّا نستمتع بالقبضى من التّمر وال ّدقيق األيّام على عهد رسول اهلل (ص) وأبي بكر حتّى نهى عنه عمر في شأن .عمرو بن حريث 62 63
Qurtubiy, Tafsirul Qurtubiy, Jz. 2, Uk. 388 Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 3, Uk. 182 115
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 115
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
“Tulikuwa tukifanya Mut’a kwa funda la tende na unga kwa masiku kadhaa wakati wa zama za Mtume (s.a.w.w.) na Abu Bakar, kisha Umar aliikataza kutokana na tukio la Amru ibn Hureith.”64
Riwaya hii ni mfano tu wa Riwaya nyingi zilizo kama hii. Pili: Riwaya zinazoelezea kuharamishwa kwa Mut’a katika zama za Mtume (s.a.w.w.) zinagongana na kupingana zenyewe kwa zenyewe, baadhi yake zinasema iliharamishwa Khaybar, na baadhi zinasema iliharamishwa wakati ilipokombolewa Makka, nyingine zinasema iliharamishwa wakati wa vita vya Tabuk, nyingine zinasema iliharamishwa wakati wa siku ya Awtwasi. Hali hii inabainisaha ya kwamba riwaya hizi ni za uzushi kutokana na kutokuwa na muelekeo mmoja. Kutokana na ukweli na uhalali wa ndoa hii, mwandishi wa tafsiri ya Manar anasema: “Tulisema katika mjadala ya kwamba Umar aliikataza ndoa ya Mut’a kutokana na jitihada yake na Maswahaba waliafiki rai yake, lakini baadaye ikatubainikia ya kwamba tulikosea, basi tunamuomba msamaha Mwenyezi Mungu kutokana na kosa hilo.”65 Ni wazi kwamba si Umar wala mtu mwingine aliye na haki ya kuharamisha jambo katika sheria za Mwenyezi Mungu, hata hao Maimamu Watoharifu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) ambao ndio Makhalifa wa kweli wa Mtume (s.a.w.w.) nao pia hawana haki hii, na huku baadhi ya watu kudai kwamba ni jitihada ya Umar, ukweli wa mambo ni kwamba Uislamu haukubaliani na jitihada mbele ya maandiko yaliyothibiti hukumu yake na kuwa wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.) Na miongoni wa watu ambao hawakukubaliana na uamuzi wa Khalifa Umar juu ya uharamu wa ndoa ya Mut’a ni Ibn Jureij, ambaye alikuwa ni mwanachuoni mkubwa miongoni mwa wanachuoni wa Makka, yeye ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa wa kuandikwa Hadithi baada ya kupita muda mrefu wa amri ya kukatazwa kuandikwa, amri iliyoanzwa kutolewa na Khalifa wa kwanza hadi kufikia zama za ufalme wa Umar bin Abdul Aziz. Jina la mwanachuoni huyo linadhihirika katika sanadi za wapokezi karibu katika vitabu vyote vya Hadithi, vikiwemo vitabu sita vilivyo sahihi kwa mujibu wa itikadi ya Kissuni. Wakati wa siku za mwisho wa uhai wake aliwaita watoto wake na kuwausia, miongoni mwa usia wake aliwatajia majina ya wanawake sitini, na kuwaambia kwamba hao ni mama zao wa kambo, aliofunga nao ndoa ya Mut’a, kwa hivyo wasije wakawaoa. Dhahabiy amemueleza mwanachuoni huyo kama ifuatavyo: “IbnJureij ni Imamu na mwenye kuhifadhi, ni mwanachuoni wa Haram (Makka), pia anajulikana kwa 64 65
Muslim, Sahihu Muslim, Jz. 4, Uk.1 Tafsirul Manar, Jz. 5, Uk. 16 116
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 116
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
Abul-Walid na Abu Khalid, Abdul Malik bin Abdul Aziz ibn Jureij… ni mkaazi wa Makka, ni mwanchuoni ni mtu aliyeandika vitabu vingi na ni mmoja wa wataalamu wa Hadithi.” Katika kuendelea kumzungumzia habari zake, Dhahabiy amemnukuu Imamu Ahmad akisema: “Ibn Jureij alikuwa ni chombo cha elimu, na ni wa kwanza kuandika vitabu.” – Ama kuhusiana na ndoa hii ya Mut-a Dhahabiy anasema: “Amesema Jariir:Ibn Jureij alikuwa akiona uhalali wa ndoa ya Mut’a, na alioa wanawake sitini.”66 Imam Shafi’i naye amenukuliwa akisema: “Ibn Jureij alifanya Mut’a na wanawake tisini, na wakati wa usiku alikuwa akitumia dawa kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume.”67 Pia Ibn Jureij katika kujipendezesha zaidi kwa akina mama alikuwa akizitia rangi nyeusi nywele zake na kuvaa mavazi yenye thamani.68 La kushangaza zaidi ni kwamba baadhi ya wanachuoni wa Kisunni wanaona ya kwamba Aya ya sita ya Suratul Muuminuna imekuja kuifuta ndoa ya Mut’a, kama kwamba hawakuzingatia kuwemo Mut’a katika orodha ya ndoa. Ndoa ya Mut’a ni rehema kwa Jamii: Ni tabia ya kila mwanadamu kuwa na matamanio ya kimwili, iwapo matamanio haya hayakukidhiwa katika njia iliyo sahihi, kinyume chake yatakidhiwa katika njia ya haramu, kwani ni jambo lisilo na shaka yoyote ile kwamba, matamanio ya mwanadamu hayawezi kumalizwa kwa mara moja. Kutokukidhi matamanio ya kimapenzi ni kuingia katika vita vya kimaumbile, kwa hivyo njia iliyo sahihi ni kuitosheleza nafsi kwa kuishibisha kutokana na tatizo la matamanio ya kimwili, hilo litakamilika kwa kufuata njia sahihi. Wataalamu wa elimu ya Saikolojia wanaona kwamba, matamanio ya kijinsia ndio matamanio ya asili ya matamanio mengine. Ikiwa hali ndio kama hii, kuna suala linajitokeza, ikiwa mtu asiyekuwa na uwezo wa kuoa ndoa ya daima, au ikiwa kuna mtu aliyeoa lakini yuko katika safari ndefu ambayo inamtenganisha na mke wake kwa kipindi kirefu, na akakumbana na matatizo ya matamanio ya kimwili ambayo yanahitaji kutatuliwa na kuridhishwa, au hali ikiwa kama hivi ilivyo leo katika maisha yetu, ya kuwafanya vijana wengi wachelewe kuoa kutokana na muda wa kusoma kuwa mrefu, na anapomaliza hana uhakika wa kupata ajira, unadhani ni jambo gani anatakiwa afanye kijana huyo katika hali kama hii? Je! Inawapasa watu wa aina hii wajihisi kama wanavyofanya baadhi ya watawa? Dhahbiy, Tadhkiratul Hufadh, Jz. 1, Uk. 170 Dhahabiy, Sayru A’lami Nnubalai, Jz. 6 68 Kitabu kilichotangulia 66 67
117
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 117
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
Au wapewe uhuru wa kufanya wapendavyo katika kuondosha matamanio yao? Au itawapasa wafuate njia ya tatu isiyo na gharama kubwa kama ilivyo kwa ndoa ya kudumu na iliyo na suluhisho la tatizo la matamanio? Kimukhtasari ni kwamba, ndoa ya kudumu si ndoa inayokidhi matamanio ya kijinsia katika zama hizi na pia katika zama zilizopita, wala kuweza kufanywa na watu wa matabaka yote katika jamii. Kilicho mbele yetu ni mambo mawili, ama kuruhusu uhuru wa kufanya mapenzi kama ilivyo leo katika nchi za Ulaya pamoja na Marekani, au kulisuluhisha tatizo hili kwa njia ya kuruhusu ndoa ya Mut’a kama ilivyokuwa katika zama za Mtume (s.a.w.w.) Hoja Dhidi ya Ndoa ya Mut’a: Ni jambo linalofahamika kwa watu wengi kwamba, kuna hoja mbali mbali zinazotolewa dhidi ya Mut’a, tunapenda hapa tuzitaje baadhi yake na kuzitolea majibu japo kwa mukhtasari. Baadhi ya watu wanauliza, kuna tofauti gani kati ya zinaa na ndoa ya Mut’a? Je, zote hizi si kuuza mwili kwa thamani maalumu, huku wakijifichia sitara kile kinachoitwa akdi katika Mut’a, na hiyo akdi ni ibara tu iliyo fupi sana? Jawabu: Wale ambao wanayakariri maneno haya mara kwa mara ni kwamba bado hawajajua madhumuni ya ndoa ya Mut’a na uhalisia wake, kwani Mut’a si tu ibara mbili zinazosemwa na kisha mwanamke kuwa halali kwa mwanamme, bali kuna hukumu kama zilivyo katika ndoa ya kawaida (ya kudumu), kwani mwanamke aliyefunga akdi ya ndoa ya Mut’a anabakia katika hifadhi ya mume wake mpaka muda waliokubaliana kumalizika, muda unapomalizika ni wajibu kwa mwanamke kukaa eda kwa siku arobaini na tano au hedhi mbili kwa mwenye kupata siku zake za mwezi, ili ibainike ya kwamba amepata ujauzito kwa huyo mume wake wa kwanza au hakupata. Ni wajibu kwake kukaa eda hata kama alitumia njia ya kuzuia mimba, na iwapo amepata mtoto itampasa mume kumuangalia mtoto huyo kama anavyomuangalia mtoto wa ndoa ya kudumu, na kupatiwa haki zake zote za kimsingi, ama katika zinaa na uasherati hakuna hata hukumu moja miongoni mwa hukumu hizi, je itakuwa ni sawa Mut’a kufananishwa na zinaa? Ni kweli kwamba kuna baadhi ya tofauti kati ya ndoa ya Mut’a na ndoa ya kudumu, kama vile kutorithiana kati ya wanandoa wawili wa ndoa ya Mut’a na baadhi ya hukumu nyingine, lakini tofauti hizi hazifanyi ndoa hii kuwa sawa na zinaa au umalaya. Hoja nyingine wanayoitoa ni kwamba, baadhi ya watu huichukulia ndoa ya Mut’a kama ni kimbilio na sitara ya kufanyia ufisadi na uchafu. Jawabu la hoja hii ni kwamba, ni kanuni gani katika zama zetu hizi ambayo watu hawaitumii vibaya? Je, ndio itakuwa ni jambo lililo sahihi kuwazuilia watu 118
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 118
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
jambo lililokubalika kwa mujibu wa sheria na akili iliyotimamu, eti kwa hoja baadhi ya watu wanaitumia vibaya. Kwa mfano ikiwa baadhi ya watu wanauza mihadarati wakati wa msimu wa Hijja kwa baadhi ya mahujaji, je wajibu utakuwa ni kwa watu kuzuiliwa wasifanye ibada ya Hijja au kuzuiliwa wale wale wafanyao biashara hii chafu wasiendelee na biashara yao? Hali ndio kama hii katika ndoa ya Mut’a, ni kwamba watu hawajagundua aibu katika hukumu yake, bali wamegundua aibu kwa watumiaji, au kwa ibara iliyo sahihi zaidi ni kwamba wamegundua aibu kwa wanaoitumia vibaya hukumu hii. Lau kama serikali za Kiislamu zingelisimamia nidhamu na taratibu za ndoa ya Mut’a, basi kusingelitokea watu ambao wanaitumia vibaya fursa hii na Rehema hii itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja Wake. Tumalizie na hoja nyingine isemayo: Ndoa ya Mut’a husababisha kuwepo watoto wasiokuwa na familia, kama vile zinaa inavyosababisha watoto wasio wa kisheria. Jawabu lake ni kwamba, Jawabu la suala hililiko wazi katika jawabu la hoja iliopita, kwani watoto wa nje ya ndoa hawafungamani na wazazi wao kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, wakati ambapo watoto waliopatikana kwa kupitia ndoa ya Mut’a hawana tofauti na watoto wengine waliozaliwa kwa kupitia ndoa ya kudumu ikiwemo mirathi na haki nyingine za kijamii. – Hoja hizi zimekuja kutokana na kutokuwa makini juu ya ukweli na uhakika wa ndoa ya Mut’a. Baada ya kumaliza kutaja wajibu wa kulipa mahari, Mwenyezi Mungu amesema: “Wala si vibaya kwenu katika yale mliyoridhiana baada ya (kutoa) kile kilichowalazimu.” Yaani si vibaya kwa wanandoa wawili kukubaliana kupunguza au kuongeza mahari ikiwa kila mmoja ataridhika na suala hili. Hakuna tofauti katika hili kati ya ndoa ya kudumu au ya Mut’a, licha ya ibara hii kuja katika maudhui ya ndoa ya Mut’a. Mwenyezi Mungu amemalizia Aya hii kwa ibara isemayo: “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.” Kutokana na ibara hii Mwenyezi Mungu anataka kutufahamisha ya kwamba, hukumu zilizotajwa katika Aya hii zinamanufaa na maslahi makubwa kwa waja wake, kwani Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa maslahi yao na ni Hakimu kwa yale anayoyapitisha katika sheria zake. Mwenyezi Mungu anaendelea kuwapa maelekezo waja Wake Waumini, anasema: “Na asiyeweza miongoni mwenu kupata mali ya kuoa wanawake waungwana waumini, basi (na aoe) katika wajakazi wenu waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kuume; na Mwenyezi Mungu anajua sana imani yenu. Baadhi yenu mnatokana na baadhi; basi waoeni kwa idhini ya watu wao na muwape mahari yao kama ada wawe ni wenye kujistahi si waasherati wala wenye kujifanyia mahawara. Wa119
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 119
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
takapoolewa kisha wakafanya uchafu, basi itakuwa adhabu juu yao ni nusu ya adhabu iliyowekwa kwa waungwana. Hayo ni kwa mwenye kuchelea mashaka katika nyinyi. Na mkisubiri ni bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.” Aya hii inaelezea masharti yanayotakiwa kufuatwa ikiwa mtu anataka kumuoa mwanamke mjakazi, inaanza kwa kutaja sharti ya kwanza isemayo: “Na asiyeweza miongoni mwenu kupata mali ya kuoa wanawake waungwana waumini, basi (na aoe) katika wajakazi wenu waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kuume” Kwa maana, wale wasio na uwezo wa kimali wa kuweza kuwaoa wanawake waungwana walioamini, basi inafaa kuoa wanawake wajakazi walioamini, kwani kwa kawaida mahari yao na matumizi yao ya kila siku ni madogo ikilinganishwa na wanawake walio huru. Kijakazi aliyekusudiwa hapa ni kijakazi anayemilikiwa na mtu mwingine, kwani haijuzu mtu kumuoa mjakazi wake na kumtendea kama mke, bali anakuwa huru kufanya naye mapenzi bila kupitisha akdi ya ndoa. Jambo la kuzingatiwa katika Aya hii ni kwamba haifai kuoa kijakazi asiyekuwa Mwislamu. Mwenyezi Mungu anamalizia kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu anajua sana imani yenu.” Anawaeleza Waumini ya kwamba wao hawana haki ya kuchunguza kwa undani imani za wajakazi wanaotaka kuwaoa, bali watosheke na hali ya nje ya imani yao, ama ndani ni Mwenyezi Mungu tu Ndiye anayeijua, kwani Yeye Ndiye peke yake anayetambua mambo ya siri. Baadhi ya watu walikuwa wakichukia kuwaoa wajakazi, Mwenyezi Mungu alilijua jambo hilo, kwa hivyo alisema: Baadhi yenu mnatokana na baadhi.” Anamaanisha ya kwamba, nyinyi mnatokana na baba mmoja na mama mmoja, kwa hivyo haikupasini kuchukia kuwaoa wajakazi, kwani wao hawana tofauti yoyote na nyinyi katika maumbile ya kibinadamu, na wanalingana nanyi katika utukufu wa kiroho, na utukufu wa kila mtu unatokana na uchaji Mungu wake na si kingine. - Mukhtasari wa maneno ni kwamba, hakika wajakazi ni wanadamu kama nyinyi na nyinyi nyote ni kama kiungo kimoja. Miongoni mwa masharti ya kusihi ndoa ya mjakazi ni kupata idhini ya bwana wake, kinyume chake ndoa itakuwa batili, kama alivyoeleza Mwenyezi Mungu: “Basi waoeni kwa idhini ya watu wao.” Katika kuamiliana na mjakazi inapasa kuwa katika muamala wa kibinadamu na haipasi kufanywa kama ni chombo cha starehe au bidhaa, katika ibara hii, mjakazi amezingatiwa kama ni sehemu ya familia, kwa hivyo ni lazima ipatikane idhini ya ndoa kutoka kwa wale wanaowamiliki. Mwenyezi Mungu anataja sharti jingine kwa kusema: “…na muwape mahari yao kama ada.” Katika ibara hii tunajifunza ya kwamba, mahari atakayopewa 120
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 120
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
lazima yalingane na nafasi yake, na mahari hayo yatakuwa milki yake kama Aya inavyoashiria, licha ya kuwepo baadhi ya rai za wafasiri zinazoeleza ya kwamba mahari yanatakiwa wapewe wale wanaowamiliki, rai hii haiwafikiani na dhahiri ya Aya, pamoja na kuwepo baadhi ya Riwaya wanazozitegemea katika rai yao. Pia tunafaidika katika ibara hii ya kwamba haifai kumdhulumu mjakazi katika kuainisha mahari, kwani hiyo ni haki yake ya kimsingi ambayo inapasa apewe bila ya kudhulumiwa kwa sababu tu yeye ni mjakazi. Sharti jingine alilolitaja Mwenyezi Mungu ni kwa mwanamme kuchagua mjakazi mwema mwenye heshima na adabu, amesema: “Wawe ni wenye kujistahi si waasherati wala wenye kujifanyia mahawara.” Maana nyingine ya hawara ni kimada, ikiwa na maana mwanamke mzinifu katika hali ya usiri wa hali ya juu sana, kinyume chake ni kahaba. Hapa inadhihirika sababu ya kutajwa aina zote mbili za wazinifu. Baada ya sharti hili, hapa panatajwa aina ya adhabu ya zinaa kwa mwanamke mjakazi, Mwenyezi Mungu anasema: “Watakapoolewa kisha wakafanya uchafu, basi itakuwa adhabu juu yao ni nusu ya adhabu iliyowekwa kwa waungwana.” Mwenyezi Mungu anataja sababu ya Waumini waungwana kuruhusiwa kuwaoa wajakazi, anasema: “Hayo ni kwa mwenye kuchelea mashaka katika nyinyi.” Ni wazi kwamba hukumu ya kuoa wajakazi ni kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi waliyonayo baadhi ya watu, kiasi ya kutokuwa na uwezo wa kuoa mwanamke muungwana, kwa hivyo haifai kwa mtu mwenye uwezo wa kiuchumi kumuoa mwanamke mjakazi. Huenda hekima kubwa ya kuzuiliwa kuoa wajakazi katika zama hizo, ni kutokana na wajakazi wengi kukosa malezi ya heshima na adabu, kwa hivyo ilikuwa inakhofiwa kwa watoto kuathirika na tabia za mama zao, kwa hivyo ndio maana Uislamu ukahimiza suala la kuwaacha watumwa huru, ili waondokane na tabia mbaya walizokuwa nazo, na wakati huo huo ukafungua milango ya kuoana wao kwa wao. Hukumu hii haipingani na hali ya baadhi ya wajakazi waliokuwa wakisifika kwa tabia nzuri, kwa hivyo hukmu ya Waumini kuwaoa wajakazi ililenga katika hali ya kukosa malezi mazuri kwa wajakazi walio wengi katika zama hizo, ama ikiwa mjakazi ni mwenye malezi na tabia nzuri hakuna ubaya kuolewa na Muumini mwenye uwezo, kama walivyofanya Maimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) Jambo la msingi la kuzingatia, ni kwamba lililozuiwa ni kuwaoa wajakazi kwa mtu mwenye uwezo wa kuoa waungwana, ama mwenye kumiliki mjakazi ana haki ya kulala naye bila ya kizuizi chochote. Mwenyezi Mungu anamalizia Aya hii kwa kusema: “Na mkisubiri ni bora kwenu.” Yaani ikiwa watu watavumilia kutowaoa wajakazi na hawatojiingiza
121
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 121
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
katika vitendo vya zinaa,itakuwa ni jambo bora zaidi na lenye maslahi kwao: “Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.” Atakusameheni yale mliyoyafanya kutokana na kutokujua au kwa kughafilika na ni Mwenye huruma nyingi kwenu. Katika wito huu mkubwa kwa Waumini, Mwenyezi Mungu anamalizia kwa Aya tatu zilizobakia, kwa kusema: “Mwenyezi Mungu anataka kuwabainishia na kuwaongoza mwendo wa waliokuwa kabla yenu na awatakabalie toba. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima. Na Mwenyezi Mungu anataka kuwatakabalia toba, na wale ambao hufuata matamanio wanataka mkengeuke mkengeuko mkubwa. Mwenyezi Mungu anataka kuwahafifishia. Na mtu ameumbwa hali yakuwa ni dhaifu.” Kwa Nini Kukawekwa Masharti Haya? Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja masharti mbali mbali yanayohusiana na suala la ndoa, huenda kukajitokeza masuala katika baadhi ya vichwa vya watu, masuala hayo ni kama yafuatavyo: Kuna lengo gani la kuwekwa masharti haya yote? Na kuna umuhimu gani wa kuwepo kwa kanuni hizi? Kwa nini Waumini wasipewe uhuru wa kufanya wanavyoona wao ili na wao wastarehe kama vile wasiokuwa waumini wanavyostarehe bila ya mipaka? Aya tulizozinakili hapo juu ni jawabu tosha kwa masuala haya, kwani Mwenyezi Mungu anasema: “Mwenyezi Mungu anataka kuwabainishia na kuwaongoza mwendo wa waliokuwa kabla yenu na awatakabalie toba.” Yaani Mwenyezi Mungu anakubainishieni ukweli kwa kupitia kanuni hizi na kukuelekezeni kule kuliko na maslahi yenu, huku akielewa ya kwamba kanuni hizi haziwahusu nyinyi tu, ni kwamba zilikuwepo na kufuatwa na watu wema waliokuwepo kabla yenu, zaidi ya hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu anataka kukusameheni na kukurudishieni neema ambazo alizisitisha kwa sababu ya kwenda kwenu kinyume na njia ya haki. “Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.” Anazijua siri na hekima zilizomo katika kanuni alizo kuwekeeni, kwani huziweka kwa ujuzi Wake na hekima Zake. Kisha Mwenyezi Mungu anatilia mkazo zaidi hayo aliyokwisha yaeleza, anasema: “Na Mwenyezi Mungu anataka kuwatakabalia toba, na wale ambao hufuata matamanio wanataka mkengeuke mkengeuko mkubwa.” Anakusudia ya kwamba, kwa kupitia kanuni hizi anataka kukurejesheeni neema alizozizuia kutokana na uzito
122
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 122
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
wa madhambi yenu, lakini wale waliobobea katika maasi wanapenda wakuoneni na nyinyi mmeingia katika maasi kama wao, kwa hivyo hizi kanuni alizokuwekeeni ndizo zenye manufaa kwenu kuliko huo uhuru unaodaiwa na watu wengine, ni uhuru uliozungukwa na ufisadi. Pia Aya hizi ni jawabu tosha kwa wale wanaoishi katika zama hizi, ambao wanapinga kuwepo kwa kanuni zilizowekwa katika suala la mapenzi ya kijinsia, na huku zikiwaambia ya kwamba: Uhuru bila ya mipaka hauna faida yoyote isipokuwa kueneza ufisadi na uchafu katika jamii. Leo tunashuhudia kwa macho yetu magonjwa sugu na yale yasio na kinga wala dawa yatokanayo na zinaa iliyokithiri, pia kuongezeka kwa watoto wa mitaani ambao asilimia kubwa wanatokana na zinaa, watoto wa aina hii ndio chanzo kikubwa cha ujambazi na uhalifu katika mataifa mengi. Mwisho kabisa Mwenyezi Mungu anamalizia kwa kusema: “Mwenyezi Mungu anataka kuwahafifishia. Na mtu ameumbwa hali yakuwa ni dhaifu.� Hii ni ishara juu ya hukumu na kanuni zilizotajwa katika ndoa ya wajakazi, zina lengo la kukhafifishiwa Waumini, kwani mwanadamu ameumbwa akiwa ni kiumbe dhaifu, pindi anapokumbana na matamanio ya kijinsia na kumzunguka kila upande huhangaika huku na kule katika kuiondosha hali hiyo, kutokana na huruma ya Mwenyezi Mungu kwa kiumbe huyo dhaifu amemuwekea njia ya kukidhi matamanio yake, hata kama ni mjakazi ikiwa hana uwezo wa kuoa muungwana, ili asije kutumbukia katika ufisadi na balaa.
123
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 123
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI
ْ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اط ِل إِ اَّل أَ ْن ِ ين آ َمنُوا اَل َتأ ُكلُوا أَ ْم َوالَ ُك ْم َب ْي َن ُك ْم ِب ْال َب َ اض ِم ْن ُك ْم َو اَل َت ْقتُلُوا أَ ْن ُف َس ُك ْم إِ َّن اللهََّ َك َ َت ُك ان َ ون ِت َج ٍ ار ًة َع ْن َت َر َ ِب ُك ْم َر ِحي ًما َو َم ْن َي ْف َع ْل َ ٰذلِ َك ُع ْد َوا ًنا َو ُظ ْل ًما َف َس ْو ارا ً صلِي ِه َن ْ ُف ن َ َو َك يرا إِ ْن َت ْج َت ِنبُوا َك َبا ِئ َر َما تُ ْن َه ْو َن َع ْن ُه ً ان َ ٰذلِ َك َعلَى اللهَِّ َي ِس نُ َك ِّف ْر َع ْن ُك ْم َسيِّ َئا ِت ُك ْم َونُ ْد ِخ ْل ُك ْم ُم ْد َخ اًل َك ِري ًما َو اَل َت َت َمنَّ ْوا َما َُّض َل الله ْ يب ِم َّما َْض ُك ْم َعل َّ َف َ ٌ ص اك َت َسبُوا ع ب ى ٰ ع ب ه ب ِّ ِْض ل َ َ ِ ال َن ِ ِ لر َج ٍ ِ ْ يب ِم َّما ْ اسأَلُوا اللهََّ ِم ْن َف َ ضلِ ِه إِ َّن اللهََّ َك َ اك َت َسب ٌ ص ان ْ ْن َو ِ َولِلنِّ َسا ِء َن ِب ُك ِّل َش ْي ٍء َعلِي ًما “Enyi ambao mmeamini! Msiliane mali zenu baina yenu kwa batili; ila itakapokuwa ni biashara kwa kuridhiana baina yenu. Wala msijiue. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye rehema kwenu. Na atakayefanya hilo kwa uadui na dhulma, tutamtia motoni. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi. Mkijiepusha na (madhambi) makubwa mnayokatazwa, basi tutawafutia makosa yenu (madogo) na tutawatia mahali patukufu. Wala msitamani aliyowafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko baadhi nyingine. Wanaume wana fungu katika walichokichuma na wanawake wana fungu katika walichokichuma. Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila Zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.” (Qur’ani 4:29-32)
Uchumi Mzuri ni Sababu ya Utulivu wa Jamii: Aya ya kwanza kati ya Aya hizi nne, inaelezea msingi wa kisheria unaodhibiti uchumi katika Uislamu. Aya inawahutubia Waumini kwa kusema: “Enyi ambao mmeamini! Msiliane mali zenu baina yenu kwa batili;” Hii ni wazi kwamba kutumia mali ya mtu mwingine pasi na haki au bila ya sababu inayokubalika kiakili ni jambo lisilofaa na ni haramu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Ulaji wa mali kwa batili na dhulma unaingia katika kila muamala wa kimali, ambapo upande mmoja 124
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 124
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
utaudhulumu upande mwingine, kama vile, riba, kamari, utapeli, ghushi, biashara ya vitu vya maasi. Leo kwa kuenea mitandao ya simu katika kila kona, biashara ya kamari imechukuwa nafasi kubwa katika kula mali za wengine kwa njia ya haramu, huendeshwa kwa mtu kutuma neno maalumu na hukatwa kiasi fulani cha pesa, na pesa hizo zinazopatikana kutoka kwa watu wengi hununuliwa kitu na kuchaguliwa mmoja kati ya washiriki na kupewa, huku faida kubwa huenda kwa waendeshaji wa mchezo huo mchafu wa kamari. Mwenyezi Mungu anaendelea kwa kusema: “…ila itakapokuwa ni biashara kwa kuridhiana baina yenu.” Utumiaji wa mali ya mtu mwingine unafaa tu pale utakapokuwa ni katika biashara waliyokubaliana na kuridhiana kila upande, na zaidi ya hilo iwe ni katika muamala unaokubalika kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu na kwa bidhaa zilizo halali. Ndani ya Aya hii pia Mwenyezi Mungu anakataza mtu kujiuwa mwenyewe, anasema: “Wala msijiuwe.” Ibara hii inafuatiwa na ibara isemayo: “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye rehema kwenu.” Inabainisha ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mweye huruma nyingi kwa waja Wake, kwa hivyo kama vile ambavyo haridhiki kwa mtu kumuuwa mwenzake pia haridhiki kwa mtu kujiuwa mwenyewe. Hapa kuna suala linalojitokeza, nalo ni: Kuna mafungamano gani kati ya suala la mtu kujiuwa mwenyewe na utumiaji wa mali ya mwingine kwa njia ya dhulma? Jawabu la suala hili liko wazi sana, kwa ukweli ni kwamba Mwenyezi Mungu ameyataja masuala haya mawili kwa kufuatana kutokana na umuhimu mkubwa wa maisha ya kijamii. Ni kwamba ikiwa hali ya uchumi katika jamii yoyote ile si nzuri kwa sababu ya ufisadi unaofanywa na baadhi ya watu, na watu wengine kudhulumiwa mali zao, basi jamii hiyo itakuwa kama kwamba imejinyonga yenyewe, kwani kuporomoka hali ya uchumi kwa mtu mmoja mmoja ndio sababu ya kuporomoka kwa jamii nzima. Hali ya kiuchumi ilivyo hivi leo katika baadhi ya nchi, hasa zile zinazoendelea ni dalili tosha ya haya. Kwa vile Mwenyezi Mungu ni Mwenye huruma kwa waja Wake, anawatahadharisha wasije wakaingia katika miamala ya kiuchumi iliyo batili, kwani uchumi mbaya ni sababu ya kuangamia kwa jamii na kumalizika. Kisha ametoa tahadhari nyingine kwa kusema: “Na atakayefanya hilo kwa uadui na dhulma, tutamtia motoni.” Yaani mwenye kukhalifu kanuni hizi na kutozijali kwa kula mali za watu pasi na haki au mtu kujiuwa mwenyewe hatopata adhabu kali tu hapa duniani, bali atakuwa na makaazi mabaya ya Moto wa Jahannam Siku ya Kiyama, na jambo hili ni jepesi mno kwa Mwenyezi Mungu: “Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.” 125
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 125
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
Aya ya pili inasema: “Mkijiepusha na (madhambi) makubwa mnayokatazwa, basi tutawafutia makosa yenu (madogo) na tutawatia mahali patukufu.” Aya hii inakusudia ya kwamba maasi yamegawanyika sehemu mbili: Maasi makubwa na maasi madogo, na hapa Mwenyezi Mungu ametoa sharti kwa Waumini, sharti hilo ni kwamba ikiwa hawatofanya madhambi makubwa, basi yale madogo wanayoyatenda yatafutwa na kusamehewa. Kwa mtazamo wa Qur’ani madhambi makubwa ni kila maasi yaliyokemewa zaidi, na alama yake kubwa ni kule kutajwa vitisho vikali vya Moto wa Jahannama kwa anaeyatenda maasi hayo, kama vile, kumshirikisha Mwenyezi Mungu, uchawi, kuuwa nafsi pasi na haki, ulevi, zinaa n.k. Huenda pakasemwa ya kwamba Aya hii inatia motisha juu ya kutenda madhambi madogo, yaani kama kwamba inasema: Hakuna ubaya kufanya madhambi madogo, kwa sharti ya kujiepusha na madhambi makubwa. Jawabu la mushikeli huu likobayana ndani ya Aya hii hii, kwani pale Mwenyezi Mungu aliposema: “…basi tutawafutia makosa yenu.” Anakusudia ya kwamba, mtu kujiepusha na madhambi makubwa hasa katika mazingira yanayomchochea kuyafanya, basi hali hii hujenga hali ya ucha Mungu katika nafsi ya mwanadamu, ucha Mungu ambao pia utamzuia kutenda madhambi madogo. Kwa hakika Aya hii inashabihiyana na Aya ya 114 ya Suratul Hud, isemayo: “Hakika mema huondoa maovu.” Madhambi Madogo Yanapokuwa Makubwa: Jambo la kuzingatia ni kwamba, madhambi madogo hubakia kuwa madogo ikiwa madhambi hayo hayakurudiwa kutendwa mara kwa mara, au kutotendwa kwa inda na kiburi, kwani madhambi madogo hugeuka na kuwa makubwa katika hali zifuatazo: Kwanza: Kurudiwa madhambi madogo mara kwa mara, kama alivyosema Imam Sadiq (a.s.):
ال صغيرة مع اإلصرار “Dhambi haitokuwa ndogo ikiwa itarudiwa mara kwa mara.”69
Pili: Ikiwa mtendaji maasi atayadharau na kuyadogesha maasi anayoyatenda, kama Imamu (a.s.) anavyosema:
ّ أش ّد الذنوب ما استهان به صاحبه
69
Al-Kuleyniy, Usulul Kafiy, Jz. 2, Uk. 288 126
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 126
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI “Madhambi makubwa zaidi ni yale ambayo yule anayeyatenda huyadharau”70
Tatu: Iwapo mtendaji wa dhambi ataitenda kwa inda, kiburi na kuchupa mipaka, kama ilivyokuja katika baadhi ya Aya za Qur’ani, kwa mfano Mwenyezi Mungu anasema:
ُّ َفأَمَّا َمن َط َغى َو َآث َر ْال َح َيا َة الد ْن َيا َفإِ َّن ْال َج ِحي َم ِه َي ْال َم ْأ َوى “Ama yule aliyeasi. Na akapenda zaidi (maisha) ya dunia. Basi kwa hakika Jahannamu ndiyo itakayokuwa makaazi yake.” (Qur’ani 79: 37- 39).
Nne: Ikiwa mtendaji maasi ni mtu mwenye hadhi fulani katika jamii na ambaye makosa yake hayaonekani kama makosa ya mtu mwingine. Jambo hili tunalishuhudia katika Qur’ani kuhusiana na wake wa Mtume (s.a.w.w.), Mwenyezi Mungu ansema:
ُ َيا ِن َساء النَّب ِّي َمن َي ْأ ِت ِم َ اح َش ٍة ُّم َبيِّ َن ٍة ي اع ْف لَ َها َ ُض ِ نك َّن ِب َف ِ َّلله ًان َذلِ َك َعلَى ا ِ َي ِسيرا َ ْال َع َ َ ْن َو َك ُ ي ف ع ض اب ذ ْ ِ ِ “Enyi wake wa Nabii! Atakayefanya uchafu dhahiri miongoni mwenu, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.”
Tano: Iwapo mtendaji wa maasi atafurahika na kujifaharisha kutokana na kuasi kwake, imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:
من أذنب ذنبا وهو ضاحك دخل النّار وهو باك “Mwenye kutenda dhambi na ilhali anacheka, basi ataingia Motoni huku analia.”71
Sita:Mtu kudhani ya kwamba kucheleweshewa adhabu hapa duniani ni dalili ya Mwenyezi Mungu kuridhika na maasi yake, au kujiona ya kwamba yeye ana ubora fulani kwa hivyo hawezi kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu kutokana na maasi yake, kama ilivyokuja katika Suratul Mujadala, ikisimulia kauli wanazozisema ndani ya nafsi zao watu waliobobea katika maasi na wenye kiburi: 70 71
Imamu (a.s.), Nahjul Balaghah, Jz. 4, Uk. 81 Al-Hurrul Amiliy, Wasailu Shia, Jz. 15, Uk. 305 127
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 127
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
ُ ون ِفي أَ ُنف ِسه ْم لَ ْو اَل يُ َع ِّذبُ َنا اللهَُّ ب َما َن ُق َ َُو َي ُقول ول ِ ِ “Na husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa yale tunayoyasema?”
Kutokana na kauli yao hiyo Mwenyezi Mungu amewarudi kwa kuwaambia:
ير ُ ص ْ َح ْسبُ ُه ْم َج َهنَّ ُم َي َ صلَ ْو َن َها َف ِب ْئ ِ س ْال َم “Jahannamu inawatosha, wataingia hapo, na ni pahala pabaya sana pa kufika.”
Aya ya mwisho inasema: “Wala msitamani aliyowafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko baadhi nyingine. Wanaume wana fungu katika walichokichuma na wanawake wana fungu katika walichokichuma. Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu”
SABABU YA KUTEREMKA Mfasiri mashuhuri wa Qur’ani; At-Tabrasiy amesema: Imesemwa kwamba Ummu Salama; mke wa Mtume (s.a.w.w.) alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Wanaume wanapigana vita na wanawake hawapigani, na pia sisi tunapata nusu ya mirathi, basi kwa hivyo wacha na sisi tutoke pamoja na wanaume tukapigane pamoja nao, ili na sisi tupate yale wanayoyapata wao, hapo iliteremka Aya hii kwa lengo la kujibiwa matakwa yake aliyoyataka. Na katika Tafsiril Manar imeelezwa ya kwamba: Aya hii iliteremka wakati baadhi ya Waislamu waliposema: Tunatarajia kufadhilishwa zaidi juu ya wanawake huko Akhera kutokana na matendo yetu mema, kama tulivyofadhiliwa zaidi katika mirathi, ili malipo yetu yawe ni maradufu zaidi ikilinganishwa na malipo ya wanawake. Na baadhi ya wanawake nao walisema: Tunataraji ya kwamba dhambi zetu zitakuwa ni nusu ikilinganishwa na dhambi za wanaume Siku ya Kiyama kama ilivyo mirathi hapa duniani.72
72
Shiraziy,Tafsirul Amthal, Jz. 3, Uk. 208 128
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 128
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO Tofauti ya mirathi kati ya mwanaume na mwanamke iliyowekwa na Mwenyezi Mungu imezua mijadala na maneno mengi, kama tulivyoona katika sababu ya kuteremka Aya hii, huenda sababu kubwa iliyowafanya kuuliza masuala hayo ni kutokana na kughafilika kwao ya kwamba mwanamume ndiye mwenye wajibu wa kusimamia matumizi ya familia yakiwemo matumizi ya mke, hiyo ndio sababu kubwa ya mwanamume kupewa mirathi zaidi kuliko mwanamke, kutokana na kanuni hii ndio Mwenyezi Mungu akasema: “Wala msitamani aliyowafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko baadhi nyingine.” Kwasababu katika tofauti ya mirathi iliyopo kati ya mwanaume na mwanamke kuna siri iliyojificha, tofauti hiyo ikiwa ni ya kimaumbile na kijinsia au tofauti nyingine za kimwili na kiroho ambazo ndizo zilizotengeneza jamii yenu, tofauti zote hizi zimesimama katika misingi ya uadilifu na kanuni za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya maslahi ya waja Wake, na lau kama maslahi yao yangepatikana katika utaratibu usio kuwa huu, basi angewafafanulia. Kwa hivyo yoyote yule anayetamani kubadilisha mfumo huu ni kwenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu, matakwa ambayo ndio kiini cha uadilifu. Baada ya Mwenyezi Mungu kuwakataza Waumini kutamani vya wengine, anawaeleza ya kwamba hizi tofauti za kimaumbile na za kimajukumu katika hii dunia, hazitokuwepo Siku ya Kiyama, hasa ikizingatiwa kwamba huko hakuna majukumu ya watu kuwaangalia watu wengine, na pia hakutokuwa na suala la kurithiana mali, kwa hivyo kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa juhudi yake aliyoifanya hapa duniani, bila ya kuangaliwa jinsia yake, anasema: “Wanaume wana fungu katika walichokichuma na wanawake wana fungu katika walichokichuma.” Mwisho anamalizia kwa kuwataka Waumini wamuombe Mola Wao fadhila zilizoko Kwake na kheri mbali mbali badala ya kukaa na kuona kwamba amedhulumiwa kwa kujiona yeye amekuwa katika tabaka fulani au ni jinsia fulani: “Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila Zake.” Baada ya mtu kumuomba Mwenyezi Mungu itakuwa si jambo sahihi kwake kukaa tu bila ya kuchukua hatua yoyote, bali analotakiwa ni kufanya yale mambo ambayo yatamsababishia kupata hizo fadhila za Mwenyezi Mungu. “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.” Yaani ni Mtambuzi wa yale yanayohitajika katika uundaji wa jamii, kama vile tofauti ya kijinsia, kipato majukumu na mengineyo. Na pia ni Mtambuzi wa siri za watu na yale waliyoyaficha vifuani mwao, anawajua wale wote wanaotamani mambo maovu na wanaotamani mambo ya kheri yenye kuijenga jamii. 129
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 129
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI NA MOJA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ٰ َّى َحت ى ٰ ار َّ ين آ َمنُوا اَل َت ْق َربُوا َ الص اَل َة َوأَ ْنتُ ْم ُس َك َ َُتعْلَ ُموا َما َت ُقول يل َحتَّىٰ َت ْغ َت ِسلُوا ٍ ون َو اَل ُجنُبًا إِ اَّل َع ِاب ِري َس ِب َ َوإِ ْن ُك ْنتُ ْم َم ْر ضىٰ أَ ْو َعلَىٰ َس َف ٍر أَ ْو َجا َء أَ َح ٌد ِم ْن ُك ْم ِم َن ْال َغا ِئ ِط ص ِعي ًدا َطيِّبًا َ أَ ْو اَل َم ْستُ ُم النِّ َسا َء َفلَ ْم َت ِج ُدوا َما ًء َف َت َي َّم ُموا ُ وه ُك ْم َوأَ ْي ِد َ يك ْم إِ َّن اللهََّ َك ورا ً ان َع ُف ًّوا َغ ُف ِ َفا ْم َس ُحوا ِب ُو ُج “Enyi mlioamini! Msikaribie Swala na hali mmelewa mpaka myajue mnayoyasema; wala mkiwa na janaba - isipokuwa wapita njia - mpaka muoge. Na muwapo wagonjwa au mko safarini au akawa mmoja wenu ametoka chooni au mkagusana na wanawake, kisha msipate maji, basi tayamamuni na mchanga ulio twahara; mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe Mwingi wa maghufira.” (Qur’ani 4:43)
MAELEZO:
Baadhi ya Hukumu za Kifiqhi: Ndani ya Aya hii kuna hukumu mbali mbali za kifiqhi, hukumu hizo ni kama zifuatazo: Kwanza: Swala haitosihi ikiwa mtu ameswali na ilhali amelewa, hekima ya hukumu hii ni kwamba, Swala ni ibada ambayo mwanadamu huzungumza na Mola Wake na kumuomba maombi mbalimbali, kwa hivyo haya hayatimii ikiwa mwenye kuswali hayuko katika mazingatio na akili timamu, kwa hivyo Mwenyezi Mungu amewataka Waumini wajiepushe na aina yoyote ya ulevi, ili wawe na mazingatio kamili na kujua wanachokisema na kukifanya wakati wanapo muelekea Mola Wao kwa ibada, amesema: “Enyi mlioamini! Msikaribie Swala na hali mmelewa mpaka myajue mnayoyasema.” Huwenda pakajitokeza suala kama hili: Je! Kwa mujibu wa Aya hii si inaruhusika kulewa ikiwa athari yake haitabakia mpaka wakati wa Swala? Jawabu la suala hili ni kama ifuatavyo: Uislamu ulitumia utaratibu wa hatua kwa hatua katika kuharamisha baadhi ya mila na desturi mbaya zilizokuwa zikifuatwa 130
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 130
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
katika zama za kijahilia, kama tulivyoona katika kuharamishwa kwa riba. Ama kuhusiana na kuharamishwa kwa ulevi ni kwamba ulipita katika hatua zifuatazo: Kwanza:Mwenyezi Mungu alitaja kinywaji kingine kisichokuwa ulevi ambacho nacho pia kinakamuliwa katika matunda ambacho ni riziki njema, kama ilivyokuja katika Aya ya 67 ya Suratun Nahal:
َ ات النَّ ِخيل َو ُ األ ْع َناب َتتَّ ِخ ًون ِم ْن ُه َس َكراً َور ْزقا َ ذ ِ َو ِمن َث َم َر ِ ِ ِ َ َُح َسناً إِ َّن ِفي َذلِ َك آل َي ًة لَِّق ْو ٍم َي ْع ِقل ون “Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa wanaotumia akili.”
Pili: Kukatazwa kuswali ikiwa mtu amelewa na athari zake bado zikawa zimebakia hadi wakati wa Swala, kama ilivyo katika Aya hii tunayoitafsiri. Tatu:Mwenyezi Mungu alilinganisha faida na hasara zipatikanazo katika ulevi, natija ikawa hasara ni kubwa zaidi kuliko faida, kama ilivyokuja katika Aya ya 219 ya Suratul Baqara:
ْ َي ْسأَلُو َن َك َعن ْال َخ ْمر َو ْ ْسر ُق ْل ِفيه َما إ َ َّ َ اس لن ل ع ف ا ن م و ير ب ك م ث ي م ال ُ ٌ ٌ َ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ …َوإِ ْث ُم ُه َما أَ ْك َب ُر ِمن نَّ ْف ِع ِه َما “Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake…”
Na hatua ya mwisho kabisa, Mwenyezi Mungu aliharamisha ulevi kwa uwazi kabisa, kama alivyosema katika Aya ya 90 ya Suratul Maidah:
َ اب َو َ ْس ُر َو ْ ُين آ َمن َ األ ْز َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ُ نص ال ُم َ األ ِ وا إِنَّ َما ْال َخ ْم ُر َو ْال َمي َ َّ َ اج َت ِنبُو ُه لَ َعلَّ ُك ْم تُ ْفلِ ُح ون ْ ان َف ٌ ِر ْج ِ س ِّم ْن َع َم ِل الشيْط “Enyi mlioamini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani, Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.”
131
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 131
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa kweli kulikuwa hakuna njia nyingine ya kuzuia jambo ovu ambalo lilikuwa limeota mizizi katika jamii, isipokuwa kwa njia hii ya kulikataza hatua kwa hatua. Kwa hivyo Aya ilioko mbele yetu haitoi ruhusa yoyote kwa mtu kuweza kunywa ulevi, bali inazungumzia hali ya kutokuswali wakati mtu anapokuwa na ulevi kichwani mwake, na iliacha kuzungumzia hukumu ya kunywa ulevi pahala pengine mpaka itakapofika wakati wa kuharamishwa moja kwa moja na milele. Pia kutokana na kiwango walichokuwa wakikinywa watu wengi kiliwafanya wabakie katika hali ya ulevi kwa muda mrefu, na ikilinganishwa na vipindi vitano vya Swala ilikuwa si jambo rahisi kwa mlevi kudiriki wakati wa Swala akiwa na akili timamu, hii peke yake ilikuwa inaashiria kuharamamishwa ulevi wakati wote. Riwaya zilizopokelewa katika vitabu vya Kishia na Kisunni zimekwenda mbali zaidi katika kuitafsiri Aya hii, zinaelezea ya kwamba ulevi uliokatazwa kuswali nao si ulevi wa pombe au vileo vingine, bali pia ulevi wa usingizi, yaani Waumini wanakatazwa wasiingie katika Swala mpaka pale watakapoufukuza usingizi kutoka machoni mwao, ili wakitambue na kukizingatia kile wanachokisema. Huenda tafsiri hii imetokana na ibara isemayo: “Mpaka myajue mnayoyasema.” Maneno haya yanakataza kuswali katika hali yoyote ile ambayo mtu atakuwa hana mazingatio na kufahamu anachokisema katika Swala yake, ikiwa ni kwa sababu ya ulevi, usingizi au uvivu, kama ilivyopokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s.) pale aliposema:
الصالة متكاسال وال متناعسا وال متثاقال فإنّها من ّ ال تقم إلى ّ عز ّ خالل النّفاق وقد نهى اهلل وجل المؤمنين أن يقوموا إلى .الصالة وهم سكارى ّ “Usisimame katika Swala hali ya kuwa una uvivu, wala ukiwa na usingizi, wala ukijisikia mzito, kwani mambo haya ni miongoni mwa mambo ya kinafiki, na kwa hakika Mwenyezi Mungu amewakataza Waumini kuswali hali ya kuwa wamelewa”73
Pili: Kubatilika kwa Swala kwa mtu mwenye janaba, kama Aya inavyoashiria: “wala mkiwa na janaba” Lakini iwapo mtu atakuwa katika safari na akawa hana maji itamfalia kwake kutayammamu kwa ajili ya josho la janaba, na ikiwa kuna uwezekano wa kupata maji, basi atalazimika kukoga ili aruhusike kufanya ibada ya Swala: “ispokuwa wapita njia - mpaka muoge.” 73
Al-Hurrul Amiliy, Wasailu Shia, Jz. 5, Uk. 464 132
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 132
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
Pia kwa mujibu wa Aya pamepokelewa Riwaya zinazoeleza ya kwamba hairuhusiwi kwa mtu mwenye janaba kukaa msikitini, isipokuwa kwa kupita tu; kwa kuingia mlango mmoja na kutokea mlango mwingine. Hukumu hii inatokana na baadhi ya Maswahaba ambao walijenga nyumba zao pembezoni mwa msikiti wa Mtume (s.a.w.w.), kiasi kwamba milango yao ilikuwa imeambatana na msikiti kiasi cha kumfanya mpitaji apite msikitini, kwa hivyo waliruhusiwa kupita ndani ya msikiti hata kama walikuwa na janaba. Tatu: Hukumu ya kutayammamu kwa wenye nyudhuru: “Na muwapo wagonjwa au mko safarini,” katika ibara hii kwa hakika kumetajwa sababu zote zinazompelekea mtu kutayammamu, sababu ya kwanza ni pale mtu atakapokuwa atadhurika pindi akitumia maji, na sababu ya pili ni kukosekana kwa maji. Aya inaendelea kutaja nyudhuru nyingine kwa kusema: “au akawa mmoja wenu ametoka chooni au mkagusana na wanawake, kisha msipate maji, basi tayamamuni na mchanga ulio twahara.” Pia Aya imeeleza namna ya kutayammamu kwa kusema: “mpake nyuso zenu na mikono yenu.” Kwa vile Aya haikuweka mipaka ya mikono wakati wa kutayammamu kama ilivyoweka katika udhu, kwa hivyo wajibu ni kupaka sehemu ya kiwiko tu (kuanzia kwenye kifundo cha kiganja hadi ncha za vidole). Mwenyezi Mungu anahitimisha Aya hii kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe Mwingi wa maghufira.” Ni kwamba hukumu hizi alizoziweka kwa waja Wake walioamini ni kwa ajili ya kuwarahisishia kwani Yeye ni Mwingi wa kusamehe.
133
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 133
12/8/2014 2:43:39 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI NA MBILI
َ ْول َوأُولِي أ َ الر ُس َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ال ْم ِر َّ ين آ َمنُوا أَ ِطيعُوا اللهََّ َوأَ ِطيعُوا َ ِم ْن ُك ْم َفإِ ْن َت َن ول إِ ْن ُك ْنتُ ْم َّ از ْعتُ ْم ِفي َش ْي ٍء َف ُر ُّدو ُه إِلَى اللهَِّ َو ِ الر ُس َ ُتُ ْؤ ِمن ْر َوأَ ْح َس ُن َت ْأ ِويل ٌ ون ِباللهَِّ َو ْال َي ْو ِم الآْ ِخ ِر َذٰلِ َك َخي
“Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi. Na kama mkipingana katika jambo, basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, mkiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hilo ni bora zaidi na mwisho mzuri.” (Qur’ani 4:59)
Aya hii ni miongoni mwa Aya zilizo na umuhimu wa kipekee katika Qur’ani, kwa vile kuelezea kwake masuala ya uongozi na namna ya kupatikana kiongozi atakaye waongoza Waislamu katika masuala mbali mbali ya kidini na ya kijamii. Kwanza inawaamrisha Waumini kumtii Mwenyezi Mungu. Uislamu unatufunza ya kwamba ni wajibu kwa kila Muumini kuhakikisha ya kwamba utiifu wake wote unamalizikia katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kila uongozi ni wajibu uwe katika misingi aliyoiweka Mwenyezi Mungu, kwa vile Yeye ndiye Mmiliki Pekee wa ulimwengu na vilivyomo ndani yake, kwa hivyo ni wajibu kwa Muumini kutekeleza hukumu zote zitokazo Kwake: “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu.” Hatua ya pili ni kumfuata na kumtii Mtume Wake (s.a.w.w.), Mtume ambaye ni Maasumu (asiye tenda makosa) na aliyetakaswa kutokana na kila aina ya uchafu, Mtume ambaye hatamki kutokana na matakwa yake, bali matamshi yake ni Wahyi utokao kwa Mola Wake, Mtume ambaye ni mwakilishi wa Mwenyezi Mungu na ni kiunganishi kati ya Mwenyezi Mungu na waja Wake, wadhifa ambao amepewa na Mola Wake, kwa hivyo chanzo cha kutiiwa kwake ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hatua ya tatu ni kwamba Mwenyezi Mungu anaamrisha watiiwe watu waliopewa madaraka ya kusimamia masuala mbali mbali yanayohusiana na jamii ya Kiislamu katika mambo ya dini yao pamoja na dunia yao. Ni Kina Nani Hao Ululul Amri: Kuna kauli mbali mbali za wafasiri wa Qur’ani zinazoelezea muradi wa Ulul-Amri katika Aya hii, kwa mukhtasari kauli hizo ni kama zifuatazo: 134
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 134
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwanza: Baadhi ya wafasiri wa madhehebu ya Kisunni wanasema: Makusudio ya Ulul-Amri ni watawala wanaotawala kila pahala na katika kila zama, watu wenye rai hii hawakuweka sifa yoyote wanayopaswa kuwa nayo hao watawala, kwa hivyo nadharia yao hii inamaanisha kumtii mtu yeyote aliye na madaraka hata kama ni mwasi. Pili: Wafasiri wengine wa madhehebu ya Kisunni, kama vile mfasiri wa Tafsiril Manar na mfasiri wa Fii dhilalil Qur’ani na wengineo, wanasema: “Makusudio ya Ulul-Amri ni kila kiongozi aliye na mamlaka katika nyanja yoyote ile iliyo na manufaa kwa jamii, kama vile maulamaa, viongozi wa nchi na kila mwenye mamlaka, kwa sharti twaa yao isiende kinyume na sheria za Kiislamu. Tatu: Wengine wanasema ya kwamba makusudio ya Ulul-Amri ni maulamaa na watu wenye fikra nzuri, kwa sharti wawe waadilifu na wenye maarifa kamili ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake (s.a.w.w.). Nne:Pia baadhi ya maulamaa wa Kisunni wanasema ya kwamba makusudio yake ni makhalifa wanne walioshika mamlaka baada ya Mtume (s.a.w.w.). Tano: Wengine wanasema ya kwamba Ulul-Amri makusudio yake ni Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Sita: Kuna kauli nyingine isemayo ya kwamba, makusudio ya Ulul-Amri ni viongozi na makamanda wa kijeshi kwenye jeshi la Kiislamu. Saba: Wafasiri wote wa madhehebu ya Kishia wamewafikiana kwa kauli moja ya kwamba, makusudio ya Ulul-Amri ni Maimamu kumi na mbili wanaotokana na kizazi cha Bwana Mtume (s.a.w.w.), Maimamu ambao wamepewa jukumu la uongozi katika umma wa Kiislamu katika nyanja zote; za kiroho na kimaada. Na wala Aya hii haiwahusishi watu wengine wasiokuwa wao, ila yule aliyeteuliwa na wao kushika nafasi fulani, hapo itapasa na yeye kutiiwa pindi atakapotimiza masharti yanayohitajika. Kutiiwa kwa mtu aliyeteuliwa na Maimamu (a.s.) haimfanyi na yeye kuwa ni katika Ulul-Amri, bali kwa sababu ya kule kuwa ni mwakilishi na naibu wa hao Maimamu (a.s.). Utafiti Katika Nadharia Zilizotajwa: Bila ya shaka tafsiri ya kwanza haikubaliki kwa mujibu wa mafunzo ya Uislamu, kwani haiwezekani kumtii kila mtawala hata kama yeye mwenyewe hamtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.). Kutokana na ubatili wa nadharia hii wanachuoni wakubwa wa Kisunni na kishia wanapinga vikali nadharia hii. Tafsiri ya pili na ya tatu pia nazo hazinasibiani na Aya, kwani Aya haikuweka masharti ya kutosha juu ya kutiiwa hao wenye mamlaka na madaraka, kwani kuna 135
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 135
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
uwezekano mkubwa wa kuingia kwenye makosa. Ama tafsiri ya nne, inayosema UlulAmri ni makhalifa wanne tu, hii inamaanisha kutokuwepo viongozi wanaokubalika kwa Mwenyezi Mungu kati ya Waislamu baada ya wao kuondoka duniani. Zaidi ya hayo ni kwamba hakuna dalili yoyote inayothibitisha nadharia yao hiyo. Tafsiri ya tano, ambayo inamaanisha kwamba Ulul-Amri ni Maswahaba, na ile ya sita isemayo ya kwamba ni makamanda wa kijeshi katika jeshi la Kiislamu, jawabu la tafsiri hizi ni kama la tafsiri ya nne, nalo ni kwamba hakuna dalili yoyote inayothibitisha hivyo. Ama tafsiri isiyo na shaka na inayokubalika kwa mujibu wa Aya ni tafsiri ya saba, inayosema kwamba Ulul-Amri wanaostahiki kutiiwa ni Maimamu Watoharifu wanaotokana na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) Ukweli na usahihi wa tafsiri hii, ni kule Mwenyezi Mungu kuwataka Waumini wawatii watu walio na madaraka miongoni mwao, pasi na kuweka sharti lolote, kwani tohara na daraja ya umaasumu walionao Maimamu hawa inatosha kuwa ni uthibitisho tosha kwamba hawatowatoa watu kwenye haki na kuwapeleka katika upotofu kwa kukusudia au kwa kusahau, kwa hivyo twaa yao ni kama twaa ya Mtume (s.a.w.w.) hasa ikizingatiwa ya kwamba Aya imeunganisha twaa yao pamoja na twaa ya Mtume (s.a.w.w.). Nadharia inayosema ya kwamba Ulul-Amri ni lazima awe maasumu kama walivyokubaliana wanachuoni wa Kishia, pia nadharia hii inakubaliwa na mwanachuoni wa Kisunni; Fakhri Razi, isipokuwa amekuja na natija isiyo sahihi baada ya utangulizi mrefu, amesema ya kwamba: Ulul-Amri ni Ijmaa ya umma (makubaliano ya umma wa Kiislamu). Licha ya mfasiri huyu wa Kisunni kuja na mzunguko mrefu kwa lengo la kutaka kuthibitisha hilo alilolithibitisha, anakiri kwa uwazi ya kwamba Ulul-Amri waliotajwa katika Aya hii ni lazima wawe ni maasumu (wasiokosea). Ushahidi wa Hadithi: Miongoni mwa vitabu vikubwa vya Kiislamu vimebainisha wazi ya kwamba UlulAmri ni Maimam wa Kiahlul Bayt (a.s.), miongoni mwake ni kama vifutavyo: 1.
Ameandika mfasiri maarufu wa Kisunni anayejulikana kwa jina la Abu Hayyan al-Andalusiy al-Maghribiy, aliyefariki mwaka wa 756 A. H. ameandika katika tafsiri yake iitwayo al-Bahril Muhitwi,ni kwamba Aya hii imeteremka ikielezea haki ya Ali pamoja na Ahlul Bayt wake.
2.
Mwanachuoni mwingine wa Kisunni; Abu Bakar ibn Shiraziy katika kitabu chake kiitwacho Risalatul I’tiqaad, anasema: “Imepokewa kutoka kwa Ibn 136
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 136
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
Abbas ya kwamba Aya hii imeteremka kwa ajili ya kuelezea haki ya Ali (a.s.) pale Mtume (s.a.w.w.) alipomuwacha Madina wakati wa vita vya Tabuti, Ali (a.s.) alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Unaniacha pamoja na wanawake na watoto? Mtume (s.a.w.w.) alimwambia: Je, huridhiki kuwa na daraja kwangu kama ile aliyokuwa nayo Harun kwa Musa, wakati Musa aliposema kumwambia Harun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: “Na wenye mamlaka katika nyinyi.” 3. Mwanachuoni mwingine wa Kisunni na mfuasi wa madhehebu ya Kihanafi; Sheikh Sulayman al-Hanafiy al-Qunduziy, katika kitabu chake kiitwacho Yanabiiul Mawaddah amenukuu maneno yafuatayo: “Kutoka kwa Sulayman bin Qaysi, alisema nilimsikia Ali (a.s.) akisema baada ya kuendewa na mtu na kumuuliza: Nijulishe kitu kidogo sana ambacho anakuwa nacho mja aliye Muumini, na kitu kidogo sana anachokuwa nacho kafiri, na kitu kidogo sana anachokuwa nacho mja aliyepotea. Imam Ali (a.s.) alisema: Umeshauliza, sasa kaa tayari kwa kulifahamu jawabu. Ama kitu kidogo sana anachokuwa nacho mja aliyepotea ni kutomjua mja wa Mwenyezi Mungu aliye hojja kwa watu na shahidi wake kwao ambaye Mwenyezi Mungu amewaamrisha waja Wake wamtii na kuwataka wawe chini ya uongozi wake. Nilisema: Ewe kiongozi wa Waumini nielezee, ni nani hao? Alisema: Hao ni wale ambao Mwenyezi Mungu amewaambatanisha pamoja na nafsi Yake pamoja na Mtume Wake, pale aliposema: “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi.” Nilimwambia: Mwenyezi Mungu anifanye fidia kwako, nifafanulie zaidi. Alisema: Ni wale ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu amewaeleza katika matukio mbali mbali, na hata katika siku ambayo Mwenyezi Mungu alimfisha, alisema: Hakika mimi ninawaachia mambo mawili iwapo mtashikamana nayo hamtopotea baada yangu milele: Mambo hayo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, cha watu wa nyumbani kwangu.” Ama katika vitabu vya Kishia, kama vile Usulul Kaafi, Tafsirul Iyaasha, vitabu vya Sheikh Swaduq na vinginevyo, vinaweka bayana ya kwamba makusudio ya UlulAmri ni Maimamu Maasumu wanaotokana na kizazi cha Bwana Mtume s.a.w.w.), na hata baadhi ya vitabu hivyo vimetaja majina yao, moja baada ya jingine.
137
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 137
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI NA TATU
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ات أَ ِو ا ْن ِف ُروا ٍ ين آ َمنُوا ُخ ُذوا ِح ْذ َر ُك ْم َفا ْن ِف ُروا ثُ َب َ صي َب ٌة َق ال َق ْد َ ََج ِميعًا َوإِ َّن ِم ْن ُك ْم لَ َم ْن لَيُ َب ِّط َئ َّن َفإِ ْن أ ِ صا َب ْت ُك ْم ُم ْ صا َب ُك ْم َف ض ٌل ِم َن َ َأَ ْن َع َم اللهَُّ َعلَ َّي إِ ْذ لَ ْم أَ ُك ْن َم َع ُه ْم َش ِهي ًدا َولَِئ ْن أ اللهَِّ لََي ُقولَ َّن َكأَ ْن لَ ْم َت ُك ْن َب ْي َن ُك ْم َو َب ْي َن ُه َم َو َّد ٌة َيا لَ ْي َت ِني ُك ْن ُت َم َع ُه ْم َ َفأَ ُف وز َف ْو ًزا َع ِظي ًما Enyi mlioamini! Chukueni tahadhari yenu! Tokeni vikosi vikosi au tokeni nyote pamoja. Na hakika katika nyinyi kuna ambaye hukaa nyuma; na ukiwasibu msiba husema: Mwenyezi Mungu amenineemesha kwa kutokuwa nao. Na iwafikiapo fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu, husema - kama kwamba, hapakuwa na mapenzi baina yenu na yeye - laiti ningelikuwa pamoja nao nikafanikiwa mafanikio makubwa. (Qur’ani 4:71-73).
Aya ya kwanza kati ya hizi, Mwenyezi Mungu anawataka Waumini wote kwa ujumla kuwa macho dhidi ya njama za maadui zao. Pia Mwenyezi Mungu anatoa mafunzo mawili kupitia Aya hii, mafunzo ambayo yana lengo la kuibakisha jamii ya Kiislamu katika hali ya amani na usalama dhidi ya vitisho vinavyotishia uhai wao. Mwanzoni kabisa, Aya inawataka Waumini kuwa macho na waangalifu dhidi ya watu wasiowatakia mema, na inawataka wasighafilike juu ya jambo hili: “Enyi mlioamini! Chukueni tahadhari yenu!” Ama funzo la pili ni Waumini kufunzwa mbinu za kukabiliana na adui, kwa hivyo ikiwa hali itaruhusu wanatakiwa watoke baadhi ya wapiganaji makundi kwa makundi, na kama hali hiyo haitoleta tija, basi itawapasa watoke wote kwa pamoja katika kumvamia adui. Kwa hivyo ni jukumu la kamanda wa jeshi la Kiislamu kuangalia ni njia gani itafaa kati ya hizi mbili katika kukabiliana na adui. Aya hii Tukufu inatoa mafunzo kwa Waislamu wote wa zama zote popote walipo, kwamba ni wajibu wao kujiweka tayari wakati wowote ili kuweza kukabiliana na adui wakati atakapoanza uchokozi wake dhidi yao, ili waweze kulinda hadhi yao na heshima yao pamoja na
138
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 138
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
usalama wa mali zao na nafsi zao, haya yatafanikiwa ikiwa kutakuwa na maandalizi ya kiroho, kimaada (silaha) na ujuzi wa kupambana. Pia Waumini wanatakiwa wachukue tahadhari kwa kufuata mafunzo ya Dini yao na kujiepusha na tamaduni za kigeni zisizo kubalika katika Uislamu, na vile vile kuwa wakakamavu katika kufanya kazi kwa bidii ili kunyanyua uchumi ambao ni sababu ya kuweza kumiliki silaha nyingi na zilizo bora. Kwa hakika lau kama Waislamu watashikamana na mafunzo haya na kuyatekeleza vilivyo katika maisha yao, basi wasingekuwa katika hali hii waliyonayo leo; hali ya kushindwa, hali ya unyonge na hali iliyojaa matukio yenye maumivu makali. Baada ya Mwenyezi Mungu kutoa amri ya kupigana jihadi na kuchukua tahadhari dhidi ya maadui, Aya zinazofuatia zinaelezea misimamo ya wanafiki wakati panapotokea vita na kubainisha usaliti wao. Kwa hakika wao huwa wanajizuia kushiriki katika vita vya Jihadi: “Na hakika katika nyinyi kuna ambaye hukaa nyuma;” Na wakati Mujahidina wanaporudi kutoka katika uwanja wa vita au wanapopata habari za mapambano yao, na kama ikiwa Waislamu wameshindwa au kujeruhiwa katika vita, wanafiki huzungumza kwa mbwembwe na furaha ya kwamba Mwenyezi Mungu amewanemeesha neema iliyo kubwa sana kwa kule kutoshiriki kwao katika vita pamoja na Waumini: “Na ukiwasibu msiba husema: Mwenyezi Mungu amenineemesha kwa kutokuwa nao.” Ama ikiwafikia habari ya ushindi kwa Waumini na kujizolea ngawira, misimamo ya wanafiki hawa hubadilika kwa kuonesha masikitiko na majuto makubwa kwa kule kutoshiriki kwao katika vita, na huzungumza kama kwamba wao wana mafungamano ya hali ya juu pamoja na Waislamu: “Na iwafikiapo fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu, husema - kama kwamba hapakuwa na mapenzi baina yenu na yeye - laiti ningelikuwa pamoja nao nikafanikiwa mafanikio makubwa.” Aya inaonesha nadharia ya ushindi waliyonayo wanafiki, wao hawaoni mtu kupata shahada katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni ushindi na nusra, bali wanaona ni balaa na msiba, ushindi na mafanikio kwao ni kujikusanyia mirundiko ya mali na ngawira. Kwa masikitiko makubwa ni kwamba watu hawa wenye nyuso mbili wanapatikana katika kila jamii, ni watu wanaobadilika haraka sana pindi Waumini wanapopata mafanikio au hasara. Watu hawa hawako tayari kuwasaidia Waumini pale wanapofikwa na maafa, bali wanalojali ni kupata faida nono na ngawira nyingi pindi Waislamu wanapowashinda maadui katika vita vya jihadi.
139
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 139
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI NA NNE
ََّيا أَُّي َها ال َ ُ ُ َ َ يل اللهَِّ َف َت َبيَّنُوا َو اَل َت ُقولُوا ب س ي ف م ْت ب ر ض ا ذ إ وا ن م آ ين ذ ْ َ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ْ ُ لِ َم ْن أَْل َقىٰ إلَي ُّ ض ال َح َيا ِة َ ون َع َر َ الس اَل َم لَ ْس َت ُم ْؤ ِم ًنا َت ْب َت ُغ الد ْن َيا َّ ْك ُم ِ ُ َُّلله ُ ُ َ َ ير ٌة َك َذٰلِك ك ْنتُ ْم ِم ْن َقبْل َف َم َّن ا َعليْك ْم َف َت َبيَّنُوا َ َف ِع ْن َد اللهَِّ َم َغا ِن ُم َك ِث َ ُان ِب َما َت ْع َمل َ إِ َّن اللهََّ َك يرا ً ون َخ ِب “Enyi mlioamini! Mtakaposafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakikisheni wala msimwambie mwenye kuwapa Salaam: wewe si muumini. Mnataka mafao ya duniani na kwa Mwenyezi Mungu kuna ngawira nyingi! Hivi ndivyo mlivyokuwa nyinyi hapo mbeleni, na Mwenyezi Mungu akawaneemesha. Basi hakikisheni; hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa mnayoyatenda.” (Qur’ani 4:94)
SABABU YA KUTEREMKA Riwaya mbali mbali zimeelezea sababu nyingi za kuteremka Aya hii, lakini sababu hizo zinashabihiyana sana. Ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anarudi kutoka katika vita vya Khaybar, alimpeleka Usama ibn Zayd pamoja na kundi la Waislamu kwenda kwa Mayahudi waliokuwa wakiishi katika kijiji cha Fadak kwa lengo la kuwalingania katika Dini ya Kiislamu au kukubali kuishi chini ya dola ya Kiislamu na wao kulipa kodi, mmoja kati ya Mayahudi aliyekuwa akiitwa Murdas alipata habari juu ya kuja kwa jeshi la Kiislamu, na yeye alikuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa wakimpwekesha Mwenyezi Mungu na kumuamini Mtume (s.a.w.w.) pamoja na ujumbe aliokuja nao, alipopata habari ya kuendewa na jeshi la Kiislamu alitoka huku akiwa amechukua mali zake pamoja na watoto wake na kuelekea kwenye majabali ili akawapokee Waislamu, Usama alipopita karibu na yule Myahudi aliwatolea salamu Waislamu,Usama alidhani ya kwamba mtu huyo alikuwa akidhihirisha Uislamu kwa kukhofia nafsi yake na kuilinda mali yake isije ikachukuliwa ngawira, lakini Usama alimuuwa mtu huyo na kisha akaihodhi mali yake, na habari ilipomfikia Mtume (s.a.w.w.) alisikitika sana na akatoa kauli ya kwamba huenda Usama alikuwa hajui yale yaliokuwa katika nafsi ya mtu huyo, kwani huenda akawa ni mwenye kusilimu kikweli kikweli, baada ya hapo ndipo 140
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 140
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii, ikiwataka Waislamu wasikatae imani ya mtu kwa lengo la kutaka kujikusanyia ngawira.74
MAELEZO Katika Aya hii Waislamu wanatakiwa wachukue tahadhari ya hali ya juu katika kuzilinda roho za watu wasio na makosa, kwa kujiepusha na tuhuma zinazoelekezwa kwa watu hao: “Enyi mlioamini! Mtakaposafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakikisheni wala msimwambie mwenye kuwapa Salaam: wewe si muumini.” Aya hii inawata Waumini wawakubali na kuwakaribisha kwa kifua kipana wale wote wanaodhihirisha Uislamu, na wasiwe na dhana mbaya juu ya imani yao, pia inawakataza isiwe tamaa ya kutaka kujikusanyia mali ndio sababu ya kuwatuhumu watu katika imani yao, au kuwauwa kwa hoja eti wao ni maadui wa Uislamu, Aya inasema: “Mnataka mafao ya duniani.” Aya inawaeleza ya kwamba hiyo mali wanayoitarajia kuipata kwa kuwauwa watu baada ya kuwatuhumu si mali yenye kudumu, kwani wao wenyewe hawataishi milele na hata hii dunia ambayo wao wanaishi ndani yake nayo pia haidumu, jambo wanalotakiwa walijue ni kwamba neema kubwa na ya kudumu inapatikana kwa Mwenyezi Mungu kwa sharti mtu kufuata mafunzo yote ya Uislamu: “Na kwa Mwenyezi Mungu kuna ngawira nyingi!” Pia Aya inaelezea vita vilivyokuwa vikitokea wakati wa zama za kijahilia, vita hivyo vilikuwa vikipiganwa kwa lengo la kupora mali za watu wengine: “Hivi ndivyo mlivyokuwa nyinyi hapo mbeleni,” Baada ya hapo Aya inataja neema za Mwenyezi Mungu na ukarimu wake kuwa ndivyo vitu vilivyowatoa wao kutokana na ujinga huo wa kupigana kwa ajili ya kupora mali za wengine, kwa hivyo ni wajibu wao waishukuru neema hii kwa kufanya uchunguzi kabla ya kuchukua hatua yoyote dhidi ya maisha ya wengine: “Na Mwenyezi Mungu akawaneemesha. Basi hakikisheni; hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa mnayoyatenda.” Vita Vya Jihadi Havina Lengo la Kujitajirisha: Aya hii inabainisha wazi ya kwamba vita vya jihadi havina lengo la kujikusanyia ngawira na utajiri, kwa hivyo ni wajibu wa kila Mwislamu anayeingia katika uwanja wa mapambano kuondosha dhana hii katika fikra zake, bali inampasa tangu katika 74
Shiraziy, Tafsirul Amthal, J.3 Uk.397 141
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 141
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
hatua ya mwanzo kudhihirisha imani ya Dini yake na huku akiwa na lengo la kutaka amani na suluhu iwapo upande wa pili utakuwa tayari kufanya hivyo kwa lengo la kuepusha umwagaji damu, hata kama Waislamu watajiona kuwa wana uwezo wa kumshinda adui, hayo ni kwa sababu lengo la vita katika Uislamu si kujitanua kimipaka na kuteka mali za wengine, bali lengo lake kuu ni kuwakomboa watu kutokana na minyororo ya ibada ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Pia Aya inawakumbusha Waislamu namna walivyokuwa wakifuata sera za kijahilia, kwani walikuwa wanabeba fikra za kujikusanyia mali kwa njia yoyote ile ikiwemo kuanzisha vita na kusababisha umwagikaji wa damu bila ya sababu yoyote ile ya msingi, lakini kutokana na baraka pamoja na utukufu wa Uislamu wameepukana na balaa la kumwaga damu zao wenyewe kwa wenyewe.
142
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 142
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI NA TANO
َ ين آ َمنُوا ُكونُوا َق َّوا ِم َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ٰ َين ِب ْال ِق ْس ِط ُش َه َدا َء للِهَِّ َولَ ْو َعل ى َ ْأَ ْن ُف ِس ُك ْم أَو ْال َوالِ َديْن َو أ َ ال ْق َر ِب ٰيرا َفاللهَُّ أَ ْولَى ً ين إِ ْن َي ُك ْن َغ ِنيًّا أَ ْو َف ِق ِ ِ َ َ ْ ُ ْ ُ َّ ََ ا ُ ْر ضوا َفإِ َّن ِ ِب ِه َما فل َتت ِبعُوا ال َه َوىٰ أ ْن َت ْع ِدلوا َوإِ ْن َتل ُووا أ ْو تع َ ُان ِب َما َت ْع َمل َ اللهََّ َك يرا ً ون َخ ِب “Enyi mlioamini! Kuweni wenye kuusimamisha uadilifu, mtoao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu au wazazi wawili na akraba. Akiwa ni tajiri au fukara basi Mwenyezi Mungu anawastahiki zaidi. Basi msifuate hawaa ili mfanye uadilifu. Na mkiupotoa au mkaachana nao basi Mwenyezi Mungu ana habari ya myatendayo.” (Qur’ani 4:135).
Uadilifu wa Kijamii: Aya inaanza kueleza jambo muhimu katika masuala ya kijamii, jambo hilo kutekeleza uadilifu kwa kila mtu bila ya upendeleo, kwa hivyo imewataka kujipamba na sifa hii iliyo njema: “Enyi mlioamini! Kuweni wenye kuusimamisha uadilifu.” Kwa mujibu wa misingi ya lugha ya Kiarabu neno ‘Qawwamina’ linamaanisha kufanya kitu kwa wingi, kwa hivyo Aya inawataka Waumini wafanye uadilifu katika kila hali na katika kila zama na pahala, mpaka ifikie kiwango cha kuwa uadilifu ni sehemu ya utamduni wao na tabia yao ya kila siku. Katika kutilia mkazo suala la uadilifu Aya inataja ushahidi, ikimaanisha ni juu ya kila Muumini kuwa mwadilifu wakati anapotoa ushahidi, na afanye hivyo kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, na wala asijali iwapo nafsi yake itadhurika iwapo atatoa ushahidi wa haki na wa ukweli au watadhurika wazazi wake au jamaa zake wengine wa karibu: “Mtoao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu au wazazi wawili na akraba.” Aya hii imeteremka baada ya kushuhudia dhulma iliyokuwa ikitendwa katika zama za kijahiliya, kwani haki ilikuwa ikitolewa kwa misingi ya kiukoo na kikabila, na wenye haki walikuwa wakinyimwa haki zao pale ambapo walikosa jamaa na ndugu wa kuwatetea katika vyombo vya sheria, suala la haki na uadilifu lilikuwa halina 143
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 143
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
nafasi. Mizizi ya dhulma iliyoota katika zama za kijahiliya iliendelea kutoa matawi yake hata baada ya kuja kwa Mtume (s.a.w.w.), kama inavyosimuliwa na Ibn Abbas ya kwamba, baadhi ya Waislamu wapya walipofika Madina walikuwa wakijizuia kutoa ushahidi pale walipoona kwamba haki haiko kwa jamaa zao, na ushahidi wao utawasababishia madhara juu yao, hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipoteremsha Aya hii ili kuwaonya Waumini hao waachane na tabia hii inayochukiza. Pia Aya inataja kitu kingine kinacho changia kutotekelezwa uadilifu, kitu hicho ni mali, kwa hivyo Waumini wanapewa tahadhari wasije wakaghilibika kwa mali ya matajiri kwa lengo la kuinyonga haki, vile vile ufakiri nao usiwe ni sababu ya mtu kukubali kuhongwa au kudai haki isiokuwa yake hata kama mtu ataendelea kuwa fakiri, kwani Mwenyezi Mungu anajua zaidi hali za wale ambao natija za ushahidi wa uadilifu utakuwa dhidi yao, kwani mwenye mali au cheo hawezi kumdhuru shahidi mwadilifu kwani shahidi huyo yuko katika himaya ya Mwenyezi Mungu, na wala fakiri hatolala njaa kwa sababu ya kutoa ushahidi wa uadilifu: “Akiwa ni tajiri au fukara basi Mwenyezi Mungu anawastahiki zaidi.” Katika kutilia mkazo zaidi mafunzo haya, Aya inawataka Waumini wajiepushe na kufuata matakwa ya nafsi zao: “Basi msifuate hawaa ili mfanye uadilifu.” Ibara hii inabainisha wazi ya kwamba chanzo kikubwa cha dhulma na jeuri ni kufuata matamanio ya nafsi. Aya inamalizia kwa kushadidia na kutilia umuhimu suala la uadilifu katika maisha ya kijamii, kwa kueleza ya kwamba Mwenyezi Mungu anawaona waja Wake na anajua vyema kila wanacho kifikiria na kukifanya, anaona na kumshuhudia kila ambaye humzuilia mwenye haki haki yake, au yule anayeigeuza haki, au kujiepusha na kufanya haki baada ya kumbainikia, anasema: “Na mkiupotoa au mkaachana nao basi Mwenyezi Mungu ana habari ya myatendayo.” Aya hii inathibitisha namna Uislamu ulivyoupa kipaumbele uadilifu katika maisha ya kijamii, msisitizo juu uadilifu uliorudiwa mara kwa mara ni ushahidi tosha juu madai haya, lakini jambo la kusikitisha kwa Waislamu ni kuwa mbali sana na mafunzo haya matakatifu yanayotoka kwa Mola Wao, bila ya shaka hii ndio siri kubwa ya Waislamu kuwa nyuma katika maisha yao ya kijamii.
144
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 144
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI NA SITA
ْ ين آ َمنُوا آ ِمنُوا باللهَِّ َو َر ُسولِ ِه َو ََّيا أَُّي َها ال َ َ اب الَّ ِذي َن َّز َل ت ك ال ذ ِ ِ ِ ِ َ ُ ْ َعلَىٰ َر ُسولِ ِه َو َّلله َ ت ك ال ِ اب الَّ ِذي أ ْن َز َل ِم ْن َقبْل َو َم ْن َي ْك ُف ْر ِبا ِ ِ ْلآ َّ ْ ًا َ ضل َ َو َم اَل ِئ َك ِت ِه َو ُكتُ ِب ِه َو ُر ُسلِ ِه َوال َي ْوم ا ِخ ِر َف َق ْد ض اَلل َب ِعي ًدا ِ “Enyi mlioamini! Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Kitabu ambacho amemteremshia Mtume Wake na Kitabu alichokiteremsha kabla. Na mwenye kumkakataa Mwenyezi Mungu na Malaika Wake na vitabu Vyake na Siku ya Mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali.” (Qur’ani 4:136)
SABABU YA KUTEREMKA Imenukuliwa kutoka kwa ibn Abbas ya kwamba Aya hii iliteremka kuhusiana na baadhi ya watu wazito miongoni mwa Ahlul kitabi, kama vile Abdallah ibn Salam, Asad ibn Ka’b na ndugu yake; Asyad ibn Ka’b na wengineo, sababu yenyewe ilikuwa ni kama ifuatavyo: Walimwendea Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia ya kwamba, wao wamemwamini yeye na Kitabu alichoteremshiwa (Qur’ani) na pia wamemwamini Nabii Musa na Taurati na pia wamemwamini Uzeyri, na wala hawakuwaamini Mitume wengine, hapo iliteremka Aya hii ikiwaelezea umuhimu wa kuiamini Mitume yote pamoja na vitabu vyote vilivyoteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.75
MAELEZO Aya inabainisha ya kwamba maneno yaliyomo humu yanawahusu baadhi ya Ahlul kitabi ambao waliukubali Uislamu, lakini kutokana na ukaidi wao walikataa kuamini yale yaliyokuja kabla ya Uislamu miongoni mwa Mitume na vitabu vilivyoteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa ile dini waliokuwa wakiifuata (Nabii Musa pamoja na Taurati), Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hii akiwausia umuhimu wa kuamini Mitume yote na Vitabu vilivyoteremshwa kwao, kwani Mitume wote wamepelekwa na Mola Aliye Mmoja na lengo lao lote ni moja, kwa hivyo itakuwa haileti maana halisi kwa kuwaamini baadhi na kuwakataa wengine, kwani ukweli 75
Kitabu kilichotangulia,Uk.494 145
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 145
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
mmoja hauwezi kugawanyika, kwa hivyo Aya Tukufu imekuja kuwaambia: “Enyi mlioamini! Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Kitabu ambacho amemteremshia Mtume Wake na Kitabu alichokiteremsha kabla. Na mwenye kumkataa Mwenyezi Mungu na Malaika Wake na vitabu Vyake na Siku ya Mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali.” Tukiachia kuangalia sababu iliyosababisha mpaka kuteremshwa Aya hii, ni kwamba Aya inawahusu watu Waumini wote walio na itikadi ya kwamba Uislamu ndio Dini yao, lakini imani yao hiyo ikawa haijaingia ndani ya mishipa ya damu yao, kwa hivyo inawataka na kuwaamrisha wawe waumini wa kikweli kweli, kwa kufuata mafunzo yote yatokayo kwa Mola Wao. Pia maneno haya yanaelekezwa kwa wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume Yake yote, lakini bado wakawa hawajaamini baadhi ya vipengele vingine vinavyoonekana ni vidogo katika Uislamu. Kutokana na mafunzo yaliyomo katika Aya hii inabainika ya kwamba Waumini wa kikweli kweli wana wajibu wa kuwaamini Mitume wote pamoja na Vitabu vyote walivyokuja navyo Mitume waliotangulia pamoja na Malaika wa Mwenyezi Mungu, kwani kutoamini haya kunapingana na hekima ya Mwenyezi Mungu katika matendo Yake. Je! Inawezekana kwa Mwenyezi Mungu Aliye na hekima kuuacha umma wa Kiislamu bila ya kiongozi atakayeendeleza kazi iliyofanywa na Mitume baada ya wao kutawafu?! Kuna suala linalojitokeza katika Aya hii, suala hilo linasema: Je! Malaika waliotajwa katika Aya hii ambao Waumini wanawajibu wa kuwaamini, ni Malaika wanaofanya kazi ya kupeleka Wahyi tu, kwa vile wana mafungamano juu ya imani ya Mitume pamoja na vitabu vilivyoteremshwa kwao, au inawahusu Malaika wote? - Jawabu la suala hili ni kama ifuatavyo; kama vile kulivyo na baadhi ya Malaika waliopewa kazi ya Wahyi, baadhi ya Malaika wamepewa kazi katika nyanja nyingine, kama vile upuliziaji roho, kutia sura watoto katika matumbo ya mama zao, kunyesha mvua na nyinginezo, kwa hivyo kuamini kuwepo Malaika wanaofanya kazi hizi ni sehemu katika kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kinyume chake ni upotevu ulio wazi kabisa na kuwa mbali na njia iliyonyooka, kama Aya inavyobainisha: “Na mwenye kumkakataa Mwenyezi Mungu na Malaika Wake na vitabu Vyake na Siku ya Mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali.” Katika Aya hii ni wazi kwamba Muumini wa kweli ni yule anayeami misingi mitano ya imani, kama kulivyo na umuhimu mkubwa kwa mtu kumwamini Mwenyezi Mungu pamoja na Siku ya Kiyama, vile vile kuna umuhimu mkubwa wa kuamini Vitabu vilivyoteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mitume pamoja na Malaika.
146
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 146
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI NA SABA
َين أ ََّيا أَُّي َها ال َ ين آ َمنُوا اَل َتتَّ ِخ ُذوا ْال ْ ُ َ ون ْال ُم ْؤ ِم ِن َ َ ين د ن م ء ا ي ل و ر ف ا ك ذ ْ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ْ ُ ون أَ ْن َت ْج َعلُوا للِهَِّ َعلَي َ ْك ْم ُس ْل َطاًنا ُم ِبي ًنا إِ َّن ال ُم َنا ِف ِق َ أَتُ ِري ُد ين ِفي َ ْالد ْر ِك أ َّال ْس َف ِل ِم َن الن َّ َ يرا إِاَّل الَّ ِذ ين َتابُوا ً ص ِ ار َولَ ْن َت ِج َد لَ ُه ْم َن ِ ٰ ُ َّللِه َ ْ صلَ ُحوا َو صوا ِدي َن ُه ْم ِ َفأول ِئ َك َم َع ُ َص ُموا ِباللهَِّ َوأَ ْخل ْ ََوأ َ اع َت َُّين أَ ْج ًرا َع ِظي ًما َما َي ْف َع ُل الله َ ين َو َس ْو ْف ي َ ُؤ ِت اللهَُّ ْال ُم ْؤ ِم ِن َ ْال ُم ْؤ ِم ِن َ ِب َع َذ ِاب ُك ْم إِ ْن َش َك ْرتُ ْم َوآ َم ْنتُ ْم َو َك ان اللهَُّ َشا ِك ًرا َعلِي ًما “Enyi mlioamini! Msiwafanye makafiri kuwa marafiki badala ya waumini. Je, mnataka awe nayo Mwenyezi Mungu hoja dhahiri juu yenu. Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini motoni. Hutakuta kwa ajili yao msaidizi. Ila wale waliotubu na wakatengeza (mwendo wao) na wakashikamana na Mwenyezi Mungu na wakamtakasia Mwenyezi Mungu dini yao, basi hao watakuwa pamoja na waumini na Mwenyezi Mungu atawapa waumini malipo makubwa. Mwenyezi Mungu ana haja gani ya kuwaadhibu kama mtashukuru na mtaamini na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye shukrani Mjuzi.” (Qur’ani 4:144-147)
MAELEZO Aya inawatahadharisha Waumini pamoja na kuwakataza kutowategemea na kutowafanya marafiki wanafiki na makafiri badala ya Waumini wenzao: “Enyi mlioamini! Msiwafanye makafiri kuwa marafiki badala ya waumini.” Aya inaeleza bayana ya kwamba kuwategemea makafiri na kuwafanya marafiki ni miongoni mwa makosa makubwa, kwani ni jambo linalopelekea kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na ndio maana adhabu yake ikawa ni kali sana kwa kila mwenye kwenda kinyume na makatazo haya: “Je, mnataka awe nayo Mwenyezi Mungu hoja dhahiri juu yenu.” Aya ya pili inaelezea hali za wanafiki ambao wamefanya marafiki na baadhi ya Waumini walioghafilika, ni kwamba Siku ya Kiyama watawekwa katika tabaka la chini kabisa la Moto ili upate kuwaumiza zaidi kuliko wakaazi wengine wa Motoni, na hakuna yeyote atakayekuwa na uwezo wa kuwaokoa kutokana na adhabu hiyo: 147
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 147
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
“Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini motoni. Hutakuta kwa ajili yao msaidizi.” Ni wazi, kwa mujibu wa Aya hii na nyinginezo, kwamba wanafiki ni maadui zaidi wa Waislamu, na pia wao ni viumbe vinavyowekwa mbali zaidi na Rehema za Mwenyezi Mungu. Hii ndio sababu adhabu yao kuwa kubwa zaidi Siku ya Kiyama. Kwa hakika watu hao wanastahiki adhabu hiyo kwani ndio wanaowasababishia Waislamu kila aina ya matatizo na mashaka katika Dini yao na maisha yao kwa ujumla. Watu hawa ni kama mbwa mwitu waliojivisha ngozi ya kondoo katika kundi la kondoo, wao hudhihirisha sura ya Uislamu na imani ya hali ya juu, na pindi Waumini wanapowakunjulia vifua kwa kukaa nao kwa wema ndipo wanapoanza kuwahujumu nyuma ya migongo yao kwa kutumia silaha zao zenye sumu. Kwa kweli maadui wa aina hii ni hatari zaidi kuliko wale wanaotangaza wazi wazi uadui wao dhidi ya Waislamu. Aya ya tatu inabainisha kwa uwazi kwamba pamoja na mtu kutumbukia katika shimo la unafiki na kuwadhuru Waislamu, bado mlango wa toba kwa ajili ya kurejea kwa Mwenyezi Mungu uko wazi ikiwa ataamua kikwelikweli kubadilika na kufanya mambo mema na kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu: “Ila wale waliotubu na wakatengeza (mwendo wao) na wakashikamana na Mwenyezi Mungu na wakamtakasia Mwenyezi Mungu dini yao,” Mwisho wa watu hawa wenye kutubia ni kuwa ni wenye kufaulu na kujumuishwa pamoja na kundi la Waumini: “basi hao watakuwa pamoja na waumini.” Na Mwenyezi Mungu atawapa Waumini malipo makubwa sana na ya hali ya juu: “Na Mwenyezi Mungu atawapa waumini malipo makubwa.” Jambo la kuzingatia ni kwamba watu hawa waliotubia na hatimaye kuwekwa katika kundi moja na Waumini, ni kwamba malipo ya wale Waumini ambao tokea mwanzo walikuwa na imani thabiti isiyotetereka malipo yao yatakuwa makubwa zaidi ikilinganishwa na wale waliotubia kutokana na maovu waliyokuwa wakiyatenda. Jambo jingine la kuzingatia ni kwamba Aya imeweka bayana malipo watakayoyapata wanafiki Siku ya Kiyama, malipo hayo ni kama vile kuwekwa katika tabaka la chini la Moto wa Jahannamu. Ama kuhusiana na malipo ya Waumini, Mwenyezi Mungu ametosheka kwa kusema ya kwamba watapata thawabu na malipo makubwa, hii ni ishara ya wazi ya kwamba malipo ya Waumini hayana kiwango wala kikomo, kiasi ambacho inakuwa vigumu kwa akili ya mwanadamu kuweza kufahamu uhalisia wake.
148
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 148
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI NA NANE
َ ُْقو ِد أُ ِحلَّ ْت لَ ُك ْم َبهي َم ُة أ ََّيا أَُّي َها ال ُ ين آ َمنُوا أَ ْو ُفوا ب ْالع ْ ال َ ام إِ اَّل ع ن ذ َ ِ ِ ِ ِ ُ َما ي ُْتلَىٰ َعلَي الص ْي ِد َوأَ ْنتُ ْم ُح ُر ٌم إِ َّن اللهََّ َي ْح ُك ُم َما َّ ْر ُم ِحلِّي َ ْك ْم َغي ُري ُد ِي “Enyi mlioamini! Tekelezeni mapatano. Mmehalalishiwa wanyama wenye miguu minne, ila wale mnaotajiwa bila kuhalalishiwa mawindo mkiwa katika Ihramu. Hakika Mwenyezi Mungu anahukumu atakavyo.” (Qur’ani 5:1)
MAELEZO Ulazima wa Kutekeleza Ahadi: Aya hii tukufu inawataka Waumini wajibidiishe kutekeleza mikataba yote waliokubaliana miongoni mwa mambo mbali mbali kama vile biashara, mikopo, mirathi n.k. Jambo linalopasa kuzingatiwa katika Aya hii ni neno ‘Uquudi’ neno hili limekuja katika hali ya wingi likiwa na maana ya kufunga kamba mafundo upande mmoja, au kuzifunga kamba mbili kwa pamoja. Kwa hivyo maana ya ndani ya Aya hii yanatokana na maana hii, kwa hivyo kila ahadi au makubaliano yanatambulikana kwamba ni ahadi inayopaswa kutekelezwa, sawa ahadi hiyo ikiwa ni kwa mtu na mtu au kwa mtu na Mola Wake. Mfasiri Alusiy katika tafsiri yake Ruhul Ma’niy, amemnukuu Raghib Asfahaniy akisema: “Ahadi ziko za aina tatu: Ahadi kati ya mja na Mola Wake, ahadi kati ya mja na nafsi yake na ahadi kati ya mja na mja mwenzake.”76 Ahadi ni suala lililo na upana sana katika maisha ya Mwislamu, kwani pia linajumuisha kuitekeleza hata kama ni pamoja na asiyekuwa mwislamu. - Baada ya Aya kuelezea suala la ahadi, inaelezea hukumu nyingine miongoni mwa hukumu za Kiislamu, hukumu hiyo inahusiana juu ya uhalali au uharamu wa baadhi ya wanyama. Wanyama wa mifugo waliokusudiwa katika Aya hii ni ngamia, ng’ombe na mbuzi, wanyama hawa ni halali kuliwa. Ama wanyama ambao asili yake ni halali kuliwa lakini kwa sababu ya mtu kuwemo katika ihramu ya Hijja au Umrah ni haramu kwake kuwinda, kwa hivyo pia si halali kula kilichowindwa. 76
Alusiy, Ruhul Maaniy,’Maudhui ya Ayah hii.’ 149
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 149
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
Mwishoni mwa Aya Mwenyezi Mungu anasisitiza ya kwamba pindi anapoamua kutoa hukumu yoyote, huitoa na kuibainisha bila ya kuterereka, kwani Yeye ni Mtambuzi wa maslahi ya waja Wake kuliko yeyote yule, anasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anahukumu atakavyo.�
150
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 150
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA ISHIRINI NA TISA
َّ ين آ َمنُوا اَل تُ ِحلُّوا َش َعا ِئ َر اللهَِّ َو اَل َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ْر ْال َح َرا َم َو اَل َ الشه ْ ون َف َ ين ْال َبي َ ْت ْال َح َرا َم َي ْب َت ُغ َ آم ض اًل ِم ْن ِّ ْال َه ْد َي َو اَل ْال َق اَل ِئ َد َو اَل ْ ِّه ْم َو ِر ُ اص َطا ُدوا َو اَل َي ْج ِر َمنَّ ُك ْم َش َن آن ْ ض َوا ًنا َوإِ َذا َحلَْلتُ ْم َف ِ َرب ُ ص ُّد وك ْم َع ِن ْال َم ْس ِج ِد ْال َح َر ِام أَ ْن َت ْع َت ُدوا َو َت َعا َونُوا َ َق ْو ٍم أَ ْن ْ ْ َْ لإ ْ َ ْ َّ َا ان َواتَّ ُقوا ِ َعلى ال ِب ِّر َوالتق َوىٰ َول َت َعا َونُوا َعلى ا ِث ِم َوال ُع ْد َو ُ اللهََّ إ َّن اللهََّ َش ِدي ُد ْال ِع َقاب ُح ِّر َم ْت َعلَي َّ ْك ُم ْال َم ْي َت ُة َو الد ُم َولَ ْح ُم ِ ِ ُ ْ ْ َّ ُوذ ُة َو ْال ُم َت َر ِّد َية ُ َّلله ُ َ ْال ِخ ْنزير َو َما أ ِهل لِ َغيْر ا ِ ب ِه َوال ُم ْن َخ ِن َقة َوال َم ْوق ِ ِ ِ ِ َ ُ ُ َّ َّا َ َ َ ُ َ ُّ ُع إل َما ذكيْت ْم َو َما ذ ِب َح َعلى ص ِب ُ الن َّ يحة َو َما أكل َ َوالنَّ ِط ِ ُ السب َ َْوأَ ْن َت ْس َت ْق ِس ُموا ب أ َ س الَّ ِذ ين َك َف ُروا ِم ْن َ ال ْز اَل ِم َذٰلِ ُك ْم ِف ْس ٌق ْال َي ْو َم َي ِئ ِ َ َ ْ ْ ْ ِدي ِن ُك ْم َف اَل َت ْخ َش ْو ُه ْم َو اخ َش ْو ِن ال َي ْو َم أ ْك َمل ُت لَ ُك ْم ِدي َن ُك ْم َوأ ْت َم ْم ُت ُ َعلَي ُ ض ْ يت لَ ُك ُم الإْ ِ ْس اَل َم ِدي ًنا َف َم ِن اض ُط َّر ِفي ِ ْك ْم ِن ْع َم ِتي َو َر ور َر ِحي ٌم ٌ ف لإِِ ْث ٍم َفإِ َّن اللهََّ َغ ُف ٍ ْر ُم َت َجا ِن َ ص ٍة َغي َ َم ْخ َم “Enyi mlioamini! msivunje heshima ya alama za Mwenyezi Mungu wala ya mwezi mtakatifu, wala ya wanyama wa kuchinja, wala ya vigwe, wala ya wale wakusudiao kwenda kwenye Nyumba Tukufu kutafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi. Na mkishatoka kwenye Ihramu, basi windeni. Wala kule kuwachukia watu waliowazuilia kufika Msikiti mtukufu, kusiwapelekee kuwafanyia jeuri. Na saidianeni katika wema na takua wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. Mmeharamishiwa nyamafu na damu na nyama ya nguruwe, na aliyechinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliyekufa kwa kunyongeka, na aliyekufa kwa kupigwa, na aliyeanguka, na aliyepigwa pembe, na aliyeliwa na mnyama ila mliowachinja, na aliyechinjiwa mizimu. Na kuagulia kwa mburuga. Hayo yote ni ufasiki. Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu,
151
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 151
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
basi msiwaogope na mniogope Mimi. Leo nimewakamilishia dini yenu na kuwatimizia neema Yangu na nimewapendelea Uislamu kuwa dini. Basi aliyefikwa na dharura bila kuelekea kwenye dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.” (Qur’ani 5:2-3)
MAELEZO Hukumu Nane Katika Aya Moja: Katika Aya ya kwanza miongoni mwa Aya hizi mbili inataja hukumu za Mwenyezi Mungu zilizomuhimu sana, hukumu ambazo zilishuka mwishoni mwa maisha ya Mtume (s.a.w.w.), hukumu zote hizo au nyingi zao zinahusiana na suala la kuizuru nyumba ya Mwenyezi Mungu (Al-Kaaba). Hukumu hizo ni kama zifuatazo: 1.
