Worksheet (Swahili) | Jinsi ya Kupona kutoka kwenye Kufeli

Page 1

An InnovatorsBox ® Innovation karatasi ya kazi

Jinsi ya Kupona kutoka kwenye Kufeli Kurudia Ujasiri wangu wa Ubunifu

Kufanya jambo lolote jipya huwa hatarishi na

tunaruhusu mambo yaliyopita yatuzuie

hutia hofu. Hata unapofanya mahesabu yako na

kuthubutu na kufikia ubora wetu. Tunafahamu

kuweka mikakati, wakati mwingine kushindwa

kuwa kupona kunachukua muda na kujaribu

na kukataliwa huwa hakuepukiki. Ni kwa jinsi

kitu kipya kwahitaji ujasiri wa ubunifu. Chati

gani unaokota vipande vyako na kusonga

hii inakupa maswali ya kukufanya utafakari

mbele pale jambo likienda vibaya? Kama

juu ya matukio ya kushindwa na kukataliwa

hatufahamu jinsi i tunaweza kusonga mbele

yaliyopita,na kukuwezesha kujitengenezea

na kuacha nyuma kukataliwa na kushindwa,

ujasiri wa ubunifu.

1) Uelewawa hisia zetu unaweza kutusaidia kuchanganua kufeli na kukataliwa. Badala ya kurudia jinsi ilivyotokea, ni vema kutafakari juu ya ‘kwa nini’ umepata hisia hizo. Kwa nini nahisi kuumizwa na tukio hili? Kwa nini nahisi kana kwamba nilifeli? Kwa nini nahofia jambo ( Hint: Are they curious, diverse, playful? ) hili kutokea tena?

2) Kufeli kunaweza kuwa mwalimu mzuri. Thomas Edison alisema, “Sijafeli mara moja. Nimejifunza kwamba ,vitu elfu kumi visivyofanya kazi.” Ninaweza kujifunza nini kutoka kwenye tukio hili na nitafanya nini tofauti wakati ujao?

1

INNOVATORSBOX LLC © 2019. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA.


3) Kufeli pia kunaweza kutuimarisha. Ni kwa njia gani tukio hili linaweza kuniimarisha, kuniongezea ujasiri, na kunifanya mtu mwenye kustahimili changamoto zijazo?

4) Mikakati yakinifu inaweza kukusaidia kujiandaa kukabili makosa yajayo. Ninaweza kufanya nini tofauti wakati ujao ili kuboresha uwezo wangu wa kukabili kufeli au kukataliwa? Ni vitu gani vilivyo ndani ya uwezo wangu ninavyoweza kufanya Ni vitu vipi vilivyopo nje ya uwezo wangu ninavyotakiwa kutovihofia? Vitu ninavyoweza kufanya tofauti kiujumla:

Vitu vilivyopo ndani ya uwezo wangu:

Vitu vilivyopo nje ya uwezo wangu:

5) Ni muhimu kujua jinsi ya kupona, bila kujalisha ukubwa wa jeraha lako. Ni vitu vipi vitatu vyenye manufaa ninavyoweza kufanya ninapotaka kusonga mbele na kuacha kukataliwa na kufeli nyuma? Kwa mfano, ni watu gani ninaoweza kuzungumza nao? Je, ninaweza kuandika ama kufanya mazoezi yoyote ya kunirejeshea ujasiri wangu wa ubunifu? 1. 2. 3.

2

INNOVATORSBOX LLC Š 2019. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA.


Tumia nafasi hii kuchora ama kuandika zaidi hisia zako kuhusu kufeli ama kukataliwa.

Kufeli kunaweza kusiepukike unapotaka kuwa mbunifu, lakini hiyo haimaanishi haupaswi kuchukua muda kupona. Tunatumaini kuwa maswali haya yamekusaidia kutafakari na kuchochea ujasiri wako ukisonga mbele. Kwa msaada zaidi, waone wanasaikolojia, matabibu, washauri, na marafiki zako.

Kitabu Kinachopendekezwa: Emotional First Aid: Healing, Rejection, Guilt, Failure and Other Everyday Hurts by Dr. Guy Winch

Kitabu Kinachopendekezwa: Rethink Creativity: How to Innovate, Inspire, and Thrive at Work by Monica Kang

ANGALIZO: InnovatorsBox inaelewa kwamba kujikongoja kutoka kwenye kukataliwa na kufeli kunaweza kuwa kugumu kuliko kupitia chati. Chati hii haijadhumuniwa kutumika kutoa huduma za tiba ya akili unazoweza kuhitaji. Ikiwa unahitaji msaada wa ziada, tafadhali tafuta mwanasaikolojia, tabibu au mtaalamu wa kukupatia msaada zaidi. info@InnovatorsBox.com INNOVATORSBOX.COM

3

Tafadhali kuwa huru kusambaza Chati za Uvumbuzi za InnovatorsBoxÂŽ. Hakikisha unarejea InnovatorsBox.com baada ya kila matumizi.

INNOVATORSBOX LLC Š 2019. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.