Waumini wanatakiwa wasivunje heshima ya alama za Dini ya Mwenyezi Mungu: “Enyi mlioamini! msivunje heshima ya alama za Mwenyezi Mungu.”
2.
Aya inawataka Waumini waiheshimu miezi mitukufu (Mfunguo pili, Mfunguo tatu, Mfunguo nne na Mwezi wa Rajabu), na wala wasiingie katika vita kwenye miezi hii, isipokuwa pale watakapoanzwa kushambuliwa, hapo watakuwa na haki ya kujihami: “Wala ya mwezi mtakatifu,”
3.
Ni haramu kuchinjwa kwa wanyama waliokusudiwa kuchinjwa katika ibada ya Hijja kabla ya kufika pahala paliporuhusiwa kisheria kuchinjwa wanyama, ikiwa mtu atawachinja, basi nyama yake itakuwa ni haramu kuliwa: “Wala ya wanyama wa kuchinja, wala ya vigwe,”
4.
Aya inakataza kubughudhiwa na kusumbuliwa kwa mahujaji waliokwenda kuizuru nyumba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hata wale waliokwenda kwa ajili ya kufanya biashara katika mji huo mtukufu wa Makka, ni wajibu wa wahusika wawape uhuru wa kufanya ibada zao kwa wasaa, kwani mahujaji wamepewa kinga kutoka kwa Mwenyezi Mungu wakati wote wanapokuwa katika eneo takatifu la Makka, kama Aya inavyosema: “Wala ya wale wakusudiao kwenda kwenye Nyumba Tukufu kutafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi.”
152
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 152
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
5.
Ni haramu kwa mtu aliyehirimia amali ya Hijja au Umrah kuwinda, lakini baada ya kumaliza ibada zake anaruhusiwa kufanya hivyo: “Na mkishatoka kwenye Ihramu, basi windeni.”
6.
Aya inawakataza Waislamu wasiwazuie na kuwadhikisha wale watu walio wadhikisha Waislamu kabla ya wao kuingia katika Uislamu, asili ya jambo hili ni kutokana na tukio la Suluhu ya Hudaybiya, wale Waislamu waliozuiliwa kuingia Makka wakati huo, nao walijaribu kutaka kuwazuia wale waliofanya hivyo kwa lengo la kulipiza kisasi, lakini ni kwamba watu wale baadaye waliingia katika Uislamu, kwa hivyo wanakatazwa kuchukua hatua za ulipizaji kisasi: “Wala kule kuwachukia watu waliowazuilia kufika Msikiti mtukufu, kusiwapelekee kuwafanyia jeuri.”
7.
Licha ya hukumu hii kuelezea masuala yanayohusiana na Hijja, lakini kwa uhakika ni hukumu inayohusiana na kila pahala panapotokea kutokuelewana baina ya watu, kwa hivyo Aya inawataka Waislamu waachane na kufufua chuki za zamani, na badala yake wasahau na kusameheana kwa yote yaliopita.
8.
Aya inatoa msisitizo kwa Waislamu kuungana na kushirikiana katika kumcha Mwenyezi Mungu na kusaidiana katika kutenda mambo mema yatakayowafaa duniani na akhera, na wala wasisaidiane katika mambo ya shari na uadui: “Na saidianeni katika wema na takua wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”
9. Ili hukumu zilizopita ziweze kutekelezwa ipasavyo, Aya inasisitiza juu ya suala la uchaji Mungu na kujiepusha na kila aina ya maasi na kuelezea adhabu kali itakayowasibu wale wanaokwenda kinyume na mafundisho ya Dini ya Kiislamu: “Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.” Kusaidiana Katika Mambo Mema: Msisitizo wa kusaidiana ulioko katika Aya ni kitu kinachozingatiwa kuwa ni miongoni mwa misingi mikubwa ya Kiislamu, suala la kusaidia linatakiwa litekelezwe katika kila nyanja, kama vile katika maisha ya kijamii, kisiasa, kiuchumi n.k. Kusaidiana katika mambo mema na ya kheri ni katika mambo yaliyo wajibu kwa Waislamu, ni haramu kusaidiana katika mambo maovu na ya shari ambayo kwa kawaida mambo hayo huwa ni sababu kubwa ya kuenea dhulma, ufisadi na jeuri katika jamii. 153
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 153
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
Amri hii ya kusaidiana kati ya Waislamu imekuja kwa lengo la kuipinga ile kanuni iliyokuwepo wakati wa ujahiliya, kanuni hiyo ilikuwa inasema: ‘Msaidie ndugu yako, akiwa ni dhalimu au mwenye kudhulumiwa.’ Katika zama za ujahiliya ilikuwa kama kundi la kabila fulani litawashambulia kabila jingine, wale watu wa kabila lililoshambulia wakiwasaidia wenzao bila ya kuangalia haki iko upande gani. Hali hii ya kijahilia bado ndio inayofuatwa leo kati ya nchi zilizoungana kwa namna moja au nyingine, marafiki wa nchi hizi wako tayari kuzisaidia nchi hizo kwa kila aina ya msaada wa kijeshi pasi na kuwa na mizani ya uadilifu; ikiwa zinadhulumiwa au kudhulumu. Kwa hakika Uislamu umekuja kuibatilisha kanuni hii ya kijahiliya, na badala yake ukawataka Waislamu wasaidiane katika mambo ya kheri tu, na kuacha kuwaunga mkono au kuwasaidia madhalimu. Kwa hivyo ni wajibu kwa Waislamu kuungana katika kuleta kheri na maendeleo katika jamii yao, na pia katika kupinga aina zote za dhulma, bila ya kuangalia dhulma hiyo inatendwa na nani. Kutokana na kanuni hii wanachuoni wa elimu ya Fiqhi wameweza kutoa hukumu ya kuharamisha kila jambo ambalo litakuwa ni sababu ya kuendeleza maasi hata kama asili yake ni halali, kwa mfano wameharamisha kuuza zabibu katika kiwanda kinachoitumia zabibu hiyo katika kutengeneza ulevi, au kuwauzia silaha maadui wa Uislamu na Waislamu, au kukodisha pahala ambapo patafanywa biashara isiyo halali kisheria. Ikiwa Waislamu watahuisha kanuni ya kusaidiana katika kuiendeleza jamii yao, na kuondosha ubinafsi au kuangalia maslahi ya kikabila au kiukoo, na kuacha kutoa aina yoyote ya msaada unaochangia udhalimu, bila shaka wataweza kuondosha kasoro na mapungufu mengi katika jamii yao. Ama kuhusiana na mahusiano ya kimataifa, lau kama baadhi ya nchi zingeacha kuzisaidia na kuziunga mkono nchi zinazozifanyia uadui nchi nyingine, basi dhulma na uadui unaofanywa kila leo usingekuwepo, lakini hali ilivyo hivi leo ni kuwepo baadhi ya nchi kuzisaidia nchi zinazo waonea raia wa nchi nyingine, huku wakitoa visingizio, eti maslahi yao yanawalazimu kufanya hivyo (kuwasaidia madhalimu), katika hali kama hii pasitarajiwe kupatikana kheri yoyote katika ulimwengu wetu huu. Aya ya pili inaanza kwa kuwaeleza Waumini baadhi ya wanyama walio haramu kuwala. Katika Aya ya kwanza ya Sura hii ya tano (Suratul Maida) tumeona ya kwamba Mwenyezi Mungu katutajia baadhi ya wanyama walio halali,na alitoa ahadi ya kwamba pia atataja baadhi ya sifa za wanyama wasio halali, ahadi hiyo ameitekeleza katika Aya hii kiasi ambacho ametaja aina kumi na moja za nyama zilizo haramu kuliwa, aina hizi pia zimerudiwa kutajwa katika Aya nyingine kwa lengo la kusisitiza uharamu wake, aina hizo kama zilivyokuja katika Aya hii ni kama ifuatavyo:
154
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 154
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
1.
Nyamafu.
2.
Damu.
3.
Nyama ya nguruwe.
4.
Mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kama walivyokuwa wakifanya wakati wa zama za kijahiliya.
5.
Aliyekufa kwa kunyongeka koo au kufa mwenyewe.
6.
Aliyekufa kwa kupigwa.
7.
Aliyekufa kwa kuanguka.
8.
Aliyekufa kwa kupigwa pembe na mnyama mwenzake.
9.
Aliyekufa kutokana na kupigwa na mnyama mkali.
10. Myama aliyechinjiwa masanamu. 11. Nyama iliyopatikana kwa njia ya kamari. Katika zama za kijahilia ilikuwa watu wanachezesha kamari na mshindi huzawadiwa nyama. Uharamu wa kamari hauko katika nyama tu bali chochote kile kitakachotolewa kitabakia kuwa ni haramu kwa matumizi yoyote yale. - Katika kusisitiza uharamu wa aina hizi za nyama, Aya inamalizia kwa kusema: “Hayo yote ni ufasiki.� Hali ya Kati na Kati Katika Ulaji wa Nyama: Katika utafiti huu tunaona ya kwamba Uislamu umefuata njia ya kati na kati katika ulaji wa nyama, huku ikitofautiana sana na baadhi ya watu hasa katika nchi za Magharibi ambao wanakula kila kitu vikiwemo vyura, na kwa upande mwingine wafuasi wa dini ya kihindu wao wamejizuia kula aina zote za nyama. Uislamu umekuja kuhalalisha nyama ya wanyama wanaokula vyakula safi na tohara na kuharamisha wanyama wanaokula najisi na mizoga. Miongoni mwa shuruti zinazomfanya mnyama kuwa halali nyama yake ni kama zifuatazo: 1.
Mnyama anayekula majani, ama mnyama anayekula nyama ya wanyama wenzake mara nyingi wanyama wa aina hii huwa hawachagui kati ya mzoga na usiokuwa mzoga, wanyama hawa ni rahisi kusibiwa na ugojwa wakati wanapokula wanyama wenzao, na pia hurithi tabia za wale wanyama wanaowala, ama wanyama wanaokula majani nyama yao huwa salama na isiyo na maradhi. 155
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 155
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
2.
Mnyama anayeliwa asiwe ni mwenye kuichukiza nafsi ya mlaji.
3.
Nyama isiache athari mbaya au madhara kwa mlaji.
4.
Wanyama wanaochinjwa kinyume na Mwenyezi Mungu wameharamishwa kutokana na kuwa ni wenye kunajisika kwa najisi ya kimaana (kiroho).
5.
Uislamu umebainisha namna ya kuchinjwa wanyama kwa ajili ya kulinda siha ya mwanadamu na kumjenga katika tabia nzuri.
Baada ya Aya kueleza hukumu mbali mbali za kifiqhi kama zilivyoainishwa, imekuja na ibara mbili zilizo na maana pana sana, ibara ya kwanza inasema: “Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope na mniogope Mimi.” Na ibara ya pili inasema: “Leo nimewakamilishia dini yenu na kuwatimizia neema Yangu na nimewapendelea Uislamu kuwa dini.” Ni Lini Mwenyezi Mungu Aliikamilisha Dini? Utafiti ulio muhimu katika ibara hizi mbili unapatikana katika neno ‘Leo’ neno ambalo limo katika kila ibara, baada ya neno hili kunafuatia maneno haya: Kukata tamaa makafiri, kukamilika Dini, kutimizwa neema na Mwenyezi Mungu na kukubali ya kwamba Uislamu ndio mfumo wa maisha kwa viumbe vyote. Wafasiri wa Qur’ani wamesema mengi kuhusiana na ibara hizi mbili, na jambo lisilo na shaka ni kwamba siku hiyo ilikuwa ni siku isiyokuwa ya kawaida katika maisha ya Mtume (s.a.w.w.). Imepokewa ya kwamba hata baadhi ya Mayahudi walisema: “Lau kama kungeteremka ibara katika vitabu vyao inayoelezea siku kama hiyo, basi wangeliifanya kuwa ni sikukuu.”77 Basi na tufanye utafiti wa kihistoria kwa kutumia vigezo mbali mbali ili tuielewe siku hiyo iliyo na umuhimu wa kipekee katika maisha ya Mwislamu. Je, unadhani ya kwamba siku hiyo ni siku ambayo Mwenyezi Mungu aliteremsha hizi hukumu za kisheria zinazobainisha halali na haramu zilizotajwa katika Aya hii?Ni jambo la wazi kabisa ya kwamba uteremshwaji wa hukumu hizi haupelekei kupewa umuhimu mkubwa kama huu, na wala haiwi sababu ya kukamilishwa Dini, kwa sababu hazikuwa hukumu za mwisho kuteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.), na pia hukumu hizi si sababu ya makafiri kukata tamaa katika kuizuia Dini isiende mbele, kwani kutajwa nyama iliyo halali na ile iliyo haramu hakuachi madhara yoyote ndani ya nafsi za makafiri. Je, makusudio ya siku hiyo ni siku ya Arafa, katika Hijja ya Mtume (s.a.w.w.) ya kuaga (Hijjatul Wada’a) kama baadhi ya wafasiri walivyopita? 77
Shiraziy,Tafsirul Amthal, Jz.3, Uk.595 156
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 156
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
Jawabu la suala hili pia nalo ni laa, kwani ishara zilizomo hazioani na tafsiri hii, kwani siku hiyo ya Arafa hakukutokea tukio lolote zito linaloweza kuwakatisha tamaa makafiri. Ama ikiwa ni wingi wa watu waliokuwa pamoja na Mtume (s.a.w.w.), ni kwamba wingi huo ulikuwepo Makka kabla ya siku ya Arafa, na kama ni hukumu za kisheria zilizoshuka siku hiyo ya Arafa, hukumu hizo zilikuwa si tishio kwa makafiri. Au makusudio ya siku hiyo, ni ile siku iliokombolewa Makka, kama baadhi ya wafasiri walivyoeleza? Jambo linalofahamika kwa uwazi kabisa ni kwamba Suratul Maidah iliteremka muda mrefu baada ya kukombolewa Makka. Au makusudio yake ni siku ilipoteremshwa suratul Bara’a? Suratul Bara’a ilipishana sana na Suratul Maidah. Tafsiri za kushangaza zaidi ni za baadhi ya wafasiri waliosema ya kwamba siku hiyo ni ile siku ya kwanza kudhihiri Uislamu na kupewa Utume Mtume Muhammad (s.a.w.w.)! Matukio haya mawili hayana mafungamano yoyote na Aya hii, hasa ikizingatiwa urefu wa zama uliopo kati yao. Kilicho bainika ni kwamba rai hizi sita zilizotolewa na baadhi ya wafasiri hakuna hata moja inayooana na kuwafikiana na Aya hii. Rai iliyobakia, ni rai inayokubaliwa na wafasiri wote wa Kishia kwa vile ni rai inayotiwa nguvu kwa Riwaya mbali mbali zilizomo katika hata vitabu vya Kisunni, seuze vya Kishia. Rai hii inaafikiana na mtiririko wa Aya. Siku hiyo ni siku ya Ghadir Khum, siku ambayo Mtume (s.a.w.w.) alimtawazisha Imam Ali (a.s.) hatamu za uongozi wa dola ya Kiislamu baada ya yeye Bwana Mtume (s.a.w.w.) atakapoiaga dunia. Jambo hilo lilifanywa kwa wazi na kwa hali iliyokuwa rasmi kabisa. Siku hiyo ndio siku ambayo makafiri walichanganyikiwa na kukata tamaa, kwa vile walikuwa wakidhani ya kwamba Uislamu utakoma mara baada ya kutawafu Mtume (s.a.w.w.). Lakini baada ya kumuona Mtume (s.a.w.w.) akimkabidhi majukumu ya uongozi mtu ambaye alikuwa hakuna mfano wake miongoni mwa masahaba, kielimu, uchamungu, ushujaa na uadilifu, mtu huyo ni Imam ali (a.s.),makafiri waliposhuhudia wenyewe namna Waislamu walivyokuwa wakimpa viapo vyao vya utii (Bay’a), makafiri hao waligubikwa na huzuni na simanzi na kukosa muelekeo katika yale waliyokuwa wakiyatarajia katika kuumaliza Uislamu, lakini kwa tukio hilo walitambua ya kwamba Uislamu ni mbichi, mkakamavu na wenye kubakia. Lau kama Mtume (s.a.w.w.) asingemuainisha mtu atakayeshika pahala pake, basi Dini ingekuwa na kasoro kubwa katika utekelezaji wa sheria zake na pia kuingiliwa na watu wasio na ujuzi katika masuala mbali mbali yanayohusiana nayo. Kwa tukio hilo Mwenyezi Mungu aliridhia kuufanya Uislamu uwe ndio utaratibu na mfumo wa maisha unaostahiki kufuatwa na kila mwanadamu.
157
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 157
12/8/2014 2:43:40 PM
WITO KWA WAUMINI
Baadhi ya Vigezo Vinavyounga Mkono Rai Hii: Katika tafsiri za Kisunni kama vile, Tafsirul Kabir, Ruhul Maaniy, na al Manaar, katika kuitafsiri Aya hii wamesema ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) hakuishi zaidi ya siku themanini na moja baada ya kuteremka Aya hii, jambo hili linaashiria wazi kwamba kwa mujibu wa siku ambayo alifariki Mtume (s.a.w.w.) ambayo ni tarehe kumi na mbili mfunguo sita kwa mujibu wa Riwaya za Kisunni na hata baadhi ya Riwaya za Kishia kama alivyoeleza Kuleyn katika kitabu chake maarufu Usulul Kaafiy ni dalili tosha ya kwamba Aya hii iliteremka siku ya tarehe kumi na nane mfungo tatu, siku hiyo ndio siku iliyotokea tukio la Ghadir Khum (Kutawalishwa Imamu Ali (a.s.) Ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w.)). Riwaya mbali mbali za Kisunni na za Kishia zimeeleza ya kwamba Aya hii iliteremka siku ya tukio la Ghadir Khum, mara baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuwaeleza Waislamu ya kwamba khalifa baada yake atakuwa Imamu Ali (a.s.), miongoni mwa Riwaya hizo ni kama zifuatazo: a.
Mfasiri maarufu wa Kissuni; ibn Jariri At-Tabariy amenakili katika kitabu chake kiitwacho Al-Wilaayah kutoka kwa Zayd ibn Arqam, ya kwamba Aya hii iliteremka siku ya Ghadir Khum, ikumuhusisha Ali ibn Abi Talib (a.s.)
b.
Alhafidh; Abu Naiim al Asfahaniy, amenakili katika Aya zilizoteremka kumuhusu Imam Ali ibn Abii Talib (a.s.) kutoka kwa Abii Saidil Khuduriy, ya kwamba katika siku ya Ghadir Khum Mtume (s.a.w.w.) alimpa Ali (a.s.) madaraka ya ukhalifa… na watu hawakukhitalifiana siku hiyo, na baadaye ikashuka Aya: “Leo nimewakamilishia dini yenu na kuwatimizia neema Yangu na nimewapendelea Uislamu kuwa dini.” Mara tu baada ya Mtume (s.a.w.w.) kumtawaza Imam Ali (a.s.) alisema: “Mwenyezi Mungu ni mkubwa kwa kuikamilisha Dini na kuitimiza neema na kuridhika Mola wangu juu ya ujumbe wangu na uongozi wa Ali (a.s.) baada yangu. Ambaye mimi ni kiongozi wake basi pia na Ali ni kiongozi wake, ewe Mola Wangu! Muunge mwenye kumuunga Ali na mfanyie uadui mwenye kumfanyia Ali uadui, na mnusuru mwenye kumnusuru Ali na mkate mwenye kumkata Ali.
c.
Mwanahistoria maarufu wa Kiislam; al-Khatib al-Baghdad amesimulia kutoka kwa Abu Huraira ya kwamba, Aya isemayo: “Leo nimewakamilishia dini yenu na kuwatimizia neema Yangu na nimewapendelea Uislamu kuwa dini,” iliteremka mara tu baada ya tukio la Ghadir Khum, kwa kutawalishwa 158
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 158
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
Ali (a.s.) uongozi baada ya Mtume (s.a.w.w.), na Umar ibn Khattab (wakati wa kutoa kiapo chake kwa Ali) alisema: Hongera ewe mtoto wa Abu Talib, umekuwa kiongozi wangu na kiongozi wa kila Mwislamu.”78 Pia Riwaya zinazothibitisha kuteremka Aya hii siku ya Ghadir Khum zimenakiliwa na ibn Kathir katika tafsiri yake, Jalal Diin katika tafsiri yake iitwayo Ad-Durrul Manthur, na vitabu vingine vya Kissuni. Ama vitabu vya Kishia Riwaya zake zimeenea katika vitabu vingi, huku zikiwa hazina tofauti na Riwaya zilizonakiliwa katika vitabu vya Kisunni. Kwa hivyo jambo hili ni jambo la umma mzima wa Kiislamu, na sio jambo linalohusiana na baadhi ya madhehebu, la kusikitisha ni kwamba hao waliolinakili katika vitabu vyao sahihi hawakulipa umuhimu wowote, na leo linaonekana ni katika matukio mageni katika historia ya Kiislamu! Maudhui ya uongozi baada ya Mtume (s.a.w.w.) yamechukua wakati mwingi kwa watafiti wa Kiislamu licha ya kuwepo Riwaya za wazi zinazothibitisha ya kwamba wenye haki hiyo ni Maimamu kutoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w.). Lakini la kusikitisha zaidi ni kwamba ni suala ambalo lilichukua roho za Waislamu mamia kwa maelfu wakiwemo Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Kwa mfano katika vita vya ngamia vilivyokuwa vikiongozwa na Bibi Aisha dhidi ya khalifa wake; Imam Ali (a.s.) Waislamu zaidi ya elfu kumi walipoteza roho zao kwa muda wa siku tatu. Muawiya ibn Abi Sufiyan naye alisababisha vifo vya watu wasiopungua elfu thelathini katika vita vya Siffin, kutokana na kupingana na khalifa wa zama zake; Imamu Ali (a.s.). Katika Qur’ani Tukufu kuna Aya mbali mbali zinazothibitisha Ukhalifa wa Imamu Ali (a.s.) baada ya Mtume (s.a.w.w.), Aya hizo zinatiliwa nguvu na Riwaya nyingi za Mtume s.a.w.w. Kwa anayetaka kuyafahamu haya anaweza kurudia katika vitabu maalumu vinavyoelezea suala hili. Mwisho kabisa, Aya imerudi katika kuzungumzia maudhui ya nyama iliyo haramu. Aya inabainisha hukumu ya mtu asiyekuwa na budi ila kula nyama iliyoharamu kutokana na njaa kali na kukosa kitu cha halali cha kuweza kuiokoa nafsi yake dhidi ya mauti. Aya imetoa ruhusa kwa mtu wa aina hiyo kuweza kula kiasi cha haja yake tu na sio kujaza tumbo, na wala asile akiwa na nia ya kutaka kupingana na amri ya Mwenyezi Mungu, kwa kufanya hivyo ndio Aya ikaashiria kuwepo msamaha wa Mwenyezi Mungu na rehema Zake kwa waja Wake wakati wanapodharurika kula visivyo halali: “Basi aliyefikwa na dharura bila kuelekea kwenye dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.”
78
Kitabu kilichotangulia, Uk.598 159
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 159
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI
ْ الص اَل ِة َف َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ َ اغ ِسلُوا ُو ُج وه ُك ْم َّ ين آ َمنُوا إِ َذا ُق ْمتُ ْم إِلَى وس ُك ْم َوأَ ْر ُجلَ ُك ْم إِلَى ِ َوأَ ْي ِد َي ُك ْم إِلَى ْال َم َرا ِف ِق َوا ْم َس ُحوا ِب ُر ُء َّ ْال َك ْع َبيْن َوإ ْن ُك ْنتُ ْم ُجنُبًا َف َ َّروا َوإِ ْن ُك ْنتُ ْم َم ْر ٰضىٰ أَ ْو َعلَى ُ اطه ِ ِ َ َ ْ ُ َ ُ َس َف ٍر أَ ْو َجا َء أ َح ٌد ِم ْنك ْم ِم َن ال َغا ِئ ِط أ ْو اَل َم ْست ُم النِّ َسا َء َفل ْم َت ِج ُدوا ُ وه ُك ْم َوأَ ْي ِد يك ْم ِم ْن ُه َما َ َما ًء َف َت َي َّم ُموا ِ ص ِعي ًدا َطيِّبًا َفا ْم َس ُحوا ِب ُو ُج ُ يُري ُد اللهَُّ لَِي ْج َع َل َعلَي َ ل ِك ْن يُري ُد لِي َ ْك ْم ِم ْن َح َرج َو ِّر ُك ْم َولِيُ ِت َّم ٰ َ ُطه ِ ِ ٍ َّ َّلله ْ ُ ُ ُ ُ ُ ْ َ َ َ َ ِن ْع َم َت ُه َعليْك ْم ل َعلك ْم َتشك ُر ون َواذك ُروا ِن ْع َم َة ا ِ َعليْك ْم َو ِم َيث َاق ُه الَّ ِذي َو َاث َق ُك ْم ِب ِه إِ ْذ ُق ْلتُ ْم َس ِم ْع َنا َوأَ َط ْع َنا َواتَّ ُقوا اللهََّ إِ َّن اللهََّ َعلِي ٌم ور ُّ ات ِ ِب َذ ِ الص ُد
“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swala, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni, na mkiwa wagonjwa au mumo safarini au akawa mmoja wenu ametoka chooni au mkagusana na wanawake, kisha msipate maji, basi tayamamuni na mchanga ulio twahara, mpake nyuso zenu na mikono yenu. Mwenyezi Mungu hapendi kuwatia katika taabu lakini anataka kuwatakasa na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu na ahadi Yake aliyoifungamanisha nanyi mliposema: Tumesikia na tumetii. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.” (Qur’ani 5:6-7)
Kujisafisha Kimwili na Kiroho: Aya zilizopita zimeelezea namna ya kukiweka kiwiliwili katika hali ya usafi kwa kula chakula kilicho kizuri na halali, ama katika Aya hii inaelezwa namna ya kuitoharisha roho na nafsi ya mwanadamu. Aya ya kwanza inataja hukumu za udhu, josho na kutayammamu kama njia ya mtu kuweza kuitoharisha nafsi yake, Aya inasema: 160
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 160
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swala, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka vifundoni.” Aya haikuelezea maeneo ya uso ambayo ni wajibu kuoshwa, lakini Riwaya mbali mbali kutoka kwa Ahlul Bayt (a.s.) zimeelezea kwa uwazi namna Mtume (s.a.w.w.) alivyokuwa akiosha uso wake mtukufu. Urefu wa uso kwa mujibu wa wanafiqhi ni kuanzia maoteo ya nywele za kichwa mpaka mwisho wa kidevu, ama upana wake ni sehemu inayoingia katika urefu wa ncha ya kidole cha gumba na kidole cha kati, hii ndio maana ya uso kisheria, kwani uso ni ile sehemu inayomdhihirikia mtu pindi anapomtazama mwenzake kwa mbele. Ama kuhusiana na mikono miwili, Aya imeeleza sehemu inayostahiki kuoshwa, sehemu hiyo ni kuanzia kwenye ncha za vidole hadi vifundoni, bila ya kuelezwa uoshaji unaanzia wapi na kuishia wapi, alimradi sehemu ya kuoshwa ni iliyotajwa. Baadhi ya watu wanadhani ya kwamba inatosha kuosha mikono mpaka kwenye viwiko (sehemu inayovaliwa saa), neno ‘ILAA’ halimaanishi ukomo (kuishia) wa kuoshwa, yaani kuanzia ncha za vidole na kumalizia vifundoni, kama wanavyodhani Ahlu Sunna, Aya haikuja kueleza namna ya kuosha mikono, bali kuelezea sehemu zinazostahiki kuoshwa katika mkono. Kwa ufafanuzi ni kama vile mtu anapomwambia fundi rangi ampakie rangi nyumba yake pindo la urefu wa mita moja, maneno haya hayamaanishi ya kwamba anatakiwa aipake kuanzia chini mpaka huo urefu wa mita moja. Riwaya mbali mbali kutoka kwa Ahlul Bayt (a.s.) zinaelezea ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitawadha kuanzia katika vifundo viwili na kumalizia kwenye ncha za vidole viwili. Jambo la kuzingatia ni kwamba vifundo pia vinastahiki kuoshwa wakati wa kutia udhu, kwani mpaka unaingia katika kitu kilichowekewa mipaka. Kuhusiana na kupaka kichwa kumekuja herufi ‘Baa’ herufi hii katika Aya hii inamaanisha kupaka baadhi tu ya kichwa na sio kichwa chote, kama Riwaya zinavyoeleza na kukubaliwa na wataalamu wa lugha ya Kiarabu, sehemu hiyo inayostahiki kupakwa ni juu ya utosi, ama kule kupaka au kuosha kichwa chote pamoja na masikio kama inavyofanywa na baadhi ya Waislamu kwa hakika ni jambo lisilokubaliana na Aya hii. Ibara hii ‘Na miguu yenu’ iliyokuja baada ya kueleza wajibu wa kupaka kichwa ni dalili ya wazi ya kwamba pia miguu nayo inastahiki kupakwa na sio kuoshwa, kama Riwaya zilizoko katika vitabu vya Kisunni zinavyoeleza hivyo. Ili maana halisi ya kupaka ikamilike inapasa sehemu inayopakwa iwe kavu na bila ya kuchukua maji mapya, unyevunyevu uliobakia baada ya kuosha mikono utatumika kupakia kichwa na miguu. 161
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 161
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
Baada ya haya, Aya inaelezea hukumu ya kuoga kwa mwenye janaba: “Na mkiwa na janaba basi ogeni.” Makusudio ya ibara hii ni kujitoharisha mwili mzima, lau kama si hivyo, basi ingetajwa hiyo sehemu inayopaswa kutoharishwa. Kwa hivyo ni wajibu kwa mwenye janaba kuoga kabla ya Swala, na josho hilo litamtosheleza kwa udhu (hakuna ulazima wa kutawadha kwa ajili ya Swala). Baada ya hapo Aya imetaja hukumu za kutayammamu kwa kusema: “Na mkiwa wagonjwa au mumo safarini au akawa mmoja wenu ametoka chooni au mkagusana na wanawake, kisha msipate maji, basi tayamamuni na mchanga ulio twahara.” Aya imetaja moja kati ya sababu za kutayammamu, sababu hiyo ni kukosekana kwa maji, na pia inaeleza ya kwamba tayammamu inakuwa pia badala ya josho kama ilivyo badala ya udhu. Kama Aya ilivyoelezea namna ya kutia udhu pia imeelezea namna ya kutayammamu kwa muhtasari kama isemavyo: “mpake nyuso zenu na mikono yenu.” Makusudio ya ibara hii kupiga kwenye kitu kinachofaa kwa kutayammam, kama vile mchanga, jiwe, changarawe, kokoto n,k. kwa kutumia viganja viwili vya mikono kisha kupakaza katika uso na mikono miwili, na sio kuuchota na kuupakaza. Miongoni mwa masharti ya hicho kitu cha kutumia kwa Tayammam ni kuwa tohara, kama Aya ilivyoeleza, kwani ni tabia ya mwanadamu kupenda kitu kizuri na tohara na mwenye kuwa na tabia ya kuchukia uchafu na najisi. Hekima ya Kutayammamu: Tukianzia na hekima inayopatikana katika udhu ni kwamba katika kutia udhu kuna faida mbili zinazopatikana: Faida ya kwanza ni ya kiafya na faida ya pili ni ya kiroho. Ni jambo lisilopingika ya kwamba kuosha uso na mikono mara tano kwa siku au kwa uchache mara tatu faida yake ya kiafya na ya kisiha haifichikani, ama kuhusiana na faida ya kiroho ni kwamba suala la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kutaka radhi Zake wakati wa kutia udhu inamaanisha ya kwamba harakati zote za udhu zinazoanzia katika uso na kumalizikia katika miguu ni kwamba wakati huo mja anakuwemo katika utiifu wa Mola Wake Mtukufu. Katika Riwaya iliyosimuliwa na Imam Ali ibn Musa inasema:
إنّما أمر بالوضوء وبدئ به ألن يكون العبد طاهرا إذا قام مطيعا له فيما أمره نقيّا من,بين يدي الجبّار عند مناجاته إيّاه األجناس والنّجاسة مع ما فيه من ذهاب الكسل وطرد النّعاس 162
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 162
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
.وتزكية الفؤاد للقيام بين يدي الجبّار “Hakika pameamrishwa udhu na kuwa ndio kianzio (cha Swala) ili mja awe tohara wakati atakapo simama mbele ya Mola Aliye Jabari wakati anapomsemesha, hali ya kumtii Yeye kwa yale aliyomuamrisha, akiwa msafi kwa kuepukana na uchafu na najisi, akiwa ni mwenye kuufukuza uvivu na usingizi, na kuutakasa moyo wakati wa kusimama mbele ya Mola Aliye Jabbari.”79
Ama hekima za kutayammamu, ni kwamba watu wengi hujiuliza: Ni faida gani inayopatikana kwa mtu pindi anapopiga viganja vyake katika mchanga na kupaka uso wake na mikono yake hasa ikizingatiwa ya kwamba mara nyingi mchanga unakuwa na uchafu pamoja na bakteria na vijidudu vingine? Jawabu la suala hili ni kwamba, pia katika kutayammamu nako kunapatikana faida mbili kama ilivyo katika udhu: Kwa kuanzia na faida ya kiroho, ni kwamba kutayammamu ni moja kati ya mambo ya ibada, na ni ibada ambayo ina unyenyekevu na ucha Mungu wa hali ya juu, kwani mwanadamu hulipaka mchanga paji lake la uso kwa mikono yake, paji ambalo ni kiungo kitakatifu sana katika mwili wake, yote hayo ni kudhihirisha utiifu wake na unyenyekevu wake usio na kifani kwa Mola Wake Mlezi. Na kama kwamba anasema katika nafsi yake: Ewe Mola Wangu, hakika paji langu pamoja na mikono yangu ni yenye kunyenyekea kwako na kutii amri zako. Baada ya mtu kukamilisha kutayammamu anaelekea kusimama mbele ya Mola Wake kwa ibada ya Swala na ibada nyingine zinazoshurutishwa kuwa na udhu au josho la wajibu. Mfumo huu unapandikiza unyenyekevu na utiifu mbele ya Mwenyezi Mungu Mola Muumba na kumlea katika kumwabudu Yeye peke Yake na kushukuru neema Zake. Ama faida ya kiafya ni kwamba katika ulimwengu wetu huu wa leo imethibitika ya kwamba katika mgongo wa ardhi kunapatikana idadi kubwa ya bakteria wanaofanya kazi ya kuangamiza virusi mbali mbali vinavyosababisha magonjwa, huku wakisaidiwa na mionzi ya jua inayopiga katika ardhi hiyo na kuiweka katika hali ya usafi na usalama. Katika kuthibitisha uwepo wa bakteria hao katika ardhi ni pale anapofukiwa mnyama katika ardhi, ni kwa masiku machache tu mnyama yule huoza na kukauka na kuweza kuondoa harufu mbaya kwa mara moja. Lau kama hali isingekuwa hivyo, basi ardhi ingekuwa ni sababu kubwa ya janga la kibinadamu kutokana na mzoga wenye harufu mbaya. Kwa hivyo si tu kwamba mchanga uko salama kutokana na uchafu bali pia ni kitoharisho kizuri kama ilivyo kwa maji isipokuwa maji huua vijidudu na kuviondosha, ama mchanga huviua tu. 79
Hurrul Amil, Wasailu Shia, Jz.1, Uk.257 163
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 163
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
Lakini miongoni mwa mambo ya kuzingatia ni kwamba mchanga au udongo unaotumika kwa kutayammamu ni lazima uwe safi na tohara kama Aya ilivyoashiria kwa kusema: “ulio twahara� Kwa hivyo basi ni vyema kwa mtu anayetaka kutayammamu kutafuta mchanga ulioko juu ya ardhi unaofikwa na mionzi ya jua na upepo, kwani mchanga wa aina hiyo uko salama dhidi ya vijidudu vibaya, na kinyume chake unakuwa na vijidudu vinavyoshambulia na kuuwa vijidudu vinavyosababisha magonjwa kwenye mwili wa mwanadamu. Hekima ya Kukoga: Baadhi ya watu huwenda wakauliza, ni kwanini Uislamu unaamrisha kukoga kwa mtu aliyepatwa na janaba na ilhali ni kiungo kimoja tu kinacho chafuka wakati wa kupatwa na janaba? Je kuna tofauti yoyote kati ya haja ndogo na manii ambapo viwili hivyo vyote vinatoka katika kiungo kimoja, wakati huku ikiwa ni wajibu kuosha tu kiungo kinachotoa haja ndogo baada ya kutoka, ama baada ya kutoka manii inapasa kuosha mwili mzima tena kwa kutekeleza josho hilo kwa utaratibu maalumu? Jawabu la suala hili ni kama ifuatavyo: Wakati wa kutoka manii ni kwamba mwili wote unapata hisia na msisimko kwa kujisikia raha, hii ni dalili ya kushiriki viungo vyote wakati wa kutoka manii, hali ni kinyume kabisa wakati wa kujisaidia haja ndogo. Zaidi ya hayo josho la janaba ni miongoni mwa mambo yanayomkurubisha mja kwa Mola Wake, kwani josho halitozingatiwa kuwa ni sahihi ikiwa muogaji hakutia nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, kwani ukweli wa mambo ni kwamba mwili na roho zinashiriki kwa kupata msisimko wakati wa kutoka manii. Au wakati watu wanapokutana kijinsia, nafsi ndio ya mwanzo kuanza kuingiwa na matamanio ya kijinsia na hatimaye mwili hukamilisha kwa kufanya yale yanayotakiwa na nafsi. Josho la janaba ni josho la kuosha mwili wote, na pia inazingatiwa kuwa ni kuiosha na kuisafisha roho kwa kule muogaji anapotia nia ya kujikurubisha kwa Mola Wake wakati anapotaka kukoga na kuwa ni moja kati ya njia za utiifu na ucha Mungu. Zaidi ya hayo ni kwamba, vile vile wajibu wa kukoga katika Uislamu unalenga katika kukiweka kiwiliwili cha Mwislamu katika hali ya usafi na unadhifu kama inavyohimizwa suala hili katika upande wa kiafya ili kuyaweka maisha yake katika hali ya furaha, kwani kuna wengi miongoni mwa watu ambao hawajishughulishi na suala la usafi wa miili yao, lakini wajibu huu wa kukoga katika Uislamu unawalazimu kuisafisha miili yao kila baada ya muda fulani. Wajibu wa uogaji wa josho la janaba utabakia kwa mtu hata kama alikoga kabla ya kupatwa na janaba. Mwishoni mwa Aya hii Mwenyezi Mungu anatueleza ya kwamba maamrisho Yake kwa waja Wake hayana lengo la kuwatia mashakani waja Wake na kuwasababishia 164
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 164
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
uzito katika maisha yao ya kila siku, bali katika maamrisho hayo kuna faida kubwa kwa wanadamu, Aya inasema: “Mwenyezi Mungu hapendi kuwatia katika taabu lakini anataka kuwatakasa na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru.” Maneno haya ya Mwenyezi Mungu yanasisitiza ya kwamba, amri pamoja na kanuni zake zote alizoziweka zinalenga katika kuwanufaisha wanadamu na kulinda maslahi yao ya kimwili na ya kiroho. Kutokana na ukweli huu ndio ikawa pale ambapo amri fulani inapokuwa inasababisha madhara kwa baadhi ya watu, Mwenyezi Mungu hutoa ruhusa ya kutekelezwa jambo jingine mbadala au kusamehewa kabisa mja kutekeleza jambo hilo. Kwa mfano kama tulivyoona katika uchambuzi wa Aya hii, asiye na uwezo wa kuyapata maji au ikiwa anayo lakini yanamsababishia madhara wakati wa kutia udhu au kukoga, basi hukumu ya mtu huyo itakuwa ni kutayammamu. Mfano mwingine ni kwa mtu asiye na uwezo wa kufunga mwezi wa Ramadhan basi ama atalazimika kuja kufunga wakati mwingine au kutoa fidia. Bila ya shaka ni jambo la wazi ya kwamba kuna baadhi ya hukumu na kanuni zinazoonekana na baadhi ya watu kwamba zinawasababishia madhara na mashaka makubwa, kama vile hukumu ya kupigana vita vya Jihadi, lakini ikilinganishwa manufaa pamoja na madhara yanayopatikana katika vita vya Jihadi, ni wazi kwamba manufaa yake ni makubwa zaidi kuliko madhara. Katika Aya zilizopita zimetaja mambo mbali mbali kama vile kukamilika kwa neema, kufaradhishiwa Waislamu wajibu wa kujitoharisha wakati wanapotaka kuswali na kukoga baada ya kupatwa na janaba na mambo mengine kama tulivyoyaona, hapa Mwenyezi Mungu anawataka Waumini wazingatie na kukumbuka neema hizi kubwa alizowaneemesha juu yao, anasema: “Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu na ahadi Yake aliyoifungamanisha nanyi mliposema: Tumesikia na tumetii. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.” Basi kuna neema gani yaliyo kubwa kama mtu kujaaliwa kuwa ni miongoni mwa Waumini na kuishi katika kivuli cha Uislamu na kuwa mbali na kila aina ya maovu na udhalimu baada ya kuwa katika hali ya upotevu na ujinga uliobobea. Kabla ya kuja kwa Uislmu katika bara Arabu watu wengi walikuwa wakiishi katika hali ya dhulma na ujahilia huku wakifuata kanuni ya msituni isemayo: ‘Mwenye nguvu mpishe.’Inamaanisha ya kwamba kila mwenye nguvu aachiwe afanye atakavyo kwani hakuna yeyote anayeweza kumzuia kufanya alitakalo. Kutokana na ujinga huo waliokuwanao na baadaye kuangaziwa na nuru ya Uislamu na kuachana na aina hizo za dhulma ndio Mwenyezi Mungu akawataka wakumbuke neema hii kubwa walioipata.
165
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 165
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI NA MOJA
َ ين آ َمنُوا ُكونُوا َق َّوا ِم َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين للِهَِّ ُش َه َدا َء ِب ْال ِق ْس ِط َو اَل ُ َي ْج ِر َمنَّ ُك ْم َش َن ْ آن َق ْو ٍم َعلَىٰ أَ اَّل َت ْع ِدلُوا ٰ اع ِدلُوا ُه َو أَ ْق َر ُب لِلتَّ ْق َو ى َ ُير ِب َما َت ْع َمل ون ٌ َواتَّ ُقوا اللهََّ إِ َّن اللهََّ َخ ِب
“Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mtoao ushahidi kwa uadilifu. Wala kuchukiana na watu kusiwapelekee kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu ndiko kunakokurubisha kwenye takua. Na Mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.” (Qur’ani 5:8)
MAELEZO Aya ya kwanza miongoni mwa Aya hizi mbili inalingana kwa kiasi kikubwa na Aya ya 135 ya sura ya 4 huku kukiwa na tofauti ndogo. Aya hiyo pamoja na Aya hizi zote kwa pamoja zinawataka Waumini kushikamana katika kufanya uadilifu katika kila nyanja ya maisha yao. Baada ya Waumini kutakiwa kuwa waadilifu, Aya inataja moja kati ya sababu zinazopelekea baadhi ya watu kutokuwa waadilifu, na kutoa onyo kali kwa wale wanaoacha kufanya uadilifu kwa sababu ya ubinafsi au ukabila, kwani kufanya hivyo ni kuwadhulumu watu wengine haki zao. Kwa hivyo ni juu ya Waumini kuelewa ya kwamba uadilifu ni kitu kilicho bora sana na kitukufu zaidi, Aya inasema: “Wala kuchukiana na watu kusiwapelekee kutofanya uadilifu.” Baada ya kutaja sababu hii inayowazuia baadhi ya watu kutowatendea haki na uadilifu wanadamu wenzao, Aya inasisitiza zaidi juu ya uadilifu kwa kusema: “Fanyeni uadilifu ndiko kunakokurubisha kwenye takua.” Na kwa vile Uislamu unazingatia ya kwamba uadilifu ni miongoni mwa nguzo kubwa za uchamungu, Aya inalisisitiza jambo hilo mara nyingine kwa kusema: “Na Mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.” Uadilifu ni Nguzo Muhimu Katika Uislamu: Ni mara nyingi kukuta jambo lililopewa umuhimu wa hali ya juu katika Uislamu kama lililovyopewa suala la uadilifu, suala la uadilifu kama lilivyo suala la tawhidi 166
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 166
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
(kumpwekesha Mwenyezi Mungu), yote kwa pamoja ni miongoni mwa mambo ya msingi yaliojengewa jengo la Dini ya Kiislamu. Kwa maneno mengine ni kwamba, kama ilivyo kwa mambo yote yanayohusiana na mambo ya kiitikadi, kimatendo, kijamii, kitabia na kisharia hayaachani na tawhidi, na pia haiwezekani yakatengana na uadilifu. Kutokana na hali hii ndio ikawa uadilifu ni miongoni mwa nguzo za Dini ya Kiislamu na kuwa ni msingi madhubuti katika misingi ya fikra za Kiislamu. Kutokana na umuhimu wa suala zima la uadilifu kuna Riwaya nyingi zinazoashiria hilo, miongoni mwa Riwaya hizo ni kama zifuatazo: Amesema Mtume s.a.w.w:
ّ الظلم عند اهلل هو ّ فإن ّ إيّاكم ّ والظلم الظلمات يوم القيامة Jiepusheni na dhulma, kwani dhulma mbele ya Mwenyezi Mungu ni giza la Siku ya Kiyama.80
Amesema tena:
السماوات واألرض ّ بالعدل قامت Mbingu na ardhi zimesimama kwa uadilifu.81
Kauli hii ya Mtume (s.a.w.w.) inazingatiwa kuwa ni miongoni mwa kauli zinazobainisha kwa uwazi na ufasaha juu ya uadilifu. Kauli hii ya Mtume (s.a.w.w.) inamaanisha ya kwamba kama vile mbingu na ardhi zilivyoumbwa kwa uadilifu, basi ni hivyo hivyo wanadamu watekeleze uadilifu katika maisha yao ya kila siku pasi na kuwadhulumu wengine. Uadilifu huu uliotumika katika kuumbwa mbingu na ardhi lau kama utakosekana kwa kitambo kidogo, basi vitu hivyo vitaharibika na kupotea, haya yanathibitishwa na Riwaya isemayo:
ّ الملك يبقى مع الكفر وال يبقى مع .الظلم Ufalme hubakia pamoja na ukafiri na wala haubakii pamoja na dhulma.82
Riwaya hii inatubainishia namna dhuluma ilivyo na uwezo wa kuuondosha utawala katika madaraka kwa haraka sana katika maisha haya ya dunia, kwani Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 3, Uk.633 Kitabu kulichotangulia 82 Kitabu kilichotangulia 80 81
167
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 167
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
pindi watawala wanapokuwa madhalimu na madikteta fujo na vurugu hutawala miongoni mwa raia na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na hatimaye utawala huo kupinduliwa au wananchi hao kudumu katika mapigano kwa muda mrefu, natija hii ya kuwepo dhulma katika jamii mbalimbali ni jambo lililo wazi katika macho na masikio ya kila mtu. Katika kuikinga jamii dhidi ya machafuko na kuporomoka, Uislamu umesisitiza sana juu ya kuwepo uadilifu kati ya watu, na haya yatapatikana tu pale kila mtu atakapotekeleza wajibu wake kwa mujibu wa mafunzo ya Uislamu.
168
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 168
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI NA MBILI
ُ ين آ َمنُوا ْاذ ُك ُروا ِن ْع َم َت اللهَِّ َعلَي َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ْك ْم إِ ْذ َه َّم َق ْو ٌم أَ ْن ُ ْس ُطوا إلَي َّ ْك ْم أَ ْي ِد َي ُه ْم َف َك ُ َيب َِّف أَ ْي ِد َي ُه ْم َع ْن ُك ْم َواتَّ ُقوا اللهََّ َو َعلَى الله ِ َ َُف ْل َي َت َو َّك ِل ْال ُم ْؤ ِمن ون “Enyi mlioamini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu, walipoazimia watu kuwanyooshea mikono yao, akaizuia mikono yao kuwafikia. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani 5:11)
MAELEZO Katika Qur’ani kuna Aya nyingi zinazowataka Waumini wakae na kufikiria neema mbali mbali walizoneemeshwa na Mola Wao, miongoni mwa Aya hizo ni Aya hii. Lengo kubwa linalotakiwa katika kujikumbusha neema hizo ni kumuwezesha mja kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza maamrisho Yake na kuachana na makatazo Yake, kwani kufanya hivyo ndiko kunakompelekea katika kuimarisha imani yake na msimamo wake katika Dini ya Mwenyezi Mungu. Wafasiri wa Qur’ani wametofautiana juu ya neema ya nusra waliyoipata Waumini, baadhi yao wanasema ya kwamba neema waliyoipata ni kule kuokolewa Mtume (s.a.w.w.) kutokana na njama ya kutaka kuuliwa, njama iliyopangwa na kabila la Bani Nadhir wakati Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Maswahaba zake walipohamia katika mji wa Madina. Wengine wanasema ya kwamba ni kutokana na tukio la Batnu Nahli ambalo lilitokea katika mwaka wa sita wa Hijria katika tukio la Sulhu Hudaybiya, pale washirikina waliokuwa wakiongozwa na Khalid ibn Walid (kabla ya kusilimu) walipopanga kuwashambulia Waislamu wakati wa kutekeleza Swala. Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kujua njama hizo aliwataka Waislamu waswali Swala ya khofu ambayo huswaliwa rakaa mbili. Kwa kufanya hivyo aliweza kuziharibu njama zao, na Waislamu waliweza kusalimika dhidi ya vitimbi vyao. Ama wafasiri wengine wanajumuisha matukio yote ya hatari yaliyotishia usalama wa Waislamu pamoja na Uislamu katika maisha yote ya kuutangaza Uislamu. Kauli hii ya mwisho inakubalika
169
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 169
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
zaidi hasa ikizingatiwa namna neno ‘Kawmu’ lilivyokuja katika Aya. Neno hilo haliko katika hali ya kuainisha kitu maalumu, bali liko katika hali ya ujumla, kwa hivyo itakuwa inawajumuisha watu wote waliojaribu kuudhuru Uislamu na Waislamu, na kutokana na fadhila zake Mwenyezi Mungu aliwaokoa Waislamu kutokana na hatari mbali mbali na kuwashinda maadui. Mwisho Aya inawataka Waumini wajilazimishe na uchamungu kama ni matokeo ya kukumbuka neema walizoneemeshwa, na pia ni dalili ya kuonesha shukurani ya neema hizo, kwani kufanya hivyo ni kuziendeleza neema hizo na kubakia nazo katika maisha yao yote ya dunia na kuendelea nazo kwa uzuri na ubora zaidi katika maisha yao mara tu baada ya kuiaga dunia, inasema: “Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu.” Ni wazi kwamba kumtegemea Mwenyezi Mungu haimaanishi ya kwamba mtu aachane na majukumu yake au asitumie zana zinazofaa katika maeneo mbali mbali, bali inamaanisha yakwamba pale mtu anapotumia vipawa vyake inampasa azingatie ya kwamba vipawa vyake hivyo havitokani na uwezo wake wa kimali au kiakili, bali ni vitu alivyoruzukiwa na Mwenyezi Mungu. Pindi mtu anapokuwa na mawazo haya basi ataondokewa na majivuno, kujiona pamoja na ubinafsi, na pia ataondokewa na khofu na wasiwasi pale atakapokabiliwa na matatizo mbali mbali katika maisha yake hata yawe ni makubwa kiasi gani, kwani mtu wa aina hii wakati wote anakuwa na imani ya kwamba Mwenyezi Mungu anamuona na yuko pamoja na yeye na Yeye ndiye Mwenye uwezo wa kumuondoshea matatizo yake, kwani Yeye ni Muweza wa kila kitu. Katika kutangulizwa amri ya kumcha Mwenyezi Mungu kabla ya ile ya kumtegemea ni ishara ya kwamba uangalizi wa Mwenyezi Mungu na himaya Yake ni mambo wanayoyapata wanaomcha Yeye tu.
170
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 170
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI NA TATU
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اه ُدوا ِفي ِ ين آ َمنُوا اتَّ ُقوا اللهََّ َوا ْب َت ُغوا إِلَ ْي ِه ْال َو ِسيلَ َة َو َج َ َس ِبيلِ ِه لَ َعلَّ ُك ْم تُ ْفلِ ُح ون “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na tafuteni njia ya kumfikia, mfanye juhudi katika njia Yake ili mpate kufaulu.” (Qur’ani 5:35)
MAELEZO Aya hii inaelezea mambo matatu ambayo anatakiwa kila Muumini wa kweli kushikamana nayo ili kujihakikishia kufaulu hapa duniani na kesho akhera, mambo hayo ni kama yafuatavyo: 1.
Kujipamba na uchamungu, “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu”
2.
Kutafuta njia sahihi ya kumfikia Mwenyezi Mungu Mtukufu. “Na tafuteni njia ya kumfikia.”
3.
Kujitahidi katika kuitetea na kuisimamia Dini ya Mwenyezi Mungu. “Mfanye juhudi katika njia Yake…”
Natija ya kushikamana na maamrisho haya ya Mwenyezi Mungu ni kufanikiwa katika maisha ya dunia na ya akhera, kama Aya inavyo malizia, “… ili mpate kufaulu.” Kutokana na kuelezwa kwa kina suala la uchaji Mungu na namna ya kuitetea na kuilinda Dini ya Mwenyezi Mungu, basi katika kitabu chetu hiki tutazungumzia zaidi juu ya kutawasali kama tunavyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kupitia Aya hii. Maana ya neno ‘Kutawasali’ ni kutaka kujikurubisha kwenye kitu kwa kupitia kitu kingine, kwa hivyo neno ‘Tawasuli’ katika Aya hii lina maana mbali mbali, neno hili linajumuisha kila jambo ambalo litakuwa ni sababu ya mtu kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, na tawasuli iliyo na umuhimu zaidi kuliko zote ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.) na kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu na kufanya ibada zilizo wajibu kama Swala, Swaumu, Hijja, kuunga udugu, kutoa mali kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu kwa wazi na kwa siri na kila aina ya matendo mema, kama anavyosema Imam Ali a.s: 171
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 171
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
“Hakika kitu bora wanachotawasalia wenye kutawasali kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kupigana Jihadi katika njia ya Yake, kwani hiyo (Jihadi ) ndio kilele cha Uislamu na kusimamisha Swala, kwani hiyo ni sheria ya Kiislamu, na kutoa Zaka kwani hiyo ni faradhi iliyo wajibu, na kufunga mwezi wa Ramadhani, kwani hiyo ni kinga dhidi ya adhabu, na kuizuru Nyumba (Al-Kaaba) na kufanya Umrah kwani mawili haya yanaondoa ufukara na kusafisha madhambi, na kuunganisha udugu, kwani jambo hili linazidisha mali na umri, na kutoa sadaka kwa siri kwani hili linafuta dhambi, na kutoa sadaka kwa wazi, kwani hili linazuia kifo kibaya…”83 Vile vile kutawasali kwa kupitia Mitume, Maimam na mawalii nako pia kunaingia katika maana hii pana ya neno ‘Tawasuli’ kwani nako kunamfanya mja kuwa karibu na Mwenyezi Mungu. Ukuruba huo utapatikana iwapo mtu atafuata mwenendo wao kwa ukamilifu, au kwa kuwataka wamuombe Mola Wao ili awakidhie haja zao na kusamehewa makosa yao kwa misingi ya kwamba wao ni watu walio karibu zaidi na Mwenyezi Mungu na hukubaliwa maombi yao zaidi kuliko watu wengine. Basi wale ambao wameliangalia suala la kutawasli katika maana moja tu watakuwa wamekosea, kwani neno ‘Tawasuli’ kama tulivyoashira linamaanisha kufanya kitu chochote ambacho kitampatia mfanyaji radhi za Mwenyezi Mungu na kuwa karibu Naye. Jambo muhimu la kuzingatia hapa ni kwamba, kutawasali hakumaanishi kutaka kitu kwa Mtume au Imamu, bali ina maana kwa mtu Muumini kujipinda na kujitahidi katika kufanya mambo mema na kufuata mienendo ya hao Mitume na Maimamu na baada ya hapo kutafuta uombezi kwa Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwao, hatua hii ya mwisho ni moja kati ya ibada, kwani ni kuonesha namna ya heshima kwao na kujishughulisha nao na kuwa na mapenzi kwao. Hali hii haina athari yoyote ya ushirikina kama wanavyodhani baadhi ya watu, na wala haipingani na Aya nyingine katika Qur’ani tukufu. Kutawasali Katika Qur’ani: Katika Qur’ani kuna Aya mbali mbali zinazoashiria kwa uwazi ya kwamba mtu anapohitaji kitu kwa Mwenyezi Mungu kwa kupitia (kutawasali) kwa mtu mwema hakuna madhara yoyote ya kiitikadi, na kufanya hivyo si kosa. Kwa mfano katika Aya ya 64 ya Sura ya 4, Mwenyezi Mungu anasema: 83
Kitabu kulichotangulia, Uk. 695 172
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 172
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
َ َولَ ْو أَنَّ ُه ْم إ ْذ َظلَ ُموا أَ ْن ُف َس ُه ْم َجا ُء اس َت ْغ َف َر لَ ُه ُم ْ اس َت ْغ َف ُروا اللهََّ َو ْ وك َف ِ ُ الر ُس َّلله َ ول لَ َو َج ُدوا ا َت َّوابًا َر ِحي ًما َّ “Na lau kwamba wao walipojidhulumu wangekujia wakaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu na wakaombewa maghufira na Mtume, wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutakabali toba Mwenye kurehemu.” (Surat An-Nisaa 4:64)
Mfano mwingine, ni pale ndugu zake Nabii Yusuf (a.s.) walipomuendea baba yao; Nabii Yaqub (a.s.) na kumuomba awatakie msamaha kwa Mwenyezi Mungu kutokana na maovu yao, Nabii Yaqub (a.s.) alikubali ombi lao na alilitekeleza, hayo tunayakuta katika Aya ya 97 na 98 ya Sura ya 12, Mwenyezi Mungu anasema:
َ ين َق َ ال َس ْو َ اط ِئ ف ْ َقالُوا َيا أََبا َنا ِ اس َت ْغ ِف ْر لََنا ُذنُو َب َنا إِنَّا ُكنَّا َخ الر ِحي ُم َّ ور ُ أَ ْس َت ْغ ِف ُر لَ ُك ْم َربِّي إِنَّ ُه ُه َو ْال َغ ُف “Wakasema: Ewe baba yetu! Tuombee maghufira kwa dhambi zetu, hakika sisi tulikuwa ni wenye hatia. Akasema: Nitawaombea maghufira kwa Mola Wangu. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Surat Yusuf 12:97-98)
Mfano wa tatu tunaukuta katika Aya ya 114 ya Sura ya 9, pale Nabii Ibrahim (a.s.) alipoahidi kumuombea msamaha baba yake, Mwenyezi Mungu anasema:
َ اهي َم َ َو َما َك ل ِبي ِه إِ اَّل َع ْن َم ْو ِع َد ٍة َو َع َد َها إِيَّا ُه ُ اس ِت ْغ َف ْ ان َ ار إِب ِْر ِ أ ََاهي َم أ َ َفلَ َّما َت َبي ل َّوا ٌه َحلِي ٌم َ َّن لَ ُه أَنَّ ُه َع ُد ٌّو للِهَِّ َت َب َّرأَ ِم ْن ُه إِ َّن إِب ِ ْر “Na haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila ni kwa sababu ya ahadi aliyofanya naye, lakini ilipompambanukia kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye. Hakika Ibrahim alikuwa mpole sana na mnyenyekevu.” (Surat at-Tawba 9:114)
Hii ni baadhi ya mifano michache kati ya mingi iliyomo katika Qur’ani inayothibitisha ya kwamba suala la mtu kutaka kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa msaada wa mtu mwingine halina mushikeli wowote katika mafunzo ya Uislamu. 173
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 173
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
Kutawasali Katika Riwaya: Riwaya mbali mbali zilizopokelewa kwa njia ya Kishia au Kisunni, zinaashiria ya kwamba tawasuli kwa maana tuliyoielezea haina mushkeli wowote, bali inazingatiwa kuwa ni miongoni mwa mambo mazuri. Katika kulithibitisha hili tutajaribu kutaja baadhi ya Riwaya hizo kwa mujibu wa vitabu vya wanachuoni wa Kiahli Sunna, ama kwa upande wa madhehebu ya Kishia hatutolitolea ushahidi, kutokana na umaarufu wake na kutendwa mara kwa mara, na ndio wao wanaoshambuliwa na Waislamu wengine kwa kulitekeleza jambo hili la kutawasali. Katika kitabu Wafaul Wafai cha mwanachuoni maarufu wa Kisunni anayeitwa Samhudiy, ameyasema haya: “Hakika kutafuta msaada na shifaa (maombezi) kwa kupitia kwa Mtume (s.a.w.w.) au kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kutawasali kwa heshima na cheo cha Mtume (s.a.w.w.) ni jambo linalofaa kabla ya kuzaliwa kwake na baada ya kuzaliwa na baada ya kufariki dunia na katika maisha yake ya kaburini na katika Siku ya Kiyama.” Baada ya maneno yake haya, Samhudiy amenukuu Riwaya iliyopokelewa na Umar ibn Khattab, Riwaya hiyo inaelezea namna Nabii Adam (a.s.) alivyotawasali kwa kupitia Mtume (s.a.w.w.), Nabii Adam (a.s.) alifanya hivyo kutokana na maarifa aliyokuwa nayo juu ya ubora na utukufu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambaye atakuja katika zama zijazo, Nabii Adam (a.s.) katika kutawasali alisema maneno yafuatayo:
َّ رب إنّي أسألك ّ بحق محمّد لما غفرت لي “Ewe Mola Wangu! Hakika mimi natawasali kwa haki ya Muhammad kwa yale utakayo nisamehe.”
Baada ya hapo Samhudiy amenukuu Riwaya nyingine iliyopokelewa na wapokezi mashuhuri na makini katika upokezi wao, kama vile An-Nasaiy na At-Tirmidhiy, kama ni dalili ya kuthibitisha kusihi kutawasali kwa Mtume (s.a.w.w.) katika maisha yake. Muhtasari wa tukio hilo ni kwamba, mtu mmoja alimuomba Mtume (s.a.w.w.) amuombee shifaa (ponyo) mgonjwa wake, Mtume (s.a.w.w.) alimuamuru aseme maneno yafuatayo:
الرحمة يا الّله ّم إنّي أسألك ّ نبي ّ ّ وأتوجه إليك بنبيّك مح ّمد توجهت بك إلى ربّي في حاجتي لتقضي لي اللّه ّم ّ مح ّمد إنّي ... اشفعه 174
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 174
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
“Ewe Mola Wangu! Kwa hakika mimi ninakuomba na kukuelekea Wewe kwa kupitia kwa Mtume wako; Muhammad, Mtume wa rehema, ewe Muhammad! Mimi namuelekea Mola Wangu kwa kupitia kwako katika shida yangu ili anikidhie, ewe Mola Wangu mponyeshe yeye (mgonjwa wangu)…”
Baada ya tukio hili Samhudiy anaendelea kuelezea tukio jingine la tatu linaloashiria kujuzu kutawasali kwa Mtume (s.a.w.w.) baada ya kufariki kwake, anasema: “Siku moja katika zama za ukhalifa wa Uthman ibn Affan, mtu mmoja aliyekuwa na shida fulani alikwenda katika kaburi la Mtume (s.a.w.w.) alikaa karibu na kaburi la Mtume (s.a.w.w.) na akaanza kumuomba Mwenyezi Mungu kwa kusoma dua hii:
الرحمة يا الّله ّم إنّي أسألك ّ نبي ّ ّ وأتوجه إليك بنبيّك مح ّمد توجهت بك إلى ربّك أن تقضي حاجتي ّ مح ّمد إنّي “Ewe Mola Wangu! Hakika mimi ninakuomba na kukuelekea Wewe kwa kupitia kwa Mtume Wako; Muhammad, Mtume wa rehema, ewe Muhammad! Mimi namuelekea Mola Wangu kwa kupitia kwako ili anikidhie haja yangu.”
Mara baada ya kusoma dua hii, Samhudiy anaeleza ya kwamba mtu huyo alikidhiwa haja zake.84 Kwa kumalizia tunapenda kunukuu Riwaya isiyo na shaka yoyote hata kwa wafuasi wa madhehebu ya Kiahli Sunna, kwani Riwaya hiyo iko katika kitabu kilicho sahihi zaidi baada ya Qur’ani tukufu, Riwaya hiyo inasimuliwa kutoka kwa Anas bin Malik ya kwamba, pale ambapo watu walisibiwa na ukame mkali Umar bin Khattab alikuwa akitawasali kwa kupitia kwa Abbas ibn Abdul Muttalib, Umar alisema:
نتوسل إليك بنبيّنا صلى اهلل عليه وآله وسلّم ّ الّله ّم إنّا كنّا . فيسقون: قال,نتوسل إليك بع ّم نبيّنا ّ فتسقينا و إنّا “Ewe Mola wangu! Hakika sisi tulikuwa tukitawasali kwako kwa kupitia Mtume wetu (s.a.w.w.) na ukituteremshia mvua, na hivi sasa tunatawasali kwako kwa kupitia ami wa Mtume wako. Anas akasema: Waliteremkiwa na mvua.”85 84 85
Kitabu kilichotangulia Bukhari, Sahihul Bukhariy, Jz.2 Uk.16, Mlango wa Istisqai 175
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 175
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
ANGALIZO: Katika maudhui haya tumeona ni vyema kutoa angalizo kama ifuatavyo: 1.
Tumeelezea ya kwamba kutawasali haimaanishi kutafuta ufumbuzi wa matatizo kutoka kwa Mtume au walii, bali maana yake ni kumfanya Mtume au walii kuwa njia ya kupitishia maombi kwenda kwa Mwenyezi Mungu, ili aweze kuyatatua, kwa ukweli kabisa jambo hili la kutawasali kwa Mitume au Maimamu au mawalii ni kuonesha heshima na mapenzi ya hali ya juu kwa watu hawa walio na utukufu mbele ya Mwenyezi Mungu. Jambo la kushangaza ni kuwepo baadhi ya Waislamu kudai ya kwamba jambo hili ni miongoni mwa mambo ya kishirikina, na ilhali ushirikina ni kuitakidi kuwepo anayeshirikiana na Mwenyezi Mungu katika sifa Zake na vitendo Vyake, na hii tawasuli tunayoizungumza haina mahusiano yeyote na mambo haya.
2.
Wapingaji wa tawasuli hutofautisha baina ya uhai wa Mitume, Maimamu na mawalii wa Mwenyezi Mungu katika maisha haya ya dunia na baada ya kufariki kwao dunia, kwa hivyo hushikilia kutokujuzu kutawasuli hasa kwa watu waliokwisha kutangulia katika haki, lakini kwa mujibu wa mafunzo ya Uislamu kila Mwislamu anatakiwa aitakidi ya kwamba maisha ya wacha Mungu ni mapana na mazuri zaidi baada ya kufariki dunia (maisha ya barzakh) ikilinganishwa na maisha ya hapa duniani, kwa mfano Qur’ani tukufu imeelezea namna maisha ya mashahidi yanavyokuwa baada ya wao kupata shahada, kiasi cha kueleza ya kwamba wao wako hai na si maiti, na watu wanakatazwa kusema wao ni maiti, bali haifai hata kudhania kwamba wao ni maiti, Mwenyezi Mungu anasema:
ُ ُ ٌ يل اللهَِّ أَ ْم َو ل ِك ْن اَل ٰ َ ات َب ْل أَ ْح َيا ٌء َو ِ َو اَل َت ُقولوا لِ َم ْن ي ُْق َتل ِفي َس ِب َ ُر ون ُ َت ْشع “Wala msiseme kwamba wale wanaouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wa hai lakini nyinyi hamtambui.” (2:154).
Amesema tena:
176
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 176
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
ُ ُ َ َو اَل َت ْح َس َب َّن الَّ ِذ يل اللهَِّ أَ ْم َو ًاتا َب ْل أَ ْح َيا ٌء ِع ْن َد ِ ين ق ِتلوا ِفي َس ِب َ ُر َز ُق ون ْ ِّه ْم ي ِ َرب “Na usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa, bali wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa.” (3: 169).
3. Baadhi ya wapingaji wa tawasuli hujaribu kueleza ya kwamba Riwaya zinazojuzisha tawasuli si sahihi, lakini kama tulivyoeleza ni kwamba si tu kwamba kutawasali kumethibiti katika Riwaya na Hadithi sahihi, bali ni jambo lililothibiti katika Qur’aniTukufu, kabla ya hizo Riwaya.
177
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 177
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI NA NNE
ُ ارىٰ أَ ْولَِيا َء َبع َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ْض ُه ْم َص َ َّين آ َمنُوا اَل َتتَّ ِخ ُذوا ْال َيهُو َد َوالن َأ ْض َو َم ْن َي َت َولَّ ُه ْم ِم ْن ُك ْم َفإِنَّ ُه ِم ْن ُه ْم إِ َّن اللهََّ اَل َي ْه ِدي ع ب ء ا ي ل و ُ ْ َ َ ِ ٍ َّ ْال َق ْو َم ُ َّ ُ َ ين َ ٌ َ ار ُع َ َ يه ْم ُس ي ض ر م م ه وب ل ق ي ف ين ذ ال ى ر ت ف م ل ا الظ ْ َ َ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ون ِف ِ ِ ْ َ ْ ْ َ َُي ُقول صي َب َنا َدا ِئ َر ٌة َف َع َسى اللهَُّ أَ ْن َيأ ِت َي ِبال َفت ِح أ ْو ِ ُون َن ْخ َشىٰ أَ ْن ت َ ُص ِب ُحوا َعلَىٰ َما أَ َس ُّروا ِفي أَ ْن ُف ِس ِه ْم َنا ِد ِم ين ْ أَ ْم ٍر ِم ْن ِع ْن ِد ِه َفي ُ َو َي ُق ٰ َين آ َمنُوا أ َ هَ ُؤ اَلءِِ الَّ ِذ َ ول الَّ ِذ ين أَ ْق َس ُموا ِباللهَِّ َج ْه َد أَ ْي َما ِن ِه ْم َ اس ِر ين ْ َإِنَّ ُه ْم لَ َم َع ُك ْم َح ِب َط ْت أَ ْع َمالُ ُه ْم َفأ ِ ص َب ُحوا َخ “Enyi mlioamini! Msiwafanye kuwa marafiki Mayahudi na Manaswara; wao kwa wao ni marafiki. Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu. Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunaogopa yasitusibu majanga. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo Kwake, wakawa wenye kujuta kwa yale waliyoyaficha katika nafsi zao. Na watasema walioamini: Hivi hawa ndio wale walioapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa viapo vyao vigumu, ya kwamba wao wako pamoja nanyi? Zimepomoka amali zao na wamekuwa wenye hasara.” (Qur’ani 5:51-53)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasiri wengi wa Qur’ani wameeleza ya kwamba, baada ya vita vya Badri Ubada ibn Swamit al-Khazrajiy alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumueleza ya kwamba yeye ana marafiki wa Kiyahudi, na anataka kuvunja urafiki na wao kwa vile wanawatishia Waislamu vita, na badala yake anataka kuwa rafiki wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake tu, ama Abdullah bin Abi Farfadh ambaye alikuwa na mafungamano pamoja na Mayahudi alitoa udhuru ya kwamba anachelea kusibiwa na matatizo (iwapo atakata mafungamano na Mayahudi), na akakiri wazi wazi ya kwamba
178
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 178
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
yeye anawahitaji Mayahudi. Mtume (s.a.w.w.) alionesha wasiwasi wake kwa Abdullah juu ya kuendeleza urafiki pamoja na Mayahudi, huku akiashiria ya kwamba urafiki uliopo kati ya Abdullah na Mayahudi ni hatari sana, baada ya Abdullah kuona hali inaendelea hivyo, alitamka wazi ya kwamba ameamua kuacha mafungamano na urafiki kati yake na Mayahudi, hapo ndipo ilipoteremka Aya hii ya mwisho kwa lengo la kuwatahadharisha Waislamu juu ya kuwa na mafungamano kati yao pamoja na Mayahudi na Manasara.86
MAELEZO Aya hizi tatu zinawakemea Waislamu kwa ukali dhidi ya kufanya urafiki na watu wasiokuwa katika Dini yao, Aya ya kwanza inawakataza Waumini kufanya mafungamano na Mayahudi na Manasara na kuwategemea, hii inamaanisha ya kwamba, imani juu ya Mwenyezi Mungu inampelekea mtu kutokuwa na urafiki na Mayahudi na Manasara ikiwa mafungamano hayo yanalenga katika kuudhuru Uislamu na Waislamu, kama Aya ilivyoanza kusema: “Enyi mlioamini! Msiwafanye kuwa marafiki Mayahudi na Manaswara.” Kutokana na sababu ya kuteremka Aya hizi, haimaanishi kutofaa kuwa na mafungamano ya kibiashara kati ya Waislamu na Wasiokuwa Waislamu, bali lililokusudiwa ni kwa Waislamu kukatazwa kuwa na urafiki nao katika mambo yatakayo pelekea kudhoofika Uislamu na Waislamu. Baada ya Mwenyezi Mungu kuwakataza Waumini kutokuwa na mafungamano na wasiokuwa wao, anaelezea sababu ya kutoa katazo hili, anasema: “Wao kwa wao ni marafiki.” Inamaanisha ya kwamba wao Mayahudi na Manasara wao wanajishughulisha zaidi katika kujinufaisha wao wenyewe tu, na wala hawapendi kuwaona wasiokuwa wao wako katika neema. Na Mwislamu yeyote atakayekhalifu amri hii na badala yake kujikurubisha kwao, basi atapata malipo kama watakayoyapata hao Mayahudi na Manasara, kama Aya inavyobainisha kwa kusema: “Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao.” Ni jambo la wazi kabisa ya kwamba Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu na wanaozifanyia khiyana nafsi zao na pia kuwafanyia khiyana Waislamu: “Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” Aya inayofuata inaelezea namna baadhi ya watu walio na ugonjwa katika nafsi zao wakitoa udhuru ili waweze kuendelea kufungamana kiurafiki na wale wasiokuwa katika Dini yao miongoni mwa Mayahudi na Manasara, eti kwa kuchelea masaibu yatakayowapata kutoka kwao iwapo watakata urafiki pamoja nao, Waislamu hao walikuwa wakidhani ya kwamba pindi siku moja Mayahudi na Manasara watakapopata 86
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 4, Uk. 34 179
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 179
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
nguvu na kuwa watawala watawanyanyasa na kuwafanyia kila aina ya dhulma wale waliojitenga nao kwa kukata urafiki. Baada ya Mwenyezi Mungu kulijua hilo lililokuwemo katika nafsi za baadhi ya Waislamu, aliliweka wazi na kulisimulia kwa kusema: “Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunaogopa yasitusibu majanga.” Baada ya udhuru wao huo walioutoa wa kutaka kuendelea kufungamana na wasiokuwa wao kwa kuhofia masaibu yao pindi watakaposhika hatamu za uongozi, Mwenyezi Mungu anawajibu watu hao kwa kuwaambia, hata kama hao Mayahudi na Manasara ndio watakaokuwa watawala na kuendesha serikali, basi Waislamu watawajibika kuvumilia na kusubiri na kuwa na yakini ya kwamba Mwenyezi Mungu atawanusuru na hatimaye mamlaka ya kuendesha serikali yatarudi katika mikono yao, na hapo watajutia kwa yale waliyoyaficha katika vifua vyao (urafiki kati yao na Mayahudi na Manasara), Mwenyezi Mungu anasema: “Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo Kwake, wakawa wenye kujuta kwa yale waliyoyaficha katika nafsi zao.” Kwa hakika jawabu hili la Mwenyezi Mungu kwa watu hawa linabeba mambo mawili: Jambo la kwanza: Ni kawaida ya kwamba fikra kama hizi huwa zinatoka kwa watu walio na ugonjwa katika nafsi zao na ambao imani zao huwa zinalegalega. Watu wa aina hii siku zote huwa wanamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya. Jambo la pili: Ni namna Mwenyezi Mungu alivyokabiliana nao kwa kutumia hoja kama walizozitoa za kutokata mafungamano na watu ambao ni maadui wa Uislamu na Waislamu, kwani dhana yao ya kwamba mamlaka ya dola yatakuwa kwenye mikono ya Mayahudi na Manasara, basi Mwenyezi Mungu anawapa matumaini na hakikisho la wazi ya kwamba mwisho wa yote hayo ushindi pamoja na uongozi wa dola utakuwa katika mikono ya Waislamu, kwa hivyo hakuna sababu ya kuwakumbatia na kuwafanya marafiki Mayahudi na Manasara. Mwisho wa Aya Mwenyezi Mungu anatueleza namna utakavyokuwa mwisho wa wanafiki. Ni pale tu ushindi mnono watakaoupata Waumini, hapo ndipo ukhalisia wa wanafiki utakapobainika. Waumini watasema kwa mshangao mkubwa: Je,watu hawa ndio waliokuwa wakieneza zile propaganda zao kwenu huku wakila yamini ya kwamba wao walikuwa pamoja nasi, basi ni vipi leo hali imefikia hivi! Aya inaweka wazi maneno hayo kwa kusema: “Na watasema walioamini: Hivi hawa ndio wale walioapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa viapo vyao vigumu, ya kwamba wao wako pamoja nanyi? Zimepomoka amali zao na wamekuwa wenye hasara.” Kutokana na unafiki wa watu hawa itakuwa amali zao njema walizozifanya ni zenye kupotea bure, hakuna malipo yoyote watakayoyapata, kwani vitendo vyao
180
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 180
12/8/2014 2:43:41 PM
WITO KWA WAUMINI
hawakuvifanya katika misingi ya ikhlasi na uchamungu, kwa hivyo watakuwa ni wenye kupata hasara ya dunia na ya akhera. Kuwategemea Wageni: Licha ya sababu ya kuteremka Aya hizi zinazowahusisha watu wawili, ambao ni Ubada bin Samit na Abdullah bin Ubayy, lakini Aya hizi hazikomei kwao na yale waliyoyatenda, bali ni kwa sababu ni watu wawili waliokuwa wakibeba fikra mbili tofauti katika jamii, mmoja wao alikuwa akimtaka mwenzake kuachana na mafungamano na watu ambao si wafuasi wa Dini yao ya Kiislamu, na pia alimkataza asiwategemee wao katika maisha yao. Ama fikra ya upande wa pili inaona ya kwamba, kila mtu au kila taifa katika ulimwengu huu uliojaa matatizo na masaibu mbali mbali, inahitajika kwa kila mtu au taifa kuwa na mafungamano na maelewano ya dhati kabisa na watu wengine, na kwa wakati mwingine mahitajio yanaelekea kuomba msaada na kuungwa mkono na wageni, kwani urafiki hauwachi kuwa na faida, na faida hiyo inatarajiwa kuweza kuzaa matunda siku yoyote ile. Qur’ani tukufu imekemea vikali fikra hii ya pili, na kutoa tahadhari kwa Waislamu ili wasije wakatumbukia katika mtego kama huu ambao natija yake ni mbaya na hupelekea majuto yasiyo na kikomo. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba baadhi ya Waislamu wamejisahaulisha katazo hili la Mwenyezi Mungu kupitia katika Kitabu chake kitukufu, na badala yake wamewafanya wageni kuwa ndio tegemeo lao la kisiasa, utamaduni, kielimu, kiulinzi na kiuchumi. Historia inatuonesha ya kwamba sababu kubwa ya Waislamu kudhoofika katika nyanja mbali mbali za maisha ni kukhalifu amri hii na badala yake kufuata mrengo usio sahihi, mfano mzuri ni nchi ya Hispania ambayo ilikuwa katika himaya ya dola ya Kiislamu, lakini leo nchi hiyo sio tu kwamba Waislamu wameikosa, bali ni katika nchi zenye uadui wa wazi dhidi ya Uislamu. Kabla ya nchi hiyo kuanguka katika mikono ya Wakristo, inatuonesha wazi kwamba pale Waislamu walipojitegemea wenyewe katika kila nyanja ni namna gani walivyoweza kujenga utamaduni wa kibinadamu ulioipamba nchi yote ya Hispania na baadhi ya nchi jirani, lakini mambo yaligeuka ghafla baada ya watawala wa Kiislamu kukhalifu maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Na hata leo katika maisha yetu haya tunashuhudia mabalaa na matatizo ya kila aina yanayowasibu Waislamu katika kila kona ya dunia, haya yote ni kwa sababu ya kwenda kinyume na mafunzo ya Uislamu na kuwategemea wageni katika kila kitu. La kushangaza zaidi ni kwamba bado Waislamu hawajazinduka licha ya ukubwa wa matatizo yanayowateremkia siku baada ya siku. Mgeni ni mgeni tu, vyovyote tutakavyoshirikiana naye katika maisha na kusaidiana katika nyanja mbali mbali, 181
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 181
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
kutatokea siku atatuacha mkono, hasa katika wakati tunaohitaji msaada wake zaidi, na lililo baya zaidi ni kuelekeza mashambulizi yake kwetu tena bila ya huruma. Ni juu ya Waislamu kuwa waangalifu zaidi katika zama hizi kwa kuitikia wito ulioko katika Qur’ani tukufu na wala wasimtegemee yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na uwezo wao wa kimaarifa na nguvu ambazo wameruzukiwa na Mola Wao Muumba. Kutokana na tabia hii ya kuwategemea na kuwakumbatia wageni, wamejihisi ya kwamba haiwezekani nchi masikini kuweza kupiga hatua za kimaendeleo bila ya misaada yao, kwa hivyo kila leo wanatoa mashariti magumu kwa nchi hizo masikini, masharti ambayo ni yenye kudhalilisha. Ni hivi karibuni tu tumemsikia Waziri Mkuu wa Uingereza alivyowapa sharti la udhalilishaji viongozi wa nchi masikini, sharti ambalo linawataka viongozi hao wawape uhuru wale wanaotaka kufanya ndoa za jinsia moja, kinyume chake wasitarajie kupata misaada kutoka serikali ya Uingereza! La kusikitisha zaidi ni kwamba chama cha Waziri Mkuu huo, kijulikanacho kwa jina la Conservative ni chama rafiki cha chama cha upinzani hapa Tanzania, na katika uchaguzi wa mwaka 2005 na 2010 kilitoa misaada ya baiskeli, pikipiki, magari na fedha taslimu kwa chama hicho pinzani.87 Sasa hali itakuwajwe iwapo chama hicho kitafanikiwa kuendesha serikali! Mtume (s.a.w.w.) alijishughulisha sana na jambo hili, kiasi ambacho alikataa msaada wa Mayahudi watatu ambao walimueleza Mtume (s.a.w.w.) ya kwamba wao wako tayari kujiunga na Waislamu dhidi ya washirikina katika vita vya Uhud, Mtume (s.a.w.w.) alihofia ya kwamba idadi hii ndogo ya Mayahudi ingeweza kuwaathiri na kusababisha udhaifu katika safu ya Waislamu na kuacha kuwasaidia Waislamu hasa katika wakati ambao watahitaji zaidi msaada wao, na badala yake ni kujiunga katika kundi la maadui wao.
87
Gazeti la Jambo Leo, toleo la Ijumaa, Novemba 4, 2011, Na. 791, Uk. 1 na 5. 182
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 182
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI NA TANO
َُّف َي ْأ ِتي الله َ ين آ َمنُوا َم ْن َي ْر َت َّد ِم ْن ُك ْم َع ْن ِدي ِن ِه َف َس ْو َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ َ ين أَ ِع َّز ٍة َعلَى ْال َكا ِف ِر َ ُحبُّو َن ُه أَ ِذلَّ ٍة َعلَى ْال ُم ْؤ ِم ِن ين ِ ُح ُّب ُه ْم َوي ِ ِب َق ْو ٍم ي ُ يل اللهَِّ َو اَل َي َخ ْ ون لَ ْو َم َة اَل ِئم َ ٰذلِ َك َف َ َ اه ُد ض ُل اف َي ِ ُج ِ ون ِفي َس ِب ٍ ُ اس ٌع َعلِي ٌم إنَّ َما َولِي ْ اللهَِّ ي ُّك ُم اللهَُّ َو َر ُسولُ ُه ِ ُؤ ِتي ِه َم ْن َي َشا ُء َواللهَُّ َو ِ َّ ون ْ الص اَل َة َوي َ ُُؤت َ ين يُ ِقي ُم َ ين آ َمنُوا الَّ ِذ َ َوالَّ ِذ الز َكا َة َو ُه ْم َّ ون َ ُون َو َم ْن َي َت َو َّل اللهََّ َو َر ُسولَ ُه َوالَّ ِذ َ َرا ِكع َِّين آ َمنُوا َفإِ َّن ِح ْز َب الله َ ُه ُم ْال َغالِب ُون “Enyi mlioamini! Atakayeritadi dini yake miongoni mwenu, basi Mwenyezi Mungu atawaleta watu anaowapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa waumini, wenye nguvu juu ya makafiri, wenye kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anayelaumu. Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua. Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui. Na atakayemtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wale walioamini, basi kundi la Mwenyezi Mungu ndio watakaoshinda.” (Qur’ani 5:54-56)
MAELEZO Baada ya kumalizika maudhui ya wanafiki, katika Aya hii Mwenyezi Mungu anatusimulia habari za watu wanaoritadi (wanaoiacha Dini ya Uislamu), Aya hii inatoa onyo na kuelezea yale yatakayomsibu kila Mwislamu atakayeachana na Dini yake ya Uislamu na kufuata dini nyingine, Aya inatoa hakikisho ya kwamba, Mwislamu atakayeritadi asidhanie kufanya kwake hivyo atamdhuru Mwenyezi Mungu, au Waislamu watapata hasara yoyote ile katika Dini yao na maendeleo ya maisha yao, ni kwamba Mwenyezi Mungu amechukua ahadi ya kuleta watu watakaokuwa wahami
183
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 183
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
wazuri wa Dini hii tukufu, Aya inaeleza wazi kwa kusema: “Enyi mlioamini! Atakayeritadi dini yake miongoni mwenu, basi Mwenyezi Mungu atawaleta watu,” Aya haikuishia hapo tu, bali imeelezea sifa za watu ambao watakuwa na majukumu ya kuulinda Uislamu na Waislamu, Aya inaeleza sifa ya kwanza ya watu hao kwa kusema: “Anaowapenda nao wanampenda,” Ni kwamba watu hao hawafikiri isipokuwa kumridhisha Mwenyezi Mungu. Sifa ya pili na ya tatu ya watu hao ni kuonyesha heshima ya hali ya juu na unyenyekevu usio na kifani kwa Waumini wenzao, na wakati huo huo wakiwa ni mashupavu na mashujaa wasiotetereka mbele ya maadui wa Uislamu, kama Aya isemavyo: “Wanyenyekevu kwa waumini, wenye nguvu juu ya makafiri,” Sifa ya tatu: Ni kwamba jambo linalowashughulisha katika vichwa vyao ni kuiona Dini ya Mwenyezi Mungu inapiga hatua mbele: “Wenye kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu,” Sifa yao ya nne: Ni kwamba hawajali na wala hawashughulishwi na baadhi ya maneno yanayotoka kuelekezwa kwao na lawama za hapa na pale katika kutekeleza wajibu wao utokao kwa Mola wao: “Wala hawaogopi lawama ya anayelaumu.” Watu wa aina hii ambao wana uwezo wa kiafya na nguvu za kupambana na adui, pia wanamiliki ujasiri wa kuweza kukabiliana na baadhi ya mila na desturi zisizo sahihi ambazo hutendwa na watu walio wengi katika jamii na kuwafanyia dharau na istihzai wale wanaopambana nazo. Ni wazi katika jamii nyingi kunakuwa na watu wazuri wanaosifika kwa sifa njema, lakini wengi wao wanashindwa kuwa wajasiri wa kuweza kukemea mambo maovu yanayofanywa na watu walio wengi katika jamii zao kwa sababu ya hofu na woga uliowatawala katika nafsi zao, watu wa aina hii kwa haraka hujitenga na jamii na kuwaacha waovu waendelee kufanya ufisadi wao katika jamii, lakini mtu mtengenezaji wa jamii na kizazi chake utamuona ni mwenye ujasiri wa hali ya juu wa kukabiliana na uovu kwa lengo la kuitengeneza jamii. Aya inamalizia kwa kuelezea ya kwamba upatikanaji wa daraja hii tukufu, ni kutokana na ihsani ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, baada ya mwanadamu mwenyewe kukubali kuishi katika kivuli cha Qur’ani, Aya inasema: “Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.” Baada ya Mwenyezi Mungu kuwataka Waumini wasiwafanye marafiki watu wasiokuwa waumini wenzao na kutowafanya wategemezi wa kuwasaidia pindi wafikwapo na shida, kama tulivyoona katika Aya ya 51 ya Sura ya 5, hapa anawaeleza kwa uwazi wale wanaostahiki kufanywa marafiki, viongozi na wategemezi katika maisha yao, Aya inasema: “Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume 184
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 184
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
Wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Bila ya shaka yoyote kwa kila Mwislamu anaamini na kukubali ya kwamba, Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ndiye peke Yake anayestahiki kuabudiwa na kutiiwa katika kila kitu alichokiamrisha na kuachana na yote aliyoyakataza, na kuchukua uongofu na mfumo mzima wa maisha kutoka Kwake, na pia kumtii na kumsikiliza Mtume Wake, kwani Yeye ndiye aliyemtuma. Kumtii Mtume (s.a.w.w.) ni sawasawa na kumtii Mwenyezi Mungu. Jambo lenye utata au lisilojulikana na Waislamu wengi ni kuhusiana na hii nafsi ya tatu ambayo nayo pia inampasa kila Muumini kumtii na kumfuata, kwani kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake itakuwa bado Mwislamu hajafikia ukamilifu wa imani yake, kwani Mwenyezi Mungu alipozungumza kwa kupitia Aya hii alikuwa akiwahutubia Waumini kwa kuwaambia : “Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Ni Akina Nani Hao Walioamini? Bila ya shaka katika kuiangalia ibara hii tunaona kwamba imekuja katika hali ya wingi (Plural form), kama kwamba inatoa nafasi kwa kila ambaye atatoa sadaka wakati anaporukuu. Ukweli wa ibara hii tutaupata pale tu tutakaporudi katika sababu ya kuteremka Aya hii. Wafasiri wengi wameeleza ya kwamba Aya hii iliteremka wakati Imamu Ali ibn Abi Talib (a.s.) alipotoa sadaka ya pete yake wakati alipokuwa amerukuu. Baada ya kuendewa na muombaji aliyekuwa na shida, Imamu Ali (a.s.) alinyoosha mkono wake na yule masikini muombaji aliichukua ile pete, na hapo Aya hii ikamteremkia Mtume (s.a.w.w.)88Ama matumizi ya lugha yaliyotumika hapa, kwa maana ya kuja hali ya wingi lakini mlengwa ni mmoja, jambo hili sio geni katika Qur’ani tukufu, kwa mfano katika Aya ya 173 ya Sura ya 3, Mwenyezi Mungu anasema: “Ambao waliambiwa na watu kwamba watu wamewakusanyikia, basi waogopeni…” Iliposemwa: “Waliambiwa na watu…” Tamko la watu liko katika wingi, lakini aliyesema ni mtu mmoja tu, naye ni Nuaymu ibn Masud. Na kuna Aya nyingi zilizo katika mfumo huu, kwa hapa na tutosheke na Aya hii moja. Tukirudi katika Aya tunayoichambua, pia imekuja katika hali ya wingi lakini mlengwa ni mtu mmoja, ambaye ni Imamu Ali ibn Abi Talib (a.s.). Kwa hivyo basi wa kuwatawalia mambo ya Waumini ni Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w.) na Imamu Ali (a.s.) peke yao, hasa ukizingatia kwamba Aya imeanza kwa neno ‘ Innamaa’ likimaanisha kuwa ni wao tu na asiyekuwa wao hastahiki nafasi hiyo. Kama vile 88
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 4, Uk. 34 185
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 185
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
ambavyo kuna baadhi ya watu wanaotilia shaka juu ya nafasi ya Imamu Ali (a.s.) katika Aya hii kwa misingi ya kilugha, pia wako wanaotia shaka kwa misingi ya unyenyekevu aliokuwa nao Imamu Ali (a.s.) wakati alipokuwa anaswali, miongoni mwa hao ni Fakhru Raziy, anasema: “Ni kwamba Ali (a.s.) alikuwa anajulikana namna alivyokuwa na unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu, hasa wakati anaposwali, kiasi ambacho watu waliitumia nafasi ya kuswali kuweza kumtoa mshale uliokuwa katika mguu wake bila ya kuhisi maumivu, basi ni vipi itawezekana kusikia sauti ya muombaji wakati alipokuwa anaswali?” Jawabu la suala hili ni kama ifuatavyo: Watu wenye msimamo huu wameghafilika ya kwamba, kusikia sauti ya mwenye shida, na Imamu Ali (a.s.) kutaka kumsaidia, si dalili ya mtu kutoka katika unyenyekevu, bali ni miongoni mwa mambo yanayopelekea kuwa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, na Imamu Ali (a.s.) alikuwa akielekeza moyo wake kwa Mwenyezi Mungu bila kufikiria kitu kingine, ni jambo lililo wazi kwamba, kufungamana na viumbe vya Mwenyezi Mungu ndiko kufungamana na Muumba, na kutoa sadaka wakati wa kuswali inazingatiwa kuwa ni kutekeleza ibada ndani ya ibada nyingine, na wala sio kufanya jambo lililo haramu ndani ya ibada. Wapinzani wa Imamu Ali (a.s.) wameonesha upinzani wao mwingine kwa madai ya kwamba neno ‘ Waliyyu’ lililomo katika Aya hii maana yake ni rafiki au mwenye kunusuru. Jawabu la hoja hii ni kwamba, hapa haiwezekani neno hili likawa na maana ya rafiki au mwenye kunusuru, kwa sababu sifa hizi anatakiwa awe nazo kila Mwislamu juu ya Mwislamu mwenzake na wala haziwahusu tu Waumini wanaotoa zaka wakati wanaposwali. Watu hawa hawakuishia hapa, bali wametoa hoja mbalimbali kutaka kuthibitisha ya kwamba Imamu Ali ibn Abi Talib (a.s.) sio mlengwa katika Aya hii. Kwa kutotaka kukuchosha ndugu msomaji wa kitabu chetu hiki nakuomba utosheke na hoja zao hizo, na majibu yetu ni kama tulivyo yabainisha. Aya ya mwisho ambayo inakamilisha maudhui haya, inaweka bayana ya kwamba, nusra na ushindi utakuwa ni wa wale tu ambao wataamua kuwa chini ya uongozi wa Mwenyezi Mungu, Mtume wake (s.a.w.w.) na wale walioamini wakiwa na sifa zilizotajwa katika Aya iliyotangulia, huku Aya ikiwasifu hao ambao wamekubali kuwatii hao, kuwa ni katika kundi la Mwenyezi Mungu wenye kunusuriwa na kushinda milele, Mwenyezi Mungu anasema: “Na atakayemtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wale walioamini, basi kundi la Mwenyezi Mungu ndio watakaoshinda.”
186
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 186
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI NA SITA
َ ين آ َمنُوا اَل َتتَّ ِخ ُذوا الَّ ِذ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين اتَّ َخ ُذوا ِدي َن ُك ْم ُه ُز ًوا َولَ ِعبًا َ ِم َن الَّ ِذ ار أَ ْولَِيا َء َواتَّ ُقوا اللهََّ إِ ْن َ ين أُوتُوا ْال ِك َت َ اب ِم ْن َق ْبلِ ُك ْم َو ْال ُك َّف َ ُك ْنتُ ْم ُم ْؤ ِم ِن َ الص اَل ِة اتَّ َخ ُذ وها ُه ُز ًوا َولَ ِعبًا َذٰلِ َك َّ ين َوإِ َذا َنا َديْتُ ْم إِلَى َ ُِبأَنَّ ُه ْم َق ْو ٌم اَل َي ْع ِقل ون “Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki wale walioifanyia mzaha na mchezo dini yenu katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu na makafiri. Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni waumini. Na mnaponadi Swala, wanaifanyia mzaha na mchezo. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasiokuwa na akili.” (Qur’ani 5: 57-58)
SABABU YA KUTEREMKA Miongoni mwa washirikina wawili waliokuwa wakiitwa Rufaat na Suweid walijifanya wamesilimu kisha walijiunga pamoja na wanafiki, baadhi ya Waislamu walikuwa na usuhuba na watu hao wawili na kuwaonyeshea mapenzi ya hali ya juu, hapo ndipo zilipoteremka Aya hizi mbili zikiwa na lengo la kuwakataza Waislamu na tabia yao ya kuwapenda watu hao wawili. Ama sababu ya kipekee ya kuteremka Aya ya pili, ni pale baadhi ya Mayahudi na Manasara walipokuwa wanasikia sauti ya adhana au kuwaona Waislamu wakiswali walikuwa wakiwafanyia kejeli na mzaha, kwa hivyo Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hii kwa lengo la kuwatahadharisha Waislamu juu ya kuwa na urafiki na mapenzi na watu wa aina hii.89
MAELEZO Mwenyezi Mungu anawaonya waja Wake wema juu ya kuwafanya marafiki wanafiki na maadui wa Uislamu, kama Aya isemavyo: “Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki wale walioifanyia mzaha na mchezo dini yenu katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu na makafiri.” Na katika kutilia mkazo katazo hili, Aya imeendelea kusema: “Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni waumini.” Ikimaani89
Kitabu kilichotangulia, Uk.59 187
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 187
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
sha ya kwamba kuwapenda maadui wa Uislamu hakuendani sambamba na wala hakukubaliani na imani thabiti na uchajimungu. Aya ya pili inaelezea ni endelezo la Aya ya kwanza, kwani nayo inakataza kuwapenda wanafiki na baadhi ya watu waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manasara), ambao walikuwa wakizidhihaki hukumu za Kiislamu na kuzichezea shere, Aya inaashiria moja kati ya hukumu hizo, ambayo ni ibada ya Swala: “Na mnaponadi Swala, wanaifanyia mzaha na mchezo.” Baada ya hapo Aya inaeleza ya kwamba watu walikuwa wanazichezea shere hukumu za Kiislamu kwa sababu ya ujinga wao wa kuikataa haki: “Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasiokuwa na akili.” Adhana ni Alama Kubwa ya Uislamu: Katika kila zama kunakuwa na alama maalumu inayotumika katika kuwaita watu wake na kuwatia ari na shauku katika kutekeleza kile wanachoitiwa, kwa mfano, wakristo hutumia kengele katika kuwaita waumini wao kutekeleza ibada zao. Na Uislamu umeleta adhana kama ni kitu cha kutumiwa katika kuwaita Waislamu katika kutekeleza ibada ya Swala, wito huu unaotumiwa na Waislamu umebainika ya kwamba ni wito ulio na athari nzuri katika nyoyo za watu hata wasiokuwa Waislamu ikilinganishwa na miito ya dini nyingine. Mfasiri mmoja wa Qur’ani ajulikanaye kwa jina la Sayyid Muhammad Ridha, ameandika katika tafsiri yake iitwayo Tafsirul Manaar ya kwamba, baadhi ya wakristo wenye misimamo mikali wakati wanaposikia adhana, hawana budi ila kukiri athari kubwa ya kiroho wanayoipata katika nafsi zao. Mfasiri huyo pia anasema: “Baadhi ya Waislamu waliwashuhudia baadhi ya Wakristo wakisikiliza adhana kati ya moja ya miji ya Misri.”90 Ni wito gani wenye ladha na mvuto, na shauku ya kuusikiliza, kuliko wito huu unaoanza kwa jina la Mwenyezi Mungu na kushuhudia Upweke Wake, na Utume wa Mtume Wake (s.a.w.w.), na kuwaita watu katika mafanikio na kwenye amali njema, na mwisho pia humalizia kwa jina la Mwenyezi Mungu. Ni wito ambao uko katika ibara fupi zilizopangika, lakini zikibeba ujumbe mzito! Kutokana na umuhimu wa adhana, Riwaya mbali mbali zimekuja kusisitiza kwamba kabla ya Swala kusomwe adhana, na kuonesha ubora anaoupata muadhini, anasema Mtume s.a.w.w:
ّ .المؤذنون أطول النّاس أعناقا يوم القيامة “Waadhini ni watu watakaokuwa na shingo ndefu zaidi Siku ya Kiyama.”91 90 91
Kitabu kilichotangulia, Uk.61 Muslim, Sahih Muslim, Jz. 2, Uk. 5, Mlango wa ‘Fadhlul Adhana’ 188
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 188
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
Utukufu huu watakaoupata ni kwa sababu ya wito wao kwa watu kuelekea katika ibada iliyo bora zaidi, kwani sauti ya adhana inayosikika kutoka katika minara ya misikiti ni wito unaotoa uhuru kwa kila anayeuitikia, kwani hukubali kuacha kila jambo lililoko mbele yake, au kuacha kumtumikia mwanadamu na kwenda kusimama mbele ya Mola Muumba wa kila kitu, huku akimwambia: “Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na Wewe tu ndiye tunayekutaka msaada.” Wito huu hutia ghera katika nyoyo za Waumini, huwasababishia hofu maadui wa Uislamu, na pia unazingatiwa kwamba ni nembo na alama ya kubakia Uislamu. Dalili ya haya ni kule kukiri mmoja kati ya watu wa Uingereza ambaye alisimama mbele ya wakristo na kuwaeleza ya kwamba: “Kwa vile jina la Mtume Muhammad (s.a.w.w.) linatajwa katika minara ya kuadhinia, na kwa vile Kaaba ni yenye kubakia, na kwa vile Qur’ani inaelekeza na kutoa mwongozo kwa Waislamu, haitowezekana kuota mizizi ya siasa za Uingereza katika nchi za Waislamu.” Kushuka Wahyi wa Adhana kwa Mtume (s.a.w.w.): Baadhi ya Riwaya zilizonakiliwa katika vitabu vya Kiahli Sunna, zinaelezea visa vya kushangaza juu kushushwa adhana, Riwaya hizo hazinasibiani kabisa na ukhalisia wa namna ya upatikanaji hukumu na sheria katika Dini ya Kiislamu. Riwaya zilizonukuliwa ni kwamba, baada Mtume (s.a.w.w.) kuwauliza na kuwashauri Maswahaba zake juu ya kupatikana njia ya kuwajulisha watu wakati wa Swala, baadhi yao walitoa pendekezo la kupeperushwa bendera maalumu, baadhi walisema pawashwe moto, na baadhi yao walisema papigwe kengele. Mwisho wake ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) hakukubaliana na rai hata moja kati ya hizo. Kilichofuata ni kwamba, Abdullah ibn Zayd na Umar ibn Khattab kila mmoja kati yao alimuona mtu katika ndoto akimuamrisha asome adhana kama ni alama ya kuwafahamisha Waislamu juu ya kuingia wakati wa Swala, na walifundishwa namna ya kuadhini. Baada ya kumsimulia Mtume (s.a.w.w.) alikubaliana nao. Hakika riwaya hii ya kupangwa inamdhalilisha Mtume (s.a.w.w.), kwani inaonesha ya kwamba, badala ya Mtume (s.a.w.w.) kutegemea Wahyi kutoka kwa Mola Wake, anategemea ndoto walioiona Maswahaba wake katika hukumu ya adhana! Ukweli wa suala hili tutaupata katika Riwaya zilizopokelewa kutoka kwa Ahlul Bayt (a.s.), Riwaya hizo zinaonesha ya kwamba asili ya adhana ni Wahyi alioshushiwa Mtume (s.a.w.w.). Imamu Sadiq (a.s.) aliliweka wazi hili kwa kusema: “Wakati Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa ameweka kichwa chake katika mapaja ya Imamu Ali (a.s.), mara aliteremka Jibril na akamfundisha Mtume (s.a.w.w.) namna ya kuadhini na kukimu Swala. Mtume (s.a.w.w.) alinyanyua kichwa chake na kumuuuliza Imam Ali (a.s.) 189
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 189
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
ikiwa amesikia sauti ya adhana ya Jibril. Imamu Ali (a.s.) alijibu kwa kusema: Ndio. Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza mara ya pili ikiwa ameihifadhi, Imamu Ali akajibu: Ndio. Hapo Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Imamu Ali (a.s.) amwite Bilal -ambaye alikuwa ni mtu mwenye sauti nzuri- ili amfundishe Adhana na Iqama. Imamu Ali (a.s.) alimwita Bilal na kumfundisha adhana na iqama.92 - Kwa maelezo zaidi yanayohusiana na maudhui ya adhana na iqama, unaweza kurudia katika kitabu Annasu Wal Ijtihadu cha Sayyid Abdul Husein Sharafu Din, Uk. 128.
92
Hurrul Amiliy, Wasailu Shia, Jz. 4, Uk. 612 190
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 190
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI NA SABA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ات َما أَ َح َّل اللهَُّ لَ ُك ْم َو اَل ِ ين آ َمنُوا اَل تُ َح ِّر ُموا َطيِّ َب َ ُح ُّب ْال ُم ْع َت ِد ين َو ُكلُوا ِم َّما َر َز َق ُك ُم اللهَُّ َح اَل اًل ِ َت ْع َت ُدوا إِ َّن اللهََّ اَل ي َ َُطيِّبًا َواتَّ ُقوا اللهََّ الَّ ِذي أَ ْنتُ ْم ِب ِه ُم ْؤ ِمن اخ ُذ ُك ُم اللهَُّ ِباللَّ ْغ ِو ِ ون اَل يُ َؤ َ ْاخ ُذ ُك ْم ب َما َع َّق ْدتُ ُم أ َ ال ْي َم ارتُ ُه إِ ْط َعا ُم َ ان َف َك َّف ِ ِفي أَ ْي َما ِن ُك ْم َو َٰل ِك ْن يُ َؤ ِ ُ ِون أَ ْهل َ ين ِم ْن أَ ْو َس ِط َما تُ ْط ِع ُم َ َع َش َر ِة َم َسا ِك يك ْم أَ ْو ِك ْس َوتُ ُه ْم أَ ْو َص َيا ُم َث اَل َث ِة أ ار ُة أَ ْي َما ِن ُك ْم ي ُ َت ْح ِر َ َّام َذٰلِ َك َك َّف ِ ير َر َق َب ٍة َف َم ْن لَ ْم َي ِج ْد َف ٍ ُ اح َف ُظوا أَ ْي َما َن ُك ْم َك َذٰلِ َك يُ َبي ِّن اللهَُّ لَ ُك ْم آ َيا ِت ِه لَ َعلَّ ُك ْم ْ إِ َذا َحلَ ْفتُ ْم َو َ َت ْش ُك ُر ون “Enyi mlioamini! Msiharamishe vizuri alivyowahalalishia Mwenyezi Mungu. Wala msipituke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaopituka mipaka. Na kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu vilivyo halali na vizuri; na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye nyinyi mnamwamini. Mwenyezi Mungu hawachukulii kwa viapo vyenu vya upuuzi; lakini anawachukulia kwa mlivyoapa kwa nia. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa wastani wa mnavyowalisha watu wenu, au kuwavisha, au kumwacha huru mtumwa. Na asiyeweza kupata (hayo), basi afunge siku tatu. Hayo ndiyo kafara ya viapo vyenu. Na vichungeni viapo vyenu. Namna hii Mwenyezi Mungu anawabainisha Aya Zake ili mpate kushukuru.” (Qur’ani 5:87-89)
SABABU YA KUTEREMKA Kuna Riwaya mbali mbali zinazoelezea sababu ya kuteremka Aya hizi, miongoni mwa hizo ni Riwaya isemayo: Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisimulia baadhi ya mambo yatakayotokea Siku ya Kiyama, na namna mahakama ya Mwenyezi Mungu itakavyoendesha hukumu. Maelezo haya yaliweza kutingisha baadhi ya nafsi za Waislamu, hata baadhi yao wakawa wanalia, kwa hivyo baadhi ya Mas191
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 191
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
wahaba wakaazimia kuacha baadhi ya starehe halali za kidunia, na badala yake wajishughulishe na ibada tu. Hata Imamu Ali (a.s.) aliapa kwa Mwenyezi Mungu ya kwamba atalala wakati wa usiku kwa muda mdogo sana na wakati uliobakia atafanya ibada. Ama Uthman bin Madh-uni yeye alikusudia kujitenga na mke wake ili ajishughulishe na ibada. Siku moja mke wa Uthman bin Madhu-uni alikwenda kwa Bibi Aisha, alipofika alimuuliza: Ni kwa nini siku hizi hujipambi? Alijibu: Nijipambe kwa ajili ya nani?! Naapa kwa Mwenyezi Mungu, mume wangu hajanikaribia (hajakutana nami kimwili) tangu muda kadha wa kadha, kwani amejitenga nami kwa lengo la kujiweka mbali na starehe za kidunia. Habari hii ilipomfikiaMtume (s.a.w.w.) aliwaendea Maswahaba na kuwaeleza ya kwamba, mwenendo wao huo haukubaliani na mafunzo aliyokuja nayo, na yoyote atakayejiweka mbali na mafunzo yake, basi hatokuwa pamoja naye, baadaye aliwakusanya watu na kuwaambia: “Watu wana nini! Wamejizuia na kulala na wake zao, chakula, vitu vizuri, usingizi na starehe za kidunia. Jueni ya kwamba mimi sikuamrisheni muwe kama makasisi na watawa, kwani si katika Dini yangu kuacha nyama wala wanawake, na kushinda katika mahekalu. Hakika matembezi ya umma wangu ni Swaumu na utawa wao ni Jihadi. Mwabuduni Mwenyezi Mungu na wala msimshirikishe na chochote, nendeni Hijja na fanyeni Umra, na simamisheni Swala, na toeni Zaka na fungeni Ramadhani, na simameni katika njia ya sawa, naye Mwenyezi Mungu atakusimamisheni katika njia hiyo, hakika wameangamia waliokuwa kabla yenu, kwa kujishadidia (kujilazimisha) mambo, basi Mwenyezi Mungu naye akawashadidishia…” Wale watu ambao waliazimia kujilazimisha mambo walisimama na kusema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Tulikula kiapo kwa ajili ya kufanya hayo, sasa tufanyeje?” Hapo ndipo Aya hizi zikateremka kama jawabu la suala lao. Hakuna budi kusema ya kwamba, baadhi ya viapo walivyoapa, kwa mfano kiapo cha Uthaman ibn Madh-uni, ni kiapo kisichokuwa cha kisheria kwa vile kinasababisha madhara makubwa kwa mwanamke, kwani kinamnyima haki zake za kibinadamu. Ama kiapo cha Imamu Ali (a.s.) cha kukesha usiku kwa ibada, jambo lake lilikuwa ni jambo la halali, lakini faida inayopatikana katika Aya ni kwamba, ni vyema kwa mtu asifanye hivyo siku zote na kwa muda mrefu, kiasi cha kuwanyima wengine haki zao za kimsingi.93 93
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 4, Uk. 132 192
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 192
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO Katika Aya hizi kunapatikana hukumu za Kiislamu zilizo muhimu sana. Baadhi yake zimekuja zikiwa ni mara ya kwanza kuwekwa, na nyingine zimekuja kutoa msisitizo wa hukumu za zamani, kwani kama ilivyokuja katika Riwaya mbalimbali ya kwamba Sura hii ni miongoni mwa Sura zilizoteremka mwishoni mwa maisha ya Mtume (s.a.w.w.). Aya ya kwanza inaashiria namna baadhi ya Waislamu walivyokuwa wakijiharamishia baadhi ya neema za Mwenyezi Mungu, kwa hivyo Mwenyezi Mungu aliwakataza jambo hilo kwa kusema: “Enyi mlioamini! Msiharamishe vizuri alivyowahalalishia Mwenyezi Mungu.” Katika kuelezewa hukumu hii na kutakiwa Waislamu wasijiharamishie mambo ambayo ni halali kwao, na yenye manufaa makubwa katika maisha yao, na pia waachane na fikra za ukristo, ambao wakubwa zao wamejinyima haki yao ya kimaumbile ya mtu kuwa na mwenza ili kuweza kukidhi haja za kimwili, kwa hivyo Uislamu umeitangaza hukumu hii kwa kinywa kipana, kupinga utawa na kujiweka mbali na starehe halali za kidunia. Pia ni haramu kwa mtumiaji wa neema hizo za Mwenyezi Mungu kuzitumia kwa fujo kwa kuvuka kiwango kinachotakiwa, kama Aya inavyomalizia kwa kusema: “Wala msipituke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaopituka mipaka.” Aya inayofuata, Mwenyezi Mungu anawataka Waumini kunufaika na neema Zake kwa njia za halali kama anavyosema: “Na kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu vilivyo halali na vizuri.” Jambo la msingi katika kunufaika na neema hizo ni kuzingatia uadilifu na uchaji Mungu: “Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye nyinyi mnamwamini.” Inamaanisha ya kwamba, imani yenu juu ya Mwenyezi Mungu inawalazimuni kuziheshimu sheria za Mwenyezi Mungu na kuzingatia kutotoka katika mipaka yake, hata pale mnapojinufaisha na neema za Mwenyezi Mungu. Pia Aya inatufunza ya kwamba kuharamisha mambo ya halali hakuendani sambamba na uchaji Mungu, kwani uchaji Mungu wa kikweli kweli unampelekea mwanadamu kutoichupa mipaka ya Mwenyezi Mungu katika nyanja zote. Baada ya Aya hii, Aya inayofuata inazungumzia viapo anavyoviapa mwanadamu wakati anapojiharamishia mambo yaliyo halali kwake na katika mambo mengine, hapa tunaweza kusema ya kwamba, viapo viko vya aina mbili: Aina ya kwanza: viapo vya kipuuzi, kama Mwenyezi Mungu anavyosema: “Mwenyezi Mungu hawachukulii kwa viapo vyenu vya upuuzi.” Kiapo cha upuuzi ni kiapo ambacho mtu humtoka bila ya kukusudia kuapa juu ya jambo fulani, bali huwa ni maneno tu yanayomtoka wakati anapozungumza, kama tunavyowashuhudia baadhi ya watu wakisema: Wallahi…, Haki ya Mungu…Pia viapo vya aina hii 193
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 193
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
humtoka wakati mtu anapokuwa katika hali ya hasira na ghadhabu au katika hali ya kulazimishwa. Viapo vya aina hii havina athari yoyote kwa Mwenyezi Mungu, kwa maana mtu hatoadhibiwa ikiwa hatotekeleza lile aliloliapia. Aina ya Pili: Kiapo cha kukusudia, kinachoapwa katika hali ya mazingatio na ufahamu kamili, bila ya kutenzwa nguvu na mtu yoyote. Iwapo mtu hakutekeleza kile alichokiapa, basi atakuwa ni mwenye makosa na mwenye kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu, ikiwa hatoomba msamaha, kama Aya inavyoendelea kusema: “Lakini anawachukulia kwa mlivyoapa kwa nia. Jambo la kuzingatia ni kwamba, makusudio na azma ya hali ya juu katika kuapa haitoshelezi katika kukifanya kiapo kiweze kusihi, bali pia kunahitajika kuapia kitu cha halali, na mtu aape kwa jina la Mwenyezi Mungu peke Yake. Kwa hivyo mtu akiapa kwa jina la Mwenyezi Mungu juu ya kutekeleza jambo lililo halali atalazimika kutoa kafara ikiwa hatotekeleza hilo aliloliapia. – Kafara ya kiapo kisichotekelezwa inapatikana katika Aya hii hii, kafara hiyo ni kufanya moja kati ya mambo matatu: Jambo la Kwanza:Kuwalisha masikini kumi. Katika kuwazuia watu wasitoe kiwango kidogo na aina mbaya ya chakula cha fidia, Aya imebainisha aina na kiwango kinachostahiki: “Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa wastani wa mnavyowalisha watu wenu.” Jambo la Pili: Kuwavisha masikini, Aya inasema: “Au kuwavisha.” Kwa kawaida mavazi yanayotakiwa kuvishwa ni mavazi ya kawaida yanayositiri mwili, kama vile ilivyopokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) katika kuitafsiri Aya hii, alisema ya kwamba ni vipande viwili vya nguo (shati na suruali). Katika suala la nguo pia inapasa iwe ni ya kiwango cha kati na kati kama ilivyo katika chakula. Licha ya hivyo kuna rai inayosema ya kwamba nguo ya aina yoyote inatosheleza iwapo tu itakuwa ni yenye kusitiri mwili, kwa vile Aya haikubainisha sifa ya nguo. Jambo la Tatu: Kuacha huru mtumwa, Aya inasema: “Au kumwacha huru mtumwa.” Katika kumuacha mtumwa huru kuna kauli mbili za wanachuoni. Kauli ya kwanza ni ile inayoshurutisha kumuacha huru mtumwa aliye Mwislamu, na kauli nyingine haishurutishi hivyo, kwa hivyo inafaa kumuacha mtumwa yeyote bila ya kuzingatia imani yake. Kwa ufafanuzi zaidi suala hili limezungumziwa kwa kina katika vitabu vya fiqhi. Lakini kwa vile katika zama zetu hizi hakuna mtu anayeishi katika hali ya utumwa, basi itampasia yule anayestahiki kutoa kafara kuchagua moja kati ya kafara mbili zilizotangulia. Bila ya shaka kafara hizi tatu zinatofautiana sana thamani zake, huenda sheria hii imewekwa ili kila mtu aangalie namna ya hali inavyomruhusu. Pamoja na hivyo kuna watu wasiokuwa na uwezo wa kufanya hata moja kati ya mambo hayo, kwa hivyo Mwenyezi Mungu
194
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 194
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
amewawekea hukumu nyingine, nayo ni kufunga: “Na asiyeweza kupata (hayo), basi afunge siku tatu.” Kwa hivyo funga hii ya siku tatu ni kwa wale tu wasiokuwa na uwezo wa kutekeleza moja kati ya kafara tatu. Baada ya hapo Mwenyezi Mungu anasisitiza juu ya utekelezaji wa hukumu hii kwa kusema: “Hayo ndiyo kafara ya viapo vyenu.” Kwa wale wanaoona ya kwamba baada ya kutoa kafara wanaweza kurudia kukhalifu viapo vyao bila ya wao kuhukumiwa, ni kwamba hali si kama hivyo wanavyodhani, bali Mwenyezi Mungu anawaonya juu ya hilo, na pindi watakaporudia tena watawajibika kutoa kafara na ni jambo la haramu kuacha kutoa kafara, Aya inasema: “Na vichungeni viapo vyenu.” Kwa kumalizia Aya inaweka wazi ya kwamba hukumu zote za Mwenyezi Mungu zinalenga katika kumnufaisha mwanadamu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla, ili waishi maisha ya furaha na amani katika dunia hii, na kupata radhi Zake huko akhera: “Namna hii Mwenyezi Mungu anawabainisha Aya Zake ili mpate kushukuru.”
195
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 195
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI NA NANE
َ ْاب َو أ َ ْْس ُر َو أ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ُ ص ال ْز اَل ُم َ ال ْن ِ ين آ َمنُوا إِنَّ َما ْال َخ ْم ُر َو ْال َمي َ َّ ْ ُاج َت ِنبُو ُه لَ َعلَّ ُك ْم ت َّون إن َ ُري ُد ي ا م ح ل ف ُ ْ ان َف ٌ ِر ْج َ ِ ِ س ِم ْن َع َم ِل الشيْط ِ ِ َ الشي َّ ُ ْط َ ان أَ ْن يُو ِق َع َب ْي َن ُك ُم ْال َع َدا َو َة َو ْال َب ْغ ْس ِر ِ ضا َء ِفي ْال َخ ْم ِر َو ْال َمي َ الص اَل ِة َف َه ْل أَ ْنتُ ْم ُم ْن َته ُون َّ ص َّد ُك ْم َع ْن ِذ ْك ِر اللهَِّ َو َع ِن ُ َو َي َ الر ُس ْ اح َذ ُروا َفإِ ْن َت َولَّيْتُ ْم َف اعلَ ُموا َّ َوأَ ِطيعُوا اللهََّ َوأَ ِطيعُوا ْ ول َو ُ أَنَّ َما َعلَىٰ َر ُسولَِنا ْال َب اَل ُغ ْال ُم ِب ين “Enyi mlioamini! Hakika pombe na kamari na mizimu na mburuga ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni nayo, ili mpate kufaulu. Hakika Shetani anataka kuwaingizia uadui na bughudha baina yenu kwa pombe na kamari na kuwazuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali. Basi je, mtakoma?Na mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na tahadharini. Na mkikengeuka basi jueni kuwa ni juu ya mtume wetu kufikisha (ujumbe) tu waziwazi.” (Qur’ani 5:90-92)
SABABU YA KUTEREMKA Imepokewa kutoka kwa Sa’d ibn Abi Waqqas akisema: “Hakika Aya hii imeteremka kwa sababu yangu. Ni pale mmoja kati ya Answari alipotayarisha chakula na kutualika pamoja na baadhi ya watu, basi walikula chakula na kunywa ulevi, hayo yalitokea kabla ya Uislamu kuharamisha ulevi. Wakati ulevi ulipofika katika vichwa vyao, ikawa kila mmoja anajifakharisha juu ya mwingine, na kila wakati ikawa sauti zao zinapanda juu, mpaka ikafikia hadi mmoja wao akachukua mfupa wa nyumbu na kunipiga nao katika pua yangu. Nilihisi maumivu makali, ndipo niliposimama na kwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na nikamsimulia yale yaliyotokea, hapo ndipo Aya hii ikateremka.” Na katika Musnad Ahmad na Sunanu Abi Daud na Sahih An-Nasai na Sunanu Tirmidhiy, wamesema ya kwamba: “Umar ibn Khattab alikuwa akilewa kupita kiasi, 196
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 196
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
na ikawa anamuomba Mwenyezi Mungu ateremshe hukumu bayana kuhusiana na ulevi, na wakati ilipoteremka Aya 219 ya Suratul Baqara isemayo: “Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake…” Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuwasomea, ikawa bado Umar anakariri dua yake ya kuomba ili ishushwe Aya iliyo wazi zaidi kuhusiana na uharamu wa ulevi, kwa hivyo Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya ya 43 ya Sura ya 4 isemayo: “Enyi mlioamini! Msiikaribie Swala na ilhali mmelewa…” Mtume (s.a.w.w.) aliwasomea Aya hii, lakini bado Umar aliendelea kuomba mpaka pale ilipoteremka Aya hii tunayo ielezea. Aya hii inaweka bayana juu ya uharamu wa ulevi, na baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuwasomea Maswahaba zake, Umar alisema: Tumemaliza, tumemaliza (tumefikia lengo tulilokuwa tunalitaka).94
MAELEZO Awamu za Kuharamishwa Ulevi: Katika Aya ya 43 ya Suratun Nisai Mwenyezi Mungu aliwataka Waumini wasiikaribie Swala ilhali bado wana ulevi katika vichwa vyao. Hii ilikuwa ni awamu ya pili katika kuharamishwa ulevi. Mwenyezi Mungu alitumia ibara hiyo kutokana na tabia ya kunywa ulevi ilivyokithiri katika jamii ya Waarabu katika zama za kijahilia na hata baada ya kuja Uislamu, ilifikia hadi mpaka ikawa inasemwa: Mapenzi ya Waarabu wa kijahilia yalikuwa yako zaidi katika mambo matatu: Mashairi, ulevi na vita. Pia baadhi ya Riwaya zinaashiria ya kwamba, hata baada ya kuharamishwa ulevi, ilikuwa ni jambo zito kwa baadhi ya Waislamu kuachana nao, mpaka ikawa wengine wanasema: “Hatukuharamishiwa kitu kilicho kizito zaidi kwetu kama ilivyo ulevi!”95 Ni wazi kwamba lau kama Uislamu ungetaka kuharamisha janga hili kubwa la ulevi bila ya kutumia njia ya hekima kwa kuzingatia hali ya kijamii ilivyokuwa, basi isingewezekana kutekelezwa jambo hili na ingekuwa ni vigumu kwa watu wengi kuitii amri ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo ukaamua kutumia njia ya kuuharamisha kwa awamu, huku ukiiandaa na kuitayarisha akili kuweza kuipokea amri ya uharamu wake, ili kuweza kuing’oa mizizi ya janga la ulevi katika jamii, kwani ulevi ulikuwa ni ada na tabia iliyokuwa imeota mizizi katika nafsi zao na kutembea katika damu 94 95
Kitabu kilichotangulia, Uk. 139 Suyutiy, Durrul Manthur, Jz. 2, Uk. 315 197
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 197
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
zao. Hatua ya kwanza ya kuharamishwa ulevi ilianzia katika mji wa Makka, pale Mwenyezi Mungu alipobainisha ubaya wa unywaji wa ulevi, anasema:
َ ات النَّ ِخيل َو ُ األ ْع َناب َتتَّ ِخ ًون ِم ْن ُه َس َكراً َور ْزقا َ ذ ِ َو ِمن َث َم َر ِ ِ ِ َ َُح َسناً إِ َّن ِفي َذلِ َك آل َي ًة لَِّق ْو ٍم َي ْع ِقل ون
“Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa wanaotumia akili.” (Qur’ani, Annahli: 67).
Katika Aya hii Mwenyezi Mungu ametaja aina mbili za vitu vinavyopatikana katika mitende na mizabibu: Aina ya kwanza ni ulevi, na aina ya pili ni riziki nzuri, kwa hivyo ulevi ukilinganishwa na riziki nzuri ni ishara ya wazi ya kwamba ni kinywaji kisicho na manufaa katika kiwiliwili cha mwanadamu. Kutokana na kuota mizizi suala la ulevi, ilistahiki kutumika ibara ya aina hii. Licha ya ulevi kuwa ni kinywaji cha kujistareheshea kwa wengi miongoni wa watu wa zama hizo, pia ilikuwa ni kitega uchumi chao kikubwa, na hata pale Waislamu walipohamia katika mji wa Madina, waliendelea na biashara yao hiyo, huko Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya inayoharamisha ulevi, lakini kwa lugha nyepesi, amesema:
ْ َي ْسأَلُو َن َك َعن ْال َخ ْمر َو ْ ْسر ُق ْل ِفيه َما إ َ َّ َ اس لن ل ع ف ا ن م و ير ب ك م ث ي م ال ُ ٌ ٌ َ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ...َوإِ ْث ُم ُه َما أَ ْك َب ُر ِمن نَّ ْف ِع ِه َما “Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake…” (Qur’ani, al-Baqarah: 219).
Aya inaelezea ya kwamba manufaa ya kiuchumi yatokanayo na biashara ya kamari na ulevi ni madogo mno ikilinganishwa na madhara yake, madhara ya ulevi katika jamii ya leo yako wazi zaidi, kwani tunaziona serikali zikitumia pesa nyingi katika kuwatibu raia wao walioathirika kutokana na ulevi kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kama vile walevi kujitumbukiza katika ngono holela na bila ya kutumia hizo kinga walizoziweka wahamasishaji wa zinaa! Pesa za kuwashughulikia watu wa aina hii ni nyingi zaidi kuliko faida inayokusanywa na serikali kutoka katika biashara na viwanda vinavyotengeneza pombe. 198
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 198
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
Licha ya Aya kuelezea ya kwamba manufaa yanayopatikana katika ulevi ni madogo ikilinganishwa na faida, Waislamu waliendelea kutumia ulevi kama starehe yao na wengine kama ni moja ya vyanzo vyao vya kuwaingizia kipato kwa ajili ya maisha yao, hapo ndipo Mwenyezi Mungu akatumia hatua ya tatu ya kuwakataza wale wanaolewa wahakikishe wanakuwa na akili timamu, akili isiochanganyika na ulevi pale wanapotaka kufanya ibada, amesema:
ْ ال َت ْق َرب ْ ُين آ َمن َ الص َ وا َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ارى َحتَّ َى َّ ُوا َ ال َة َوأَنتُ ْم ُس َك ْ َتعْلَ ُم َ ُوا َما َت ُقول ...ون “Enyi mlioamini! Msiikaribie Swala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayoyasema…” (Qur’ani: 4:43)
Mwenyezi Mungu anawaeleza kwa wazi Waislamu ya kwamba wasisimamishe Swala ilhali wamelewa, mpaka pale watakapotambua yale wanayoyasema katika Swala zao. Hii haimaanishi ya kwamba ulevi ulikuwa ni halali, bali ilikuwa unapita katika hatua moja baada ya nyingine katika kuwalea Waislamu na kuwaweka tayari kupokea amri ya kuacha ulevi milele, hapo itakapotoka amri ya mwisho juu ya uharamu wa ulevi, baada ya kuota mizizi katika nafsi zao kwa muda mrefu. Kutokana na tabia hii iliyokuwa imeota mizizi katika nafsi za Waislamu wengi, Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya zenye makatazo ya ulevi kwa kutumia njia mbali mbali, kwa mfano; tukirudi katika Aya hizi tunazozichambua, ameanza kwa kusema:
َ اب َو َ ْس ُر َو ْ ُين آ َمن َ األ ْز َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ُ نص ال ُم َ األ ِ وا إِنَّ َما ْال َخ ْم ُر َو ْال َمي َ َّ َ اج َت ِنبُو ُه لَ َعلَّ ُك ْم تُ ْفلِ ُح ون ْ ان َف ٌ ِر ْج ِ س ِّم ْن َع َم ِل الشيْط “Enyi mlioamini! Hakika pombe na kamari na mizimu na mburuga ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni nayo, ili mpate kufaulu.”
Hapa Mwenyezi Mungu anawaeleza Waumini ya kwamba, kwenda kinyume na yale waliotakiwa kuyatenda au kuyaacha hakuendani sambamba na uhalisia wa imani ya Kiislamu. Na pia ni kwamba Mwenyezi Mungu ameuweka ulevi katika safu ya masanamu ili kuwatanabahisha ya kwamba madhara ya ulevi na kamari 199
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 199
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
hayatofautiani na madhara ya kuabudu masanamu, kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:
.شارب الخمر كعابد الوثن “Mnywaji ulevi ni kama mwenye kuabudu masanamu.”96
Pia katika Aya hii tunajifunza ya kwamba, ulevi, kamari, kuabudu masanamu na kupiga ramli, mambo yote hayo yamezingatiwa kuwa ni uchafu na ni katika mienendo ya shetani. Mwishoni mwa Aya Mwenyezi Mungu anatoa amri ya kujiepusha na mambo hayo machafu, kwa kuleta toba ya kikweli kweli. Aya inamalizia kwa Mwenyezi Mungu kuwaambia Waumini: “ili mpate kufaulu.” Anamaanisha ya kwamba iwapo jamii itaendelea kuyafanya haya mambo maovu, basi jamii hiyo haitokuwa na mafanikio yoyote wala kuwa na ustawi mzuri wa maisha yao. Katika Aya inayofuata inataja baadhi ya madhara ya ulevi na kamari yanayotoka kwa shetani kupitia katika makatazo haya: “Hakika Shetani anataka kuwaingizia uadui na bughudha baina yenu kwa pombe na kamari na kuwazuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali. Basi je, mtakoma?Na mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na tahadharini.” Aya inamalizia kwa ibara isemayo: “Basi je, mtakoma?” Baada ya Mwenyezi Mungu kutoa msisitizo juu ya kuachana na mambo haya maovu, anauliza: Je! Kuna yeyote atakayeweza kutoa sababu ya msingi juu ya faida ya ulevi na kamari. Kutokana uzito na mkazo wa kuharamishwa ulevi kupitia Aya hizi tunamshuhudia Khalifa wa pili; Umar ibn Khatab, ambaye alikuwa ni miongoni mwa wanywaji ulevi – kama wafasiri wa madhehebu ya Kiahli Sunna wanavyoeleza - aliziona Aya zilizopita hazitoshelezi katika kuufanya ulevi kuwa haramu, lakini ilipoteremka Aya hii alisema: “Tumemaliza! Tumemaliza.” Katika kusisitizwa hukumu za uharamu wa mambo haya, Mwenyezi Mungu anawaamrisha Waumini wajipambe na ucha Mungu, kwa kufanya hivyo ndipo watakapoweza kuachana na kila walilokatazwa na kutenda yote waliyoamrishwa, anasema: “Na mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na tahadharini.” Baada ya hapo anatoa ahadi ya kuwaadhibu wale wote wanaokwenda kinyume na maamrisho Yake, na jukumu la Mtume (s.a.w.w.) ni kufikisha tu: “Na mkikengeuka basi jueni kuwa ni juu ya Mtume Wetu kufikisha (ujumbe) tu waziwazi.” Madhara Yatokanayo na Kamari: 96
Shawkaniy, Fat-hul Qadir, Jz.2, Uk. 73 200
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 200
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
Qur’ani tukufu imetaja baadhi ya madhara yanayopatikana katika ulevi, madhara zaidi ya ulevi yanatangazwa katika takwimu mbali mbali hasa katika nchi zilizo na walevi wengi duniani. Kwa mfano katika nchi ya Uingereza, kati ya watu 2249 waliosibiwa na ugonjwa wa akili, ni watu 53 tu kati ya hao waliopatwa na ugonjwa huo kwa njia za kawaida, ama waliobaki wameupata kwa sababu ya ulevi. Katika nchi ya Marekani takwimu zinaonesha ya kwamba asilimia 85 ya wagonjwa wa Kisaikolojia ni kutokana na ulevi. Pia takwimu za nchi hiyo zinasema ya kwamba wagonjwa wa maradhi ya Kisaikolojia ndani ya mwaka mmoja, ni wengi Zaidi, ikilinganishwa na Wamarekani waliokufa katika vita vya pili vya dunia, sababu kubwa ni unywaji pombe na uvutaji sigara. Msomi mmoja wa Uingereza anayejulikana kwa jina la Bentam, anasema: “Unywaji wa ulevi umewafanya watu wa Kaskazini kuwa wapumbavu na umewafanya watu wa Kusini kuwa wendawazimu…, hakika Dini ya Kiislamu inaharamisha aina zote za ulevi, jambo hili ni miongoni mwa mambo yanayoupa hadhi Uislamu.” Katika nchi ya Ufaransa, kila siku watu 440 wanakufa kutokana na unywaji pombe. Nchi ya Uingereza inapoteza mamilioni ya dola kutokana na wafanyakazi wa nchi hiyo kutohudhuria kwa wakati kazini, kutokana na kunywa pombe kupita kiasi. Ama kuhusiana na madhara ya kamari takwimu zinaonesha kama ifuatavyo: Asilimia 30 ya ujambazi, asilimia 90 ya wizi, asilimia 50 ya uzinifu, asilimia 10 ya utovu wa adabu, asilimia 30 ya talaka, asilimia 40 ya kupigana na kujeruhiyana na asilimia 5 ya watu kujiuwa wenyewe, yote haya yanasababishwa na kamari katika nchi ya Marekani.97 Ndugu Muumini haya yanayofanyika leo kwa kupitia mitandao ya simu za mikononi, kwa mteja kutakiwa kuandika neno fulani na kulituma na hatima yake kukatwa kiwango fulani cha pesa, na pesa hizo kupewa baadhi ya watu wanaoitwa washindi, kwa kweli hiyo pia nayo ni kamari, kwa hivyo ni juu yetu kujiepusha nayo ili tusije tukafikwa na hayo yanayowafika wenzetu.
97
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 4, Uk. 141 201
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 201
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THELATHINI NA TISA
ُ الص ْي ِد َت َنالُ ُه أَ ْي ِد َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ يك ْم َّ ين آ َمنُوا لََيبْلُ َونَّ ُك ُم اللهَُّ ِب َش ْي ٍء ِم َن ْ اح ُك ْم لَِيعْلَ َم اللهَُّ َم ْن َي َخ ُاف ُه ب َ ْ ْب َف َم ِن ى َب ْع َد َ ٰذلِ َك َفلَ ُه ٰ اع َت َد ي غ ال ُ َو ِر َم ِ ِ ٌ َع َذ اب أَلِي ٌم “Enyi mlioamini! Hakika Mwenyezi Mungu atawajaribu kwa baadhi ya mawindo yatakayofikiwa na mikono yenu na mikuki yenu, ili Mwenyezi Mungu amjue ni nani anayemwogopa kwa ghaibu. Basi atakayeruka mipaka baada ya hayo, atapata adhabu iumizayo.” (Qur’ani 5:94)
SABABU YA KUTEREMKA: Katika mwaka ambao ilipatikana sulhu ya Hudaybiya, Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Maswahaba wake walikusudia kufanya ibada ya Umrah. Wakati walipokuwa tayari wameshahirimia ibada hiyo na kuelekea katika mji wa Makka, waliwakuta wanyama wengi wa porini, kutokana na wingi wa wanyama hao baadhi yao walikuwa wakipita karibu na mahema ya Waislamu, walikuwa na uwezo wa kuwawinda kwa mikuki na hata kwa kuwakamata kwa mikono yao. Kwa hivyo Aya hii iliteremka kwa lengo la kuwatahadharisha Waislamu juu ya uwindaji wa wanyama baada ya wao kuwa katika ihramu, na hiyo idadi kubwa ya wanyama wanayoiona ni mtihani kwao. Hukumu za Uwindaji wakati wa Ihramu: Aya hii inaelezea hukumu ya uwindaji wa wanyama wa nchi kavu na wale wanaoishi katika maji kwa mtu ambaye tayari ameshahirimia ibada ya Hijja au Umra. Aya inaeleza yale ambayo yatatokea katika kitongoji cha Hudaybiya, jambo ambalo si la kawaida la kuonekana wanyama wa porini kwa wingi na kuwa karibu na wanadamu, hakika jambo hilo lilikuwa ni mtihani mzito kwao, hasa ikizingatiwa ni namna gani Waislamu hao walivyokuwa na haja ya nyama za wanyama hao, hakika kuzuiliwa wanyama hao katika mazingira waliokuwa nayo ilikuwa ni mtihani mkubwa sana kwao. 202
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 202
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
Katika kusisitizwa hukumu ya uharamu wa jambo hili, Aya inaendelea kusema: “Ili Mwenyezi Mungu amjue ni nani anayemwogopa kwa ghaibu.” Katika ibara hii haimaanishi ya kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa hajui yale yaliyomo katika nyoyo za watu, la hashaa! Na alitaka kutambua kwa njia ya mtihani! Bali alitaka kuyadhihirisha kwa watu yale yaliyomo katika nyoyo za watu wengine baada ya Yeye kuyatambua vyema, kwani si jambo la haki kuwaadhibu watu kwa mujibu wa nia zao na yale yaliyomo vifuani mwao, bali inapasa yadhihirike kwa matendo yao ili hoja ipate kusimama. Aya inamalizia kwa kusema: “Basi atakayepituka mipaka baada ya hayo, atapata adhabu iumizayo.” Hii ni dalili ya wazi ya kwamba kila mwenye kutenda katazo alilolikataza Mwenyezi Mungu ni kuonesha dharau na kejeli juu ya sheria Zake, na hakuna malipo atakayoyapata ila ni adhabu yenye kuumiza.
203
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 203
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ الص ْي َد َوأَ ْنتُ ْم ُح ُر ٌم َو َم ْن َق َتلَ ُه ِم ْن ُك ْم َّ ين آ َمنُوا اَل َت ْقتُلُوا ُم َت َع ِّم ًدا َف َج َزا ٌء ِم ْث ُل َما َق َت َل ِم َن النَّ َع ِم َي ْح ُك ُم ِب ِه َذ َوا َع ْد ٍل ِم ْن ُك ْم َ ار ٌة َط َعا ُم َم َسا ِك ص َيا ًما َ َه ْديًا َبالِ َغ ْال َك ْع َب ِة أَ ْو َك َّف ِ ين أَ ْو َع ْد ُل َذٰلِ َك َ وق َو َب َ لَِي ُذ َ َال أَ ْم ِر ِه َع َفا اللهَُّ َع َّما َسل ف َو َم ْن َعا َد َف َي ْن َت ِق ُم اللهَُّ ِم ْن ُه َ يز ُذو ا ْن ِت ٌ َواللهَُّ َعز ً ص ْي ُد ْال َب ْح ِر َو َط َعا ُم ُه َم َت اعا لَ ُك ْم ق َ ام أُ ِح َّل لَ ُك ْم ِ ٍ ْ َّلله ُ َّار ِة َو ُح ِّر َم َعلَي َ ص ْي ُد ال َب ِّر َما ُد ْمتُ ْم ُح ُر ًما َواتَّ ُقوا ا َّ َِول َ لسي َ ْك ْم َ الَّ ِذي إِلَ ْي ِه تُ ْح َش ُر ون “Enyi Mlioamini! Msiue windo na hali mko katika Ihram. Na miongoni mwenu atakayemuua kwa kusudi, basi malipo (yake) yatakuwa ni mfano wa aliyemuua katika wanyama wa kufugwa, kama watavyohukumu waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama apelekwe Al-Kaaba (kama sadaka); au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; au badala ya hayo ni kufunga; ili aonje ubaya wa jambo lake. Mwenyezi Mungu amekwisha yasamehe yaliyopita; na atakayerudia, Mwenyezi Mungu atampa adhabu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu Mwenye kuadhibu. Mmehalalishiwa kuvua baharini na chakula chake, kwa manufaa yenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa kuwinda bara maadamu mko katika Ihram. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye Kwake mtakusanywa.” (Qur’ani 5:95-96).
Aya hizi ni mtiririko wa Aya iliyopita, sababu ya kuteremka kwao ni moja. Aya ya kwanza katika kifungu cha Aya hizi inatoa hukumu ya wazi zaidi na ya mkato juu ya uharamu wa uwindaji baada ya mtu kuhirimia ibada ya Hijja au Umrah ikilinganishwa na Aya iliyopita, inasema: “Enyi Mlioamini! Msiue windo na hali mko katika Ihram.” Kuna suala linalojitokeza kwa wanachuoni wa Kiislamu, suala hilo ni hili, je uharamu wa uwindaji wa wanyama unawajumuisha wanyama wote; wanaoliwa na wasioliwa, au ni kwa wale wanaoliwa tu? Kuna tofauti ya jawabu katika suala hili, kwa upande wa wanachuoni wa madhehebu ya Ahlu Sunna, kwa mfano, Abu Hanifa, yeye anasema: “Inawajumuisha wanyama wote.” Na Imamu
204
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 204
12/8/2014 2:43:42 PM
WITO KWA WAUMINI
Shafi anasema: “Ni kwa wale wanyama wanaoliwa tu.” Ama wanachuoni wote wa madhehebu ya Ahlul Bayti (a.s.) wamekubaliana kwa kauli moja ya kwamba hukumu hii inawajumuisha wanyama wote. Kwani katika kuwinda kunakuwa na malengo tofauti, wako wanaowinda kwa ajili ya nyama au kwa ajili ya kupata ngozi zao au kwa ajili ya kujikinga na shari zao. Licha ya yote hayo jambo la kuzingatia katika hukumu hii ni kwamba wanyama walioharamu kuwindwa ni wale wanyama wa porini tu, kwani wanyama wa kufugwa huwa hawawindwi. Baada ya hapo Aya inataja hukumu ya kafara kwa mtu atakayewinda hali yuko katika ihramu ya Hijja au Umra, inasema: “Na miongoni mwenu atakayemuua kwa kusudi, basi malipo (yake) yatakuwa ni mfano wa aliyemuua katika wanyama wa kufugwa,” Usawa unaokusudiwa katika Aya hii ni usawa wa maumbile na sio usawa wa thamani, kwa mfano iwapo mtu atawinda swala atalazimika kutoa fidia ya mbuzi, na iwapo kutatokea tatizo la kujulikana usawa unaofanana na myama aliyewindwa, basi hapo itapasa watafutwe watu wawili waadilifu ili wote kwa pamoja wathibitishe ni mnyama gani analingana naye: “Kama watavyohukumu waadilifu wawili miongoni mwenu.” Ama kuhusiana na pahala panapostahiki kuchinjwa huyo mnyama wa kafara, Aya inatubainishia hilo kwa kusema: “Mnyama apelekwe Al-Kaaba (kama sadaka).” Jambo lililo mashuhuri kwa wanachuoni wetu ni kwamba, mnyama wa kafara kwa aliyewinda wakati wa ibada ya Umra anatakiwa achinjwe Makka, ama wa ibada ya Hijja anatakiwa achinjwe Mina, hukumu hii haiyendi kinyume kabisa na Aya, kwani Aya hii iliteremka kuhusiana na ihramu ya Umra kama tulivyoona. Aya inaendelea kuelezea hukumu ya kafara, inasema ya kwamba sio lazima iwe ni kuchinja mnyama, bali anaweza kuchagua moja kati ya mambo mengine mawili: “au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; au badala ya hayo ni kufunga.” Licha ya Aya kutoeleza idadi ya masikini wanaostahiki kulishwa wala idadi ya siku zinazotakiwa kufungwa, kwa hakika hukumu hizi mbili kuwepo pamoja na kule kutajwa idadi ya masiku ya kufunga katika hukumu nyingine, ni jambo la wazi ya kwamba ulishaji wa masikini halikuachwa kwa kila mtu aamue idadi aipendayo, wala kufunga siku atakazo, bali hukumu hizi zinatakiwa zitekelezwe kwa mujibu wa thamani ya mnyama anayestahiki kuchinjwa. Ama namna ya kulinganisha kati ya kufunga na kulisha masikini, Riwaya zinatufunza ya kwamba kila kibaba kimoja (gramu 750) cha nafaka inayotumika zaidi alishwe masikini mmoja na kwa idadi hiyo hiyo ya kibaba kimoja itakuwa ndio saumu ya siku moja. Riwaya nyingine zinaashiria ya kwamba kila vibaba viwili vya chakula itakuwa funga ya siku moja. Maelezo zaidi ya hukumu hii ni vyema kurudi katika vitabu vya fiqhi.
205
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 205
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
Suala jingine linalojitokeza ni kwamba, iwapo mtu atatenda kosa la kuwinda, anaruhusiwa kuchagua moja kati ya kafara hizi tatu, au atalazimika afuate utaratibu huu uliotajwa, kwa kuanza na kuchinja, ikiwa hana uwezo alishe masikini, na akishindwa afunge?Wanachuoni wametofautiana juu ya hukumu hii, lakini dhahiri ya Aya inaonesha juu ya mtu kuwa na haki ya kuchagua kafara ya kuifanya.98 Aya imetaja lengo la kafara hizi kwa kusema: “…ili aonje ubaya wa jambo lake.” Mwenyezi Mungu hatomwadhibu mtu iwapo alitenda jambo lolote ovu kabla ya kushusha Aya ya kulikataza: “Mwenyezi Mungu amekwisha yasamehe yaliyopita.” Ama yule ambaye anatambua uharamu wa uwindaji, lakini kwa ufedhuli na jeuri akathubutu kufanya hivyo na akakataa kutoa kafara au akawa anarudia kosa hilo mara kwa mara na kila anaporudia hutoa kafara, basi mtu wa aina hiyo atakuwa ameiweka pabaya nafsi yake: “Na atakayerudia, Mwenyezi Mungu atampa adhabu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu Mwenye kuadhibu.” Baada ya kuelezwa uharamu wa kuwinda wanyama pori, Aya inayofuata inaelezea hukumu ya uwindaji wa wanyama wa baharini: “Mmehalalishiwa kuvua baharini na chakula chake,” Baadhi ya wafasiri wametafsiri ya kwamba aina hii ya wanyama wa baharini ni wale samaki waliokufa na kuelea juu ya maji. Kauli hii inapingwa na Sheikh Makarimu Shiraziy, kwa kusema: “Hakika samaki wa aina hii ni haramu, licha ya kuwepo baadhi ya riwaya zilizopokelewa na Ahlu Sunna juu ya uhalali wake.” Sheikh anaelezea uhalali wa samaki unavyopatikana: “Makusudio ya dhahiri ya Aya hii ni kwamba, chakula ni kile kitu kinachoandaliwa kutokana na samaki waliovuliwa, kwani Aya inalenga katika kuhalalisha mambo mawili: Kwanza ni kuwinda, na pili, ni chakula kitokanacho na mawindo. Na kwa mnasaba huu, ndio kukawa na Fatwa mashuhuri za wanachuoni wa madhehebu ya Ahlul Bayt (a.s.) zinazotegemea maana hii, kutokana na yale yanayohusiana na kuwinda wanyama wa ardhini, kwani uwindaji huu sio tu wenyewe ni haramu, bali hata nyama yake pia ni haramu.”99Baada ya hapo Aya inandelea kwa kusema: “Kwa manufaa yenu na kwa wasafiri.” Yaani msisumbuke kutokana na kuzuiliwa nyama ya kuwindwa nchi kavu, ili kuzuia usumbuvu, ni halali kwenu kula wanyama waliovuliwa baharini hata kama muko katika mavazi ya Ihramu. Licha ya uhalali huu, haimaanishi ya kwamba kila kinachovuliwa kwenye maji (baharini na kwingineko) ni halali kuliwa, kwani Aya haikuja kuelezea uhalali wa wanyama waishio kwenye maji, bali inalenga juu ya uhalali wa kuvua kwenye maji 98 99
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.4, Uk.153 Kitabu kilichotangulia, Uk. 153 206
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 206
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
na kinachovuliwa, kwa sharti kiwe ni halali kuliwa tokea mwanzo, kwani pia si kila kinachowindwa nchi kavu kinakuwa na uasili wa uharamu. Katika kusisitiza uharamu wa kuwinda nchi kavu, Aya imerudia kwa mara ya pili kulieleza hilo: “Na mmeharamishiwa kuwinda bara maadamu mko katika Ihram.” Na katika kusisitiza juu ya umuhimu wa kufuata sheria zote zilizotangulia kutajwa, Aya inahitimisha kwa kusema: “Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye Kwake mtakusanywa.” Hekima Ya Kuharamishwa Kuwinda: Ni wazi kwamba ibada ya Hijja na Umrah ni miongoni mwa ibada ambazo zinamtenganisha mwanadamu na ulimwengu wa kimaada, na badala yake kumchukua kwenye ulimwengu wa kiroho, kwani humkataza kuingia katika mijadala isio na faida, kukutana kimwili kwa wanandoa, kujipamba na kadhalika, haya yote yanalengo la kumlea mwanadamu ili afikie katika ukamilifu unaotakiwa. Na pia lau kama ingeruhusiwa kwa watu wanaofanya ziara katika mji huo mtakatifu kuwinda, basi wanyama hao wangemalizika, kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoingia humo kila siku. Uharamu huu unalengo la kulinda mazingira ya mji huo, kwani pia ni haramu kwa watu hao kukata mti na matawi yake. Si tu ni haramu kuwinda, bali hata kumuonesha mwindaji mnyama au sehemu wanapopatikana wanyama, kama Imamu as-Sadiq (a.s.) anavyotufunza kwa kusema pale alipomkataza mmoja kati ya wafuasi wake:
ّ الصيد وأنت حرام وال أنت حالل في ال ّ تستحلن شيئا من ّ وال تدلّ ّن وال ا,الحرم محل محرما فيصطاده وال تشير إليه ّ ّ فيستحل من أجلك .فإن فيه فداء لمن تع ّمده “Usijihalalishie uwindaji pale unapokuwa ni haramu kwako (unapokuwa katika ihramu ya Hijja au Umrah) na wala pale inapokuwa ni halali kufanya hivyo wakati unapokuwa katika Haramu (Mji wa Makka), na wala usimuoneshe anayeruhusiwa kuwinda na wala asiyeruhusiwa ili asije akawinda kutokana na wewe kumuonyesha, kwani kuna fidia kwa mwenye kufanya hivyo kwa makusudi.”100
100
Al-Kulayniy, Usulul Al-Kafiy, Jz. 4, Uk. 381 207
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 207
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI NA MOJA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين آ َمنُوا اَل َت ْسأَلُوا َع ْن أَ ْش َيا َء إِ ْن تُ ْب َد لَ ُك ْم َت ُس ْؤ ُك ْم َُّآن تُ ْب َد لَ ُك ْم َع َفا اللهَُّ َع ْن َها َوالله ُ ين يُ َن َّز ُل ْال ُق ْر َ َوإِ ْن َت ْسأَلُوا َع ْن َها ِح َ ص َب ُحوا ِب َها َكا ِف ِر ين ٌ َغ ُف ْ َور َحلِي ٌم َق ْد َسأَلَ َها َق ْو ٌم ِم ْن َق ْبلِ ُك ْم ثُ َّم أ “Enyi Mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatawachukiza. Na mnapoyauliza inapoteremshwa Qur’ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu ameyasamehe hayo; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mpole. Waliyauliza watu waliokuwa kabla yenu kisha wakawa makafiri kwayo.” (Qur’ani 5:101-102)
SABABU YA KUTEREMKA Sababu ya kuteremshwa Aya hizi mbili zinatofautiana kama ilivyo katika vitabu vya Hadithi na vya tafsiri ya Qur’ani, lakini sababu inayonasibiana zaidi na uteremshwaji wa Aya mbili hizi ni vile ilivyonakiliwa na mfasiri At-Tabarasiy katika kitabu chake kijulikanacho kwa jina la Majma’ul Bayaan, anasema: Kutoka kwa Imamu Ali (a.s.) alisema: Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anawakhutubia Maswahaba zake kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhishia ibada ya Hijja.” Hapo Ukasha ibn Muhswin, katika mapokezi mengine pamesemwa kuwa alikuwa ni Suraqa ibn Malik, akauliza: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Je, wajibu huo wa kuhiji ni kila mwaka? Mtume (s.a.w.w.) hakumjibu, huku akirudia kuuliza kwa mara mbili au tatu. Baada ya hapo Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Una nini? Ni vipi umejiamini, lau ningesema ndiyo, naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu lau ningesema ndiyo basi ingewajibishwa, na iwapo ingewajibishwa msingeweza. Na iwapo mngeacha kufanya hivyo (kuhiji kila mwaka) mngekufuru, basi niacheni (kuniuliza) kama mimi nilivyoacha, kwani wameangamia wale waliokuwepo kabla yenu kutokana na kuuliza sana na kuzozana na Mitume wao, basi ninapokuamrisheni jambo, lifanyeni kwa kadiri ya uwezo wenu, na pia ninapokukatazeni jambo basi jiepusheni nalo.”101 Licha ya sababu hii iliyopelekea kuteremshwa kwa Aya hizi mbili, inafaa izingatiwe ya kwamba mtu asije akadhani ya kwamba Qur’ani inafunga mlango 101
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 4, Uk. 163 208
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 208
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
wa mtu kuuliza au kuhoji juu ya jambo kwa minajili ya kutaka kufahamu, kwani Qur’ani kwa uwazi kabisa inawaamuru watu kurejea kwa watambuzi wa mambo kwa kuwauliza ili watanue maarifa yao, Mwenyezi Mungu anasema: “Basi waulizeni wajuao ikiwa nyinyi hamujui.” Bali katazo linalokusudiwa katika Aya hizi ni kuuliza masuala yasiyo na faida kwa muulizaji, au kuuliza kwa lengo la kubishana, au kuuliza kwa ajili ya kuwafanya wasikilizaji waachane na fikra za muongeaji na badala yake waunge mkono fikra za muulizaji.
MAELEZO Maswali ya Ziada: Bila ya shaka swali ni ufunguo wa elimu na maarifa, hivyo basi mchache wa kuuliza anakuwa na uchache wa elimu, kwa hivyo Qur’ani Tukufu pamoja na Hadithi mbali mbali vinawahimiza watu na kutoa uhuru wa kuuliza wasiyoyajua. Lakini hakuna uhuru usio na mipaka, kwani suala la kuuliza nalo lina mipaka yake, ikizingatiwa ya kwamba kufichikana kwa baadhi ya mambo kuna manufaa makubwa zaidi kwa jamii. Kwa hivyo katika mambo kama haya si vyema kwa mtu kung’ang’ania kuuliza ili kutaka kujua undani wake. Hali kama hii huwa tunaishi nayo katika maisha yetu, kwa mfano, madaktari wengi wanaonelea bora kumficha mgonjwa baadhi ya magonjwa sugu na yanayohatarisha maisha yake, na badala yake huwapa habari ndugu zake kwa sharti wasimueleze mgonjwa wao. Kutokana na uzoefu imethibitika ya kwamba iwapo mgonjwa atajua kinachomsibu, itakuwa ni sababu ya kuchelewa kupata nafuu kutokana na khofu kubwa inayomtawala baada ya kutambua ukubwa wa tatizo lake. Vilevile ikiwa ugojwa wake si mkubwa, basi ni bora kwa mgonjwa asimuulize daktari masuala mengi,kwani kwa kufanya hivyo huenda daktari akakasirika na kutoa majibu yasiyo na faida kwa mgojwa. Pia katika maisha ya watu kwa ujumla, ni vyema watu wakadhaniana dhana nzuri kati yao ili kuepusha kuuliza mambo mengi dhidi yao, mambo ambayo lau watakuwa hawatambui itakuwa ni bora kwao kuliko kuyatambua, kwani kila mtu ana mapungufu yake, na iwapo mapungufu ya watu wengine yatawekwa bayana, basi itakuwa ni sababu ya kutoelewana na kutosaidiana kati yao, kwani huenda ikawa mtu katika jamii yake ni mwenye hadhi fulani, lakini kasoro zake zinapobainika hupoteza hadhi yake kwa haraka sana. Kwa hivyo inampasa kwa kila mtu kuacha kufuatilia maisha ya watu kwa kuuliza hiki na kile katika mambo yasiyo na faida yoyote. 209
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 209
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
Bila ya shaka katika mipangilio na mikakati mbali mbali ya kijamii mambo yanahitaji kuwa siri mpaka pale yatakapofikia kikomo cha kukamilika kwake, kinyume chake ni kwamba, ikiwa yatafichuka kabla ya kukamilika, basi itakuwa ni sababu ya kuchelewa kukamilika au kutokamilika kabisa. Hii ni baadhi tu ya mifano ya yale mambo ambayo inawapasa watu wasishikilie kutaka kuyajua, kwa hivyo ni juu ya viongozi wa nyanja mbalimbali kutokudhihirisha baadhi ya mambo iwapo hakuna shinikizo kali la kupelekea kufanya hivyo, kutokana na sababu hii ndio Qur’ani ikaja na amri hii inayosema: “Enyi Mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatawachukiza.” Lakini kutokana na baadhi ya watu kung’ang’ania kuuliza na kukosa jawabu ya masuala yao, huenda ikapelekea shaka kwa baadhi ya watu, na hasara ikawa ni kubwa zaidi kuliko faida. Kutokana na Qur’ani kutambua vyema hali hii ndio maana ikasema: “Na mnapoyauliza, inapoteremshwa Qur’ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu ameyasamehe hayo; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mpole.” Ama hukusu huo uzito unaotarajiwa kupatikana wakati Qur’ani inateremka ni kwa sababu ya kuuliza mambo ambayo yalikuwa yaelezwe ufafanuzi wake kwa kupitia njia ya Wahyi (Qur’ani). Na watu wanatakiwa wasidhanie ya kwamba Mwenyezi Mungu ameghafilika pindi anapoacha kuelezea baadhi ya mambo, na kutokana na huruma Yake kwa waja Wake ni kwamba amewasamehe kutokana na hayo waliyoyatenda. Imamu Ali (a.s.) anasema:
ّ وح ّدد لكم,إن اهلل افترض عليكم فرائض فال تضيّعوها وسكت, ونهى عن أشياء فال تنتهكوها,حدودا فال تعتدوها .لكم أشياءولم يدعها نسيانا فال تتكلّفوها “Hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhishia mambo yaliyo lazima kuyatenda, basi msiyaache, na amekuwekeeni mipaka (sheria), basi msiichupe, na amekukatazeni mambo, basi msiyatende, na amenyamazia baadhi ya mambo, basi msijikalifishe nayo.”102
Aya inayofuatia inaeleza uzito anaoweza kuupata mtu anayeng’ang’ania kuuliza hata kama mwenye kuulizwa atajizuia kutoa jawabu kwa kulinda maslahi ya muulizaji, lakini iwapo muulizwaji atalazimika kujibu baada ya shinikizo la muulizaji, hapo muulizaji atakuwa amejifunga na atalazimika kutekeleza kwa mujibu wa maswali yake. Hali kama hii inabainishwa na Qur’ani kwa kule kuwepo watu waliouliza 102
Ibn Abil Hadid, Sharhu Nahjul Balghah, Jz.18, Uk.268 210
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 210
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
na baada ya kupatiwa majawabu ya maswali yao waliyapinga na kuasi, Mwenyezi Mungu anasema: “Waliyauliza watu waliokuwa kabla yenu kisha wakawa makafiri kwayo.” Wafasiri wa Qur’ani wana kauli mbali mbali kuhusiana na hao watu waliouliza, baadhi ya wafasiri wanasema Aya hii inawahusu wanafunzi wa Nabii Isa (a.s.) pale walipoomba wateremshiwe chakula kutoka mbinguni, na kilipoteremshwa waliasi. Na wengine wanasema inawahusu watu wa Nabii Saleh (a.s.) pale walipotaka miujiza mbalimbali kutoka kwake. Kwa kweli kauli hizi hazioani na Aya hizi kwani lililokatazwa hapa ni kuuliza kwa kutaka kujua yaliyofichikana na sio maombi. Huenda kauli sahihi ikawa ni ile inayowahusisha wana wa Israili pale walipotakiwa kuchinja ng’ombe ili kupata ushahidi wa mtu aliyefanya tendo la mauwaji. Tunawashuhudia watu hao namna walivyokuwa wakimuelekezea Nabii Musa (a.s.) maswali mengi yanayohusiana na huyo ng’ombe, wakati ilikuwa inatosha kuchukua ng’ombe yoyote na kumchinja, lakini kutokana na maswali yao ya mara kwa mara iliwalazimu kupoteza juhudi na mali nyingi katika kumpata ng’ombe mwenye sifa zilizotajwa kutokana na maswali yao, kwani haikuwa rahisi kupatikana, kiasi cha kufikia hali ya kutotekeleza walichotakiwa kukifanya. Katika tamko lake Mwenyezi Mungu lisemalo: “kisha wakawa makafiri kwayo.” Kuna kauli mbili kuhusiana na ibara hii: Kauli ya Kwanza: Makusudio ya ukafiri ni kuasi sheria za Mwenyezi Mungu. Kauli ya Pili: Makusudio ya ukafiri ni kutokuwa na imani juu ya moja au zaidi kati ya misingi mitano ya Dini (Tauhidi, Uadilifu, Utume, Uimamu, Kiyama). Hii inatokana na mwenye kusikia majibu yasiyo mfurahisha kukanusha katakata asili ya maudhui yenyewe na nafasi ya mwenye kujibu, kama vile baada ya mgojwa kusikia jawabu kutoka kwa daktari, huenda akampinga daktari huyo na kudai ya kwamba hana utaalamu wowote. Mwishoni mwa maelezo haya tunapenda kurudia tena ya kwamba, Aya hizi hazimzuii mtu kuuliza suala la kimantiki lenye lengo la kutaka kujua na kujiongezea maarifa, bali kinachokatazwa ni kuuliza masuala yasiyo na umuhimu wala ulazima, au yale ambayo kutojulikana na wengine ni bora zaidi kuliko kujulikana kwake.
211
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 211
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI NA MBILI
ُ ين آ َمنُوا َعلَي ُ ْك ْم أَ ْن ُف َس ُك ْم اَل َي َ ض ُّر ُك ْم َم ْن َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ض َّل إِ َذا ُ اه َت َديْتُ ْم إلَى اللهَِّ َم ْرجع ْ َ ُُك ْم َج ِميعًا َفيُ َنبِّئُ ُك ْم ِب َما ُك ْنتُ ْم َت ْع َمل ون ِ ِ “Enyi mlioamini! Jiangalie nafsi zenu. Hawawadhuru waliopotea ikiwa mmeongoka. Marejeo yenu nyote ni kwa Mwenyezi Mungu; atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.” (Qur’ani 5:105)
MAELEZO Kila Mtu na Majukumu Yake: Aya hii ina mafungamano makubwa na Aya iliyo kabla yake; inayosema:
ّيل لَ ُه ْم َت َعالَ ْو ْا إلَى َما أَ َ للُه ْ ُالر ُسول َقال َ َوإ َذا ِق وا َح ْسبُ َنا ِ َّ نز َل ا َوإِلَى ِ ِ َ ...َما َو َج ْد َنا َعل ْي ِه آ َباء َنا “Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na kwa Mtume, husema: Yanatutosha yale tuliyowakuta nayo baba zetu…” (Qur’ani 5:104)
Aya hii inaelezea juu ya watu wenye kufuata mila,dini na desturi za mababa zao hata kama mambo hayo yalikuwa kinyume na akili iliyo timamu seuze kuwa kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo Qur’ani imekuja kuwaonya dhidi ya tabia hii ya kuwafuata na kushikamana na watu kwa misingi ya kiukoo na kikabila bila ya kuipa akili nafasi yake ya kuamua njia iliyo sahihi. Bila shaka watu wa aina hii wanapotakiwa kuachana na fikra zao hizo, hupitikiwa na swali katika akili zao kwa kujiuliza: Ikiwa sisi tutajitenga na wazee wetu, heshima yao itakuwa ni ipi? Na ikiwa sisi tutaachana na itikadi hii, sasa itakuwaje hali ya wale ambao bado wanashikamana na itikadi hii? Kutokana na maswali haya yanayopita katika mawazo yao, jawabu la Qur’ani likawa ni: “Enyi mlioamini! 212
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 212
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
Jiangalie nafsi zenu. Hawawadhuru waliopotea ikiwa mmeongoka.” Baada ya hapo Aya inaelezea maudhui ya Siku ya Kiyama na watu kuhesabiwa na kila mmoja kulipwa stahiki yake: “Marejeo yenu nyote ni kwa Mwenyezi Mungu; atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.” Ufahamu Mbaya: Baadhi ya watu wameifahamu vibaya Aya hii, kwa kudhani ya kwamba Aya hii inatoa nafasi kwa Mwislamu kuacha kazi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya na kutosheka tu na kujikalifisha mwenyewe katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu, pahala ambapo hupatolea ushahidi ni katika ibara isemayo: “Enyi mlioamini! Jiangalie nafsi zenu. Hawawadhuru waliopotea ikiwa mmeongoka.” Kuna Riwaya zinazoonesha ya kwamba fikra hii potofu ilikuwepo hata katika zama ilipoteremka Aya hii. Jubeir ibn Nufeil anasema: Nilikuwa katika mkusanyiko wa Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) tukiwa tumekaa mbele ya Mtume (s.a.w.w.), na mimi nilikuwa ndio mdogo wao zaidi kiumri, na hapo mazungumzo yaliyokuwa yakizungumzwa yalikuwa ni juu ya kuamrishwa mema na kukataza maovu. Nilikatisha maneno na kusema: Je, haikushuka katika Qur’ani Aya isemayo: “Enyi mlioamini! Jiangalie nafsi zenu. Hawawadhuru waliopotea ikiwa mmeongoka.” (Akimaanisha ya kwamba katika Aya hii hakuna wajibu wa kuamrisha mema na kukataza mabaya). Mara ikawa watu waliokuwepo hapo wananielekezea lawama na kasoro huku wakisema: Ni kwa nini unatolea ushahidi kwa Aya ya Qur’ani bila ya kuifahamu maana yake na tafsiri yake? Nilijuta sana kutokana na niliyoyasema, na walirejea kwenye mazungumzo yao ya mwanzo. Na baada ya kumalizika kwa kikao walinikabili na kuniambia: Wewe bado ni kijana mdogo, ulijaribu kutoa maelezo yanayohusiana na Qur’ani bila ya kutambua maana yake, na huenda ukaishi kwa muda mrefu, hapo utakuja kuwaona watu namna watakavyozungukwa na ubakhili na kutawaliwa na rai zao na kila mmoja kutegemea rai yake. Itakapofika zama hiyo kuwa na hadhari sana ili yule aliyepotea miongoni mwao asije akakudhuru (hii inamaanisha ya kwamba Aya inaashiria katika zama hizo).103 Na leo hivi tunawashuhudia wale wanaopenda raha wakati panapozungumzwa kuhusu wajibu wa kuamrisha mema na kukataza mabaya wanatoa ushahidi kwa kupitia Aya hii ili kutaka kuonesha ya kwamba mambo hayo si wajibu. Kwa kweli wanachokifanya ni kupotosha maana halisi ya Aya. Bila ya shaka yoyote hakuna kupingana kati ya wajibu huu (kuamrisha mema na kukataza mabaya) na yale yaliyomo katika Aya hii kutokana na sababu zifuatazo: 103
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 4, Uk. 174 213
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 213
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwanza: Aya imebainisha kwa uwazi kabisa ya kwamba kila mmoja atahesabiwa kivyake, na upotevu wa watu wengine hautowadhuru wale walioongoka hata kama ni jamaa wa karibu, kwa hivyo ni kutowafuata na badala yake ni kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu barabara. Pili: Aya inaashiria hali ambayo hupelekea kazi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya kutokuleta mabadiliko yoyote, au kutokukamilika kwa sababu ya kutokukamilika masharti ya utekelezaji wake. Katika hali kama hiyo, wale wanaosimamia kazi hii huhisi uchungu na kuchoshwa, na huku wakijiuliza ni nini cha kufanya, hapo Aya inawajibu kwa kuwaambia: Msijali, hakika nyinyi mmetekeleza yale ambayo mlipaswa kuyafanya na wala wale waliopotea hawatoweza kuwadhuru nyinyi iwapo mtaendelea na kushikamana na njia ya uongofu. Haya tunayaona katika Riwaya tulioitaja hapo juu na pia katika Riwaya nyingine kama ile ambayo Mtume (s.a.w.w.) aliposema baada ya kuulizwa sababu ya kuteremka Aya hii:
فإذا رأيت ال ّدنيا,إئتمروا بالمعروف وتناهوا عن المنكر ّ مؤثّرة وشحا مطاعا وهوى متّبعا وإعجاب كل ذي رأي .برأيه بخويصة نفسك وذر عوامهم “Amrisheni mema na katazeni mabaya, pindi utakapoona dunia ni yenye kupendwa zaidi na ubakhili ni wenye kutiiwa na matamanio ndio yenye kufuatwa na kila mmoja kuvutiwa na rai yake, basi ikifikia hali hiyo ni juu yako kuishughulikia nafsi yako na kuachana na watu wengine.”104
Kwa hali yoyote ile suala la kuamrisha mema na kukataza mabaya ni wajibu ambao hauepukiki isipokuwa tu pale ikiwa kazi hiyo haitoleta tija yoyote au kukosekana kwa masharti yake.
104
Al-Andalusiy, Al-Muharrirul Wajiz Fii Tafsiril Kitabil Aziz, Jz. 2, Uk. 249 214
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 214
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI NA TATU
َ ين آ َمنُوا َش َها َد ُة َب ْي ِن ُك ْم إِ َذا َح َ ض َر أَ َح َد ُك ُم ْال َم ْو ُت ِح َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين َصيَّ ِة ْاث َنان َذ َوا َع ْدل ِم ْن ُك ْم أ ْ َ َ ْ ْر ُك ْم إِ ْن أَ ْنتُ ْم ي غ ن م ان ر آخ و و ال ْ َ َ ِ ِ ٍ ِ ِ ِ ْأ َ َ ْ ُ ُ ُ َ صي َبة ال َم ْو ِت َت ْح ِب ُسو َن ُه َما َ ض َفأ ِ صا َب ْتك ْم ُم ِ ض َربْت ْم ِفي ال ْر ْ َ َِم ْن َب ْع ِد َّ ا ار َتبْتُ ْم اَل َن ْش َت ِري ِب ِه َث َم ًنا ْ ان ِباللهَِّ إِ ِن ِ الصل ِة فيُق ِس َم َ ان َذا ُق ْر َبىٰ َو اَل َن ْكتُ ُم َش َها َد َة اللهَِّ إِنَّا إِ ًذا لَ ِم َن الآْ ِث ِم َ َولَ ْو َك ين َفإِ ْن َُع ِث َر َعلَىٰ أ ُ آخ َران َي َ اس َت َح َّقا إ ْث ًما َّ َ ان َم َقا َم ُه َما ِم َن م و ق ف ا م ه ن ُ ْ َ َ ِ ِ ِ ْأ َ َ اس َت َح َّق َعلَيْه ُم َّال َّلله ْ َ َ َ ال ْول َيان َ ان ِبا ِ ل َش َها َدتُ َنا أ َح ُّق ِم ْن م س ُق ي ف ين ذ ْ َ ِ ِ ِ ِ ِ ْ َ َ َّ َ َ َ ُ َ اع َت َد ْي َنا إِنَّا إِ ًذا ل ِم َن الظالِ ِم ْ َش َها َد ِت ِه َما َو َما ين ذٰلِك أ ْد َنىٰ أ ْن َيأتوا َّ ب ٌ الش َها َد ِة َعلَىٰ َو ْج ِه َها أَ ْو َي َخ ُافوا أَ ْن تُ َر َّد أَ ْي َم ان َب ْع َد أَ ْي َما ِن ِه ْم ِ ْ ْ َُّلله َّلله َ اس ِق ين ْ َواتَّ ُقوا ا َ َو ِ اس َمعُوا َوا اَل َي ْه ِدي ال َق ْو َم ال َف “Enyi mlioamini! yanapomfikia mauti mmoja wenu, wakati wa kuusia, ushahidi kati yenu ni wa waadilifu wawili miongoni mwenu. Au wengine wawili wasio kuwa katika nyinyi mnapokuwa safarini na msiba wa mauti ukawafikia. Mtawazuia wawili hao baada ya swala, na waape kwa Mwenyezi Mungu mkiwa na shaka (kwa kusema): Hatupokei thamani yoyote kwa haya hata kama ni jamaa wala hatufichi ushahidi wa Mwenyezi Mungu, hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi. Ikigundulika kuwa wawili hao wamestahiki dhambi, basi wengine wawili watasimama mahali pao katika wale ambao wamestahiki (kudai); washike nafasi ya wa mwanzo waape kwa Mwenyezi Mungu (kwa kusema): Ushahidi wetu ni haki zaidi kuliko wa wale; na sisi hatukupita kiasi; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa madhalimu. Hiyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi ulio sawa au wataogopa visije vikaletwa viapo vingine baada ya viapo vyao. Na mcheni Mwenyezi Mungu na msikie. Na hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi mafasiki.” (Qur’ani 5:106-108).
215
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 215
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
SABABU YA KUTEREMKA Mfasiri wa Qur’ani; At-Tabarasiy na baadhi wa wafasiri wengine wanasema yakwamba Aya hizi ziliteremka kutokana na mmoja miongoni mwa Waislamu aliyejulikana kwa jina la Ibn Abi Mariyah ambaye alikuwa na wadogo wake wawili wasio Waislamu. Watu hao wakijulikana kwa majina ya Tamim na Uday. Siku moja wote kwa pamoja walitoka katika mji wa Madina kwa lengo la kufanya biashara, walipofika njiani Ibn Abi Mariyah aliumwa, aliandika wasia na kisha aliuficha katika mizigo yake, aliwataka wale wadogo zake waipeleke mizigo yake kwa familia yake, baada ya hapo Ibn Abi Mariyah akafariki dunia. Baada ya kufariki waliifungua mizigo na kuchukua vitu vingi vya thamani na iliobakia waliifikisha kwa familia yake. Baada ya kuifungua walikuta kuna upungufu wa vile ambavyo Ibn Abi Mariyah aliondoka navyo, na mara waliukuta wasia nakuona maandishi ya vitu vilivyoibwa. Baada ya wale ndugu wawili kuelezewa habari hiyo, walikataa madai ya kwamba wao wamevichukua vitu hivyo huku wakidai ya kwamba wamekabidhi vitu vyote walivyopewa. Shauri lao lilipelekwa kwa Mtume (s.a.w.w.), hapo ndipo zikamshukia Aya hizi.105
MAELEZO Miongoni mwa mambo ambayo Uislamu umeyapa kipaumbele ni suala zima la udhibiti na uhifadhi wa mali za wengine, na kuhakikisha haki inasimama katika jamii, ikiwemo haki ya warithi kupata wanachostahiki, na zaidi ikiwa warithi hao ni watoto wadogo, na katika kuhakikisha haki hiyo haipotei, Mwenyezi Mungu amewataka Waumini kufanya kila ambacho kitapelekea kuziba miyanya ya dhulma, anasema: “Enyi mlioamini! yanapomfikia mauti mmoja wenu, wakati wa kuusia, ushahidi kati yenu ni wa waadilifu wawili miongoni mwenu.” Sehemu hii ya Aya ya Mwenyezi Mungu inatoa mwongozo wa kuhifadhiwa mali ya wengine kwa kushuhudilishwa mashahidi wawili walio Waislamu tena wawe waadilifu, lakini ikiwa hali ya kuwapata walio Waislamu imeshindikana, hasa ikiwa watu wamo kwenye safari, basi itafaa hata kwa wasio Waislamu ilhali tu watakuwa ni wenye kutegemewa kuwa wataifikisha haki kwa wenyewe. Na walengwa kwa wasio Waislamu ni wale tu walioteremshiwa kitabu (Mayahudi na Manasara) ama washirika hawastahiki kuwa mashahidi, Aya inafafanua hayo kwa kusema: “Au wengine wawili wasio kuwa katika nyinyi mnapokuwa safarini na msiba wa mauti ukawafikia.” Hapa tunajifunza ya kwamba iwapo kuna uwezekano wa kuwapata Waislamu katika kusimamia ushahidi, haitofaa kushuhudiwa na wasiokuwa Waislamu. 105
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 4, Uk. 177 216
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 216
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
Aya inaendelea kubainisha namna ya kubainisha ukweli wa mambo ikiwa kutaonekana kuna dhulma yoyote itakayotendeka, hapo mashahidi watatakiwa kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu katika kuthibitisha madai yao na kukanusha watakayoona wamesingiziwa dhidi yao: “Mtawazuia wawili hao baada ya swala, na waape kwa Mwenyezi Mungu mkiwa na shaka (kwa kusema):” Katika kiapo chao watatakiwa kubainisha ya kwamba wao si wenye kukubali kuuza haki ya wengine kwa manufaa ya dunia yenye kupita, hata kama ushahidi watakaoutoa utakuwa hauna maslahi na jamaa zao, kwa hivyo watasema katika kuuapa kwao: “Hatupokei thamani yoyote kwa haya hata kama ni jamaa wala hatufichi ushahidi wa Mwenyezi Mungu, hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi.” Pia Aya imeelezea wakati wa hao mashahidi kula kiapo iwapo watashukiwa kufanya udanganyifu kwa kile walichoaminiwa, wakati huu ni baada ya Swala, Aya haikueleza ni baada ya Swala gani, ila Riwaya mbalimbali zinaonesha ni baada ya Swala ya Alasiri, huenda ni kutokana na kutumiwa wakati huo kupitisha hukumu za kesi mbalimbali zilizokuwa zikipelekwa kwa Mtume (s.a.w.w.) Ama kwa wasio waislamu itakuwa ni baada ya ibada zao. Mwenyezi Mungu ameuteua wakati huo kwani kuna uzito fulani kwa mtu kudanganya katika muda ule tu anapomaliza ibada ya Swala: “Mtawazuia wawili hao baada ya swala, na waape kwa Mwenyezi Mungu mkiwa na shaka.” Aya inayofuata inaeleza ya kwamba ikiwa itabainika ya kwamba mashahidi wamefanya khiyana dhidi ya haki ya warithi, basi hao warithi watasimama na kutoa ushahidi unaothibitisha haki yao: “Ikigundulika kuwa wawili hao wamestahiki dhambi, basi wengine wawili watasimama mahali pao katika wale ambao wamestahiki (kudai); washike nafasi ya wa mwanzo.” Hao mashahidi wawili wa upande wa warithi na wao wataapa kwa jina la Mwenyezi Mungu katika ushahidi wao, “Waape kwa Mwenyezi Mungu (kwa kusema): Ushahidi wetu ni haki zaidi kuliko wa wale; na sisi hatukupita kiasi; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa madhalimu.” Aya ya mwisho katika maudhui haya inabainisha hekima ya hukumu zilizotajwa katika Aya zilizotangulia; kama vile hukumu ya ushahidi, hukumu ya kula kiapo ikiwa kutaonekana kumefanyika udanganyifu na kiapo hicho kutolewa baada ya Swala mbele ya mjumuiko wa watu wengi, na warithi kutoa ushahidi wao ikiwa wataona kuna mbinu za kunyimwa haki yao. Hali hii inawafanya mashahidi kuwa waangalifu wakubwa katika ushahidi wao, ama kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu au kwa kuwaogopa watu, ndio Mwenyezi Mungu akasema: “Hiyo inaelekea zaidi ya
217
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 217
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
kwamba watatoa ushahidi ulio sawa au wataogopa visije vikaletwa viapo vingine baada ya viapo vyao.” Na katika kusisitiza kushikamana na hukumu zilizotangulia kutajwa, Aya inamalizia kwa kusema: “Na mcheni Mwenyezi Mungu na msikie. Na hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi mafasiki.”
218
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 218
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI NA NNE
ُ ُّين َك َف ُروا َز ْح ًفا َف اَل تُ َول َ ين آ َمنُوا إِ َذا لَ ِقيتُ ُم الَّ ِذ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ وه ُم َ ْأ ً ال أَ ْو ُم َت َحي ِّزا َ ار َو َم ْن يُ َولِّ ِه ْم َي ْو َم ِئ ٍذ ُدب َ ال ْد َب ٍ ُر ُه إِ اَّل ُم َت َح ِّر ًفا لِ ِق َت َ إِلَىٰ ِف َئ ٍة َف َق ْد َبا َء ِب َغ ير ُ ص َ ض ٍب ِم َن اللهَِّ َو َم ْأ َوا ُه َج َهنَّ ُم َو ِب ْئ ِ س ْال َم ََّل ِك َّن الله َ ْت إِ ْذ َر َمي َ وه ْم ولكن اللهََّ َق َتلَ ُه ْم َو َما َر َمي ُ َُفلَ ْم َت ْقتُل ٰ َ ْت َو َ َر َمىٰ َولِيُ ْبلِ َي ْال ُم ْؤ ِم ِن ين ِم ْن ُه َب اَل ًء َح َس ًنا إِ َّن اللهََّ َس ِمي ٌع َعلِي ٌم َذٰلِ ُك ْم َ وه ُن َك ْي ِد ْال َكا ِف ِر ين ِ َوأَ َّن اللهََّ ُم “Enyi mlioamini! Mnapokutana vitani na wale waliokufuru, basi msiwageuzie migongo. Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi, hakika amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu; na makazi yake ni Jahannam, napo ni mwishilio muovu. Hamkuwaua nyinyi, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua, na hukutupa wewe ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu Ndiye aliyetupa. Ili awajaribu waumini majaribu mazuri. Hakika Mweyezi Mungu ni Msikivu, Mjuzi. Ndiyo hivyo! Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye adhoofishaye vitimbi vya makafiri.” (Qur’ani; 8:15-18)
MAELEZO Ni Haramu Kukimbia Vita: Aya hizi zinatoa katazo kwa Waumini kukimbia vita pindi wanapokabiliana na adui, hata kama adui ataonekana kuwa na nguvu zaidi kuliko jeshi la Waislamu, kwani kigezo cha kushinda vita kwa Waislamu baada ya kujiandaa kwa kiasi wanachoweza ni kumtegemea Mwenyezi Mungu. Wala Uislamu hauangalii ushindi kwa ukubwa wa jeshi, kwani Waislamu waliweza kuwashinda maadui wao katika vita vya Badri licha ya uhaba wa zana za kivita na uchache wa wapiganaji: “Enyi mlioamini! Mnapokutana vitani na wale waliokufuru, basi msiwageuzie migongo.” Hata kama mambo yatawawia magumu Waislamu, hawana budi kuendelea na mapambano hadi dakika ya mwisho, na ikitokea kuwageuzia migongo maadui wao, 219
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 219
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
basi iwe ni kwa ajili ya kutengeneza nguvu katika kukabiliana nao na sio kukimbia moja kwa moja: “Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo, isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi, hakika amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu; na makazi yake ni Jahannam, napo ni mwishilio muovu.” Hapa Qur’ani inatufunza namna ya kutumia mbinu za kiakili katika kumshinda adui. Waislamu wanaweza kufanya ujanja kama kwamba wanakimbia ili kuwafanya maadui kuwa na furaha ya ushindi na kughafilika na silaha zao, na hapo Waislamu kuitumia nafasi hiyo kutoa kipigo kikali dhidi yao, au njia nyingine ni pale mpiganaji anapokuwepo pahala peke yake, hapo anaruhusika kuondoka sehemu hiyo na kwenda kujiunga na kikosi ili kupambana na adui kwa nguvu moja, hizi ndizo hali mbili tu ambazo mpiganaji anaruhusiwa kuwageuzia mgongo maadui. Kidhahiri hali hizi zinaonekana kama ni kuwakimbia maadui lakini kwa undani ni moja kati ya ujanja wa kivita, kama inavyosemwa: ‘Vita ni ujanja’. Ama yule ambaye amekimbia moja kwa moja kwa kuhofia kufikwa na mauti, si kwamba tu ataghadhibikiwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kwa kuishi maisha ya madhila, bali mafikio yake ya Siku ya Kiyama yatakuwa ni katika Moto uunguzao. Imepokewa kutoka kwa Imamu Ridha (a.s.) baada ya kuulizwa hekima ya kuharamishwa kukimbia katika vita, alijibu kwa kusema:
ّ وحرم اهلل الفرار من ,الزحف لما فيه من الوهن في ال ّدين ّ السالم وترك ّ واإلستخفاف ّ بالرسل واألئ ّمة العادلة عليهم والعقوبة على إنكار ما دعوا إليه من,نصرتهم على األعداء بالربوبيّة وإظهار العدل وترك الجور وإماتة الفساد ّ اإلقرار وما يكون من, لما في ذلك من جرءة العد ّو على المسلمين ّ عز ّ السبي والقتل وإبطال دين اهلل .وجل وغيره من الفساد ّ “Na Mwenyezi Mungu ameharamisha kukimbia kwenye vita kwani kufanya hivyo ni kuidhoofisha Dini na kuwadharau Mitume pamoja na Maimamu waadilifu (a.s.), na kuacha kuwatetea dhidi ya maadui, na ni kupinga yale waliyoyalingania, kama vile kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kudhihirisha uadilifu na kuacha jeuri na kutofanya ufisadi. Pia kukimbia vita kunatoa fursa kwa adui kuwashambulia Waislamu,
220
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 220
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
kuwateka, kuwauwa na kuipinga Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kufanyika ufisadi wa kila aina.”106
Kuthibiti katika uwanja wa mapambano na kubakia hapo hadi mwisho wake, ilikuwa ni miongoni mwa sifa bora za Imamu Ali (a.s.), ameashiria mwenyewe sifa hii ili iwe ni kigezo kwa kila Mwislamu wa kweli, anasema:
ّ الزحف ّ قط ولم يبارزني أحد ّ أفر من إال سقيت ّ إنّي لم .األرض من دمه “Hakika mimi sijapata kukimbia katika vita asilani, wala hakuna yeyote aliyepambana nami isipokuwa niliinywesha ardhi damu yake.”107
Aya inayofuata inawataka Waislamu kuondosha majigambo na majivuno pindi wanapopata ushindi dhidi ya adui yao, na kutoona nusra walioipata ni kutokana na nguvu zao na ujanja wao wa kivita. Wanatakiwa muda wote wa mapambano wamkumbuke na kumtaja Mwenyezi Mungu huku wakitambua ya kwamba Yeye ndio sababu ya kila mafanikio na ushindi, bila ya kuacha kuelekeza nyuso zao Kwake na kunyanyua mikono yao kwa kumuomba nusra na ushindi, Mwenyezi Mungu anasema: “Hamkuwaua nyinyi, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua, na hukutupa wewe ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa.” Imepokewa katika Riwaya ya kwamba siku ya vita vya Badri, Mtume (s.a.w.w.) alimtaka Imamu Ali (a.s.) ampelekee kitanga cha mkono chenye mchanga na changarawe, Imamu Ali (a.s.) alimpelekea,baada ya kupelekewa aliurusha upande waliokuwepo washirikina, na huku akisoma: “Hamkuwaua nyinyi, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua, na hukutupa wewe ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa.” Kitendo hicho cha Mtume (s.a.w.w.) kutupa mchanga upande wa washirikina kilikuwa ni kitendo cha kimiujiza, kwani mchanga huo uliweza kuwafikia maadui na kuwaingia katika macho yao kiasi cha kuwafanya kupigwa na butwaa na kujawa na hofu. Bila ya shaka dhahiri ya mambo inaonesha ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Maswahaba wake ndio waliosimama kidete katika kuupatia ushindi Uislamu katika vita vya Badri, lakini Qur’ani Tukufu inawaambia ya kwamba: Ninyi sio sababu ya kupatikana kwa ushindi, kwani mafungamano yenu ya kiroho na kiimani 106 107
Almajlisiy, Biharul Anwar, Jz. 76, Uk. 9 Rishahriy, Mizanul Hikma, Jz. 1, Uk. 143 221
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 221
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
na nguvu zenu mlizozitoa, vyote hivyo ni vipawa mlivyopewa na Mwenyezi Mungu, na harakati zenu katika jihadi ni kutokana nauwezo wa Mwenyezi Mungu katika kuitetea Dini yake. Aya inamalizia kwa kuashiria ya kwamba katika vita vya Badri kulijawa na mitihani mbali mbali kwa Waislamu kutoka kwa Mola wao, inasema: “Ili awajaribu waumini majaribu mazuri.” Kutokana na matakwa Yake Mwenyezi Mungu, aliwapa Waislamu ushindi mnono katika vita vyao vya kwanza dhidi ya maadui wao, ushindi huo ulikuwa ni mtihani mkubwa kwa Waumini hao, kwa hivyo katika hali kama hii haiwapasi kughururika na kubweteka na kumuona adui yao ni dhaifu na kwamba kama walivyomshinda leo, basi wataweza kumshinda kesho bila ya kujipanga na kuzidisha matayarisho ya kiroho, kimwili na kisilaha na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ndio maana Aya ikakhitimisha kwa kusema: “Hakika Mweyezi Mungu ni Msikivu, Mjuzi.” Inamaanisha ya kwamba amesikia sauti ya maombi ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja Maswahaba wake kumuomba Mola wao, na Mwenyezi Mungu alijua uhalisia wa imani zao, kwa hivyo akawateremshia ushindi mnono na kuwaangamiza maadui wao. Na Mwenyezi Mungu bado yuko tayari kuwapa ushindi Waumini wa kweli katika kila zama, kwa sharti la kutekeleza maagizo na maelekezo Yake katika nyanja zote za maisha, kwani mwisho mwema ni wa Waumini tu. Katika Aya ya mwisho kwenye maudhui haya, Mwenyezi Mungu anajumuisha yote yaliyotangulia ya kwamba malipo ya Waumini na ya makafiri ni kama alivyoyaeleza, anasema: “Ndiyo hivyo!” Na baada ya kueleza anakhitimisha kwa kuelezea sababu ya kufanya hivyo: “Na hakika Mwenyezi Mungu Ndiye adhoofishaye vitimbi vya makafiri.”
222
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 222
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI NA TANO
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين آ َمنُوا أَ ِطيعُوا اللهََّ َو َر ُسولَ ُه َو اَل َت َولَّ ْوا َع ْن ُه َوأَ ْنتُ ْم َ ين َقالُوا َس ِم ْع َنا َو ُه ْم اَل َي ْس َمع َ ُون َو اَل َت ُكونُوا َكالَّ ِذ َ َت ْس َمع ُون إِ َّن َُّون َولَ ْو َعلِ َم الله ْ الص ُّم ْالب َّ َش َّر َ ُين اَل َي ْع ِقل َ ُك ُم الَّ ِذ ِّ الد َو ُّ َِّاب ِع ْن َد الله َ َ ََِفيه ْم َخي ً أ َّ َ ُ ْر َ ض ون ِ ِ ْرا ل ْس َم َع ُه ْم َول ْو أ ْس َم َع ُه ْم ل َت َول ْوا َو ُه ْم ُمع “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, wala msijiepushe naye hali mnasikia. Wala msiwe kama wale wanaosema: Tumesikia; na kumbe hawasikii. Hakika wanyama waovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni viziwi, mabubu ambao hawatumii akili. Na kama Mwenyezi Mungu angelijua wema wowote kwao, angeliwasikilizisha; na kama angeliwasikilizisha, wangeligeuka wakipuuza.” (Qur’ani; 8: 20-23)
MAELEZO Walisema Wamesikia Kumbe Hawakusikia!: Aya zinawataka Waislamu kuwa watiifu wa amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika hali zote. Namna hii ambayo Aya zimekuja kuonesha uwepo wa upungufu kwa baadhi ya Waislamu katika utekelezaji wa majukumu yao ya wajibu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, na hii ndio sababu ya Aya kuja na amri hii: “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Katika kutoa msisitizo zaidi juu ya utiifu, inasema kwa kutumia mfumo mwingine: “Wala msijiepushe naye hali mnasikia.” Bila ya shaka kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni wajibu kwa watu wote, awe Muumini au asiyekuwa Muumini, lakini kwa vile wahusika na wanaokubali kutekeleza amri hii ni Waumini tu, ndio maana amri hii ikaelekezwa kwao pasi na wengine. Aya ya pili nayo inatoa msisitizo wa jambo hili la utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, inasema: “Wala msiwe kama wale wanaosema: Tumesikia; na kumbe hawasikii.” Hapa wanakusudiwa wale ambao wanatambua vyema wajibu wao lakini hawatendi, na wanasikia yanayopasa kuyatenda, lakini kusikia kwao 223
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 223
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
hakuwasaidii lolote. La kustaajabisha kwa watu hawa, wanaonekana kwamba ni Waumini lakini hawatendi kwa mujibu wa imani yao, wako mbali na maamrisho ya Dini yao! Watu hawa wana masikio yanayosikia na akili ya kuyafahamu yasemwayo, lakini kwa vile hawayafanyii kazi na kuyaingiza katika matendo yao ya kila siku, basi wao ni kama viziwi, kwani maneno ni utangulizi wa matendo, na ikiwa patakosekana matendo, basi utangulizi wowote hautakuwa na faida. Aya hizi zinawahusu Waislamu wa zama zote ambao ni wepesi wa kusema au kusikiliza wasemaji, lakini kwa bahati mbaya si watekelezaji. Na kwa vile maneno bila ya vitendo, na kusikiliza bila faida ni miongoni mwa matatizo yanayozisibu jamii mbali mbali, na sababu kubwa ya kutokuendelea, Aya nyingine imekuja kwa utaratibu mwingine wa kukemea tabia hii mbaya na kusisitiza juu ya kufuata amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, inasema: “Hakika wanyama waovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni viziwi, mabubu ambao hawatumii akili.” Na kwa vile Qur’ani Tukufu ni Kitabu kinachozingatia zaidi matendo, kwa hivyo daima inaangalia natija, huku ikizingatia ya kwamba kila mwanadamu ambaye yupo katika ulimwengu huu, ambaye hana manufaa kwa wengine, basi kuwepo kwake ni sawa na kutokuwepo, na kila kiumbe hai asiye na harakati zozote ni kama mfu, na kila kiungo cha mwanadamu kisipotumika vyema katika njia ya uongofu na manufaa ni sawa na kutokuwepo kwake. Aya hii inawalenga wale wenye masikio mazima ya kusikia, lakini hawayatumii katika kusikilizia uongofu utokao kwa Mola Wao, basi hao ni kama wale wenye matatizo ya usikivu (viziwi), na wale wenye ndimi nzuri, lakini hawazitumii ndimi hizo katika kuwalingania watu kwenye njia ya haki na kupiga vita ufisadi na dhulma; hawaamrishi mema wala hawakatazi mabaya, bali kinyume chake huzitumia neema hizi walizopewa na Mola Wao katika njia za kuwapoteza watu au katika kuitia nguvu na kuitetea batili. Watu wa aina hii ni kama mabubu wasioweza kuzungumza. Pia inawalenga wale wenye uwezo mkubwa wa kufikiri lakini hawazitumii akili zao katika kusahihisha itikadi zisizo sahihi walizozirithi kutoka kwa watu wengine, watu wa aina hii Qur’ani inawahesabu kuwa ni miongoni mwa wagonjwa wa akili. Aya inayofuata inaeleza ya kwamba lau kama watu hao kweli wako tayari kuyafuata kivitendo wanayoyasikia, basi njia ya kufikia huko ingekua nyeupe, na Mwenyezi Mungu angeondosha kila aina ya vizuizi vya usikivu: “Na kama Mwenyezi Mungu angelijua wema wowote kwao, angeliwasikilizisha.” Kuhusiana na Aya hii, imepokewa kutoka katika baadhi ya Riwaya ya kwamba, baadhi ya washirikina walimwendea Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: Lau kama utatutolea babu yetu mkubwa (Qusway ibn Kilab) kutoka katika kaburi lake akiwa hai na akashuhudia ya
224
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 224
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
kwamba wewe ni Mtume, basi sisi sote tutasilimu! Hapo ndipo Aya hii ikateremka ikiwaambia: Lau kama hayo wanayoyasema ni ya kweli, basi Mwenyezi Mungu angelitekeleza ombi lao hili kwa njia ya muujiza, lakini hao si wa kweli, wanachofanya ni kutoa visingizio mbali mbali visivyo na mashiko kwa lengo la kutoitikia ulinganio utokao kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anasema: “Na kama angeliwasikilizisha, wangeligeuka wakipuuza.” Kwa kweli waliosikia ulinganio wa haki kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) ni wengi sana, na Aya za Qur’ani kupenya katika masikio yao na kufahamu vyema maana yake, lakini waliamua tu kupinga kutokana na kuasi kwao, kwa kweli hawako tayari kufuata uongofu wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kupenda kwao dunia, hao wako katika upotevu ulio wazi kabisa. Awamu za Kusikiliza Haki: Baadhi ya wakati mwanadamu husikia maneno bila ya kuyatilia maanani. Na kuna baadhi yao ambao hukataa hata kusikiliza kinachosemwa, kama Qur’ani inavyotueleza:
ُْ َ َ َو َق َ َ ال الَّ ِذ َا َ آن َو ْال َغ ْوا ِفي ِه لَ َعلَّ ُك ْم َت ْغلِب ُون ِ ين ك َف ُروا ل َت ْس َمعُوا لِ َهذا الق ْر “Na walisema waliokufuru (kuambizana wenyewe kwa wenyewe): Msiisikilize Qur’ani hii (inaposomwa) na ipigieni makelele (isomwapo), huenda mkashinda.” (Qur’ani; 41:26).
Na mara nyingine mtu huamua kusikiliza maneno na kuyaelewa vizuri, lakini akawa hayuko tayari kuyafanyia kazi maneno hayo. Watu wa aina hii wana sifa ya unafiki kama ilivyoelezwa katika Aya ifuatayo:
َ َو ِم ْنهُم َّمن َي ْس َت ِم ُع إلَي َ ْك َحتَّى إِ َذا َخ َر ُجوا ِم ْن ِعن ِد َك َقالُوا لِلَّ ِذ ين ِ ُ ُ َّ َُّلله ُ ً َين َط َب َع ا َعل َ ال آ ِنفا أ ْولَِئ َ اذا َق َ أُوتُوا ْال ِع ْل َم َم َ وب ِه ْم ل ق ى ذ ال ك ِ ِ ُ َواتَّ َبعُوا أَ ْه َو اءه ْم “Na wako miongoni mwao wanaokusikiliza, hata wanapoondoka kwako, wanawauliza wale waliopewa elimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu 225
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 225
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
amewapiga mihuri nyoyoni mwao na wakafuata matamanio ya nafsi zao.” (Qur’ani; 47:16)
Huenda watu wa aina hii wakafikia hali mbaya zaidi, nayo ni kujiondoshea wenyewe uwezo wa kujua mema na mabaya, kiasi ambacho wanaposikia maneno ya haki wasiweze kuyaelewa na kufahamu makusudio yake. Makundi haya matatu ya watu wanatambuliwa na Qur’ani kwamba wao ni viziwi na mabubu, kwani ambaye anasikia kikweli kweli anawajibika kuelewa, kufikiria na kuweka azma ya kuyafanyia kazi. Katika zama zetu hizi, kuna watu wengi wanaotegesha masikio yao kwa ajili ya kusikiliza Aya za Qur’ani pindi zisomwapo na kuchambuliwa maana yake na huku wakiwamwagia sifa mbali mbali wenye kuzichambua Aya hizo, lakini watu hao si wenye kutenda hata chembe ya yale yaliyomo katika Aya hizo!
226
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 226
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI NA SITA
ََّيا أَُّي َها ال َّاس َتجيبُوا للِه ُ لر ُسول إ َذا َد َع ُ َ اك ْم ل و وا ن م آ ين ذ َّ ْ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ َ ْ ْ ُ َّلله ُ ُحي َ اعلَ ُموا أَ َّن ا َ َي ُحول َبي ْ يك ْم َو ْن ال َم ْر ِء َو َقل ِب ِه َوأنَّ ُه ِ ْ لِ َما ي َ صي َب َّن الَّ ِذ َ إِلَ ْي ِه تُ ْح َش ُر ين َظلَ ُموا ِم ْن ُك ْم ِ ُون َواتَّ ُقوا ِف ْت َن ًة اَل ت ٌ ِاعلَ ُموا أَ َّن اللهََّ َش ِدي ُد ْال ِع َقاب َو ْاذ ُك ُروا إ ْذ أَ ْنتُ ْم َقل ْ اص ًة َو يل َّ َخ ِ ِ َ ْون ِفي أ ُ اس َفآ َو ْ ُم ْس َت َ ض َت َخ ُاف َ ض َع ُف اك ْم ر ال ْ ُ َّون أَ ْن َي َت َخ َّط َف ُك ُم الن ِ َّ صر ِه َو َر َز َق ُك ْم ِم َن ُ َوأَيَّ َد َ َ ات لَ َعلَّ ُك ْم َت ْش ُك ُر ون ن ب م ك ْ ْ ِ الطيِّ َب ِ ِ “Enyi mlioamini! Mwitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaita kwenye lile litakalowapa uhai. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba mtakusanywa Kwake. Na jikingeni na fitna ambayo haitawasibu wale waliodhulumu miongoni mwenu peke yao, na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. Na kumbukeni mlipokuwa wachache, mkionekana wadhaifu katika nchi; mkawa mnaogopa watu wasiwanyakue; akawapa makao na akawatia nguvu kwa nusura Yake na akawapa riziki njema ili mpate kushukuru.” (Qur’ani; 8:24-26)
MAELEZO Wito Kwenye Uhai: Aya hizi zinabainisha ya kwamba wito wa Uislamu ni wito wa kuwaita watu katika uhai wa kiroho, kimwili, kielimu, kiutamaduni, kiuchumi, kisiasa, kijamii, kitabia na katika kila nyanja ya maisha ya mwanadamu. Kwa hivyo ikiwa kuna yeyote ambaye anataka kujua malengo ya Uislamu, jawabu lake ni kwamba lengo lake ni kufanikisha maisha bora kwa mwanadamu katika nyanja zote. Hivi ndivyo ambavyo Uislamu unatufunza. Katika Aya hizi kuna suala linalojitokeza nalo ni: Je, kabla ya kudhihiri Uislamu na kabla ya kuteremshwa Qur’ani watu walikuwa ni wafu? Jawabu la suala hili ni 227
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 227
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
ndiyo, walikuwa ni wafu waliokosa uhai kwa maana hii iliyoelezwa na Qur’ani, kwani kuna aina mbalimbali za uhai, kama Qur’ani ilivyoeleza: 1. Uhai wa mimea: “Tambueni ya kwamba Mwenyezi Mungu huihuisha ardhi baada ya mauti yake.” (Qur’ani; 57: 17) 2.
Uhai wa wanyama: “Hakika Yule ambaye ameihuisha ndiye atakayewahuisha waliokufa.” (Qur’ani 41:39)
3.
Uhai wa kiakili na kifikra: “Je, aliyekuwa maiti kisha tukamhuisha na tukamjaalia nuru (aliyekuwa kafiri kisha akasilimu)…” (Qur’ani; 6:122)
4.
Uhai wa milele Siku ya Kiyama: “Laiti ningelitanguliza (wema) kwa ajili ya uhai wangu (huu wa leo).” (Qur’ani; 89: 24)
5.
Uhai wa Mwenyezi Mungu usio na kikomo: “Na mtegemee (Mwenyezi Mungu) wa milele Ambaye hatokufa.” (Qur’ani; 25: 58)
Kwa hiyo pindi tunapoangalia kwa makini aina hizi za uhai tutashuhudia ya kwamba, katika zama za kijahilia watu walikuwa wakiishi katika uhai wa kinyama, huku wakiwa mbali sana na uhai wa kiroho, kiubinadamu na kiakili, ndipo Qur’ani ikaja na kuwaita katika uhai wa uhakika. Hapa tunaona udhaifu wa mawazo ya wale wanaoona ya kwamba Dini ya Kiislamu haikuja kushughulikia shughuli za maisha ya mwanadamu za kila siku na badala yake imekuja tu kujishughulisha na mambo ya kiroho. Dini ya kweli ni ile inayojishughulisha na maisha ya mwanadamu katika kila nyanja, kwani mwanadamu ameumbwa akiwa na roho pamoja na mwili. Aya inaendelea kusema: “Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba mtakusanywa Kwake.” Hapa panajitokeza swali: Ni vipi Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake? Kuhusiana na swali hili wafasiri wameeleza kauli mbalimbali: 1.
Ni ile hali ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa waja Wake, kama kwamba Mwenyezi Mungu yuko ndani ya nyoyo za wajaWake, kama Qur’ani inavyoeleza:
ُ َو َن ْح ُن أَ ْق َر ُب إلَ ْي ِه ِم َ ْص ُر ون ِ نك ْم َولَ ِكن اَّل تُب ِ “Nasi tuko naye karibu zaidi (huyo anaetoka roho) kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamuoni. (Qur’ani; 56:85)
228
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 228
12/8/2014 2:43:43 PM
WITO KWA WAUMINI
2.
Ni ile hali ya uwezo wa Mwenyezi Mungu kuweza kuzigeuza nyoyo za watu, kama tunavyosoma katika dua:
...يا مقلّب القلوب واألبصار “Ewe mwenye kuzigeuza nyoyo na macho…..”
3.
Ni ile hali ya mtu kutokuwa na uwezo wowote wa kufahamu mambo mbalimbali isipokuwa baada ya kuwezeshwa na Mwenyezi Mungu, ambaye Ndiye asili ya kila kitu.
4.
Ni uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kuweza kuitoa roho ya mja Wake pasi na kuwa na kizuizi cha aina yoyote ile.
Lakini kwa vile maana hizi hazipingani, inawezekana zote zikawa na makusudio ya sehemu hiyo ya Aya, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuona na kusimamia shughuli zote za viumbe Vyake, na mambo yote yanayomfikia mwanadamu, kama vile furaha, uhai, mauti, amani, utulivu n.k., vyoye hivi viko mikononi mwake, kwa hivyo mwanadamu hawezi kumficha Mwenyezi Mungu kitu chochote kile au kufanya kitu bila ya kuwezeshwa na Yeye, kwa hivyo si sahihi kwa mwanadamu kumtumikia asiyekuwa Mwenyezi Mungu na anapofikwa na shida akamwelekea Yeye kwa kumuomba utatuzi wa shida yake, Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu na Ndiye Mmiliki wa viumbe vyote. Kwa hivyo, kila Mwislamu anapaswa kuitikia wito wa Mtume (s.a.w.w.), kwani naye huwaita watu katika mambo yatakayowapatia uhai, kwa vile ametumwa na Mola ambaye ni Mmiliki wa uhai na uongofu, bali ni Mmiliki wa kila kitu. Katika kulisisitiza jambo hili, kama kwamba Aya inawaambia Waumini ya kwamba: Nyinyi si tu kwamba mko katika himaya ya Mwenyezi Mungu, bali mtarudi katika ulimwengu mwingine (Kiyama), kwa hivyo nyinyi mko katika himaya yake hapa duniani na pia kesho akhera (Siku ya Kiyama). Aya inayofuata inaelezea malipo mabaya kwa anayekataa wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake: “Na jikingeni na fitna ambayo haitawasibu wale waliodhulumu miongoni mwenu peke yao.” Neno ‘Fitina’ limetumika katika Qur’ani likimaanisha maana mbali mbali, kama vile: mtihani, balaa, adhabu na msiba. Ama katika Aya hii limetumika kwa maana ya adhabu na janga la kijamii ambalo huangamiza kibichi na kikavu. Hii ndio kanuni ya maisha ya kijamii, iwapo baadhi ya wanajamii wataacha wajibu wa kutekeleza mambo mema na kuacha maovu, pindi balaa itakapoingia itawasibu
229
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 229
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
waovu na wema. Kwa hivyo haifai mtu kutosheka kwa yeye kufuata kanuni za kijamii na kupuuzia wale wanaozivunja bila ya kuwaonya, kwani masuala yanayohusiana na jamii ni ya wanajamii wote. Kwa mfano, ikiwa jamii hiyo imevamiwa na majambazi na wakahitajika vijana mia moja ili kukabiliana nao, lakini wakajitokeza nusu yake tu, hapo wanajamii wote watadhuriwa na majambazi hayo; wale walioshiriki na wale waliokataa kushiriki. Kwa hivyo watu wema katika jamii wanawajibu wa kunyanyua sauti zao pindi wanapowaona wengine wanahujumu maendeleo ya jamii yao, ikiwa watakaa kimya, basi watahesabika kuwa ni washirika wa dhulma wanayofanyiwa wengine. Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:
ّ عز ّ ّ إن اهلل ّ الخاصة حتى يروا اليعذب العا ّمة بعمل وجل ّ فإذا فعلوا,المنكر بين ظهرانيهم وهم قادرون على أن ينكروا ّ ذلك .الخاصة و العا ّمة عذب اهلل ّ “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu, hawaadhibu watu wote kutokana na makosa ya baadhi ya watu mpaka aone uovu ulioenea baina yao, na huku wakiwa na uwezo wa kuukataza, basi ikiwa watafanya hivyo (wataacha kuukataza) Mwenyezi Mungu atawaadhibu watendao uovu huo na wasio utenda.”108
Aya inamalizia kwa kutoa vitisho vikali kwa watu waovu kwa kusema: “Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.” Mwenyezi Mungu anatoa angalizo dhidi ya watu waovu kubweteka na kuendelea na uovu wao kwa kutegemea ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa rehema na Mwenye kuwaonea huruma waja Wake, basi anawataka waangalie upande mwingine wa shilingi. Ni kwamba Yeye pia ni Mkali wa kuadhibu. Watambue ya kwamba balaa litawakumba hapa hapa duniani kabla ya akhera, na haya tunayashuhudia. Tunaona ni namna gani Waislamu waliishi katika neema na furaha chini ya dola ya Kiislamu iliyokuwa chini ya Mtume (s.a.w.w.), lakini baada ya kuaga dunia fitina ilianza kuwala wenyewe kidogo kidogo, na mwisho wake yale mamlaka yaliyokuwa mikononi mwa Waislamu leo hayapo, na kilicho baki ni historia tu. Hii ni kutokana na upuuzaji wao wa kanuni na sheria za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na tunapotupia jicho katika jamii zetu za Kiislamu hivi leo, tunashuhudia ni namna gani fitina ilivyotutafuna na kuendea kututafuna. Leo hatuna kifua cha kumkingia adui, baadhi ya maeneo ya Kiislamu yako chini ya utawala wa kikoloni wa Kizayuni, kukumbatia tamaduni za Kimagharibi, mmong’onyoko wa 108
Ibn Hajar, Fathul Baariy, Jz.13, Uk. 3 230
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 230
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
kimaadili, kuvunjika kwa familia, ujinga n.k. Haya yote yametokana na sisi wenyewe kama Aya inavyotueleza. Fitina hii kwa kweli imemsibu mkubwa na mdogo, na mwerevu na mjinga, na itaendelea hadi pale Waislamu watakapoamka na kukabiliana na kila aina ya ufisadi, na kila mmoja kushughulika katika kuitengeneza jamii kwa kuamrisha mema na kukataza maovu. Kwa mara nyingine Qur’ani inawashika mikono Waislamu na kwenda nao kwenye kumbukumbu za kihistoria ili wajikumbushe humo ni namna gani hapo mwanzo walivyokuwa wachache, madhaifu na masikini na hatimaye kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya Dini yao na dunia yao. Kupitia somo hili la historia huenda wakafaidika nalo na kujizatiti, ili wafikie hatua kama walizofikia mwanzo. Anasema Mwenyezi Mungu: “Na kumbukeni mlipokuwa wachache, mkionekana wadhaifu katika nchi; mkawa mnaogopa watu wasiwanyakue.” Hapa Mwenyezi Mungu anatupa taswira ya hali ya uchache na unyonge waliokuwa nao Waislamu, kiasi kwamba walikuwa kama sufi inayopeperuka angani, na adui alikuwa na uwezo wa kuwanyakua wakati wowote autakao yeye. Hivyo ndivyo walivyokuwa Waislamu katika mji wa Makka kabla ya kuhamia Madina pamoja na Mtume (s.a.w.w.), na pia hata baada ya kuhamia Madina kwani kulikuwa na nguvu kubwa za kiadui zilizokuwa zimewazunguka, kama vile Warumi na Wafursi. Aya inamalizia kutaja malipo mazuri yanayotokana na misimamo yao thabiti katika kutetea haki na kupinga dhulma ya aina yoyote ile: “Akawapa makao na akawatia nguvu kwa nusura Yake na akawapa riziki njema ili mpate kushukuru.”
231
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 231
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI NA SABA
َ الر ُس َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ول َو َت ُخونُوا أَ َما َنا ِت ُك ْم َّ ين آ َمنُوا اَل َت ُخونُوا اللهََّ َو ََّاعلَ ُموا أَنَّ َما أَ ْم َوالُ ُك ْم َوأَ ْو اَل ُد ُك ْم ِف ْت َن ٌة َوأَ َّن الله َ َوأَ ْنتُ ْم َتعْلَ ُم ْ ون َو ِع ْن َد ُه أَ ْج ٌر َع ِظي ٌم “Enyi mlioamini! Msimfanyie hiyana Mwenyezi Mungu na Mtume na mkahini amana zenu na hali mnajua. Na jueni kwamba mali zenu na watoto wenu ni fitna. Na hakika kwa Mwenyezi Mungu yako malipo makubwa.” (Qur’ani; 8:27-28)
SABABU YA KUTEREMKA Kuna Riwaya mbali mbali zinazoelezea sababu ya kuteremka Aya mbili hizi, miongoni mwa hizo ni Riwaya iliyopokewa kutoka kwa Imamu al-Baqir na Imamu as-Sadiq (a.s.) ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliwaamrisha Waislamu wawazingire Mayahudi wa ukoo wa Bani Quraydha. Mzingiro ulipotimiza siku ishirini na moja, Mayahudi hao walilazimika kutaka suluhu, na pendekezo lao ni kukubali waruhusiwe wahame kutoka katika mji wa Madina na badala yake wakaishi katika mji wa Sham (Syria), lakini Mtume (s.a.w.w.) alilikataa pendekezo lao, na kuwaambia: Wanalazimika kukubaliana na hukumu itakayotolewa na Sa’d ibn Muadh, lakini wao walimuomba Mtume (s.a.w.w.) awapelekee Abu Lubaba (Sahaba wa Mtume (s.a.w.w.) ili waonane naye. Huyu (Abu Lubaba) alikuwa na mahusiano ya kiurafiki pamoja nao, kwani hata baadhi ya mali zake na watu wa familia yake walikuwa kwa hao Mayahudi. Mtume (s.a.w.w.) aliwakubalia ombi lao na Abu Lubaba alipelekwa kwao. Baada ya kuwasili walimuuliza: “Je, kuna maslahi yoyote ikiwa watakubali hukumu ya Sa’d ibn Muadh?” Abu Lubaba aliashiria katika shingo yake, akimaanisha ikiwa watakubali kuhukumiwa na Sa’d basi wote watauwawa. Hapo Jibril (a.s.) aliteremka kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumpasha habari ya yale aliyoyasema Abu Lubaba. Baada ya Abu Lubaba kutafakari alichokifanya alisema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, nitabaki hapa kwani ninajua ya kwamba nimemfanyia khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Baada ya hapo Aya hizi ziliteremka na kufichua khiyana yake dhidi ya Uislamu. Abu Lubaba alirudi kwa Mtume (s.a.w.w.) akiwa ni mwenye kujutia kitendo chake
232
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 232
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
hicho huku akiwa amebeba kamba na kwenda kujifunga mwenyewe kwenye moja ya nguzo za msikiti wa Mtume (s.a.w.w.), huku akisema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Sitokula wala kunywa chochote mpaka nifariki dunia au Mwenyezi Mungu anisamehe.” Abu Lubaba alibakia katika hali hiyo kwa muda wa siku saba bila ya kula wala kunywa, mpaka akapoteza fahamu, na hapo Mwenyezi Mungu alimkubalia toba yake. Waislamu walimpelekea habari ya kusamehewa kwake, lakini aliapa kwa Mwenyezi Mungu ya kwamba hatoifungua kamba aliyojifunga mpaka aendewe na Mtume (s.a.w.w.) na yeye Mtume (s.a.w.w.) ndio amfungue. Mtume (s.a.w.w.) alimwendea na akaifungua kamba, baada ya kufunguliwa kamba alisema: Ili toba yangu ikamilike, inanipasa niuhame mji wa watu wangu, mji ambao nimemuasi Mwenyezi Mungu ndani yake, na mali yangu yote niitoe sadaka, Mtume (s.a.w.w.) alimwambia: Inatosha kutoa sadaka theluthi moja tu ya mali yako.109
MAELEZO Sababu Za Khiyana:Kwanza kabisa Mwenyezi Mungu anawaelekea Waumini na kuwaambia: “Enyi mlioamini! Msimfanyie hiyana Mwenyezi Mungu na Mtume.” Kumukhini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni kutoa siri za kivita za Waislamu kwa maadui wa Uislamu, au kuwatia nguvu maadui wakati wa kupambana nao, au katika hali ya ujumla, nayo ni kuacha mambo ya wajibu na kufanya yaliyo haramu, kwani imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas ya kwamba: “Kuacha jambo miongoni mwa mambo ya wajibu katika Uislamu ni kumfanyia khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Aya inaendelea kusema: “Na mkahini amana zenu.” Maana ya ‘Kukhini’ ni kujizuia kumpa mtu haki yake baada ya kuahidi kufanya hivyo, kwa hivyo neno hili ni kinyume cha neno ‘Uaminifu’. Mara nyingi neno ‘Uaminifu’ huhusishwa na uaminifu wa kimali, lakini katika matamshi ya Qur’ani neno hili linajumuisha uaminifu katika vipengele vyote vya maisha ya kijamii, kama vile kisiasa, kitabia n.k. Kwa hivyo basi ardhi ya Kiislamu ni amana ya Mwenyezi Mungu aliyoiweka kwenye mikono ya Waislamu. Zaidi ya hayo, mafunzo ya Qur’ani Tukufu yanazingatiwa kwamba ni amana iliyo kubwa sana, kwani baadhi ya wanazuoni wamesema: Amana ya Mwenyezi Mungu ni maamrisho Yake na amana ya Mtume (s.a.w.w.) ni Sunna zake na amana ya Waumini ni mali zao na siri zao. Kwa kweli kutotekeleza amana ni miongoni mwa mambo maovu sana na dhambi ichukizayo mno kwa Mwenyezi Mungu, kwani mwenye kuifanyia khiyana amana 109
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 5, Uk. 401 233
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 233
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
anakuwa ni miongoni mwa wanafiki, kama ilivyopokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) pale aliposema:
إذا ح ّدث كذب وإذا وعد أخلف وإذا:عالمة المنافق ثالث .أئتمن خان “Alama za mnafiki ni tatu: Pindi anapozungumza husema uongo, na anapoahidi hukhalifu, na anapoaminiwa hufanya khiyana.”110
Uislamu unazingatia mtu kutomfanyia khiyana mwenzake ni miongoni mwa haki za msingi za kijamii, hata kama mwenye amana sio mwislamu, haifai kuikhini amana yake. Aya inaendelea Kusema: “Na hali mnajua.” Ibara hii inamaanisha ya kwamba huenda mtu akafanya khiyana bila ya kujua ya kwamba hilo analolifanya ni khiyana, lakini msiba ni mtu kufanya khiyana na ilhali anajua ya kwamba hili alifanyalo ni khiyana. Mfano wa mtu kama huyo ni kama Abu Lubaba, ambaye alimukhini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa kujua kwamba alitendalo ni tendo la khiyana, hakutenda kwa ujinga, bali ni kwa ajili ya kupenda kwake mali na watoto kupita kiasi na kutaka kujinufaisha yeye binafsi. Aya ya mwisho inawatahadharisha Waislamu dhidi ya vitu ambavyo ni vyenye kupita. Ikiwa pupa yao itakuwa ni kujikusanyia vitu hivyo tu, basi watakuwa pia wameifanyia khiyana jamii yao na kuiweka pahala pabaya, inasema: “Na jueni kwamba mali zenu na watoto wenu ni fitna.” Mali na watoto ni miongoni mwa vipimo vya kupimiwa imani ya Muumini, anaangaliwa ni namna gani imani yake itaweza kuwa thabiti ikiwa atavimiliki viwili hivi au atavikosa. Jamii nyingi za wanadamu zinapima nafasi ya mwanadamu na heshima yake katika jamii kwa kuangalia vitu hivyo, kwa hivyo mwanadamu anatahadharishwa dhidi ya kuingia katika maasi kwa lengo la kutaka kuwafurahisha watoto wake, au kujiingiza katika uchumi wa haramu ili kutaka kuzidi kujilimbikizia mali. Ni watu wangapi wanaonekana wakijilazimisha na wajibu wa Mwenyezi Mungu na hata mambo ya Sunna, lakini mara tu baada ya kubarikiwa mali hujitenga na kila jema na badala yake hujiingiza katika starehe za haramu na kujisahaulisha kila kitu cha kheri. Ama watoto bila ya shaka ni kitulizo cha moyo na kifurahisho cha macho. Pia utawashuhidia watu wengi wakishikamana na mafunzo ya Dini na kujipamba na tabia njema, lakini utawaona wanaanza kujiepusha na maelekezo ya Dini yao pindi tu wanapopingana na maslahi ya watoto wao, mapenzi ya kupita kiasi kwa watoto wao 110
Bukhariy, Sahihul Bukhariy, Jz.3, Uk.162 234
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 234
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
huwafanya wajihalalishie haramu na wajiharamishie halali! Kwa hivyo inatupasa kushikamana vyema na mafunzo ya Dini yetu hasa pale tunapoona dunia imetupa uso kwa kuneemeshwa neema mbali mbali, na ikiwa bado hatujamilikishwa neema hizo, basi tusitumie njia za haramu katika kuzitafuta, tutambue kwamba kuwa na neema ni mtihani na pia kuzikosa ni mtihani. Ni wangapi walioteleza kwa sababu ya neema walizoneemeshwa na kuwa ni wenye kulaaniwa milele! Ni juu yetu kujirekebisha haraka pale tulipokosea, kama alivyofanya Abu Lubab, na ikiwa mali ni sababu ya mtu kuingia katika mtihani mgumu, basi jambo la msingi ni kuitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu ili ilete manufaa kwa jamii yote badala ya kuwadhuru. Ibara ya mwisho katika Aya hii inatoa habari njema kwa kila mwenye kufaulu katika mtihani wa mali na watoto: “Na hakika kwa Mwenyezi Mungu yako malipo makubwa.� Namna yoyote mapenzi ya kuwapenda watoto yanavyokuwa makubwa na namna mali inavyopendwa sana, basi kwa hakika malipo ya Mwenyezi Mungu ni mengi na makubwa kuliko kitu chochote kile.
235
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 235
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI NA NANE
ََّيا أَُّي َها ال َ ين آ َمنُوا إ ْن َتتَّ ُقوا اللهََّ َي ْج َع ْل لَ ُك ْم ُف ْر َقا ًنا َوي َ ُك ِّف ْر َع ْن ُك ْم ذ ِ ِ ْ ْ َُّلله ُ ْ َسيِّ َئا ِت ُك ْم َو َي ْغ ِف ْر لَ ُك ْم َوا ذو ال َف يم ظ ع ال ل ض َ ِ ِ ِ
“Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atawajaalia upambanuzi, na atawafutia makosa yenu na atawasamehe; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu.” (Qur’ani; 8:29)
MAELEZO Uchamungu na Upambanuzi: Aya hii kama zilivyo baadhi ya Aya nyingine zilizotangulia, imekuja kutoa msisitizo juu ya kumcha Mwenyezi Mungu, huku ikieleza faida mbalimbali zitokanazo na uchamungu, faida hizo ni kama zifuatazo: 1.
Uwezo wa hali ya juu wa kupambanua haki na batili, kama Aya inavyoeleza: “Enyi mlioamini! mkimcha Mwenyezi Mungu atawajaalia upambanuzi.”
Licha ya ufupi wa ibara hii, lakini inabeba maana kubwa, ni ibara ambayo inafafanua mustakbali wa mwanadamu, mustakbali ambao umezungukwa na changamoto mbali mbali. Kwa hiyo ikiwa mwanadamu hakujipanga vizuri na kutambua namna ya kukabiliana nazo, bila ya shaka atatumbukia katika dimbwi. Njia muhimu katika kukabilana nazo ni utambuzi wa haki na batili, wema na uovu, kumtambua rafiki na adui, kutambua faida na madhara, kutambua yanayoleta furaha na karaha. Pindi mwanadamu atakapoelewa vyema mambo haya, bila ya shaka yoyote atafikia katika lengo la kuletwa kwake katika dunia hii. Tatizo kubwa wanalokabiliana nalo watu wengi ni kutoitambua batili, kutomfahamu adui na kutoitambua njia sahihi ya uongofu. Kutokana na hali hii mwanadamu anahitaji uangalifu wa hali ya juu na kuchukua hatua madhubuti katika kujielimisha. Aya inaeleza bayana kwamba haya yataweza kufikiwa iwapo mtu atashikamana na uchamungu. Sasa ni vipi uchamungu humfanya mtu kuwa mpambanuzi? Huenda 236
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 236
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
jawabu la suala hili likawa gumu kwa baadhi ya watu, lakini kwa mwenye kufikiri ataona ni namna gani kulivyo na mafungamano kati ya uchamungu na upambanuzi, na katika kuweka bayana jambo hili tunasema: Kwanza: Akili ya mwanadamu ina uwezo wa kutosha wa kufahamu uhalisia wa mambo, lakini pupa ya kupenda mali, watoto, wanawake, madaraka, ubinafsi na choyo vimekuwa ni vikwazo na vizuizi vilivyotanda katika akili ya mwanadamu, kwa hivyo katika hali hii ni vigumu kwake kuweza kupambanua baina ya haki na batili. Ama atakapoisafisha akili yake kwa maji ya uchamungu wakati huo itakuwa rahisi kwake kutambua mwanga wa haki. Pili:Tunaelewa ya kwamba ufanisi wa jambo lolote unatokana na kushikamana na haki, na kila mtu anapojikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, basi miale ya nuru iliyo mikamilifu itamuangazia katika maisha yake, na kwa hivyo maarifa yoyote atakayoyapata yatakuwa chanzo chake ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kila mwanadamu anapoendelea katika kumcha Mola Wake na kuacha maasi, basi nafsi yake itayeyuka katika nafsi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akifikia katika hali hiyo ataweza kupata elimu na maarifa katika njia isiyokuwa ya kawaida. Kwa maelezo mengine ni kwamba, moyo wa mwanadamu ni kama kioo, na ule Uungu wa Mwenyezi Mungu ni kama jua lenye kung’ara, pindi kioo cha moyo wake kitakapochafuka hakitoonesha mwanga wa jua, lakini atakapokisafisha kwa kutumia uchamungu na kuondosha takataka, hapo mwanga wa jua utapenya ndani ya kioo. Ndio maana tunasoma katika historia kuwepo kwa baadhi ya watu waliokuwa na uwezo mkubwa wa kielimu bila ya kuipata elimu hiyo kwa njia ya kufundishwa na wanadamu wenzao. Aina hii ya kutambua mambo pia imeelezwa katika Aya ifuatayo:
ْ َواتَّ ُق ُ وا اللَهّ َويُ َعلِّم … ُّك ُم اللُه “Na mcheni Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atakufundisheni…” (Qur’ani; 2:282)
Na imepokewa katika Hadithi maneno yasemayo:
المؤمن ينظر بنوراهلل “Muumini huangalia kwa nuru ya Mwenyezi Mungu.”111
Na Imamu Ali (a.s.) naye anasema: 111
Suyutiy, Durrul Manthur, Jz.4, Uk.103 237
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 237
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
.أكثر مصارع العقول تحت بروق المطامع “Matatizo mengi ya akili yako chini ya kivuli cha tamaa.”112
2.
Kutokana na upembuzi wa kiakili tunaweza kufahamu mafungamano madhubuti kati ya uchamungu na utambuzi wa mambo, kwani jamii inayoshikilia ufisadi na uovu na huku vyombo vya habari vikinyanyua sauti yake katika kuushabikia na kuutangaza uovu huo, inakuwa vigumu kwa watu wengi kuweza kupambanua kati ya haki na batili, uzuri na ubaya, na pia kutambua natija ya uovu huo, kwa hivyo sababu kubwa inayopelekea hayo ni ukosefu wa uchamungu.
Mfano mwingine, kama familia itakuwa si yenye kumcha Mwenyezi Mungu, na watoto wadogo wa familia hiyo wakawa wanakulia katika kutenda mambo maovu, itawawia vigumu siku za mbeleni kuweza kupambanua kati ya jema na baya, kwani kubobea katika maovu kunawasababisha watu kutokuwa na uweledi wa mambo na fikra nzuri hata kama watakuwa wamepiga hatua hatika maendeleo ya kiviwanda na mengineo. Kwa mujibu wa maelezo tuliyo yaeleza ni wazi kwamba jambo lolote linalopelekea kukosekana kwa uchamungu ni mojawapo ya aina ya upofu na ukosefu wa akili, ndio leo ikawa tunashuhudia mataifa yaliyoendelea kisayansi na kiteknolojia ndio mataifa yaliyo na matatizo makubwa ya kijamii na mmong’onyoko wa kimaadili. Kwa kweli uchamungu hauko kwenye matendo tu, bali pia unatakiwa uwepo katika fikra na akili, kwa maana kwamba mtu afikiri vyema pamoja na kuwa na dalili tosha juu ya mambo anayoyaitakidi na kuyaamini. Njia hii ya kufikiri ndio pekee inayotoa natija nzuri na kwa haraka sana, kwani makosa mengi ya kumuasi Mwenyezi Mungu hufanywa na wale wasiozitumia bongo zao katika kufikiri kuliko sahihi na kuwa na dalili za wazi. Kuna jambo ambalo linahitaji mazingatio, jambo hilo ni kuwepo baadhi ya Waislamu wanaodhani ya kwamba uchamungu ni ile tu hali ya kujilazimisha na usafi wa kiwiliwili na mavazi na kujiweka mbali na mambo ya kijamii na kunyamaza kwa kila ovu lifanyikalo mbele yake. Kwa kweli fikra ya aina hii ni miongoni mwa mambo yanayoirudisha nyuma jamii ya Kiislamu, kwani uchamungu huu hauzai maarifa na uoni sahihi wala haupambanui kati ya haki na batili. Baada ya kubainika malipo yanayotokana na uchamungu, turejee tena katika kutoa tafsiri iliyobakia na matunda mengine yatokanayo na uchamungu. Aya inaeleza ya kwamba licha ya uwezo wa kuweza kupambanua kati ya haki na batili 112
Ibn Abil Hadidiy, Sharhu Nahjul Balaghah, Jz.19, Uk.41 238
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 238
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
kwa mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, pia miongoni mwa matunda yake ni kupata msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kufutiwa madhambi: “Na atawafutia makosa yenu na atawasamehe.” Na kuna faida nyingine iliyo kubwa na ambayo haijui isipokuwa Mwenyezi Mungu peke Yake: “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu.” Haya ndio matunda manne yanayotoka katika mti wa uchamungu, ni dhamana kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuweza kuyapata kwa kila anayejitolea kwa dhati kabisa katika kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
239
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 239
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA AROBAINI NA TISA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ يرا ً ين آ َمنُوا إِ َذا لَ ِقيتُ ْم ِف َئ ًة َف ْاثبُتُوا َو ْاذ ُك ُروا اللهََّ َك ِث َ ون َوأَ ِطيعُوا اللهََّ َو َر ُسولَ ُه َو اَل َت َن َ لَ َعلَّ ُك ْم تُ ْفلِ ُح از ُعوا َف َت ْف َشلُوا َ الص ِاب ِر ين َو اَل َت ُكونُوا ُ َو َت ْذ َه َب ِر َّ اص ِب ُروا إِ َّن اللهََّ َم َع ْ يح ُك ْم َو َ َ ص ُّد َ َكالَّ ِذ ون َع ْن ُ اس َو َي ِ َّار ِه ْم َبط ًرا َو ِر َئا َء الن ِ ين َخ َر ُجوا ِم ْن ِد َي ٌ ون ُم ِح َ ُيل اللهَِّ َواللهَُّ ِب َما َي ْع َمل يط ِ َس ِب “Enyi mlioamini! Mnapokutana na jeshi, basi kazaneni, na mumkumbuke Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufaulu. Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wala msizozane, msije mkavunjika moyo na zikapotea nguvu zenu, na subirini; Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri. Wala msiwe kama wale waliotoka majumbani mwao kwa fahari na kujionyesha kwa watu, na kuzuilia njia ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ameyazunguka wanayoyafanya.” (Qur’ani; 8:45-47)
MAELEZO Wafasiri wanasema: “Baada ya Abu Sufiyani kuweza kuuwokoa msafara wa kibiashara wa bidhaa za Makuraishi dhidi ya mashambulizi ya Waislamu, alipeleka mjumbe kwa Makuraishi ili kuwataka warejee na wasiendelee na safari yao ya kuelekea katika kitongoji cha Badri, lakini Abu Jahli alikataa ombi hilo na kuazimia kuendelea na safari mpaka watakapofika Badri.” Kabla ya vita vya Badri, sehemu hiyo (Badri) ilikuwa ni kituo kikubwa cha kibiashara cha Waarabu. Ilikuwa ni kawaida yao kila mwaka kukutana mara moja kwa muda wa siku tatu. Mbali na biashara, katika siku hizo tatu walikuwa wakichinja ngamia na kuwala na huku wakinywa aina mbali mbali za ulevi na wanawake wakitumbuiza kwa nyimbo mbalimbali kiasi cha kunyanyua sauti zao na kuweza kufika kwenye baadhi ya vijiji vya karibu kwa lengo la kudhihirisha uwezo na nguvu zao. Lakini vilipotokea vita vya Badri walinyweshwa kinywaji cha mauti badala ya ulevi, na wanawake wao wakawa wanalia kwa maombolezo badala ya kuimba!113 113
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.4, Uk.449 240
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 240
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
Aya zilizoko mbele yetu zinazungumzia hali hii, na kuwaonya Waislamu kutotenda mfano wa matendo haya, na huku ikiwabainishia mafunzo wanayotakiwa kujifunza wanapokuwa katika mapambano dhidi ya maadui, mafunzo hayo ni kama yafuatavyo: Kwanza: Aya inawataka Waumini kuwa katika hali ya ukakamavu wa hali ya juu pindi wakutanapo na maadui: “Enyi mlioamini! Mnapokutana na jeshi, basi kazaneni.” Aya inabainisha ya kwamba moja kati ya alama za imani ya kikweli kweli ni kuwa imara wakati wa kukabiliana na maadui. Pili: Kumkumbuka Mwenyezi Mungu tena kwa wingi mno: “Na mumkumbuke Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufaulu.” Bila ya shaka Aya haimaanishi kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa njia ya ulimi tu, bali pia kwa akili na kwa fikra, kwa kufikiria ujuzi Wake, uwezo Wake usio na mipaka na rehema Zake zilizo kunjufu. Ukumbukaji wa aina hii unachangia katika kuwahamasisha wapiganaji wa Kiislamu, kwa kuhisi uwepo wa Nguvu inayowasaidia; Nguvu isiyoshindwa, na hata kama mmoja wao atauwawa atarajie kupata malipo makubwa kutoka Kwake, kwani rehema Zake ni pana sana. Kwa hivyo moja kati ya sababu za kuwashinda maadui ni kwa Waislamu kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwani jambo hili linaleta utulivu wa nafsi, ujasiri, nguvu na uwezo wa hali ya juu. Zaidi ya hayo, ni kwamba kumkumbuka Mwenyezi Mungu kunaondoa mapenzi ya kupenda zaidi mali, mke na watoto kuliko Mwenyezi Mungu, bali huondoa kila jambo linalodhoofisha safu ya Waislamu kama Imamu Zaynul-Abidiin (a.s.) anavyosema katika dua ijulikanayo kwa jina la dua ya kuwaombea watu wa mipakani:
وامح عن,وأنسهم عند لقائهم العد ّو ذكر دنياهم الخ ّداعة . واجعل الجنّة نصب أعينهم,قلوبهم خطرات المال الفتون
114
“Wakati wanapokutana na adui wasahaulishe kumbukumbu ya dunia yao yenye kudanganya, na wafutie hatari ya mali yenye kufitini kutoka nyoyoni mwao, na ifanye Pepo kuwa mbele ya macho yao.”
Tatu: Kutii amri ya kiongozi: “Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Utiifu kwa kiongozi hasa wakati wa mapambano ni moja kati ya sababu kubwa zinazopelekea ushindi, kwani bila ya kuwepo kiongozi mwenye kusikilizwa ni vigumu mno kufikia katika lengo linalokusudiwa. Na lau si kwa Waislamu kusalimu 114
Imamu Zaynul Abidin (a.s.), Swahifatu Sajjadiyah 241
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 241
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
amri kwa Mtume (s.a.w.w.) katu wasingeweza kumshinda adui, hasa kutokana na hali ya jeshi la Waislamu lilivyokuwa, ikilinganishwa na jeshi la adui. Nne: Kuwa kitu kimoja katika mapambano, na isiwe kila mmoja na lake na kusababisha mvutano na kutoelewana: “Wala msizozane, msije mkavunjika moyo na zikapotea nguvu zenu.” Mizozo na mitafaruku mbele ya adui ni udhoofishaji mkubwa wa jeshi na kumpa ushindi asioutolea jasho. Tano:Aya inatoa wito mwingine kwa Waislamu kuwa na msimamo thabiti katika hali mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo hali ya kukabiliana na adui: “Na subirini; Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri.” Hapa tunaweza kusema ya kwamba, tofauti iliyopo kati ya amri ya kwanza isemayo: “Enyi mlioamini! Mnapokutana na jeshi, basi kazaneni,” na amri hii ya tano ni kwamba, amri ya kwanza inalenga katika hali ya nje (kiwiliwili) kwa maana mpiganaji aoneshe uimara wa nguvu zake na uwezo wake mbele ya adui. Ama kutakiwa kuwa na msimamo na subira, mambo haya yanahusiana na mambo ya ndani ya nafsi ya mwanadamu (mambo ya kiroho). Sita:Mwisho kabisa Aya inawataka Waislamu wajiepushe na vitendo vya kipuuzi na visivyo na faida, na wasiwe ni watu wa kusema maneno makali yanayotofautiana na matendo, kwani huo si mwenendo wa Kiislamu, bali ni mwenendo uliokuwa ukifanywa na Abu Sufiyani na jeshi lake: “Wala msiwe kama wale waliotoka majumbani mwao kwa fahari na kujionyesha kwa watu, na kuzuilia njia ya Mwenyezi Mungu.” Kwa vile jeshi la washirikina wa Makkah lililokuwa likiongozwa na Abu Sufiyani halikuwa na lengo zuri, Mwenyezi Mungu aliliangamiza kwa kupitia mikono ya Waislamu na wengine kuwa mateka, ikawa ni mayowe na vilio badala ya nyimbo, na kububujikwa na machozi machoni mwao badala ya ulevi uliokuwa ukiingizwa vinywani mwao. Aya inahitimisha kwa ibara isemayo: “Na Mwenyezi Mungu ameyazunguka wanayoyafanya.”
242
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 242
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين آ َمنُوا اَل َتتَّ ِخ ُذوا آ َبا َء ُك ْم َوإِ ْخ َوا َن ُك ْم أَ ْولَِيا َء إِ ِن ْاس َت َحبُّوا ْال ُك ْف َر َعلَى الإ ول ِئ َك ُه ُم ٰ َ ُان َو َم ْن َي َت َولَّ ُه ْم ِم ْن ُك ْم َفأ م ي ْ َ ِ ِ َّ َ ون ُق ْل إِ ْن َك َ الظالِ ُم اج ُك ْم ُ ان آ َبا ُؤ ُك ْم َوأَ ْب َنا ُؤ ُك ْم َوإِ ْخ َوانُ ُك ْم َوأَ ْز َو ٌ يرتُ ُك ْم َوأَ ْم َو َ ال ْاق َت َر ْفتُ ُم ار ٌة َت ْخ َش ْو َن َك َسا َد َها َ وها َو ِت َج َ َو َع ِش ُ ض ْو َن َها أَ َح َّب إلَي َ َو َم َسا ِك ُن َت ْر ْك ْم ِم َن اللهَِّ َو َر ُسولِ ِه َو ِج َها ٍد ِفي ِ ْ َّصوا َحتَّىٰ َيأ ِت َي اللهَُّ ِبأَ ْم ِر ِه َواللهَُّ اَل َي ْه ِدي ْال َق ْو َم ُ َس ِبيلِ ِه َف َت َرب َ اس ِق ين ِ ْال َف “Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa mawalii ikiwa wamestahabu kufuru kuliko imani. Na atakayewafanya mawalii katika nyinyi basi hao ndio madhalimu. Sema ikiwa baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali mlizozichuma na biashara mnazohofia kuharibikiwa, na majumba mnayopenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na jihadi katika njia Yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri Yake, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu mafasiki.” (Qur’ani; 9:23-24)
MAELEZO Miongoni mwa sababu zinazoweza kuwafanya Waislamu wasipambane dhidi ya adui yao ni visingizio vya udugu na ujamaa kati yao, na haya yametokea katika historia ya Uislamu kutokana na baadhi ya Waislamu kuwa na ndugu zao wa damu waliokataa kuingia katika Uislamu. Na ilipokuja amri ya kupambana nao kutokana na maudhi yao dhidi ya Waislamu, hao wenye ndugu zao walikuwa wazito kufanya hivyo kwa kuchelea kuja kuwajeruhi au kuwauwa ndugu zao wa damu. Na kwa upande mwingine hao washirikina waliokuwa na undugu na Waislamu ndio waliokuwa wamemiliki uchumi na biashara kubwa kubwa katika mji wa Makkah, kwa hivyo ikiwa watavamiwa na kupigwa vita mali zao zitapotea na kukosa wa 243
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 243
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
kuziendeleza. Na pia Waislamu waliouhama mji wa Makkah walikuwa na nyumba zao huko walizoziacha, hivyo walikuwa wakikhofia ikiwa watawauwa washirikina basi nyumba zao zitavunjwa au kukosa soko pale watakapoamua kuziuza kwa vile washirikina watapoteza mali zao nyingi katika vita au kuamua kusitisha ibada ya Hijja katika mji wa Makkah. Aya hizi mbili zinaangaza hali hii waliokuwa nayo baadhi ya Waislamu, kwa hivyo zinaweka bayana uharamu wa kuwa na mapenzi na watu wanaompinga Mwenyezi Mungu. Aya ya kwanza kati ya hizo inasema: “Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa mawalii ikiwa wamestahabu kufuru kuliko imani.” Baada ya hapo Aya inatoa msisitizo zaidi juu ya jambo hili kwa kusema: “Na atakayewafanya mawalii katika nyinyi basi hao ndio madhalimu.” Kuna udhalimu gani ulio mbaya zaidi wa kuidhulumu nafsi kuliko mtu kuwa na mahusiano na maadui wa haki?! Dhulma ya aina hii si tu kuidhulumu nafsi, bali pia ni kuidhulumu jamii anayoishi nayo. Ama Aya ya pili inaielezea hali hii kwa uwazi zaidi huku ikizidi kutoa msisitizo na vitisho. Aya inamtaka Mtume (s.a.w.w.) awe mkali dhidi ya wale wasiotaka kupigana dhidi ya madhalimu wa kishirikina, inasema: “Sema ikiwa baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali mlizozichuma na biashara mnazohofia kuharibikiwa, na majumba mnayopenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na jihadi katika njia Yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri Yake.” Aya inabainisha wazi kwamba, kuacha kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu ni uasi mkubwa, na hayo hutokea kwa yule aliyeufungamanisha moyo wake na mapenzi ya hali ya juu ya kuipenda dunia na starehe zake. Aya inahitimisha kwa kishindo kingine dhidi ya watu wenye kutengeneza visingizio vya kujizuia na Jihadi kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu mafasiki.” Aya hizi zinaweka bayana uhalisia wa imani sahihi na kuitofautisha na ile imani iliochanganyika na unafiki, kama zilivyotofautisha kati ya Muumini wa kweli na yule mwenye imani dhaifu, kwa kubainisha ya kwamba ikiwa vitu hivi vinane,ambavyo vinne vya kwanza vinahusiana na mafungamano ya kindugu, jamaa, wazazi, watoto, na wake, na cha tano kikihusiana na jamii, na cha sita kinahusiana na masuala ya mali, cha saba kinahusiana na biashara na uchumi, na cha nane kinahusiana na makazi, basi ikiwa vitu hivi vilivyotajwa hapo juu katika Aya ni vyenye thamani zaidi na vitukufu zaidi na kupendwa zaidi na Mwislamu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kupigania Dini ya Mwenyezi Mungu, na kutekeleza amri Zake nyingine, basi kwa hakika mtu wa aina hiyo atakuwa na upungufu wa imani. Kwa hakika imani ya kweli 244
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 244
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
ni kujitoa muhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bila ya kusitasita hata kama mtu ataikosa dunia na vilivyomo ndani yake, na ambaye hatokuwa tayari kuwakosa ndugu na jamaa au anavyovimiliki kwa ajili ya kuisimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu, basi atakuwa ameidhulumu nafsi yake na jamii yake, kwani hayo anayoyachelea kufikwa nayo yatamfika kutokana na kujizuia kwake kushiriki katika Jihadi, kwani umma unaoacha kupambana dhidi ya madhalimu na mafisadi, hatima yake huingia katika udhalili na madhila makubwa.
ANGALIZO 1.
Maelezo tuliyoyatoa yanayohusiana na Aya hizi mbili hayana maana ya kukata mahusiano ya kindugu kati ya wanafamilia hata kama baadhi yao watakuwa si Waislamu, au kutochukua tahadhari juu ya masuala ya kimali na uchumi, bali makusudio yake ni kwamba vitu hivyo visiwe ni vikwazo vya utekelezaji wa matakwa ya Mwenyezi Mungu, hasa panapowajibika kuingia katika mapambano dhidi ya adui, na kama ikiwa Mwislamu hajakabiliwa na hali inayomlazimu kupambana na ndugu zake au kuachana na mali zake na badala yake kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu, hapo analazimika kuyatenda yote, kwa maana ya kushikamana na mafunzo ya Mwenyezi Mungu na kuwaunga ndugu zake na kushughulikia vyema biashara yake. Katika Suratu Luqman tunashuhudia ni namna gani mtu anavyotakiwa kuamiliana na wazazi wake ikiwa ni washirikina katika hali ya amani, Mwenyezi Mungu anasema:
َ اه َد َ َوإِ ْن َج ْس لَ َك ِب ِه ِع ْل ٌم َف اَل َ اك َعلَىٰ أَ ْن تُ ْش ِر َك ِبي َما لَي ً ْر َ وفا َواتَّب ْع َسب ُّ اح ْب ُه َما ِفي اب ُ الد ْن َيا َمع َ يل َم ْن أََن َ تُ ِط ْع ُه َما َو ِ ص ِ ِ ُ إلَ َّي ثُ َّم إلَ َّي َم ْرجع َ ُُك ْم َفأَُنبِّئُ ُك ْم ِب َما ُك ْنتُ ْم َت ْع َمل ون ِ ِ ِ “Na kama wakikushikilia kunishirikisha Mimi na yale ambayo huna ilimu nayo basi usiwatii, na kaa nao kwa wema duniani, na fuata njia ya yule anayerejea Kwangu; kisha hakika marejeo yenu ni Kwangu Mimi, Nami nitawaambia mliyokuwa mkiyatenda.” (Qur’ani; 31: 15).
245
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 245
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
2.
Yaliyokuja katika Aya hizi mbili hayawahusu watu waliopita peke yao, bali pia yanawahusu Waislamu wote wa kila zama, ikiwa Waislamu watafikia hali ya kuyatanguliza maslahi yao binafsi mbele ya matakwa ya Mwenyezi Mungu, na kuwa na mapenzi zaidi na ndugu zao na mali zao kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi mustakbali wao utakuwa mbaya, kwani watanyang’anywa urithi wao na ustaarabu wao, na maisha yao yatakuwa ndani ya mikono ya wageni na hivyo kukosa uhuru wa kujiamulia mambo yao. Kwa kweli watu kufikia katika hali hii ni kukosa ladha na utamu wa maisha. Kwa hiyo inatupasa kuyapandikiza mafunzo yanayopatikana katika Aya hizi mbili katika vifua vya vijana wa Kiislamu na iwe ndio nembo yetu, na bila ya kusahau kupandikiza roho ya kujitoa muhanga katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa lengo la kulinda mila na tamaduni za Dini yetu.
246
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 246
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI NA MOJA
َ ين آ َمنُوا إِنَّ َما ْال ُم ْش ِر ُك َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ س َف اَل َي ْق َربُوا ْال َم ْس ِج َد ٌ ون َن َج ُ ف يُ ْغ ِن َ ْال َح َرا َم َب ْع َد َعا ِم ِه ْم َه َٰذا َوإِ ْن ِخ ْفتُ ْم َعيْلَ ًة َف َس ْو يك ُم اللهَُّ ِم ْن ْ َف ْ ين اَل ي َ ُُؤ ِمن َ ضلِ ِه إِ ْن َشا َء إِ َّن اللهََّ َعلِي ٌم َح ِكي ٌم َقا ِتلُوا الَّ ِذ َِّون ِبالله َ ُح ِّر ُم ون َما َح َّر َم اللهَُّ َو َر ُسولُ ُه َو اَل َ َو اَل ِب ْال َي ْو ِم الآْ ِخ ِر َو اَل ي ُ ى يُع َ ين ْال َح ِّق ِم َن الَّ ِذ َ ون ِد َ َُي ِدين ْطوا ْال ِج ْز َي َة ٰ َّاب َحت َ ين أُوتُوا ْال ِك َت َ اغ ُر ون َ َع ْن َي ٍد َو ُه ْم ِ ص “Enyi Mlioamini! Hakika washirikina ni najis, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakitifu baada ya mwaka wao huu. Na kama mkihofia umasikini, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila Yake akitaka. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima. Piganeni na wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho wala hawaharamishi aliyoharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, wala hawashiki dini ya haki, miongoni mwa waliopewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa mkono hali wametii.” (Qur’ani: 9:28-29)
MAELEZO Aya ya kwanza inaelezea moja kati ya mambo manne aliyokwenda nayo Imamu Ali (a.s.) kwa washirikina wa Makkah katika mwaka wa tisa wa Hijiriya. Jambo hilo ni kwa washirikina kutoukaribia Msikiti Mtukufu wa Makkah. Hekima ya katazo hili ni kwamba wao ni najisi: “Enyi Mlioamini! Hakika washirikina ni najis.” Suala linalojitokeza hapa ni hili, je Aya hii ni dalili juu ya unajisi wa washirikina kwa mtazamo wa kifiqhi au si hivyo? Kuhusiana na jawabu la suala hili, kuna kauli nyingi zilizosemwa na wanachuoni wa elimu ya fiqhi na wafasiri wa Qur’ani, lakini kabla hatujaelezea makusudio yake, basi kwanza na tuanze kuchambua maana ya neno ‘Najsi.’ Raghib Asfahani anasema: “Neno Najasatu na Najsu yanamaanisha kila aina ya uchafu, na huo uchafu uko wa aina mbili: Uchafu unaoonekana na uchafu usioonekana. At-Tabarasiy naye anasema: “Kila anachojiepusha nacho mwanadamu huitwa Najisi. 247
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 247
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa hivyo neno Najsu hutumika katika mambo mengi, hata katika yale ambayo dhahiri yake si najisi, kwa mfano Waarabu huyaita Najisi maradhi ya muda mrefu au yale yasiyo na tiba, na pia mtu mwenye tabia mbaya humwita Najisi.” Kutokana na maana hizi, si sawa kuvihukumu viwiliwili vya washirikina kuwa sawa na kinyesi, damu, ulevi na najisi nyinginezo. Najisi inayokusudiwa ni najisi ya kiroho, kwa hivyo si sawa kutolea dalili Aya hii juu ya unajisi wa nje kwa washirikina, bali inafaa kutafutwa dalili nyingine ikiwa tunataka kuthibitisha hilo.115 Aya inaendelea kwa kuwaambia wale wenye mawazo ya kwamba pindi washirikina watakapoacha kwenda kwenye Msikiti Mtukufu wa Makkah, basi uchumi wao utaporomoka na kuwa mafukara: “Na kama mkihofia umasikini, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila Yake akitaka. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima.” Bila ya shaka ahadi ya Mwenyezi Mungu ilishuhudiwa na Waislamu katika zama za Mtume (s.a.w.w.) kwa vile Uislamu ulienea sehemu mbalimbali za Bara Arabu, kwa hivyo Waislamu wengi waliweza kuingia katika mji wa Makka kwa ibada ya Hijja na Umrah, na kwa hivyo kipato cha wenyeji wa Makka kikaongezeka. Na hali hiyo bado ni yenye kuendelea siku hadi siku, kwani leo tunashuhudia ni namna gani mji huo uliopo katika jangwa lisilo na maji wala chakula, lakini hivi sasa mji ni mji ulionawiri kwa kila aina ya neema na kuwa miongoni mwa vituo vikubwa vya biashara. Aya inaishia kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima.” Ni kwamba kila ambacho Mwenyezi Mungu anakiamrisha hufanya hivyo kutokana na hekima Zake, na anatambua vyema matokeo ya maamrisho Yake iwapo yatatekelezwa au kutokutekelezwa. Wajibu wa Waislamu kwa Ahlul Kitabi: Aya iliyopita imeelezea wajibu wa Waislamu juu ya washirikina, ama Aya ya pili inaelezea wajibu wao juu ya wale waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manasara). Katika Aya hii Uislamu umeweka hukumu ya kati na kati juu ya kuamiliana na watu waliopewa Kitabu ikilinganishwa kati yao na makafiri (washirikina), hii ni kwa sababu mafunzo ya Dini ya kiyahudi na kinasara yanashabihiyana na mafunzo ya Dini ya Kiislamu, isipokuwa kwa upande mwingine wana baadhi ya mambo yanayoshabihiyana na yale ya washirikina. Kutokana na hali hii Uislamu hauruhusu kuwapiga vita wakati ambapo unatoa ruhusa kupambana na washirikina wanaoelekeza mashambulizi yao dhidi ya Waislamu, kwani lengo kubwa ni kuondosha ushirikina katika nchi, na Uislamu unaruhusu kuishi pamoja na wale waliopewa Kitabu, iwapo wataheshimu 115
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 5, Uk.582 248
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 248
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
mipaka yake na kutodhihirisha uadui dhidi ya Waislamu. Miongoni mwa dalili za kuonesha ya kwamba wao wako tayari kuishi kwa amani na usalama pamoja na Waislamu ni kukubali kulipa kiwango fulani cha kodi kwa dola ya Kiislamu kwa kila mwaka. Kinyume na utaratibu huu, Uislamu unatoa ruhusa ya kupambana nao kijeshi, kwanza Aya inasema: “Piganeni na wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho.” Lakini ni namna gani Mayahudi na Manasara hawamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na ilhali kwa dhahiri ya mambo tunawaona wakishuhudia kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na kuamini kuwepo Siku ya Kiyama?Jawabu la suala hili ni kwamba, imani yao imechanganyika na mambo yasiyo sahihi, kwa mfano kuhusiana na imani juu ya Mwenyezi Mungu, wanaamini ya kwamba huyo Mwenyezi Mungu ana mtoto anayeitwa Uzeiru, na Manasara nao wanasema mtoto wake ni Yesu (Nabii Issa (a.s.)). Ama kuhusiana na mambo ya ibada ni kwamba wote kwa pamoja (Mayahudi na Manasara) wanamshirikisha Mwenyezi Mungu kwa kuwaabudu viongozi wao wa dini kwa kule kutaka msamaha wa makosa yao kutoka kwao, hali ya kuwa jambo hili ni stahiki ya Mwenyezi Mungu peke Yake. Ama imani yao juu ya Siku ya Kiyama, ni kwamba wanaitakidi kwamba ufufuo utakuwa ni wa kiroho tu bila ya mwili, kutokana na hali hii ni kwamba imani yao ina kasoro kubwa. Aya inaendelea kubainisha sababu za kupambana nao kwa kusema: “Wala hawaharamishi aliyoharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Neno ‘Mtume wake’ huenda likawa linamaanisha Nabii Musa au Nabii Isa (a.s.) kwani wote kwa pamoja si watekelezaji wa mafunzo mengi waliyokuja nayo hao Mitume, kwani ni wenye kuyafanya mengi yaliyoharamishwa na Manabii hao. Pia neno hilo huenda likawa linamaanisha Nabii Muhammad (s.a.w.w.). Kwa sababu hii Uislamu umetoa ruhusa kukabiliana kwa vile hawamuamini Mwenyezi Mungu ipasavyo na kujihalalishia yale yaliyo haramu. Aya inataja sifa ya tatu ambayo nayo ni sababu ya kupambana nao: “Wala hawashiki dini ya haki.” Ibara hii inajumuisha vipengele vilivyopita, kwani itikadi isiyo sahihi na matendo yanayokwenda kinyume na mafunzao ya Mitume ni kutokuamiliana na Dini ipasavyo, kwani wameacha mengi yanayopasa kufanywa na badala yake wameshikamana na mambo ya haramu. Kwa kuwa kwao katika hali hii, ama wakubali kuingia katika Dini ya Uislamu au wakubali kuishi kwa usalama na amani huku wakilipa kodi kila mwaka.
249
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 249
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI NA MBILI
َ ْيرا ِم َن أ ََّيا أَُّي َها ال َ ين آ َمنُوا إ َّن ْ َ ُان لََي ْأ ُكل َ ون ب ه الر و ار ب ح ال ث ك ذ ُّ ً ْ َ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ َّ َّلله َ أَ ْم َو َّ َ ين َي ْك ِن ُز َ يل ا ِ َوال ِذ َ ص ُّد ون الن ال ُ اط ِل َو َي ِ اس ِب ْال َب ِ ون َع ْن َس ِب ِ َ َّلله َّ ُ ِّ َ يل ا ِ َف َبش ْر ُه ْم ب َع َّ الذ َه َب َو ْال ِف َ ض َة َو اَل يُ ْن ِفقو يم ل أ اب ذ ب س ي ف ا ه ن َ َ ِ ِ ِ ٍ ِ ِ ٍ َ ُ ار َج َهنَّ َم َفتُ ْك َوىٰ ِب َها ِج َب اه ُه ْم َو ُجنُوبُ ُه ْم ْ َي ْو َم ي ِ ُح َمىٰ َعل ْي َها ِفي َن َ ُور ُه ْم َه َٰذا َما َك َن ْزتُ ْم ُ ل ْن ُف ِس ُك ْم َف ُذ َ وقوا َما ُك ْنتُ ْم َت ْك ِن ُز ون ُ َو ُظه ِأ “Enyi mlioamini! Hakika wengi katika watawa na makuhani wanakula mali za watu kwa batili na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu. Na wale walimbikizao dhahabu na fedha na hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi wabashirie adhabu iumizayo. Siku zitakapotiwa katika moto wa Jahannam, na kwazo vitachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao. Haya ndiyo mliyojilimbikizia, basi onjeni yale mliyokuwa mkiyalimbikiza.” (Qur’ani: 9:34-35)
MAELEZO Aya ya kwanza kati ya hizi, inatoa sura halisi ya viongozi wa dini ya kiyahudi na kinasara, viongozi ambao wamejibebesha baadhi ya kazi za Mwenyezi Mungu, kama vile kutoa msamaha wa madhambi kwa watu waliomkosea Mwenyezi Mungu! Kwa hivyo Aya inaweka bayana ya kwamba, kama vile watu hao walivyokosa sifa ya kiungu pia hawana sifa ya kuwa na nafasi katika jamii kutokana na matendo yao ya kuwadhulumu watu mali zao, Aya inasema: “Enyi mlioamini! Hakika wengi katika watawa na makuhani wanakula mali za watu kwa batili na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu.” Aya imeeleza wazi kwamba tabia hii mbaya haiwahusu wote, bali miongoni mwao, na ni wachache tu ndio wenye kujiepusha na kashfa hii ya udhalimu wa mali za waumini wao. Ni namna ipi hiyo ya viongozi wa dini hizo wanavyokula mali za watu kwa dhulma?Jawabu la suala hili tunaweza kulipata katika vipengele vifuatavyo: 1.
Ni kule kuchukua mishahara kwa kazi ya kuwapotosha watu, kwani huwa wanayaficha yale waliyokuja nayo Nabii Musa (a.s.) kupitia Taurati na Na250
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 250
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
bii Isa (a.s.) kupitia Injili. Wanafanya hivyo kwa lengo la kuwawekea watu vizuizi vya kuitambua Dini ya kweli ya Uislamu na huku wakilinda maslahi yao ya kidunia kama Qur’ani ilivyoashiria kwa kusema:
َ َ ُاب بأَ ْيديه ْم ثُ َّم َي ُقول ْ ُون َّْل لِل ٌ َف َوي ْ ين َي ُ َ َ َ ت ك ال ب ت ك ذ َ َِّون َٰهذا ِم ْن ِع ْن ِد الله ِ ِ ِ ِ ِ َ ٌ ًَ َ ا ْ َ ٌَ َ يه ْم َو َويْل ل ُه ْم ِ لَِيش َت ُروا ِب ِه ث َم ًنا قلِيل َف َويْل ل ُه ْم ِم َّما ك َت َب ْت أ ْي ِد َ ِم َّما َي ْك ِسب ُون “Basi ole wao wanaoandika Kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachukue kwacho thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao. Na ole wao kwa yale wanayoyachuma.” (Qur’ani; 2:79)
ْ َُّين َي ْكتُ ُم َ َ َ لله َ اب َو َي ْش َت ُر َٰ إِ َّن الَّ ِذ ون ِب ِه َث َم ًنا ِ ون َما أ ْن َزل ا ِم َن ال ِك َت َ ُ ًَ ا ْ ُ ُ َُُّكلِّ ُم ُه ُم الله ُ َّا َ ار َو اَل ي َّ َ الن ل إ م ه ن و ُط ب ي ف ون ل ك أ ي ا م ك ئ َ َ َ ِ قلِيل أول َ ِ ِ ْ ِِ ْ َي ْو َم ِّ ُز َا َ ٌ يه ْم َولَ ُه ْم َع َذ اب أَلِي ٌم ك ي ل و ة م ا ي ق ال َ َ َ ِ ِ ِ “Hakika wale wafichao aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu na wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipokuwa Moto: wala Mwenyezi Mungu hatawasemesha Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa; na wao wana adhabu chungu.” (Qur’ani: 2:174)
2.
Walikuwa wakipokea hongo na kumnyima haki anayestahiki, na kufanya upendeleo kwa wenye nacho pindi wanapohukumu.
3.
Na katika taratibu zao za kujikusanyia mali kwa njia zisizo halali ni kule kuwauzia watu Pepo na kutoa msamaha na kuwafutia madhambi, kutokana na kazi hizi walikuwa wanajikusanyia mali nyingi sana, na shughuli hizi bado zinaendelea kufanyika hadi leo.
Ama kuhusu uwekaji wao wa vizuizi dhidi ya Dini ya Mwenyezi Mungu, hakika jambo hili liko wazi sana, kwani walikuwa wakitumia mbinu za kupotosha maana halisi ya maandiko ya Mwenyezi Mungu au huyaficha kabisa kwa lengo la kulinda maslahi yao binafsi, na walisimama dhidi ya kila ambaye alikuwa ni kikwazo kwa 251
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 251
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
maslahi yao na kumwadhibu adhabu nzito. Lau kama si mwenendo wao huu mbaya, bila ya shaka watu wengi wengeweza kuikubali Dini Tukufu ya Uislamu. Na hadi sasa kanisa kwa kushirikiana na Mayahudi wameshika hatamu na kuelekeza nguvu zao kila upande ili kuhakikisha watu hawafikiwi na uongofu wa Dini ya Uislamu. Katika kuhusishwa Mayahudi pamoja na Manasara kuipupia dunia kwa kula mali za watu wengine kwa dhulma, Aya inayofuata inatoa hukumu ya ujumla kwa kila mwenye kujilimbikizia mali hata kama mali hiyo ameichuma katika njia ya halali. Malipo ya mtu wa aina hiyo ni kuadhibiwa vikali Siku ya Kiyama: “Na wale walimbikizao dhahabu na fedha na hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi wabashirie adhabu iumizayo.� Dhahabu na Fedha zilikuwa ndizo sarafu zilizokuwa zinatumika katika kuuza na kununulia katika zama hizo, kama inavyoendelea kutumika sarafu ya fedha katika baadhi ya nchi. Kwa hivyo hapa kinachozingatiwa ni ulimbikizaji wa mali yoyote kinyume na sheria za Uislamu, hata kama asili yake haitokani na madini ya fedha au dhahabu. Tabia ya ulimbikizaji wa mali bila ya sababu ya kisheria inaufanya uchumi udorore kwa hivyo ni sababu ya kuifanya jamii kuishi katika dimbwi la umasikini, ndio maana Uislamu ukawataka Waumini watoe mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu na katika kila jambo ambalo lina manufaa kwa viumbe, na kuacha kuzirundika, kwani kufanya hivyo kunasababisha kukosekana mzunguko katika soko, basi ikiwa watakataa kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu, basi adhabu kali yenye kuunguza miili yao inawasubiri, na adhabu hiyo kali si tu wataipata Siku ya Kiyama, bali itawaanzia hapa duniani kwa kutengwa na kuchukiwa na masikini na wenye shida mbalimbali. Ikiwa walimwengu wa zama zilizopita walikuwa hawajui utaratibu huu uliopangwa na Uislamu, bila ya shaka jambo hili kwa hivi sasa liko wazi kwa kila mtu, kwani matatizo ya kiuchumi yaliyopo ni kutokana na wale wachache wanaomiliki mali nyingi kutoziendeleza mali hizo kwa miradi ya kimaendeleo, na badala yake ni kuzirundika katika mabenki makubwa kwa kutarajia kupata riba, natija yake ni kutokea misukosuko ya kisiasa isiyokwisha na kumalizikia kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, vita ambavyo huangamiza mbichi na kavu. Ni mali ya aina gani iliyo haramu kukusanywa na kuhifadhiwa? Uislamu kama mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, kama vile unavyokataza mtu mwenye uwezo kumnyima asiye na uwezo, pia unaharamisha mtu kutumia mali yake kiholela bila ya manufaa, kwa hivyo unazingatia sana juu ya suala la utunzaji wa mali kwa matumizi ya mmiliki mwenyewe na kwa kizazi chake. Sasa ikiwa mali inayomilikiwa na mtu itatolewa zile stahiki za wajibu, kama vile Zaka, Khumsi na nyinginezo, hapo itakuwa si haramu mali iliobakia kuhifadhiwa, kama Aya
252
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 252
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
ilivyobainisha kwa kusema: “Na hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mungu.” Pindi sharti la kuitoa mali kama Mwenyezi Mungu alivyoelekeza likipatikana basi mtu huyo atasalimika dhidi ya adhabu ya Moto wa Siku ya Kiyama, na katika kusisitizia hilo Mtume (s.a.w.w.) amesema:
ّ .أي مال أ ّديت زكاته فليس بكنز “Mali yoyote iliyotolewa Zaka yake, si katika mali iliyolimbikizwa.”116
Na katika mapokezi mengine kutoka mwa Mtume (s.a.w.w.), baada ya kuulizwa na baadhi ya Maswahaba wake baada ya kuteremka Aya hii inayoelezea adhabu kali kwa wale wanaojilimbikizia mali pasi na kutoa sehemu ya wajibu, waliuliza: Je, hatuna haki ya kuwawekea akiba watoto wetu? Mtume (s.a.w.w.) aliwajibu kwa kusema:
ّ الزكاة ّ إن اهلل لم يفرض ّ و,إال ليطيب بها ما بقي من أموالكم .إنّما فرض المواريث من أموال تبقى بعدكم “Hakika Mwenyezi Mungu hakufaradhisha Zaka isipokuwa kwa lengo la kuisafisha hiyo inayobakia, na kwa hakika amefaradhisha mirathi kwa hiyo iliyobakia baada yenu (baada ya kutolewa Zaka na nyinyi mtakapofariki dunia).”117
Ni wazi kwamba, lau kama kujilimbikizia mali kwa hali yoyote ile kungekuwa ni haramu, basi kusingekuwa na hukumu ya mirathi katika Uislamu. Licha ya ruhusa hii ya kujikusanyia mali baada ya mtu kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu zilizowajibu juu yake, ni vyema kuchunga hali ya maisha ya Waislamu ilivyo, akiona ya kwamba kuna tatizo la ajira kwa vijana na yeye ana uwezo wa kuanzisha mradi utakaoweza kuwapatia ajira au kutoa mikopo na hata msaada, basi ni bora zaidi kuliko mali hiyo kukaa bila ya kuzalishwa. Abu Dharr na Utetezi wa Wanyonge: Abu Dharr alikuwa ni miongoni mwa Maswahaba watukufu wa Mtume (s.a.w.w.). Pale alipomuona Khalifa Uthman amekusanya mali nyingi katika hazina ya Wais116 117
Suyutiy, Durrul Manthur, Jz.3, Uk.232 Kitabu kilichotangulia 253
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 253
12/8/2014 2:43:44 PM
WITO KWA WAUMINI
lamu, na mali hiyo haitumiki kwa lengo la kuwatoa Waislamu katika dimbwi la umasikini na badala yake mali hiyo wanagaiwa watu wa kabila la khalifa tu (Bani Ummayah) hata kama si wenye shida ikilinganishwa na wengine, alianza kuzisoma Aya hizi kwa sauti kubwa huku akipita katika mitaa mbali mbali ya mji wa Madina. Baada ya khalifa Uthman kusikia hivyo, alikereka sana na hivyo kuamua kumuhamisha na kumpeleka katika mji wa Sham. Baada ya kufika huko aliikuta hali ya huko haitofautiani na hali ya Madina, kwani huko naye Muawiya ibn Abi Sufiyani hakuwa mbali na mwenendo wa khalifa Uthman. Aliitumia mali ya Waislamu kwa kujijengea majumba ya kifakhari na kuwaneemesha jamaa zake wa karibu. Muawiya naye hakuweza kuvumilia kusikia Aya hizi zinasomwa, akitambua kwamba yeye ni mlengwa wa Aya hizo. Alichokifanya ni kumrudisha Abu Dhar katika ardhi ya Madina, na alipofika huko aliendeleza ukumbusho wake kwa kuzisoma Aya hizo. Hapo ndipo khalifa Uthman alipoamua kwa mara nyingine kumfukuza, na mara hii alimpeleka katika sehemu iliyokuwa ikiitwa Rabdha (nje ya mji wa Madina). Rabdha ilikuwa ni sehemu isiofaa kwa maisha ya mwanadamu, kwani kulikuwa hakuna maji na hali yake ya hewa haikuwa muwafaka kwa maisha ya mwanadamu. Hali hiyo ilipelekea kukatika kwa maisha ya Abu Dharr r.a., ambaye aliyatoa maisha yake katika kueleza ukweli na kupigania haki za wanyonge. Mtume (s.a.w.w.) amezungumzia kuhusu nafasi yake kwa kusema:
ما أظلّت الخضراء وال أقلّت الغبراء من ذي لهجة أصدق .ذر ّ من أبي “Mbingu haijamfunika (mtu) wala ardhi haijambeba mtu mwenye maneno ya kweli zaidi kuliko Abu Dharri.”118
Tofauti iliyokuwepo kati ya khalifa na Abu Dharr si kwamba Abu Dharr alikuwa anayasema hayo aliyokuwa akiyasema kwa kutaka kupatiwa fungu la mali au nafasi ya uongozi kutoka kwake, la hasha! Kwani Abu Dharr alikuwa anasifika kwa sifa ya uchamungu na mwenye kutosheka na alichonacho, lakini sababu kubwa ya kutofautiana kati yao ilikuwa ni kwa khalifa kuwabagua watu katika ugawaji wa mali kwa kuwapendelea jamaa zake wa karibu kuliko Waislamu wengine, tena alikuwa akiwapa zaidi ya mahitajio yao! 118
Ahmad ibn Hanmbal, Musnad Ahmad, J. 6 Uk. 442 254
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 254
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa masikitiko makubwa kuna baadhi ya watu wanajaribu kumtetea khalifa na kumtuhumu Abu Dharr kwa kudai eti alikuwa na fikra za mfumo wa kijamaa, eti alikuwa na mawazo ya kwamba mali yote ni milki ya Mwenyezi Mungu na hakuna haki kwa mtu binafsi kuimiliki! Kwa kweli tuhuma hii ni yenye kushangaza sana, kwani Abu Dharr r.a. hakuwa mjinga wa Qur’ani Tukufu, ambayo inaeleza bayana juu ya umiliki wa mali kwa mtu binafsi, kama ilivyo katika Aya zinazoelezea hukumu ya mirathi, biashara, usia n.k. Abu Dharr alikuwa ni miongoni mwa Maswahaba waliokuwa karibu na Mtume (s.a.w.w.) akiwa ameleleka ndani ya Uislamu na kuielewa Qur’ani, maneno ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya haki ya Abu Dharr r.a. yanatosha kuwa dalili ya haya:
ما أظلّت الخضراء وال أقلّت الغبراء من ذي لهجة أصدق .ذر ّ من أبي “Mbingu haijamfunika (mtu) wala ardhi haijambeba mtu mwenye maneno ya kweli zaidi kuliko Abu Dharr.”
Na la kushangaza zaidi ni kujenga hoja za kumtetea Muawiya ambaye amerejesha ufalme katika umma huu, na leo ndio mfumo rasmi wa kisiasa katika baadhi ya nchi za Waislamu, ikiwemo miji ya Makka na Madina, iliyokuwa katika utawala wa serikali ya Mtume (s.a.w.w.). Na hicho alichokiasisi Muawiya (utawala wa kifalme na kujikusanyia mali na madaraka kwa jamaa wa mfalme) ndicho tunachokishuhudia kwenye nchi hizo!Kutokana na uwelewa mzuri wa Abu Dharr wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu alitambua vyema kwamba si haki mali ya Waislamu kutumiwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi, huku masikini na wahitaji wengine wakiachwa bila ya kupewa stahiki yao, na badala yake watawala wakijiimarisha kwa kujijengea majumba ya kifahari na manunuzi ya vitu vya anasa. Malipo ya Mwenye Kujikusanyia Mali: Aya ya pili katika maudhui haya imeweka bayana moja kati ya malipo atakayoyapata Siku ya Kiyama yule mwenye kujikusanyia mali kwa njia zisizokubalika, inasema: “Siku zitakapotiwa katika moto wa Jahannam, na kwazo vitachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao.” Wakiwa katika hali hiyo ya kuteketezwa na Moto, Malaika watawahutubia kwa kuwaambia: “Haya ndiyo mliyojilimbikizia, basi onjeni yale mliyokuwa
255
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 255
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
mkiyalimbikiza.� Kwa hakika Aya hii inatufunza ya kwamba matendo ya mwanadamu ayatendayo hayaishii patupu, bali huandikwa na kuhifadhiwa pahala penye usalama wa hali ya juu, na kuja kuoneshwa mwenyewe Siku ya Kiyama, Siku hiyo mwanadamu atakuwa ni mwenye furaha au majonzi, hayo ni kutokana na namna alivyotenda hapa duniani. Kutajwa viungo hivi vitatu haimaanishi ya kwamba viungo vingine havitoungua, bali mwili wote utaungua, huwenda hekima ya kutajwa viungo hivi ni kutokana na tabia ya mtu huyo pindi anapoendewa na masikini au muhitaji humkunjia uso wake, na mara nyingine hugeuka upande kwa kutomjali na mara nyingine huonyesha dharau zaidi kwa kumgeuzia mgongo. Bila ya shaka hizi ni baadhi ya tabia za wanyimaji, kwa hivyo viungo hivi na vinginevyo vitayeyuka zaidi katika Moto wa Jahannamu kuliko zinavyoyeyuka fedha na dhahabu.
256
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 256
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI NA TATU
ََّيا أَُّي َها ال ُ َيل ل ُ َين آ َمنُوا َما ل َ َ ْ َ ب س ي ف وا ر ف ن ا م ك ق ا ذ إ م ك ذ ُ ُ ْ َ َِّيل الله ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ْلآ َ ْاثَّ َاق ْلتُ ْم إلَى أ ْ ُّ ضيتُ ْم ِبال َح َيا ِة ُ الد ْن َيا ِم َن ا ِخ َر ِة َف َما َم َت اع ر ال ْ ِ ض أَ َر ِ ِ ْلآ َ ٌ ِّ ُ َّا َّا ُّ ْال َح َيا ِة الد ْن َيا ِفي ا ِخ َر ِة إِل َقلِيل إِل َت ْن ِف ُروا يُ َعذبْك ْم َع َذابًا ألِي ًما ُ ْر ُك ْم َو اَل َت ض ُّرو ُه َشي ًْئا َواللهَُّ َعلَىٰ ُك ِّل َش ْي ٍء َ َو َي ْس َت ْب ِد ْل َق ْو ًما َغي ير ٌ َق ِد “Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa nendeni katika njia ya Mwenyezi Mungu mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na Akhera ni kidogo tu. Kama hamwendi atawaadhibu kwa adhabu iumizayo na atawaleta watu wengine badala yenu, na hamtamdhuru chochote; Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.” (Qur’ani; 9:38-39)
SABABU YA KUTEREMKA Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas na wengineo ya kwamba Aya hizi mbili ziliteremka katika vita vya Tabuuk wakati Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anarejea Madina kutoka katika mji wa Taifu huku akiwa katika harakati za kuandaa jeshi kwa ajili ya kukabiliana na dola ya Roma. Pia imepokewa ya kwamba ilikuwa ni tabia ya Mtume (s.a.w.w.) kutoweka bayana habari ya vita kwa Maswahaba wake pale anapoazimia kupambana dhidi ya watu fulani kwa lengo la kuzuia siri za kijeshi zisije zikavuja na kuwafikia maadui wa Uislamu. Lakini kutokana na hali ilivyokuwa baada ya vita vya Tabuk aliona vyema awaeleze Waislamu kwa uwazi juu ya kupambana na jeshi la Roma, hii ni kwa sababu kupambana na dola kama Roma halikuwa jambo jepesi kama ilivyokuwa mapambano yao dhidi ya mushirikina au mayahudi, kwa hivyo Mtume (s.a.w.w.) alifanya hivyo ili kutoa fursa kwa Waislamu kujiandaa vilivyo na kujijenga kiroho. Licha ya nguvu kubwa za kijeshi walizokuwa nazo wanajeshi wa Roma, lakini pia masafa kati ya Madina na mamlaka ya Roma yalikuwa marefu sana na pia ilikuwa ni katika msimu wa kiangazi na wakati wa mavuno. Kutokana na hali 257
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 257
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
hii waliokuwa nayo Waislamu ikawawia vigumu kutoka kwenda vitani, huku baadhi yao wakisitasita katika kuitikia wito wa Mtume (s.a.w.w.). Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akaziteremsha Aya hizi, huku akiwaonya Waislamu dhidi ya kutoitikia wito wa Mtume (s.a.w.w.)119
MAELEZO Vita vya Tabuk vilitokea mwaka wa tisa wa Hijiria, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya ukombozi wa mji wa Makka. Baada ya vita vya Tabuk, Waislamu walitakiwa kujiweka tayari kwa ajili ya kupambana na dola ya Roma, dola ambayo ilikuwa ni miongoni mwa dola kubwa katika zama hizo. Baada ya Waislamu kupata habari hizo, waliingiwa na woga na mfadhaiko. Kutokana na hali hiyo, wanafaki waliweza kuitumia hali waliokuwa nayo Waislamu kueneza kasumba zao na kuwadhoofisha wale waliokuwa na udhaifu wa imani, lakini hawakuweza kufanikiwa kwa wale waliokuwa na imani thabiti. Wakati waliotakiwa kwenda vitani ulikuwa ni msimu wa mavuno, wengi wao walitumainia kujiongezea kipato. Na kwa upande mwingine masafa yalikuwa ni marefu mno, hasa ikilinganishwa namna jua lilivyokuwa kali sana, kwani ilikuwa ni msimu wa kiangazi. Hizi zilikuwa ni changamoto zilizokuwa zikiwakabili Waislamu katika kupambana na maadui zao hao. Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hizi, kwa lengo la kuwahamasisha na kuachana na hizo sababu wanazozitegemea, ambazo hazina uzito wowote ikilinganishwa na wajibu wa kupambana dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu. Hapa tunaona namna Mwenyezi Mungu alivyotumia utaratibu wa kuwataka Waislamu kwenda katika jihadi; kwanza ametumia njia ya uhamasishaji, kisha akatumia njia ya lawama, na mwisho kabisa ametumia njia ya vitisho. Ametumia njia hizi ili maneno Yake yapate kupenya katika kila kiungo cha mwanadamu, Aya inasema: “Enyi mlioamnini! Mna nini mnapoambiwa nendeni katika njia ya Mwenyezi Mungu mnajitia uzito katika ardhi?” Ibara ‘Mnajitia uzito katika ardhi?’ inamaanisha kutotaka kutoka kwenda vitani na badala yake kupenda kubakia nyumbani. Aya imekuja kuwahutubia wale waliokuwa na udhaifu wa imani miongoni mwa Waislamu na sio wote, kwani kulikuwepo miongoni mwao waliokuwa tayari kupambana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu dhidi ya yeyote na wakati wowote. Aya inaendelea kuwahutubia kwa njia ya lawama, inasema: “Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na Akhera ni kidogo tu.” Basi ni vipi mtu mwenye akili alinganishe hasara atakayoipata hapa duniani na malipo ya hali ya juu tena yasiyo na mwisho atakayoyapata Siku ya 119
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 6, Uk. 51 258
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 258
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
Kiyama!Baada ya hapo Aya ikaja na utaratibu wa vitisho kwa wavivu wa Jihadi, inasema: “Kama hamwendi atawaadhibu kwa adhabu iumizayo.” Ikiwa wale wanaopenda starehe za kidunia wanadhani ya kwamba, ikiwa wao watabweteka na kukataa kwenda kwenye Jihadi, basi harakati za Uislamu zitasimama na nuru yake itafifia, kwa hakika watakuwa wamekosea sana, kwani Mwenyezi Mungu anauwezo wa kuleta watu wengine badala yao watakaokuwa tayari kuipigania na kuitetea Dini Yake: “Na atawaleta watu wengine badala yenu.” Atawaleta watu walio na kila aina ya ubora ikilinganishwa na nyinyi, wenye imani thabiti, wakakamavu, watiifu na wenye kupenda kuitetea Dini ya Mweyezi Mungu kwa hali yoyote ile: “Na hamtamdhuru chochote.” Huu ni ukweli na uhakika utokao kwa Mwenyezi Mungu Muumba na si ndoto zisizo na ukweli: “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.”
UTAFITI 1.
Katika Aya hizi mbili Mwenyezi Mungu anatoa msisitizo wa kuipigania Dini Yake kwa kutumia vipengele saba: Kwanza: Anawahutubia waumini kwa kuwaambia: “Enyi mlioamini!” Pili: Anawaamrisha waharakishe kuelekea katika Jihadi: “Nendeni.” Tatu: Ameielezea Jihadi kuwa ni “Njia ya Mwenyezi Mungu.” Nne: Ameuliza kwa njia ya kupinga kuifadhilisha dunia badala ya akhera: “Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera?” Tano: Kutishia kwa adhabu kali Sita: Kuwaondoa wanaobweteka na kuleta wengine. Saba: Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, na wala hadhuriki ikiwa watu watakhalifu amri Zake, bali wao ndio watakaodhurika.
2.
Aya hizi zinaeleza ya kwamba iwapao nyoyo za Waislamu zitashikamana na maisha ya dunia, basi hiyo itakuwa sababu ya kudhoofika kwa Jihadi, kwa hivyo inampasa kila Mwislamu kutambua ya kwamba dunia ni pahala pa kupita na si pa kukaa milele, na ni pahala pa matayarisho ya maisha ya baadaye, kwa hivyo hakuna haja ya mtu kusitasita pindi anapoitwa na Mola Wake juu ya kutenda jambo fulani, kwani jambo hilo linalenga katika kumtayarishia maisha bora ya akhera, na vyote anavyovimiliki ataviacha hapa hapa. 259
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 259
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
Tunasoma katika dua ya Imamu Zaynul Abidina kuwa:
وامح عن,وأنسهم عند لقائهم العد ّو ذكر دنياهم الخ ّداعة . واجعل الجنّة نصب أعينهم,قلوبهم خطرات المال الفتون “Wakati wanapokutana na adui wasahaulishe kumbukumbu ya dunia yao yenye kudanganya, na wafutie hatari ya mali yenye kufitini kutoka nyoyoni mwao, na ifanye Pepo kuwa mbele ya macho yao.”120
Lau tungefahamu vyema thamani ya akhera na neema zake ikilinganishwa na zile za duniani, tungegundua ya kwamba dunia si lolote si chochote mbele ya akhera kama Mtume (s.a.w.w.) anavyotubainishia kwa kusema:
ّ و اهلل ما ال ّدنيا على األخرة إال كما يجعل أحدكم أصبعه في .الي ّم ث ّم يرفعها فينظر بم ترجع “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, thamani ya dunia mbele ya akhera ni kama vile mmoja wenu kutia kidole chake baharini kisha kukitoa, na aangalie ni kitu gani kidole hicho kimekuja nacho!”121
3.
120 121
Kuhusiana na ibara inayoeleza kwamba Mwenyezi Mungu atawabadilisha watu wengine ikiwa hao waliopo hawako tayari kuitetea Dini yake, wafasiri wa Qur’ani wana rai mbalimbali: Baadhi yao wanasema ni Waajemi, wengine wanasema ni watu wa Yemen, wengine wanasema ni wale watu walioingia katika Uislamu baada ya kuteremshwa Aya hizi na kuutoa muhanga uhai wao katika kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu.
Imamu Zaynul Abidin, Sahifatu Sajjadiya, Duau Ahli Thughur Suyutiy, Durrul Mantur, Jz.3, Uk.239 260
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 260
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI NA NNE َ الصا ِد ِق َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين َّ ين آ َمنُوا اتَّ ُقوا اللهََّ َو ُكونُوا َم َع
“Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” (Qur’ani; 9:119)
MAELEZO Aya hii iliyoko katika Suratul Bara’a, Sura ambayo imeeleza habari za wale waliokhalifu ahadi kati yao na Mwenyezi Mungu pamoja na Mtume Wake (s.a.w.w.) na kudhihirisha kwa vitendo upingaji wa imani juu ya Mwenyezi Mungu na kuwepo kwa Siku ya Mwisho, lakini kutokana na misimamo mikali waliyokuwa nayo Waumini dhidi yao, kama vile kuwatenga na kuwatanabahisha juu ya matendo yao maovu, waliweza kurejea katika njia sahihi. Ama Aya tuliyonayo inaeleza namna Muumini anavyotakiwa kuamiliana na Waumini wasiokhalifu maamrisho ya Mwenyezi Mungu na walio wakweli katika maneno yao na matendo yao. Kwanza Aya inaanza kusema: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu.” Ili kuifikia njia sahihi ya uchajimungu, njia iliyo na kila aina ya changamoto, Aya inabainisha namna ya kukabiliana na vizuizi hivyo kwa kusema: “Na kuweni pamoja na wakweli.” Wafasiri wa Qur’ani wana maoni mbalimbali kuhusiana na makusudio ya neno ‘Wakweli’ lakini ni vyema tukarudi katika Qur’ani yenyewe ili tuangalie makusudio yake. Kwa mfano katika Aya ya 177 ya Sura ya Pili, Mwenyezi Mungu anasema:
َ ْس ْال ِب َّر أَ ْن تُ َولُّوا ُو ُج وه ُك ْم ِق َب َل ْال َم ْش ِر ِق َو ْال َم ْغ ِر ِب ولكن َ لَي ْللهَّ ْ لآ ْ ْ ْ َ اب َوالنَّ ِبي ِّين ِ ال ِب َّر َم ْن آ َم َن ِبا ِ َوال َي ْو ِم ا ِخ ِر َوال َم اَل ِئ َك ِة َوال ِك َت َ َوآ َتى ْال َم َ ال َعلَىٰ ُحبِّ ِه َذ ِوي ْال ُق ْر َبىٰ َو ْال َي َتا َمىٰ َو ْال َم َسا ِك ين َ ِالسا ِئل َ َواب الص اَل َة َوآ َتى ِّ ين َو ِفي َّ اب َوأَ َقا َم َّ يل َو َّ ْن ِ الس ِب ِ الر َق ُ الز َكا َة َو ْال ُم َّ َ الص ِاب ِر َ وف َ ون ِب َع ْه ِد ِه ْم إِٰ َذا َع ين ِفي ْال َب ْأ َسا ِء َّ اه ُدوا َو َ ُ ْْ َّ ٰ ُ َ َّ َو ُ َ س أول ِئ َك ال ِذ َ الض َّرا ِء َو ِح ص َدقوا َو ُأو ل ِئ َك ه ُم َ ين ِ ين ال َبأ َ ْال ُمتَّ ُق ون 261
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 261
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
“Sio wema kuelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi tu, lakini wema ni wa anayemwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na Malaika, na Kitabu na Manabii; na akawapa mali, pamoja na kuipenda, jamaa na mayatima na masikini na mwananjia, na waombao, na katika ukombozi wa watumwa; na akasimamisha Swala na akatoa Zaka; na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wanaokuwa na subira katika shida na dhara na katika wakati wa vita. Hao ndio waliosadikisha na ndio wenye takua.”
Katika Aya hii tunaona kwamba baada ya Waislamu kukatazwa kujadiliana kuhusiana na suala la kubadilishwa Kibla, inawabainishia amali zilizo njema na bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Amali hizo ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na Malaika na Vitabu kutoka mbinguni na Manabii, kisha ni kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuwasaidia wanyonge, na kusimamisha Swala na kutoa Zaka, na kutekeleza ahadi, na kuwa na msimamo madhubuti na ukakamavu wakati wa Jihadi. Na baada ya kutaja sifa hizi, inasema ya kwamba wale ambao wanasifika kwa sifa hizi, basi hao ndio wakweli. Na katika Suratul Hujrat Aya ya 15, Mwenyezi Mungu anasema:
َ ون الَّ ِذ َ ُإِنَّ َما ْال ُم ْؤ ِمن ين آ َمنُوا ِباللهَِّ َو َر ُسولِ ِه ثُ َّم لَ ْم َي ْر َتابُوا َ َ َ َو َج يل اللهَِّ أوالئك ُه ُم ِ اه ُدوا ِبأ ْم َوالِ ِه ْم َوأ ْن ُف ِس ِه ْم ِفي َس ِب َ الصا ِد ُق ون َّ “Hakika Waumini ni wale tu waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake tena wasiwe na shaka, na wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli.” (Qur’ani; 49:15)
Aya hii nayo inatupa maana ya ‘Wakweli’ kwamba ni wale walioamini na kutenda matendo mema na kuwa na msimamo madhubuti usiotetereka. Na Aya ya 8 ya Suratul Hashir Mwenyezi Mungu anasema:
َّ َ لِْل ُف َق َرا ِء ْال ُم َهاجر ْ ُين أ ْ ار ِه ْم َوأَ ْم َوالِ ِه ْم ي د ن م وا ج ر خ ُ َ ِ ِ ِ ِ َ ين ال ِذ ِِ ْ ض اًل ِم َن اللهَِّ َو ِر ْ ون َف َ ص ُر َ َي ْب َت ُغ ون اللهََّ َو َر ُسولَ ُه ُ ض َوا ًنا َو َي ْن َ الصا ِد ُق ون َّ أوالئك ُه ُم 262
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 262
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
“Wapewe mafukara wahajiri waliotolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi Zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Hao ndio wakweli.” (Qur’ani; 59:8)
Aya hii pia inatueleza ya kwamba ‘Wakweli’ ni Waumini wenye kusubiri na kuvumilia matatizo mbalimbali yanayowakabili, na kutimuliwa kutoka majumbani mwao na kwenye mali yao, wamekubali kufikwa na yote hayo kwa lengo la kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kumnusuru Mtume Wake (s.a.w.w.). Kutokana na Aya hizi tumeweza kujifunza ya kwamba ‘Wakweli’ ni wale ambao matendo yao yanakwenda sambamba na imani ya Uislamu kwa uhalisia utakiwao, pasi na kwenda kombo, na wala hawatetereki pindi wafikwapo na masaibu na changamoto, bali huthibiti sawasawa na ikibidi kujitoa muhanga hufanya hivyo. Bila ya shaka watu wenye kusifika kwa sifa hizi wako katika daraja tofauti. Ama wale walioko katika daraja ya juu kabisa ni Maasumina (Mtume (s.a.w.w.) na watu wa nyumbani kwake waliotoharishwa). Licha ya neno ‘Wakweli’ kuwa na maana pana kama tulivyoeleza, kuna Riwaya mbalimbali zinazomaanisha ya kwamba makusudio yake katika Aya hii ni watu watoharifu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.). Kwa mfano Riwaya aliyoipokea Salim bin Qaysi al-Hilaliy ya kwamba: “Siku moja kiongozi wa Waumini (Imamu Ali (a.s.)) alikuwa na mazungumzo na kundi la watu, na miongoni mwa maneno yake alisema: ‘Nakushuhudisheni kwa Mwenyezi Mungu, je, mnatambua ya kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha Aya isemayo: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli?” Na Salman al-Farsiy akauliza: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Aya hii inawahusu watu wote au ni kwa watu maalumu? Mtume (s.a.w.w.) akamjibu: Ama wenye kuamrishwa ni waumini wote, ama walio wakweli ni watu maalumu, ambao ni Ali (ibn Abi Talib) na Mawasii (Maimamu) baada yake mpaka Siku ya Kiyama.’ Wale watu walijibu: Ndio.’” Na Riwaya nyingine imepokewa kutoka kwa Nafi’i kutoka kwa Abdallah ibn Umar: “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu kwanza amewaamrisha Waislamu wamche Mwenyezi Mungu kisha akasema:‘Kuweni pamoja na wakweli.’ Makusudio yake ni Muhammad na watu wa nyumbani kwake.’” Riwaya hii aliyoisimulia Abdallah ibn Umar ndio sahihi zaidi ikilinganishwa na ile isemayo ya kwamba makusudio ya Wakweli ni Muhammad pamoja na Maswahaba wake, kwa sababu Maswahaba walikuwa na zama maalumu za kuishi na wote wamefariki dunia, ama Maimamu wanaotokana na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) wanakuwepo katika kila zama inapokuwepo Qur’ani, kwani Mtume alipotutaka tushikamane na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu wa nyumbani kwake alieleza bayana ya kwamba vizito 263
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 263
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
viwili hivyo (Qur’ani pamoja na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.)) havitofarikiana mpaka vimfikie katika hodhi lake.122Jambo la msingi na la kuzingatia hapa ni kwamba Aya Tukufu inatutaka kumcha Mwenyezi Mungu na kuwa pamoja na Wakweli, na lau kama maana ya neno ‘Wakweli’ ingekuwa inajumuisha kila muumini wa kweli mwenye msimamo madhubuti, basi ingelazimu kusemwa; Kuweni miongoni mwa Wakweli, na sio pamoja na Wakweli. Hii ni ishara nyingine ya kwamba makusudio ya neno ‘Wakweli’ ni watu maalumu. Na kwa upande mwingine haimaanishi kwamba kuwa pamoja na Wakweli ni kusuhubiana nao au kuishi jirani na wao, bali ni kuwafuata na kwenda mwenendo wao. Dalili nyingine ya kuthibitisha ya kwamba makusudio yake ni watu maalumu, ni kwamba haiwezekani kutoka amri isiyo na mipaka juu ya kumfuata na kumtii mtu asiyekuwa Maasumu (mwenye kukosea). Kwa hivyo tukichukua Riwaya tulizozitaja kisha tukaziunganisha na Aya hii tutaweza kufahamu muradi wa neno ‘Wakweli’. Kitu cha kufurahisha kwa upande mmoja ni kwamba mfasiri maarufu wa madhehebu ya Kisunni ajulikanaye kwa jina la Fakhru Razi amekubali maana hii kwa kusema kama alivyonakiliwa na Sheikh Makarimu Shiraziy: “Hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha Waumini wawe pamoja na Wakweli, kwa hivyo basi, Aya inamaanisha ya kwamba ni wajibu kwa mtu ambaye si Maasumu kumfuata Maasumu ili asalimike na kufanya makosa, na jambo hili lipo katika kila zama, na wala hatuna dalili ya kwamba jambo hili ni makhsusi kwa zama za Mtume (s.a.w.w.) tu.” Ama kwa upande mwingine amekuja na natija ya kuhuzunisha, kwani ameendelea kusema: “Sisi tunakubali ya kwamba makusudio ya Aya ni haya, na inalazimu kuwepo maasumu katika kila zama, lakini sisi tunaona ya kwamba maasumu ni umma wote na si mtu mmoja.”123 Kwa maneno yake hayo, anakusudia kutuambia ya kwamba: “Aya hii ni dalili inayotutaka tukubali kile wanachokubaliana Waumini, na katu haiwezekani Waumini kukubaliana juu ya jambo lisilo sahihi, na huko kukubaliana kwao ni hoja kwa wengine.” Kwa maana yake hii italazimu baadhi ya Waumini wawafuate baadhi, hali hii itapelekea wafuasi kuwa wenye kufuatwa, na wakati dhahiri ya Aya imepambanua baina ya wawili hao! - Aya hii inatoa ishara ya wazi juu ya kuwepo Maasumu katika kila zama.
122 123
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.6, Uk.258 Kitabu kilichotangulia, Uk. 260 264
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 264
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI NA TANO
َوإِ ْن َن َكثُوا أَ ْي َما َن ُه ْم ِم ْن َب ْع ِد َع ْه ِد ِه ْم َو َط َعنُوا ِفي ِدي ِن ُك ْم َف َقا ِتلُوا َ ان لَ ُه ْم لَ َعلَّ ُه ْم َي ْن َته َ أَِئ َّم َة ْال ُك ْف ِر إِنَّ ُه ْم اَل أَ ْي َم ُون “Enyi mlioamini! Piganeni na wale walio karibu yenu katika makafiri na wakute kwenu ugumu; na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye takua.” (Qur’ani; 9:12)
MAELEZO Aya hii ni miongoni mwa Aya nyingi zilizomo katika Sura hii (Suratu Tawba) zinazoelezea hukumu mbalimbali zinazohusiana na vita. Kwa hivyo kwanza imeelekeza wito wake kwa Waumini kwa kusema: “Enyi mlioamini! Piganeni na wale walio karibu yenu katika makafiri.” Bila ya shaka ni wajibu kwa Waumini kupambana na kila kafiri aliyesimama dhidi ya Uislamu, lakini katika kuhakikisha ushindi inapasa kuanza na wale walio karibu zaidi, kwani hatari ya adui wa karibu ni kubwa zaidi ikilinganishwa na yule aliyeko mbali, kama vile ambavyo ulinganiaji watu kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu unapasa uanze na jamaa wa karibu, na hivyo ndivyo ambavyo Mtume (s.a.w.w.) alivyotekeleza ulinganio wake kwa kuanza na watu wake wa karibu kabla ya kuwalingania wa mbali. Bila ya shaka, iwapo adui wa mbali kinasaba atakuwa ni hatari zaidi, basi itabidi kuanza kupambana naye. Ama kuhusiana na umuhimu wa kupambana na adui wa karibu, ni kutokana na sababu zifuatazo: Kwanza: Adui wa karibu ni hatari zaidi kuliko wa mbali. Pili: Ni rahisi zaidi kumtambua adui wa karibu, kwa hivyo inakuwa rahisi kumshinda. Tatu: Kuanza kupambana na adui wa mbali mara nyingi kunasababisha kuongezeka kwa uadui, kwani huyu wa karibu ni rahisi kushirikiana na wa mbali. Nne: Matayarisho ya kivita dhidi ya adui wa karibu ni mepesi zaidi ikilinganishwa na adui wa mbali. Kutokana na sababu hizi na nyinginezo ni dhahiri kwamba kuanza kupambana na adui wa karibu ni wajibu zaidi na ni jambo lenye umuhimu wa kipekee.
265
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 265
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
Jambo la kuelewa ni kwamba Aya hii iliteremka wakati ambapo Uislamu ulikuwa umeshika hatamu karibu Bara Arabu lote, adui aliyekuwa karibu zaidi ilikuwa ni dola ya Roma. Pia inatupasa tusisahau ya kwamba, licha ya Aya hii kuelezea masuala ya kupambana na adui aliye karibu zaidi kimasafa, tunaweza kujifunza ya kwamba Aya hii pia inabeba ujumbe wa kwamba iwapo Waislamu wanataka kufanya kazi ya kulingania watu, basi ni vyema kazi hiyo ianze na jambo ambalo ni hatari zaidi kuliko jingine. Kwa mfano katika zama zetu hizi tunaona jamii ya Kiislamu inakabiliwa na tishio la kutenganishwa na mafunzo ya Dini yao, na maadui hutumia njia mbalimbali katika kufanikisha muradi wao huo. Basi ni wajibu wa walinganiaji kuwakumbusha jambo hili na kuwatahadharisha watu juu matokeo yake mabaya. Hii haimaanishi kuacha kuzungumzia mambo mengine yenye kutelekezwa katika Dini, lakini jambo la msingi ni kuchunga lililo muhimu zaidi na lenye hatari kubwa kuliko jingine. Jambo jingine lililomo katika Aya hii linalohusiana na Jihadi ni kwa Waumini kuwa na nyoyo ngumu dhidi ya adui: “Na wakute kwenu ugumu.” Hii inamaanisha ya kwamba Waislamu waoneshe ushujaa na ujasiri wao wa kupambana dhidi ya adui kwa nguvu zao zote na kwa hali yoyote ile, ili watambue ya kwamba Waislamu sio watu wa kuchezewa na kutishika na mauti. Kutokana na mafunzo haya ya Uislamu, tunashuhudia katika historia ya Kiislamu, wakati Mtume (s.a.w.w.) alipowataka Maswahaba wake kufanya ziara ya kuizuru Nyumba ya Mwenyezi Mumgu (AlKaaba), aliwataka pindi wanapofanya tawafu watufu kwa haraka na kwa ukakamavu, ili kuwaonesha maadui ya kwamba Waislamu ni watu imara na mashupavu, na miili yao iko na siha nzuri. Hali kama hii pia tunaishuhudia wakati wa kukombolewa mji wa Makka, Mtume (s.a.w.w.) aliwaamrisha Waislamu wawashe moto watakapokuwa wamekaa katika jangwa, ili kuwaonesha makafiri ukubwa wa jeshi la Kiislamu. Jambo hili lilileta faida kubwa katika nafsi zao kwa kuwazidishia mori wa kupambana dhidi ya maadu zao. Pia Mtume (s.a.w.w.) aliweza kuliweka jeshi lake sehemu ambayo Abu Sufiyani aliweza kuliona, ili aone ukubwa wa jeshi hilo. Bila ya shaka tunatambua kwamba ukombozi wa mji wa Makka ulipatikana bila ya kutumika umwagaji damu. Aya inamalizia kwa kutoa bishara njema kwa Waumini wenye kufuata taratibu hizi alizoziweka Mwenyezi Mungu: “Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye takua.” Inamaanisha ya kwamba, kuwa mgumu na kutoonesha huruma kwa adui wa Uislamu ni katika mambo yanayoambatana na uchamungu.
266
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 266
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI NA SITA
ُ اعبُ ُدوا َرب َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ْ اس ُج ُدوا َو َّك ْم َو ْاف َعلُوا ْ ين آ َمنُوا ْ ار َكعُوا َو ُ اج َت َب َ ْر لَ َعلَّ ُك ْم تُ ْفلِ ُح اك ْم ْ اه ُدوا ِفي اللهَِّ َح َّق ِج َها ِد ِه ُه َو َ ْال َخي ِ ون َو َج ُ الدين ِم ْن َح َرج ِملَّ َة أَب ُ َو َما َج َع َل َعلَي ِّ اهي َم ُه َو ي ف م ْك ْ َ يك ْم إِب ِ ِ ْر ِ ِ ٍ ُ ُ ين ِم ْن َقب ُ ُ َس َّم َ ْل َو ِفي هذا لَِيك َ اك ُم ْال ُم ْسلِ ِم الر ُسول َش ِهي ًدا َّ ون ُ َُ ُ َ الص اَل َة َوآتُوا َّ اس َفأَ ِقي ُموا ِ ََّعليْك ْم َو َتكونُوا ش َه َدا َء َعلى الن َّ ْ الز َكا َة َو ير ُ ص ِ َّص ُموا ِباللهَِّ ُه َو َم ْو اَل ُك ْم َف ِن ْع َم ْال َم ْولَىٰ َو ِن ْع َم الن ِ اع َت “Enyi ambao mmeamini! Rukuuni na sujuduni, na mwabuduni Mola Wenu, na fanyeni kheri huenda mkafaulu. Na fanyeni jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, jihadi inayomstahiki. Yeye ndiye ambaye amewachagua. Wala hakuweka juu yenu uzito katika dini. Ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye aliwaita Waislamu tangu zamani na katika hii. Ili Mtume awe shahidi juu yenu na nyinyi muwe mashahidi juu ya watu. Basi simamisheni Swala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Kiongozi bora na Msaidizi bora kabisa.” (Qur’ani; 22:77-78)
Aya hizi mbili zilizoko mwishoni mwa Suratul Hajj, zinawahutubia Waumini kwa kuwabainishia baadhi ya mafunzo ya msingi yanayohusiana na Dini yao. Aya ya kwanza inaanza kwa kusema: “Enyi ambao mmeamini! Rukuuni na sujuduni, na mwabuduni Mola Wenu, na fanyeni kheri huenda mkafaulu.” Aya imetaja nguzo mbili miongoni mwa nguzo za Swala, nazo ni rukuu na sujudu, hii yote ni kuonesha umuhimu na utukufu wa nguzo mbili hizo katika Swala. Na hii amri ya kumwabudu Mola Mlezi baada ya amri ya kurukuu na kusujudu, inajumuisha ibada zote zilizo wajibu kwa Mwislamu, na kutajwa neno ‘Mola Mlezi’ ni ishara ya kwamba ni Yeye tu anayestahiki kuabudiwa, kwani Yeye ndiye Mwenye kuwamiliki waja wote na pia ndiye Mlezi wao. Na amri juu ya kufanya mema, ni mjumuisho wa matendo yote mema bila ya kizuizi au sharti lolote. Na pale iliponukuliwa kutoka kwa Ibn Abbas ya kwamba, muradi wa matendo mema inakusudiwa kuunganisha udugu na kujipamba na tabia njema, kwa hakika mambo 267
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 267
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
haya ni miongoni mwa matendo mema, na makusudio si haya tu, bali kila tendo lenye kuridhiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Aya ya pili Mwenyezi Mungu amewaamrisha Waumini kufanya kila wawezalo katika kuiendeleza Dini Yake, anasema: “Na fanyeni jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, jihadi inayomstahiki.” Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu inamaana pana sana. Kuna jihadi ya kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu na kutekeleza anayoyaamrisha na kuacha aliyoyakataza, kuwatendea watu wema, jihadi dhidi ya nafsi na jihadi dhidi ya adui. Kutokana na mambo haya yaliyo wajibu kwa Mwislamu kuyatenda, huenda baadhi ya watu wakauliza, ni vipi mwili huu wa mwanadamu ulio dhaifu utaweza kuyatekeleza mambo yote haya? Jawabu la suala hili tunalipata katika maneno yasemayo: “Yeye ndiye ambaye amewachagua. Wala hakuweka juu yenu uzito katika dini. Ni mila ya baba yenu Ibrahim.” Mwenyezi Mungu Mwenyewe ndiye aliyewateua wanadamu miongoni mwa viumbe Wake walio wengi, kuwa na uwezo wa kuyafanya haya, hii ni dalili ya neemaZake kubwa kwa wanadamu. Na pindi watakapoangalia vyema na kufikiri vizuri, basi hawatoona kuwepo uzito wowote wa maamrisho yake, kwani maumbile yao yanalingana na mafunzo haya na ni njia ya kufikia ukamilifu wa hali ya juu, na ndani yake kuna ladha ya utamu kuliko ladha ya asali, kwani kila aliloliamrisha lina manufaa makubwa kwa mwenye kulitenda. Na haya si mambo yaliyoanza katika zama za Mtume (s.a.w.w.), bali ndio uliokuwa mwenendo wa baba wa Mitume na baba wa kila Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu; Nabii Ibrahim (a.s.). Nabii Ibrahim (a.s.) ametajwa kama ni baba wa kinasaba wa Waumini. Hii huwenda ni kwa sababu ya Waislamu wa zama hizo walikuwa ni Waarabu waliotokana na Nabii Ismail (a.s.), na Mayahudi waliotokana na Nabii ya Is’haq (a.s.). Au ni kwamba Nabii Ibrahim (a.s.) ni baba wa kiroho wa kila aliyemwamini Mwenyezi Mungu. Pia katika ibara isemayo: “Yeye aliwaita Waislamu tangu zamani na katika hii,” ni dalili ya wazi ya kwamba mafunzo haya si mazito kwa wanadamu, kwani amewaumba katika hali ya kuwa na uwezo wa kusalimu amri juu maarisho yake kama alivyokuwa Nabii Ibrahim (a.s.). Aya inaendelea kusema: “Ili Mtume awe shahidi juu yenu na nyinyi muwe mashahidi juu ya watu.” Ibara hii inawataka Waislamu wawe kigezo chema kwa watu wengine, ili iwe ni njia rahisi ya wao kuwavuta katika Uislamu. Maana ya neno ‘Shahidi’ ni yule anayepata habari kwa njia moja au nyingine juu ya kutokea jambo fulani. Kwa hivyo Mtume (s.a.w.w.) kuwa shahidi kwa Waislamu wote inamaanisha ya kwamba hupata habari juu ya matendo yao, na maana hii inanasibiana na Riwaya zinazoeleza ya kwamba kila mwisho wa wiki hutambulishwa na kupewa habari juu ya matendo ya Waislamu.
268
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 268
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
Maana nyingine ya ‘Shahidi’ ni ile hali ya kuwa matendo ya mtu kuwa mfano na kigezo kwa wengine. Kwa mantiki hii, Waislamu wote wa kweli ni mashahidi, kwani mwenendo wao unaweza kuwa ni kigezo kwa wengine kiasi cha kuwafanya washawishike na kuukubali Uislamu kirahisi, na hivi ndivyo ilivyotokea kwa mataifa mengi kuukubali Uislamu kutokana na tabia njema walizokuwa wamejipamba nazo Waislamu. Kwa hivyo kama vile ambavyo Mtume (s.a.w.w.) ni kigezo kwa Waislamu, basi ni juu yao nao kuwa kigezo chema kwa watu wengine. Kwa kumalizia Aya inasema: “Basi simamisheni Swala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Kiongozi bora na Msaidizi bora kabisa.” Hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha Waumini washikamane Naye kwa vile Yeye ni Mlinzi aliye Bora na msaidizi wa kweli kwa kila mwenye shida na matatizo mbalimbali.
269
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 269
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI NA SABA
ُ ين آ َمنُوا اَل َتتَّبعُوا ُخ ََّيا أَُّي َها ال َ الشي َّ ات َ ان َو َم ْن َيتَّ ِب ْع ْط و ط ذ َ ِ ِ ِ ِ ْ ُ ُخ ُضل ْ ْ َ الشي َّ ات ْ ان َفإِنَّ ُه َيأ ُم ُر ِبال َف ْح َشا ِء َوال ُم ْن َك ِر َولَ ْو اَل َف ْط و ط َ ِ ِ َ َ َّلله ِّ ُ ُ اللهَِّ َعلَي َ ْك ْم َو َر ْح َمتُ ُه َما َز َكىٰ ِم ْنك ْم ِم ْن أ َح ٍد أ َب ًدا ولكن ا َ ي ُزكي ْ َم ْن َي َشا ُء َواللهَُّ َس ِمي ٌع َعلِي ٌم َو اَل َي ْأ َت ِل أُولُو ْال َف الس َع ِة َّ ض ِل ِم ْن ُك ْم َو َأ ْ ين َو ْ ُؤتُوا أُولِي ْال ُق ْر َبىٰ َو ْ ْ َ َ ب س ي ف ين ر اج ه م ال ك ا س م ال ي ن ُ َ َ َ َ َِّيل الله ِ ِ ِ ِ ِِ َُّلله ُ َو ْل َيع َ ص َف ُحوا أَ اَل تُ ِحب ور ٌ ُّون أَ ْن َي ْغ ِف َر اللهَُّ لَ ُك ْم َوا َغ ُف ْ ْفوا َو ْل َي َر ِحي ٌم “Enyi ambao mmeamini! Msifuate nyayo za shetani. Na atakayefuata nyayo za shetani, basi yeye huamrisha machafu na maovu. Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema Yake, asingelitakasika miongoni mwenu yoyote kabisa. Lakini humtakasa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni Msikizi, Mjuzi. Na wale katika nyinyi wenye wasaa wasiape kutowapa walio jamaa na maskini na waliohama katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe na waachilie mbali. Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu awasamehe? Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani; 24:21-22)
MAELEZO Aya hizi mbili zinamafungamano na tukio maarufu la kusingiziwa uovu mmoja kati ya wake wa Mtume (s.a.w.w.), ni tukio ambalo liliweza kupenya katika vichwa vya baadhi ya Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) na kulivalia njuga, kwa hiyo Mwenyezi Mungu anawatahadharisha Waumini dhidi ya kuathirika na fikra za kishetani, na wasipozingatia haya, matokeo yake yatakuwa mabaya mno. Hali ya mtu kushawishiwa na shetani inakuwa ni hali ambayo inamuwia vigumu kuweza kuitambua, kwa hiyo mtu anapohisi hali ya kusukumwa kwenye maovu, basi atambue ya kwamba huo ni ushawishi unaotoka kwa shetani, kwa hiyo achukue maamuzi ya kukataa ushawi270
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 270
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
shi wake, Aya inasema: “Enyi ambao mmeamini! Msifuate nyayo za shetani. Na atakayefuata nyayo za shetani, basi yeye huamrisha machafu na maovu.” Ikiwa tutachukua maana ya shetani kuwa ni kila kiumbe kiovu na chenye kuleta uharibifu, itatulazimu kuwa na tahadhari katika nyanja zote za maisha yetu, kwani inakuwa ni vigumu kwa Muumini wa kweli kuvutwa katika maasi kwa mara ya kwanza, lakini kutokana na mambo fulani anaweza kutumbukia katika shimo la maasi, baadhi ya mambo hayo ni kama yafuatavyo: Kwanza: Kuwafanya marafiki watu waovu. Pili: Kushiriki katika vikao vya watu waovu. Tatu: Kufikiri kutenda maovu. Nne: Kutenda mambo yenye shubha (yasiyo bayana juu uhalali na uharamu wake). Tano:Kutenda madhambi madogo madogo. Sita: Kutahiniwa kwa mambo makubwa na mazito, katika hali hii baadhi ya watu huwa tayari kumuasi Mwenyezi Mungu, kwani analoangalia ni kutatuka kwa shida yake kwa hali yoyote ile. Kwa kweli hizi zote ni miongoni mwa hatua za shetani. Baada ya hapo, Aya inaeleza neema kubwa ya Mwenyezi Mungu aliyomneemesha mwanadamu: “Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema Yake, asingelitakasika miongoni mwenu yoyote kabisa. Lakini humtakasa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni Msikizi, Mjuzi.” Bila ya shaka fadhila za Mwenyezi Mungu na neema Zake zinamkinga mwanadamu dhidi ya mambo maovu na machafu. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu akili, pamoja na akili hiyo amempelekea Mitume ili kumrahisishia kupata uongofu, zaidi ya hayo ni kupata utakaso maalumu wa kiroho kutoka Kwake. Yote haya mwanadamu huyapata kutoka kwa Mwenyezi Mungu ikiwa ataamua kwa dhati kabisa kuwa mtiifu mbele ya Mola Wake Muumba, kwani Mwenyezi Mungu humuongoa yule anayetaka kuongoka na kuipigania Dini Yake kikweli kweli. Atakapofanya hivyo, hapo Mwenyezi Mungu atamshika mkono wake na kumuhifadhi dhidi ya ushawishi na wasiwasi wa shetani. Kama tulivyotangulia kusema ya kwamba Aya hizi zina mafungamano na tukio la kusingiziwa uovu mmoja kati ya wake wa Mtume (s.a.w.w.), kwa hivyo baadhi wa wafasiri wanasema Aya hii iliteremka baada ya baadhi ya Maswahaba kuapa
271
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 271
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
kwa Mwenyezi Mungu ya kwamba hawatowapa msaada wowote wale walioeneza uzushi huo kwa watu, na kutoshirikiana nao kwa lolote lile, hapo Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hii ili kuzuia mambo haya yasifanyike, na badala yake wawe ni wasemehevu kama Aya ya pili inavyosema: “Na wale katika nyinyi wenye wasaa wasiape kutowapa walio jamaa na maskini na waliohama katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe na waachilie mbali. Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu awasamehe? Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” Wafasiri wa madhehebu ya Kisunni wanasema ya kwamba Aya hii iliteremka kutokana na Abu Bakr kula kiapo ya kwamba hatompatia msaada wowote wa kimali na kiutu Mustah ibn Athatha, mtu ambaye ndiye aliyeshabikia na kueneza uovu dhidi ya mke wa Mtume (s.a.w.w.), lakini tunapoviangalia viwakilishi tunavikuta vimekuja katika hali ya wingi. Hivyo kitu kilichojitokeza baada ya kueneza uvumi huo, baadhi ya Maswahaba walichukua uamuzi wa kuwatenga na kuwakata kabisa wavumishi, ndipo Mwenyezi Mungu akawakataza kufanya hivyo kwa kupitia Aya hii. Jambo la msingi linalopaswa kutambuliwa na kila Mwislamu ni kwamba Aya za Qur’ani hazihusiani na sababu za watu maalumu walioteremshiwa peke yao, bali zinawahusu Waislamu wote mpaka kitakaposimama Kiyama, basi kwa hivyo Aya hii inawaasa Waislamu wote kwa ujumla ya kwamba wasitangulize matakwa ya nafsi zao na kuwachukulia hatua kali watu wenye makosa, bali ni vyema kwao kuwa wavumilivu na wasamehevu, kama vile ambavyo wao wanapenda kusamehewa makosa yao na Mwenyezi Mungu, na mtu kuwa msamehevu na mwenye huruma huwa amejipamba na sifa miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Katika Aya hizi kuna somo kubwa kwa Waislamu, kwani inawataka wasivuke mipaka katika kuwaadhibu wakosaji, na wala haifai kuwafukuza kutoka katika makaazi yao na kuwapeleka katika jamii isiokuwa ya Kiislamu, au kuwazuilia msaada, haya yote ni kwa ajili ya kuwazuia wasiendelee katika uovu wao au kuweza kushirikiana na adui dhidi ya Uislamu.
272
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 272
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI NA NANE
ً ين آ َمنُوا اَل َت ْد ُخلُوا بُي َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ْر بُيُو ِت ُك ْم َحتَّىٰ َت ْس َت ْأ ِن ُسوا َ ُوتا َغي َ ْر لَ ُك ْم لَ َعلَّ ُك ْم َت َذ َّك ُر ون َفإِ ْن لَ ْم ٌ َوتُ َسلِّ ُموا َعلَىٰ أَ ْهلِ َها َذٰلِ ُك ْم َخي َُتج ُدوا ِفي َها أَ َح ًدا َف اَل َت ْد ُخل َ ُؤ َذ َن لَ ُك ْم َوإ ْن ِق َّوها َحت ْ َ يل لَ ُك ُم ي ٰ ى ِ ِ َ ُار ِجعُوا ُه َو أَ ْز َكىٰ لَ ُك ْم َواللهَُّ ِب َما َت ْع َمل ْس ْ ار ِجعُوا َف ْ َ ون َعلِي ٌم لَي َُّاع لَ ُك ْم َوالله ُ َعلَي ً اح أَ ْن َت ْد ُخلُوا بُي ٌ ْر َم ْس ُكو َن ٍة ِفي َها َم َت ٌ ْك ْم ُج َن َ ُوتا َغي َ ون َو َما َت ْكتُ ُم َ َيعْلَ ُم َما تُ ْب ُد ون “Enyi ambao mmeamini! Msiingie nyumba zisizo nyumba zenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee salaam wenyewe. Hayo ni bora kwenu ili mpate kukumbuka. Na msipomkuta yoyote humo basi msiingie mpaka mruhusiwe. Na mkiambiwa rudini, basi rudini. Hivyo ni usafi zaidi kwenu na Mwenyezi Mungu anajua mnayoyatenda. Si vibaya kwenu kuingia nyumba zisizokaliwa ambazo ndani yake mna bidhaa zenu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayoyadhirisha na mnayoyaficha.” (Qur’ani; 24:27-29)
MAELEZO Aya hizi zinabainisha mafunzo ya Kiislamu yanayotakiwa kufuatwa katika maisha ya kijamii kwa lengo la kuhifadhi utu wa mwanadamu na kujenga jamii iliyo bora na yenye kuheshimiana na kushikamana. Hapa Aya inatuelezea namna ya kuingia katika nyumba ya mtu mwingine ni kitu gani kinatakiwa kifanywe, inasema: “Enyi ambao mmeamini! Msiingie nyumba zisizo nyumba zenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee salaam wenyewe.” Kwa hivyo pindi mtu anapotaka kuingia nyumba ya mtu mwingine analazimika kuashiria ya kwamba anataka kufanya hivyo na baada yake apate ruhusa ya kuingia. Neno lililotumika ni Tasta-anisuu likiwa na maana ya kuomba ruhusa, na halikutumika neno Tasta-adhinuu lenye maana ya kuomba ruhusa ya kuingia kwa namna yoyote ile. Hiyo ni kwa sababu nenoTasta-anisuu linamaana ya kuomba ruhusa ya kuingia kwa njia ya heshima, adabu na kwa upole, kwa hivyo 273
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 273
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
haitakiwi mtu kupiga makelele, kugonga mlango kwa nguvu, kutumia maneno makali au kuingia kabla ya kupewa ruhusa, na mtu akisharuhusiwa aingie kwa heshima na adabu na jambo la kwanza ni kuwasalimia wenyeji kwa maamkizi yenye mapenzi na bashasha. Kitu kikubwa cha kufikiri katika mafunzo haya yenye kuzingatia heshima na utukufu wa mwanadamu ni kule kufuatiliwa na ibara mbili, ibara ya kwanza inasema: “Hayo ni bora kwenu.” Na ibara ya pili inasema: “Ili mpate kukumbuka.” Hii ni dalili ya wazi ya kwamba hukumu hii inakubalika na kila akili ya kibinadamu, na kila mwenye kufikiria hukumu hii ataona ni namna gani ilivyobeba kheri na utengamano kati ya watu. Aya inayofuata inakamilisha mambo yaliyomo katika hukumu hii kwa kusema: “Na msipomkuta yoyote humo basi msiingie mpaka mruhusiwe.” Hapa tunajifunza ya kwamba iwapo kwa mfano katika nyumba yumo mtu ambaye hana haki ya kumruhusu mtu mwingine kuingia pasi na ruhusa ya mwenye nyumba, hapo hatokuwa na ruhusa ya kuingia, au wakati mwingine inawezekana ikawa hakuna yeyote katika nyumba na mwenyewe yuko karibu na hapo. Katika hali yoyote ile si ruhusa kwa mtu kuingia katika nyumba bila ya ruhusa ya mwenyewe. Aya inaendelea kusema: “Na mkiambiwa rudini, basi rudini.” Haifai mtu kukereka na kukasirika ikiwa hakuruhusiwa kuingia, kwani huenda wakati huo mwenye nyumba hayuko katika hali inayomfanya aruhusu mtu kuingia, au nyumba kutokuwa katika mazingira ya kuingia wageni. Baadhi ya watu pindi wanapokataliwa kuingia katika nyumba huwapelekea kufikiri mambo mbalimbali na hatima yake kuanza kupeleleza au kuchungulia ili kutaka kujua mna nini mpaka asiruhusiwe kuingia, Mwenyezi Mungu alilijua hilo mapema, ndio Aya ikaendelea kusema: “Na Mwenyezi Mungu anajua mnayoyatenda.” Hukumu ya kuomba ruhusa ya kuingia haihusiani na nyumba zote, bali kuna baadhi ya nyumba mtu anaruhusiwa kuingia pasi na kupiga hodi, yote hayo ni kwa ajili ya kuondosha uzito katika maisha ya kila siku ya wanadanu. Aya ya pili inaweka bayana juu ya hayo kwa kusema: “Si vibaya kwenu kuingia nyumba zisizokaliwa ambazo ndani yake mna bidhaa zenu.” Na inakamilisha kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu anajua mnayoyadhihirisha na mnayoyaficha.” Tunaweza kujifunza hapa ya kwamba ruhusa ya kutoomba ruhusa katika majengo haya ni kule kutokaliwa na watu kama vile magofu yasiyomilikiwa na watu maalumu, ambapo humo mtu huweza kujifunza mambo mbalimbali, au katika majengo ambayo kwa kawaida watu hawaombi ruhusa ya kuingia kama vile masoko, hospitali n.k. Pamoja na hivyo si ruhusa kuitumia fursa hii vibaya kwani Mwenyezi Mungu anajua wanayoyadhihirisha na wanayoyaficha. 274
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 274
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
UTAFITI Usalama Na Uhuru Ndani Ya Nyumba: Bila ya shaka maisha ya mwanadamu yamegawika sehemu mbili: sehemu yake binafsi na sehemu ya jamii inayomzunguka, kila sehemu katika sehemu hizi ina taratibu zake na adabu zake. Kwa mfano mtu anapokuwa katika maisha ya kijamii, analazimika kuvaa mavazi maalumu na kutenda mambo makhsusi, na mtu kuishi katika hali hii kwa muda wote wa masaa ishirini na nne kunamsababishia uchovu na hasira, kwa hivyo hupenda kuwa na uhuru kwenye baadhi ya wakati wa mchana na usiku, ili aepukane na vizuizi kadha wa kadha, na badala yake awe na familia yake na watoto wake. Kwa hivyo huamua kurejea nyumbani kwake kwa ajili ya kutafuta matakwa yake na kujiweka mbali na jamii kwa muda maalumu, na kwa hivyo hapa inapasa hali ya nyumba iwe iko katika amani na utulivu wa kutosha. Ama ikiwa kila mtu atataka kuingia ndani, hapo nyumba itakosa heshima yake na kunyang’anywa amani yake na utulivu na kuwa kama soko au barabara. Jambo hili la kulinda uhuru wa mtu katika nyumba yake ni jambo lililokuwepo katika zama zote, na hata hivi leo baadhi ya nchi zimeweka sheria ya mtu kutoingia nyumba ya mwingine bila ya ruhusa yake, na mwenye kukhalifu huadhibiwa. Na hapa tumeona katika Aya hizi ni namna gani Uislamu unavyozingatia haki hii, na si hivyo tu kuna Riwaya mbalimbali zilizokuja kusisitiza utekelezaji wake. Imepokewa kwamba siku moja Abu Said al-Khudriy aliomba ruhusa ya kuingia katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) huku akiwa ameuwelekea mlango, Mtume (s.a.w.w.) alimwambia:
.ال تستأذن وأنت مستقبل الباب “Usiombe ruhusu huku ukiwa umeuelekea mlango.”124
Kwa hiyo hapa Uislamu unatufunza pindi mtu anapopiga hodi asiuelekee mlango, na badala yake asimame upande wa kulia au kushoto. Katika Riwaya nyingine Mtume (s.a.w.w.) amesisitiza hata kupiga hodi wakati mtu anapotaka kuingia katika nyumba ya wazazi wake. Amri hii ilikuja baada ya mtu mmoja kumuuliza kwa kusema: Je, niombe ruhusa wakati ninapotaka kuingia kwa mama yangu? Mtume (s.a.w.w.) alimjibu: Ndio, yule mtu akauliza tena: Je, nimuombe ruhusa kila ninapoingia na ilhali hana mhudumu mwingine isipokuwa 124
Al-Haythamiy, Majma’u Zawaid, Jz. 8, Uk. 43 275
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 275
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
mimi? Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza: Je, unapenda umuone bila ya kuwa na nguo? Yule mtu akasema: Hapana. Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: Basi muombe ruhusa ya kuingia.125 Pia imepokewa kutoka kwa Imamu al-Baqir (a.s.) kutoka kwa Jabir ibn Abdillahi al-Ansariy, amesema: “Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alitoka akielekea nyumbani kwa binti yake; Fatima (a.s.) nami nikiwa naye, tulipofika aliomba ruhusa ya kuingia, huku akiuliza: Niingie? Bibi Fatima (a.s.) akamwambia: Ingia. Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza tena: Je, Niingie pamoja na swahiba wangu? Bibi Fatima (a.s.) akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sijajitanda. Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: Chukua mtandio ujitande. Bibi Fatima (a.s.) akafanya hivyo (akajitanda), na baada ya hapo Mtume (s.a.w.w.) akatoa salamu na Bibi Fatima (a.s.) akarudisha salamu. Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza tena: je, Niingie? Bibi Fatima (a.s.) akasema: Ingia. Mtume (s.a.w.w.) akauliza: Je, Niingie pamoja na swahiba wangu? Akjibu: Ingia na swahiba wako. Jabir akasema: hapo Mtume (s.a.w.w.) akaingia ndani na mimi pia nikaingia…”126 Riwaya hii inatufunza ni namna gani Mtume (s.a.w.w.) yeye mwenyewe alivyokuwa akichunga heshima ya watu wengine na kuzingatia uhuru wao, kwa hivyo ni juu ya kila Mwislamu kufuata nyayo zake na kumfanya kigezo cha maisha yake, kwani hakuna kigezo kilicho bora zaidi ya yeye. Imamu as-Sadiq (a.s.) naye anatufunza juu ya haki hii ya kibinadamu kwa kusema:
ّ أ ّو:اإلستئذان ثالثة والثّالثة, والثّانية يحذرون,لهن يسمعون .إن شاؤوا أذنوا و إن شاؤوا لم يفعلوا فيرجع المستأذن “Kuomba ruhusa (ya kuingia ndani) ni mara tatu: mara ya kwanza wapate kusikia, mara ya pili wapate kuchukua hadhari, mara ya tatu (wataamua) wakitaka watamruhusu na wakitaka hawatomruhusu, basi ni juu ya muombaji ruhusa kurejea.”127
Baadhi ya wafasiri wanaonelea bora kuwepo masafa ya wakati kati ya hodi zinazopigwa katika kuomba ruhusa, kwani huenda mwenye nyumba akawa hayuko katika mavazi ya kawaida au mazingara hayajawekwa sawasawa kwa kukaribishwa mgeni, na kama mgeni hakuitikiwa hodi yake au akiambiwa kwanza arejee, basi asikasirike na kuazimia kutokurejea tena kwa mtu huyo. Tabariy, Jami’ul Bayan, Jz.18, Uk. 148 Kulayniy, Usulul Kafiy, Jz. 5, Uk. 528 127 Hurrul Amiliy, Wasailu Shia, Jz. 2, Uk. 218 125 126
276
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 276
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA KHAMSINI NA TISA
َ ين َملَ َك ْت أَ ْي َمانُ ُك ْم َوالَّ ِذ َ ين آ َمنُوا لَِي ْس َت ْأ ِذ ْن ُك ُم الَّ ِذ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين لَ ْم َ ص اَل ِة ْال َف ْج ِر َو ِح ين ٍ َيبْلُ ُغوا ْال ُحلُ َم ِم ْن ُك ْم َث اَل َث َم َّر َ ْل ِ ات ِم ْن َقب َّ ُون ِث َيا َب ُك ْم ِم َن َ َت َ ضع ص اَل ِة ْال ِع َشا ِء َث اَل ُث َ الظ ِه َ ير ِة َو ِم ْن َب ْع ِد ُ َ َ ات لَ ُك ْم لَي َ َ اح َب ْع َد ُه َّن َط َّو ُاف ون ٌ ْه ْم ُج َن ٍ َع ْو َر ِ ْس َعليْك ْم َو اَل َعلي َُّات َوالله ُ َعلَي َ ُ ُ ْك ْم َبع ُ ْض َك َ ٰذلِ َك يُ َبي ِ ِّن اللهَُّ لَ ُك ُم الآْ َي ٍ ْضك ْم َعلىٰ َبع َ َْعلِي ٌم َح ِكي ٌم َوإ َذا َبلَ َغ أ ُ ال ْط َف اس َت ْأ َذ َن ْ ال ِم ْن ُك ُم ْال ُحلُ َم َف ْل َي ْس َت ْأ ِذنُوا َك َما ِ َُّلله َُّلله ُ َ َ ُ ين ِم ْن َق ْبلِ ِه ْم َك َذٰلِك يُ َبي َ الَّ ِذ ِّن ا لك ْم آ َيا ِت ِه َوا َعلِي ٌم َح ِكي ٌم “Enyi ambao mmeamini! Na wawatake ruhusa, wale ambao imewamiliki mikono yenu ya kuume na wale ambao hawajafikia baleghe miongoni mwenu, mara tatu kabla ya Swala ya Alfajiri na wakati mnapovua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Swala ya Isha. Ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Aya; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima. Na watoto wanapofikia kubaleghe basi na watake ruhusa, kama walivyotaka ruhusa wa kabla yao. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Aya Zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.” (Qur’ani: 24:58-59)
MAELEZO Utaratibu Maalumu wa Kuingia Kwa Wazazi Wawili: Aya hizi mbili ni miongoni wa Aya nyingi zilizomo ndani ya Suratan-Nur zinazoelezea mambo yanayohusu kulinda heshima ya watu wengine. Aya hizi nazo zinatoa mafunzo kwa watoto walio baleghe na wale wasio baleghe kuomba ruhusa kabla ya kuingia kwa wazazi wao kama Mwenyezi Mungu anavyosema: “Enyi ambao mmeamini! Na wawatake ruhusa, wale ambao imewamiliki mikono yenu ya kuume na wale ambao 277
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 277
12/8/2014 2:43:45 PM
WITO KWA WAUMINI
hawajafikia baleghe miongoni mwenu, mara tatu kabla ya Swala ya Alfajiri na wakati mnapovua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Swala ya Isha. Ni nyakati tatu za faragha kwenu.” Hapa Mwenyezi Mungu anawahutubia Waumini wenye watoto au watumwa au wajakazi kuwafundisha watoto wao namna ya kufanya pindi wanapotaka kuingia sehemu ya wazazi hasa katika nyakati tatu, nyakati ambazo kwa kawaida huwa ni nyakazi za mapumziko na za faragha baina ya wanandoa. Bila ya shaka watoto wanaolengwa katika Aya hii ni wale wenye uelewa juu ya mahusiano kati ya mke na mume, kwa hiyo wanatakiwa waamrishwe kuomba ruhusa waingiapo kwa wazazi wao. Lakini kinyume na nyakati hizo tatu za faragha, itakuwa hakuna tatizo lolote kwa wazazi na kwa hao watoto kuingia katika chumba cha wazazi wao bila ya kupiga hodi ili kuondosha uzito juu yao: “Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Aya; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.” Katika Aya ya pili Mwenyezi Mungu anabainisha hukumu ya watoto waliokwisha baleghe kwa kusema: “Na watoto wanapofikia kubaleghe basi na watake ruhusa, kama walivyotaka ruhusa wa kabla yao.” Hukumu ya watoto walio baleghe na wale ambao hawajabaleghe inatofautiana, ambao hawajabaleghe wanatakiwa kuomba ruhusa kwenye nyakati tatu tu, hii ni kutokana na kuwa na mahitaji mengi kutoka kwa wazazi wao, ama waliokwisha baleghe wanatakiwa kuomba ruhusa kila wakati wanapotaka kuonana na wazazi wao ndani ya chumba cha wazazi. Hukumu hii ni makhsusi wakati wa kuingia katika chumba chao tu. Kwa kutilia mkazo na katika kuonesha umuhimu wa hukumu hii, Aya inahitimisha kwa kusema: “Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Aya Zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.” Hekima Ya Kuomba Ruhusa Ya Kuingia Ndani: Hakuhitajiki kutumia nguvu katika kung’oa baadhi ya mizizi ya maovu katika jamii, hasa maovu yanayotokana na mahusiano kati ya mwanamke na mwanamume, bali kinachohitajika ni jamii kuelimishwa mafunzo ya Kiislamu na kushikamana nayo. Ndio maana Uislamu haukuacha kuelezea namna ya kuingia katika nyumba ya watu au watoto na wafanyakazi kuomba ruhusa pindi wanapotaka kuingia katika chumba cha wazazi. Hii ni dalili ya kutoghafilika kwa Dini ya Kiislamu juu ya kujenga jamii imara yenye kuheshimiana. Kwa masikitiko, licha ya mafunzo haya yaliyo bora yaliyoelezwa na Mwenyezi Mungu, ni mara chache kuona yameandikwa au kusikika yakizungumzwa katika mihadhara, licha ya kuwa ni katika mambo yaliyo wajibu kwa kila Mwislamu. Na hata kama tutaona ya kwamba ni katika mambo yasio waji278
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 278
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
bu, basi pia inahitajika kuzungumziwa. Kuna baadhi ya watu wanaodhani ya kwamba watoto hawatambui masuala ya kijinsia au wafanyakazi wa ndani hawajishughulishi na kutaka kujua kinachoendelea, lakini ukweli wa mambo ni kwamba watoto wanaathirika na hali hiyo seuze wakubwa. Kwa wazazi kutowachunga watoto wao dhidi ya mambo wasiyopaswa kuyaona huenda watoto hao wakasibiwa na matatizo ya kisaikolojia na hata kupelekea kujenga chuki kubwa kwa wazazi wao. Hapa ndipo tunapojua umuhimu mkubwa wa mafunzo haya ya Uislamu. Kwa hiyo tunawasihi wazazi kuwafunza watoto wao mafunzo haya, na kuchukua kila tahadhari wanapokuwa katika faragha dhidi ya kuonwa na watoto wao. Si hayo tu bali inapasa kuwalaza watoto wakubwa mbali na chumba cha wazazi. Mtume (s.a.w.w.) anasema:
.بي في المهد ينظر إليهما ّ إيّاكم وأن يجامع ّ الرجل امرأته ّ والص “Tahadharini juu ya mtu kumuingilia mke wake na huku kuna mtoto katika kitanda akiwaangalia.”128
128
Almajlisiy, Biharul Anwar, J. 100 Uk. 295 279
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 279
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI
ُ ين آ َمنُوا ْاذ ُك ُروا ِن ْع َم َة اللهَِّ َعلَي َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ْك ْم إِ ْذ َجا َء ْت ُك ْم ُجنُو ٌد ََفأَ ْر َس ْل َنا َعل َ ُان اللهَُّ ِب َما َت ْع َمل َ يحا َو ُجنُو ًدا لَ ْم َت َر ْو َها َو َك ون ي ً ْه ْم ِر ِ َ ْ ُ ُ ُ َ َ يرا إِ ْذ َجا ُءوك ْم ِم ْن َف ْو ِقك ْم َو ِم ْن أ ْس َفل ِم ْنك ْم َوإِذ َز اغ ِت ً ص ِ َب َ ْأ ُّ َِّون بالله ُ وب ْال َح َناج َر َو َت ُار َو َبلَ َغ ِت ْال ُقل ُّ َ ُ الظنُو َنا ُه َنالِ َك ن ظ ْص ب ال ُ َ ِ ِ َ ُابْتُلِ َي ْال ُم ْؤ ِمن ون َو ُز ْل ِزلُوا ِز ْل َز اًال َش ِدي ًدا “Enyi ambao mmeamini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu; pale yalipowafikia majeshi, tukayapelekea upepo na majeshi msiyoyaona na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda. Walipowajia kutoka juu yenu na kutoka chini yenu; na macho yakakodoka na nyoyo zikapanda kooni, na mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali. Hapo waumini walijaribiwa na wakatikiswa mtikiso mkali.” (Qur’ani; 33:9-11)
MAELEZO Aya hizi na nyinginezo katika Sura hii zinaelezea mtihani mkubwa na mgumu waliokumbana nao Waislamu katika kutahiniwa kiwango cha imani walichonacho kwa njia ya vitendo. Katika Aya hizi, Mwenyezi Mungu anaelezea tukio la kihistoria katika historia ya Uislamu. Tukio hilo ni tukio la vita vya Ahzab (Handaki). Ni tukio ambalo liligeuza sura ya hali ya mambo kwa Waislamu kwa kuibuka na ushindi mnono, ushindi huo ulikuwa ni ufunguo wa ushindi mwingine. Katika vita hivyo maadui waligeuza migongo yao na kushindwa kupanga jambo lolote lenye madhara kwa Waislamu. Vita vya Ahzab viliweza kuwashinda maadui wa vikundi mbalimbali na kuharibu miundo mbinu ya maisha yao na kuifanya Dini ya Kiislamu kusonga mbele. Kwa mara ya kwanza vita hivyo vilionesha cheche zake dhidi ya Mayahudi wa Bani Nadhir ambao walikwenda katika Mji wa Makka na kuhadaiwa na Makuraish ya kwamba watakuwa pamoja nao bega kwa bega katika mapambano yao dhidi ya Mtume (s.a.w.w.) hadi mtu wa mwisho, kisha wakafuatia watu wa kabila la Ghatfan, na wao pia walijiandaa dhidi ya Mtume (s.a.w.w.) na kuwaita washirika 280
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 280
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
wao wawasaidie, kama vile watu wa makabila ya Bani Asad na Bani Saliim. Baada ya hawa wote kuhisi madhara watakayoyapata kutoka kwa Waislamu, waliungana pamoja dhidi ya Uislamu kwa lengo la kuufuta kabisa na kumuua Mtume (s.a.w.w.) na Maswahaba wake, na kusibakie kitu kinachoitwa Uislamu. Ama Waislamu baada ya kuona maandalizi haya ya kijeshi yalioelekezwa dhidi yao, walikusanyika na kushauriana la kufanya baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Mtume (s.a.w.w.), na baada ya mashauriano wakakubaliana na mawazo ya Salman Al-Farisy ya kuchimba mahandaki pembezoni mwa mji wa Madina ili maadui wasiweze kuwafikia kwa urahisi. Vita hivi pia vinajulikana kwa jina la vita vya Handaki kutokana na mahandaki yaliochimbwa. Kwa kweli kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Waislamu, kiasi cha kuzifanya nyoyo (roho) kufikia kooni (walikaribia kufariki dunia) kutokana na maandalizi makubwa ya kijeshi dhidi yao, hali wao wakiwa na jeshi dogo tena lenye uchache wa zana za kivita. Na kwa upande mwingine kulikuwa na kikundi cha wanafiki miongoni mwao, kilichokuwa kikieneza fikra potofu miongoni mwa waislamu, kwa maslahi ya adui. Katika vita hivyo maadui walikuwa elfu kumi, huku Waislamu wakiwa elfu tatu, na maandalizi ya makafiri yakiwa ni ya hali ya juu kiasi cha kuwafanya baadhi ya Waislamu wajione kwamba mwisho wao umewadia. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kuteremsha kipigo kingine kwa makafiri na kuwafichua wanafiki waliomo katika safu ya Waislamu, na kuwafedhehesha wale waliokuwa wakila njama dhidi ya Uislamu na Waislamu. Mwisho wa mapambano Waislamu ndio walioibuka washindi, kwani Mwenyezi Mungu aliuamrisha upepo uvume kwa kasi kubwa. Upepo huo uliweza kuyang’oa mahema ya makafiri na kuzipoteza silaha zao na kukaingia khofu kubwa katika nyoyo zao, na si hivyo tu, bali pia aliwapeleka Malaika ili wawasaidie Waislamu. Zaidi ya hayo ni uwezo mkubwa aliompa Ali ibn Abi Talib kuweza kupambana na hatimaye kumuua Amru ibn Abdiwuddi. Kutokana na hali hiyo makafiri walilazimika kukimbia, na kwa hivyo hawakuweza kufanya chochote chenye madhara kwa Waislamu. Kutokana na vita hivi Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya kumi na saba, na miongoni mwa hizo ni Aya hizi tatu tulizozinakili katika kijitabu chetu hiki. Kwa hiyo baada ya kupita muda tokea siku vilipotokea vita hivyo, Mwenyezi Mungu anawataka Waumini wajikumbushe namna alivyowaneemesha miongoni mwa neema Zake, anasema: “Enyi ambao mmeamini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu; pale yalipowafikia majeshi, tukayapelekea upepo na majeshi msiyoyaona na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.” Hapa Waislamu wanatakiwa kujikumbusha na kufikiria neema za Mwenyezi Mungu, na kutambua ya 281
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 281
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
kwamba siku zote Yeye yuko na wamchao, na katu hayuko tayari kuwaona Waumini wanakaliwa juu na maadui wa Uislamu. Aya ya pili inaeleza hali waliyokuwa nayo Waislamu kabla ya kuanza mapambano, baada ya kuona wingi wa maadui na maandalizi yao, huku wao wakiwa wachache wa wapiganaji na silaha: “Walipowajia kutoka juu yenu na kutoka chini yenu; na macho yakakodoka na nyoyo zikapanda kooni, na mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali. Hapo waumini walijaribiwa na wakatikiswa mtikiso mkali.” Aya hii inaashiria namna maadui walivyokuwa wameuzunguka mji wa Madina kila upande, na kutokana na hali hiyo baadhi ya Waislamu wakaingiwa na khofu kubwa kiasi cha kuwafanya wakodoe macho kama vile mtu anayekaribia kukata roho, na huku wakiwaza dhana potofu dhidi ya Mwenyezi Mungu. Hii ni kutokana na Waislamu hao kutokuwa na imani iliyokamilika. Hao ndio wanaoelezwa katika Aya ifuatayo ya kwamba walitingishwa mtingisho mkubwa. Pengine walikuwa wakidhania ya kwamba watashindwa na maadui watapata ushindi kutokana na maandalizi yao makubwa, na hapo itakuwa ndio mwisho wa Uislamu, na ile ahadi ya ushindi aliyoitoa Mtume (s.a.w.w.) katu haitotimia. Bila shaka fikra kama hizi ni dalili ya udhaifu mkubwa wa Imani. Hali hii ni kama ile iliyojitokeza wakati wa vita vya Uhud, kama Mwenyezi Mungu anavyosimulia kwa kusema:
َ َو َطآ ِئ َف ٌة َق ْد أَ َه َّم ْت ُه ْم أَ ُنف ُس ُه ْم َي ُظ ُّن ْر ْال َح ِّق َظ َّن َ ون ِباللِهّ َغي …اهلِيَّ ِة ِ ْال َج “…Na kundi jingine nafsi zao ziliwashughulisha hata wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyokuwa ya haki, dhana ya kijinga…”
Na bila shaka walengwa katika Aya hii ni Waumini waliokuwa na imani dhaifu na wale waliokuwa wapya katika Uislamu, na hili ni jambo la kawaida kutokea kwa watu wa aina hiyo. Kwa hakika mtihani wa Mwenyezi Mungu ulikuwa umefika pahala pazito kwa Waislamu, kama Aya inavyosema: “Hapo waumini walijaribiwa na wakatikiswa mtikiso mkali.” Mtihani huo ulikuwa mgumu na mzito kwa wale walioanza kupatwa na wasiwasi wa kishetani kabla ya mapambano kuanza, na ni jambo la kawaida mtu anaposongwa na mawazo mwili wake kutoacha kudhihirisha yale anayoyawaza. Kwa vile Waumini hao walikuwa wakiwaza kushindwa na adui yao, walionesha taharuki na woga baada ya maadui kudhihirisha nguvu zao. Mfano wa wazi wa kizaazaa na taharuki iliyowakumba Waislamu ni pale majemedari watano wa 282
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 282
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
Kikuraishi wakiongozwa na Amru ibn Abdiwuddi walipoweza kuyaruka mahandaki na kuingia upande wa Waislamu na huku wakinadi: “Je,kuna yeyote wakuweza kupambana nasi?” Umar ibn Abdiwuddi ndiye ambaye alikuwa akionesha kejeli zaidi kwa Waislamu kwa maneno yake ya kifedhuli na istihizai. Alikuwa akisema: “Enyi Waislamu, nyinyi mnadai ya kwamba atakayeuwawa kati yenu atakwenda Peponi! Basi kuna yeyote kati yenu aliye na hamu ya kwenda Peponi nimpeleke Peponi?” Kutokana na kizaazaa na kiwewe kilichokuwa kimewatanda Waislamu wengi, wote walinyamaza kimya, na hakuna aliyekuwa tayari kukabiliana na Amru ibn Abdiwuddi isipokuwa Ali ibn Abi Talib (a.s.) (Simba wa Mwenyezi Mungu mwenye kushinda) ndiye mtu peke yake aliyethubutu kunyanyua sauti yake na kuwa tayari kupambana naye. Na kwa kweli aliweza kumuuwa adui huyo aliyekuwa akiogopwa na kila mtu, na ikawa ni ushindi mwingine kwa Waislamu na neema kubwa kwa umma kupitia kwa Imamu Ali (a.s.). Kwa hiyo pia ni juu yetu kuweza kufikiria na kujikumbusha neema mbali mbali za Mwenyezi Mungu anazotuneemesha kila siku na kila dakika, ili tuoneshe shukrani juu na neema hizo, na shukrani kubwa ni kutekeleza maamrisho yake na kuachana na makatazo yake, kwani thamani ya neema Zake kwetu haziwezi kulingana na thamani ya kitu chochote, kwani mtu huwa tayari kutoa kila anachokimiliki ikibidi kupata tiba ya kimoja kati ya viungo vyake. Kwa hivyo pale tunapokuwa wazima wa afya tusivitumie viungo vyetu, nguvu zetu, na mali zetu katika kumuasi Mwenyezi Mungu, na badala yake tuvitumie katika maamrisho yake, na kwa kufanya hivi tutakuwa tumeonesha shukrani ya hali ya juu Kwake na kwa neema Zake.
283
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 283
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI NA MOJA
ْ ِّحو ُه ب َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ُك َر ًة ً ين آ َمنُوا ْاذ ُك ُروا اللهََّ ِذ ْك ًرا َك ِث ُ يرا َو َسب ُ ُصلِّي َعلَي ًص ا ْ ْك ْم َو َم اَل ِئ َكتُ ُه لِي ُخ ِر َج ُك ْم ِم َن َ يل ُه َو الَّ ِذي ي ِ ََوأ ُّ ُالظل ُّ ات إلَى َ ان ِب ْال ُم ْؤ ِم ِن َ ور َو َك ين َر ِحي ًما َت ِحيَّتُ ُه ْم َي ْو َم َي ْل َق ْو َن ُه الن م َ ِ ِ ِ َ َ َ َس اَل ٌم َوأَ َع َّد ل ُه ْم أ ْج ًرا ك ِري ًما “Enyi ambao mmeamini! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi. Na mumsabihi asubuhi na jioni. Yeye Ndiye anayewaswalia na malaika wake, ili awatoe vizani na kuwatia kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu waumini. Maamkuzi yao siku ya kukutana Naye yatakuwa ni Salaam. Na amewaandalia malipo yenye heshima.” (Qur’ani: 33:41-44)
MAELEZO Aya hizi zinawaelekeza Waumini namna ya kufanya ili kujiandaa na jukumu la kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu wengine. Aya ya kwanza inaanza kwa kusema: “Enyi ambao mmeamini! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi. Na mumsabihi asubuhi na jioni.” Kwa vile vitu vinavyochangia kughafilika ni vingi sana, hasa ikizingatiwa kwamba mchango unaotokana na wasiwasi wa shetani katika kumghafilisha mwanadamu ni mkubwa sana, njia pekee ya kupambana na hali hiyo ni kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi sana, kwa maana ya kufikiria uwezo wake na utukufu wake, si kumkumbuka kwa ulimi tu. Kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi ndiko kunakoleta nuru na mwangaza katika matendo yote ya mwanadamu. Ndio maana Mwenyezi Mungu akawataka Waumini wajipambe na sifa ya kumkumbuka katika hali zote, wakati wa ibada wamkumbuke kwa kuhudhurisha nyoyo zao na kumtakasa, na pia wamkumbuke wakati wanapoingiwa na ushawishi wa kumuasi ili iwe ni kizuizi cha wao kuendelea kumuasi, na sababu ya kuleta toba kwa haraka na kurejea katika njia ya sawa, na wamkumbuke wakati wa neema ili wapate kumshukuru kutokana na neema Zake, na wamkumbuke wakati wa balaa na msiba ili watu wavumilie na kusubiri. 284
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 284
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa muhtasari, Waumini wasiache kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika kila harakati za maisha yao kwa kujiepusha mbali na yote yanayomkasirisha na kutenda yote anayoyaridhia. Tunasoma katika jawabu la Mtume (s.a.w.w.) pale alipoulizwa na Abu Said al-Khudriy: “Ni mja gani atakayekuwa na daraja bora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama?” Alisema: ‘Ni wale wanaomtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi.’” Baada ya jawabu hilo, Abu Said alimuuliza tena Mtume (s.a.w.w): Je, mtu huyo ni bora kuliko mwenye kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Mtume (s.a.w.w.) alimjibu kwa kusema:
ّ لو ضرب بسيفه في الكفار والمشركين حتى ينكسر ّ ويختضب دماَ لكان .الذاكرون أفضل درجة منه “Lau kama mtu huyo atawapiga makafiri na washirikina kwa upanga wake mpaka
upanga uvunjike na utapakae damu, basi wenye kumtaja Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko yeye.”129
Hii ni kutokana na kwamba Jihadi ya kweli haipatikani pasi na kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi. Hapa tunaweza kujifunza kwamba kuna njia nyingi za kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kama vile kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa ulimi kwa kutumia tasbihi Zahara (a.s.) kwa kusema ‘Allahu Akbar’ mara 34, ‘Alhamdu Lillahi’ mara 33, na ‘Subhanallah’ mara 33. Na katika baadhi ya maneno ya wafasiri wanasema ni kutaja Majina Matukufu ya Mwenyezi Mungu na kumtakasa kutokana na kila sifa isiyolingana Naye. Haya ni baadhi tu ya makusudio ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na kama maelezo yalivyotangulia kwamba ni kumkumbuka katika kila nyanja ya maisha, kama alivyotaka kukumbukwa asubuhi na jioni. Katika kutaja wakati huu ni kuonesha mwanzo wa siku na mwisho wake. Kwa hivyo kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi na katika muda wote (asubuhi na jioni) hakuwezi kukamilika ikiwa kutakosekana mazingatio ya utambuzi wa mtu kuitambua nafasi yake na wajibu wake kwa Muumba wake, na kuona kwamba kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni chakula cha kuishibisha akili yake kama vile anavyolishibisha tumbo lake kwa aina mbalimbali ya vyakula na vinywaji, kama ilivyokuja katika Aya isemayo: “Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua.” (Qur’ani; 13:28). Mtu ambaye imani yake itathibiti sawasawa 129
Timidhiy, Sunan Tirmidhiy, Jz. 5, Uk. 127 285
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 285
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
bila kutetereka kutokana na kumkumbuka Mwenyezi Mungu mara kwa mara ndiye atakayeambiwa Siku ya Kiyama aingie katika Pepo ikiwa ni malipo ya kazi yake hiyo, kama Aya hizi zisemavyo:
ً ضي َّة ْ س ْال ُم ْط َم ِئنَّ ُة ُ َيا أَيَّتُ َها النَّ ْف ِ اض َي ًة َّم ْر ِ ِّك َر ِ ار ِج ِعي إِلَى َرب َفا ْد ُخلِي ِفي ِع َبا ِدي َوا ْد ُخلِي َجنَّ ِتي “Ewe nafsi yenye kutulia! Rudi kwa Mola Wako, hali ya kuwa unaridhika (kwa utakayoyapata,) na (Mwenyezi Mungu) aridhike na wewe. Basi ingia katika (kundi) la waja Wangu (wema). Na ingia katika Pepo Yangu.”
Na Aya inayofuata inaeleza natija inayopatikana katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, inasema: “Yeye Ndiye anayewaswalia na malaika wake, ili awatoe vizani na kuwatia kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu waumini.” Kutokana na rehema yake hii amejiwekea ahadi ya kuwaongoa waja Wake na pia Malaika nao wanafanya kazi hiyo hiyo. Kwa hivyo basi, Mwenyezi Mungu anawateremshia waja Wake rehema na Malaika wanawaombea msamaha, kama ilivyokuja katika Aya nyingine isemayo:
َ ون ْال َع ْر َ ِّح َ ُين َي ْح ِمل َ الَّ ِذ ِّه ْم ُ ُسب َ ش َو َم ْن َح ْولَ ُه ي ِ ون ِب َح ْم ِد َرب َ ين آ َمنُوا َربَّ َنا َو ِسع ْ َوي َ ون لِلَّ ِذ َ ون ِب ِه َو َي ْس َت ْغ ِف ُر َ ُُؤ ِمن ْت ُك َّل َش ْي ٍء ْ َّر ْح َم ًة َو ِع ْلماً َف َ اغ ِف ْر لِلَّ ِذ اب َ ين َتابُوا َواتَّ َبعُوا َس ِبيلَ َك َو ِق ِه ْم َع َذ ْ يم ح ج ال َ ِ ِ “Wale wanaokibeba Kiti cha Enzi (cha Mwenyezi Mungu) na wale wanaokizunguka, wanamtukuza Mola Wao na kumsifu na wanamuamini na wanawaombea msamaha walioamini (wanasema): Ewe Mola Wetu! Umekienea kila kitu kwa rehema na elimu, basi wasamehe waliotubu na kuifuata njia Yako na waepushe dhidi ya adhabu ya Jahannamu.” (Qur’ani: 40:7)
Aya inatoa bishara njema kwa wale wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi sana, ikieleza ya kwamba wenye kufanya hivyo wamefanikwa kwa kupata rehema za Mwenyezi Mungu na maombezi ya Malaika Wake, huku nyoyo zao na 286
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 286
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
akili zao ziking’ara kwa nuru ya uongofu, elimu, na uchamungu. Bishara nyingine ni kuwepo mafungamano ya dhati kati ya mja na Mola wake. Na pia Aya inatoa dhamana ya kwamba mja mwenye kusifika na sifa hii katu hachezewi na shetani, kwani Mwenyezi Mungu anapoonesha mafungamano na mja Wake ni dalili ya kwamba mja huyo amefikia daraja ya utakaso wa hali ya juu, na shetani ametamka wazi kwamba hatothubutu kuwaghilibu na kuwapoteza waja wenye kusifika na sifa hiyo, kama Qur’ani inavyotuthibitishia kwa kusema:
ُ َال َفبع َّزت َك أ َ ص َ ل ْغ ِو َينَّ ُه ْم أَ ْج َم ِع ين ِ َين إِ اَّل ِع َبا َد َك ِم ْن ُه ُم ْال ُم ْخل ِ ِ ِ َ َق “Akasema: Naapa kwa haki ya utukufu Wako, bila ya shaka nitawapoteza wote (watoto wa huyu Adam). Isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliotakaswa.” (Qur’ani; 38: 82-83)
Aya ya mwisho inaeleza daraja na malipo ya Waumini wenye kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, malipo hayo yametajwa katika ibara fupi, lakini iliyobeba maana nzito, inasema: “Maamkuzi yao siku ya kukutana Naye yatakuwa ni Salaam.” Tunaelewa ya kwamba maana ya maamkizi ni ile hali ya kutakiana kheri na baraka, kwa hivyo Siku hiyo ya Kiyama maamkizi watakayoamkiana ni yale yaliobeba ujumbe wa kutakiana salama, amani na kusalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Maamkizi hayo ni mwendelezo wa rehema za Mwenyezi Mungu na Malaika Wake kwa wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi hapa duniani, kwani Siki hiyo Malaika kila watakapokutana na Waumini hao hawatoacha kuwaamkia kwa maamkizi yenye kuwatakia amani kutoka kwa Mola Wao, kama ilivyobainishwa pahala pengine katika Qur’ani Tukufu:
ِّ ُ ُ ال ٌم َعلَي َ َ ُال ِئ َك ُة َي ْد ُخل َ اب َس َ َوال َم ص َب ْرتُ ْم َ ْكم ِب َما ٍ ْهم ِّمن كل َب ِ ون َعلي َّ َف ِن ْع َم ُع ْق َبى ار ِ الد “Na Malaika wanawaendea katika kila mlango. (Wakiwaambia): Amani iwe juu yenu kwa sababu mlisubiri. Basi ni neema ilioje ya nyumba ya Akhera (kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu).” (Qur’ani: 13:23-24)
Baada ya Waumini kupata maamkizi mema, Aya inahitimisha kwa kusema: “Na amewaandalia malipo yenye heshima.” Kwa kweli ibara hii fupi imekusanya neema 287
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 287
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
zote za Mwenyezi Mungu watakazozipata Waumini wenye kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi.
UTAFITI Pindi mtu anapomkumbuka Mwenyezi Mungu mara kwa mara moyo wake hujaa maarifa ya kutambua uwezo wa Mwenyezi Mungu na kujaa hekima ya hali ya juu, kwani Yeye ana Majina mazuri na Sifa Njema na ametakasika dhidi ya kila baya. Kuendelea kumkumbuka Mwenye Sifa za aina hii kuna msukuma mwanadamu katika kufanya mambo mema na yenye manufaa kwake na kwa jamii inayomzunguka na kuwa mbali na maovu, kwani ile nuru ya Sifa Zake Mwenyezi Mungu huenea katika akili na moyo wa mwanadamu. Kwa kumkumbuka mwabudiwa wa aina hii kunapelekea hisia za kuwa Naye wakati wowote, hisia za aina hii huwa ni kizuizi kati ya mwanadamu dhidi ya kutenda maovu. Kumkumbuka Mwenyezi Mungu kuna maana ya kukumbuka uangalizi Wake kwa mja, kukumbuka Siku ya Kiyama na malipo watakayoyapata waja, kukumbuka mahakama ya kiadilifu itakayoendeshwa na Mwenyezi Mungu, kukumbuka neema Zake na adhabu Yake… Ukumbukaji wa aina hii ndio unaoisafisha nafsi ya mwanadamu na kumfanya kuwa mkakamavu na moyo wake kujaa maarifa, na kutokana na mantiki hii imepokewa kutoka kwa Imamu Ali (a.s.) akitueleza ya kwamba hakuna kikomo katika kumtaja na kumkumbuka Mwenyezi Mungu, anasema:
ّ إال ّ إال وله ح ّد ينتهي إليه ّ ما من شيء الذكر فليس له ح ّد .ينتهي إليه “Kila kitu kina mpaka wake isipokuwa ukumbusho (kumkumbuka MWenyezi Mungu), huo hauna ukomo unaoishia.”130
Na imepokewa kutoka kwa Imamu as-Sadiq (a.s.) akisema:
ّ عز ّ فرض اهلل ّ اهن فهو ح ّد ّ فمن أ ّد،وجل الفرائض وشهر،هن ّ ،حج ح ّده ،إال الذكر ،رمضان فمن صامه فهو ّ والحج فمن ّ 130
Al-Kulayni, Usulul Kafiy, Jz. 2, Uk. 498 288
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 288
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
ّ عز ّ فإن اهلل ّ ولم يجعل له ح ّدًا،وجل لم يرض منه بالقليل ،ينتهي إليه “Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha mambo, basi mwenye kuyatekeleza atakuwa ametekeleza kiwango anachostahiki, mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani atakuwa ametekeleza kiwango chake, mwenye kuhiji atakuwa ametekeleza kiwango chake, isipokuwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu haridhiki na kukumbukwa kuliko kuchache, na wala hajaweka mpaka unaoishia (hajaweka kiwango maalumu).
Kisha Imamu alisoma Aya ifuatayo:
ْ ْ وهب ً ص ُ ِّح يال َياأَُّي َهاالذين:ثم تال ُ أمنواذ ُك ُرواهلل ذكرااً َك ِثيراً َو َسب ِ َُك َر ًة َوأ “Enyi mlioamini! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumkumbuka. Na mtakaseni asubuhi na jioni.”131
Pia tunasoma katika Hadithi ya kwamba nyumba inayosomwa Qur’ani ndani yake na kukithirishwa kutajwa Mwenyezi Mungu, hukithiri baraka zake na kuhudhuriwa na Malaika, na mashetani hukimbia kutoka humo, na nyumba hiyo hutoa mwanga wenye kuwaangazia viumbe vya mbinguni kama vile jua, mwezi na nyota zinavyowaangazia viumbe vya ardhini. Kwa kumalizia maudhui haya yenye umuhimu wa kipekee katika maisha ya mwanadamu tumsikilize Mtume (s.a.w. w.) anavyotuambia:
.من أعطي لسانا ذاكرا فقد أعطي خير ال ّدنيا واألخرة “Mwenye kupewa ulimi wenye kukumbuka, basi atakuwa amepewa kheri ya dunia na akhera.”132
131 132
Kitabu kilichotangulia Alhuweiziy,Tafsiru Nuru Thaqlayn, Jz. 4, Uk. 285 289
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 289
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI NA MBILI
ُ ات ثُ َّم َطلَّ ْقتُ ُم َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ وه َّن ِم ْن ِ ين آ َمنُوا إِ َذا َن َك ْحتُ ُم ْال ُم ْؤ ِم َن ََقبْل أ َوه َّن َف َما لَ ُك ْم َعل َ ْ ُ ْه َّن ِم ْن ِع َّد ٍة َت ْع َت ُّدو َن َها َف َمتِّع ُ ُوه َّن ي س م ت ن ُّ َ ِ ِ ُ َو َس ِّر ُح احا َج ِميل ً وه َّن َس َر “Enyi ambao mmeamini! Mkiwaoa wanawake waumini kisha mkawaacha kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayoihisabu. Hivyo wapeni cha kuwaliwaza na waacheni mwachano mzuri.” (Qur’ani; 33:49)
MAELEZO Aya hii inaelezea baadhi ya mambo yanayohusiana na talaka, ambayo moja kati ya hayo ni kutokuwepo sheria ya kukaa eda kwa mwanamke aliyeachwa kabla ya kukutana kimwili na mume wake: “Enyi ambao mmeamini! Mkiwaoa wanawake waumini kisha mkawaacha kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayoihisabu.” Kutajwa wanawake Waumini katika Aya hii haimaanishi kwamba haifai kuoa mwanamke asiyekuwa Mwislamu, bali ni kutilia mkazo na umuhimu juu ya kuoa mwanamke Mwislamu na aliye Muumini wa kweli. Pia Aya inaonesha kwamba mwanamke kukaa eda ni haki ya mwanamume iwapo itakuwa amekutana kimwili na mke wake huyo kisha kumtaliki, hii ni kwa sababu katika hali hiyo yamkinika mwanamke akapata ujauzito, na bila ya kukaa eda na kisha kuolewa na mume mwingine itakuwa ni kupoteza nasaba ya mtoto. Na vilevile eda hutoa fursa kwa mume na mke waliokutana kimwili kuweza kujirudi na kufikiria upya kurejesha jengo lao la ndoa kwa mara nyingine, kwani huenda ikawa talaka imetokea kwa sababu zisizo na msingi. Pia Mwanamke kukaa eda ni haki ya mume, haki ambayo hana budi kuwa nayo mpaka mwanamke amalize muda wake, na hairuhusiwi kuikataa haki hiyo. Jambo la pili analopasa kufanyiwa mwanamke aliyetalikiwa kabla ya kuguswa ni kupewa kitu kama zawadi inayolingana na hadhi yake. Kitu hicho ni kwa ajili ya kuliwazwa kutokana na mazingira ya talaka iliyotoka: “Hivyo wapeni cha kuwaliwaza.” Bila shaka mwanamke mwenye kuachwa katika hali hii itamlazimu 290
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 290
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
mwanamume kumpa kiliwazo (kitoka nyumba) ikiwa hawakukubaliana kiwango maalumu cha mahari wakati wa akdi (kufunga ndoa), kama ilivyoelezwa katika Aya ifuatayo:
ْ ض ُ اح َعلَي َّ ُ وه ُّن أَ ْو َت ْف ِر ُ ْك ْم إِن َطلَّ ْقتُ ُم النِّ َساء َما لَ ْم َت َم ُّس وا َ ال ُج َن َّ لَه ُ يض ًة َو َمتِّع َ ُن َف ِر وس ِع َق َد ُر ُه َو َعلَى ْال ُم ْق ِت ِر َق ْد ُر ُه ِ ُوه َّن َعلَى ْال ُم َ وف َح ّقًا َعلَى ْال ُم ْح ِس ِن ين ُ َم َتاعاً ِب ْال َمع ِ ْر “Hapana ubaya kwenu mkiwapa talaka wanawake ambao hamjawagusa au kuwabainishia mahari yao. Lakini wapeni cha kuwaliwaza, mwenye wasaa kiasi awezacho na mwenye dhiki kiasi awezacho. Wapeni maliwazo haya kwa mjibu wa sheria, hali ya kuwa ni wajibu kwa watendao mema.”
Na kama itakuwa ameachwa kabla ya kuguswa na kutajwa kiwango cha mahari italazimu apewe nusu ya mahari, kama Aya hii isemavyo:
ْ وه َّن َو َق ْد َف َر َّ ضتُ ْم لَه ُ ْل أَن َت َم ُّس ُ َوإِن َطلَّ ْقتُ ُم َ ُن َف ِر يض ًة ِ وه َّن ِمن َقب َّ َضتُ ْم إ ُ ون أَ ْو َيع ُ ال أَن َيع ُص ْ ف َما َف َر َ ْف ْف َو الَّ ِذي ِب َي ِد ِه ُع ْق َد ُة ْ َف ِن ْ ْف ُ النِّ َكاح َوأَن َتع ...وا أَ ْق َر ُب لِلتَّ ْق َوى ِ “Na mkiwapa talaka kabla ya kuwagusa, na mmekwisha wawekea hayo mahari makhsusi, basi wapeni nusu ya mahari mlioagana, isipokuwa ikiwa wanawake wenyewe wamesamehe, au mume ambaye kifungo cha ndoa kimo mikononi mwake awe amesamehe. Na kusameheana ndiko kuliko karibu zaidi na uchamngu…” (Qur’ani; 2:237)
Jambo jingine katika maudhui haya ni kumuacha kwa muacho wa kibinadamu,wenye heshima, usio na chuki na aina yoyote ya dhulma, kama Aya inavyohitimisha: “Na waacheni mwachano mzuri.” Katika kutilia msisitizo zaidi wa hukumu hii Mwenyezi Mungu anasema tena:
ٌ ْس ان ُ اك ِب َمع ٌ وف أَ ْو َت ْس ِر ٍ ْر َ َفإِم ٍ يح ِبإِ ْح َس 291
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 291
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
“Basi ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri…”
Maisha ya ndoa yanapasa kuwa katika misingi ya kibinadamu, na pia wakati wa talaka, haifai mtu pindi anapoazimia kumtaliki mke wake kumdhulumu mahari yake na haki zake nyingine, na kutumia maneno ya ujeuri na ufedhuli, kamwe tabia hizi hazikubaliki katika Uislamu.
292
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 292
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI NA TATU
َ ين آ َمنُوا اَل َت ْد ُخلُوا بُي ْ ُوت النَّ ِب ِّي إِ اَّل أَ ْن ي َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ُٰؤ َذ َن لَ ُك ْم إِلَى َ اظ ِر ين إَِنا ُه ولكن إِ َذا ُد ِعيتُ ْم َفا ْد ُخلُوا َفإِ َذا َط ِع ْمتُ ْم َط َع َ ام َغي ِ ْر َن ٍ ْ ان ي َ يث إِ َّن َذٰلِ ُك ْم َك َ َفا ْن َت ِش ُروا َو اَل ُم ْس َت ْأ ِن ِس ُؤ ِذي النَّ ِب َّي ٍ ين لِ َح ِد ُ َف َي ْس َت ْح ِيي ِم ْن ُك ْم َواللهَُّ اَل َي ْس َت ْح ِيي ِم َن ْال َح ِّق َوإِ َذا َسأَ ْلتُ ُم وه َّن ُوه َّن ِم ْن َو َرا ِء ِح َجاب َذٰلِ ُك ْم أَ ْط َه ُر لِ ُقل ُاسأَل ُ ً َم َت وب ُك ْم ْ اعا َف ٍ ِ َُو ُقل َ ان لَ ُك ْم أَ ْن تُ ْؤ ُذوا َر ُس َ وب ِه َّن َو َما َك ول اللهَِّ َو اَل أَ ْن َت ْن ِك ُحوا ِ َ َّلله ُ َ اج ُه ِم ْن َب ْع ِد ِه أ َب ًدا إِ َّن َذٰلِك ْم َك ان ِع ْن َد ا ِ َع ِظي ًما إِ ْن تُ ْب ُدوا َ أَ ْز َو َ َ ان ب ُك ِّل َش ْي ٍء َعلِي ًما اَل ُج َن ُ َ ََّلله ْه َّن ِ َ َشي ًْئا أ ْو تُ ْخفو ُه َفإِ َّن ا َك ِ اح َعلي ِفي آ َبا ِئ ِه َّن َو اَل أَ ْب َنا ِئ ِه َّن َو اَل إِ ْخ َوا ِن ِه َّن َو اَل أَ ْب َنا ِء إِ ْخ َوا ِن ِه َّن َو اَل ََّين الله َّ أَ ْب َنا ِء أَ َخ َوا ِت ِه َّن َو اَل ِن َسا ِئ ِه َّن َو اَل َما َملَ َك ْت أَ ْي َمانُه َ ُن َواتَّ ِق َ إِ َّن اللهََّ َك ان َعلَىٰ ُك ِّل َش ْي ٍء َش ِهي ًدا “Enyi ambao mmeamini! Msiingie majumba ya Mtume ila mkipewa ruhusa ya kwenda kula, sio kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni. Na mkishakula, tawanyikeni msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii, naye anawastahi nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa haki. Na mnapowaomba chombo cha nyumbani, basi waulizeni nyuma ya mapazia. Hilo linasafisha zaidi nyoyo zenu na zao. Haiwafalii nyinyi kumuudhi Nabii wala kuwaoa wake zake kabisa. Hakika hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Mkidhihirisha chochote au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. Hapana ubaya kwao kwa baba zao, wala watoto wao, wala kaka zao, wala watoto wa kaka zao, wala watoto wa dada zao, wala wanawake wao, wala wale waliomilikiwa na mikono yao ya kuume. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.” (Qur’ani: 33:53-55)
293
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 293
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
SABABU YA KUTEREMKA Anas ibn Malik, ambaye alikuwa mtumishi wa Mtume (s.a.w.w.) anaeleza sababu ya kuteremka Aya ya kwanza kati ya hizi kama ifuatavyo: “Siku moja Mtume (s.a.w.w.) aliniamuru niwaalike Maswahaba zake nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha mchana, ikawa linakuja kundi linakula kisha linaondoka na kuja kundi jingine, kisha nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakubakia yoyote kati ya wale niliowaalika isipokuwa amekuja, Mtume (s.a.w.w.) akaniamuru niondoshe busati, nikafanya hivyo na watu wote wakaondoka isipokuwa watu watatu walibakia katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) na huku wakizungumza, Mtume (s.a.w.w.) alipoona ya kwamba wale watu wamerefusha mazungumzo, aliondoka na mimi nikaondoka kwa kudhani ya kwamba wale watu watatanabahi na kuondoka kwenda kwenye shughuli zao, Mtume (s.a.w.w.) aliingia katika chumba cha Aisha, kisha akatoka na kurudi, alipofika aliwakuta wale watu bado wamekaa na kuendelea na mazungumzo yao, hapo Aya hii ikateremka kwa lengo la kuwafahamisha namna ya kuamiliana na Mtume (s.a.w.w.) Pia kwa mujibu wa baadhi ya Riwaya ni kwamba Aya ya pili kati ya hizi iliteremka kutokana na baadhi ya majirani wa kiume walikuwa wakienda kuazima baadhi ya vitu kwa wake wa Mtume (s.a.w.w.). Bila shaka uazimaji wao huo wa vitu ulikuwa ni wa kawaida kulingana na haja za kimaisha, lakini Aya iliteremka kwa ajili ya kulinda heshima na hadhi ya wake wa Mtume (s.a.w.w.), na badala yake kutakiwa kuwaazima au kuwaomba vitu wakiwa katika hali ya kutowaona sura zao. Na Riwaya nyingine zinasema kwamba baadhi ya Maswahaba walisema: “Ni vipi Mtume (s.a.w.w.) ameweza kuwaowa wanawake wetu, basi pindi atakapofariki tutawaowa wake zake.” Hapo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii ili kuharamisha kuwaowa wake wa Mtume (s.a.w.w.), na hapo ikawa ndio mwisho wa njama zao mbaya dhidi ya Mtume (s.a.w.w.)133
MAELEZO Kwa mara nyingine Mwenyezi Mungu anatoa maelekezo kwa Waumini juu ya namna ya kuamiliana na Mtume Wake (s.a.w.w.) pamoja na wake zake kwa kupitia Aya hizi. Kwa kuanzia wanaelezwa kwamba haifai mtu kwenda kula isipokuwa baada ya kupata mwaliko rasmi, na waende kwa wakati mahsusi wa chakula, sio kwenda kabla ya kuiva na kuanza kuigeuza nyumba na kuwa baraza ya mazungumzo: “Enyi ambao mmeamini! Msiingie majumba ya Mtume ila mkipewa 133
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 13, Uk. 325 294
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 294
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
ruhusa ya kwenda kula, sio kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni. Na mkishakula, tawanyikeni msiweke mazungumzo.” Hivi ndivyo ambavyo Aya ilivyoweka bayana mafunzo haya, mafunzo ambayo yalikuwa hayatekelezwi na baadhi ya watu katika zama hizo. Licha ya mafunzo haya kuelekezwa katika nyumba za Mtume (s.a.w.w.), lakini haimaanishi kuishia katika nyumba hizo peke yake, bali haifai kuingia katika nyumba ya mtu yeyote bila ya idhini yake, kama tulivyokwishaona katika Aya ya 27 ya Surat an-Nur, na pia tumeona ni namna gani Mtume (s.a.w.w.) alivyokuwa akiomba ruhusa pale alipotaka kuingia katika nyumba ya binti yake; Bibi Fatima (a.s.). Pia mtu atakapoalikwa ajitahidi sana kuchunga wakati wa kwenda, akiambiwa aende saa fulani, basi asiende kabla ya wakati huo, ili asije akamshughulisha mwenyeji wake kwa mambo aliyokuwa hakuyapangilia, na baada ya kumaliza aliloitiwa aombe ruhusa ya kuondoka, isipokuwa atakapohisi ya kwamba kuendelea kubakia hakutomkera mwenyeji wake, kwani baadhi ya wenyeji hupendelea kuzungumza sana na wageni wao, ama ikiwa mwaliko alioalikwa ni wa mlo tu, basi si sawa kurefusha kikao baada ya kutimiza wito. Kwa kweli kwenda kinyume na mafunzo haya kunapelekea kuudhika kwa mtu aliyetoa mwaliko, na kufanya hivyo hakuendani na tabia za Kiislamu. Baada ya hapo Aya inaeleza sababu ya hukumu hii: “Hakika hayo yanamuudhi Nabii, naye anawastahi nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa haki.” Ni jambo lisilo na shaka ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) hakuwa ni mwenye kusitasita wala kumuogopa yoyote katika kubainisha haki juu ya mambo yaliyokuwa hayahusiani na mambo yake binafsi, na hapa ingemjengea taswira mbaya kwa watu lau kama hukumu hii ingetoka kwake, lakini ni Mwenyewe Mwenyezi Mungu aliyeonesha nafasi ya Mtume Wake kwa wanadamu, na huu ndio utaratibu ulio mzuri mno wa mtu kunyanyuliwa daraja na utukufu. Aya inaendelea kutaja hukumu nyingine, hukumu hiyo inahusiana na sitara ya wanawake: “Na mnapowaomba chombo cha nyumbani, basi waulizeni nyuma ya mapazia.” Tabia ya majirani kuazimana baadhi ya vitu ni jambo ambalo lipo hadi katika zama zetu na litaendelea kuwepo, kwani hakuna anayejitosheleza kwa kila kitu. Na hata nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) haikuwa nje ya mwenendo huu, kwa hivyo Mwenyezi Mungu aliweka taratibu ya kuweza kupata huduma hiyo, licha ya wake hao wa Mtume (s.a.w.w.) kujifunika na kuisitiri miili yao, lakini Mwenyezi Mungu alitaka kuwepo na heshima zaidi katika nyumba hiyo, kwa hivyo akawataka watu (wanaume) waombe vitu hivyo wakiwa nyuma ya pazia au mlango. Hukumu hii, kama tulivyosema inahusiana na wake wa Mtume (s.a.w.w.) tu, ama wasiokuwa wao 295
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 295
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
wanaweza kuazimisha vitu hata kama wataonekana, jambo la msingi ni kuwa katika sitara kamili kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Amri hii maalumu kwa wake wa Mtume (s.a.w.w.) ni kutokana na kuwepo baadhi ya watu kutaka kuchunguza na kupeleleza kinachoendelea katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) hasa baada ya Mtume (s.a.w.w.) kumuoa Bibi Zaynab binti Jahshi, ndoa ambayo ilileta gumzo kwa watu, kwa vile Bibi huyo alikuwa ni mtalaka wa mtoto wa Mtume wa kumlea; Zaydi. Kutokana na mila za Warabu ilikuwa ni fedheha kwa mtu kuoa ndoa kama hiyo, lakini katika kufuta mila hiyo potofu iliyokuwa imeota mizizi kwa miaka mingi ilimlazimu Mtume (s.a.w.w.) mwenywe ndio aiondowe kwa vitendo baada ya kupata amri kutoka kwa Mola Wake. Na kwa upande mwingine kulikuwa na watu waliotamka wazi ya kwamba wanasubiri tu Mtume (s.a.w.w.) aage dunia ili wawaowe wake zake, wengine walifikia hadi kuwataja majina yao! Natija ya hukumu hii inabainishwa na ibara hii ya Aya: “Hilo linasafisha zaidi nyoyo zenu na zao.” Mambo waliyoyafanya, kama vile kwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) katika wakati usiostahiki, kukaa muda mrefu baada ya kula chakula na kuzungumzia suala la kufunga ndoa na wake wa Mtume (s.a.w.w.) baada ya kufariki dunia, yalikuwa ni mambo yaliyokuwa yakimuudhi sana Mtume (s.a.w.w): “Haiwafalii nyinyi kumuudhi Nabii.” Hukumu nyingine iliyomo humu ni uharamu wa kuwaowa wake wa Mtume (s.a.w.w): “Wala kuwaoa wake zake kabisa. Hakika hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.” Suala linaloweza kujitokeza katika hukumu hii ni vipi Mwenyezi Mungu ameharamisha kuolewa kwa wake wa Mtume (s.a.w.w.) baada ya kufariki kwake, huku ikizingatiwa ya kwamba baadhi yao walikuwa bado ni vijana?Jawabu lake ni kama ifuatavyo: Kwanza: Baadhi ya watu walikuwa wanataka kuwaowa kama njia ya kulipiza kisasi, kwa madai yao kwamba Mtume (s.a.w.w.) amewaowa dada zao na mashangazi zao n.k. Kwa hivyo watu hao walikuwa na lengo la kuwavunjia heshima wake zake na kumvunjia heshima Mtume (s.a.w.w.). Pili: Baadhi ya watu wengine walichukulia suala la kuowa wake wa Mtume (s.a.w.w.) ni jambo la kuwapandisha daraja wasiostahiki katika jamii, au kuitumia nafasi hiyo kupotosha mafunzo ya Uislamu kwa madai kwamba wao wanajua yale ambayo wengine hawayajui kwa vile wanaishi na waliokuwa wake wa Mtume (s.a.w.w.). Baadhi ya wafasiri wa madhehebu ya Ahlus-Sunna wameeleza bayana baadhi ya wale waliotamka waziwazi kwamba watafunga ndoa na wake wa Mtume (s.a.w.w.)
296
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 296
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
baada ya kufariki kwake, miongoni mwao ni Talha ambaye alisema: “Ikiwa nitaishi baada ya Muhammad, basi nitamuoa Aisha.”134 Lau kama Mwenyezi Mungu hakutoa hukumu hii ya kuharamisha ndoa hizo, basi hali ya vita vya Jamal (Ngamia ) vilivyokuwa vikiongozwa na Bibi Aisha, Talha na Zubeir dhidi ya Imamu Ali (a.s.) vingechukua sura mbaya zaidi, kwani ingetarajiwa Talha kuwa mume wa Aisha! Hakika Yule ambaye anazitambua dhamira za viumbe Vyake ametoa hukumu ya kuzuia ndoa ya aina hiyo iliyokuwa ina malengo mabaya, na badala yake akawataka Waislamu wote kwa ujumla wao watambue kwamba hao ni mama zao! Na ni kwanini wake hao walikubali nafasi hii ya umama kwa maridhawa ya nafsi zao? Baadhi ya wakati hutokea mambo muhimu katika maisha ya mwanadamu, hapo hupaswa kuyapa kipaumbele na ikibidi kujitoa muhanga na mtu kuachana na baadhi ya haki zake. Na kila mtu anapopanda daraja, majukumu yake yanaongezeka, na bila shaka, wake wa Mtume (s.a.w.w.) wamepata daraja na heshima kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya kuwa wake wa kipenzi chake (s.a.w.w.), kwa hivyo kwa daraja hiyo waliyoipata wanastahiki kujinyima baadhi ya mambo. Kwa sababu hii wake wa Mtume (s.a.w.w.) walikuwa wakiishi kwa kuheshimiwa sana na Waislamu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.), na wao walikuwa radhi kutokana na hali yao hiyo ya kutoolewa tena. Aya ya pili inatoa tahadhari kali kwa kusema: “Mkidhihirisha chochote au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.” Ni ishara ya wazi kwamba Mwenyezi Mungu anatambua mikakati yao ya kumuudhi Mtume (s.a.w.w.), ikiwa ni hiyo waliyoitamka au waliyoificha katika nyoyo zao, hakika Yeye anatambua vyema kila kitu, na anaamiliana na kila mtu kutokana na matendo yake.
UTAFITI Kutokana na maelezo ya Aya zilizotangulia, tunapenda tueleze baadhi ya vipengele vinavyohusiana na maudhui ya Aya hizi: 1.
Ugeni:
Uislamu umelipa umuhimu sana suala la ugeni na mgeni, mpaka kiasi cha Mtume (s.a.w.w.) kutamka ya kwamba: “Mgeni ni muongozaji wa Pepo.”135Umuhimu wa mgeni na wajibu wa kuheshimiwa ni jambo lililopewa nafasi katika mafunzo ya Uislamu. Inazingatiwa kwamba ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kama Mtume (s.a.w.w.) anavyotueleza: 134 135
Ar-Raziy, Tafsiru Raziy, Jz.25, Uk.225 Al-Majlisiy, Biharul Anwar, Jz.72, Uk. 460 297
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 297
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
وما تلك: قالوا,إذا أراد اهلل بقوم خيرا أهدى إليهم هدية ّ :الهدية؟ قال الضيف ينزل برزقه ويرتحل بذنوب أهل .البيت “Pindi Mwenyezi Mungu anapowatakia watu kheri, huwazawadia zawadi, Maswahaba waliuliza: Ni zawadi gani hiyo? Mtume (s.a.w.w.) aliwajibu: Ni mgeni, huja na riziki yake na huondoka na dhambi za watu wa nyumba anayofikia.”136
Na siku moja Mtume (s.a.w.w.) aliendewa na mtu na kumueleza ya kwamba yeye anatia udhu vizuri na kusimamisha Swala na kutoa Zaka kila muda unapofika, humkaribisha mgeni… Mtume (s.a.w.w.) akamwambia mtu huyo:
ّ بخ ّ بخ ّ . وما لجهنّم عليك سبيل إن كنت كذلك,بخ “Hongera, tena hongera na hongera tena, Moto wa Jahannamu hauna nafasi kwako ikiwa kweli unafanya hivyo.”
2.
Kuzingatia Wepesi Kwa Mgeni:
Licha ya Uislamu kumpa umuhimu mkubwa mgeni, haifai mtu kujikalifisha zaidi ya uwezo wake katika kumhudumia mgeni wake, kwa hivyo kipimo cha huduma kwa mgeni ni kuangalia hali ya mwenyeji na mgeni, na pia mwenyeji asifanye ubahili ikiwa hali yake ya kiuchumi ni nzuri, pia mgeni asitarajie zaidi ya hicho alichoandaliwa kutoka kwa mwenyeji wake, Imamu as-Sadiq (a.s.) anasema:
وما أدري أيّهما أعجب! الّذي,المؤمن ال يحتشم من أخيه أو المتكلّف ألخيه؟,يكلّف أخاه إذا دخل عليه أن يتكلّف له “Muumini hamkasirikii ndugu yake (Muumini mwenzake), na sijui ni yupi anaeshangaza zaidi kati ya wawili, ni yule ambaye anamkalifisha mwenzake wakati wa kuhudumiwa! Au ni yule anayejikalifisha kwa ajili ya ndugu yake?”
Na Salman al-Farisy amepokea kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema: 136
Kitabu kilichotangulia, Uk.461 298
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 298
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
ّ أن ال نتكلّف .للضيف ما ليس عندنا وأن نق ّدم إليه ما حضرنا “Tusijikalifishe kwa ajili ya mgeni kwa kile tusichokuwa nacho, na tumuandalie kile tulicho nacho.”137
Kwa kweli mgeni ni zawadi kutoka mbinguni, kwa hivyo inapasa kuhudumiwa na kukirimiwa na kupewa heshima ya hali ya juu na hata pale anapoamua kurudi nyumbani, kama Mtume (s.a.w.w.) anavyosema:
ّ من ّ حق .البر ّ الضيف أن تمشى معه فتخرجه من حريمك إلى “Miongoni mwa haki za mgeni ni kutembea naye kwa kutoka naye hadi nje (kumuadisha).”
Pia ni wajibu kwa mwenyeji kuhakikisha anampatia mgeni wake mahitaji ya msingi kwa muda wote anaokuwa nyumbani kwake. Baadhi ya wageni wanakuwa na haya kiasi cha kutoweza kusema ya kwamba wanahisi njaa, bali ni wajibu kumpelekea chakula, ikiwa anakihitaji atakula, kama anavyotufunza Imamu as-Sadiq (a.s.) kwa kusema:
أكلت اليوم شيئا؟ ولكن قرب:ال تقل ألخيك إذا دخل عليك ّ ,إليه ما عندك .فإن الجواد من بذل ما عنده “Usimuulize ndugu yako akujiapo:Je, leo umeshakula chochote? Lakini mkaribishe kwa ulichonacho, kwani mtu mkarimu ni yule mwenye kutoa alichonacho.”138
Na miongoni mwa mambo yaliyo wajibu kwa mwenyeji ni kutokidharau kile alichomwandalia mgeni wake, kwani neema ya Mwenyezi Mungu inahitaji kutukuzwa na kuheshimiwa vyovyote iwavyo, lakini leo imezoeleka kwa watu kuwaambia wageni wao kwamba: Tulichopata ni hiki kidogo ambacho hakilingani na nanyi! Na pia inapasa kwa mgeni kushukuru na kuridhika na chochote kitakachoandaliwa kwa ajili yake, kwani hakuna riziki ndogo, kama Imamu as-Sadiq anavyotufunza tena kwa kusema: 137 138
Ajluniy, Kashful Khifai, Jz.1, Uk.206 Shahrudiy, Mustadriku Safinatil Bihar, Jz.6, Uk.489 299
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 299
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
هلك امرؤ احتقر ألخيه ما يحضره و هلك امرؤ احتقر من .أخيه ما قدم إليه “Ameangamia mtu ambaye anamdharau ndugu yake kutokana na kile alichoandaliwa na ameangamia mtu ambaye anadharau kilekile alichomuandalia ndugu yake.”139
3.
Wajibu wa Mgeni:
Kama vile ambavyo mwenyeji anawajibu juu ya mgeni wake, pia mgeni anawajibu juu ya mwenyeji wake. Baadhi ya wajibu huo ni kama ulivyotajwa katika Riwaya zilizotangulia, ama mambo mengine ni kukubali maelekezo ya mwenyeji wake, kama vile kutakiwa kukaa au kulala pahali fulani, hapo atapaswa na kulazimika kufuata maelekezo hayo, kama Imamu as-Sadiq (a.s.) anavyosema:
إذا دخل أحدكم على أخيه في رحله فليقعد حيث يأمر صاحب ّ الرحل الرحل أعرف بعورة بيته من ال ّداخل ّ فإن صاحب ّ .عليه “Pindi mmoja wenu atakapoingia kwenye msafara wa ndugu yake, basi akae pale atakapoamrishwa na mwenyeji wake, kwani yeye ni mtambuzi zaidi juu ya sitara ya nyumba yake kuliko huyo mgeni.”140
Aya ya mwisho katika maudhui haya inasema: “Hapana ubaya kwao kwa baba zao, wala watoto wao, wala kaka zao, wala watoto wa kaka zao, wala watoto wa dada zao, wala wanawake wao, wala wale waliomilikiwa na mikono yao ya kuume. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.” Baadhi ya wafasiri wanasema kwamba Aya hii iliteremka kutokana na baba wa wake za Mtume (s.a.w.w.) na watu wengine wa karibu kumuuliza Mtume (s.a.w.w.) ya kwamba na wao wanalazimika kuwa nyuma ya pazia pindi wanapohitaji kitu kutoka kwa wake wa Mtume s.a.w.w? Hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipoteremsha Aya hii na kubainisha hukumu hii, ya kwamba watu wa karibu wa wake wa Mtume 139 140
Al-Kulayniy, Usulul Kafiy, Jz.6, Uk.276 Hurrul Amil, Wasailu Shia Jz. 5, Uk. 322 300
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 300
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
(s.a.w.w.), ambao ni maharimu zao (ni haramu kuoana nao), kwa wao hakuna tatizo lolote kuonana nao uso kwa uso. Katika Aya hii kumetajwa watu wa aina sita ambao wanaruhusika kuonana na wake wa Mtume (s.a.w.w.) bila ya kuwepo kizuizi cha pazia, lakini hukumu hii si kwa watu hao tu, bali ni kwa kila ambaye ananasibiana na wake hao kinasaba katika wale ambao ni haramu kuowana nao. Kwa hiyo katika hukumu hii wanaingia wajomba na baba wakubwa na wadogo. Watu hawa tunaweza kuwadiriki pale walipotajwa watoto wa ndugu wa kiume na watoto wa ndugu wa kike, kwa vile uharamu unakuwa pande zote mbili. Ama kutokutajwa maharimu wengine kama vile baba wa mume na watoto wa mume, ni kutokana na hukumu hii kuhusishwa na wake wa Mtume (s.a.w.w.) peke yao, na pia wakati ilipoteremka Aya hii baba wa Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameshafariki dunia, na alikuwa hana mtoto mkubwa wa kiume. Na pia kutotajwa ndugu wa kunyonya ni kutokana na umashuhuri katika sheria ya Kiislamu ya kwamba watu wa aina hii huingia katika hukumu ya ndugu wa kinasaba katika suala la ndoa. Ibara ya mwisho katika Aya hii inayosema: “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu,” ni kutoa msisitizo juu ya suala la hijabu na sitara kwa mwanamke na kila kinachowaweka mbali na maasi. Na msingi wa jambo hilo ni uchamungu, kwani pasi na uchamungu hakuna wema wowote unaoweza kusimama. Jambo la kuzingatia pale Aya iliposema: “Wala wanawake wao,” ni kwamba inakusudia wanawake wa Kiislamu, kwa hivyo si vyema kwa wanawake wa Kiislamu kutokuwa na hijabu mbele ya wanawake wasio Waislamu, kwani wanawake hao (wasio Waislamu) ni rahisi kwao kueleza maumbile yao kwa waume zao.
301
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 301
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI NA NNE
َ ون َعلَى النَّ ِب ِّي َيا أَُّي َها الَّ ِذ َ ُُّصل صلُّوا َ ين آ َمنُوا َ إِ َّن اللهََّ َو َم اَل ِئ َك َت ُه ي ْ ين ي َ ُؤ ُذ َ َعلَ ْي ِه َو َسلِّ ُموا َت ْسلِي ًما إِ َّن الَّ ِذ ون اللهََّ َو َر ُسولَ ُه لَ َع َن ُه ُم ْ ين ي ُّ اللهَُّ ِفي َ ُؤ ُذ َ الد ْن َيا َوالآْ ِخ َر ِة َوأَ َع َّد لَ ُه ْم َع َذابًا ُم ِهي ًنا َوالَّ ِذ ون ْ َ ْال ُم ْؤ ِم ِن ْ ات ب َغيْر َما اح َت َملُوا بُ ْه َتا ًنا َوإِ ْث ًما ْ اك َت َسبُوا َف َق ِد ِ ِ ِ ين َوال ُم ْؤ ِم َن ُم ِبي ًنا “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika Wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu. Hakika wale ambao wanamuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha. Na wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na waumini wanawake pasi na wao kufanya, hakika wamebeba dhulma kubwa na dhambi kubwa.” (Qur’ani: 33:56-58)
MAELEZO Licha ya kuwa Aya hii haianzi na wito kwa Wauumini kama kusudio la kitabu hiki, lakini wito huo pia unapatikana baada ya maneno machache, na kutokana na umuhimu wa ibada hii tumeona ni vyema tuiorodheshe, kwa lengo la kuwakumbusha Waumini wajibu wao juu ya Mtukufu wa daraja (s.a.w.w.). Baada ya utafiti katika Aya zilizopita, tumeona ni namna gani Waislamu wanatakiwa kulinda heshima ya Mtume (s.a.w.w.) na kutomuudhi. Aya ya kwanza inaanza kuzungumzia mapenzi ya Mwenyezi Mungu pamoja na Malaika Wake juu ya Mtume (s.a.w.w.), na baada ya hapo inawaamuru Waumini kuiga mwenendo huo, na Aya inayofuata inataja adhabu kali kwa wale wasioonesha mapenzi yao kwake na badala yake kumuudhi kwa aina mbalimbali za maudhi. Na Aya ya mwisho inahitimisha kwa kutaja adhabu kwa wale wanaowaudhi Waumini. Aya ya kwanza inaanza kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika Wake wanamswalia Nabii.” Ni daraja kubwa iliyoje aliyonayo Mtume (s.a.w.w.) kiasi
302
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 302
12/8/2014 2:43:46 PM
WITO KWA WAUMINI
cha kumfanya Mola wa walimwengu na Malaika wote waliopewa kazi mbalimbali za kuendesha shughuli katika mbingu na ardhi kumtakia rehema na Amani. Basi ikiwa hali ndio hiyo, enyi Waumini jiungeni pamoja na Mola Wenu kwenye amali hiyo: “Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” Hakika yeye Mtume (s.a.w.w.) ni johari ya walimwengu wote, na johari hii Mwenyezi Mungu ameiweka kwenu, mnaishi nayo, basi msiidharau na kuidogesha, na wala msisahau nafasi yake kwa Mwenyezi Mungu na Malaika Wake. Yeye ni mtu mtakatifu anayeishi nanyi, lakini si mtu kama watu wengine, bali yeye ni mkusanyiko wa maumbile yote ya Mwenyezi Mungu! Tuangalie baadhi ya maneno yaliyomo katika Aya hii: Kwanza: neno Yuswalluuna ni kitendo kinachoendelea, hii inamaanisha ya kwamba, Mwenyezi Mungu na Malaika wake daima na bila ya kusita wanamtakia rehema na amani Mtume (s.a.w.w.) Pili: neno Sallimuu katika neno hili baadhi ya wafasiri wanasema ya kwamba lina maana ya kumtolea salamu Mtume (s.a.w.w.) kwa kusema: Assalamu alayka yaa Rasula llahi. Wanaokubaliana na maana hii huwa wanasema: Swalla llahu Alayhi Wasalam mara tu baada ya kutaja jina lake. Ama Sheikh Makarimu Shiraziy anasema neno hili katika Aya hii lina maana ya unyenyekevu na kusalimu amri kwa Mtume (s.a.w.w.), kwani neno hili linashabihiyana na lile lililoko katika Aya ya 65 ya SuratanNisai, pale Mwenyezi Mungu aliposema:
َ ُح ِّك ُم َ ال َو َرب َ َف َ وك ِفي َما َش َج َر َب ْي َن ُه ْم ثُ َّم َ ِّك ْ ال ي َ ُُؤ ِمن ال َ ون َحتَّ َى ي ًوا َت ْسلِيما ْ ُسلِّ ُم ْ َيج ُد َ ضي َ وا ِفي أَ ُنف ِس ِه ْم َح َرجاً ِّم َّما َق َ ْت َوي ِ “Naapa kwa haki ya Mola Wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye mwamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayotoa, na wanyenyekee kabisa.” (Qur’ani: 4:65).
Na pia maana hii inapatikana katika Riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Imamu as-Sadiq (a.s.) pale Abu Baswir aliposema: “Hakika tunaelewa namna ya kumswalia Mtume, basi ni namna gani ya kumsalimia?” Imamu as-Sadiq alimjibu kwa kusema: “Ni kusalimu amri kwake katika mambo mbalimbali.”141Ama dalili ya wale wanaoona ya kwamba neno hili lina maana ya kutoa salamu ni kutokana na Riwaya ya Ka’ab, pale aliposema: “Baada ya kuteremka Aya hii tulisema: 141
Almajlisiy, Biharul Anwar, Jz. 17, Uk. 19 303
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 303
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
Tumeshajua namna ya kukutolea salamu juu yako, basi ni vipi tukuswalie? Mtume (s.a.w.w.) akasema: Semeni:
ّ الله ّم صل على مح ّمد وآل مح ّمد كما صلّيت على إبراهيم وآل إبراهيم إنّك حميد مجيد وبارك على مح ّمد وآل مح ّمد .كما وباركت على إبراهيم وآل إبراهيم إنّك حميد مجيد “Ewe Mola wangu! Mrehemu Muahammad na aali zake Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kuhimidiwa Mwenye kutukuzwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim naaali Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kuhimidiwa Mwenye kutukuzwa.”142
Kwa mujibu wa Riwaya hii imetubainikia maana ya Swala na Salamu kwa Mtume (s.a.w.w.). Licha ya kuwepo maana hizi mbili tofauti kwenye neno Sallimuu lakini kwa kuzingatia kwa undani maana hizo kuna uwezekano wa maana hizo kuunganishwa na kuwa kitu kimoja, kwa njia ya kauli na kivitendo, kwani mwenye kumsalimia kwa kumtakia rehema na amani kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni kutambua kwamba yeye ni Nabii ambaye anastahiki kutiiwa amri zake. Katika Riwaya hii ya Ka’ab na Riwaya nyingine nyingi katika vitabu vya wanachuoni wa madhehebu ya Kisunni na Kishia kuna maelezo na maelekezo ya namna ya kumswalia Mtume (s.a.w.w.), yeye pamoja na jamaa zake, na hivi ndivyo Waislamu wanavyoitekeleza ibada hii adhimu ambayo ni sehemu (nguzo) katika Swala zetu za wajibu na zisizo za wajibu. Lakini la kusikitisha ni pale anaposwaliwa Mtume (s.a.w.w.) nje ya hizo Swala tano za wajibu na zile zisizo za wajibu. Hatuwasikii jamaa wa Mtume (s.a.w.w.) wakijumuishwa katika kuswaliwa Mtume (s.a.w.w.) kama alivyoagiza, bali watu husikika wakisema au kuandika Swalla llahu alayhi wasallam, badala ya Swalla llahu alayhi waalihi wasallam, licha ya Mtume (s.a.w.w.) kukataza kuswaliwa Swala ambayo haitowajumuisha jamaa zake, kwani amesema:
: وما الصالة البتراء ؟ قال, علي الصالة البتراء ّ ال تصلّوا 142
Ibn Kathir, Tafsirul Qur’anil Adhim, Jz.3, Uk.515 304
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 304
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
ّ اللهم:تقولون اللهم: بل قولوا,صل على مح ّمد وتمسكون ّ .صل على مح ّمد وعلى آل مح ّمد “Msiniswalie swala iliyokatika (kigutu), Masahaba wakauliza: Ni ipi hiyo Swala iliyokatika ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Mtume aliwajibu: Ni kusema, Allahumma swali alaa Muhammad kisha mkanyamaza, lakini kwa kufupisha semeni: Allahumma swali alaa Muhammad wa alaa Aali Muhammad.”143
Kwa mujibu wa Hadithi hii wanachuoni wa Kisunni wamekubaliana juu ya wajibu wa kuingizwa neno Aali Muhammad katika Swala wakati wa kusoma tashahudi ya kwanza na ya pili. Zaidi ya haya, Imamu Shafi anazingatia kutokusihi kwa Swala iwapo mtu ataacha kuwatakia rehema jamaa wa Mtume (s.a.w.w.), anasema:
فرض من اهلل في القرآن نزله
ياآل بيت رسول اهلل حبّكمو
ّ يصل عليكم ال صالة له من لم
كفاكم من فضل القدر أنّكمو
“Enyi watu wa nyumba ya Mtume, kupendwa kwenu ni faradhi (lazima) kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika Qur’ani ameteremsha (42: 23), inatosha kwenu kuwa ni heshima kubwa mliyonayo, kuwa yeyote asiyewatakia rehema hana Swala.”144
Kwa kuzingatia Hadithi hizi za Mtume (s.a.w.w.) pamoja na maneno haya mazito kutoka kwa Imamu Shafi, inatupa taswira halisi juu nafasi ya jamaa wa Mtume (s.a.w.w.) (Ahlulbayt (a.s.)) katika Uislamu na daraja waliyo nayo, kiasi ya kufanywa kuwa ni moja kati ya mambo yanayoifanya Swala ya mwenye kuswali kuwa sahihi! Bali nafasi yao si hiyo tu, bali wao ndio warithi wa Mtume (s.a.w.w.) baaada yake kama mwenyewe Mtume (s.a.w.w.) anavyosema:
أنا تارك فيكم ثقلين أولهما كتاب اهلل فيه الهدى والنور فخذوا بكتاب اهلل واستمسكوا به فحث على كتاب اهلل ورغب فيه ثم ّ أذكركم اهلل في أهل بيتي ّ قال وأهل بيتي أذكركم اهلل في أهل 143 144
Al-Qanduziy, Yanabiul Mawadda Lidhawil Qurba, Jz.1, Uk.38 Az-Zarnadiy al-Hanafiy,Nadhmu Duraru Simtwayni, Uk.18 305
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 305
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
ّ بيتي .أذكركم اهلل في أهل بيتي “Mimi nakuachieni vizito viwili. Cha kwanza: Ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ndani yake kuna uongofu na nuru, basi kishikeni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamane nacho. Basi akahimiza juu ya (kushikamana na) Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuwataka (watu) wakipende. Kisha akasema: ‘Na Ahlu Bayti (watu wa nyumba yangu), nakukumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu watu wa nyumba yangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu watu wa nyumba yangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu watu wa nyumba yangu.”145
Katika kuthibitisha zaidi maneno haya ya Mtume (s.a.w.w.) mfasiri maarufu wa Qur’ani; Ibnu Kathir anasema: Hakika imethibiti katika kitabu sahihi ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema katika khutba yake aliyoitoa Ghadir Khum, ya kwamba:
أحدهما,تمسكتم به لن تضلّوا بعدي ّ إنّي تاركم فيكم ما إن كتاب اهلل حبل ممدود من السماء إلى:أعظم من اآلخر األرض وعترتي أهل بيتي ولن يفترقا حتى يردا على . فنظروا كيف تخلفوني فيهما,الحوض “Hakika mimi ninawaachieni vile ambavyo mkishikamana navyo hamtopotea baada yangu, kimojawapo ni kitukufu zaidi kuliko kingine: (Cha kwanza) Ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ambacho ni kamba iliyonyooshwa kutoka mbinguni hadi ardhini, na (cha pili) ni Kizazi changu changu watu wa nyumbani kwangu, na viwili hivyo kamwe havitaachana mpaka vitakaponifikia katikaHodhi, basi angalieni ni vipi mtanifuata kwenye viwili hivyo.”146
Mtume (s.a.w.w.) hakutosheka na kuyasema hayo tu, bali ametutajia idadi ya hao Makhalifa kwa kusema:
.ال يزال اإلسالم عزيزاً إلى اثنى عشر خليفة “Uislamu hautoacha kuwa na nguvu kwa vile watatawala Makhalifa kumi na 145 146
Muslim, Sahihul Muslim, Babu Fadhaaili Aliy, Jz.7, Uk.123 Tirmidhiy, Sunanu Tirmidhiy,Babu Manaqibu Ahlilbayt Nnabiyy (s.a.w.w.) Jz.5, Uk.329 306
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 306
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
mbili.”147
Mtume (s.a.w.w.) ametukataza kuwafundisha watu hao pamoja na Qur’ani, au kuwatangulia kwa kutanguliza letu, amesema:
. فال تق ّدموهما لتهلكوا وال تعلّموهما فإنّهما أعلم منكم... “Musivitangulie (vizito hivyo viwili), mtaangamia na wala msivifundishe kwani vitu hivyo vinajua zaidi kuliko nyinyi.”
Ama kuhusu suala la kutoandikwa Swalla llahu Alayhi Waalihi Wassalam (s.a.w.w.) katika vitabu vya Hadithi vya madhehebu ya Kissuni ni kutokana na khofu waliyokuwa nayo watu ya kuwaogopa Banu Ummaya, ambao walichukia kuona pameandikwa maneno hayo.148 Aya ifuatayo inaelezea adhabu kwa wale ambao hawaoneshi heshima kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume (s.a.w.w.): “Hakika wale ambao wanamuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha.” Tumeaamua kueleza Aya hii na inayofuata, licha ya kwamba Aya hizi hazibebi katazo au amri kuwaelekea Waumini, bali kilichotufanya tufanye hivyo ni kwamba tumeona ni namna gani Waislamu walivyomuudhi na kumkasirisha Mtume (s.a.w.w.) kama tulivyoshuhudia katika Aya iliotangulia. Baadhi ya wafasiri wamesema ya kwamba, kumuudhi Mwenyezi Mungu ni mtu kufuata ukafiri au upagani, kwani kumuudhi Mwenyezi Mungu si jambo jingine isipokuwa kumghadhibisha. Na wengine wamesema ni ile hali ya kumuudhi Mtume Wake (s.a.w.w.) na Waumini kwa ujumla. Ama kumuudhi Mtume (s.a.w.w.) ni jambo lililo na maana pana sana, linajumuisha ukafiri, upagani, uzushi, tuhuma, kukhalifu maamrisho ya Mwenyezi Mungu, au maudhi kama yale tuliyoyaona katika Aya iliyotangulia na katika Aya ya 61 ya SuratTawba, kwa kusema kwamba yeye ni msikilizaji tu wahabari kutoka kwa watu na kuzipasha kwa wengine kama zilivyo, Aya inasema:
ْ ين ي َ ُون النَّ ِب َّي َو ِي ُقول َ ُؤ ُذ َ َو ِم ْن ُه ُم الَّ ِذ ون ُه َو أُ ُذ ٌن “Na miongoni mwao wako wanaomuudhi Mtume kwa kusema: Yeye ni sikio tu (msiikilizaji).” 147 148
Nawawiy, Sharhu Muslim, Kitabul Imara, Jz.12, Uk.201 Al-Kahlaniy, Subulu Ssalaam, Jz.1, Uk.193. 307
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 307
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
Na pia inajumuisha kuwaudhi watu wake wa karibu, kama Hadithi hii isemavyo:
.فاطمة بضعة منّى فمن أغضبها أغضبني “Fatima ni sehemu yangu, basi mwenye kumghadhibisha amenighadhibisha mimi.”149
Na katika Hadithi nyingine anasema:
ّ .إن فاطمة بضعة منّى يؤذيني ما آذاها “Hakika Fatima ni sehemu yangu, yananiudhi mimi yale yenye kumuudhi yeye.”150
Ama maana ya ‘Laana’ ni hali ya kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu zisizo na kikomo, laana ni aina mbaya ya adhabu hasa ikiwa laana hiyo itamsibu mtu hapa duniani na akhera kama ilivyo katika Aya hii. Aya ya mwisho nayo inazungumzia ubaya wa kuwaudhi Waumini, hii ni kuonesha daraja waliyo nayo mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.), inaseama: “Na wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na waumini wanawake pasi na wao kufanya, hakika wamebeba dhulma kubwa na dhambi kubwa.” Kuandaliwa adhabu hii kwa watu wenye tabia ya kuwaudhi Waumini ni kwa sababu ya mafungamano yaliyopo kati ya Mwenyezi Mungu na wale waliomwamini Yeye, pia kati yao na Mtume (s.a.w.w.), na hayo maudhi yao dhidi ya Waumini hayatokani na ubaya wowote waliowatendea, bali ni kutokana na chuki zao binafsi tu. Basi ni wazi ikiwa watatenda makosa yanayostahili kuadhibiwa kwa njia yoyote ile watastahiki kufanyiwa hivyo kwa mujibu wa sheria, kwani katika Uislamu hakuna mtu aliye juu ya sheria. Uzito na ubaya wa kumuudhi Muumini pia tunaushuhudia katika maneno ya Imamu as-Sadiq (a.s.) pale aliposema:
ّ عز ّ إن اهلل ّ . ليأذن بحرب منّي من آذى عبدي المؤمن:وجل يقول “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Ametangaza vita kutoka Kwangu yule anayemuudhi mja Wangu Muumini.”151
Al-Amin, A’yanu Shia, Jz.1, Uk.297 Tabraniy, Al-Mu’jamul Kabir, Jz.22, Uk.405 151 Al-Majlisiy, Biharul Anwar, Jz.72, Uk.152 149 150
308
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 308
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
Baadhi ya wafasiri wanasema ya kwamba Aya hii iliteremka kutokana na baadhi ya watu katika mji wa Madina kueneza uvumi wa aina mbali mbali dhidi ya Waumini na kuwatuhumu kwa mambo wasiyoyafanya, na hata Mtume (s.a.w.w.) hakusalimika na maudhi ya watu hao. Hali hii bado inashuhudiwa hivi sasa katika jamii mbali mbali, kwani kuna watu ambao kazi zao ni kueneza uongo na tuhuma ili kuwapaka matope Waumini ili wasionekane ni watu wa maana katika nyuso za watu. Kwa kweli Qur’ani Tukufu imewakabili na kuwadhibiti watu hawa kwa maneno makali, na kueleza ya kwamba hayo wayasemayo ni uongo mtupu na ni wenye kubeba mzigo wa madhambi migongoni mwao. Katika Hadithi nyingine Mtume (s.a.w.w.) anaelezea hali ya watu hao itakavyokuwa Siku ya Kiyama, anasema:
من بهت مؤمنا أو مؤمنة أو قال فيه ما ليس فيه أقام اهلل ّ تعالى يوم القيامة على .تل من نار حتّى يخرج م ّما قاله فيه “Mwenye kumsingizia Muumini mwanamume au Muumini mwanamke kwa kitu asichonacho, Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atamsimamisha mtu huyo juu ya kilima cha Moto ili akitoe kile alichomsingizia.”152
152
Al-Hindiy, Kanzul Ummal, Hadithi Na. 7924 309
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 309
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI NA TANO
َ ين آ َمنُوا اَل َت ُكونُوا َكالَّ ِذ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ وسىٰ َف َب َّرأَ ُه اللهَُّ ِم َّما َ ين َآذ ْوا ُم َ َقالُوا َو َك ان ِع ْن َد اللهَِّ َو ِجيهًا “Enyi ambao mmeamini! Msiwe kama wale ambao walimuudhi Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtakasa na waliyoyasema; naye alikuwa ni mwenye heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani: 33:69)
MAELEZO Katika Aya zilizopita tumeona ni jinsi gani ni wajibu kwa kila Mwislamu kuweka heshima ya hali ya juu kwa Mtume (s.a.w.w.) na kujiepusha na kila linalomuudhi. Kwenye Aya hii Mwenyezi Mungu anaelekeza makatazo yake kwa Waumini ili wasiwe ni wenye kumuudhi Mtume wao kama vile walivyofanya wana wa Israil kwa Nabii Musa (a.s): “Enyi ambao mmeamini! Msiwe kama wale ambao walimuudhi Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtakasa na waliyoyasema; naye alikuwa ni mwenye heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.” Mitume wengi waliudhiwa na watu wao, lakini kitendo cha Mwenyezi Mungu kumuanisha Musa (a.s.) katika Aya hii ni kutokana na Nabii huyo kuudhiwa zaidi ikilinganishwa na Manabii wengine. Zaidi ya hao baadhi ya maudhi yanashabihiyana na maudhi ya wanafiki katika kumuudhi Mtume (s.a.w.w.). Qur’ani haikubainisha ni aina gani ya maudhi aliyokuwa akiudhiwa Nabii Musa (a.s.), lakini kutokana na tafiti mbalimbali za wafasiri wameeleza maudhi hayo kama ifuatavyo: 1.
Nabii Musa pamoja na Nabii Harun (a.s.) walikwenda katika mlima. Mara watu wakaeneza uvumi ya kwamba Musa anataka kumuua Nabii Harun, lakiniMwenyezi Mungu alibainisha uzushi wa watu hao.
2.
Wakati Qarun alipotakiwa kutoa zaka ya sehemu ya mali yake, alipanga mpango wa kumfedhehesha Nabii Musa (a.s.) kwa kumrubuni mwanamke asherati ili aseme ya kwamba Nabii Musa (a.s.) alizini naye, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu njama hiyo iligeuka kuwa mwiba kwa Qarun, kwani alichokifanya mwanamke huyo ni kuthibitisha ya kwamba Nabii 310
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 310
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
Musa (a.s.) ni mtu mwema na mwenye kujitakasa na kila aina ya uchafu. 3.
Baadhi ya watu walimtuhumu ya kwamba ni mchawi, lakini Mwenyezi Mungu aliweza kumsafisha na tuhuma hizo kwa kumpa miujiza mikubwa iliyowashangaza watu hao.
4.
Watu wajinga miongoni mwa wana wa Israil walikuwa wakimtuhumu ya kwamba ana mbalanga na ukoma katika mwili wake, kwa vile alikuwa hakogi pamoja nao akiwa hana nguo.
5.
Kuna wale ambao mara kwa mara walimtaka awaoneshe Mwenyezi Mungu waziwazi, wengine wakimwanbia kwamba wamechoka kula chakula cha aina moja, wengine wakisema kwamba hawako tayari kuingia Palestina kupambana dhidi ya adui, na kumwambia kwamba aende yeye pamoja na Mola Wake wakapambane dhidi ya adui, baada ya kumshinda ndipo wao wataingia!
Kwa kweli Aya imejumuisha aina zote za maudhi kutoka kwa wana wa Israili kwa Nabii Musa (a.s.) kwani watu hao walimuudhi kwa aina mbalimbali za maudhi, na maudhi yao hayatofautiani na maudhi ya watu wa Madina kwa Mtume (s.a.w.w.), kama vile kudai ya kwamba ni muongo, kumtuhumu mke wake kwamba amefanya khiyana katika ndoa, upinzani na upingaji baada ya kumuoa Bibi Zaynab, namna walivyokuwa wakimwita pale walipokuwa wakimuhitaji pasi na kutumia taratibu za kawaida (wakimuita kwenye madirisha), na mengi mengineyo. Kutokana na daraja aliyokuwa nayo Nabii Musa (a.s.) kwa Mwenyezi Mungu, maadui hawakuweza kufanikiwa katika maudhi yao, kwani Mwenyezi Mungu alimlinda na kuonesha kwamba hayo wamfanyiayo hayana msingi wowote. Huo ndio utaratibu Wake wa kuwasafisha Mawalii Wake. Ameyafanya hayo kwa Nabii Yusuf, pale mke wa waziri alipomtuhumu, na pia kwa Bibi Maryam (a.s.) kwa kumuwezesha mtoto wake mchanga (Nabii Isa (a.s.)) kutamka matamshi ya kumsafisha na kila tuhuma mbaya, na hivyo kuziba midomo ya wana wa Israili waliokuwa wakienda huku na kule katika kueneza tuhuma dhidi yake. Aya hii kama zilivyo Aya nyingine haiishii hukumu yake katika zama za Mtume (s.a.w.w.) peke yake, bali inawahusu Waislamu wote katika zama zote, kwani kuna wale ambao husikika wakimdogesha Mtume (s.a.w.w.) kwa kudai ya kwamba haipaswi kusifiwa kwani anashabihiyana na watu wengine! Na pia tutambue kuwa kumuudhi Mtume (s.a.w.w.) huthibiti kwa kuwaudhi watu wa nyumbani kwake kama Riwaya zilivyotangulia katika maudhui yaliotangulia.
311
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 311
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI NA SITA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ُصلِ ْح لَ ُك ْم ْ ين آ َمنُوا اتَّ ُقوا اللهََّ َو ُقولُوا َق ْو اًل َس ِدي ًدا ي َ ُطع اللهََّ َو َر ُسولَ ُه َف َق ْد َف ْ أَ ْع َمالَ ُك ْم َو َي ْغ ِف ْر لَ ُك ْم ُذنُو َب ُك ْم َو َم از ي ن ِ ِ َف ْو ًزا َع ِظي ًما “Enyi ambao mmeamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni kauli ya sawa. Atawatengenezea matendo yenu na atawaghufiria dhambi zenu. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, hakika amefuzu kufuzu kukubwa.” (Qur’ani; 33:70-71)
MAELEZO Baada ya uchambuzi wa Aya mbalimbali zilizoonesha namna baadhi ya watu walivyokuwa wakiwaudhi Mitume na Waumini, sasa tunaona miongoni mwao hao waliokuwa wakiwaudhi watu walikuwemo Waislamu, katika kutibu ugonjwa huo wa kijamii Mwenyezi Mungu amemshushia Mtume Wake Aya hii, badala ya kuzungumza maneno yasiyofaa na yenye kuwaudhi watu. Wazungumze maneno mazuri yenye kujenga upendo kati yao, maneno yenye kuimarisha jamii na yenye nasaha kwa ajili ya mustakabali wao, maneno ya ukweli yasiyo na uongo ndani yake, na haya yote yataweza kupatikana kwa mtu kujipamba na pambo la uchamungu, kwani ndilo jambo la kwanza waliloamrishwa Waumini, na bila ya kumuogopa Mwenyezi Mungu haya hayawezi kusimama, na haya tunayashuhudia katika nchi mbalimbali zenye mifumo ya kisekyula ambazo zimeunda idara mahasusi kwa lengo la kueneza uongo dhidi ya Uislamu na Waislamu. Aya inayofuata inaeleza natija na mambo atakayoyapata mwenye kusema maneno mazuri: “Atawatengenezea matendo yenu na atawaghufiria dhambi zenu.” Kwa hakika uchamungu ni msingi mkubwa wa kuutengeneza ulimi na ni chemchemu ya maneno ya kweli na ya haki, na maneno ya haki ni moja kati ya mambo yanayoyafanya matendo ya mtu kuwa mazuri, na pale vitendo vinapokuwa vizuri basi hiyo huwa ni sababu kubwa ya kusamehewa madhambi mbalimbali, kwani: “Mema hufuta maovu.” 312
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 312
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
Wanachuoni wa elimu ya nafsi wanasema: “Ulimi ni kiungo chenye baraka na kheri nyingi zaidi kuliko kiungo kingine, na ni njia bora zaidi katika kumfikisha mwanadamu katika uongofu na uchamungu, lakini pia kiungo hicho ni hatari zaidi na chenye kuchuma madhambi mengi kuliko kiungo kingine miongoni mwa viungo vya mwanadamu kiasi cha kufikia idadi ya madhambi thelathini miongoni mwa madhambi makubwa hufanywa na kiungo hicho chenye umbile dogo.”153 Na katika maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na ulimi anasema:
اليستقيم إيمان عبد حتّى يستقيم قلبه واليستقيم قلبه حتّى .يستقيم لسانه “Imani ya mwanadamu haiwi katika msimamo mzuri mpaka moyo (akili) wake utakapokuwa katika msimamo mzuri, na wala moyo wake hauwi katika msimamo mzuri mpaka pale ulimi wake utakaponyooka.”154
Na pia maneno yanayohusiana na ulimi tunayapata kutoka kwa Imamu Zaynul Abidin (a.s.) akisema:
ّ إن لسان ابن آدم يشرف ّ كيف:كل يوم على جوارحه فيقول اهلل اهلل: ويقولون. نحن بخير إن تركتنا:أصبحتم؟ فيقولون . إنّما نثاب بك ونعاقب بك: ويناشدونه ويقولون,فينا “Hakika kila siku ulimi wa mwanadamu huongoza viungo vyake (vya mwanadamu), ulimi huviuliza viungo: Mmeamkaje? Hujibu: Sisi tuko salama ikiwa utatuacha kama tulivyo, na huendelea kusema: Tahadhari sana nasi, kwani sisi hulipwa mema kwa sababu yako na pia huadhibiwa kwa sababu yako.”155
Kuna riwaya mbalimbali zinazoelezea faida na hasara zinazopatikana kutokana na namna mtu anavyoutumia ulimi wake, kutokana na hali hii kuna riwaya isemayo ya kwamba, Mtume (s.a.w.w.) kila alipokuwa akipanda katika mimbari alikuwa haachi kuisoma Aya hii isemayo: Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.13, Uk. 365 Al-Mahmudiy, Nahju Sa’ada, Jz.7, Uk.373 155 Al-Majlisiy, Biharul Anwar, Jz.68, Uk.278 153 154
313
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 313
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
ًال َس ِديدا ً ين آ َمنُوا اتَّ ُقوا اللهََّ َو ُقولُوا َق ْو َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ “Enyi ambao mmeamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni kauli ya sawa.”
Katika ibara ya mwisho ya Aya inaeleza malipo makubwa zaidi atakayoyapata mwenye kujipamba na sifa ya uchamungu ikiwemo kusema maneno mazuri yenye manufaa kwa wengine: “Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, hakika amefuzu kufuzu kukubwa.” Malipo yaliyotajwa hapa zaidi ya kusamehewa makosa, ni malipo ambayo ni vigumu kuelezeka, ni malipo ambayo hakuna yeyote anayetambua uhalisia wake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
314
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 314
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI NA SABA
ْ ص ْر ُك ْم َوي َُثب َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ِّت أَ ْق َدا َم ُك ْم ُ ص ُروا اللهََّ َي ْن ُ ين آ َمنُوا إِ ْن َت ْن َ َْسا لَ ُه ْم َوأ َ َوالَّ ِذ ض َّل أَ ْع َمالَ ُه ْم ً ين َك َف ُروا َف َتع “Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu Naye atawanusuru na ataithibitisha miguu yenu. Na waliokufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao. Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.” (Qur’ani: 47:7-8)
MAELEZO Aya hii ni miongoni mwa Aya zinazotoa hamasa kwa Waumini katika kupigana vita vya Jihadi dhidi ya maadui, na kueleza bayana ya kwamba, moja kati ya alama za imani ya kweli ni mtu kuwa tayari kukabiliana na adui. Kumnusuru Mwenyezi Mungu kunamaanishi kuinusuru Dini Yake, mafunzo Yake, sheria Zake, na Mtume Wake, ndio maana hata katika baadhi ya Aya panapotajwa kumnusuru Mwenyezi Mungu huambatanishwa na kumnusuru Mtume Wake pia, kama ilivyo katika Aya hii isemayo:
َ الصا ِد ُق َ نص ُر ون َّ ون اللهََّ َو َر ُسولَ ُه أُ ْولَِئ َك ُه ُم ُ َو َي “Na wanamnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi hao ndio Waislamu wa kweli.” (Qur’ani:59:8).
Licha ya kuwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ni uwezo usio na kifani, ni uwezo usio na kikomo, uwezo wa viumbe hauna uzito wowote mbele ya uwezo Wake, Mwenyezi Mungu amewataka Waumini wamnusuru si kwa sababu ya kwamba Yeye ni dhaifu, bali ni kwa lengo la kuwafahamisha Waislamu umuhimu wa Jihadi kwa kutumia usemi huu uliojaa fasaha. Natuangalie hizo ahadi alizozitoa kwa mujahidina pale watakapoitetea Dini yao, kwanza anasema: “Naye atawanusuru.” Ni namna gani inavyokuwa hiyo nusra?
315
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 315
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa hakika njia za kupata nusra ya Mwenyezi Mungu ni nyingi sana, kama vile kuimakinisha imani katika nyoyo zao na kuzijaza uchamungu, na kuwapa nguvu na ukakamavu zaidi, na kuwafanya wafikiri vizuri na kuwa watulivu katika kupanga na kuamua mambo. Na kwa upande mwingine huwapelekea Malaika wa kuwasaidia katika mapambano yao dhidi ya maadui, huwafanya watu wavutike na maneno yao na busara zao, na harakati zao kuwa ni zenye kuzaa matunda. Bila shaka nusra ya Mwenyezi Mungu humzunguka Muumini nje ya kiwiliwili chake na kupenya ndani ya nafsi yake na roho yake. Ama kuhusiana na ahadi nyingine ni pale aliposema: “Na ataithibitisha miguu yenu.” Jambo la kuwa mkakamavu mbele ya adui ni ishara ya ushindi, kwani ni wale tu wenye subira na uvumilivu ndio wanaoshinda vita, kama vile tunavyojifunza katika kisa cha Taluti ambaye alikuwa ni kiongozi mahiri wa kijeshi kwa upande wa wana wa Israili dhidi ya majeshi yaliyokuwa yakiongozwa na Jaluti. Waumini wachache waliokuwa pamoja na Taluti ndio walioweza kulishinda jeshi kubwa lililokuwa na zana za kutosha za kivita. Miongoni mwa mambo muhimu waliyoyafanya Waumini hao ni kumuelekea Mola Wao na kumuomba awajaalie kuwa wakakamavu na awape ushindi dhidi ya maadui, kama vile Mwenyezi Mungu anavyobainisha katika Aya isemayo:
ًصبْرا ْ ُوت َو ُجنُو ِد ِه َقال ْ َولَ َّما َب َر ُز َ ُوا لِ َجال َ وا َربَّ َنا أَ ْف ِر ْغ َعلَ ْي َنا ْ َو َثب َ انص ْر َنا َعلَى ْال َق ْو ِم ْال َكا ِف ِر ين ُ ِّت أَ ْق َدا َم َنا َو
“Na walipotoka kupambana na Jaluti na majeshi yake walisema: Ewe Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu makafiri.”
Katika Aya inayofuata inaweka wazi ya kwamba kuiambatanisha miguu katika ardhi (ukakamavu) ni sababu ya kumshinda adui, Mwenyezi Mungu anasema:
َ ُُوهم ِبإِ ْذ ِن اللِهّ َو َق َت َل َدا ُوو ُد َجال ُ َف َه َزم وت “Basi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (watu wa Taluti) waliwatimua (maadui wao), na Daudi akamuuwa Jaluti…” 316
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 316
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
Kutokana na hali inayoendelea, ni kwamba jeshi la maadui siku zote huwa ni kubwa na lenye kila aina ya silaha na zana za kivita ikilinganishwa na jeshi la Kiislamu, hali hii huwenda ikawashughulisha baadhi ya mujahidina wakati mwingine kwa kujawa na majonzi na simanzi. Aya ifuatayo inawaeleza Waumini hali inavyokuwa kwa maadui wa Uislamu licha ya kudhihirisha ubabe wao: “Na waliokufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao.” Kwa hakika kuna tofauti kubwa kati ya makundi haya mawili. Tumeona ni vipi Mwenyezi Mungu anavyowatia nguvu na kuwamakinisha Waumini. Ama kwa upande wa maadui zao huwa ni maangamizi na hasara ya mali na nafsi, na hukosa wa kuwanusuru pale mambo yanapopamba moto, kama vile Waumini wanavyopata msaada na nusra kutoka kwa Malaika. Hakika matendo ya Waumini hupata baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ama vitimbi vya maadui huwa kama pamba yenye kupeperushwa na upepo. Aya ya mwisho inaelezea sababu za kushindwa watu hawa (maadui wa Uislamu) inasema: “Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.” Jambo la kwanza Mwenyezi Mungu ameleta Dini yenye kumpwekesha Yeye, lakini watu hawa wameiweka Dini hiyo nyuma ya migongo yao na wakashikamana na ushirikina. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameamrisha haki na uadilifu, usafi wa nafsi na uchamungu, lakini hawa wameyakataa yote haya na wakashikamana na dhulma na ufisadi, na pale wanaposomewa Aya za Mwenyezi Mungu nyoyo zao huchukia mno, kwa hivyo ni jambo la kawaida kwa watu hawa kushindwa na matendo yao kupotea patupu. Ni mambo mengi aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, lakini kwa masikitiko hata baadhi ya Waislamu wanayachukia mambo hayo. Wako ambao hawataki kuona sheria ya Kiislamu inatawala katika nchi zao, na wako tayari kupambana vikali dhidi ya kila ambaye hunyanyua sauti yake ya kutaka sheria hiyo ichukue nafasi yake katika maisha ya wanadamu. Kwa hiyo kila mmoja achukue tahadhari ili asiwe ni miongoni mwa wachukiaji wa mambo yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake: “Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.”
317
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 317
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI NA NANE
َ الر ُس َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ْطلُوا َّ ين آ َمنُوا أَ ِطيعُوا اللهََّ َوأَ ِطيعُوا ِ ول َو اَل تُب َ أَ ْع َمالَ ُك ْم إِ َّن الَّ ِذ يل اللهَِّ ثُ َّم َماتُوا َو ُه ْم َ ين َك َف ُروا َو ِ ص ُّدوا َع ْن َس ِب ار َفلَ ْن َي ْغ ِف َر اللهَُّ لَ ُه ْم ٌ ُك َّف “Enyi ambao mmeamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume; wala msiviharibu vitendo vyenu. Hakika ambao wamekufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria.” (Qur’ani; 47:33-34)
MAELEZO Aya ya kwanza inawataka wale Waumini wenye kutenda kwa mujibu na imani yao wazidi kufanya hivyo, na wale ambao vitendo vyao vinapingana na imani zao basi wafanye hima kurudi kwa Mwenyezi Mungu kwa kushikamana na maamrisho Yake na kuachana na makatazo Yake, kwani mtu hawi Muumini wa kweli ikiwa hatoonesha utiifu kamili kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake: “Enyi ambao mmeamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume;” Sababu ya kuteremshwa Aya hii ni kutokana na watu wa ukoo wa Bani Asad kuingia katika Uislamu, na siku moja walikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na wakamwambia: “Kwa hakika sisi tunakupenda zaidi kuliko tunavyozipenda nafsi zetu, na sisi pamoja na watu wetu ni rehani ya amri yako.” Lakini namna watu hao walivyokuwa wakizungumza walikuwa wakijionesha ya kwamba wao ni wazuri wenye fasaha zaidi kuliko Mtume (s.a.w.w.), hapo ndipo Aya hii ya kwanza ikateremshwa.156 Ibara ya mwisho inamalizia kwa kusema: “Wala msiviharibu vitendo vyenu.” Hii ni dalili ya kwamba matendo maovu huathiri vibaya matendo mema kidogo kidogo, na si hivyo tu kuna baadhi ya matendo huporomosha matendo yote mema, kama kwamba hakuna wema wowote alioutenda Mwislamu, kama vile ushirikina, kujionesha katika kufanya ibada (riya), majigambo, majivuno n.k. Aya ya mwisho inatoa angalizo kwa wale wasiotaka kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.) kwamba hawatopata msamaha wowote kutoka kwa Mwenyezi Mungu 156
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.16, Uk. 391 318
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 318
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
ikiwa watakufa katika hali hiyo ya uasi pasi na kurejea katika Dini ya haki na mafunzo sahihi ya Dini hiyo: “Hakika ambao wamekufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria.”
UTAFITI Mambo Yanayoporomosha Matendo Mema: Kuna Aya nyingi sana ambazo zimewatahadharisha Waumini juu ya matendo yao kuporomoka, na hatimaye kuwa sawa na makafiri katika malipo Siku ya Kiyama. Kwa hakika kuna tofauti kubwa kati ya kufanya vitendo vizuri vyenye kumridhisha Mwenyezi Mungu na kuvihifadhi vitendo hivyo visizidiwe na wingi wa uovu au ukubwa wa tendo ovu. Vitu ambavyo hupelekea kuanguka na kuporomoka matendo mema ya mwanadamu ni mengi, miongoni mwa hivyo ni kama ifuatavyo: 1.
Masimango,maudhi na kujionesha, kama Mwenyezi Mungu anavyosema:
ق ُ ِص َدقَاتِ ُكم بِا ْل َمنِّ َواأل َذى َكالَّ ِذي يُنف َ يَا أَيُّ َها الَّ ِذ َ ين آ َمنُو ْا الَ تُ ْب ِطلُو ْا ّس َوالَ يُ ْؤ ِمنُ بِ ه اآلخ ِر ِ اللِ َوا ْليَ ْو ِم ِ َمالَهُ ِرئَاء النَّا “Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama anayetoa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho.” (Qur’ani: 2:264)
2.
Kujivuna, kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:
.العجب يأكل الحسنات كما تأكل النّار الحطب “Majivuno yanakula wema kama vile moto unavyokula kuni.”157
3.
157
Choyo, Riwaya iliyopokewa kuhusiana na choyo inashabihiyana na hiyo riwaya inayohusiana na majivuno, anasema Mtume (s.a.w.w):
Al-Ayniy, Umdatul Qariy, Jz.11, Uk.77 319
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 319
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
ّ ,إيّاكم الحسد .فإن الحسد يأكل الحسنات كما تأكل النّار الحطب “Jihadharini na choyo, kwani choyo hula wema kama vile moto unavyokula kuni.”158
Kwa hiyo jambo la msingi katika kuhakikisha mema yanabakia ni mtu kujichunga ili asitumbukie katika maovu, kinyume chake itakuwa ni kazi bure, Mwenyezi Mungu anasema:
ُولَ َق ْد أ َ وح َي إلَي َ ْك َوإِلَى الَّ ِذ ين ِم ْن َق ْبلِ َك لَِئ ْن أَ ْش َر ْك َت لََي ْح َب َط َّن َ ِ ِ َ اس ِر ين ِ َع َملُ َك َولََت ُكو َن َّن ِم َن ْال َخ
“Na kwa hakika yamefunuliwa kwako na kwa wale waliokuwa kabla yako (maneno haya): Kama ukimshirikisha (Mwenyezi Mungu) bila shaka amali zako zitaruka patupu na utakuwa ni miongoni mwa wenye kula hasara.”
Kwa kweli katika kuyahifadhi matendo mema kuna uzito na ugumu wa hali ya juu sana, kwa hiyo inapasa kwa kila Muumini kuchukua hatua za makusudi katika kulitekeleza jambo hili, anasema Imamu Muhammad al-Baqir (a.s.):
.اإلبقاء على العمل أش ّد العمل “Ni kazi kubwa kuibakisha amali njema.”159
Baada ya maneno haya ya Imamu al-Baqir (a.s.) kuna mtu aliuliza: Ni namna gani ya kuibakisha amali njema? Imamu alimjibu kwa kusema:
,سرا ّ الرجل بصلة وينفق نفقة هلل وحده ال شريك له فكتب له ّ يصل . ث ّم يذكرها فتمحى فكتب له رياء,ث ّم يذكر فتمحى فكتب له عالنيّة 158 159
Sijistaniy, Sunan Abi Daud, Babu La’n, Jz.2, Uk. 457 Rishahriy, Mizanul Hikma, Jz.2, Uk. 1021 320
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 320
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI “Ni kwa mtu kuwaunga ndugu zake na kutoa sadaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Peke yake Asiye na mshirika. Kwa kufanya hivyo huandikiwa thawabu kwa kufanya kitendo kwa siri. Kisha kama kitendo hicho atakisimulia, hapo zile thawabu za siri kufutwa na kuandikwa za dhahiri, kisha kama atakisimulia tena, zile thawabu zake hufutwa na kuandikwa kuwa ni kitendo cha kujionesha.”160
Kwa hiyo ni wajibu wetu kushikamana na mafunzo na amri ya Mwenyezi Mungu isemayo: “Wala msiviharibu vitendo vyenu.”
160
Alkafiy, Usulul Kafiy, Jz.2, Uk. 296 321
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 321
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SITINI NA TISA
ََّيا أَُّي َها ال ََّْن َي َدي اللهَِّ َو َر ُسولِ ِه َواتَّ ُقوا الله ِّ ين آ َمنُوا اَل تُ َق َ َ ي ب وا م د ذ ُ َ ِ ِ إِ َّن اللهََّ َس ِمي ٌع َعلِي ٌم “Enyi ambao mmeamini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mjuzi.” (Qur’ani: 49:1)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasiri wameeleza sababu mbalimbali zinazohusiana na uteremkaji wa Aya hii, miongoni mwa hizo ni pale Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kuelekea katika kijiji cha Khaybar alitaka kumuacha mtu fulani katika mji wa Madina ili asimamie mambo ya Waislamu, lakini Umar alipendekeza mtu mwingine, hapo Aya hii ikateremka, huku ikiwataka Waumini wasitangulize lao mbele ya lile lililoamuliwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.) Wafasiri wengine wanasema: Ilikuwa baadhi ya watu wakisema, lau ingetuteremkia Aya ingekuwa vyema, hapo Aya hii ikateremka ili kukataza tabia hiyo. Wengine wanasema: Aya hii iliteremka kutokana na baadhi ya Waislamu kutekeleza ibada fulani kabla ya kufika wakati wake.161
MAELEZO Makusudio ya kutotanguliza kitu mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni kuacha kutoa rai juu ya jambo ambalo wameliamua na kulikatia shauri. Licha ya sababu zilizoelezwa na wafasiri, Aya inatoa maana pana juu ya ubaya wa kutanguliza kitu mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Aya inakusudia kutanguliza kila jambo na mipango yoyote au kufanya kinyume na maagizo yao, kwani hata katika taratibu za uongozi haistahiki kwa muongozwa kutanguliza jambo lake mbele ya kiongozi. Pamoja na hayo haimaanishi ya kwamba haifai kumshauri Mtume (s.a.w.w.) bali jambo lisilofaa ni mtu kuchukua maamuzi kabla ya Mtume (s.a.w.w.) hajawafikiana na jambo kadhaa, au mtu kuleta mjadala mrefu kwa yale ambayo Mtume (s.a.w.w.) 161
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.16, Uk. 5 322
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 322
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
ameyatolea hukumu na maamuzi, hasa ikizingatiwa kwamba Mtume (s.a.w.w.) ni mtu asiyetenda makosa. Kufuata Mafunzo Ya Uislamu Kikamilifu: Suala la uongozi wa jambo lolote lile haliwezi kutimia hata kama kiongozi ni mzuri na mtaalamu ikiwa kutakosekana utiifu kwa kiongozi huyo. Kwani ni mara ngapi jeshi lenye nguvu limeweza kushindwa kutokana na kupinga amri ya kiongozi, na hata Waislamu pale walipokhalifu amri ya Mtume (s.a.w.w.) matokeo yake ilikuwa ni kushindwa na kuonjeshwa machungu, kama vile ilivyotokea katika vita vya Uhud. Katika kulipa umuhimu suala hili Mwenyezi Mungu analieleza katika ibara fupi, lakini iliyojaa kila sababu ya ushindi na mafanikio ya dunia na ya akhera: “Enyi ambao mmeamini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Makusudio ya Aya kama tulivyooana ni kwamba haifai kumtangulia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika mambo ambayo wao ndio waamuzi na mwanadamu lake ni kusikiliza, kutii na kutekeleza tu. Katika historia ya Kiislamu kuna baadhi ya matukio yanayoonesha baadhi ya watu kutanguliza yao kwa kukhalifu amri ya Mtume (s.a.w.w.) na kushikamana na ya kwao, baadhi ya matukio hayo ni kama yafuatayo:
162
1.
Wakati Mtume (s.a.w.w.) alipotoka pamoja na Maswahaba zake kuelekea Makka kwa lengo la kuukomboa mji huo, ikiwa ni katika mwezi wa Ramadhani, walipofika katika nyumba ya Kara’i al-Ghamimu, Mtume (s.a.w.w.) aliomba apelekewe maji, baada ya kupelekewa alikunywa maji hayo, pia baadhi ya Maswahaba walikunywa, lakini la kushangaza baadhi ya Maswahaba hawakuafikiana na kufungua funga yao baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuwataka wafanye hivyo, basi Mtume (s.a.w.w.) aliwaita kuwa ni waasi.162
2.
Tukio jingine ni pale Mtume (s.a.w.w.) alipokwenda Makka kufanya ibada ya Hijja pamoja na Maswahaba mnamo mwaka wa kumi Hijiria, Hijja ambayo inajulikana kwa Hijjatul-Wada’a. Baada ya kufanya ibada katika mji wa Makka, Mtume (s.a.w.w.) alimwamrisha mmoja kati ya Maswahaba zake atangaze ya kwamba yule ambaye hakutoka na mnyama wake kwa ajili ya kuchinja avue nguo zake za ihramu na avae nyingine na anaruhusiwa kufanya yale yaliyokuwa yamezuiliwa kwake, na hizo ibada alizozifanya ni ibada za Umra, na yule ambaye yuko na mnyama wake abakie na nguo zake za ihramu na si halali kwake kufanya yaliyozuilika kwake, na baada ya hapo atafanya ibada ya Hijja… Kisha Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Lau kama mimi nisingetoka na
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.16, Uk. 521 323
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 323
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
mnyama basi ningevua ihramu na kuwa huru kutokana na yale yaliyoharamishwa, na ibada niliyoifanya ingekuwa ni ibada ya Umra, basi ambaye hakuja na mnyama awe huru kwa kufanya yale yaliyoharamishwa kwake.” Lakini Maswahaba wengi walikataa amri hiyo na kusema: “Ni vipi tutajihalalishia mambo na hali bado Mtume (s.a.w.w.) yuko katika vazi la ihramu, je, si ni jambo baya ikiwa tutaelekea kufanya ibada ya Hijja huku vichwa vyetu vinatiririka maji ya josho (josho la janaba)?” Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kusikia maneno yao hayo alikasirika na kuwalaumu sana.163 3.
Tukio jingine ni kutokana na kisa maarufu kijulikanacho kama ‘Jeshi la Usamah.’ Tukio hilo lilitokea pale Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa katika siku zake za mwisho za kuaga dunia, aliwaamrisha Waislamu wajiunge na jeshi la Usamah ibn Zayd kwa ajili ya kupambana na wanajeshi wa dola ya Roma, lakini baadhi ya Muhajirina na Answari walikataa amri hiyo kwa hoja ya kwamba hawawezi kumuacha Mtume (s.a.w.w.) kutokana na hali aliyokuwa nayo. Mtume (s.a.w.w.) aliwalaani wale wote waliokhalifu amri yake.164
4.
Jambo jingine ni ‘Tukio la Karatasi.’ Tukio hili lilitokea wakati Mtume (s.a.w.w.) akiwa mgonjwa kitandani na akiwa katika masiku ya mwisho ya uhai wake. Aliagiza apelekewe karatasi na kalamu ili awaandikie Waislamu usia ambao utakuwa ni dira ya kuwapeleka katika njia iliyo sawa katika maisha yao yote, lakini Umar ibn Khattab alikataa katakata kutekelezwa agizo hilo kwa madai ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) amezidiwa na ugonjwa na Qur’ani inatosheleza. Kilichotokea ni mvutano kati ya wale waliotaka amri ya Mtume itekelezwe na wale waliomuunga mkono Umar kupinga amri ya Mtume (s.a.w.w.). Kelele zilipozidi Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia: “Niondokeeni, kwani haifai kuzozana mbele yangu!”165
Haya ni baadhi tu ya matukio yanayoashiria namna gani watu walivyotanguliza mambo yao mbele ya Mtume (s.a.w.w.) na jinsi msimamo wa Mtume (s.a.w.w.) ulivyokuwa. Kwa hiyo ndugu msomaji bado Aya inatutaka na sisi kuhakikisha matendo yetu hayavuki mipaka ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kama si hivyo tutafikwa na yale yaliyowafika wale waliokhalifu, kwani wako walioitwa waasi,waliokasirikiwa,waliolaaniwa na waliotimuliwa katika hadhara ya Mtume (s.a.w.w.), na Mtume akafariki dunia wakiwa katika hali ya kulaaniwa na kufukuzwa. Kitabu kilichotangulia. Al-Hasahaniy, Shawahidu Tanzil, Jz.1, Uk.338 165 Muslim, Sahihu Muslim, Kitabul Wasia, Hadithi Na. 22 163 164
324
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 324
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ص ْو ِت النَّ ِب ِّي َو اَل ْ َين آ َمنُوا اَل َت ْر َفعُوا أ َ ص َوا َت ُك ْم َف ْو َق ْ َت ْج َه ُروا لَ ُه ب ُ ْض َ َ ْض أَ ْن َت ْح َب َط أَ ْع َمالُ ُك ْم ع ب ل م ك ع ب ْر ه ج ك ل و ق ال ْ َ َ ْ َ ِ ِ ِ ٍ ِ ِ َ َّ ُّ ين َي ُغ َ ض َ ون إِ َّن ال ِذ َ ُر ول ُ َوأَ ْنتُ ْم اَل َت ْشع ْ ون أ ِ ص َوا َت ُه ْم ِع ْن َد َر ُس َ اللهَِّ أوالئك الَّ ِذ ين ا ْم َت َح َن اللهَُّ ُقلُو َب ُه ْم لِلتَّ ْق َوىٰ لَ ُه ْم َم ْغ ِف َر ٌة َوأَ ْج ٌر َ َع ِظي ٌم إِ َّن الَّ ِذ ات أَ ْك َث ُر ُه ْم اَل ِ ين يُ َنا ُدو َن َك ِم ْن َو َرا ِء ْال ُح ُج َر َون َولَ ْو أ َُي ْع ِقل َص َب ُروا َحتَّىٰ َت ْخ ُر َج إل َّ َ ْه ْم لَ َك َ ْرا لَ ُه ْم ي م ه ن ً ان َخي ُ ْ َ ِ ِ ور َر ِحي ٌم ٌ َواللهَُّ َغ ُف “Enyi mlioamini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaanguka, na hali hamtambui. Kwa hakika ambao wanateremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amezitia mtihani nyoyo zao kwa takua. Hao watakuwa na maghufira na ujira mkubwa. Hakika ambao wanakuita nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili. Na lau wao wangelingojea mpaka uwatokee ingelikuwa kheri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani: 49:2-5)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasiri wanasema: Aya hii iliteremka pale watu wa kabila la Tamimu walipoingia katika mji wa Madina, na walipofika katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w.) walimwita Mtume (s.a.w.w.) kwa sauti ya juu wakati akiwa ndani ya nyumba yake, kwa kusema: “Ewe Muhammad toka uje tuna shida na wewe.” Sauti hizo zilimkera na kumuudhi sana Mtume (s.a.w.w.), na alitoka na kuwaendea, alipofika walisema: “Tumekuja ili tujifakharishe, kwa hivyo mruhusu mshairi wetu na khatibu wetu wazungumze kuhusiana na ubora wa kabila letu.” Mtume (s.a.w.w.) aliwaruhusu kufanya hivyo. Khatibu wao alisimama na kuanza kuzungumzia ubora na sifa mbalimbali ambazo nyingi zake zilikuwa si za kweli. Mtume (s.a.w.w.) alimuamuru Thabit ibn Qaysi ili awajibu watu hao. Alisimama na kutoa khutba ambayo iliweza kufunika yale yote aliyoyazungumza khatibu wao. 325
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 325
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
Baadaye alisimama mshairi wao na kutoa shairi la kusifia kabila lao, mara Hasan ibn Thabit alisimama na kumjibu kwa shairi zito. Mmoja kati ya wakubwa wa kabila hilo aitwae al-Aqra’a alisema: “Hakika mtu huyu (Muhammad) khatibu wake ni hodari kuliko khatibu wetu na mshairi wake ni mahiri kuliko mshairi wetu na pia sauti yake ni yenye kufika mbali zaidi kuliko sauti ya mshairi wetu…” Mtume (s.a.w.w.) aliaamuru wapewe zawadi watu hao huku akitarajia nyoyo zao huenda zikavutika na Utume wake. Kwa kweli Aya hii inaangalia hali hii na hali ya kumuita Mtume (s.a.w.w.) kwa sauti ya juu pale anapokuwa ndani ya nyumba. Pia kuna sababu nyingine ya kuteremka Aya hii kama ilivyoelezwa na wafasiri: Katika mwaka wa tisa wa Hijiria wakati makabila mbalimbali yalipokuwa yakienda kwa Mtume (s.a.w.w.) kwa lengo la kuingia katika makubaliano ya amani au kuweka mikataba ya kuishi chini ya utawala wa dola ya Kiislamu, alipofika mwakilishi wa kabila la Tamimu kwa Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakar alisema: Al-Qa’aqa’a ndio awe mwakilishi wao. Umar naye akapendekeza awe al-Habis ibn Aqra’a. Abu Bakar alimwambia Umar: “Naona unataka kunipinga.” Umar alimjibu ya kwamba hana lengo la kumpinga katu. Sauti zao za kupingana zilipaa juu, na hapo Aya hii ikateremka, ili kuwakataza wasinyanyue sauti zao mbele ya Mtume (s.a.w.w.)166
MAELEZO Kunyanyua sauti juu ya sauti ya Mtume (s.a.w.w.) ni moja kati ya mambo ya utovu wa nidhamu, kwani Mtume (s.a.w.w.) ana nafasi maalumu na heshima mahsusi katika jamii. Na hili ni jambo ambalo ni nadra kufanywa hata mbele ya mzazi au mwalimu, basi vipi iweje kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kufanyiwa hivyo!? Pia katika kulinda heshima ya Mtume (s.a.w.w.) haifai kumwita kwa kumkatisha jina, kama vile kusema: Ewe Muhammad, bali inatakiwa aitwe kwa kusema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Iwapo mtu anamwita Mtume (s.a.w.w.) kwa nanma hii iliyokatazwa kwa lengo la kumuudhi kwa makusudi, basi jambo hilo litakuwa ni ukafiri wa wazi na ni sababu ya kuporomoka kwa matendo yote mema. Katika Aya zilizopita tumezungumzia kwa kina namna matendo mema yanavyoporomoka kwa kukosa thawabu, jambo hili pia nalo ni moja kati ya mambo yanayoporomosha matendo mema. Kwa hiyo kuna haja kubwa sana ya kuchunga ndimi zetu wakati tunapozungumza kuhusiana na Nabii wetu Muhammad (s.a.w.w.) ili matendo yetu yasije yakapotea bure. Unyanyuaji wa sauti unaokatazwa mbele ya Mtume (s.a.w.w.) ni ule wenye kupelekea kumuudhi, ama unyanyuaji wenye maslahi kwa watu hauna matatizo yoyote, kwani baada ya kuteremka Aya hii, Thabit bin Qays ambaye alikuwa ni 166
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 16, Uk. 509 326
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 326
12/8/2014 2:43:47 PM
WITO KWA WAUMINI
khatibu wa Mtume (s.a.w.w.), mtu huyo alikuwa na kawaida ya kunyanyua sauti wakati anapokhutubia, alisema: “Mimi ndiye niliyenyanyua sauti mbele ya Mtume (s.a.w.w.), kwa hiyo matendo yangu yameporomoka, na mimi ni mtu wa motoni… habari ilipomfikia Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yeye ni katika watu wa Peponi.” Bila shaka Mtume (s.a.w.w.) alisema hivyo kwa kujua kwamba sauti aliyokuwa akiinyanyua ilikuwa ni sauti ya haki, sauti ya ulinganiaji wa Dini ya Mwenyezi Mungu. Mfano mwingine ni pale Ibn Abbas aliponyanyua sauti yake baada ya kuamrishwa na Mtume (s.a.w.w.) kuwaita wale waliokimbia katika vita vya Uhud, ili warejee katika uwanja wa mapambano. Aya inayofuata inaonesha umuhimu wa kushusha sauti mbele ya Mtume (s.a.w.w.) na namna Mwenyezi Mungu atakavyowalipa watu hao: “Kwa hakika ambao wanateremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amezitia mtihani nyoyo zao kwa takua. Hao watakuwa na maghufira na ujira mkubwa.” Katika Aya hii kuna ibara isemayo: “Kwa hakika ambao wanateremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Na katika Aya iliyotangulia kuna ibara isemayo: “Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii.” Ibara hizi mbili zinaashiria ya kwamba mtu huyu ambaye baadhi ya watu wanamkosea adabu ni Nabii wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kwa hiyo kumvunjia heshima ni sawa na kumvunjia heshima Mwenyezi Mungu, na kumheshimu yeye ni kumuheshimu Mwenyezi Mungu. Watu wanaomuwekea heshima Mtume (s.a.w.w.) hufanya hivyo kwa sababu wametambua nafasi yake na cheo chake kwa Mwenyezi Mungu, kutokana na utambuzi huo, Mwenyezi Mungu huzitakasa na kuzisafisha nyoyo za watu hao kwa maji ya uchamungu na hupata msamaha Wake na hatimaye kulipwa malipo makubwa yasio na kifani. Aya ya mwisho inaashiria ujinga wa wale wanaoziweka nyuma ya migongo yao amri za Mwenyezi Mungu, na kutotambua utukufu wa Mtume (s.a.w.w.): “Hakika ambao wanakuita nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili.” Ni akili gani inayomfanya mtu amwite kwa makelele mtu ambaye ametumwa na Mwenyezi Mungu, kama vile walivyofanya watu wa kabila la Bani Taminu pale walipomwita Mtume (s.a.w.w.) kwa sauti yenye kumkera kwa kusema: Ewe Muhammad, hebu toka uje huku! Kimsingi, kila akili ya mtu inapokuwa timamu hutambua kwa kiwango cha juu na kuwaheshimu wengine, hasa wale wenye utukufu kwa Mwenyezi Mungu, na kumkosea mtu adabu ni dalili ya ukosefu wa akili.
327
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 327
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
UTAFITI Katika Aya zilizotangulia tunajifunza ni namna gani Uislamu unavyotufunza juu ya kuwaheshimu wale walio na nafasi muhimu katika jamii, hasa ikiwa watu hao ni wale walioteuliwa na Mwenyezi Mungu katika kuwaongoa watu. Kwa kweli kuna riwaya mbalimbali zinazotilia mkazo juu ya suala zima la adabu na heshima kwa ujumla, miongoni mwa riwaya hizo ni kama zifuatazo: Anasema Imamu Ali a.s:
.األدب حللجدد “Adabu ni pambo ling’aralo daima.”167
Imamu as-Sadiq a.s: anasema:
ّ وما: قيل,خمس من لم تكن فيه لم يكن فيه مستمتع هن يا , وحسن الخلق, والحياء, والعقل, أل ّدين:ابن رسول اهلل؟ قال .وحسن األدب “Asiyekuwa na mambo matano, hawi ni mwenye furaha. Akaulizwa: Ni mambo gani hayo ewe mtoto wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Alijibu: Ni Dini, akili, haya, tabia nzuri na adabu nzuri.”168
Kunyanyua Sauti Kwenye Kaburi La Mtume (s.a.w.w.): Baadhi ya wanachuoni na wafasiri wa Qur’ani wanasema: Haifai kunyanyua sauti mbele ya Mtume (s.a.w.w.) wakati wa uhai wake na pia baada ya kifo chake. Ni wazi kwamba ikiwa unyanyuaji wa sauti katika kaburi lake ni unyanyuaji usio na faida na wenye kuonesha kutomwekea heshima, basi unyanyuaji huo haufai, kwani heshima ya mwanadamu inatakiwa ibakie hata baada ya kifo chake. Ama ule unyanyuaji wa sauti wenye kulenga katika kuwanufaisha watu, bila ya shaka ni unyanyuaji unaofaa na wenye baraka zake, kwani unyanyuaji wa aina hiyo pia ulifanyika mbele yake wakati wa uhai wake, na baadhi ya wakati ulikuwa ni kutokana na amri yake.
167 168
Rishahriy, Mizanul Hikma, Jz.1, Uk.53 Al-Majlisiy, Biharul Anwar, Jz.66, Uk.369 328
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 328
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI NA MOJA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ صيبُوا ِ ُاس ٌق ِب َن َبإٍ َف َت َبيَّنُوا أَ ْن ت ِ ين آ َمنُوا إِ ْن َجا َء ُك ْم َف َ ص ِب ُحوا َعلَىٰ َما َف َع ْلتُ ْم َنا ِد ِم ْ ين َو اعلَ ُموا أَ َّن ْ َُق ْو ًما ِب َج َهالَ ٍة َفت َ ُْك ْم ِفي َك ِثير ِم َن أ ُ ُطيع ُ ِف َ يك ْم َر ُس ال ْم ِر لَ َع ِن ُّت ْم ولكن ِ ول اللهَِّ لَ ْو ي ٍ ُ ان َو َزيَّ َن ُه ِفي ُقلُوب ُك ْم َو َك َّر َه إلَي ُ َّب إلَي ْْك ُم الإ ََّالله َ ْك ُم ْال ُك ْف َر م ي ب ح َ َ َ ِ ِ ِ ِ َٰ ُ َّلله ًا َ َ َو ْال ُف ُس ْ ون ف َ اش ُد َ ص َي َّ ان أول ِئ َك ُه ُم ْ وق َو ْال ِع ِ ضل ِم َن ا ِ الر َو ِن ْع َم ًة َواللهَُّ َعلِي ٌم َح ِكي ٌم “Enyi ambao mmeamini! Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda. Na jueni kuwa yuko kati yenu Mtume wa Mwenyezi Mungu. Lau angeliwatii katika mambo mengi, bila ya shaka mngelitaabika. Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezea Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na akauchukiza kwenu ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walioongoka. Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema Zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.” (Qur’ani: 49:6-8)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasiri wengi wanasema ya kwamba Aya hii iliteremka kwa Walid ibn Uqba. Ni pale alipotumwa na Mtume (s.a.w.w.) kwenda kukusanya Zaka katika kabila la Banil-Mustalaq. Walid alipokelewa kwa furaha kubwa, lakini kutokana na uhasama uliokuwepo katika zama za kijahilia kati ya Walid na watu hao, Walidi alidhani ya kwamba wanataka kumuua. Bila ya Walidi kuchunguza ukweli wa mambo alirejea kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia kwamba watu hao wamekataa kutoa Zaka. Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kupewa habari hizo, aliazimia kwenda kupambana nao kwani kitendo chao hicho ni ishara ya kutoka katika Uislamu (kuritadi). Baadhi ya wafasiri wameongezea kusema ya kwamba baada ya Walidi ibn Uqba kupeleka habari hizo, Mtume (s.a.w.w.) alimuamuru Khalid ibn Walid ibn Mughira aende kwa watu wa kabila la Banil-Mustalaq na asiwafanye lolote kabla ya 329
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 329
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
kuchunguza ukweli wa kauli ya Walidi ibn Uqba. Khalid aliwaendea na kufika huko usiku na aliwasambaza majajusi wake ili waangalie ukweli wa mbambo. Majajusi hao walirudi kwa Khalid na kumpasha habari ya kwamba watu hao ni Waislamu wa kweli na wamewasikia wakiadhini na kuswali. Wakati wa asubuhi Khalid naye akafanya upelelezi wake, aligundua ya kwamba yale waliyoyasema wapelelezi aliowatuma ni ya kweli, na baada ya hapo Khalid akarudi kwa Mtume (s.a.w.w.) na akamwambia yale aliyoyashuhudia huko, na hapo Aya hii ikateremka, na baada ya kuteremka Mtume (s.a.w.w.) alisema maneno yafuatayo:
.التّأني من اهلل والعجلة من الشيطان “Upole (kutokuwa na haraka ya mambo) unatoka kwa Mwenyezi Mungu na harakaharaka hutokana na shetani.”169
MAELEZO Aya inawataka Waumini wasiwe na haraka ya kuchukua hatua dhidi ya wengine, ikiwa chanzo cha habari hizo ni kutoka kwa mtu asiye mkweli, kabla ya kuchunguza ukweli wa kauli yake: “Enyi ambao mmeamini! Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni.” Kisha Aya inataja sababu ya kufanya uchunguzi: “Msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.” Lau kama Mtume (s.a.w.w.) angekubaliana na kauli ya Walid ibn Uqba na kuwaona watu wa kabila la Bani al-Mustalaq kuwa ni wenye kutoka katika Dini, na kuchukua hatua za kupambana dhidi yao, bila shaka ingekuwa janga kubwa la kibinadamu ambalo lingewashukia watu hao wasiokuwa na hatia yoyote ile! Katika Aya hii kuna ishara ya kwamba baadhi ya Maswahaba walikuwa wakitaka pachukuliwe hatua za kijeshi dhidi ya kabila la Bani al-Mustalaq, lakini Aya ikawaeleza ya kwamba jambo hilo ni la kijinga na hatima yake ni majuto. Katika Aya hii wataalamu wa elimu ya Usulul-Fiqhi wanaitolea dalili juu ya wajibu wa kushikamana na kauli ya mtu mmoja ikiwa mtu huyo ni mkweli na mwadilifu katika kauli zake, kwani Aya inaamrisha kufanya uchunguzi kwa habari ya mtu muovu, ama asiyekuwa na sifa hiyo hapahitajiki kufanya uchunguzi, maelezo zaidi yako katika vitabu vya elimu hiyo kwa yule anayehitaji kujua zaidi.
169
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 16, Uk. 524 330
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 330
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
UTAFITI Majuto Ni Mjukuu: Katika Aya hii kuna ibara isemayo: “Na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.” Ibara hii inaashiria ya kwamba suala la watu kuzua uongo kwa wengine ni jambo lililoota mizizi tangu enzi na enzi, na kurithiwa na wakoloni na madikteta mbalimbali ili kutengeneza mazingira ya kuwahadaa watu wajinga kwa lengo la kupora utajiri wao na rasilimali zao. Walikuja na ahadi mbalimbali zenye mvuto kwa wananchi, lakini hatima yake walioneemeka ni watu wa familia zao na nchi zao, kwani hadi sasa pamoja na kuambiwa nchi hizo ni huru bado zinachangia katika uchumi wa nchi za Kimagharibi kwa mbinu mbalimbali, kama vile uwekezaji, biashara huru, utandawazi, demokrasia n.k. Lau kama Waislamu wangekuwa ni watekelezaji wa amri za Mola Wao, ikiwemo ile iliyomo katika Aya hii, basi wasingekuwa katika hali hii ya unyonge na udhalili, kwani wangetambua hadaa wafanyiwazo na nchi za Magharibi! Aya inayofuata inatilia mkazo juu ya maudhui ya Aya iliyopita, inasema: “Na jueni kuwa yuko kati yenu Mtume wa Mwenyezi Mungu. Lau angeliwatii katika mambo mengi, bila ya shaka mngelitaabika.” Aya hii inakusudia kuwaambia wale waliokuwa na azma ya kupambana dhidi ya watu wa kabila la Bani al-Mustalaq baada ya Walid kupeleka habari ya uongo kwa Mtume (s.a.w.w.) ya kwamba wao ni watu wenye bahati kubwa kwa kuwa pamoja na Mtume (s.a.w.w.) akiishi nao, ni mtu ambaye ana mafungamano na Mwenyezi Mungu kwa kumshushia Wahyi, kwa hivyo kama kuna jambo lolote ni vyema kurudi kwake kabla ya kuchukua hatua, hasa ikiwa kuna jambo ambalo litapelekea kumwagika damu za wengine, basi wasitarajie kukubaliwa kila wanalotaka kulifanya, kwani Mtume (s.a.w.w.) ni mtambuzi zaidi juu ya manufaa ya wanadamu. Aya inaendelea kutaja vipawa vyingine walivyopewa watu hao: “Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezea Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na akauchukiza kwenu ukafiri, na upotovu, na uasi.” Maneno haya ya Mwenyezi Mungu ni ishara ya ukarimu Wake kwa wale wanaotaka kuongoka, kwani kila mwenye azma hiyo Mwenyezi Mungu humtayarishia mazingira ya kufikia lengo lake hilo, kwani siku zote Mwenyezi Mungu anapenda kuwaona waja Wake wanachagua na kufuata njia ya haki wao wenyewe pasi na kutenzwa nguvu, na ndio maana akawapelekea Mitume waliokuwa na Vitabu vitakatifu kutoka Kwake Yeye Mwenyezi Mungu. Kimaumbile nafsi ya mwanadamu inapenda imani sahihi, usafi wa moyo na uchamungu na kuchukia ukafiri na mambo maovu, lakini kinachowafanya watu 331
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 331
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
wengi kumuasi Mwenyezi Mungu ni kutokana na malezi wanayolelewa na jamii inayowazunguka. Ibara ya mwisho kabisa katika Aya hii inasema: “Hao ndio walioongoka.” Inakusudiwa kwamba, ikiwa watu wataweza kulinda na kuhifadhi vipawa hivi vinavyotoka kwa Mwenyezi Mungu (hali ya kimaumbile ya kupenda imani na kuchukia ukafiri), bila shaka yoyote ile watu hao wataufikia uongofu sahihi wa Mwenyezi Mungu. Aya ya mwisho itokayo kwamba hali ya kinafsi ya kupenda imani sahihi na kuchukia ukafiri ni vipawa na tunzo itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake wote: “Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema Zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.” Kwa hekima zake na elimu yake imempelekea kuviambatanisha vitu hivyo katika nyoyo za wanadamu ili iwe ni njia ya kufikia lengo la kuumbwa kwao na kupata malipo makubwa aliyowaaandalia wale wenye kufaidika navyo.
332
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 332
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI NA MBILI
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ى أَ ْن َي ُكونُوا ٰ ين آ َمنُوا اَل َي ْس َخ ْر َق ْو ٌم ِم ْن َق ْو ٍم َع َس َّ ْرا ِم ْنه ُن َو اَل ً ْرا ِم ْن ُه ْم َو اَل ِن َسا ٌء ِم ْن ِن َسا ٍء َع َسىٰ أَ ْن َي ُك َّن َخي ً َخي ْ َ ْأ ْ ُ َُ ُ س اِال ْس ُم ْال ُف ُس وق َب ْع َد َ اب ِب ْئ ِ َتل ِم ُزوا أ ْنف َسك ْم َو اَل َت َنا َب ُزوا ِبالل َق َّ الإْ ي َمان َو َم ْن لَ ْم َيتُ ْب فأوالئك ُه ُم َ الظالِ ُم ون ِ ِ “Enyi ambao mmeamini! Kaumu isidharau kaumu nyingine, huenda wakawa bora kuliko wao; wala wanawake kwa wanawake wengine, huenda wakawa bora kuliko wao. Wala msitiane kasoro, wala msibezane kwa majina, ni uovu kutumia jina baya baada ya imani. Na wasiotubu, hao ndio madhalimu.” (Qur’ani: 47:11)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasiri wamesema kwamba Aya hii ina sababu zaidi ya moja zilizopelekea kuteremka kwake. Kuhusiana na ibara isemayo: Enyi ambao mmeamini! Kaumu isidharau kaumu nyingine, huenda wakawa bora kuliko wao.” Iliteremka kutokana na Thabit ibn Qaysi, ambaye alikuwa khatibu wa Mtume (s.a.w.w.). Thabit bin Qaysi alikuwa na tatizo la usikivu, ilikuwa ni kawaida yake anapoingia msikitini hukaa pembezoni mwa Mtume (s.a.w.w.) ili apate kumsikia vizuri. Siku moja alichelewa kuingia msikitini huku watu wakiwa wameshamaliza kuswali na kila mmoja amekaa sehemu yake. Wakati alipokuwa anaingia alikuwa akiwapembua watu waliokaa na huku akisema: “Sogeeni.” Alifika kwa mtu mmoja na kumwambia: Kaa hapa,hii hapa nafasi yako, Thabit alikaa huku akiwa amekasirika, akamuuliza yule mtu: “Wewe ni nani?” Yule mtu akamjibu: “Mimi ni fulani ibn fulani, (alitaja jina lake na la baba yake).” Thabit akamwambia: “Wewe ni fulani mtoto wa mwanamke fulani (alitaja jina la mama yake badala la baba yake).” Yule mtu kusikia hivyo aliona aibu na kuinamisha kichwa chake, hapo ibara hii ikateremka kwa lengo la kuwakataza Waislamu tabia hiyo. Ama ibara isemayo: “Wala wanawake kwa wanawake wengine, huenda wakawa bora kuliko wao.” Inasemwa ya kwamba iliteremka kutokana na baadhi
333
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 333
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
ya wanawake kumfanyia dharau Ummu Salama; Mmoja kati ya wake wa Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu alikuwa akivaa nguo maalumu, au kutokana na ufupi wa kimo aliokuwa nao. Sehemu hii ya Aya iliteremshwa kwa lengo la kukatazwa mwenendo wao huo.170
MAELEZO Dharau na kejeli ni miongoni mwa mambo yasiyokubalika kabisa katika Uislamu. Tukirudi nyuma kidogo na kuangalia Aya mbili zilizoitangua Aya hii tunaona ni namna gani Uislamu ulivyoweka utaratibu wa upatanishi pale Waislamu wanapozozana, na kama ikiwa baadhi ya kikundi kitakataa suluhu basi kinatakiwa kiadhibiwe, hiyo ni kutokana na Uislamu kutambua ya kwamba Waumini ni ndugu na si marafiki tu. Aya hii tunayoichambua hapa inatoa kinga ya kuzuia mizozo na magomvi ndani ya jamii ya Kiislamu kwa kusema: “Enyi ambao mmeamini! Kaumu isidharau kaumu nyingine, huenda wakawa bora kuliko wao; wala wanawake kwa wanawake wengine, huenda wakawa bora kuliko wao.” Mwenyezi Mungu anawataka Waumini, wake kwa waume kuacha kudharauliana, kukejeliana, kufanyiana istihzai na kila jambo lenye kumuudhi mwingine, kwani mambo haya ni chanzo kikubwa cha vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyosababisha umwagikaji mkubwa wa damu za watu wasio na hatia. Mara nyingi suala la dharau kwa wengine husababishwa na baadhi ya watu pale wanapojiona wanamiliki baadhi ya vitu kuliko wengine, kama vile mali, au kuona ana sura nzuri kuliko wengine au anatokana na kabila fulani au kujiona ana elimu zaidi kuliko wengine. Ama Uislamu unaangalia na kupima ubora wa mtu kutokana na uchajiMungu unaofungamana na usafi wa moyo, utakaso katika ibada, unyeyekevu na tabia nzuri. Pamoja na hayo, haifai kusema ya kwamba yeye ni bora kuliko wengine, kwani kufanya hivyo ni kuwadharau wengine, kwani kujikweza ni miongoni mwa tabia mbaya sana ambayo husababisha madhara katika jamii. Aya inaendelea kusema: “Wala msitiane kasoro.” Hali hii ya kutiana kasoro hujitokeza pale baadhi ya watu wanapoanza kufuatilia habari za wengine, namna wanavyoishi kwa lengo la kutafuta kasoro na kuzitangaza kwa wengine. Ibara ifuatayo inasema: “Wala msibezane kwa majina.” Katika zama zilizopita na kuendelea hadi katika zama zetu hizi kuna baadhi ya watu wenye tabia ya kuwaita watu wengine majina yenye kuwachukiza, majina ambayo huharibu utu wao. Na baya zaidi ni pale mtu aliyekuwa amepewa jina baya kutokana na matendo yake maovu na jina hilo 170
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.16, Uk.524 334
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 334
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
kuendelea kuitwa hata baada ya yeye kutubia! Kwa kweli Uislamu umekemea vikali tabia hii mbaya ambayo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea dharau na kejeli kwa wengine. Kuna kisa kimoja kinachomuhusu Bibi Safiya aliyekuwa mke wa Mtume (s.a.w.w.). Bibi Safiya alikuwa ni mtu mwenye asili ya kiyahudi. Baada ya kusilimu na kuolewa na Mtume (s.a.w.w.), siku moja alikutwa na Mtume (s.a.w.w.) akilia. Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza sababu ya kilio chake, alijibu: “Hakika Aisha ananitia kasoro kwa kuniita, ewe binti wa Kiyahudi.” Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: Kwanini hukumwambia: “Baba yangu ni Harun na ami yangu ni Musa na mume wangu ni Muhammad.” Kama tulivyotangulia kusema ya kwamba tukio hili ni miongoni mwa sababu za kuteremka Aya hii. Hivyo basi si sawa kuendelea kumwita mtu aliyeingia katika Uislamu kwa majina yale yanayonasibiana na itikadi yake ya zamani kama Aya inavyoendelea kusema: “Ni uovu mkubwa baada ya imani.” Aya inahitimisha kwa kusema: “Na wasiotubia, hao ndio madhalimu.” Yeyote ambaye hatorudi kwa Mwenyezi Mungu kwa kutubia makosa yake baada ya katazo hili, na badala yake akaendelea kuwadharau Waumini, kuwakejeli, kuwaita majina mabaya yenye kuwakera, hiyo itakuwa ni dhulma kubwa aitendayo dhidi yao. Kuna dhulma gani iliyo kubwa kama hii ya kuutibua moyo wa Muumini, moyo ambao ni chimbuko la mapenzi ya mja kwa Mola Wake! Dhulma ambayo inachafua jina la mtu na kuvunja utu wake na kusababisha aibu katika uso wake! Kwa hiyo milango ya toba iko wazi kwa kila apendaye kufanya hivyo, ili kujinasua na udhalimu huu wenye kumchukiza Mwenyezi Mungu Mtukufu.
335
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 335
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI NA TATU
َّ ْض َّ يرا ِم َن َ الظ ِّن إِ َّن َبع َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ الظ ِّن إِ ْث ٌم ً اج َت ِنبُوا َك ِث ْ ين آ َمنُوا ً ْض ُك ْم َبع ُ َو اَل َت َج َّس ُسوا َو اَل َي ْغ َت ْب َبع ُح ُّب أَ َح ُد ُك ْم أَ ْن َي ْأ ُك َل ِ ْضا أَي ٌ لَ ْح َم أَ ِخي ِه َمي ًْتا َف َك ِر ْهتُ ُمو ُه َواتَّ ُقوا اللهََّ إِ َّن اللهََّ َت َّو اب َر ِحي ٌم “Enyi ambao mmeamini! Jiepusheni na dhana nyingi. Hakika baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipeleleze, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je, anapenda mmoja wenu kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani: 49:12)
SABABU YA KUTEREMKA Aya hii iliteremka kutokana na Maswahaba wawili wa Mtume (s.a.w.w.) kumsengenya Salman al-Farisy na Usamah ibn Zaydi. Hiyo ni kutokana na Maswahaba hao kumtuma Salman kwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) ili awapatie chakula, Mtume (s.a.w.w.) alimuagiza aende kwa Usamah ambaye katika zama hizo alikuwa na dhamana ya hazina ya mali za Waislamu. Usama alimwambia Salman: “Hivi sasa hakuna chakula ndani ya hazina…,” Basi wale Maswahaba wawili walimsema Usamah kwa kudai kwamba yeye ni bahili, na wakasema kuhusiana na Salman: “Lau tungemtuma kutuletea maji kutoka katika kisima cha Samiha maji yake yangekauka (Kisima cha Samiha kilikuwa na maji mengi sana).” Baada ya hapo waliondoka kuelekea kwa Usamah kwa lengo la kumfanyia ujajusi. Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia: “Mimi naona alama za kula nyama katika vinywa vyenu.” Wakasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sisi hatujala nyama leo.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Nyinyi mmekula nyama ya Salman na Usamah.” Hapo Mwenyezi Mungu akaiteremsha Aya hii kwa lengo la kuwakataza Waislamu kusengenya.171
171
Kitabu kilichotangulia, Uk. 545 336
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 336
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO Aya hii ni mwendelezo wa kinga dhidi ya mizozo katika jamii. Katika Aya iliyopita tumeona ni mambo gani yanayosababisha mizozo na kupelekea mapigano, sasa hapa Mwenyezi Mungu anatupa kinga nyingine ili tuweze kujenga jamii iliyo bora na yenye kupendana, anaanza kwa kusema: “Enyi ambao mmeamini! Jiepusheni na dhana nyingi. Hakika baadhi ya dhana ni dhambi.” Makusudio ya dhana nyingi ni zile dhana ambazo huonekana ni nzuri kwa mtazamo wa watu walio wengi. Kimsingi dhana za aina hii si kama zinakatazwa, kama ilivyokuja katika Aya ya 12 ya Suratun-Nuur:
ًات بأَ ُنف ِسه ْم َخيْرا ْ ون َو ْالم ْ لو ال إِ ْذ َس ِمعْتُمُو ُه َظ َّن ْالم َ ُُؤ ِمن ِ ِ ُ ُؤ ِم َن
“Mbona mliposikia (habari) hii, wanaume Waislamu na wanawake Waislamu hawakuwadhania wenzao mema…”
Lakini kilichokatazwa ni dhana nyingi ambazo baadhi yake huwa si sahihi: “Hakika baadhi ya dhana ni dhambi.” Ikiwa kutakuwa na mchanganyiko kati ya dhana sahihi na zile zisizo sahihi, jambo analotakiwa Muumini ni kujiepusha nazo zote kwani hajui ni ipi iliyo sahihi, kwa vile huandikiwa dhambi kwa kila anayemdhania mwenzake dhana mbaya. Kuhusiana na suala la dhana kuna suala linaloweza kujitokeza, ni kwa nini imekatazwa kudhania na wakati dhana ni jambo la kinafsi ambalo halimo katika udhibiti wa mwanadamu? - Jawabu la suala hili tunaweza kulijibu kama ifuatavyo: 1.
Kilichokatazwa ni kule kuchukua maamuzi yanayotokana na dhana, kwa hivyo haifai mtu kuchukua hatua na maamuzi kutokana na dhana iliyoko akilini mwake. Kwa hiyo kosa ni kule kuchukua maamuzi kwa mujibu wa dhana. Ndio maana Mtume (s.a.w.w.) akasema:
ّ وله,ثالث في المؤمن اليستحسن فمخرجه من,منهن مخرج ّ سوء ّ أال ّ الظ ّن ...يحققه “Haipendezi kwa Muumini kuwa na mambo matatu, kwani kuna (njia) ya kuepukana na mambo hayo, kuepukana na dhana mbaya ni kutoitolea maamuzi…”172 172
Shahrudiy, Mustadraku Safinatil Bihar, Jz. 7, Uk. 38 337
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 337
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
2.
Mwanadamu anaweza kujiepusha na dhana mbaya kwa kufikiria dhana nyingine inayokwenda kinyume nayo, kama vile kufikiria kutotenda tendo hilo, ikiwa mtu anadhaniwa kutenda jambo baya, kwa kufanya hivi hali hiyo itaondoka kidogokidogo na hatimaye kwisha kabisa. Hivi ndivyo Uislamu unavyotufunza kama ilivyopokelewa kutoka kwa Imamu Ali (a.s.) akisema:
وال,ضع أمر أخيك على أحسنه حتّى يأتيك ما يغلّبك منه تظنّن بكلمة خرجت من أخيك سوءا وأنت تجد لها في الخير .محمال “Liweke jambo la ndugu yako katika hali iliyo nzuri zaidi, mpaka ikujie yakini itakayobadilisha mawazo yako, na wala usidhanie vibaya kutokana na kauli itokayo kwa ndugu yako, na hali unaweza kuipatia ufumbuzi mzuri.”173
Kwa hiyo Uislamu unatutaka tuwadhanie wengine dhana nzuri, kwani kuna madhara makubwa anayoyapata mtu mwenye tabia ya kuwadhania wengine dhana mbaya, kama anavyosema Imamu Ali (s.a):
ّ من لم يحسن ظنّه استوحش من .كل أحد “Asiye na dhana nzuri hujitenga na kila mtu.”174
Vyovyote vile, mafunzo haya ni moja kati ya mambo yanayojenga mafungamano ya watu katika jamii na kuwafanya waishi kwa upendo kati yao. Aya inaendelea kusema: “Wala msipeleleze.” Katazo hili ni katika mambo yaliyomo katika uwezo wa mwanadamu mwenyewe, yeye ndiye mwamuzi wa kutenda hili au kutolitenda, ni tofauti na suala la dhana kama tulivyotangulia kusema, ya kwamba ni jambo la kinafsi ambalo haliko katika milki ya mwanadamu. Kwa hakika dhana mbaya ndio chanzo kikubwa kinachopelekea ujasusi na upelelezi wa habari za watu ambazo kikawaida zinatakiwa ziwe katika hali ya faragha. Uislamu hauruhusu kufichua siri za watu, na badala yake unataka kila mtu awe katika hali ya amani katika maisha yake. Na lau kama Uislamu ungeruhusu kila mtu kufanya kazi ya ujasusi kwa wengine, bila shaka heshima za watu zingeondoka 173 174
Hurrul Amily, Wasailu Shia, Jz. 12, Uk. 302 Rishahriy, Mizanul Hikma, Jz. 2, Uk.1787 338
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 338
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
na hali ya maisha ya watu ingekuwa ni ya wasiwasi na kutoaminiana. Pamoja na katazo hili, haimaanishi kutokuwepo kitengo maalumu cha upelelezi cha serikali ya Kiislamu kinachohusika na usalama wa nchi na watu wake, lakini kitengo hicho hakina haki ya kupeleleza maisha binafsi ya watu. Aya inamalizia kwa kueleza katazo la mwisho kwa kusema: “Wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi.” Dhana mbaya ni sababu ya ujasusi, na ujasusi hupelekea kuibua aibu za watu, na hapo inaanza shughuli za kusengenya. Uislamu unakataza mambo haya yote. Katika kuonesha ubaya wa usengenyaji, Aya ineleza hilo kwa kutumia mfumo uliojaa fasihi ya hali ya juu, inasema: “Je, anapenda mmoja wenu kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo!” Bila shaka heshima ya Mwislamu na utukufu alionao ni kama nyama ya mwili wake, na kule kuvunjiwa heshima na kuaibishwa katika jamii ni sawa na kuila nyama yake! Mtu anayesengenywa huwa yuko mbali na msengenyaji. Ni kama mfano wa mtu aliyefariki, ambaye anakuwa hana uwezo wowote wa kujitetea kwa lolote lisemwalo dhidi yake, hivyo kutokana na kutokuwepo wakati panapotajwa aibu zake ni sawa na maiti, ambaye hawezi kujitetea, hiyo ndio sababu Mwenyezi Mungu akauliza: “Je, anapenda mmoja wenu kuila nyama ya nduguye aliyekufa?” Bila shaka tashbihi hii inabainisha ubaya wa hali ya juu na dhambi kubwa azipatazo msengenyaji. Kwa vile baadhi ya watu ni wenye kusibiwa na tabia ya kusengenya, basi inawapasa kurudi kwa Mola Wao haraka na kuomba msamaha kama Aya inavyohitimisha kwa kusema: “Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu” Kwanza hakuna budi kuishi katika hali ya uchamungu, kisha kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa kuomba msamaha. Kwa kufanya hivyo ndipo ambapo rehema za Mwenyezi Mungu zitawafunika waliokuwa wakikhalifu amri Zake. Kutokana na uzito na ubaya wa usengenyaji na kuchunguza stara za watu, Mtume (s.a.w.w.) anamzingatia mtu mwenye kutenda kosa hilo kuwa mbali na imani juu ya Uislamu, anasema:
يا معشر من آمن بلسانه ولم يؤمن بقلبه! التغتابوا المسلمين فإنّه من تتّبع عورة أخيه تتّبع اهلل,وال تتّبعوا عوراتهم .عورته ومن تتّبع اهلل عورته يفضحه في جوف بيته 339
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 339
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI “Enyi wale mlioamini kwa ndimi zao na wala hazikuamini nyoyo zao! Msiwasengenye Waislamu na wala msifuatilie siri zao, kwani mwenye kufuatilia siri za ndugu yake, Mwenyezi Mungu atazifuatilia siri zake, na ambaye siri zake zitafuatiliwa na Mwenyezi Mungu, atamfedhehesha ndani ya nyumba yake.”175
Pia imepokewa riwaya nyingine kwamba, Mwenyezi Mungu alimpelekea Wahyi Nabii Musa (a.s.) na kumwambia:
و من مات, من مات تائبا من الغيبة فهو آخر من يدخل الجنّة .مصرا عليه فهو أ ّول من يدخل النّار ّ “Mwenye kufariki hali ya kuwa ni mwenye kutubia kutokana na kusengenya, atakuwa mtu wa mwisho kuingia Peponi, na mwenye kufariki hali ya kuwa ni mwenye kusengenya, atakuwa wa mwanzo kuingia Motoni.”176
Tiba ya Usengenyaji Na Namna Ya Kutubia: Usengenyaji kama ilivyo kwa dhambi nyingine hubadilika hatua kwa hatua mpaka kugeuka na kuwa ugojwa wa kisaikolojia, kiasi cha kumfanya msengenyaji kusikia raha wakati anapomsengenya mtu. Kutokana na hali hii inapasa kwa msengenyaji kuchukua hatua za kuondosha sababu zinazopelekea kutenda kosa hili, miongoni mwa sababu hizo ni kama vile: Choyo, chuki, ubahili, majigambo, ubinafsi n.k. Hatua inayofuata ni kuitakasa nafsi yake na kufikiria adhabu kali iliyoandaliwa kwa wenye kusengenya, na achukue mazoezi ya kuulinda ulimi wake ili usije ukajiingiza tena katika dhambi hii kubwa, na baada ya hapo atubie toba ya kweli kwa kumuomba msamaha yule aliyemsengenya ikiwa ataweza kufanya hivyo. Ikiwa atahisi uzito au akiona akifanya hivyo itakuwa sababu ya kuamsha hisia za ugomvi, au ikiwa mwenye kusengenywa ameshafariki, basi amuombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu na kujilazimisha kufanya matendo mema, huenda Mwenyezi Mungu akamsamehe kutokana na baraka ya matendo mema.
175 176
Naraqiy, Jami’u Sa’dat, Jz. 2, Uk. 233 Al-Mirza Annuriy, Mustadrakul Wasail, Jz. 9, Uk. 126 340
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 340
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
Maeneo Yanayoruhusiwa Kusengenya: Kusengenya ni miongoni mwa madhambi makubwa yaliyokatazwa kupitia Aya mbali mbali pamoja na riwaya za Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu watoharifu watokanao na nyumba ya Mtume (s.a.w.w.), lakini kanuni hii ni kama kanuni nyingine za Kiislamu. Kuna pahala inaruhusika kutumika, miongoni mwake ni kama vile wakati mtu anapotaka ushauri kwenye ndoa au kushirikiana na mtu fulani katika biashara, hapo sheria inamlazimu aliyetakiwa ushauri kuelezea uhalisia wa mtu hata kama ana aibu fulani anatakiwa azitaje, lakini la kuzingatia ni kueleza kiwango kinachohitajika tu. Pia mtu ambaye humuasi Mwenyezi Mungu waziwazi, kiasi cha kuwa mashuhuri katika uasi wake, hakuna ubaya wowote kutaja aibu za mtu wa aina hiyo. Kama vile ambavyo kusengenya ni haramu, pia kusikiliza ni haramu, kwa hivyo tujikinge na aina zote mbili ili tusalimike na adhabu ya Mwenyezi Mungu.177
177
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 16, Uk. 558 341
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 341
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI NA NNE
ََّيا أَُّي َها ال َُؤ ِت ُك ْم ِك ْفل ََّين آ َمنُوا اتَّ ُقوا الله ُ ْ َ ْن ِم ْن ي ي ه ل و س ر ب وا ن م آ و ذ ُ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ َُّلله َ ورا َت ْم ُش ور ٌ ون ِب ِه َو َي ْغ ِف ْر لَ ُك ْم َوا َغ ُف ً َُر ْح َم ِت ِه َو َي ْج َع ْل لَ ُك ْم ن ْ ُ َ َ َّا ْ ون َعلَىٰ َش ْي ٍء ِم ْن َف َ اب أَ اَّل َي ْق ِد ُر ض ِل ِ َر ِحي ٌم لَِئل َيعْل َم أ ْهل ال ِك َت ْ ضل ْ ُؤ ِتي ِه َم ْن َي َشا ُء َواللهَُّ ُذو ْال َف ْ اللهَِّ َوأَ َّن ْال َف ْ ض َل ِب َي ِد اللهَِّ ي يم ظ ع ال َ ِ ِ ِ “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na mwaminini Mtume Wake, atawapa sehemu mbili katika rehema Yake, na atawajaalia muwe na nuru ya kwenda nayo, na atawaghufiria. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu. Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uweza wowote juu ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Na fadhila zote zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye fadhila kuu.” (Qur’ani:57:28-29)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasiri wengi wamesema ya kwamba Aya hizi zimeteremka kutokana na sababu ifuatayo: Mtume (s.a.w.w.) alimpeleka Ja’far ibn Abi Talib kwa mfalme wa Najashi (Ethiopia) ili amlinganie kwenye Uislamu. Ja’far alikuwa amefuatana na watu sabini, wote wakiwa wamepanda wanyama. Najashi alikubali kuingia katika Uislamu. Wakati walipokuwa wanaondoka, baadhi ya watu wa Ethiopia waliokuwa wameamini pamoja na Najashi walisema: “Turuhusu tuje tumsalimie huyo Mtume (Mtume Muhammad (s.a.w.w.)).” Ja’far alikubali, na watu hao waliondoka pamoja nao. Walipofika Madina waliwaona Waislamu namna walivyokuwa wakarimu wa hali ya juu, waliomba ruhusa na kusema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi tuna mali nyingi, na tumewaona Waislamu namna walivyo na ukarimu wa hali ya juu, tunaomba uturuhusu tuondoke ili tukalete mali zetu ili nasi tuwakirimu Waislamu.” Mtume (s.a.w.w.) aliwaruhusu, walikwenda na kisha wakarudi na mali na wakawapa Waislamu. Hapo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya zifuatazo:
342
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 342
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
ْ اه ُم َّال َون َوإ َذا ي ُْتلَىٰ َعل َ ُ َ َ َ ْ ْ ُ ُ َ َ ْ ْ ْه ْم ي ن م ُؤ ي ه ب م ه ه ل ب ق ن م اب ت ك ال ن ي ت آ ين ذ َ ْ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ُ َ َقالُوا آ َمنَّا ِب ِه إِنَّ ُه ْال َح ُّق ِم ْن َربِّ َنا إِنَّا كنَّا ِم ْن َق ْبلِ ِه ُم ْسلِ ِم ين أوالئك َ ْي َ ص َب ُروا َو َي ْد َر ُء السيِّ َئ َة َّ ون ِب ْال َح َس َن ِة َ ْن ِب َما ِ ُؤ َت ْو َن أ ْج َر ُه ْم َم َّر َتي ُ َو ِم َّما َر َز ْق َن َ اه ْم يُ ْن ِف ُق ون “Wale tuliowapa Kitabu kabla yake wanakiamini hiki. Na wanaposomewa wanasema: Tunaiamini. Hakika hii ni Haki inayotoka kwa Mola Wetu Mlezi. Hakika sisi kabla yake tulikuwa ni Waislamu tulionyenyekea. Basi hao watapewa ujira wao mara mbili kwa walivyovumilia, na wakaondoa ubaya kwa wema, na wakatoa katika tuliyowaruzuku.” (Qur’ani: 28:52-54)
Wale watu waliopewa Kitabu waliposikia ibara ya Aya isemayo: “Basi hao watapewa ujira wao mara mbili kwa walivyovumilia,” waliwaelekea Waislamu na kuwaambia: Enyi Waislamu! Yule aliyeamini Kitabu chenu na Kitabu chetu (Injili) malipo yao ni sawasawa, basi nyinyi mna ubora gani zaidi kuliko sisi? Hapo ndipo Aya hizi zikateremka: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na mwaminini Mtume Wake, atawapa sehemu mbili katika rehema Yake, na atawajaalia muwe na nuru ya kwenda nayo, na atawaghufiria. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu. Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uweza wowote juu ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Na fadhila zote zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye fadhila kuu.” Aya hizi ziliteremka ili kuonesha tofauti ya malipo kati yao.178
MAELEZO Kwa kuanzia, Aya inasema: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na mwaminini Mtume Wake.” Wafasiri wametofautiana kuhusiana na mhutubiwa wa Aya hii. Wako wanaosema wahutubiwa ni Waumini, ikiwaeleza ya kwamba imani ya kijuujuu haitoshi kwa mtu, bali ni kuwa na imani thabiti yenye kufungamana na uchamungu na matendo mema, ili waweze kupata malipo makubwa yaliyoandaliwa na Mwenyezi Mungu. Na wengine wanasema: Wahutubiwa hapa ni wale waliopewa Kitabu, ambao wanaamini Vitabu vilivyotangulia pamoja na Mitume, wanatakiwa 178
Kitabu kilichotangulia, Jz. 18, Uk. 92 343
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 343
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
washikamane na uchamungu ili na wao wawe ni miongoni mwa watakaopata malipo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kauli iliyo sahihi zaidi ni kauli ya kwanza, kwani inanasibiana na sababu ya kuteremka kwa Aya hizi, kwa hiyo walengwa ni wale Waumini waliokuwa na udhaifu katika imani zao, kiasi cha kutofungamanisha imani zao pamoja na vitendo vyao, kwa hiyo Mwenyezi Mungu anawataka wawe Waumini madhubuti kwa kuonesha utekelezaji wa hali ya juu katika kila wanaloamrishwa na Mola Wao na kuachana na makatazo Yake. Aya inakamilisha kwa kutaja neema kubwa tatu watakazozipata Waumini wenye sifa ya kumcha Mwenyezi Mungu: “Atawapa sehemu mbili katika rehema Yake, na atawajaalia muwe na nuru ya kwenda nayo, na atawaghufiria. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” Wafasiri wameelezea maana ya ‘Kupewa sehemu mbili katika Rehema Yake’ ni kwamba watu hao watapata malipo mema ya dunia na ya akhera. Na baadhi wamesema ni ile hali ya mwendelezo wa malipo mema huku yakizidishwa mara kwa mara. Ama maana ya ‘Kufanywa kuwa na nuru wanayokwenda nayo’ ni nuru ya imani ambayo itakuwa inang’ara mbele ya Waumini kutokana na giza la Siku ya Kiyama, kama ilivyo katika Aya ifuatavyo:
َ َ ور ُه ْم َبي َ َي ْو َم َت َرى ْال ُم ْؤ ِم ِن يه ْم ُ ُنات َي ْسعى ن ِ ين َو ْال ُم ْؤ ِم ِ ْن أ ْي ِد …َو ِبأَيْما ِن ِه ْم “Siku utakapowaona Waumini wanaume na Waumini wanawake nuru yao inakwenda mbele yao...” (Qur’ani; 57:12)
Na baadhi ya wafasiri wamesema kwamba makusudio yake ni nuru ya Qur’ani ambayo inawaangazia Waumini hapa duniani, kama anavyosema Mwenyezi Mungu: “Hakika imekujieni nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Kitabu chenye kubainisha.” (Qur’ani; 5:15). Bila shaka Aya inamaana pana na wala malipo haya hayahusiani na hapa duniani tu, au akhera peke yake. Kwa maana nyingine ni kwamba imani thabiti na uchamungu wa hali ya juu huondosha vizuizi katika nyoyo za Waumini, kiasi cha kuwafanya kubainikiwa na uhalisia wa mambo bila ya kizuizi chochote kile. Malipo ya tatu ni kupata msamaha wa madhambi, kwani bila hili mwanadamu hawezi kupata neema yoyote kutoka kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, ikiwa atakuwa na madhambi, kwani neema Zake ni kwa wale waliosalimika na adhabu Yake na kisha kuangaziwa na nuru kutoka Kwake Mwenyezi Mungu. 344
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 344
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
Aya ya mwisho inayomalizia maudhui haya inasema: “Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uweza wowote juu ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Na fadhila zote zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye fadhila kuu.” Aya hii ni jawabu kwa baadhi ya Ahlulkitabi ambao walidhani kwamba wana malipo sawa na Waislamu licha ya kutokumwamini Mtume (s.a.w.w.). Ama wale waliomwamini Mtume (s.a.w.w.) miongoni mwao bila shaka wana malipo mara mbili: Malipo yanayotokana na kuamini Mitume iliyopita na malipo kwa sababu ya kumwamini Mtume (s.a.w.w.). Kwa hiyo hapa ina wajibu kwamba makusudio ya watakaopata malipo mara mbili ni Waislamu kwa kule kuamini kwao Mitume yote iliyotangulia na kumwamini Mtume (s.a.w.w.). Ama watu waliopewa Kitabu ambao wamekataa kumuamini Mtume (s.a.w.w.) hawana malipo yoyote kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na wanatakiwa watambue kwamba rehema za Mwenyezi Mungu haziko katika milki yao, hata waweze kumgawia wamtakaye wao na kumnyima wamtakaye. Pia Aya hii inabeba ujumbe kwa Mayahudi na Manasara kutokana na madai yao ya kwamba Pepo na Rehema nyingine za Mwenyezi Mungu hakuna atakayezipata isipokuwa wao tu, kama vile Mwenyezi Mungu alivyowanukuu wakisema:
َّ َوقالُوا لَ ْن َي ْد ُخ َل ْال َجنَّ َة إ َ ال َم ْن كان ُهوداً أَ ْو َنصارى ِت ْل َك ِ ُ ُ ُ َ ُرها َنك ْم إِ ْن ك ْنت ْم صا ِد ِق ين ْ أَما ِن ُّي ُه ْم ُق ْل هاتُوا ب “Na walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Yahudi au Mkristo. Hayo ni matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli.” (Qur’ani; 2:111).
UTAFITI Uchamungu Na Upambanuzi: Qur’ani Tukufu imeelezea faida mbalimbali zitokanazo na uchamungu, miongoni mwa hizo ni kuondoka vizuizi katika moyo na akili ya mwanadamu. Kuna Aya nyingi katikaQur’ani zinazoashiria kuwepo mafungamano ya imani na uchamungu pamoja na upambanuzi, miongoni mwa hizo ni Aya zifuatazo:
345
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 345
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
ًوا اللَهّ َي ْج َعل لَّ ُك ْم ُف ْر َقانا ْ وا إَن َتتَّ ُق ْ ُين آ َمن َ يا أَُّي َها الَّ ِذ “Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atakupeni kipambanuo…” (Qur’ani; 8:29)
Aya nyingine inasema:
ّللاَ َويُ َعلِّ ُم ُك ُم ه َّواتَّقُو ْا ه ُللا “… na mcheni Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atakufundisheni…” (Qur’ani; 2:282)
Kwa hakika imani thabiti itakapokita katika moyo wa mwanadamu huondosha vizuizi vya ujahili, ubinafsi, choyo n.k. na badala yake hujaa mwanga na kuweza kuijua haki kwa urahisi na kwa uhalisia wake. Ama imani yenye kuyumbayumba na kutingishwa na kila upepo uvumao, imani isiyo na uchamungu, imani hiyo haimsaidii mwanadamu kwa lolote, bali humwangamiza, anasema Imamu Ali (a.s.):
من اتّبع هواه أعماه, ال عقل مع هوى,ال دين مع هوى .وأص ّمه وأذلّه وأضلّه “Hakuna Dini pamoja na matamanio ya nafsi, hakuna akili pamoja na matamanio ya nafsi, mwenye kufuata matamanio ya nafsi yake humpofua na kumfanya kuwa kiziwi na humdhalilisha na humpoteza.”179
Haya ni malipo anayoyapata yule ambaye yuko mbali na uchamungu hata kama atadai ya kwamba anaamini kila kinachopasa kuaminiwa katika Dini. Imani yenye kumuokoa mwanadamu ni ile yenye kufungamana na uchamungu wa kweli.
179
Kitabu kilichotangulia, Uk. 98 346
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 346
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI NA TANO
ْ اج ْوا بالإْ ْثم َو ََّيا أَُّي َها ال َ ين آ َمنُوا إ ُ َا َ َ َ َ َ َ ْ َ ان و د ع ال ن ت ت ل ف م ْت ي اج ن ت ا ذ ذ ُ ْ َ َ َ ِ ِ ِ ِِ ِ َّ ْ َّلله اج ْوا ِبال ِب ِّر َوالتَّ ْق َوىٰ َواتَّ ُقوا ا َ ال ِذي َّ ْص َي ِت َ ول َو َت َن ِ َو َمع ِ الر ُس َ الشي َّ ى ِم َن ُإلَ ْي ِه ت َ َّ َّ َ ان لَِي ْح ُز َن الَّ ِذ َ ين آ َمنُوا ْط ٰ و ج الن ا م ن إ ون ر ش ح ُ ْ ْ َ َ ِ ِ ِ ْ ْ َّلله َّلله ْ َّ َّا َ َ ً َ ْس ِب َ ُار ِه ْم َشيْئا إِل ِبإِذ ِن ا ِ َو َعلى ا ِ َفل َي َت َوك ِل ال ُم ْؤ ِمن ون ِّ ض َ َولي “Enyi mlioamini! Mnaponong’onezana msinong’onezane kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumwasi Mtume. Bali nong’onezaneni kwa kutenda mema na takua. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye Kwake mtakusanywa. Kwa hakika minong’ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe walioamini; na wala hatawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani: 58:9-10)
SABABU YA KUTERMKA Aya hii inamafungamano na Aya iliokuja kabla yake, Aya hiyo inasema:
َ ين نُهُوا َع ِن النَّ ْج َوىٰ ثُ َّم َيعُو ُد َ أَلَ ْم َت َر إِلَى الَّ ِذ ون لِ َما نُهُوا َع ْن ُه ْ ْ ْلإ َ ول َوإ َذا َجا ُء وك َّ ْص َي ِت َ َو َي َت َن ِ ان َو َمع ِ اج ْو َن ِبا ِث ِم َوال ُع ْد َو ِ ِ الر ُس ُِّك ب ِه اللهَُّ َو َي ُقول َُّون ِفي أَ ْن ُف ِسه ْم لَ ْو اَل يُ َع ِّذبُ َنا الله َ َ َّو َك ب َما لَ ْم ي َ ِ ُحي ِ ْ َحي ِ ُ ب َما َن ُق ير ُ ص ْ ول َح ْسبُ ُه ْم َج َهنَّ ُم َي َ صلَ ْو َن َها َف ِب ْئ ِ س ْال َم ِ “Kwani huwaoni wale waliokatazwa kunong’ona, kisha wakayarudia yale waliyokatazwa, na wakanong’onezana juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumwasi Mtume? Na wakikujia hukuamkia sivyo anavyokuamkia Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa haya tuyasemayo? Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Ni marejeo mabaya sana.” (Qur’ani: 58:8) 347
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 347
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
Sababu ya kuteremka Aya hii ni kutokana na Mayahudi na wanafiki waliokuwa wakinong’onezana baina yao mbele ya Waislamu na huku wakiwaashiria Waislamu kwa macho yao, na kutokana na hali hiyo Waislamu walihuzunika na kukasirishwa, na wakapeleka malalamiko yao kwa Mtume (s.a.w.w.). Mtume (s.a.w.w.) aliwakataza wasinong’onezane mbele ya Waislamu, lakini hawakukatazika, waliendelea na kitendo chao hicho, na hapo Aya ikateremka ili kutilia mkazo ubaya wa kitendo chao hicho. Kwa vile mara nyingi Mayahudi na wanafiki walipokuwa wakinong’onezana walikuwa wakiwasema Waislamu, kwani walipokuwa wakifanya kitendo hicho walikuwa wakikonyezana kwa kuwaashiria Waislamu, Mwenyezi Mungu akawataka Waumini wanaponong’onezana wasinong’onezane kwa yale yenye madhara kati yao na wasipange mikakati ya kumpinga Mtume (s.a.w.w.) kwa yale anayowaamrisha, na badala yao wanong’onezane juu ya yale yenye manufaa kwa Dini yao na dunia yao: “Enyi mlioamini! Mnaponong’onezana msinong’onezane kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumwasi Mtume. Bali nong’onezaneni kwa kutenda mema na takua. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye Kwake mtakusanywa.” Katika Aya hii tunajifunza ya kwamba, Waislamu wanaponong’onezana wanawajibika kutopanga kutenda maovu na yale yanayowaudhi wengine, na wanong’onezane juu ya kuusiana mambo mema na wasiwe kama wanavyofanya Mayahudi na wanafiki. Aya ya mwisho inatoa onyo kwa wale wanaoendeleza minong’ono yenye madhara, inasema: “Kwa hakika minong’ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe walioamini; na wala hatawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu.” Hapa inapasa ieleweke kwamba shetani hawezi kumdhuru yeyote bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu angetaka asingempa uwezo wa kuwa na uamuzi wa kufanya wema na uovu kama alivyompa mwanadamu, kwani kila kitokeacho katika ulimwengu kiko katika uwezo wa Mwenyezi Mungu, hata uwezo wa moto kuunguza au upanga kuweza kukata, kilichobaki ni maamuzi ya mwanadamu kuzitumia neema hizi, ama kwa wema au kwa shari. Na njia ya kuepukana dhidi ya madhara ya shetani na vishawishi vyake viovu ni kumtegemea Mwenyezi Mungu peke Yake.
348
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 348
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
UTAFITI Aina Za Kunong’ona: Kunong’ona kumegawika sehemu tano kwa mujibu wa aina tano za hukumu za kisheria: Kwanza: Kunong’onezana kuliko haramu. Huku hupatikana ikiwa kutapelekea maudhi kwa wengine, kama Aya ilivyotangulia kuashiria. Pili: Kunong’onezana kuliko wajibu kama kutakuwa na jambo linalolazimu kunong’onwa, na kinyume chake ikiwa litazungumzwa bayana litasababisha madhara kwa Waislamu. Tatu: Kunong’onezana kunakopendeza, kama mtu kufanya wema na kumnong’oneza yule anayeujua ili ausitiri wengine wasijue. Nne: Kunong’onezana kunakochukiza. Tano:Kunong’onezana kuliko halali. Kimsingi ikiwa hakuna sababu yoyote ya msingi kunong’ona kunakuwa ni jambo lisilopendeza na kunaharibu heshima ya kikao, na shetani hupata nafasi ya kupandikiza chuki kwa wale ambao hawakushirikishwa katika kunong’ona, Mtume (s.a.w.w.) anasema:
ّ ,إذا كنتم الثالثة فال يتناجى إثنان دون صاحبهما .فإن ذلك يحزنه “Pindi mnapokuwa watu watatu, basi wawili wasinong’onezane na kumwacha mwenzao, kwani hilo linamuhuzunisha.”180
180
Muslim, Sahihu Muslim, Jz. 7, Uk. 13 349
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 349
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI NA SITA
ْ يل لَ ُك ْم َت َف َّس ُحوا ِفي ََّيا أَُّي َها ال َ ين آ َمنُوا إ َذا ِق َ س َف ْاف َس ُحوا ل ا ج م ال ذ َ َ ِ ِ ِ ِ َّ َُّلله َ َي ْف َسح اللهَُّ لَ ُك ْم َوإ َذا ِق َ يل ا ْن ُش ُزوا َفا ْن ُش ُزوا َي ْر َف ِع ا ال ِذ ين آ َمنُوا ِ ُ ِ ُ ْ ْ َّ َُّلله ُ َ َ َ ات َوا ِب َما ت ْع َمل َ ِم ْن ُك ْم َوال ِذ ير ٌ ون خ ِب ٍ ين أوتوا ال ِعل َم َد َر َج “Enyi mlioamini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika vikao, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atawafanyia nafasi. Na mkiambiwa: ondokeni, basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua daraja walioamini miongoni mwenu, na waliopewa ilimu. Na Mwenyezi Mungu kwa mnayoyatenda anazo habari.” (Qur’ani; 58:11)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasiri wanasema kwamba Aya hii iliteremka siku ya Ijumaa wakati Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa katika sehemu iliyokuwa inajulikana kwa jila la Swaffa, akiwakirimu wale walioshiriki vita vya Badri miongoni mwa Muhajirina na Maansari. Mara wakaja wapiganaji wengine ambao walichelewa kikaoni. Walipofika walisimama na kumsalimia Mtume (s.a.w.w.) na Mtume (s.a.w.w.) akawarudishia salamu yao, kisha wakawasalimia wale waliotangulia, na wao wakawarudishia salamu, bado wakawa katika hali ile ya kusimama huku wakisubiri wafanyiwe nafasi ya kukaa. Mtume (s.a.w.w.) alifahamu kwamba watu hao walichoka kusimama. Alipita katika safu na kuwataka wale waliokaa ambao hawakushiriki katika vita wasimame na wawape nafasi wale walioshiriki vita, lakini wengine walichukizwa na kitendo hicho cha Mtume (s.a.w.w.), mpaka wale waliokuwa na ugonjwa katika nafsi zao (wanafiki) wakasema: “Je, nyinyi si mnadai ya kwamba swahiba wenu huyu ni mwadilifu kati ya watu? Tunaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, hatujaona uadilifu wowote aliowafanyia watu hawa! Watu wamechukua nafasi zao kwa kupenda kukaa karibu na Mtume wao, amewainua na kuwaweka wale waliochelewa.” Wakati Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akiwataka watoe nafasi kwa wengine alikuwa akiwaambia: “Mwenyezi Mungu amrehemu mtu ambaye hutoa nafasi kwa ajili ya ndugu yake.” Ikawa wale wenye imani madhubuti wanaondoka kwa haraka sana na kuwapa nafasi wahusika.181 181
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 18, Uk. 128 350
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 350
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO Kuwaheshimu Walio Tangulia Katika Kheri: Aya hii inaelezea adabu nyingine itakiwayo katika kikao kwa kusema: “Enyi mlioamini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika vikao, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atawafanyia nafasi.” Iwapo mtu amechelewa katika kikao, ni vyema kwa waliotangulia kusogea ili kumfanyia nafasi ya kukaa. Adabu hii ni moja kati ya mambo yanayochangia katika kuimarisha mapenzi. Kwa kweli Uislamu ni Dini iliyokuja na utaratibu kamili wa maisha ya mwanadamu, kwani haikuacha jambo hili ambalo ni sehemu katika maisha ya kijamii, jambo ambalo huwezi kulikuta katika kanuni za mifumo mingine. Katika ibara isemayo: “Na Mwenyezi Mungu atawafanyia nafasi.” Wafasiri wanasema maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu atawakunjulia nafasi katika Pepo, hayo ni malipo kwa wale wanaochunga heshima za vikao katika dunia. Na kwa vile malipo ya wenye kuwapa nafasi wenzao hayakuanishwa, na hayo waliyoyataja wafasiri ni sehemu yake tu, basi Waislamu wenye kufuata mafunzo haya watarajie malipo zaidi ikiwa ni kuyapata Peponi huko akhera au hata hapa duniani, au katika fikra au katika maisha ya umri wenye baraka, au katika kuzidishiwa mali. Na hakuna ajabu yoyote kwa Mwenyezi Mungu kumlipa mja wake malipo haya yote kwa kitendo hiki kinachoonekana na wengi kutokuwa na uzito mkubwa, kwani hutoa malipo kwa mujibu aonavyo Yeye na si kwa kiwango cha matendo yetu. Wakati mwingine watu wanakuwa wengi kiasi cha kujaza nafasi za walengwa wa kikao, au wale wenye hadhi maalumu kukosa nafasi, basi wale watakaotakiwa kuondoka na kutoa nafasi kwa watu hao wafanye hivyo bila ya kinyongo: “Na mkiambiwa: ondokeni, basi ondokeni.” Tunaelewa kwamba baadhi ya watu wanaohudhuria kwenye kikao hawawezi kusimama kwa sababu ya ugonjwa au uzee, kwa hiyo inawapasa vijana kutoa nafasi kwa watu hao na kwa wale wenye nafasi maalumu katika jamii hata kabla ya kuambiwa ili kuonesha heshima juu ya watu hao. Baada ya hapo, Aya inataja malipo kwa mwenye kutekeleza adabu hii ya kikao, inasema: “Mwenyezi Mungu atawainua daraja walioamini miongoni mwenu, na waliopewa ilimu.” Hii ni ishara ya kwamba, pindi Mtume (s.a.w.w.) anapowataka wengine wasimame na kutoa nafasi kwa wengine, hafanyi hivyo kwa upendeleo, bali kuna sababu maalumu, kama vile kuonesha heshima kubwa kwa wale waliotangulia katika Uislamu na kutoa mchango wao na mali katika kuutetea, na pia kuwaheshimu wale wenye elimu zaidi kuliko wengine kwani watu hao wana malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na ni watu wenye heshima kubwa sana. 351
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 351
12/8/2014 2:43:48 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa vile wengine hutekeleza mafunzo haya na kuonesha heshima kwa walio juu yao kwa moyo safi na kwa ikhlasi, na wengine hufanya kwa kulazimishwa au kwa kujionesha, ndio Mwenyezi Mungu akamalizia katika Aya hii kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu kwa mnayoyatenda anazo habari.”
UTAFITI Nafasi ya Wanachuoni: Licha ya Aya kuteremka kwa ajili ya maudhui maalumu, lakini ina maana pana, na katika jambo jingine tunaloweza kujifunza hapa ni nafasi ya wale wenye elimu. Katika Aya Mwenyezi Mungu anatueleza ya kwamba daraja ya mtu hunyanyuka kutokana na mambo mawili: Imani na Elimu. Baada ya mtu kumwamini Mwenyezi Mungu na mambo yote anayopasa kuamini hakuna kitu kilichobora zaidi kuliko elimu, kwani hata yule ambaye huuwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu daraja yake ni ya chini ikilinganishwa na mwanachuoni, kama riwaya hii inavyosema:
ّ مداد العلماء أفضل من دماء .الشهداء “Wino (maandishi) wa wanachuoni ni bora kuliko damu ya mashahidi.”182
Kwani hata mpiganaji Jihadi hujua umuhimu na ubora wa jihadi kupitia kwa wanachuoni. Mwanachuoni pia atakuwa na nafasi ya kuweza kuwashufaiya (kuwaombea) baadhi ya watu Siku ya Kiyama, kama Mtume (s.a.w.w.) anavyotueleza:
ّ األنبياء ث ّم العلماء ث ّم:يشفع يوم القيامة ثالثة .الشهداء “Siku ya Kiyama watu wa aina tatu watashufaiya wengine: Mitume kisha wanachuoni kisha mashahidi.”183
Kwa hakika njia pekee ya kufikia ukamilifu na kupata radhi za Mwenyezi Mungu ni kuwa na imani thabiti na elimu sahihi ya Uislamu, na hakuna uongofu wowote bila ya vitu hivi. 182 183
Ghaffariy, Dirasatu Fii ilmi Diraya, Uk. 247 AlQazwiniy, Sunan Ibn Majah, Jz. 2, Uk.,1443 352
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 352
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI NA SABA
ُ ْن َي َد ْي َن ْج َو َ الر ُس َ ول َف َق ِّد ُموا َبي َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اك ْم َّ اجيْتُ ُم َ ين آ َمنُوا إِ َذا َن ور ٌ ْر لَ ُك ْم َوأَ ْط َه ُر َفإِ ْن لَ ْم َت ِج ُدوا َفإِ َّن اللهََّ َغ ُف ٌ ص َد َق ًة َ ٰذلِ َك َخي َ ُ ْن َي َد ْي َن ْج َو َ َر ِحي ٌم أَأَ ْش َف ْقتُ ْم أَ ْن تُ َق ِّد ُموا َبي ات َفإِ ْذ لَ ْم ٍ ص َد َق َ اك ْم ُ اب اللهَُّ َعلَي َّ الص اَل َة َوآتُوا الز َكا َة َوأَ ِطيعُوا َّ ْك ْم َفأَ ِقي ُموا َ َت ْف َعلُوا َو َت َ ُير ِب َما َت ْع َمل ون ٌ اللهََّ َو َر ُسولَ ُه َواللهَُّ َخ ِب “Enyi mlioamini! Mnaponong’onezana na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kunong’ona kwenu. Hiyo ni kheri kwenu na usafi zaidi. Na ikiwa hamkupata cha kutoa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu. Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kunong’ona kwenu? Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi simamisheni Swala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na Mwenyezi Mungu ana habari kwa mnayoyatenda.” (Qur’ani: 58:12-13)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasiri wanasema kwamba Aya hizi ziliteremka kutokana na baadhi ya watu waliokuwa na uwezo wa kimali kukithirisha kunong’ona na Mtume (s.a.w.w.). Kwa vile jambo hili lilikuwa likichukua muda mwingi wa Mtume (s.a.w.w.), Waislamu wanyonge hawakufurahishwa na hilo, kwani hata wengine walifikia kudhani kwamba Mtume anawapa kipaumbele watu hao kuliko wao, ndio hapo Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hizi na kuwataka watoe sadaka kila wanapotaka kunong’ona na Mtume (s.a.w.w.). Wale watu matajiri walilalamikia hukumu hii na baada yake hukumu hii ikafutwa na ikawa ni ruhusa kwa wote kunong’ona na Mtume (s.a.w.w.) katika mambo ya kheri na yanayolenga katika kumtii Mwenyezi Mungu.184
184
Shitaziy, Tafsirul Amthal, Jz. 18, Uk. 135 353
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 353
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO Sadaka Kabla Ya Kunong’ona: Katika maudhui yaliyotangulia kulikuwa na maudhui yaliyokuwa yanazungumzia suala la kunong’ona pamoja na hukumu zake, na katika Aya hizi ni mwendelezo wa jambo hilo lililochukua nafasi katika Surat Mujadalah. Aya inaanza kwa kusema: “Enyi mlioamini! Mnaponong’onezana na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kunong’ona kwenu.” Hukumu hii imekuja kama ilivyoelezwa katika sababu ya kuteremka. Ni kwamba matajiri walikuwa wakichukua muda mrefu katika kunong’onezana na Mtume (s.a.w.w.), kiasi cha Mtume kukereka na jambo hilo. Mwenyezi Mungu akateremsha hukumu ya kutanguliza kutoa sadaka kabla ya kuanza kunong’onezana naye. Jambo hili lilikuwa mtihani mkubwa kwao, na kwa upande mwingine lilikuwa na faida kwa mafakiri na masikini, na pia kumuondoshea kero Mtume (s.a.w.w.) Aya inaendelea kusema: “Hiyo ni kheri kwenu na usafi zaidi.” Jambo la kutoa sadaka kabla ya kunong’onezana na Mtume (s.a.w.w.) lililenga katika kuwanufaisha matajiri, kwa kulipwa ujira pindi watakapotekeleza amri hiyo, na pia kuleta kheri na baraka kwa masikini, kwani sadaka hiyo ingetumika katika kuwatatulia shida zao, na pia sadaka ni utakaso wa mali ya matajiri na utakaso wa nyoyo za masikini dhidi ya choyo na husda dhidi ya matajiri. Mwenyezi Mungu aliweka hukumu hii ili kupunguza wimbi la matajiri katika kunong’nezana na Mtume (s.a.w.w.) kwa kutoa sadaka, kwani kabla ya hukumu hii ilikuwa ni vurugu, na Mtume (s.a.w.w.) hakutaka kuwakataza yeye mwenyewe, bali alitarajia kwamba Mwenyezi Mungu ataingilia kati hali hiyo, kama alivyofanya kwa wale waliokuwa wakikithirisha mazungumzo ndani ya nyumba yake. Utoaji wa sadaka kabla ya kunong’ona na Mtume (s.a.w.w.) haukuwa wajibu kwa watu wote, kwani ingekuwa hivyo, wale masikini wasingeruhusika kumnong’oneza Mtume (s.a.w.w.) katika mambo ambayo wasingependa kujulikana na wengine. Jambo hilo lilikuwa ni wajibu tu kwa wale waliokuwa na uwezo, kamaAya inavyoendelea kusema: “Na ikiwa hamkupata cha kutoa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” Kwa hakika jambo la kutoa sadaka katika mazingira hayo, lilikuwa ni mtihani mzito kwa Waislamu wengi, kwani kwa ujumla wao walijizuia na hukumu hiyo isipokuwa Sahaba mmoja tu, naye ni Imamu Ali ibn Abi Talib (a.s.). Hapo kilibainika kile ambacho kilipasa kubainika, na Waislamu wakapata funzo kubwa katika hilo, baada ya hapo ikateremka Aya ya kuifuta hukumu hiyo, kama isemavyo: “Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kunong’ona kwenu?” Hapa ilibainika namna 354
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 354
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
walivyokuwa na mapenzi makubwa ya kupenda mali kuliko kunong’onezana na Mtume (s.a.w.w.). Na pia imebainika ya kwamba minong’ono yao haikuwa na umuhimu mkubwa kwao, na lau kama ingekuwa na umuhimu wengetoa sadaka na kuendelea nayo, hasa ikizingatiwa kwamba Mwenyezi Mungu hakuainisha kiwango maalumu cha sadaka kinachopasa kutolewa, kwani ingewezekana hata kutoa kiwango kidogo sana cha mali, lakini hawakufanya hivyo! Aya inaendelea kusema: “Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi simamisheni Swala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na Mwenyezi Mungu ana habari kwa mnayoyatenda.” Kutajwa msamaha katika Aya hii ni dalili ya wazi kwamba walimkosea Mtume (s.a.w.w.) kwa kumkera kutokana na minong’ono yao pamoja naye, na kuwa ni sababu ya kuwazuilia wengine kupata kuzungumza na Mtume (s.a.w.w.), hasa wale waliokuwa na hali duni, mpaka wakafikia wakati nao wakakasirishwa na tabia ya watu hao matajiri. Licha ya ibara hii ya Aya kutotaja kwa uwazi juu ya kubatilishwa hukumu ya kutoa sadaka kabla ya kunong’onezana na Mtume, lakini dhahiri ya mambo hukumu hiyo ilibatilishwa. Ama kule kutakiwa kusimamisha Swala na kutoa Zaka na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, amri hii imekuja kwa lengo la kutia mkazo juu ya utekelezaji wa nguzo hizo muhimu katika Uislamu, na pia kuwazindua ya kwamba hata kama wataendelea kunong’onezana, basi wasighafilike na majukumu makubwa waliyobebeshwa migongoni mwao.
UTAFITI Mtu Pekee Aliyetoa Sadaka Kabla Ya Kusema Siri na Mtume: Wafasiri wengi wa Kishia na wale wa Kisunni wameeleza wazi kwamba, mtu pekee aliyethubutu kutoa sadaka kabla ya kuanza kunong’ona na Mtume (s.a.w.w) ni Imamu Ali ibn Abi Talib (a.s.). Imepokewa kutoka kwake akisema:
ّ عز ّ آية في كتاب اهلل وجل لم يعمل بها أحد قبلي وال يعمل فكنت,فصرفته بعشرة دراهم كان لي دينار,بها أحد بعدي ّ .بي تص ّدقت بدرهم ّ ّإذا جئت إلى الن “Katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeitekeleza kabla yangu, na hakuna yeyote atakayeitekeleza baada yangu. Nilikuwa
355
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 355
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
na dinari moja, na nikaibadilisha na kupata dirhamu kumi, ikawa kila ninapokwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) nikitoa sadaka dirhamu moja.”185
Na katika hili, Umar ibn Khattab anasema:
ّ كان لعلّي ثالثة! لو كانت في واحدة ّ منهن لكانت إلي ّ أحب , وإعطاؤه راية يوم خيبر, تزويجه فاطمة:من حمر النّعم .وآية النّجوى “Ali alikuwa na mambo matatu, ningependa zaidi kuwa na moja kati ya hayo kuliko kuwa na ngamia mwekundu: Kwa kumuoa Fatima, na kupewa bendera siku ya vita vya Khaybar, na kuwa mhusika pekee wa Aya ya kusema siri na Mtume.”186
Kwa hakika jambo hilo lilikuwa ni fadhila kubwa na fakhari ya kipekee kwa Imamu Ali (a.s.), lakini la kusikitisha baadhi ya watu hawaoni kwamba jambo hilo lilinyanyua daraja yake na utukufu wake. Imamu Ali (a.s.) hakuwa ni mtu mwenye uwezo wa kimali, bali alikuwa ni mtu mwenye maisha ya kawaida, na hata baadhi ya siku alikuwa akishindia maji, kama kisa maarufu cha kuteremka Suratu Dahri kinavyoeleza. Baada ya kutoa sadaka Imamu Ali (a.s.) alipata muda wa faragha wa kuwa na Mtume (s.a.w.w.) hasa ikizingatiwa kulikuwa hakuna mwingine aliyekuwa akisubiri kufanya hivyo kwa vile hawakuwa tayari kutoa mali yao kwa lengo la kunong’ona na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) Watu wenye mawazo hayo ya kutotambua daraja ya juu ya Ali, kama watasoma sehemu ya Aya kwa mazingatio wataachana na rai yao hiyo, ni pale iliposema: “Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kunong’ona kwenu?” Pia maneno yaliyotoka kwa Umar ibn Khattab ni ushahidi tosha juu ya utukufu na ubora wa Imamu Ali (a.s.) juu Maswahaba wengine. Kuna fadhila mbali mbali za Imamu Ali (a.s.) zilizokuja kupitia Aya mbalimbali za Qur’ani na Hadithi za Mtume (s.a.w.w.), hayo yote ni kuonesha nafasi ya kipekee aliyonayo katika Uislamu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.).
185 186
Ibn Kathir, Tafsirul Qur’anil Adhim, Jz.4, Uk.349. Qurtubiy, Tafsirul Qurtubiy, Jz.17, Uk.302 356
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 356
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
Hekima Ya Kuwekwa Sadaka na Hatimaye Kufutwa: Kila mwenye kusoma Aya hizi na kuzifahamu, hatoacha kupitikiwa na swali hili katika ubongo wake: Ni kwa nini paliwekwa sheria ya kutoa sadaka kabla ya kunong’onezana na Mtume (s.a.w.w.) na kisha sheria hiyo ikafutwa, tena ndani ya kipindi kifupi? Jawabu la swali hili tayari limeshajibiwa na maelezo yaliyotangulia, hasa ikizingatiwa sabubu iliyopelekea kuteremka Aya hizi. Kwani lengo kubwa lilikuwa ni kupimwa wale wanaojionesha ya kwamba wana mapenzi makubwa na Mtume (s.a.w.w.), kwa hivyo kila wakati wako naye, wanapanga mipango mbalimbali inayohusiana na maendeleo ya Dini ya Mwenyezi Mungu na mustakabali wa Uislamu, lakini ikadhihiri ya kwamba mapenzi yao hayo ni pale mambo yanapokuwa bure, ama pale panapohitajika kutoa mali yao hawakotayari kuonesha mapenzi yao kwake. Zaidi ya hayo hukumu hii iliacha athari kwa Waislamu ya kwamba si vyema kumshughulisha Mtume (s.a.w.w.) kwa mambo yasiyo na ulazima na kumpotezea wakati wake, na pia kuwafanya wale wenye shida zao kukosa kutatuliwa, mpaka kuweza kumdhania vibaya Mtume (s.a.w.w.). Kwa hivyo hukumu hii ilikuwa imewekwa kwa muda maalumu, na pale lilipopatikana lile lililokusudiwa Mwenyezi Mungu aliifuta, kwani kuendelea na hukumu hiyo kungesababisha uzito kwa Waislamu, hasa pale mtu anapokuwa na jambo ambalo lahitaji kuwa katika hali ya usiri mkubwa. Suala la ufutwaji wa hukumu katika Qur’ani ni kwamba tangu mwanzo hukumu inayowekwa huwa inawekwa kwa muda maalumu, na baada ya kupatikana kilichokusudiwa huondoshwa hukumu hiyo moja kwamoja au kuletwa hukumu mbadala.
357
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 357
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI NA NANE
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ س َما َق َّد َم ْت لِ َغ ٍد َواتَّ ُقوا ٌ ين آ َمنُوا اتَّ ُقوا اللهََّ َو ْل َت ْن ُظ ْر َن ْف ََّين َن ُسوا الله َ ون َو اَل َت ُكونُوا َكالَّ ِذ َ ُير ِب َما َت ْع َمل ٌ اللهََّ إِ َّن اللهََّ َخ ِب َون اَل َي ْس َتوي أ ََفأ ْ اه ْم أَ ْن ُف َس ُه ْم أوالئك ُه ُم ُ اس َ َّاب الن ْ ُ َ ُ ار ح ص ق ف ال س ن ْ َ َ ِ ِ ِ َ اب ْال َجنَّ ِة ُه ُم ْال َفا ِئ ُز ُ ص َح ُ ص َح ون ْ َاب ْال َجنَّ ِة أ ْ ََوأ “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayoyatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda. Wala msiwe kama wale waliomsahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio mafasiki. Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi. Watu wa Peponi ndio wenye kufuzu.” (Qur’ani; 59:18-20)
MAELEZO Aya ya kwanza miongoni mwa Aya hizi inazidi kutoa msisitizo kwa Waumini juu ya suala la uchaji Mungu, kwani huko ndiko kunakopelekea kukumbuka na kufikiria juu ya Siku ya Kiyama: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayoyatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.” Pia msisitizo juu ya uchamungu uliomo katika Aya hii ni msisitizo juu ya kutenda matendo mema na kuachana na kila kitendo kilichoharamishwa na Mwenyezi Mungu, na kila mtu anajukumu juu ya nafsi yake katika kuhakikisha haya yanafanyika. Baada ya amri juu ya uchamungu na kufikiria mara kwa mara Siku ya Kiyama, Aya inayofuata inasema: “Wala msiwe kama wale waliomsahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio mafasiki.” Kwa hakika misingi mikubwa ya uchamungu ni kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa kufuata kanuni Zake na kuichunga nafsi isiingie katika maasi, na pia kumuhudhurisha Mwenyezi Mungu kila pahala mtu anapokuwepo. Jambo jingine ni kujikumbusha namna hali itakavyokuwa Siku ya Kiyama, namna watu watakavyosimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu 358
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 358
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
wakisubiri kuhukumiwa katika mahakama yenye uadilifu wa hali ya juu, mahakama ambayo itakuja na kila kitendo kilichotendwa na mwanadamu, ikiwa kikubwa au kidogo. Ukumbukaji wa mara kwa mara juu ya mambo haya ndio uliokuwa utaratibu wa mafunzo ya Mitume kwa watu wao. Kwa hiyo ughafilikaji wa mambo haya ndio sababu kubwa ya kumfanya mtu kupotoka na kuingia katika kumuasi Mwenyezi Mungu na kumfanya aishi kama mnyama asiye na mchunga, kwani mtu wa aina hiyo anakuwa hana haja yoyote ya kufanya matendo mema kwa ajili ya Siku ya mwisho. Kughafilika juu ya Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiyama kunamfanya mtu kuwa na kiburi, kwani hujiona ni mwenye kujitosheleza na hamuhitaji Mwenyezi Mungu katika maisha yake, na huona kwamba dunia ndipo pahala pekee pa kuishi, na mauti ndio mwisho wa mwanadamu. Baada ya mwanadamu kufikia hali hii huwa hazuiliki katika kutenda lolote baya, kama vile kuuwa, ubadhirifu wa mali za umma, ufisadi n.k., ndio maana Mwenyezi Mungu akasema: “Hao ndio mafasiki.” Katika kukurubisha hatari wanayoipata wale wenye kumsahau Mwenyezi Mungu, Aya haikusema: Wala msimsahau Mwenyezi Mungu. Bali imesema: “Wala msiwe kama wale waliomsahau Mwenyezi Mungu.” Hii ni kumaanisha kwamba kuna watu walioishi katika hali ya kumsahau Mwenyezi Mungu, kwa maana kusahau mafunzo Yake, hata baada ya wao kutamka Shahada mbili, watu ambao baadaye walisifika kwa sifa ya unafiki. Mwenyezi Mungu ameweka alama ya kuwatambua watu hao kama anavyosema:
َ ون ِب ْال ُم ُ ون َو ْال ُم َنا ِف َق ُ ات َبع َ ْض َي ْأ ُم ُر َ ْال ُم َنا ِف ُق نك ِر ٍ ْضهُم ِّمن َبع ْ ون أَ ْي ِد َي ُه ْم َن ُس ُ وف َو َي ْق ِب َ ض وا اللَهّ َف َن ِس َي ُه ْم إِ َّن ُ َو َي ْن َه ْو َن َع ِن ْال َمع ِ ْر َ اس ُق َ ْال ُم َنا ِف ِق ون ِ ين ُه ُم ْال َف “Wanafiki wanaume na wanafiki wanawake ni hali moja, wanaamrisha maovu na kukataza mema, na wanafumba mikono yao. Wamemsahau Mwenyezi Mungu na Yeye amewasahau, hakika wanafiki ni mafasiki.” (Qur’ani; 9:67).
Aya ya mwisho inaelezea tofauti iliyopo kati ya wale wanaomcha Mwenyezi Mungu na kukumbuka hali ya Siku ya Mwisho, na kukumbuka kwao huko kukawasukuma katika kufanya matendo mema, na wale ambao waliozama katika madhambi kwa kujighafilisha na mafunzo ya Uislamu, inasema: “Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi.” Watu hao hawalingani namna wanavyoishi hapa duniani, hawalingani katika kufikiri na hawatolingana katika maisha ya akhera, kwani watu wa aina hizi mbili kila kundi linamwelekeo wake na mitazamo 359
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 359
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
yenye kutofautiana. Kundi moja liko kwenye kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kujiandaa na Siku ya mwisho na kusimamia uadilifu hapa duniani, na kundi jingine limezama katika starehe za dunia, halisikii mwadhini wala mchota maji msikitini, kwa hiyo mwanadamu ana uhuru wa kuamua awepo katika kundi gani. Na mwishoni Aya inamalizia kwa kusema: “Watu wa Peponi ndio wenye kufuzu.” Kufuzu kwa watu wema kunaanzia hapa duniani kabla ya akhera, kwani ndio ambao huishi katika utulivu wa nafsi, na pale panapotokea mapambano dhidi yao, wao ndio wenye kushinda. Na pia hasara na kushindwa kwa wale wenye kughafilika huanzia hapa duniani.
UTAFITI Yanayostahiki Kutendwa: Aya imesisitiza juu ya mtu kujiandaa kwa ajili ya Siku ya Kiyama kwa kutenda matendo mema, kwani hiyo ndio rasilimali za uhakika zitakazomfaaa Siku hiyo, Siku ambayo mali na watoto havitakuwa na nafasi, kwani kile ambacho mwanadamu hakukitenda mwenyewe au kuwa na mchango katika kukifanikisha kitakuwa hakina nafasi katika Siku hiyo nzito. Mtume (s.a.w.w.) amewahimiza Waislamu kutoa sadaka ya kitu chochote chenye manufaa hata kama kitu hicho kitaonekana kuwa na thamani ndogo, yote hayo ni ili iwe ni kinga dhidi ya adhabu ya Siku ya Kiyama, amesema:
ولو, ولو ببضع بصاع ولو قبضة,تص ّدقوا ولو بصاع من تمر ّ ولو, ولو تمرة,ببضع قبضة ,بشق تمرة فمن لم يجد فكلمة طيّبة ّ ألم أجعلك, ألم أفعل بك, ألم أفعل بك: فيقال له,فإن أحدكم يلقى اهلل فيقول اهلل تبارك. بلى: ألم أجعلك ماال وولدا؟ فيقول,سميعا بصيرا فينظر قدامه وخلفه وعن: قال, فانظر ما ق ّدمت لنفسك:وتعالى يمينه وعن شماله فال يجد شيئا يقي به وجهه من النّار “Toeni sadaka, japo pishi moja ya tende, japo sehemu katika pishi, japo funda moja, japo sehemu ya funda, japo tende moja, japo ubale wa tende, na asi360
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 360
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
yekuwa na uwezo nayo, basi azungumze maneno mazuri, kwani kila mmoja wenu atakutana na Mwenyezi Mungu, na aambiwe: Je, sijakufanyia hili na lile? Je,sijakufanyia hili na lile? Je, sijakufanya ni mwenye kusikia na kuona? Je, sijakujaalia kuwa na mali na watoto? Atajibu: ‘Hapana, umenifanyia yote hayo.’ Mwenyezi Mungu atasema: Angalia kile ulichokitanguliza kwa ajili ya nafsi yako. Anasema: Ataangalia mbele yake na nyuma yake, na kuliani kwake na kushotoni kwake, na kuna ambaye hatoona chochote kile kitakachouokoa uso wake dhidi ya Moto.”187
Tunasoma katika Hadithi nyingine kwamba, siku moja Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amekaa pamoja na baadhi ya Maswahaba wake, mara wakaingia watu wa kabila la Mudharri, huku wakiwa wamebeba silaha zao kwa ajili ya kushiriki katika vita vya Jihadi, na nguo zao zikiwa zimechakaa. Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuwaona katika hali ile, na pia aliona dalili za kukosa nguvu na kuwa na njaa, uso wake ulisawijika sana. Aliamrisha watu wakusanyike msikitini, na alipanda mimbari yake na kuwahutubia: “Ama baada ya hayo, tambueni ya kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha katika Kitabu chake maneno yafuatayo: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayoyatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.” Basi toeni sadaka kabla hamjakosa uwezo wa kutoa sadaka, toeni sadaka kabla ya kuingia kizuizi cha kutoa sadaka, mtu atoe sadaka japo dinari yake moja, mtu atoe sadaka japo dirhamu yake moja, mtu atoe sadaka wema wake, mtu atoe sadaka miongoni mwa shairi yake, katika tende zake, na wala mtu asidharau kitu katika sadaka japo kama ni ubale wa tende.’” Baada ya kusikia maneno hayo, mtu mmoja kati ya Maansari alisimama na akampa Mtume (s.a.w.w.) mfuko uliokuwa na sadaka. Kwa kweli ilidhihiri furaha kubwa katika uso wa Mtume (s.a.w.w.), kisha akasema: “Mwenye kuanzisha jambozuri katika Uislamu, na akalitenda jambo hilo, mtu huyo atakuwa na malipo yatokanayo na jambo hilo, pia atapata malipo ya kila mwenye kulitenda jambo hilo, bila ya kupunguziwa malipo yao. Na mwenye kuanzisha jambo baya katika Uislamu na akalitenda jambo hilo, basi mtu huyo atapata madhambi yatokanayo na jambo hilo, pia atapata madhambi ya kila mwenye kulitenda jambo hilo, bila ya kupunguziwa madhambi yao.” Maswahaba waliposikia maneno hayo, walitawanyika na kila mmoja alikwenda kuchukua alichokuwa nacho na kukileta kwa Mtume (s.a.w.w.), na baadaye Mtume (s.a.w.w.) alivikusanya na kuwagaia wale wote. Jambo lolote jema analolifanya 187
Alkafiy, Usulul Kafiy, Jz. 4, Uk. 4 361
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 361
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
mwanadamu atalikuta mbele ya Mwenyezi Mungu likiwa ni lenye kuthaminishwa kwa thamani ya juu kabisa, kama anavyosema:
ًِّن َخيْر َتج ُدو ُه ِعن َد اللهَِّ ُه َو َخيْراً َوأَ ْع َظ َم أَ ْجرا ُ َُ ِ ٍ ْ َو َما تُ َق ِّدمُوا أِلنف ِسكم م “…Na kheri yoyote mnayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu, mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu imekuwa bora zaidi ikiwa na thawabu kubwa sana.” (Qur’ani; 73: 20).
362
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 362
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA SABINI NA TISA
ين آ َمنُوا اَل َتتَّ ِخ ُذوا َع ُد ِّوي َو َع ُد َّو ُك ْم أَ ْولَِيا َء تُ ْل ُق َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ َ ون َ ْه ْم ِب ْال َم َو َّد ِة َو َق ْد َك َف ُروا ِب َما َجا َء ُك ْم ِم َن ْال َح ِّق ي ْ ُخ ِر ُج َ ون إِلي ِ َّاك ْم أَ ْن تُ ْؤ ِمنُوا باللهَِّ َرب ُ ول َوإي ُ الر ُس َ ِّك ْم إِ ْن ُك ْنتُ ْم َخ َر ْجتُ ْم ِج َها ًدا َّ ِ ِ ضا ِتي تُ ِس ُّر َ َ ِفي َس ِبيلِي َوا ْب ِت َغا َء َم ْر َ ْه ْم ِب ْال َم َو َّد ِة َوأََنا أَ ْعلَ ُم ون إِلي ِ ض َّ ب َما أَ ْخ َفيْتُ ْم َو َما أَ ْعلَ ْنتُ ْم َو َم ْن َي ْف َع ْل ُه ِم ْن ُ َ َ ْ َ يل ب الس ء ا و س ل د ق ف م ك َّ ْ َ َ َ ِ ِ ِ َ َ َ ُ ْ ْ ْسطوا إلَي ُ إ ْن َيث َق ُف ُ ْك ْم أ ْي ِد َي ُه ْم َوأل ِس َن َت ُه ْم وك ْم َي ُكونُوا لَ ُك ْم أ ْع َدا ًء َو َيب ُ ِ ِ َ َ ُ ُ ُ ْ َ َ ُ السو ِء َو َو ُّدوا ل ْو َتكف ُر َ ون ل ْن َت ْن َف َعك ْم أ ْر َحا ُمك ْم َو اَل أ ْو اَل ُدك ْم ِب ُّ ص ُل َب ْي َن ُك ْم َواللهَُّ ِب َما َت ْع َملُ َ ير َق ْد َكا َن ْت لَ ُك ْم صٌ ون َب ِ َي ْو َم ْال ِق َيا َم ِة َي ْف ِ اهي َم َوالَّ ِذ َ ُرآ ُء ين َم َع ُه إِ ْذ َقالُوا لِ َق ْو ِم ِه ْم إِنَّا ب َ أُ ْس َو ٌة َح َس َن ٌة ِفي إِب َ ْر ِ ِم ْن ُك ْم َو ِم َّما َت ْعبُ ُد َ ون اللهَِّ َك َف ْر َنا ِب ُك ْم َو َب َدا َب ْي َن َنا َو َب ْي َن ُك ُم ون ِم ْن ُد ِ ْال َع َدا َو ُة َو ْال َب ْغ َ اهي َم ضا ُء أََب ًدا َحتَّىٰ تُ ْؤ ِمنُوا ِباللهَِّ َو ْح َد ُه إِ اَّل َق ْو َل إِب َ ْر ِ لبي ِه أََ َ ل ْس َت ْغ ِف َر َّن لَ َك َو َما أَ ْملِ ُك لَ َك ِم َن اللهَِّ ِم ْن َش ْي ٍء َربَّ َنا َعلَي َ ْك أِ ِ ْك أََن ْب َنا َوإلَي َ َت َو َّك ْل َنا َوإلَي َ ير َربَّ َنا اَل َت ْج َع ْل َنا ِف ْت َن ًة لِلَّ ِذ َ ين ص ُ ْك ْال َم ِ ِ ِ َ ْ ْ اغ ِف ْر لََنا َربَّ َنا إنَّ َك أ ْن َت ال َعز ُ َك َف ُروا َو ْ يز ال َح ِكي ُم لَ َق ْد َك َ ان لَ ُك ْم ِ ِ يه ْم أُ ْس َو ٌة َح َس َن ٌة لِ َم ْن َك َ ان َي ْر ُجو اللهََّ َو ْال َي ْو َم الآْ ِخ َر َو َم ْن َي َت َو َّل ِف ِ َفإِ َّن اللهََّ ُه َو ْال َغ ِن ُّي ْال َح ِمي ُد “Enyi mlioamini! Msiwafanye adui Zangu na adui zenu kuwa marafiki, mkiwapa mapenzi, na wao wamekwishaikataa haki iliyowajia, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamwamini Mwenyezi Mungu, Mola Wenu. Mnapotoka kwa ajili ya 363
12/8/2014 2:43:49 PM
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 363
WITO KWA WAUMINI
Jihadi katika Njia Yangu na kutafuta radhi Yangu, mnafanya upenzi nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayoyaficha na mnayodhihirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu basi amepotea njia ya sawa. Wakiwakuta wanakuwa maadui zenu, na wanawakunjulia mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri. Hawatawafaa jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda. Hakika nyinyi mna kigezo kizuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunawakataa; na umekwisha kudhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapomwamini Mwenyezi Mungu peke Yake. Isipokuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea maghufira; wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola Wetu! Juu Yako tumetegemea, na Kwako tumerudi, na Kwako ndio marejeo. Mola Wetu! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru; na tughufirie, Mola Wetu! Hakika Wewe Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. Kwa yakini kimekuwa kigezo kizuri kwenu katika mwendo wao, kwa anayemtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kugeuka basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.” (Qur’ani; 60:1-6)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasiri wengi wanasema ya kwamba Aya ya kwanza kati ya hizi, imeteremka kuhusiana na Haatib ibn Abi Balta’at, na kisa chenyewe kinaanza kama ifuatavyo: Sara aliyekuwa mjakazi wa Abi Amru ibn Sayfiy bin Hisham, alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) kutoka Makka hadi Madina. Ilikuwa ni baada ya kupita miaka miwili tangu kutokea vita vya Badri, Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza: Je, wewe umekuja hali ya kuwa ni Mwislamu? Alijibu: Hapana. Akamuuliza tena: Je, umekuja kuhamia hapa? Alijibu: Hapana. Akamuuliza tena: Ni kipi kilichokuleta? Alisema: “Nyinyi mlikuwa ndio jamaa zangu na mabwana zangu, na mabwana wangu wameshaondoka (wameuwawa), na nimefikwa na shida kubwa, na nimekuja kwenu ili mnisaidie chakula na mavazi.” Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza: Kwa nini vijana wa Makka wamekuacha katika hali hii? (Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza hivyo kwasababu bibi huyo alikuwa mwimbaji maarufu na akijipatia kipato chake kwa kazi hiyo. Alijibu: “Hawajanikodi tangu kumalizika kwa vita vya Badri (Hii ni ishara ya namna Makuraisha wa Makka walivyopata hasara katika vita hivyo). Mtume (s.a.w.w.) aliwataka watu wa ukoo wa Banil Muttalib wamsaidie mtu huyo, watu hao waliitikia wito huo na kumsaidia Sara. Wakati Sara alipokuwepo huko Madina, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akijitayarisha kwenda kuukomboa mji wa Makka, Haatib ibn Balta’at alikwenda kwa Sara na 364
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 364
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
akaandika barua na kumpa Sara ili aipeleke kwa watu wa Makka, pia alimpa msaada wa chakula na mavazi na dirhamu kumi. Barua ya Haatib bin Abi Balta’at kwa watu wa Makka ilikuwa imeiandikwa maneno yafuatayo: “Kutoka kwa Haatib ibn Abi Balta’at kwa watu wa Makka, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu anakujieni, kwa hivyo chukueni tahadhari.” Baada ya barua ile kumkabidhi Sara na kuanza kuondoka, Jibrili alimwendea Mtume (s.a.w.w.) na kumweleza aliyoyafanya Haatib ibn Abi Balta’at. Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Ali ibn Abi Talib, Ammar, Umar, Zubair, Talha, Miqdad bin As-wad na Abu Marthad, wote hao walikuwa wamepanda farasi. Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia nendeni mpaka sehemu inayoitwa Rawdhatu Khaakh, hapo mtamkuta mwanamke akiwa na barua kutoka kwa Haatib ibn Abi Balta’at kuwapelekea washirikina, mnyang’anyeni barua hiyo. Maswahaba hao wa Mtume (s.a.w.w.) walitoka mpaka wakafika ile sehemu waliyoelekezwa na wakamkuta Sara, wakamuuliza: Iko wapi barua? Sara aliapa kwa Mwenyezi Mungu yakwamba hana barua yoyote. Walianza kupekua mizigo yake, na hawakuikuta kwa hivyo wakaazimia kurudi, Imamu Ali (a.s.) akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Hatujaongopewa wala kuambiwa ni waongo.” Hapo Imamu Ali (a.s.) alichomoa upanga wake na kuunoa, na akamwambia Sara: “Itoe barua au nitaikata shingo yako.” Sara kuona hali hiyo, aliitoa barua katika misokoto ya nywele zake, kisha wakampelekea Mtume (s.a.w.w.) barua ile. Mtume (s.a.w.w.) alimuagiza Haatib aje kwake, baada ya kufika alimuuliza: “Je, unaijua barua hii.” Haatib akasema: Ndio. Akamuuliza tena: Ni kitu gani kilichokufanya kuandika barua hii? Akasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tangu niingie katika Uislamu sijawahi kukufuru, na wala sijawahi kukufanyia udanganyifu tokea nilipokunasihi, na wala sijawahi kuwapenda washirikina tangu nilipotengana nao, lakini hakuna yeyote kati ya Muhajirina isipokuwa ana jamaa, na mimi nilikuwa mgeni wao na familia yangu iko nao. Nilichelea juu ya familia yangu, nilitaka niwe na mafungamano nao. Nilitambua wazi ya kwamba Mwenyezi Mungu atawapelekea balaa lake na barua yangu hii haitowasaidia na kuwakinga na lolote.” Mtume (s.a.w.w.) alimkubalia udhuru wake na kumsamehe. Umar ibn Khattab alisimama na kusema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, niruhusu niikate shingo ya mnafiki huyu.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Umar, ni kipi kilichokujulisha (kwamba ni mnafiki), huenda Mwenyezi Mungu amewaangalia watu waliopigana vita vya Badri na kuwasamehe, kwa kusema: “Fanyeni mtakacho kwani nimeshawasamehe.” Aya inatutaka tufahamu ni namna gani mahusiano yetu yanatakiwa yawe baina yetu kama Waislamu kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine mahusiano kati
365
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 365
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
yetu na maadui wa Uislamu. Pia Aya inatueleza ya kwamba inampasa kila Muumini wa kweli kukata mahusiano na maadui wa Mwenyezi Mungu.188
MAELEZO Natija Ya Mahusiano Na Maadui Wa Mwenyezi Mungu: Tumejifunza ya kwamba, sababu iliyopelekea kushuka Aya hizi ni kutokana na kitendo kibaya kilichofanywa na mmoja miongoni mwa Waislamu aliyekuwa akijulikana kwa jina la Haatib ibn Abi Balta’at. Licha ya kwamba alikuwa hana lengo la kuwafanyia khiyana Waislamu, lakini kitendo hicho ni moja kati ya mambo yanayodhihirisha mapenzi kwa maadui wa Uislamu. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hizi ili kuwaonya Waislamu dhidi ya kurudia kitendo hicho kiovu, kama Aya inavyoanza kusema: “Enyi mlioamini! Msiwafanye adui Zangu na adui zenu kuwa marafiki, mkiwapa mapenzi, na wao wamekwishaikataa haki iliyowajia, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamwamini Mwenyezi Mungu, Mola Wenu. “ Aya inasisitiza ya kwamba wale wanaowaonea choyo na kukuchukieni ni maadui wa Waislamu, basi inakuwaje Waislamu wawanyooshee watu hao mkono wa urafiki! Pia watu hao wanaitikadi tofauti na ile ya Waislamu, na wameonesha uadui wa wazi dhidi ya Waislamu, kwa kuwapiga vita, kuwaudhi na hata kuwafukuza kutoka katika mji wao. Na wanaona kwamba imani ya Waislamu juu ya Mwenyezi Mungu ni kosa kubwa, ndio ikawa sababu ya kuwafanyia mabalaa yote hayo. Kwa kweli si jambo sahihi kuwafanya marafiki watu hao, na kuchukua hatua za kuwaokoa dhidi ya mkono wa sheria kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu wakiongozwa na Mtume (s.a.w.w.) Kisha Aya inaendelea kusema: “Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia Yangu na kutafuta radhi Yangu, mnafanya upenzi nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayoyaficha na mnayodhihirisha.” Ikiwa Waislamu wanampenda Mwenyezi Mungu kikwelikweli, na walihama kutoka katika mji wao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na ni wenye kupenda Jihadi kwa ajiliya kupata radhi Zake, basi ikiwa lengo lao kubwa ni hili, si sahihi kwa Mwislamu kuonesha urafiki kwa maadui wa Uislamu kwa njia za kujificha, na ilhali Mwenyezi Mungu anatambua siri kama vile anavyotambua dhahiri. Aya inahitimisha kwa kusema: “Na mwenye kufanya hayo kati yenu basi amepotea njia ya sawa.” Ile dhana ya kudhani ya kwamba akifanya maovu kwa siri haonekani na Mwenyezi Mungu ni dhana potofu kabisa, dhana ambayo inamfanya mwenye kuwa nayo kuwa mbali na haki, kwani dhana ya 188
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.18, Uk.234 366
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 366
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
aina hii ndio inayompelekea mwanadamu kumuasi Mwenyezi Mungu, ikiwemo hili la kuwakumbatia maadui wa Mwenyezi Mungu. Katika Aya inayofuata Mwenyezi Mungu anazidi kusisitiza juu ya kujiepusha na jambo hili ovu, anasema: “Wakiwakuta wanakuwa maadui zenu, na wanawakunjulia mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri.” Ni vipi Waislamu wawapende watu hawa wenye chuki, husda na choyo dhidi yao, na wanajipanga kuendeleza maudhi kwa kila njia, kwa kuwashambulia Waislamu kwa kutumia mikono yao na kuwaudhi kwa ndimi zao. Na lengo lao kubwa ni kuwaona wamerudi katika ukafiri au kutenda yale ambayo hayanasibiani na mafunzo ya Dini ya Kiislamu hata kama watu watadai ya kwamba wamemwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Aya inayofuata, Mwenyezi Mungu anamjibu Haatib na kila mwenye kuwa na fikra kama zake, kwani Mtume (s.a.w.w.) alipomuuliza sababu ya kuwaandikia barua watu wa Makka alijibu ya kwamba alifanya hivyo kwa vile kulikuwa na jamaa zake wa damu katika mji wa Makka, kwa hiyo angependa wasisibiwe na mashambulizi ya Waislamu, anasema: “Hawatawafaa jamaa zenu, wala watoto wenu.” Jamaa wa karibu pamoja na watoto ambao wanamshirikisha Mwenyezi Mungu hawana manufaa yoyote kwa Waumini, hapa duniani na Siku ya Kiyama. Basi haifai kuwakumbatia watu hao ambao ni maadui wa Mwenyezi Mungu, kwani kitendo hicho kinamkasirisha Mwenyezi Mungu, na hayuko tayari kuona maadui Zake wanaridhishwa. Aya inaeendea kwa kusema: “Siku ya Kiyama; Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu.” Huu ni msisitizo ya kwamba wenye kumtii Mwenyezi Mungu makazi yao yatakuwa Peponi, na wale wenye kumuasi watapata adhabu ya milele. Kwa hiyo kigezo kitakachotumika katika kupata neema za Mwenyezi Mungu ni imani iliyofungamana na vitendo na siyo suala la undugu na ujamaa, kwani Siku hiyo jamaa wa karibu watakimbiana. Mwishoni kabisa Aya inamalizia kwa kusema: Na Mwenyezi Mungu anaona mnayoyatenda.” Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.” Mwenyezi Mungu anatambua vyema kila kinachofanywa na mwanadamu. Anatambua kimefanywa kwa nia gani, anajua yale yaliyotendeka kwa dhahiri na kwa siri. Kwake hakufichikani jambo lolote, na ushahidi wa hayo ni jambo alilolifanya Haatib kwa usiri mkubwa, lakini ameweza kuidhihirisha kwa manufaa ya Uislamu na Waislamu. Kwa hakika elimu ya Mwenyezi Mungu ya kujua ya dhahiri na ya siri ni jambo lenye umuhimu mkubwa katika maisha ya mwanadamu, kwani wakati wote huhisi kwamba yuko katika mwonekano wa Mwenyezi Mungu kwa lolote lile alitendalo, bali hata lile alipitishalo katika moyo wake kabla ya kulitenda. Kwa hiyo hapa tunajifunza
367
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 367
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
kwamba uchamungu wa kweli utafikiwa pale tu mwanadamu atakapomtambua Mwenyezi Mungu kwa moyo safi. Mwenyezi Mungu ametumia utaratibu wa kurahisisha mafunzo yake kwa waja Wake kwa kutumia mifano mbalimbali, katika kuwaonesha Waislamu msimamo wanaotakiwa kuwa nao dhidi ya maadui wao. Anawaambia wanatakiwa wajifunze kupitia Nabii Ibrahim (a.s.) pamoja na wafuasi wake, Aya inasema: “Hakika nyinyi mna kigezo kizuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye.” Nabii Ibrahim (a.s.) anatambuliwa kuwa ni baba wa Mitume. Anatoa darasa kubwa juu ya moyo safi katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, namna alivyoipigania Dini ya Mwenyezi Mungu, mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na msimamo wake mkali dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo basi, kila mwenye kutaka mafanikio ya dunia na ya akhera hana budi kumweka mbele Mtume huyu kwa kumwangalia ni namna gani aliyatekeleza hayo na mengineyo. Nabii Ibrahim (a.s.) pamoja na Maswahaba zake walisimama kidete dhidi ya maadui na kuwaambia kwamba wao hawako pamoja nao, kama Aya inavyoendelea kusema: “Walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu.” Huu ndio msimamo madhubuti unaopasa kuchukuliwa na kila Mwislamu dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu, kwa kuwaambia kinagaubaga kwamba hawaridhiki nao na wala hawako pamoja nao. Hapa inanikumbusha baada ya kulipuliwa kituo cha kimataifa cha kibiashara pamoja na jengo la Wizara ya Ulinzi ya Marekani mwaka 2001, Raisi wa nchi hiyo wakati huo; George Bush aliwataka walimwengu kwamba, ama wawe pamoja naye, au wawe pamoja na magaidi, Bush anaamini ya kwamba kila asiyekuwa pamoja na Marekani ni gaidi. Ni kiongozi mmoja tu aliyetangaza waziwazi ya kwamba, nchi yake haiko pamoja na Marekani na wala haiko pamoja na magaidi. Kiongozi huyo ni kiongozi mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran; Ayatullahil-Udhmaa, Imamu Ali Khamenei. Kwa kweli ni mfuasi sahihi wa nyayo za Nabii Ibrahim (a.s.) pamoja na Maswahaba zake. Nabii Ibrahim (a.s.) na wafuasi wake waliendelea kuonesha misimamo yao kwa kusema: “Tunawakataa; na umekwisha kudhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapomwamini Mwenyezi Mungu peke Yake.” Wamewaeleza wazi kwamba wataendelea kujitenga nao na kutoshirikiana nao kwa lolote lile kwa vile watu hao wanaendeleza ukafiri na uadui dhidi ya Waumini. Hali hii ya kuwakataa maadui wa Uislamu ilikuwa inajumuisha watu wote katika zama za Nabii Ibrahim (a.s.) isipokuwa kwa baba (baba mkubwa) yake, kwani alikuwa akidhani baba yake
368
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 368
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
huyo ataweza kuachana na ukafiri wake na kuingia katika Dini sahihi aliyokuja nayo, Aya inasema: “Isipokuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea maghufira; wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu.” Nabii Ibrahim (a.s.) alichukua ahadi ya kumuombea msamaha ami yake huyo kwa Mwenyezi Mungu, lakini alipoona kwamba si mtu mwenye kuelekea katika Dini sahihi alichukua msimamo ule ule wa kuwatenga maadui wa Mwenyezi Mungu, kama Qur’ani inavyotuambia:
َ اهي َم َّ لبي ِه إ َ َو َما َك ال َعن َّم ْو ِع َد ٍة َو َع َد َها إِيَّا ُه ُ اس ِت ْغ َف ْ ان َ ار إِب ِ ِ ِْر ِ أ َ َفلَ َّما َت َبي ألوا ٌه َحلِي ٌم َّ اهي َم َ َّن لَ ُه أَنَّ ُه َع ُد ٌّو للِِهّ َت َب َّرأَ ِم ْن ُه إِ َّن إِب ِ ْر “Wala haikuwa kwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake isipokuwa ni kutokana na ahadi aliyoahidiana naye, lakini ilipombainikia kwamba yeye (huyo baba yake) ni adui wa Mwenyezi Mungu alijiepusha naye, kwa hakika Ibrahim alikuwa mwingi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu na mvumilivu.” (Qur’ani; 9:114)
Kwa hiyo Waislamu wanatakiwa wajifunze kutoka kwa Nabii huyu pamoja na wafuasi wake, namna walivyokuwa na misimamo madhubuti dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu, na wasiwe kama Haatib namna alivyofanya. Bila ya shaka katika kuwalingania kunahitaji kuonesha mapenzi na upole wa hali ya juu, lakini mambo yakigeuka kwa watu hao kuonesha uadui dhidi ya Waislamu, hapo itabidi Waislamu wabadilishe misimamo yao kwa watu hao. Na kwa vile kuchukua misimamo mikali dhidi ya maadui na kupambana nao si jambo jepesi, kutokana na wingi wao na namna walivyojilimbikizia silaha nzito nzito za maangamizi, inahitaji kumtegemea Mwenyezi Mungu katika hilo, kama Aya inavyomalizia kwa kusema: “Mola Wetu! Juu Yako tumetegemea, na Kwako tumerudi, na Kwako ndio marejeo.” Katika ibara hii tunagundua mambo matatu ya msingi yanayohitajika katika kukabiliana na adui, mambo hayo ni: Kumtegemea Mwenyezi mungu, kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa kumuomba msamaha, na la mwisho ni kuitakidi kwamba marejeo ya viumbe ni kwa Mwenyezi Mungu. Kila jambo kati ya haya ni sababu ya kutokea jingine na wakati huo huo ni kisababishwa, kwa mfano, imani juu ya kurejea kwa Mwenyezi Mungu inapelekea kumfanya mtu kuomba msamaha, na msamaha unasababisha kujengeka roho ya kumtegemea Mwenyezi Mungu katika nafsi ya mwanadamu. Katika Aya ifuatayo, Nabii Ibrahim (a.s.) na wafuasi wake
369
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 369
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
wanamwelekea Mwenyezi Mungu kwa kumuomba zaidi na zaidi ili wasije wakarudi nyuma wakati wa kukabiliana na maadui, wanasema: “Mola Wetu! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru.” Mtihani utokao kwa makafiri ambao waumini wanaomba usiwasibu ni ile hali ya kushindwa katika mapambano na kudhoofika imani zao, kwani mara nyingi watu wanapokuwa wanapigania jambo fulani na kutofanikiwa hutia mashaka juu ya jambo hilo, badala ya kusoma mazingira na kutafuta sababu ya msingi iliyopelekea kushindwa. Katika Uislamu hakuna hasara yoyote kwa mpiganaji, ikiwa atashida na kuendelea kuishi au kama atauwawa, jambo la msingi ni kuingia katika mapambano akiitakidi ya kwamba analolifanya ni kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na sio maslahi yake binafsi. Aya inaendelea kusema: “Na tughufirie, Mola Wetu! Hakika Wewe Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” Nguvu ya Mwenyezi Mungu haishindiki na Hekima Yake ipo katika kila kitu. Dua hii huenda ikawa ni kuomba msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kutokana na nafsi ya mwanadamu kumili katika kuwapenda maadui wa Mwenyezi Mungu. Haya ni mafunzo yanayopasa kufuatwa na kila Mwislamu, na pale mtu anapokuwa kama Haatib, basi arejee kwa Mwenyezi Mungu haraka kwa kumuomba msamaha. Na kwa mara nyingine Mwenyezi Mungu anawasisitiza Waumini juu ya kufuata nyayo za Nabii Ibrahim (a.s.) pamoja na wafuasi wake, anasema: “Kwa yakini kimekuwa kigezo kizuri kwenu katika mwendo wao, kwa anayemtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” Hao si kigezo kwa Waumini katika misimamo yao dhidi ya maadui tu, bali ni kigezo chema katika masuala ya kiroho, kama vile kumuomba dua Mwenyezi Mungu ili awarahisishie mambo yao na kuwasamehe makosa yao, kama tulivyoona katika Aya zilizopita. Manufaa yote ya kuwafanya kigezo watu hao yanarudi kwa Waislamu wenyewe na si kwa mwingine, kama Aya inavyomalizia kusema: “Na mwenye kugeuka basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.” Kufungamana na maadui ni kuwazidishia nguvu ambazo baadaye watazitumia dhidi ya Waislamu, na hapo watakuwa ni wenye kushinda na kuwatawala Waislamu. Hapo hakuna huruma yoyote watakayoipata kutoka kwao, hata watoto na wazee wasiojiweza watanyimwa haki zao za msingi.
370
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 370
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
UTAFITI Vigezo Vyema: Kwa kawaida matendo ya mwanadamu na kauli yake huwa ni kwa mujibu wa kile anachokiamini moyoni mwake. Kwa kawaida kuwepo watu wakamilifu katika jamii ni sababu kubwa kwa jamii hiyo kuweza kufikia katika maendeleo iwapo wataamua kwa dhati kufuata nyayo za watu hao. Kwa sababu hii, baadhi ya watu wameweza kuongoka kutokana na kauli pamoja na matendo ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Maimamu watoharifu na Mitume wengine kwa ujumla. Kwa hiyo suala la umaasumu (kutotenda makosa) kwa watu hao ni jambo la msingi katika kufikia uongofu wa uhakika, na jambo hili la umaasumu kwa watu hao limethibiti katika Qur’ani Tukufu na katika maneno ya Mtume (s.a.w.w.) Si hivyo tu, bali kila Mwislamu anatakiwa awe kigezo chema kwa wengine kwa vitendo vyake kabla ya maneno yake, kama Imamu as-Sadiq (a.s.) anavyotuambia kwa kusema:
. وال تكونوا دعاة بألسنتكم,كونوا دعاة النّاس بأعمالكم “Kuweni walinganiaji watu kwa vitendo vyenu, na wala msiwe walinganiaji kwa ndimi zenu.”189
Kwa hiyo hatuna budi kuvifanya vyema vitendo vyetu ili viwavutie wengine, na hatimaye waamue kuingia katika Dini yetu, na hivi ndivyo walivyofanya Waislamu wa mwanzo. Walitawanyika katika sehemu mbalimbali za dunia, na waliweza kuwabadilisha watu kwa tabia zao, kwani nchi nyingi na zenye Waislamu wengi zaidi kama vile Indonesia waliukubali Uislamu kwa njia hii na si kwa kuvamiwa kijeshi na kulazimika kuukubali Uislamu, bado nafasi ya kufanya hivi tunayo. Udugu Katika Uislamu: Miongoni mwa mambo yanayowaunganisha wanadamu ni itikadi, kwa hiyo Uislamu umetilia mkazo juu ya kuwepo mapenzi na mafungamano kati ya Waislamu, na umeutanguliza udugu wa imani kuliko udugu wa damu ikiwa watu watatofautiana katika imani. Mapenzi ya Mwislamu na kuchukia kwake kuwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa maana ampende aliyeamrishwa kumpenda na amchukie anayestahiki kuchukiwa, kama anavyosema Imamu as-Sadiq (a.s.): 189
Al-Majlisiy, Biharul Anwar, Jz.5, Uk.198 371
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 371
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
ّ من .أحب هلل وأبغض هلل وأعطى هلل ومنع هلل فقد استكمل إيمان “Mwenye kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mtu huyo ni mkamilifu wa imani.”190
Katika maudhui haya muhimu katika Uislamu, maudhui ambayo ni kipimo kikubwa cha imani ya Mwislamu, yamechukua nafasi kubwa katika Sura hii (Suratul Mumtahina), kwani kuna Aya nyingine tatu zinazoelezea hukumu ya jambo hili. Katika Aya hizo tatu, Aya ya kwanza inawaeleza Waislamu namna hali ya mapenzi itakavyoweza kujitokeza kati yao na washirikina katika kipindi kijacho, inasema:
َُّين َعا َديْتُم ِّم ْنهُم َّم َو َّد ًة َوالله َ ْن الَّ ِذ َ َع َسى اللهَُّ أَن َي ْج َع َل َب ْي َن ُك ْم َو َبي ور َّر ِحي ٌم ٌ ير َواللهَُّ َغ ُف ٌ َق ِد “Huenda Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu, na Mwenyezi Mungu ni Muweza na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu.” (Qur’ani: 60:7)
Ahadi hii ya Mwenyezi Mungu ilitimia mwaka wa nane wa Hijiria, pale Mwenyezi Mungu alipowaneemesha Waislamu ushindi wa kuikomboa Makka. Hapo wakazi wa Makka wakaingia katika Uislamu makundi kwa makundi, na hapo mawingu ya giza yakaondoka katika maisha yao na kuangaziwa na nuru ya mapenzi na urafiki. Aya zifuatazo zinaelezea ni makafiri wa aina gani Waislamu wanaweza kufanya nao urafiki, na ni wa aina ganiambao si ruhusa kuwa na urafiki pamoja nao, zinasema:
َّاك ُم اللهَُّ َعن ال ُ ُخر ُج ُ ُين لَ ْم ي َُقا ِتل ُ اَل َي ْن َه ْ ين َولَ ْم ي ِّ َ وك ْم الد ي ف م وك ذ ْ ِ ِ ِ ِ ِ َِم ْن ِد َيار ُك ْم أ َوه ْم َوتُ ْق ِس ُطوا إل َ ْ ُ َ ُح ُّب ْال ُم ْق ِس ِط ين ي ر ب ت ن ُّ َ ِ ْه ْم إِ َّن اللهََّ ي ِ ِ ِ َ ُ َّ َُّلله ُ ُ ُ ِّ ين َقا َتلوك ْم ِفي َ إِنَّ َما َي ْن َهاك ُم ا َع ِن ال ِذ ين َوأ ْخ َر ُجوك ْم ِم ْن ِ الد َ ار ُك ْم َو َظ اج ُك ْم أَ ْن َت َولَّ ْو ُه ْم َو َم ْن َي َت َولَّ ُه ْم ٰ َاه ُروا َعل ِ ى إِ ْخ َر ِ ِدَُي َّ ول ِئ َك ُه ُم َ الظالِ ُم ون ٰ َ َفأ 190
Sajistaniy, Sunan Abi Daud, Jz.2, Uk.403 372
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 372
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
“Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia ihsani na uadilifu wale ambao hawakupigana nanyi kwa ajili ya Dini wala hawakukufukuzeni kutoka majumbani kwenu, hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao uadilifu. Kwa hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kwa wale ambao wanapigana nanyi katika Dini na kukufukuzeni kutoka majumbani mwenu na kusaidia katika kufukuzwa kwenu, (anakukatazeni) kuwafanya marafiki. Na wale wawafanyao marafiki, basi hao ndio madhalimu.” (Qur’ani 60: 8-9)
Kwa mujibu wa Aya hizi, Qur’ani Tukufu imewagawa washirikina katika makundi mawili: Kundi la kwanza, ni lile lililowapiga Waislamu wazi wazi na kusimama dhidi yao na kupambana nao kwa kutumia silaha na kuwafukuza kwa nguvu kutoka majumbani mwao. Hukumu ya Uislamu kwa mujibu wa watu hawa ni kujizuia kufanya nao urafiki, na kutokuwa na mapenzi na mafungamano yoyote yale yawayo. Kundi la pili ni kundi ambalo licha ya kuwa na itikadi inayokwenda kinyume na itikadi ya Uislamu, lakini si vibaya kwa Waislamu kuwafanyia na kuwadhihirishia mapenzi watu hao, ikiwa tu watu hao hawaoneshi uadui dhidi ya Waislamu kwa njia yoyote ile, na iwapo Waislamu watawekeana mkataba wowote na watu wa kundi hili inawapasa wautekeleze na kuamiliana nao kwa wema na uadilifu, na haya yalitokea katika historia ya Uislamu, pale watu wa ukoo wa Khaza’awalipokuwa na mkataba wa kuishi kwa salama na amani na bila ya kugombana pamoja na Waislamu. Kwa mujibu wa hukumu hii inampasa kila Mwislamu kukabiliana kwa ujasiri mkubwa na kila mwenye kuudhuru Uislamu na Waislamu, kwani hukumu hii haiwahusu watu wa Makka tu, bali ni hukumu inayowajumuisha Waislamu wote popote walipo na katika zama zote.
373
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 373
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI
ْ ين آ َمنُوا إ َذا َجا َء ُك ُم ََّيا أَُّي َها ال ُ َ ْ ُ ُات َفا ْم َت ِحن َ وه َّن ه م ات ن م ؤ م ال ذ ُ ُ ٍ اج َر َ ِ ِ ِ ِ ُ ات َف اَل َت ْر ِجع ُ اللهَُّ أَ ْعلَ ُم ِبإِي َما ِن ِه َّن َفإِ ْن َعلِ ْمتُ ُم ُوه َّن إِلَى ٍ وه َّن ُم ْؤ ِم َن َّ ْال ُك َّ ون لَه ُ ُُن َوآت َ ُّار اَل ُه َّن ِح ٌّل لَ ُه ْم َو اَل ُه ْم َي ِحل وه ْم َما أَ ْن َف ُقوا َو اَل ف ِ ُ َ ُ ُ َ َ ُ ُ ُ وه َّن إِذا آ َتيْت ُم ُ اح َعليْك ْم أ ْن َت ْن ِك ُح ور ُه َّن َو اَل ت ْم ِسكوا َ وه َّن أ ُج َ ُج َن اسأَلُوا َما أَ ْن َف ْقتُ ْم َو ْل َي ْسأَلُوا َما أَ ْن َف ُقوا َذٰلِ ُك ْم ُح ْك ُم ْ ص ِم ْال َك َوا ِف ِر َو َ ِب ِع َاللهَِّ َي ْح ُك ُم َب ْي َن ُك ْم َواللهَُّ َعلِي ٌم َح ِكي ٌم َوإ ْن َفا َت ُك ْم َش ْي ٌء ِم ْن أ ْ اج ُك ْم و ز َ ِ ِ َ َ ْ ُ َ َّ إلَى ْال ُك َ ار َف َع َاقبْتُ ْم َفآتُوا الَّ ِذ اج ُه ْم ِمثل َما أ ْن َفقوا ف ُ ين َذ َه َب ْت أ ْز َو ِ ِ َ َّ َّلله ُ َ ُ َّ َ َُواتقوا ا ال ِذي أ ْنت ْم ِب ِه ُم ْؤ ِمن ون “Enyi mlioamini! Wakiwajia wanawake Waumini waliohama, basi wafanyieni mtihani. Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao; Mkijua kuwa ni waumini, basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali yao, wala wanaume hao si halali yao wanawake hao. Na wapeni hao walichotoa. Si vibaya kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa. Na takeni mlichokitoa, na wao watake walichokitoa. Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayowahukumu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. Na akitoroka yeyote katika wake zenu kwenda kwa makafiri, tena ikatokea mkapata ngawira, basi wapeni waliokimbiwa na wake zao kiasi cha mahari waliyoyatoa. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamwamini.” (Qur’ani 60: 10-11)
SABABU YA KUTEREMKA Baadhi ya wafasiri wanasema kwamba, Aya hizi ziliteremka baada ya Mtume (s.a.w.w.) kutiliana saini ya makubaliano aliyokubaliana na Makureishi wa Makka katika kitongoji cha Hudaybiya, maarufu kwa ‘Sulhu Hudaybiya’. Miongoni mwa makubaliano hayo ilikuwa ni iwapo mtu wa Makka atahama na kwenda Madina kwa Mtume (s.a.w.w.) arudishwe Makka, na kama ikiwa mtu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) atakwenda Makka mtu huyo hana haki ya kurudishwa alikotoka
374
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 374
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
(Madina). Baada ya kusainiwa makubaliano hayo, na kabla ya watu kutawanyika, Bibi Sabiiat bint Harth al-Aslamiyat, ambaye alikuwa Mwislamu alifika Hudaybiya na kutaka kujiunga na kundi la Waislamu, mara mume wake ambaye alikuwa si mwislamu aliwasili na kumwambia Mtume (s.a.w.w): “Ewe Muhammad, nirejeshee mke wangu, kwani tumekubaliana umrejeshe mtu ambaye atakuja kwako, na haya hapa maandishi hayajakauka.” Hapo ndipo Aya zikateremka, zikianza kuwaambia Waumini kwamba wanapojiliwa na Waumini wanawake wenye kuhamia Madina kutoka Makka, kwanza wawafanyie mtihani. Ibn Abbas amesema kwamba, wafanyiwe mtihani kwa kuapishwa ikiwa kweli wamehama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na hawakufanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya kidunia. Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiwafanyia mtihani huo kwa kuwaapisha, na pale anapobainikiwa ya kwamba kweli mwanamke aliyehama alihama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, alikuwa akimzuia kurudi alikotoka, na alichokuwa akifanya ni kuwarudishia mahari yao na gharama walizowagharamikia.191
MAELEZO Kufidia Gharama Kwa Waislamu Na Makafiri: Katika maudhi ya Aya zilizopita zimezungumzia namna ya kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kukata mahusiano dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu, ama maudhui ya Aya hizi ni kuhusiana na mamna ya kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na namna ya kuamiliana na wale walioachana na mila potofu na badala yake kushikamana na Dini ya haki. Maudhui yanaanza katika Aya ya kwanza kwa kuelezea wanawake wenye kuhama. Aya hii imekusanya vipengele saba vinavyohusiana na wanawake wenye kuhama, na pia imetaja vipengele vingine vihusianavyo na wanawake washirikina. Kipengele cha kwanza: Mtihani kwa wanawake waliohama. Mwenyezi Mungu anawaelekea Waumini kwa kusema: “Enyi mlioamini! Wakiwajia wanawake Waumini waliohama, basi wafanyieni mtihani.” Licha ya Aya kuwaita wanawake wa aina hiyo kwamba ni Waumini, kutokana na kuthibitishwa hilo na watu wawili waadilifu, lakini hilo halitoshi kutokana na hali ilivyokuwa wakati huo, kwa hivyo ikawekwa hukumu ya kutahiniwa juu ya imani yao ili kupata uthibitisho mkubwa zaidi. Namna ya mtihani ilikuwa ni kula kiapo kwamba kuhama kwao ni kwa ajili ya Uislamu na si kwa sababu ya kumpenda mtu fulani, au kupenda kuishi Madina n.k. Kuna rai nyingine inayosema namna 191
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.18, Uk.256 375
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 375
12/8/2014 2:43:49 PM
WITO KWA WAUMINI
walivyokuwa wakitahiniwa wanawake hao, rai hiyo ni kutokana na Aya ya 12 ya Sura hii hii (Suratu Mumtahina) inayosema:
َ ْ َ ْ ات يُ َباي ْع َن َك َعلَىٰ أَ ْن اَل ي َ ُش ِر ْك َن ِ ُ َيا أ ُّي َها النَّ ِب ُّي إِذا َجا َءك ال ُم ْؤ ِم َن َ ِباللهَِّ َشي ًْئا َو اَل َي ْس ِر ْق َن َو اَل َي ْز ِن ين َو اَل َي ْقتُ ْل َن أَ ْو اَل َد ُه َّن َو اَل ْ َي َْن أ ْ ين ببُ ْه َتان َي َ ُ َ َ َ ْ ْصي َن َك ِفي د ي ي ب ه ن ي ر ت ف ت أ َ ِ يه َّن َوأَ ْر ُجلِ ِه َّن َو اَل َيع ِ ِ ِ ِ ٍ ِ َّلله َّلله َّ اس َت ْغ ِف ْر لَه َّ وف َف َب ِاي ْعه ور َر ِحي ٌم ٌ ُن ا َ إِ َّن ا َ َغ ُف ُ َمع ْ ُن َو ٍ ْر
“Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake waumini wakakubai kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaouzua baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema. Basi peana nao baia na uwatakie maghufira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani: 60:12)
Mtihani huo haukuwa ni kithibitisho tosha juu ya ukweli wa imani za wanawake hao, kwani kuna uwezekano mtu akaapa kwa kuthibitisha jambo fulani, lakini ikawa ni uongo. Kutokana na uwezekano wa kufanyika udanganyifu katika kuapa, ndio Mwenyezi Mungu akahitimisha Aya kwa kusema: “Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao.” Kipengele cha Pili: Mwenyezi Mungu anasema: “Mkijua kuwa ni waumini, basi msiwarudishe kwa makafiri.” Licha ya kwamba makubaliano katika mkataba ni kwamba watu wa Makka waliosilimu wakienda Madina inapaswa warejeshwe Makka, sharti hilo liliwahusu wanaume tu na sio wanawake, kwa hiyo Mtume (s.a.w.w.) hakumrejesha mwanamke yeyote kwa makafiri, kwani mwanamke Mwislamu kuishi na mwanamume kafiri kunamuweka pahala hatari kuhusiana na imani yake. Hii ni kutokana na hali yake ya kimaumbile na kule kumtegemea mwanamume katika mahitajio yake ya kila siku. Kipengele cha Tatu: Kwa hakika hukumu iliyomo katika kipengele hiki ni kama cha kipengele kilichopita, kimekuja kwa njia ya msisitizo, Mwenyezi Mungu anasema: “‘Wanawake hao si halali yao, wala wanaume hao si halali yao wanawake hao.” Imani na ukafiri ni vitu viwili tofauti havistahiki kukutana katika nyumba moja, na suala la ndoa ni lazima wanandoa waowane (wafanane) katika imani na tabia, bila ya hivyo mustakabali wake utakuwa si mrefu na usioleta tija katika maisha. Suala la kuendelea kwa ndoa kati ya watu wawili wenye imani tofauti lilikuwa linaendelea 376
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 376
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
mwanzoni mwa Uislamu bila ya kuzuiwa, kutokana na jamii ya Kiislamu kuwa katika mzingiro wa kijamii na kutengwa, lakini baada ya mizizi ya Uislamu kushika vizuri na Waislamu kupata nguvu, amri ya kukatazwa na kuvunjwa ndoa hizo ilitolewa na hasa baada ya Suluhu ya Hudaybiya, kama Aya hii inavyoweka bayana juu ya jambo hili. Kipengele cha Nne: Ilikuwa ni tabia ya Waarabu hata kabla ya Uislamu kutoa mahari kwa ajili ya ndoa, kama Aya ilivyoashiria kwa kusema: “Na wapeni hao walichotoa.” Hapa kwa vile mwanamke ndiye aliyejitoa katika ndoa, italazimu wale waume wa kwanza ambao ni makafiri warejeshewe mahari yao ili kufidia hasara waliyoipata ya kuwakosa wake zao hao. Hukumu hii bado imebakia hata kama wana ndoa wote ni Waumini, iwapo mwanamke atadai talaka ni juu yake kurejesha mahari yote aliyopewa. Hukumu hii ilikuja kutokana na baadhi ya Maswahaba kuona ya kwamba wanawake hao wahamiaji hawastahiki tena mahari kwa vile walipokea mahari kutoka kwa waume wao wa zamani,na kwa vile hazina ya mali ya Kiislamu ilikwishawarejeshea waume hao wa zamani fidia ya mahari yao. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu ameeleza bayana ya kwamba si ruhusa wanawake hao kuolewa bure, pasi na kupewa mahari yao. Na Uislamu unataka kila mwanamke apewe mahari yake kwa lengo la kuchunga utu wake na heshima yake. Mwanamke Muumini anapotaka kujitenga kutoka katika ndoa yake na mume asiyemuumini, hapahitajiki talaka, lakini hakuna budi kwa mwanamke huyo kukaa eda. Kipengele cha Sita: Ama ikiwa mwanamume ameingia katika Uislamu na mwanamke akabakia katika ukafiri wake, katika hali hiyo ndoa itavunjika, kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu pale aliposema: “Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa.” Baadhi ya wanachuoni wamesema hukumu ya uharamu wa kumuoa mwanamke asiye Mwislamu ni kwa ndoa ya kudumu tu, ama ndoa ya mut’a (ya muda) inajuzu. Kisha wakahitalifiana tena kuhusu wanawake wa Kiyahudi na Kinasara, baadhi yao wanaona inafaa kuolewa na Mwislamu, na wengine wakasema ya kwamba uharamu wa ndoa hii ni kwa kila mwanamke asiye Mwislamu. Maelezo zaidi utaweza kuyapata katika vitabu mbalimbali vya kifiqhi. Kipengele cha Saba: Kipengele hiki kinahusiana na wanawake waliotoka katika Uislamu na kukimbilia kwa makafiri. Katika hali hii Waislamu nao wana haki ya kudai mahari yao kama vile makafiri walivyopewa haki hii, Aya inasema: “Na takeni mlichokitoa, na wao watake walichokitoa.” Hivi ndivyo Uislamu unavyozingatia uadilifu katika haki na hukumu. Unapigania kila mmoja kupata haki yake anayostahiki bila ya kuangalia imani yake.
377
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 377
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
Mwishoni mwa Aya Mwenyezi Mungu anasisitiza kutekelezwa hukumu zote zilizopita kwa moyo safi, anasema: “Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayowahukumu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.” Hakika hukumu hizi zinatokana na elimu Yake Mwenyezi Mungu, ni hukumu zilizojaa busara na hekima, kwani ni hukumu zinazochunga haki za kila mtu katika jamii. Aya ya mwisho kwenye maudhui haya inaendelea kueleza hukumu hizi kwa kusema kwamba, ikiwa mwanamke Mwislamu atatoka katika Uislamu na kukimbilia kwa makafiri, na halafu kukatokea mapigano kati ya Waislamu na makafiri, na Waislamu wakashinda na kupata ngawira, basi ni wajibu kwa Waislamu kutenga mali kwa ajili ya wale waliokimbiwa na wake zao: “Na akitoroka yeyote katika wake zenu kwenda kwa makafiri, tena ikatokea mkapata ngawira, basi wapeni waliokimbiwa na wake zao kiasi cha mahari waliyoyatoa. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamwamini.” Na kwa mujibu wa mafunzo haya, inamaanisha ya kwamba, ikiwa wanawake hao wanaishi na hao wanaume makafiri, walioshindwa katika vita, basi walazimishwe kurejesha mahari kwa wale Waislamu waliokuwa waume wa wanawake hao waliotoka katika Uislamu, kama vile ilivyo wajibu kwa Waislamu kuwarejeshea mahari wale wanaume makafiri ambao wake zao walisilimu na kukimbilia Madina. Na mwisho kabisa, Aya inamalizia kwa kuwataka Waislamu wote kujipamba na vazi la uchamungu katika maisha yao yote yakiwemo haya ya kurudisha mahari kwa makafiri kutokana na wake wao kuingia katika Uislamu: “Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamwamini.” Kwa mujibu wa riwaya, ni kwamba jambo hili la wanawake kutoka kwenye Uislamu na kurudi katika ukafiri, lilifanywa na wanawake sita, na Mtume (s.a.w.w.) aliwapa waume zao mahari waliyoitoa kutokana na ngawira za vita.192 Uadilifu hata kwa Maadui: Kutokana na Aya tulizozichambua, zinaonesha namna Uislamu unavyozingatia suala la uadilifu, kwani asili ya Uislamu ni kuzingatia uadilifu katika uwekaji wa sheria zake, kwani lengo lake kubwa ni kuhakikisha kheri na mafanikio yanapatikana kwa kila mmoja bila ya kuzingatia imani yake. Ama kwa upande mwingine wa kanuni za kisekyula,tunashuhudia namna kanuni hizo zilivyokosa uadilifu na haki, kwani zinawapa haki tabaka fulani na kuwanyima wengine! 192
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 18, Uk. 263 378
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 378
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa kweli haki hizi zilizowekwa na Uislamu ni dalili ya wazi juu ya ukweli na ubora wa Dini hii tukufu na uthibitisho wa juu wa Utume wa Mtume wetu (s.a.w.w.), na ni kuonesha namna alivyotoa juhudi zake katika kuhakikisha kwamba kila mmoja anapata haki yake, na kuona uadilifu ndio dira ya hukumu zote bila ya kuwepo ubaguzi wa aina yoyote ile.
379
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 379
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI NA MOJA
ََّيا أَُّي َها ال َض َب اللهَُّ َعل َ ين آ َمنُوا اَل َت َت َولَّ ْوا َ َ ْه ْم َق ْد َي ِئ ُسوا ي غ ا م و ق ذ ً ْ ِ ِ ِ ِْم َن الآ َار ِم ْن أ ُ ص َحاب ْال َّ س ْال ُك َ ُور ب ق ف ئ ي ا م ك ة ر خ ُ ْ َ َ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ “Enyi mlioamini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia. Hao wamekwishakata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyowakatia tamaa watu wa makaburini.” (Qur’ani; 60:13)
MAELEZO Hii ni Aya ya mwisho ya Suratul Mumtahina, katika Aya ya mwanzo Mwenyezi Mungu ameanza kwa wito wa kuwaita Waumini, na akawataka wakate mafungamano yote ya udugu na urafiki na makafiri wenye kuwapiga vita Waislamu. Katika Aya hii anahitimisha kwa kurudia wito huo huo, lengo ni kuwasisitiza Waumini juu ya ubaya wa jambo hili. Anaanza kwa kusema: “Enyi mlioamini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia.” Ni jambo la hatari sana kwa Waislamu kuwapa siri zao watu wa aina hii, kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wao na wa mali zao, kama vile ambavyo ni sababu kubwa ya kuidhoofisha Dini ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya wafasiri wanaona kwamba ‘Watu waliokasirikiwa’ ni Mayahudi, maana hii inanasibiana na sababu iliyofanya kuteremshwa Aya hii, kwani baadhi ya Waislamu mafukara walikuwa wakienda kwa Mayahudi na kuwapa siri za Waislamu kwa lengo la kujipatia kitu chochote, hapo Aya ikateremshwa ili kuwakataza dhidi ya mwenendo wao huo. Licha ya hayo Aya inamaana pana, kwani inajumuisha maadui wote wa Kiislamu, kwani hasira za Mwenyezi Mungu si kwa Mayahudi peke yao, bali pia zimeelezwa kuwapata wanafiki kama ilivyo katika Aya hii:
َّ ات َ ِّالظان َ ات َو ْال ُم ْش ِر ِك َ َويُ َع ِّذ َب ْال ُم َنا ِف ِق ين ِ ين َو ْال ُم ْش ِر َك ِ ين َو ْال ُم َنا ِف َق َ َِّبالله َض َب اللهَُّ َعل َالس ْو ِء َعل ُ َ َّ َ ْه ْم َولَ َع َن ُه ْم ي غ و ء و الس ة ر ئ ا د م ْه ي ن ظ َّ َّ ْ ْ َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ َ َ يرا ً ص ِ َوأ َع َّد ل ُه ْم َج َهنَّ َم َو َسا َء ْت َم 380
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 380
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
“Na awaadhibu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na washirikina wanaume na washirikina wanawake, wanaomdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya. Utawafikia mgeuko mbaya. Na Mwenyezi Mungu awakasirikie na kuwalaani na kuwaandalia Jahannam; nayo ni marejeo mabaya kabisa.” (Qur’ani 48:6)
Kwa hiyo Aya inanasibiana na Aya ya mwanzo ya Surat Mumtahinah. Aya inabainisha sababu ya kuwakata hao kwa dalili iliyo wazi, inasema: “Hao wamekwishakata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyowakatia tamaa watu wa makaburini.” Ni kwa sababu wale waliokufa hali ni makafiri, wataona malipo ya matendo yao katika makaburi yao, na kwa vile hawatopata tena nafasi ya kurudi tena ili kuja kufanya yale waliyopaswa kuyafanya, watakuwa ni wenye kukata tamaa moja kwa moja ya kupata nusra ya Mwenyezi Mungu siku ya kufufuliwa. Kwa hiyo na hawa waovu waliozama katika dhulma na maasi wamefikia hali ya kukata tamaa ya kuokoka dhidi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu, kama vile walivyokata tamaa wafu makafiri. Watu wenye kusifika na sifa hii, si watu wa kuaminika kwa lolote lile, kwa hiyo si haki kwa Waumini kijikurubisha kwao kwa kuwafanyia urafiki na mapenzi, kwani wameshakata tamaa ya kupata rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ndio maana ikawa wao kila siku wanatenda madhambi makubwa makubwa na dhulma za wazi bila ya kificho wala aibu! Si haki kwa Waumini kufungamana na watu hao. Leo tunawashuhudia Wazayuni (Mayahudi) namna wanavyowaangamiza watoto, wazee na wanawake wa Palestina kwa kutumia silaha nzito, na kushambulia mashule na mahospitali kwa madai kwamba wanalinda usalama wao, huku macho ya mataifa makubwa yakikodoka, bali wao ndio watoaji wa silaha hizo, na kwa vile wamekata tamaa ya rehema za Mwenyezi Mungu, dhulma hiyo hawatoikomesha, na itakoma pale tu Waislamu wao wenyewe watakapoamua na kusema: “Sasa basi, unatosha unyama walioufanya.” Na hatua ya kwanza isiyogharimu jasho ni kukata uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara na wazayuni hao, kama namna Mwenyezi Mungu alivyotuelekeza, lakini kwa masikitiko zile nchi zinazotarajiwa kuwa na msimamo mkali dhidi yao, ndio marafiki wao wakubwa, na pia ni marafiki wakubwa na dola hizo zinazochangia dhulma hiyo! Hakuna manufaa yoyote watakayoyapata ikiwa watakwenda kinyume na miongozo ya Mola Wao Mlezi, Mola aliyeumba ulimwengu na wanadamu na kuwawekea taratibu za kuishi ili kufikia maisha yenye furaha na amani.
381
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 381
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI NA MBILI
َ ُون َما اَل َت ْف َعل َ ُين آ َمنُوا لِ َم َت ُقول َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ َ ون َكب َُِّر َم ْق ًتا ِع ْن َد الله َ ُين ي َُقا ِتل َ ُح ُّب الَّ ِذ َ ُأَ ْن َت ُقولُوا َما اَل َت ْف َعل ون ِفي َس ِبيلِ ِه ِ ون إِ َّن اللهََّ ي ٌ ص ًّفا َكأَنَّ ُه ْم بُ ْن َي ُ وص ٌ ص ُ ان َم ْر َ “Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?Ni chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda. Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaopigana katika Njia Yake kwa safu kama kwamba wao ni jengo lililojengwa kwa risasi.” (Qur’ani: 61:2-4)
SABABU YA KUTEREMKA Wafasri wametaja sababu mbalimbali zinazohusiana na kuteremka Aya hizi, huku kukiwa na tofauti ndogo sana. Miongoni mwa yale waliyoyasema ni kama ifuatavyo:
193
1.
Aya imeteremka kwa watu waliokuwa Waumini, watu hao walisema: Pindi maadui wakitujia, katu hatutokimbia na wala hatutorudi nyuma, lakini watu hao hawakutekeleza walichokisema, kwani wakati wa vita vya Uhud baadhi yao walikimbia, mpaka wakasababisha Mtume (s.a.w.w.) akajeruhiwa na kuvunjwa meno yake ya mbele.
2.
Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja malipo makubwa watakayoyapata wale waliouwawa katika vita vya Badri, baadhi ya Maswahaba walisema: Ikiwa haya ndio malipo ya kufa katika vita, katu hatutokimbia katika vita vijavyo, lakini walikimbia katika vita vya Uhud, na Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hizi, kwa lengo la kuwalaumu.
3.
Kabla ya kuteremshwa hukumu ya kupigana Jihadi, baadhi ya Waislamu walitaka waelezwe jambo lililo bora ili walitende, na haukupita muda mrefu, Mwenyezi Mungu aliwapa habari kwamba jambo lililobora zaidi ni kuwa na imani ya kweli na kupigana katika vita vya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Lakini vita vilipowadia hawakuonekana ni wenye kufanya hivyo, bali walitoa nyudhuru mbalimbali. Aya ziliteremka ili kuwalaumu kutokana na tabia yao hiyo.193
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.18, Uk.278 382
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 382
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
MAELEZO Katika Aya hizi, Mwenyezi Mungu anaanza kwa kuelekeza lawama kwa wale wasiotekeleza wayasemayo. Anasema: “Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?” Licha ya kwamba Aya zimeteremka kutokana na sababu tulizotangulia kuzitaja, lakini maana ya Aya hii inaingia kwa kila ahadi inayowekwa na Mwislamu kisha asiitimize, na kwa hivyo lawama kutoka kwa Mwenyezi Mungu zitamshukia kila mwenye kufanya hivyo. Aya inaendelea kwa kusema: “Ni chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda.” Maneno mazito, majigambo ya kila aina katika vikao mbalimbali,kudai kwamba uwezo wa kupambana na adui upo wakati wowote, na kwamba tutamshushia kipigo kikali, lakini mambo yanapoiva na kupamba moto, vitendo vinakuwa tofauti na maneno yaliyosemwa. Kwa hakika jambo hili linamkera sana Mwenyezi Mungu, na mja kufanya hivi ni kujisababishia ghadhabu na hasira kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Sayyid Tabatabai anasema: Kuna tofauti kati ya mtu kusema kitu katika hali ya kutokuwa tayari kukifanya kitu hicho na yule ambaye hatekelezi kile alichokisema kwa uthabiti, mtu wa kwanza anasifa ya unafiki na mtu wa pili ni mwenye udhaifu katika utekelezaji.” Vyovyote vile, Aya inajumuisha hali yoyote ile ya makusudi ya kwenda kinyume na kile mtu alichokisema, na hiyo itakuwa ni katika kuvunja ahadi. Baadhi ya wanachuoni wamesema hata nadhiri anayoiweka Mwislamu kisha asiitekeleze inaingia katika hukumu hii. Tunasoma katika barua ya Imamu Ali (a.s.) aliyomwandikia Malik al-Ashtar:
والخلف يوجب القت...إيّاك أن تعدهم فتتّبع موعدك بخلفك ُر َم ْقتاً ِعن َد اللهَِّ أَن َت ُقولُوا َما َ َكب:عند اهلل النّاس قال اهلل تعالى َ ُاَل َت ْف َعل .ون “Jihadhari kuwapa ahadi, unapowaahidi tekeleza ahadi yako… na kutotekeleza ahadi kunapelekea kuchukiwa na Mwenyezi Mungu na watu, Mwenyezi Mungu amesema: ‘Ni chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda.’”194 194
Imamu Ali (a.s.) Nahjul Balaghah, Jz.3 Uk.109 383
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 383
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
Baada ya hapo, linafuata jambo muhimu katika hukumu za Kiislamu. Jambo hilo ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Aya inasema: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaopigana katika Njia Yake kwa safu kama kwamba wao ni jengo lililojengwa kwa risasi.” (Qur’ani 60:2-4) Jambo la kuzingatia katika Aya hii ni kwamba, Mwenyezi Mungu hakuhimiza tu kupigana vita, bali amehimiza vita hivyo viwe ni katika kutafuta radhi Zake, hali ya kuwa kitu kimoja, kama vile jengo lililoshikana vizuri. Waislamu wanatakiwa pindi wanapokuwemo katika mapambano dhidi ya adui yao, wawe ni wenye kushikamana pamoja, lao liwe ni moja, wajiepushe na kuleta mizozo ambayo kwa kawaida husababisha udhaifu katika vita, na ni silaha kubwa ya adui kuweza kujinyakulia ushindi wa bure.
UTAFITI Umuhimu wa Umoja wa Kiislamu: Jambo muhimu katika kuhakikisha ushindi ni kuungana na kuwa kitu kimoja mbele ya adui wakati wa mapambano. Jambo hili si katika uwanja wa kivita peke yake, bali hata katika vita vya kiuchumi na siasa, kinyume chake hatutoweza kufanya chochote chenye maslahi nasi. Mwenyezi Mungu alipowafananisha Waumini wenye kushikamana pamoja na jengo madhubuti, ni kwa sababu maadui ni kama maji yenye kufurika, maji yanayosomba kila kitu, lakini maji hayo hushindwa kuisomba nyumba iliyojengwa kwa umakini na ustadi wa hali ya juu. Kwa hivyo Waislamu wakiwa katika hali kama hii katika sehemu zote za maisha si rahisi kukaliwa juu na adui yoyote yule, na kinyume chake wataangamizwa wote bila ya kubakia yeyote. Kwa majonzi makubwa, ni kwamba mafunzo haya mazuri yamesahauliwa na Waislamu walio wengi, hali ya umoja haipo, ni kila mmoja na lake, kiasi ya kupelekea kudhoofishana wenyewe kwa wenyewe kwa maslahi ya adui. Umoja wa Kiislamu si maneno tu ya kuzungumzwa, bali kwanza kuna haja ya kuungana katika imani na malengo. Haya yatatokea tu ikiwa kutakuwa na kusafiana nia na kujilazimisha kushikamana na mafunzo ya Qur’ani Tukufu, na kwenda mwenendo sahihi katika maisha ya kila siku. Ikiwa Mwenyezi Mungu Muumba anatangaza kwa uwazi kwamba anawapenda waja Wake wenye kupigana katika jihadi wakiwa kama jengo lililoshikana vizuri, basi wakati huo huo anatangaza kwamba ghadhabu Zake na hasira Zake zitakuwa kwa wale wenye kutengana na kukatana mapande. Na haya tunayashuhudia, kwani kila mmoja anashuhudia ni namna gani kikundi kidogo cha Mayahudi walivyozinyakua ardhi za Waislamu na 384
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 384
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
kuzitawala kwa nguvu za kijeshi, licha ya idadi ya Waislamu kuwa kubwa sana ikilinganishawa na idadi ya Mayahudi. Kauli Bila ya Vitendo: Wakati mwingine ulimi huyadhihirisha yale yaliyofichwa katika nyoyo. Ikiwa ulimi utazungumza yale ambayo hayakukusudiwa na moyo, basi jambo hilo humpelekea mtu huyo kuwa na sifa ya unafiki. Leo jamii nyingi zimekumbwa na mtihani wa kukosa kuaminiana, sababu kubwa iliyopelekea hayo ni hii hali ya kutotekeleza yale wanayoyaahidi, na hayo yanawafanya kukosa uaminifu, heshima na kupoteza haiba yao kwa watu wanaowaahidi. Kwa hiyo ndugu Waislamu tujitahidi sana kusema yale tunayoweza kuyafanya, na kuyatenda tuyasemayo, ili tusiingie katika ghadhabu za Mwenyezi Mungu.
385
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 385
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI NA TATU
ََّيا أَُّي َها ال ُ ار ٍة تُ ْنج ُ ُّين آ َمنُوا َه ْل أَ ُدل َ َ ْ َ اب ذ ع ن م م يك ج ت ٰ ى ل ع م ك ذ َ َ ْ ْ َ َ ِ ِ ِ ٍ ِ َ َأ َّلله َ اه ُد َ ُيم تُ ْؤ ِمن يل ا ِ ِبأ ْم َوالِ ُك ْم ل ِ ِ ون ِباللهَِّ َو َر ُسولِ ِه َوتُ َج ِ ون ِفي َس ِب ٍَ ُ ُ ُ ُ ُ ُ ُ َ َ َ ُ َ ْر لك ْم إِ ْن ك ْنتُ ْم َتعْل ُم ون َي ْغ ِف ْر لك ْم ذنُو َبك ْم ٌ َوأ ْنف ِسك ْم َ ٰذلِك ْم َخي َ ْات َت ْجري ِم ْن َت ْح ِت َها أ ار َو َم َسا ِك َن َطيِّ َب ًة ِفي ُ ال ْن َه ٍ ََّويُ ْد ِخ ْل ُك ْم َجن ِ ْ ات َع ْد ٍن َذٰلِ َك ْال َف ْو ُز ْال َع ِظي ُم َوأُ ْخ َرىٰ تُ ِحبُّو َن َها َن َِّص ٌر ِم َن الله ِ ََّجن َ يب َو َب ِّش ِر ْال ُم ْؤ ِم ِن ٌ َو َف ْت ٌح َق ِر ين “Enyi mlioamini! Je, niwajulishe biashara itakayowaokoa na adhabu iliyo chungu? Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua. Atawasamehe dhambi zenu, na atawatia katika Mabustani ambayo hupita mito chini yake, na maskani nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa. Na kinginecho mkipendacho - nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi ulio karibu. Na wabashirieni Waumini!” (Qur’ani 61:10-13)
MAELEZO Aya zilizotangulia zimeonesha umuhimu wa imani na kujitolea katika kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu, na katika Aya hizi Mwenyezi Mungu anazidi kutoa msisitizo juu ya mambo haya mawili kwa kutumia mifano iliyo mizuri katika kuihimiza nafsi kwenye mambo haya ya kheri. Mambo haya ni sababu ya kila mafanikio ya Waislamu katika maisha yao. Aya zinaanza kwa kusema: “Enyi mlioamini! Je, niwajulishe biashara itakayowaokoa na adhabu iliyo chungu?” Licha ya kwamba imani na kupigana Jihadi ni katika mambo ya wajibu, lakini hapa Mwenyezi Mungu hakutumia utaratibu wa amri kama ilivyo katika Aya nyingi, bali ametumia utaratibu wa kuvishabihisha viwili hivyo na biashara, jambo ambalo linatamaniwa na watu wengi kufanywa, hasa ikizingatiwa kwamba wafanyabiashara ndio wenye kushikilia uchumi katika mataifa yote ya dunia. 386
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 386
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu ameanza kwa suala lenye kuamsha hisia za kibinadamu kutaka kujua ni biashara gani hiyo, na mara tu baada ya suala hilo amekuja na jawabu kwa kusema: “Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu.” Na kwa vile Mwenyezi Mungu si muhitaji kwenye biashara hii, bali maslahi ya biashara hii itarudi kwa Waumini wenyewe, ndio akamalizia maneno kwa kusema: “Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.” Kitu cha kuzingatia hapa ni kwamba, licha ya Aya hizi kuwahutubia Waumini, na wakati huo huo kuwataka waamini na wapigane Jihadi, ni ishara kwamba imani itakiwayo ni imani iliyo halisi, imani isiyotetereshwa na chochote kile, imani iliyokita katika moyo na si katika ncha ya ulimi, imani ya mtu ambaye yuko tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani tumeona katika Aya nyingine zikiwataka Waumini waamini, kama ilivyo katika Aya ifuatayo:
ْ ُوا آ ِمن ْ ُين آ َمن َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ...وا “Enyi mlioamini! Aminini…” (Qur’ani 4:136)
Imani juu ya Mwenyezi Mungu siku zote inakwenda sambamba na imani juu ya Mtume Wake, kama vile ambavyo Jihadi inabeba mambo mawili: Nafsi na mali, kwani vita vyote vinahitaji wapiganaji na maandalizi, zikiwemo silaha, hapo ndipo ushindi utakapopatikana. Na katika kuiangalia Aya kwa undani, tunaona Mwenyezi Mungu ametanguliza Jihadi kwa mali kabla ya nafsi, si kwa sababu yakuwa na umuhimu mkubwa zaidi kuliko nafsi, bali ya kuwa ni ndio utangulizi wa Jihadi kwa nafsi, kwani mahitaji ya kivita hayawezi kupatikana ikiwa hakuna mali. Bishara hii yenye faida kubwa ina mambo matatu ya msingi: Kwanza ni mnunuzi ambaye ni Mwenyezi Mungu, pili: ni wateja, ambao ni Waumini, tatu: Ni bidha, ambazo ni mali na nafsi. Na baada ya hapo linafuatia jambo la nne ambalo ni thamani ya kununulia bidhaa hizo kama ilivyoelezwa katika Aya ifuatayo: “Atawasamehe dhambi zenu, na atawatia katika Mabustani ambayo hupita mito chini yake, na maskani nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa.” Aya inataja thamani ya kununulia bidhaa za imani juu ya Mwenyezi Mungu na nafsi pamoja na mali anazoziuza Muumini kumuuzia Mwenyezi Mungu. Malipo yaliomo katika Aya hii ni malipo yatakayolipwa Siku ya Kiyama. Malipo ya kwanza kabisa ni kusamehewa 387
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 387
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
dhambi, kwani dhambi ndilo jambo linalomkera Muumini katika nafsi yake, na baada ya kupata hakikisho hili kutoka kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka nafsi yake itatulia na kujisiakia raha. Mwenyezi Mungu anataja thamani nyingine ya kununulia vitu hivyo katika Aya ifuatayo kwa kusema: “Na kinginecho mkipendacho - nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi ulio karibu.” Malipo haya ni malipo ambayo Mwenyezi Mungu atawalipa waja Wake Waumini hapa duniani. Ni uzuri gani ulioje wa biashara hii, biashara ambayo ina malipo ya papo kwa hapo na malipo ya baadaye (Siku ya Kiyama), na mlipaji akiwa ni Mwenyezi Mungu, Mpaji na Mwenye kujitosheleza kwa kila kitu, Mola ambaye hapungukiwi pale atowapo. Biashara hii imepata baraka zote kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwanza ikiwa ni ruhusa ya kufanya biashara hii, pili, Yeye ndiye mteja na ananunulia kwa kitu chenye thamani na hadhi ya hali ya juu kuliko chochote kile, kwa hivyo anatoa pongezi kubwa kwa wale Waumini wenye kuifanya biashara hii, kwakusema: “Na wabashirieni Waumini!” Kuna Riwaya inayozungumzia yale yaliyojiri usiku wa Aqaba. Ni usiku ambao Mtume (s.a.w.w.) alikutana kwa siri na watu waliokuwa wakiishi karibu na mji wa Madina. Abdallah ibn Rawaha alimwambia Mtume (s.a.w.w.): “Weka masharti ya Mola Wako na ya kwako namna upendavyo.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Nashurutisha kwa Mola Wangu, ya kwamba Msimwabudu isipokuwa Yeye tu, na wala msimshirikishe pamoja naye kitu chochote, na ninawashurutisha kuhusu mimi ya kwamba, msinizuilie kutoa nafsi zenu na mali zenu.” Abdallah ibn Rawaha alimuuliza Mtume (s.a.w.w.): “Tutapata nini ikiwa tutafanya hivyo?” Mtume (s.a.w.w.) akamjibu: “Mtapata Pepo.” Abdallah akasema: “Kwa kweli ni biashara ambayo hatutoivunja na wala hatutokubali ivunjwe.”195
UTAFITI Ushindi wa Karibu: Ni jambo lililo maarufu kwamba, ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kuwapa ushindi wa karibu Waumini ni jambo lililotokea, si tu kwa upande wa masuala yanayohusiana na itikadi, bali pia katika masuala ya kivita. Kuhusiana na ushindi huo wa karibu, wafasiri wamejaribu kutaja makusudio mbalimbali ya ushindi huo. Baadhi yao wamesema: Makusudio ya ushindi wa karibu katika Aya hii ni ushindi wa kukombolewa Makka, na wengine wakasema ni kufunguliwa nchi ya Irani na maeneo yaliyokuwa yakitawaliwa na dola ya Roma. Na wengine wakasema ya kwamba Aya 195
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 18, Uk. 305 388
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 388
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
hii inajumuisha ushindi wote waliopata Waislamu baada ya kuukubali Uislamu na kupambana dhidi ya maadui, ushindi ambao waliupata ndani ya siku chache. Na kwa vile Mwenyezi Mungu anawaita Waumini kwa kupitia Aya hii, kwa hiyo Aya inajumuisha Waumini wote katika zama zote, kwa hiyo biashara hii ni kwa kila Muumini, na hivyo kila mwenye kufuata masharti ya kuingia katika biashara hii atapata malipo kama waliyoyapata wa mwanzo. Na haya tunayashuhudia katika maisha yetu, Waumini wa kweli wameweza kuushangaza ulimwengu kutokana na ushindi walioupata licha ya uhaba wa maandalizi yao katika mapambano waliyopambana dhidi ya maadui zao. Dunia ni Mahala pa Biashara Kwa Wachamungu: Siku moja Imamu Ali (a.s.) alimsikia mtu ambaye alikuwa na tabia ya kusema uongo sana na kuilaumu dunia, Imamu (a.s.) alimwambia: “Ewe mwenye kuilaumu dunia, mwenye kughururika na ghururi zake, mwenye kuhadaiwa na undani wake, unaghururishwa na dunia kisha unailaumu!... Hakika dunia ni nyumba ya ukweli kwa mwenye kuisadiki na ni nyumba ya mawaidha kwa mwenye kuwaidhika nayo… na nimahala pa kufanyia biashara kwa wale wenye mapenzi na Mwenyezi Mungu, humo wanachuma rehema za Mwenyezi Mungu na kupata faida ya Pepo.” 196 Na pia kuna Hadithi isemayo kwamba: “Dunia ni shamba la akhera.”197 Imeshabihishwa hivi kwa kumaanisha kwamba ni mahala pa kujikusanyia thawabu kwa kufanya matendo mema, na malipo makubwa ya kazi hiyo yanatoka kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama. Kwa kweli biashara wanayoifanya Waumini katika dunia hii ni kumuuzia Mwenyezi Mungu vitu vyao visivyo na thamani mbele Yake, lakini malipo anayoyatoa katika manunuzi ni makubwa kiasi cha kutoweza kufikirika katika akili ya mwanadamu, kwani biashara hii hailengi tu kupata faida za kidunia, bali inalenga mbali zaidi, nako ni kuepukana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na mfano wa maana hii ni tamko lake Mwenyezi Mungu pale aliposema:
ْ ََّإ َّن الله َ اش َت َرىٰ ِم َن ْال ُم ْؤ ِم ِن ين أَ ْن ُف َس ُه ْم َوأَ ْم َوالَ ُه ْم ِبأَ َّن لَ ُه ُم ِ ُ ُ ُ ْ َّلله ْ ْ َ َ َ ون َويُق َتل َ يل ا ِ َف َيقتُل َ ال َجنَّة ي َُقا ِتل ون َو ْع ًدا َعل ْي ِه ِ ون ِفي َس ِب 196 197
Imamu Ali (a.s.),Nahjul Balaghah, Jz.4, Uk.32 Almajlisiy, Usulul Kafiy, Jz.68, Uk. 225 389
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 389
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
ُ يل َو ْال ر ق ْ َِّآن َو َم ْن أَ ْو َفىٰ ِب َع ْه ِد ِه ِم َن الله ِ َح ًّقا ِفي التَّ ْو َرا ِة َوالإْ ِ ْن ِج ِ ْش ُروا ِب َب ْي ِع ُك ُم الَّ ِذي َبا َيعْتُ ْم ِب ِه َو َذٰلِ َك ُه َو ْال َف ْو ُز ْال َع ِظي ُم ْ َف ِ اس َتب “Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba wao wapate Pepo, wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo wanaua na kuuawa. Ni ahadi aliyojilazimisha kwa haki katika Tawrat na Injil na Qur’ani. Na ni nani atekelezaye zaidi ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliofanya Naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.” (Qur’ani 9:111)
390
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 390
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI NA NNE
َ ار اللهَِّ َك َما َق ُ يسى اب َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ْن َم ْر َي َم َص َ ين آ َمنُوا ُكونُوا أَ ْن َ ال ِع ْ ال ِْل َ صاري إلَى اللهَِّ َق ْ َِّين َم ْن أ َ اري َ ار و ح ال ن ي ار و ح ل ُص َ َ َ ُّون َن ْح ُن أَ ْن َ َ َ ِ ِ ِ ِ َ َّ ٌ ٌ َ َ َ َ اللهَِّ َفآ َم َن ْت طا ِئ َفة ِم ْن َب ِني إِ ْس َرا ِئيل َو َك َف َر ْت طا ِئ َفة َفأيَّ ْد َنا ال ِذ ين َ اه ِر ين ْ َآ َمنُوا َعلَىٰ َع ُد ِّو ِه ْم َفأ ِ ص َب ُحوا َظ “Enyi mlioamini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyosema Isa bin Maryam kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu! Basi taifa moja la Wana wa Israili liliamini, na taifa jingine lilikufuru. Ndipo tukawaunga mkono walioamini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.” (Qur’ani 61:14)
MAELEZO Aya hii ambayo ni Aya ya mwisho katika Surat Saffu inazungumzia juu ya suala la Jihadi kama ilivyokuwa katika Aya za mwanzoni mwa Sura hii, isipokuwa napo hapa Mwenyezi Mungu ametumia utaratibu mwingine wa kufikisha ujumbe huo, Aya inaanza kwa kusema. “Enyi mlioamini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu.” Ni fakhari kubwa kwa Muumini kujipamba na sifa hii, kwani ni kujitegemeza kwa Yule Mwenye nguvu asiye shindika. Mola Huyu mwenye kila aina ya uwezo anawataka waja Wake wamnusuru na kumsaidia katika kuisimamisha Dini Yake, kwa kweli fakhari hii haina mfano wake. Licha ya kwamba makusudio yake ni kumnusuru Mtume (s.a.w.w.), lakini katika kufanya hivyo ni kumnusuru Mwenyezi Mungu, na kimsingi huu ni upeo wa mbali sana wa rehema Zake kwa waja Wake wenye kumwamini Yeye. Baada ya hapo Mwenyezi Mungu anaweka wazi mfano wa kihistoria, kuonesha ya kwamba Njia hii tukufu ya kuipigania Dini Yake haikukosa watu waliokuwa na hamu na hamasa ya hali ya juu katika kuiandama, anasema: “Kama alivyosema Isa bin Maryam kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu?” Kwa ujasiri mkubwa na ufakhari usio na kikomo wanafunzi hao walieleza kwa moyo safi kwamba wao wako tayari kutoa 391
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 391
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
kila walichonacho ili kuona Dini ya Mwenyezi Mungu inasimama katika jamii. Aya inaeleza juu ya hilo kwa kusema: “Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu!” Kwa kweli walikuwa kama walivyosema, walibeba bendera ya kheri na uongofu na kuisimika katika nafsi zao kabla ya kufanya hivyo kwa wengine. Waliweza kupambana dhidi ya maadui wa haki na wale walioukataa Ujumbe aliokuja nao Nabii Isa (a.s.), kama Aya inavyoendelea kusema: “Basi taifa moja la Wana wa Israili liliamini, na taifa jingine lilikufuru.” Hapa ndipo ambapo msaada wa Mwenyezi Mungu unapowafika wale waliojitolea kuwa wasaidizi wa kuifikisha Dini hiyo pale panapostahiki. Mwenyezi Mungu anasema: “Ndipo tukawaunga mkono walioamini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.” Mwenyezi Mungu anawaambia Waumini kwamba: Hata nyinyi wanafunzi na Maswahaba wa Muhammad, nafasi hii tukufu na yenye heshima mnaweza kuipata, kwa sharti muwe kama vile walivyokuwa wanafunzi wa Nabii Isa, Mwenyezi Mungu atakunusuruni, atakusaidieni katika kuwashinda maadui zenu, na nyinyi ndio mtakaoibuka washindi. Ahadi hii yenye fakhari ya aina yake haiwahusu Maswahaba peke yao, bali ni kwa kila Muumuni mwenye kuitikia wito huu na kupita pale walipopita wanafunzi wa Nabii Isa (a.s.), kwa kujitolea katika kuisimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu. Jambo la msingi kwa Mwislamu ni kutokukata tamaa kwani ahadi ya ushindi imetolewa na Mwenyezi Mungu, ikiwa tu masharti ya kutenda kazi hiyo yatatimizwa. Ni Akina Nani Hao Wanafunzi Wa Nabii Isa (a.s.)? Neno ‘Hawariyyuuna’ likimaanisha ‘Wanafunzi’ limekuja mara tano katika Qur’ani Tukufu. Neno hili linamaanisha wanafunzi maalumu kumi na mbili wa Nabii Isa (a.s.), majina ya wanafunzi hao yanapatikana katika kitabu cha Bibilia, kwenye Injili ya Luka na Matayo. Asili ya neno hili ni ‘Hawara’ likiwa na maana ya kukoga na kujing’arisha. Wameitwa hivyo kwa sababu nyoyo zao zilikuwa ni safi, kwani walikuwa watiifu wa amri za Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake. Si hayo tu wakati wote walikuwa wakiwalingania wengine kwenye Dini sahihi ya Mwenyezi Mungu ili nao wafikie kwenye usafi huo, kwani Nabii Isa (a.s.) alikuwa akiwatuma sehemu mbalimbali kwa ajili ya kufikisha Ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu, na wao walikuwa tayari wakati wote kujitolea katika kazi hiyo tukufu, pia walikuwa ni watu waliokuwa na mapenzi makubwa kwa Nabii Isa (a.s.) kwa kufuata kila analowaamrisha. Wanafunzi hao kwa ujumla wao walibakia katika utiifu hadi mwisho wa maisha yao, isipokuwa mmoja tu, ambaye alikuwa akiitwa Yuda Askariyoti. Huyu 392
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 392
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
alifukuzwa na Nabii Isa, na mwisho alimfanyia usaliti. Katika kuonesha umuhimu na ubora wa wanafunzi hao, siku ambayo Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa sehemu iitwayo Aqaba aliwaambia Maswahaba zake hapo: “Nendeni, na mchague watu kumi na mbili miongoni mwenu, ili wawe wasimamizi wa mambo ya watu wao, kama vile walivyokuwa wanafunzi kwa Nabii Isa.�198
198
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz. 18, Uk. 311 393
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 393
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI NA TANO
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اس َع ْوا َّ ِين آ َمنُوا إِ َذا نُو ِد َي ل ْ لص اَل ِة ِم ْن َي ْو ِم ْال ُج ُم َع ِة َف َ ْر لَ ُك ْم إِ ْن ُك ْنتُ ْم َتعْلَ ُم ون َفإِ َذا ٌ ْع َذٰلِ ُك ْم َخي َ إِلَىٰ ِذ ْك ِر اللهَِّ َو َذ ُروا ْال َبي َ ْالص اَل ُة َفا ْن َت ِش ُروا ِفي أ ُ ْ ض َوا ْب َت ُغوا ِم ْن َف ر ال ت ي ض ق ْ َّ َ َِّض ِل الله ِ ِ ِ َ َ َ َ َ يرا لَ َعلَّ ُك ْم تُ ْفلِ ُح ار ًة أ ْو ل ْه ًوا ً َو ْاذ ُك ُروا اللهََّ َك ِث َ ون َوإِذا َرأ ْوا ِت َج َّ َ ضوا إلَ ْي َها َو َت َر ُك َْ ْو ٌ وك َقا ِئ ًما ُق ْل َما ِع ْن َد اللهَِّ َخي ِ ْر ِم َن الله ِ ُّ انف َُّار ِة َوالله َ َ از ِق ين الر ْر ي خ َّ ُ َ َو ِم َن التِّ َج ِ “Enyi mlioamini! Ikinadiwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, kama mnajua. Na itakapokwisha Swala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu; na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufaulu. Na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.” (Qur’ani 62:9-11)
SABABU YA KUTEREMKA Kumeelezwa sababu ya kuteremka Aya hizi, na hasa Aya ya mwisho kati ya hizi ya kwamba, kuna kipindi mji wa Madina ulisibiwa na uhaba wa chakula, na kile kilchokuwepo kilipanda bei sana, siku moja Dayhat ibn Khalifa aliingia Madina akitokea Sham huku akiwa na bidhaa ya mafuta, na wakati huo Mtume (s.a.w.w.) akiwa anakhutubu siku ya Ijumaa. Watu waliokuwemo msiktini walitoka kufuatia bidhaa hiyo ili wasije wakaikosa, na ni watu wachache tu waliobakia msikitini pamoja na Mtume (s.a.w.w.), na hapo Aya ikateremka ili kuwakataza tabia yao hiyo. Na baada ya kitendo chao hicho cha kutoka na kufuata biashara, Mtume (s.a.w.w.) alisema:
394
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 394
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
والذي نفسي بيده لو تتابعتم حتّى ال يبقى أحد منكم لسال بكم .الوادى نارا “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mkononi Mwake, lau mngetoka nyote na asibakie mtu, jangwa lingewamiminia moto.”
Na siku nyingine ilisadifu siku ya Ijumaa Mtume (s.a.w.w.) akiwa amesimama akitoa khutba, aliwasili tena Dayhat ibn Khalifa akitokea Sham na bidhaa mbalimbali za chakula, na alipofika sokoni akapiga ngoma kwa lengo la kuwataarifu wateja waende wakanunue, zama hizo Dayhat alikuwa bado hajaingia katika Uislamu. Watu waliokuwemo msikitini walitoka na kubakia kumi na wawili tu, hapo Mtume (s.a.w.w.) akasema:
.لو ال هؤالء لسومت عليهم الحجارة من السماء “Lau kama si hawa waliobakia, wengeteremshiwa mawe kutoka mbinguni”
Hapo ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii.199
MAELEZO Mkusanyiko Mkubwa wa Kisiasa Kila Wiki: Swala ya Ijumaa ni moja kati ya mambo yanayoleta utulivu katika imani za Waislamu, na pia katika maisha yao ya kila siku. Aya inaanza kuwataka Waumini kwa ujumla wao kutekeleza wajibu huo mara tu wasikiapo muadhini akiadhini kuwaita watu kwenye Swala hiyo, inasema: “Enyi mlioamini! Ikinadiwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, kama mnajua.” Baada ya mwadhini kuadhini ni wajibu kwa Waumini kuacha shughuli zao za kimaisha na kuelekea kwenye Swala hiyo ambayo ni ukumbusho mkubwa wa kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na huko kuelekea kwenye Swala ya Ijumaa ni bora na ni jambo lenye manufaa zaidi kuliko kuendelea na harakati za kimaisha kwa lengo la kujiongezea kipato kisicho cha kudumu. Ni wazi kwamba, kukatazwa kuuza na kununua baada ya adhana ya Swala ya Ijumaa haimaanishi mambo hayo mawili tu, bali kila jambo lenye kumshughulisha mtu na hatimaye kuikosa Swala 199
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.18, Uk.332 395
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 395
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
hiyo. Msisitizo huu wa kukimbilia katika Swala uko hata katika Swala nyingine kama riwaya zinavyosema, miongoni mwa hizo ni riwaya ifuatayo:
الصالة فال تأتوها وأنتم تسعون وأتوها وأنتم ّ إذا أقيمت ...السكينة ّ تمشون وعليكم “Pindi inapokimiwa Swala msiiendee katika hali ya kuharakisha, bali iendeeni huku mnatembea, na jilazimisheni kuiendea kwa upole…”200
Riwaya hii inatufunza kufika mapema msikitini, kwa kufanya hivyo haya yaliokatazwa hayatatokea, kwani Swala itakimiwa wakati kila mmoja akiwa tayari ameshakaa sehemu yake. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu kuhimiza kuharakisha kwenda kwenye Swala ya Ijumaa ni kuonesha umuhimu wa pekee wa Swala hii kwa Waislamu, hasa ikizingatiwa Swala hii hutanguliwa na khutba mbili kabla ya kuswaliwa, khutba ambazo zinatakiwa ziwakumbushe watu kumcha Mwenyezi Mungu na wajibu mwingine, kuwazindua watu, hasa wale walioghafilika na kusahau wajibu wao, na pia zizungumzie mustakabali wa Uislamu na Waislamu n.k. Ama baada ya kumalizika kwa ibada hii, hapo Waislamu wanaruhusiwa kurudi katika harakati zao mbalimbali za maisha ya kila siku: “Na itakapokwisha Swala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu; na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufaulu.” Ni jambo la wazi kwamba kutawanyika katika ardhi kwa lengo la kutafuta riziki baada ya Swala ya Ijumaa si jambo la wajibu, licha ya kuwa ni jambo la msingi katika maisha. Hapa Aya haimaanishi ya kwamba ni lazima watu wakatafute riziki, bali ni ruhusa kufanya hivyo kwa anayependa, baada ya kitendo hicho kuharamishwa baada ya kunadiwa Swala. Ama kuendelea kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni jambo la wajibu katika hali yote atakayokuwa nayo Mwislamu, ikiwa ni katika Swala au katika harakati za kujitafutia maisha, kwa maana kuitafuta riziki katika misingi iliyowekwa na Uislamu, kwa kujiepusha na mambo ya haramu, kama vile wizi, utapeli, ufisadi na mengineyo. Kumkumbuka Mwenyezi Mungu mara kwa mara kunajenga hali ya uchamungu katika nafsi ya mwanadamu na kumweka mbali na maasi, na hiyo ndio njia yenye mafanikio kwa Mwislamu. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamalizia Aya kwa kusema: “…ili mpate kufaulu.” 200
Bukhariy, Sahihul Bukhariy, Jz. 1, Uk. 218 396
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 396
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
Aya ya mwisho, Aya ambayo ndio chanzo cha kuteremka Aya hizi, inawakaripia wale ambao walitoka kwenda kufuata bidhaa huku wakimwacha Mtume (s.a.w.w.) akiwa katika mimbari akikhutubu: “Na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama.” Lakini Mwenyezi Mungu akamtaka Mtume wake awaeleze kwamba wito wa Mwenyezi Mungu wa kuwaita waja Wake kwenye ibada ya Swala ni bora kuliko huo wito wa wafanyabiashara: “Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.” Ni jambo la wazi kwamba kuhudhuria Swala ya Ijumaa na kusikiliza mawaidha kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) ni jambo ambalo halilingani kwa ubora na jambo jingine lolote lile. Na ikiwa kuna wale wanaodhani ya kwamba riziki yao hawatoipata, basi wako kwenye makosa kwa kudhania kwao hivyo, kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa watoao riziki. Ilikuwa ni kawaida kwa Mtume (s.a.w.w.) kutoa khutba ya Swala ya Ijumaa akiwa amesimama, kama anavyosimulia Jabir ibn Abdillahi al-Ansariy akisema: “Katu sijawahi kumuona Mtume (s.a.w.w.) akitoa khutba huku akiwa ameketi kitako, na yeyote atakayewaambia kwamba alikuwa akitoa khutba na huku ameketi kitako basi msimwamini.” Na katika riwaya nyingine inasema kwamba, siku moja Abdallah ibn Mas’ud aliulizwa: “Je Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitoa khutba akiwa amesimama?” Alijibu kwa kusema: “Ndiyo, je hamjasikia kauli yake Mwenyezi Mungu pale aliposema: “Na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama.” Jambo la kusimama wakati wa kutoa khutba limekuwa ni jambo la wajibu kwa mwenye kutoa khutba ya Ijumaa, na jambo hilo lilifanywa na Maswahaba wote waliokuja baada ya Mtume (s.a.w.w.) na kuendelezwa na khatibu wa khutba ya Swala ya Ijumaa, ila ni mtu mmoja katika historia ya Uislamu aliyekhalifu mwenendo huu, na mtu huyo ni Muawiya ibn Abi Sufiyani, pale alipokuwa mtawala (mfalme) wa Waislamu, alionekana katika baadhi ya siku akitoa khutba huku akiwa amekaa kitako!201
UTAFITI Swala ya Mwanzo ya Ijumaa Katika Uislamu: Imepokewa kwamba, kabla ya Mtume (s.a.w.w.) kuhamia Madina, Waislamu wa huko walikuwa wakizungumza wao kwa wao kwa kusema: “Mayahudi wanasiku yao maalumu wanayokusanyika na kufanya ibada kwa pamoja, ambayo ni siku ya Jumamosi, na Manasara nao wanakusanyika kufanya ibada kwa pamoja siku ya Jumapili, 201
Suyutiy, Durrul Manthur, Jz.6, Uk.222 397
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 397
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
basi ni kwa nini na sisi hatuchagui siku yetu ambayo itakuwa ni siku ya kukusanyika, na siku hiyo iwe ni kabla ya siku ya Jumamosi, (siku hiyo ilikuwa ikijulikana katika zama hizo siku ya al-Ghuruba) kwa lengo la kufanya ibada na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi zaidi? Baada ya kuwafikiana juu ya hilo, walikwenda kwa mmoja kati ya watu waliokuwa wanaheshimika sana, aliyekuwa anajulikana kwa jina la As’ad ibn Zurara ili aongoze ibada hiyo, As’ad alifanya hivyo, walikusanyika nakuswali Swala ya jamaa na kuwatolea mawaidha, kisha akawataka wachinje kondoo kwa ajili ya chakula cha mchana na usiku kwa Waislamu. Hii ndio iliyokuwa Ijumaa ya mwanzo katika Uislamu. Ama Ijumaa ya mwanzo kuswaliwa na Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Maswahaba zake ilikuwa ni baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuwasili Madina na kutoa khutba yake ambayo ndio ya kwanza kuitoa katika mji huo. Umuhimu wa Swala ya Ijumaa: Dalili ya wazi juu ya ubora na umuhimu wa Swala ya Ijumaa unaonekana katika Aya hizi ambazo tumeshazitolea ufafanuzi, kwani Mwenyezi Mungu anawataka Waumini wote kuacha shughuli zote hata kama ni za kujitafutia riziki kwa ajili ya kujikimu na familia zao mara tu wanapomsikia muadhini wa Swala ya Ijumaa. Na pia imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:
ّ فمن تركها في حياتي أو,إن اهلل تعالى فرض عليكم الجمعة فال جمع اهلل شمله وال,بعد موتي إستخفافا بها أو جحودا لها أال وال, أال والزكاة له, أال وال صالة له,بارك له في أمره . حتّى يتوب,بر له ّ أال وال, أال وال صوم له,حج له ّ “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu, amewafaradhishieni Swala ya Ijumaa, basi mwenye kuiacha katika uhai wangu au baada ya kufa kwangu kwa kuidharau au kuipinga kabisa, Mwenyezi Mungu hatomkusanyia mtu huyo mambo yake na wala hatombariki katika mambo yake, na tambueni ya kwamba mtu huyo atakuwa hana Swala, na tambueni ya kwamba mtu huyo atakuwa hana Zaka, na tambueni ya kwamba mtu huyo atakuwa hana Hijja, na tambueni ya kwamba mtu huyo atakuwa hana Funga, na tambueni ya kwamba mtu huyo atakuwa hana wema wowote ule, mpaka pale atakapotubia.”202 202
Hurrul Amiliy, Wasailus-Shia, Jz.7, Uk.302 398
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 398
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
Riwaya nyingine inayoelezea umuhimu wa Swala ya Ijumaa ni ile inayosema kwamba siku moja Mtume (s.a.w.w.) aliendewa na mtu na kusema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimejiandaa siku nyingi kwa ajili ya ibada ya Hijja, lakini sijawafikishwa (sijaweza kukamilisha gharama zake)!” Mtume (s.a.w.w.) alimwambia mtu huyo:
.حج المساكين ّ عليك بالجمعة فإنّها “Jilazimishe kuswali Swala ya Ijumaa, kwani hiyo ni Hijja ya masikini.”203
Hii ni kwa sababu ule umuhimu wa Waislamu kukusanyika pamoja katika ibada ya Hijja na faida zinazopatikana, mambo hayo pia yanapatikana katika mjumuiko wa Swala ya Ijumaa. Na pia kuna riwaya mbalimbali zinazoelezea kwamba yule mwenye kuacha Swala ya Ijumaa huwa katika daraja pamoja na wanafiki, pale ambapo Swala hiyo ni wajibu wa kipekee, ama katika zama hizi za kughibu kwa Imamu Mahdi, Swala hii ni wajibu wa hiyari, kwa Mwislamu kuchagua kati ya kuswali Swala ya Ijumaa au Swala ya Adhuhuri. Hekima ya Swala ya Ijumaa: Swala ya Ijumaa ni ibada yenye faida kubwa kwa Waislamu kwa kule kuwajumuisha pamoja, kwani huonesha roho ya umoja na upendo kati yao, na pia ni kinga kubwa ya maasi, kwa vile kunakuwa na ukumbusho kila wiki kwa kupitia khutba mbili za Swala hiyo zinazowahimiza Waislamu kumcha Mwenyezi Mungu. Ama kuhusiana na mambo yanayowahusu Waislamu katika maisha yao ya kijamii, kiuchimi na kisiasa, Swala ya Ijumaa ni mkusanyiko mkubwa wa pili baada ya mkusanyiko wa ibada ya Hijja, kama tulivyoona katika riwaya iliyotangulia, Mtume (s.a.w.w.) akieleza ya kwamba Swala ya Ijumaa ni Hijja kwa yule asiye na uwezo wa kwenda kufanya ibada ya Hijja kwenye mji wa Makka. Mkusanyiko unaochukua nafasi ya tatu kwa Waislamu ni ule mkusanyiko wa kila siku katika kuswali Swala tano za wajibu. Swala ya Ijumaa ina nafasi kubwa kwa Waislamu, ikiwa makhatibu pamoja na mambo mengine watazungumzia masuala yanayoigusa jamii, kama vile uchumi, siasa, tabia n.k., kwa kufanya hivyo mkusanyiko huu utakuwa na baraka na kheri nyingi, kama zifuatazo:
203
1.
Kuthibisha umoja kati ya Waislamu, jambo ambalo litawatia khofu maadui.
2.
Kuhuisha mambo ya kiroho kwa Waislamu.
Kitabu kilichotangulia, Uk.300 399
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 399
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
3.
Kupatikana njia ya Waislamu kusaidiana katika kutatua kero zao.
4.
Kuwaamsha watu katika kutekeleza mafunzo ya Uislamu, na kujua haki zao za kijamii na kisiasa.
Kwa kutekelezwa haya, siku zote maadui wa Uislamu na wale wa ubinadamu wataingiwa na khofu kila Siku ya Ijumaa inapowasili. Mambo haya ndio yaliyoifanya serikali ya Kiislamu iliyokuwa ikiongozwa na Mtume (s.a.w.w.) kuwa na nguvu za kuweza kuziporomosha dola kubwa, na hata dola za kifisadi zilizokuwa zikiongozwa na baadhi ya Waislamu, kama vile dola ya Bani Umayya. Kwa maana hii ndio ikawa uasi wa mwanzo dhidi ya serikali za kidhalimu katika historia ya Uislamu uliokuwa ukiongozwa na Maimamu Maasumu ulikuwa ukianzia kuwakataza watu kuswali nyuma ya maimamu walioteuliwa na viongozi wa serikali hizo. Kwa mfano katika tukio la Ashura, baadhi ya mashia walikusanyika kwenye nyumba ya Sulayman ibn Sard na kukubaliana kumwandikia barua Imamu Husein. Barua hiyo ilikuwa ikisema kama ifuatavyo: “… na Nuuman ibn Bashir yuko kwenye kasri ya mfalme, sisi hatutokusanyika naye katika Swala ya Ijumaa, wala hatutotoka naye kwenda kwenye Swala ya Idi, na lau tungejua ya kwamba wewe umetoka kutujia, basi tungemtoa ili ukutane naye katika mji wa Sham…”204 Na Imamu Sajjad (a.s.) anasema hivi katika katika Sahifa yake:
ّ الله ّم إن هذا المقام لخلفائك وأصفيائك ومواضع أمنائك في .الرفيعة الّتي اختصصتهم بها قد ابتزوها ّ ال ّدرجة “Ewe Mola wangu, nafasi hii ni ya Makhalifa wako na Wateule wako, na pahala pa Waaminifu wako walioko katika daraja ya juu, ni pahala ulipowachagulia wao tu, lakini (watawala madhalimu) wamepora mahali hapo.”
Katika khutba ya Ijumaa inapaswa Waislamu waelezwe mikakati yote iliyoelekezwa juu yao ili kumfanya adui ahisi amefeli katika njama zake dhidi yao. Na katika kuonesha hekima ya Swala hii, tunaona katika Fiqhi ya Ahlulbayt (a.s.) imebainisha kwamba haifai kusimamishwa zaidi ya Swala moja ya Ijumaa ikiwa masafa ya Swala moja na nyingine ni chini ya farsakh moja, kama ambavyo mtu aliye umbali wa farsakhi mbili (Kilomita kumi na moja) anaweza kuhudhuria Swala ya Ijumaa. Kwa hivyo Swala za Ijumaa, zinazosaliwa nchini ya kilomita moja hazisihi, na ile itakayoanza mwanzo ndio yenye kusihi. Hii yote ni kwa ajili ya kupatikana kwa lengo la mkusanyiko wa 204
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.18, Uk.341 400
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 400
12/8/2014 2:43:50 PM
WITO KWA WAUMINI
Siku hiyo tukufu katika siku za wiki. Kwa masikitiko makubwa yenye kuhuzunisha nyoyo, mkutano huu wa Waislamu wa kila wiki, umehodhiwa na baadhi ya watawala katika nchi nyingi za Waislamu, kiasi cha kuifanya ibada hii kupoteza malengo yake, na badala yake imekuwa ni siku ya kujikosha watawala hao na kusifiwa kwa sifa wasizostahiki. Na kibaya zaidi huteuliwa mashekhe wa kupanga khutba na kupitiwa kabla ya kusambazwa katika misikiti! Miongoni mwa mambo muhimu zaidi katika Swala za Ijumaa katika mwaka mzima ni ile Swala iswaliwayo siku ya Arafa. Ni Swala ambayo huhudhuriwa na idadi kubwa zaidi ya waumini, ya laiti lau kama mkusanyiko huo wa watu utatumika vizuri katika kuwazindua Waislamu katika mambo yahusianayo na Dini yao pamoja na mustakabali wa maisha yao katika nyanja mbalimbali kama vile kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k. basi utaleta mafanikio makubwa katika umma. Kwa hakika inapasa kila mwenye uchungu na Dini hii kulia kutokana na upotoshwaji wa makusudi wa hazina hii ya Kiislamu, hazina iliyobeba mambo ya kiroho na ya kimwili, kwa hivyo kama vile Mwenyezi Mungu alivyowataka kukimbilia kwenye Swala ya Ijumaa, basi kuna haja ya kufanya haraka zaidi katika kuirudisha Swala hiyo katika uhalisia wake ili malengo yatimie. Adabu ya Swala ya Ijumaa na Khutba Mbili: Baada ya kukamilika masharti ya Swala ya Ijumaa, hapo itawajibika kwa kila mwanamume aliyefikia umri wa kubaleghe kuiswali Swala hii ikiwa atakuwa na uwezo wa kuhudhuria, na si wajibu kwa wazee wasiojiweza, wasafiri na wanawake. Idadi ya chini kabisa ya washiriki ni wanaume watano walio na wajibu wa kuiswali Swala hiyo. Swala ya Ijumaa ina rakaa mbili, ikitanguliwa na khutba mbili. Ni mustahabu (vizuri) kwa imamu kudhihirisha sauti wakati wa kusoma Suratul-Fatiha na Sura nyingine. Ni vizuri zaidi kusoma Suratul- Jumaa katika rakaa ya kwanza baada ya Suratul- Fatiha, na katika rakaa ya pili Suratul- Munafiqun. Pia ni mustahabu kuleta kunuti katika rakaa ya kwanza kabla ya kurukuu na katika rakaa ya pili baada ya kurukuu. Ni wajibu kusomwa khutba mbili kabla ya Swala hali ya kusimama, na khutba itolewe na mtu ambaye ataongoza Swala. Ni wajibu kwa khatibu kunyanyua sauti wakati wa khutba, ili wasikie waliohudhuria na kuifahamu. Na kwa waliohudhuria wanapaswa kukaa kimya na kumsikilza khatibu katika hali ya kumuelekea khatibu. Inapasa kwa khatibu kuwa na uwezo wa kuzungumza kwa umakini na ufasaha, na kujua mahitajio ya watu na shida zao na kuwaelekeza namna ya kuzitatua shida hizo. Na ni wajibu awe na mwenendo wenye kuwavutia watu wanaomzunguka, huku khutba yake 401
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 401
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
ikiwa inawaelekeza watu kushikamana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kuachana na makatazo yake. Na katika jambo la kupendeza zaidi kwa khatibu ni kuvaa mavazi nadhifu na yaliyo mazuri zaidi, na kujipaka manukato, akiwa ni mwenye kuelekea msikitini kwa upole na utulivu, na baada tu ya kupanda mimbari aanze kuwatolea salamu Waumini waliohudhuria Swala, huku akiwa amesimama akiwaelekea, na kushika upanga au fimbo, na baada ya kumaliza adhana aanze kutoa khutba yake. Khutba ianze kwa kumsifu Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.) na kuwausia watu kumcha Mwenyezi Mungu, na kusoma sura moja miongoni mwa Sura fupi, na namna hii hii afanye katika khutba ya pili, ila ataongezea kuwaswalia Maimamu Watoharifu baada ya kumswalia Mtume (s.a.w.w.) na kuwaombea msamaha Waumini wanawake na wanaume na dua nyingine mbalimbali. Jambo la msingi kwa khatibu katika khutba zake ni kuyapa kipaumbele zaidi mambo yanayoihusu jamii katika nyanja ya Dini na mambo ya kidunia. Na kuwazindua juu ya mikakati ya maadui dhidi ya Uislamu na Waislamu na namna ya kukabiliana nayo. Kwa kufanya hivi ndipo lengo la kufaradhwisha Swala hii litakapopatikana, kama Imamu Ridha anavyosema: “Kwa hakika pamewekwa khutba siku ya Ijumaa, kwa vile ni siku ya mkusanyiko wa watu, kwa hiyo kiongozi apate fursa ya kuwatolea mawaidha na kuwahimiza katika kumtii Mwenyezi Mungu na kuwakataza kutenda maovu, na kuwaeleza yale yaliyo na manufaa katika Dini yao na dunia yao, na awape habari za yale yaliyojiri kwao, yale yenye manufaa na madhara‌ Kwa hakika khutba mbili zimewekwa ili kwenye khutba hizo asifiwe Mwenyezi Mungu na kutakaswa pamoja na kutukuzwa, na pia kwa ajili ya kuomba haja mbalimbali na kuwaonya watu na kuwaombea dua na kuelezwa yale ambayo ni mazuri yenye maslahi kwao na yale yaliyo mabaya ambayo yanamadhara. Masharti ya Swala ya Ijumaa: Miongoni mwa masharti ni kwa imamu kutimiza masharti kama yalivyo kwa Swala nyingine, kama vile uadilifu na mengineyo. Baadhi ya wanachuoni wanaona kwamba Swala hii si wajibu wa kipekee katika zama ambazo Imamu Maasumu yuko ughaibuni, na badala yake inakuwa ni wajibu wa hiyari, kwa mtu kuamua kuswali Swala ua Ijumaa au Swala ya Adhuhuri, kwani kuwepo kwake ndiko lengo la Swala hii linapokamilika, na kuhusiana na hili kuna kauli mbalimbali za wanachuoni, kwa zaidi utaweza kuyapata maelezo katika vitabu maalumu vya Fiqhi ya Uislamu.205
205
Shiraziy, Tafsirul Amthal, Jz.18, Uk.344 402
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 402
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI NA SITA
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين آ َمنُوا اَل تُ ْل ِه ُك ْم أَ ْم َوالُ ُك ْم َو اَل أَ ْو اَل ُد ُك ْم َع ْن ِذ ْك ِر َ اس ُر ون َوأَ ْن ِف ُقوا ِم ْن َما ِ اللهَِّ َو َم ْن َي ْف َع ْل َ ٰذلِ َك فأوالئك ُه ُم ْال َخ ُ ْ َ ْل أَ ْن َي ْأ ِت َي أَ َح َد ُك ُم ْال َم ْو ُت َف َي ُق ول َر ِّب لَ ْو اَل ِ َر َزق َناك ْم ِم ْن َقب َ َ َ الصالِ ِح ين َولَ ْن َّ ص َّد َق َوأَ ُك ْن ِم َن َّ َيب َفأ ٍ أ َّخ ْر َت ِني إِلَىٰ أ َج ٍل َق ِر َ ُير ِب َما َت ْع َمل ون ٌ يُ َؤ ِّخ َر اللهَُّ َن ْف ًسا إِ َذا َجا َء أَ َجلُ َها َواللهَُّ َخ ِب “Enyi mlioamini! Zisiwashughulishe mali zenu, wala watoto wenu, kuacha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio wenye hasara. Na toeni katika tulichowapa kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, kisha aseme: Mola Wangu! Mbona hukuniakhirishia muda kidogo nikatoa sadaka, na kuwa katika watu wema? Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapofika ajali yake; na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.” (Qur’ani 63: 9-11)
MAELEZO Kupenda dunia na mali kupita kiasi ni miongoni mwa sababu kubwa zinazomfanya mtu kuwa mnafiki. kutokana na hali hii, ndio maana Mwenyezi Mungu akawa anawatahadharisha Waumini sana dhidi ya kutumbukia katika shimo hili lenye hatari kubwa kwa maisha ya mwanadamu hapa duniani na mustakabali wake, anaanza kama Aya isemavyo: “Enyi mlioamini! Zisiwashughulishe mali zenu, wala watoto wenu, kuacha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio wenye hasara.” Licha ya kwamba mali na watoto ni miongoni mwa mambo ambayo mtu anaweza kuyatumia katika kumtii Mwenyezi Mungu na kupata radhi zake, lakini inayumkinika mambo hayo yakawa ni kizuizi kikubwa kinachomzuia mwanadamu dhidi ya Mola Wake Muumba ikiwa hatochukua tahadhari ya hali ya juu katika kuamilia nayo. Bila tahadhari katika kuamiliana na hayo, kunamfanya mwanadamu kusahau lengo lake la kuletwa hapa duniani na badala yake hujiingiza katika maasi na ufisadi wa kila aina na hatima yake ni kuondoka hapa duniani na kuelekea akhera akiwa hana wema wowote alioufanya utakaomsaidia huko. Kwa kweli hiyo ndio hasara kubwa 403
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 403
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
atakayoipata, kwani baada ya watu kufufuliwa wataishi maisha yasiyo na mwisho, na wala hakutakuwa na namna yoyote ile ya kufanya ili kuepukana na adhabu ya milele. Aya inayofuata inawataka Waumini watoe vile walivyoruzukiwa na Mola Wao, ili iwe ni moja kati ya sababu za kuokoka na adhabu ya Siku ya Kiyama, inasema: “Na toeni katika tulichowapa kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, kisha aseme: Mola Wangu! Mbona hukuniakhirishia muda kidogo nikatoa sadaka, na kuwa katika watu wema?” Amri ya utoaji katika Aya hii inajumuisha aina zote za utoaji, ikiwa ni utowaji ulio wajibu au ule usio wa wajibu (Mustahabbu). Utoaji wa aina mbalimbali za mali ni katika mambo yenye manufaa kwa mtoaji kabla ya kuwa na manufaa kwa mpewaji, na hilo atalitambua zaidi yule aliyejizuia kutoa, kwani wakati wa kuiaga dunia utakapomfikia atasema: “Mola Wangu! Mbona hukuniakhirishia muda kidogo nikatoa sadaka, na kuwa katika watu wema?” Kwa hiyo hakuna haja kwa Muumini kuwa bahili kwa kuwanyima wengine kile ambacho Mwenyezi Mungu amekipitisha kwake ili awape wengine. Kuna idadi kubwa ya watu wanaosibiwa na mshituko na fazaa kubwa pindi safari ya kuelekea akhera inapowadia. Hii ni kutokana na utajiri mkubwa walionao, utajiri ambao hawakuutumia katika njia inayostahiki kisheria, ilikuweza kuendelea kustarehe katika safari yake hiyo anayokwenda. Wakati huo anachokifanya ni kuomba kupatiwa fursa ya kuweza kuendelea kuishi japo kwa muda mfupi ili ayafanye yale yote ambayo kwa muda wa maisha yake marefu hakutaka kuyafanya. Lakini bahati haiji mara mbili, kwani utaratibu ambao Mwenyezi Mungu amejiwekea na kutokwenda kinyume nao, ni pale muda wa mtu wa kuondoka unapofika ni kuondoka tu, kama anavyosema katika Aya ifuatayo: “Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapofika ajali yake.” Na katika Aya nyingine amesema: “
َ اع ًة َو َ َفإ َذا َجاء أَ َجلُ ُه ْم َ ال َي ْس َت ْق ِدم َ ال َي ْس َت ْأ ِخ ُر ُون َ ون َس ِ “Basi utakapofika muda wao huo (wa kuondoka duniani) hawatakawia hata kitambo kidogo na wala hawatatangulia.” (Qur’ani 7:34)
Aya inamalizia kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.” Mwenyezi Mungu ameweka kumbukumbu ya kila alifanyalo mwanadamu, kwa hivyo kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa stahiki yake bila kudhulumiwa.
404
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 404
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
Unafiki wa Kiitikadi na wa Kivitendo: Unafiki unamaana pana sana, kwani unafiki ni kila aina ya jambo linalodhihirishwa ambalo haliendani sawiya na imani iliyoko moyoni, na mfano mzuri ni unafiki wa kiitikadi, kama vile ilivyoelezwa katika Suratul Munafiqun, namna walivyokuwa wakidai ya kwamba wao ni waumini lakini ukweli wa mambo walikuwa wanaficha ukafiri katika vifua vyao, Mwenyezi Mungu anasema:
ُ ون َقالُوا َن ْش َه ُد إنَّ َك لَ َر ُس ُ إ َذا َجا َء َك ْال ُم َنا ِف َ ول اللهَِّ َواللهَُّ َيعْلَ ُم إِنَّ َك ق ِ ِ ْ ُ َُّلله ْ َ َ َ ين لكا ِذب َ لَ َر ُسول ُه َوا َيش َه ُد إِ َّن ال ُم َنا ِف ِق ُون “Wanapokujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa hakika wewe ni Mtume Wake. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanafiki ni waongo.” (Qur’ani; 63:1)
Ama unafiki wa kivitendo ni kule baadhi ya watu kusifika na sifa ya Uislamu, na kufanya baadhi ya matendo yanayothibitisha Uislamu wao, lakini wakati huo huo hufanya matendo mengine yanayokwenda kinyume na imani ya Uislamu, kama vile kusema uongo, kuvunja ahadi, kufanya khiyana baada ya kuaminiwa n.k., kwani imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema:
ّ ثالث من وإن صام وصلّى وزعم أنّه,كن فيه كان منافقا ّ وإذا ح ّدث, من إذا أتمن خان:مسلم . وإذا وعد أخلف,كذب “Mwenye kuwa na mambo matatu ni mnafiki hata kama atafunga na kuswali na kudai ya kwamba yeye ni Mwislamu: Ambaye akiaminiwa hufanya khiyana, na akizungumza husema uongo, na akiahidi hatekelezi ahadi.”206
Na katika riwaya nyingine amesema:
.ما زاد خشوع الجسد على مافي القلب فهو منافق عندنا 206
Hurrul Amiliy, Wasailu Shia, Jz.15, Uk.340 405
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 405
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
“Ambaye atazidisha unyenyekevu wa mwili zaidi ya ule uliomo moyoni, basi mtu huyo ni mnafiki kwetu sisi.”207
Na Imamu Ali (a.s.) naye anasema:
ّ .إن المنافق ينهى وال ينتهى ويأمر بما ال يأتي “Hakika mnafiki anakataza wala yeye hajikatazi, na anaamrisha kile ambacho yeye hakifanyi.”208
Kwa hiyo hata wale wanaokataa kutoa vile walivyopewa na Mola Wao wanaingia katika kundi hili la unafiki wa kivitendo, hata kama watajidhihirisha na matendo mengine yaliyo mema, kwani kinachotakiwa kwa kila mtu baada ya kuamini misingi ya Dini au nguzo za imani ni kutekeleza yale yote yaliyoamrishwa katika Uislamu na kujiweka mbali na kila jambo ovu, Mwenyezi Mungu anasema:
ْ ُوا ا ْد ُخل ْ ُين آ َمن َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ...الس ْل ِم َك َّآف ًة ِّ وا ِفي
“Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu…” (Qur’ani; 2:208)
207 208
Alkafiy, Usulul Kafiy, Jz.2, Uk.369 Kitabu kilichotangulia 406
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 406
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI NA SABA
َ َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اج ُك ْم َوأَ ْو اَل ِد ُك ْم َع ُد ًّوا لَ ُك ْم ِ ين آ َمنُوا إِ َّن ِم ْن أ ْز َو ُ وه ْم َوإ ْن َتع َ ْ َف ور َر ِحي ٌم ٌ ص َف ُحوا َو َت ْغ ِف ُروا َفإِ َّن اللهََّ َغ ُف ْ ْفوا َو َت ِ ُ احذ ُر إِنَّ َما أَ ْم َوالُ ُك ْم َوأَ ْو اَل ُد ُك ْم ِف ْت َن ٌة َواللهَُّ ِع ْن َد ُه أَ ْج ٌر َع ِظي ٌم َفاتَّ ُقوا اللهََّ َما َ ْرا َ َ َ ل ْن ُف ِس ُك ْم َو َم ْن ي ُوق ْ اس َت َطعْتُ ْم َو ْ ِاس َمعُوا َوأ ِطيعُوا َوأ ْن ِف ُقوا َخي ً أ ً ضوا اللهََّ َق ْر ُ ون إِ ْن تُ ْق ِر َ ُش َّح َن ْف ِس ِه فأالئك ُه ُم ْال ُم ْفلِ ُح ضا َح َس ًنا َي ور َحلِي ٌم ٌ اع ْف ُه لَ ُك ْم َو َي ْغ ِف ْر لَ ُك ْم َواللهَُّ َش ُك ِ ُض “Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui zenu. Basi tahadharini nao. Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu. Hakika mali zenu na watoto wenu ni mtihani. Na kwa Mwenyezi Mungu kuna ujira mkubwa. Basi mcheni Mwenyezi Mungu vile muwezavyo, na sikieni, na tiini, na toeni, itakuwa heri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atawazidishia maradufu, na atawaghufiria. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukrani, Mpole.” (Qur’ani 64: 14-17)
MAELEZO Aya ya mwanzo kati ya hizi, inatoa tahadhari kwa Waumini dhidi ya kupenda mali, watoto na wanawake kupita kiasi, mpaka ikawa ni sababu ya kuingia katika kumuasi Mwenyezi Mungu, au kutotekeleza wajibu unaostahiki kutekelezwa. Aya inaanza kwa kusema: “Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui zenu. Basi tahadharini nao.” Kuna mambo mbalimbali yanayodhihirisha uadui huo, kama vile baadhi ya watoto na wake kumzuia baba yao au mume wao asitoke kwenda katika mambo yanayohuwisha Dini, kama vile kushiriki katika Jihadi, kufikisha Ujumbe wa Uislamu n.k. Na baadhi ya wakati uadui huo huufanya kwa mandhari ya kumuonesha mapenzi na kumfanyia huduma mbalimbali. Kwa hiyo Muumini atakapofikiwa na hali hiyo, hakuna haja ya kusitasita, bali analotakiwa ni kufanya yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na kuachana na yale wanayoyataka watu wa familia yake. Kwani yale ya Mwenyezi Mungu ndio yenye kheri na 407
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 407
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
faida kwake hapa duniani na kesho akhera. Hivi ndivyo ambavyo Mwenyezi Mungu anavyotoa tahadhari juu ya jambo hili kwa kupitia Aya hii na kusisitiza katika Aya nyingine, kama ilivyo katika Aya hii ifuatayo:
َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ين آ َمنُوا اَل َتتَّ ِخ ُذوا آ َبا َء ُك ْم َوإِ ْخ َوا َن ُك ْم أَ ْولَِيا َء إِ ِن ْْ ُ ْ َ لإ ان َو َم ْن َي َت َولَّ ُه ْم ِم ْن ُك ْم فأوالئك ُه ُم ْ ِ اس َت َحبُّوا الكف َر َعلى ا ِي َم َّ َ الظالِ ُم ون “Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa mawalii ikiwa wamestahabu kufuru kuliko imani. Na atakayewafanya mawalii katika nyinyi basi hao ndio madhalimu.” (Qur’ani 9:23)
Bila shaka Aya imeweka bayana kwamba si watoto wote au wake wote hufanya hivyo, bali ni baadhi yao. Katika kuzuia muamala mkali na mbaya kwa wanafamilia, baada ya ibara ya mwanzonimwa Aya, ibara inayofuatia Mwenyezi Mungu anataka watu wawe waadilifu kwa familia zao, isiwe ni kutojishughulisha katika kuwapatia mahitaji yao, Aya inaendelea kusema: “Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” Katika tukio la kusingiziwa uovu mke wa Mtume (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu kuwaeleza ubaya wa kitendo chao hicho, baadhi ya Waislamu walikula yamini ya kwamba hawatowapa msaada wowote ule wale walioeneza uzushi huo hata kama ni jamaa zao wa karibu, hapo Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya isemayo:
ْ َو اَل َي ْأ َت ِل أُولُو ْال َف ْ الس َع ِة أَ ْن ي ُٰؤتُوا أُولِي ْال ُق ْر َبى َّ ض ِل ِم ْن ُك ْم َو ْ َ َو ْال َم َسا ِك ُ يل اللهَِّ َو ْل َيع َ اج ِر ص َف ُحوا أَ اَل ْ ْفوا َو ْل َي ِ ين ِفي َس ِب ِ ين َوال ُم َه َ تُ ِحب ور َر ِحي ٌم ٌ ُّون أَ ْن َي ْغ ِف َر اللهَُّ لَ ُك ْم َواللهَُّ َغ ُف “Na wale katika nyinyi wenye wasaa wasiape kutowapa walio jamaa na maskini na waliohama katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe na waachilie mbali. Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu awasamehe? Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani 24:22)
408
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 408
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
Kama vile ambavyoAya inawataka Waumini wawe na msimamo madhubuti mbele ya familia zao kwa kutoyumbishwa na kusababishiwa kutokuwa na utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, pia wanatakiwa wawe ni wenye kusamehe na kupuuzia mbali makosa waliyotendewa, na huko ndiko kusamehe kwa kweli, na huu ndio msimamo wa kati na kati unaopaswa kufuatwa na kila Mwislamu. Aya inayofuata inaeleza tabia ya mali na watoto ilivyo, inasema: “Hakika mali zenu na watoto wenu ni mtihani. Na kwa Mwenyezi Mungu kuna ujira mkubwa.” Maelezo yanayohusiana na mtihani wa mali na watoto katika kumfanya mtu kufuata njia isiyo sawa tumeshayaeleza katika Aya zilizopita. Katika Aya hii tunakuta kwamba mali ya aina yoyote ile pamoja na watoto ni mtihani mkubwa kwa mwanadamu, kwani kuvutika sana na mali na mapenzi makubwa kwa watoto kunamfanya mtu kwenda mwendo ambao haumridhishi Mwenyezi Mungu Muumba, kwani asili ya vitu hivyo ni mtihani kama Aya ilivyobainisha. Na Imamu Ali (a.s.) anasema: “Mmoja wenu asiseme: Ewe Mola Wangu, hakika mimi najilinda kwako dhidi ya mtihani kwani hakuna yeyote yule isipokuwa ni mwenye kupatwa na mtihani, lakini mwenye kutaka kujikinga, basi na ajikinge dhidi ya kupotoshwa na mtihani, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Tambueni! Hakika mali yenu na watoto wenu ni mtihani.”209 Aya inayofuata inasema: “Basi mcheni Mwenyezi Mungu vile muwezavyo, na sikieni, na tiini, na toeni, itakuwa heri kwa nafsi zenu.” Kwanza, Mwenyezi Mungu amewaamrisha waja wake kuachana na madhambi, kisha kutii amri Zake, na suala la kutoa linarudiwa tena ikiwa ni moja kati ya amri Zake zinazostahiki kutiiwa na kutekelezwa na kila Muumini. Kisha anaeleza kwamba faida ya kutekeleza amriZake inarudi kwa mtekelezaji. Na amri ya kumcha Mwenyezi Mungu kwa kadiri ya uwezo, haipingani na Aya isemayo:
ْ وا اتَّ ُق ْ ُين آ َمن َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ وا اللَهّ َح َّق تُ َقا ِت ِه “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha.” (Qur’ani 3:102)
Ni kweli kwamba haiwezekani mtu kutekeleza uchajimungu kwa jambo lililoko nje ya uwezo wake, na asiye na uwezo wa kutekeleza wajibu wake husamehewa kwa hilo. Katika kutilia umuhimu wa kutoa, Aya inamalizia kwa kusema: “Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.” Makusudio ya ‘Uchoyo wa nafsi’ ni ubakhili wa kupindukia. Hali hii ni moja kati ya vizuizi vya utoaji wa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu, na yeyote mwenye kusalimika na 209
Imamu Ali (a.s.),Nahjul Balaghah, Jz.4, Uk.20 409
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 409
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
sifa hii atakuwa ni mwenye kufaulu, kwani mtu huyo atakuwa na sifa ya ukarimu badala ya ubakhili, na hapo ndipo atakapostahiki kupata malipo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Imamu Sadiq (a.s.) anaielezea hali hii kwa kusema:
.شح نفسه ّ من أ ّدى الزكاة فقد وقى “Mwenye kutoa Zaka, atakuwa amejiokoa na ubahili wa nafsi yake.”210
Na katika huhimiza juu ya utoaji wa mali na kutoa tahadhari dhidi ya ubahili, Aya inayofuata inasema: “Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atawazidishia maradufu, na atawaghufiria. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukrani, Mpole.” Ni uzuri ulioje wa maneno haya ya Mwenyezi Mungu ambayo yamekaririwa mara nyingi katika Qur’ani Tukufu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Muumba Mwenye kumiliki vyote vilivyomo mbinguni na ardhini, Mwenye kuwapa waja Wake neema mbalimbali, anatoa ahadi ya kuwalipa zaidi ya vile alivyowakopa. Kwa hakika huu ni ukarimu ambao hakuna baada yake ukarimu kuliko huu! Kwa upande mmoja, Aya hii inatufunza umuhimu wa kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kwa upande mwingine inaashiria ukarimu wa Mwenyezi Mungu usio na kikomo, kwani hakuna kiwango maalumu cha thawabu atakachopewa mtoaji, kama ilivyokuja katika Aya ifuatayo:
َ َ ين يُ ْن ِف ُق َ َم َث ُل الَّ ِذ ْع َ يل اللهَِّ َك َم َث ِل َحبَّ ٍة أَ ْن َب َت ْت َسب ِ ون أ ْم َوالَ ُه ْم ِفي َس ِب َُّف لِ َم ْن َي َشا ُء َوالله ُ اع َ َس َن ِاب َل ِفي ُك ِّل ُس ْنبُلَ ٍة ِما َئ ُة َحبَّ ٍة َواللهَُّ ي ِ ُض اس ٌع َعلِي ٌم ِ َو “Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba; katika kila shuke pana punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mjuzi.” (Qur’ani 2:261)
210
Al-Huweyziy,Tafsiru Nuru Thaqlqyn, Jz.5, Uk.346 410
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 410
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI NA NANE
ُ ِين آ َمنُوا ُقوا أَ ْن ُف َس ُك ْم َوأَ ْهل َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ اس ً يك ْم َن ُ َّارا َو ُقو ُد َها الن َ ْص ون اللهََّ َما أَ َم َر ُه ْم ُ ار ُة َعلَ ْي َها َم اَل ِئ َك ٌة ِغ اَل ٌظ ِش َدا ٌد اَل َيع َ َو ْال ِح َج ْ ون َما ي َ ُؤ َم ُر َ َُو َي ْف َعل ون “Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu. Hawamwasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa.” (Qur’ani 66:6)
MAELEZO Aya inawakhutubia Waumini, kwa kuwataka wawafanyie watoto wao na wake zao yale ambayo yatakuwa ni kinga kwao dhidi ya Moto wa Jahannam, inasema: “Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” Kinga hiyo hupatikana kwa kupewa malezi mazuri na kufunzwa vyema mafunzo ya Dini yao na kuhakikisha wanayatekeleza ipasavyo, na kuwaandalia mazingira mazuri yanayoendana na misingi ya Uislamu. Katika kufanikisha hili, inapasa kuanza matayarisho tangu kwenye hatua za mwanzo za kutaka kujenga jengo la familia; hatua za kuchagua mke, na hatua za kutafuta kizazi, na pia hatua za mwanzo baada ya kupatikana kizazi, kwani haki za mke hazimalizikii katika kumpatia chakula, mavazi na makaazi, bali lililo muhimu zaidi ni kupatiwa mafunzo sahihi ya Uislamu. Kuwaacha watoto na mama zao bila ya kuwafuatilia katika mienendo yao kwa kuwapa miongozo sahihi kunapelekea kwenye maangamizi na hatimaye ni kuingia Motoni wao na wasimamizi wao, kwa hiyo kila Muumini wa kweli ni lazima atambue kuwa jukumu lake ni kuhakikisha wanaishi maisha ya Kiislamu ili kuepukana na janga hilo. Mwenyezi Mungu ameeleza kwamba vitu vitakavyoufanya Moto kuendelea kuwaka ni watu na mawe. Hapa inaamaanisha ya kwamba Moto huo unatofautiana na moto wa hapa duniani, Moto wa Jahannam utaanzia ndani ya nafsi ya mwanadamu. Ama kuhusiana na mawe ambayo nayo ni asili ya Moto wa Jahannam, baadhi ya wafasiri wamesema mawe hayo ni yale waliyoyachonga washirikina na kuyaabudu. Kwa vile watu hao waliyaheshimu masanamu hayo, Mwenyezi Mungu atayachoma pamoja nao ili iwathibitikie kwamba si lolote wala si chochote. Aya inamalizia kwa kusema: “Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu. Hawamwasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa.” 411
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 411
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
Kutokana na usimamizi huo wa Malaika wenye kutekeleza amri zote za Mola Wao, ni dalili ya kwamba Siku hiyo hakuna atakayeweza kukimbia, na wala Malaika hao hawatowaonea huruma waovu hao kutokana na vilio vyao, njaa, kiu na fazaa kubwa watakayokuwa nayo,kwani Malaika watakaopewa kazi ya kusimamia Moto wa Jahannam, ni Malaika wakali, wenye roho ngumu, ni Malaika maalumu walioumbwa kwa kazi hiyo tu, huku wakijua kwamba hapo si mahali pa kustarehe, bali ni mahali pa mashukio ya ghadhabu za Mwenyezi Mungu kwa wale watakaoingizwa humo. Ugumu wa Malika hao kwa watu wa Motoni, hauwatoi katika kufanya kazi zao kwa uadilifu na kutii amri za Mwenyezi Mungu, Malaika hao ni wenye kufanya kila wanachoamrishwa na Mola Wao pasi na kuongeza lao au kupunguza kitu, kwani utiifu wa Malaika juu amri za Mwenyezi Mungu ni jambo la kimaumbile kwao, wapende wasipende wao ni wenye kutii amri Zake. Kwa hivyo wasimamizi hao hawatochukua hongo wala mlungula kutoka kwa yeyote ili asalimike na adhabu au apunguziwe. Siku hiyo mtu hatofaliwa na lolote isipokuwa matendo yake mema, kama Aya mbalimbali zinavyobainisha, baadhi yake ni kama zifuatazo:
ْ ون إ اَّل َم ْن أََتى اللهََّ ب َق ٌ َي ْو َم اَل َي ْن َف ُع َم ُال َو اَل َبن َ يم ل س ب ل َ ِ ٍ ِ ِ ٍ
“Siku ambayo haitafaa mali wala wana. Isipokuwa mwenye kuja kwa Mwenyezi Mungu na moyo uliosalimika.” (Qur’ani 26: 88-89)
UTAFITI Malezi kwa Familia: Ni wazi kwamba, kazi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya ni wajibu kwa watu wote, lakini majukumu ya Mwislamu kwa upande wa mke wake na watoto wake ni wajibu wenye nguvu zaidi, kama mafunzo ya Qur’ani pamoja na riwaya mbalimbali yanavyoeleza. Mfano wa wazi ni Aya hii tuliyoitaja katika maudhui haya. Aya inawataka Waumini watoe juhudi zao kuhakikisha familia zao zinaishi katika kufuata mafunzo sahihi ya Uislamu, kwa kuacha maasi na kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Kama vile ambavyo baba hujishughulisha katika kuwalisha na kuwavisha watoto wake na kuwapatia elimu na mafunzo mbalimbali, basi juhudi kama hizo au zaidi ya hizo wazifanye katika kuwapatia mafunzo sahihi ya Dini yao, kwani maisha marefu zaidi na yasiyo na mwisho yanahitaji mafunzo haya ili mtu aweze kuishi vyema katika maisha hayo. Na kwa vile jamii yoyote ile huundwa na familia, kwa hivyo kwanza Uislamu 412
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 412
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
unamtaka kila kiongozi wa familia kuitengeneza familia yake, na iwapo kila mmoja atasimamia vyema malezi ya watu wake, hapo ndipo ambapo jamii yote itatengamaa kwa njia nyepesi na rahisi. Wajibu huu kwa wazazi ni muhimu zaidi katika zama zetu hizi kwani kila leo tunaona ni namna gani jamii inavyoharibika, jamii iliyovamiwa na kila aina ya uovu na ufisadi, jamii ambayo inaona fakhari kutenda mambo ya haramu, kumuona yule ambaye anajiepusha na mambo haya amechelewa au amepitwa na wakati. Ni jamii ambayo inategemea uchumi wake kutoka kwenye vyanzo vya kueneza uharibifu na ufuska, kama vile ulevi, ukahaba, wasichana wadogo kuvishwa mavazi ya kuwakashifu na kupita mbele ya watu, wakiwemo wale waliopewa mamlaka ya kuwaongoza watu (viongozi wa nchi). Kwa masikitiko makubwa mambo haya yanabaraka zote za serikali, kwa kupewa ruhusa ya kufanya hivyo, na zaidi ya hayo hupewa ulinzi ili uharibifu huu uendelee! Leo madawa ya kulevya ni tatizo ambalo hakuna uwezekano wa kumalizika, kwa sababu wafanyao biashara hiyo ni baadhi ya viongozi wa nchi na matajiri wakubwa. Matajiri ambao hata siku moja hutosikia wamefungwa, kwani wanaposhikwa wanakuwa tayari kutoa kiwango chochote cha pesa ili waachiwe, na kwa vile mtu anapoamka asubuhi hukimbilia kutafuta maisha ni vigumu kwa wanaopewa hongo hizo kizikataa. Watu masikini wanaotumia madawa hayo baada ya kukosa shughuli za kufanya ndio waliojaa magerezani, huku waletaji na wauzaji wakubwa wakiendeleza hujuma zao kwa jamii! Kwa kweli kuna haja kwa kila kiongozi wa familia kuwa na utaratibu maalumu katika kuhakikisha anailea vyema familia yake, hasa kutokana na ukubwa wa tatizo linaloikabili jamii, kinyume chake ni kwamba familia nzima itaingia katika moto wa dunia kabla ya moto wa akhera. Imepokewa kwamba mmoja kati ya Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza Mtume (s.a.w.w.) baada ya kuteremka Aya hii: “Ni kwa namna ipi niwakinge watu wangu dhidi ya Moto?” Mtume (s.a.w.w.) alimjibu kwa kusema:
إن أطاعوك, وتنهاهم ع ّما نهاهم اهلل,تأمرهم بما أمر اهلل . وإن عصوك كنت قد قضيت ما عليك,كنت قد وقيتهم “Waamrishe yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, na wakataze yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, ikiwa watakutii utakuwa umeshawaokoa, na kama wakikuasi utakuwa umeshatekeleza wajibu wako.”211
Na katika riwaya nyingine Mtume (s.a.w.w.) anasema: 211
Kitabu kilicotangulia, Uk.372 413
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 413
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
فاألمير الذي على النّاس,كلكم راع وكلكم مسؤول عن رعيته والرجل راع على أهله بيته وهو راع عليهم وهو مسؤول عنهم ّ والمرإة راعية على بيت بعلها وولده وهي مسؤولة,مسؤول عنهم فكلّكم, وعبد الجل راع على مال سيّده وهو مسؤول عنه,عنهم .راع و كلكم مسؤول عن رعيته “Nyote ni wachunga, na kila mmoja ataulizwa kuhusiana na watu wake. Kiongozi wa nchi ni mchunga kwa raia kwa hivyo ataulizwa kuhusiana na raia wake, na mume ni mchunga kwa watu wake naye ataulizwa kuhusiana nao, na mke ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwa mume wake na watoto wake, naye atakuja kuulizwa kuhusiana nao, na mtumwa wa mtu ni mchunga wa mali za bwana wake, basi ataulizwa juu ya mali hizo. Basi nyinyi nyote ni wachunga, na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya anachokichunga.”212
Pia Mtume (s.a.w.w.) anatuelekeza baadhi ya mafunzo tunayopaswa kuwafunza watoto wetu, anasema:
حب نبيّكم وحب أهل بيته:أدبو أوالدكم على ثالث خصالل ّ وقراءة القرآن فإن حملة القرآ في ظل اهلل يوم ال ظل إال ظل مع .أنبيائه وأصفيائه “Wafundisheni watoto wenu mambo matatu: Kumpenda Mtume wenu, na kuwapenda watu wa nyumbani kwake (Ahlulbayti (a.s.)), na kusoma Qur’ani, kwani wenye kuibeba Qur’ani watakuwa katika kivuli cha Mwenyezi Mungu katika Siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli chake,wakiwa pamoja na Manabii Wake na Mawalii Wake.”213
Na kwa kufunga maudhui haya Imamu Ali (a.s.) anasema:
.علموا أنفسكم وأهليكم الخيرا وأدبوهم “Jifunzeni nyinyi wenyewe pamoja na watu wenu mambo mema na muwaadabishe.”214 Ibn Habban, Sahihu Ibn Habban, Jz.10, Uk.343 Suyutiy, Al-Jami’u Swaghir, Jz.1, Uk.51 214 Suyutiy, Durrul Manthur, Jz.6, Uk.244 212 213
414
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 414
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
WITO WA THEMANINI NA TISA
ُ وحا َع َسىٰ َرب َ َيا أَُّي َها الَّ ِذ ُّك ْم أَ ْن ً ص ُ ين آ َمنُوا تُوبُوا إِلَى اللهَِّ َت ْو َب ًة َن َ ْات َت ْجري ِم ْن َت ْح ِت َها أ ُ ُ ْ ِّ َ َّ ُ َ ار ُ ال ْن َه ِ ٍ يُكف َر َعنك ْم َسيِّ َئا ِتك ْم َويُ ْد ِخلك ْم َجن ْ َي ْو َم اَل ي َ ور ُه ْم َي ْس َعىٰ َبي َ ُخ ِزي اللهَُّ النَّ ِب َّي َوالَّ ِذ ْن ُ ُين آ َمنُوا َم َع ُه ن َ ْ ور َنا َو َ ُيه ْم َو ِبأَ ْي َما ِن ِه ْم َي ُقول اغ ِف ْر لََنا إِنَّ َك َ ُون َربَّ َنا أَ ْت ِم ْم لََنا ن ِ أ ْي ِد ير ٌ َعلَىٰ ُك ِّل َش ْي ٍء َق ِد “Enyi mlioamini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli! Asaa Mola Wenu akawafutia maovu yenu na akawaingiza katika Pepo ambazo hupita mito chini yake. Siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii. Na walioamini pamoja naye, nuru yao inakwenda mbele yao na kuumeni, na huku wanasema: Mola Wetu! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.” (Qur’ani 66:8)
MAELEZO Njia ya mwanzo ya uokovu ni kutubia kwa Mwenyezi Mungu na kung’oa mizizi yote ya madhambi. Sio kila wakati mtu anapotubia toba yake inakubalika. Toba inayokubalika ni ile tu ambayo inalengo la kurudi kwa Mwenyezi Mungu kwa kutaka radhi Zake na kuogopa adhabu Yake. Ni toba ambayo haina lengo jingine lolote, kama vile kukhofia jamii, au kujiepusha na dhambi kwa sababu tu ya kujikinga na baadhi ya athari mbaya za kidunia, bali ni toba ambayo mwanadamu anatubia kutokana na dhambi kisha hujizuia kurudia dhambi hiyo hadi mwisho wa maisha yake. Aya inaanza kwa kusema: “Enyi mlioamini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli!” Toba ya kweli ni ile toba ya kujutia dhambi na kuchukua azma ya dhati kabisa ya kutorudia tena dhambi hiyo, na ikiwa kama kuna wajibu fulani aliotakiwa kuutekeleza, lakini kutokana na uasi wake hakuutekeleza itamlazimu autekeleze ili toba yake ipate kuthibiti. Na kama kuna haki za watu pia itamlazimu kuzirejesha haki hizo. Kwa kufanya hivi ndipo ambapo Mwenyezi Mungu huyafuta maovu ya mwenye kutubu.
415
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 415
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
Kutokana na hayo, tunaweza kuzifupisha nguzo za toba kwenye mambo matano: Kuacha dhambi, kujuta, kuazimia kutorejea tena, kulipa wajibu aliouacha na kurudisha haki za watu, na kuomba msamaha. Kwa kufanya mambo haya hapo mja atakuwa ametubu toba ya kweli inayomuhakikishia kufutiwa madhambi yake, kwa sharti aanze kuishi katika kivuli cha Uislamu katika maisha yake yote mpaka siku ya kuondoka kwake katika dunia hii. Imepokewa kwamba siku moja Muadha ibn Jabal alimuuliza Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na toba iliyo ya kweli, Mtume (s.a.w.w.) alimjibu kwa kusema:
ّ أن يتوب التّائب ث ّم ال يرجع في الذنب كما ال يعود اللّبن إلى ّ .الضرع “Ni mtubiaji kutubu, kisha asirejee katika dhambi, kama vile ambavyo maziwa hayarejei katika chuchu (matiti).”215
Kutokana na maneno haya ya Mtume (s.a.w.w.), inapasa toba iweze kuleta mabadiliko na mapinduzi ya kweli ndani ya nafsi ya mwanadamu, na kufunga njia zote za kurudia katika makosa ya zamani, katika hali ambayo haitoi uwezekano wa kurudia maasi kama vile ambavyo maziwa hayawezi kurudi tena katika chuchu zake baada ya kukamuliwa. Baada ya hapo Aya inaeleza faida zinazopatikana kutokana na toba ya kweli, inasema: “Asaa Mola Wenu akawafutia maovu yenu na akawaingiza katika Pepo ambazo hupita mito chini yake. Siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii. Na walioamini pamoja naye, nuru yao inakwenda mbele yao na kuumeni, na huku wanasema: Mola Wetu! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.” Kwa mujibu wa ibara hii ya Aya, kuna faida tano watakazozipata wale wenye kutubia toba ya kweli, faida hizo ni kama zifuatazo:
215
1.
Watapata msamaha wa dhambi.
2.
Wataingia kwenye Pepo iliyojaa neema za Mwenyezi Mungu.
3.
Hawatofedheheshwa katika Siku hiyo iliyo ngumu, Siku ambayo kitawekwa wazi dhahiri shahiri kila kilichotendwa na mwanadamu.
4.
Nuru itokanayo na imani sahihi na matendo mema itakuwa mbele yao ikiwaongoza njia ya kwenda Peponi.
Al-Ardabiyliy, Zubdatul Bayan, Uk. 572 416
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 416
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
5.
Nyoyo zao zitakuwa ni zenye kumuelekea Mwenyezi Mungu zaidi kuliko zilivyokuwa kabla ya hapo, huku wakiwa na matarajio ya kukamilishiwa nuru yao na msamaha wa dhati wa makosa yao.
UTAFITI Toba ni Mlango wa Rehema za Mwenyezi Mungu: Kitu ambacho humkabili yule anayetaka kumuelekea Mwenyezi Mungu ni vishwawishi vya shetani, kiasi cha kumfanya kuweza kuingia katika maasi. Na pindi mja anapobobea katika kumuasi Mwenyezi Mungu huona ni bora aendelee kufanya hivyo kwani hudhania maasi aliyoyafanya hayawezi kusamehewa. Dhana hii haikubaliki katika Uislamu, kwani milango ya kurudi kwa Mwenyezi Mungu iko wazi kwa kila mkosaji. Mwenyezi Mungu amewataka wakosaji warudi Kwake kwa kutubia toba ya kweli, na kukata tamaa ni jambo lisilotakiwa kama Mwenyezi Mungu anavyosema:
َ ُق ْل َيا ِع َبا ِد َي الَّ ِذ ين أَ ْس َر ُفوا َعلَىٰ أَ ْن ُف ِس ِه ْم اَل َت ْق َن ُطوا ِم ْن َر ْح َم ِة ُّ اللهَِّ إ َّن اللهََّ َي ْغ ِف ُر الر ِحي ُم َّ ور ُ وب َج ِميعًا إِنَّ ُه ُه َو ْال َغ ُف َ ُالذن ِ “Sema: Enyi waja Wangu waliozifanyia israfu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani 39:53)
Na Imamu Ali ibn Husein Zaynul Abidin (a.s.) anasema:
,إلهي أنت الذي فتحت لعبادك بابا إلى عفوك س ّميته التّوبة فما عذر من أغفل دخول.ًصوحا ُ َّ تُوبُوا إِلَى اللهَِّ َت ْو َب ًة ن:فقلت !الباب بعد فتحه “Ewe Mola wangu! Wewe ndiye Ambaye uliwafungulia waja wako mlango wa msamaha wako na ukauita Toba, na ukasema: Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo
417
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 417
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
ya kweli. Hana udhuru (sababu ya msingi) yule ambaye ameghafilika kuingia katika mlango huo, baada ya kufunguliwa.!”216
Na kuna riwaya mbalimbali zilizokuja kutilia umuhimu suala la kutubia, kama Imamu al-Baqir anavyosema:
ّ إن اهلل تعالى أش ّد فرحا بتوبة عبده من رجل ّ أضل راحلته في ليلة ظلماء فوجدها “Mwenyezi Mungu anafurahi zaidi pale mja Wake anapotubia, kuliko furaha ya mtu aliyepotelewa na mnyama wake usiku wa kiza, kisha akamuona.”217
Lakini inapasa kuelewa kwamba toba si tu kutingisha ulimi peke yake wakati wa kutubia, bali ni lazima sharti zote zilizoelezwa zikamilike ili mtu asamehewe. Na wakati masharti yote yatakapokamilika, hapo ndipo mtu atakapovuna matunda ya toba yake, kwa kufutiwa makosa yake yote, kama ilivyopokewa kutoka kwa Imamu al-Baqir (a.s.) pale aliposema:
والمقيم على الذنب وهو,التائب من الذنب كمن ال ذنب له .مستغفر منه كالمستهزء “Mwenye kutubia kutokana na dhambi ni kama vile asiyewahi kutenda dhambi, na mwenye kuendelea kufanya dhambi na huku anaomba msamaha ni kama mwenye kucheza shere.”218
HITIMISHO Aya hizi tulizozikusanya katika kitabu hiki, zimetubainishia kwamba imani sahihi juu ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake haikamiliki ikiwa Muumini hatotekeleza kwa vitendo yale yote aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.) na kuachana na yale waliyoyakataza, kwani imani bila ya matendo mema ni imani pungufu na isiyomfaa mwanadamu chochote. Ni ushahidi wa wazi kwamba imani sahihi Imamu Zaynul Abidin,Swahifatu Sajjadiya, Dua ya kuuwaga mwezi wa Ramadhani Hurrul Amiliy, Wasailu Shia, Jz.16, Uk.73 218 Kitabi kilichotangulia, Uk.74 216 217
418
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 418
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
na thabiti si kwa mtu kutamani au kujipamba na mavazi fulani ambayo kwa kawaida huvaliwa na wachamungu, bali imani ya kweli ni ile hali ya mtu kuwa mzinguzi katika hali yote ya maisha yake juu ya Mwenyezi Mungu na vyote anavyotakiwa kuviamini, na baada ya hapo kujipamba kwa matendo mazuri na kujiepusha na kila ovu. Kwenye Aya hizi kuna maamrisho mbalimbali, lakini jambo lililokaririwa zaidi ni juu ya Waumini kumcha Mwenyezi Mungu, kwani bila ya Muumini kubeba hisia za uchamungu katika nafsi yake, si rahisi kuyatekeleza maamrisho mengine au kujiepusha na makatazo. Ama kwa upande wa makatazo, jambo lililosisitizwa zaidi ni kutowafanya marafiki walio maadui wa Uislamu, kwani kujikurubisha kwa watu hao na kusuhubiana nao ni sababu kubwa kwa maadui hao kumfanya huyo Muumini chombo chao cha kueneza propaganda zao, na kutumiwa katika kuudhuru Uislamu na kueneza maovu katika jamii. Aya zimewaweka Waumini wenye kutekeleza yaliyokatazwa katika daraja moja na makafiri, bali zinawazingatia kwamba wao pia ni makafiri, kwa sababu makariri siku zote huenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kufanya yale aliyoyakataza. Aya zimetuonesha kwamba imani iko katika madaraja tofauti. Kwa hiyo zimewataka Waumini wafanye kila juhudi kuweza kufikia katika kilele cha imani, kwani miongoni mwa Aya hizi zimewataka Waumini waamini. Baadhi ya yale yaliyokatazwa kwenye Aya hizi, humtoa mwenye kuyatenda katika Uislamu na kumporomoshea yale yote mazuri aliyoyatenda. Kwa hiyo ndugu zangu Waislamu hatuna budi kukaza mikanda katika kutekeleza yale yote yaliyomo katika Aya hizi na kuachana na yale yaliyokatazwa, ili ithibiti kwamba kweli sisi ni Waumini, na tuwe miongoni mwa wale wanaoitwa na Mwenyezi Mungu kwa wito Wake huu “Enyi mlio amini!” Ewe Mola Wetu! Vikunjue vifua vyetu kwa Qur’ani, na viwezeshe viwiliwili vyetu kuweza kuitekeleza Qur’ani, na yang’arishe macho yetu kwa Qur’ani, na zitamkishe ndimi zetu Qur’ani, kwa rehema Zako, na Swala na Salamu zimwendee Mtume wetu pamoja na jamaa zake uliowatoharisha.
419
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 419
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36.
i) ii)
Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A. S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A. S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudhar Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur’an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur’an Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) 420
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 420
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI 37. 38. 39. 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78.
Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana Upendo katika Ukristo na Uislamu Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya Sala Mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an Yatoa Changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu 421
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 421
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120.
Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raj’ah) Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini Mtoto mwema Adabu za Sokoni Na Njiani Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 422
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 422
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI 121. 122. 123. 124. 125. 126. 127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137. 138. 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150. 151. 152. 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162.
Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad Safari ya kuifuata Nuru Fatima al-Zahra Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) Khairul l’Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? Tabaruku Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili Vikao vya furaha Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Kuhuzunika na Kuomboleza Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mjadala wa Kiitikadi Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 423
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 423
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180. 181. 182. 183. 184. 185. 186. 187. 188. 189. 190. 191. 192. 193. 194. 195. 196. 197. 198. 199. 200. 201. 202. 203. 204.
Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) Uadilifu katika Uislamu Mahdi katika Sunna Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo Abu Talib – Jabali Imara la Imani Ujenzi na Utakaso wa Nafsi Vijana na Matarajio ya Baadaye Historia maana na lengo la Usalafi Ushia – Hoja na Majibu Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu Takwa Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa Tawheed Na Shirki Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr Adabu za vikao na mazungumzo Hija ya Kuaga Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 424
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 424
12/8/2014 2:43:51 PM
WITO KWA WAUMINI 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 227. Yafaayo kijamii 228. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 229. Mkakati wa Kupambanana Ufakiri 230. Mtazamo Mpya - Mwanamke katika Uislamu 231. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 232. Imam Mahdi Na Bishara Ya Matumaini 233. Jihadi 234. Majanga Na Jukumu La Jamii 235. Muhadhara wa Maulamaa 236. Mashairi ya Kijamii 237. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 238. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 239. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 240. Yusuf Mkweli 241. Hotuba Za Kiislamu Juu ya Haki Za Binadamu 242. Ugaidi wa Kifikra katika Medani ya Kidini 243. Wito kwa Waumini: “Enyi Mlioamini”
425
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 425
12/8/2014 2:43:52 PM
WITO KWA WAUMINI
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.
Amateka Ya Muhammadi (s.a.w.w) Na Aba’ Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.
Livre Islamique
426
34_14_Wito Kwa Waumin_6_Dec_2014.indd 426
12/8/2014 2:43:52 PM