JAHAZI issue 02 - Kilimanjaro Fast Ferries, AZAM Marine

Page 40

Swahili story time / Wakati wa hadithi

OPERESHENI DAKABU by Joseph Shaluwa

To make your ferry journey fly by, here is a gripping short story to read. Joseph Shaluwa is a Tanzanian writer known for his page-turning works full of intrigue and suspense. Operesheni Dakabu (Operation Dakabu) is a short story specially written for Jahazi by Joseph and centres on Inspector Mark, who, the day after getting married, is tasked with uncovering a plot to stage a political riot. Enjoy!

M

UITO wa simu iliyokuwa mezani ulimgutusha pale kitandani alipokuwa amelala, lakini aliipuuza. Simu kwa wakati ule haikuwa na maana kabisa kwake. Msichana mrembo Upendo, alikuwa kando yake, akionyesha kumhitaji sana ndiye aliyekuwa na maana na thamani kuliko chochote. Ilikuwa ni asubuhi ya kwanza kwao kama wanandoa. Kwa miaka mitatu ya uchumba, hawakuwahi kulala hadi asubuhi hata mara moja. Ilikuwa siku yao muhimu sana. Mark alimgeukia Upendo, kisha akamwambia: “Kuna watu wanaojua kuharibu starehe za wenzao. Hivi ni nani ambaye hajui kuwa jana nimetoka kuoa? “Nani ambaye hajui kuwa nipo fungate na mke wangu tukitafuta mtoto?” Upendo akabaki anamwangalia tu usoni bila kujibu. Pengine angalia yake ilikuwa jibu tosha, kwamba anamsuta kwa kitendo chake cha kutokuwa mwerevu. “Mbona hujibu kitu?” akauliza Mark. “Unashindwa nini kuizima?” “Lakini mke wangu Upendo, mara hii umesahau kuwa mimi ni polisi?” “Kwahiyo?” “Muda wote nipo kazini!” Eti muda wote nipo kazini! Akawaza Upendo akimkata Mark jicho la kebehi. Mark alielewa alichokuwa akimaanisha mkewe. Alimhitaji faraghani. Akiwa mawazoni, simu ikaita tena. Mara moja akaichukua... Paaa! Moyo wake ukashtuka. Ilikuwa simu kutoka ofisini – Makao Makuu – kwa bosi wake – Mkuu wa Kitengo cha Kazi Maalum. 38

Kitengo hiki kilisimamiwa na Mkurugenzi wa Upelelezi Maalum, Kamishna Msaizidi wa Polisi (ACP), Kelvin Kayanda. Kilifanya kazi kwa karibu na idara ya Usalama wa Taifa. Tofauti ya kitengo hiki na vingine vilivyopo kwenye Jeshi la Polisi, huripoti moja kwa moja kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Kwa kawaida, kitengo hiki hufanya kazi ya kuhakikisha inachunguza, inathibiti na kuwakamata wanaohusika na uharibifu wa amani ya nchi. Kupigiwa simu moja kwa moja na ACP Kelvin Kayanda kulimpa picha Mark, kuwa kulikuwa na jambo zito linalohitaji usaidizi wake. Hapo akawa na uhakika kuwa fungate imeshaharibika. Mara moja akapokea! “Jambo!” sauti nzito ya ACP Kelvin Kayanda ilisikika kutoka upande wa pili. “Jambo afande.” “Najua upo fungate, lakini kwa ajili ya taifa lako, nakuomba ofisini ndani ya saa mbili kutoka sasa, asante sana,” akasema ACP Kayanda, kisha akakata simu. Ulikuwa wito wa dharura. Amri. Hapakuwa na majadiliano. Insp. Mark akabaki anaitazama ile simu kwa ghadhabu, kisha akamgeukia mkewe na kumwambia: “Samahani mpenzi, ni simu kutoka ofisini. Amenipigia bosi mwenyewe. Natakiwa kazini sasa hivi.” “Nilijua tu.” “Samahani mpenzi wangu.” “Itanisaidia nini.”

nchi kwanza kabla ya ndoa yake. Ndiyo kiapo chake kilivyokuwa. Akajitoa kitandani na kujiandaa. Kama Upendo ataniacha kwa ajili ya kazi na aniache tu! Akawaza Mark akimalizia kufunga mkanda. “Kitu kimoja cha muhimu unatakiwa kufahamu, nakupenda sana Upendo. Lakini ndoa yetu, maisha yetu hayatakuwa na maana bila kazi. Acha nikafanye kazi,” akasema Insp. Mark akimwangushia mkewe busu mwanana. Upendo hakujibu, aliishia kulia. Inp. Mark hakujali. Akaondoka zake.

INSP. Mark alimalizia kupandisha ngazi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam. Alitembea mpaka kaunta, kisha akakata kulia na kupandisha ngazi kuelekea ofisini kwa ACP Kelvin Kayanda. Uzuri ni kwamba, hoteli waliyoamua kukaa kwenye fungate lao la kwanza, ilikuwa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, alipotokea, ilikuwa wakae hapo kwa wiki moja kabla ya kwenda Visiwani Comoro kumalizia fungate lao. Lakini kwa sababu ya kazi, amelazimika kumuacha mkewe mbichi, Upendo na kwenda kazini. Alipoufikia mlango, akagonga mara moja na kuingia. “Nimefurahi umeitikia wito, tena kwa wakati. Nisikupotezee muda. Unatakiwa kusafiri leo kwenda Kahama. Tumeshaandaa ndege kwa ajili ya safari hiyo. Maelekezo yote ya

Insp. Mark hakuwa na muda wa kubembelezana na mkewe. Alitakiwa kuifikiria

safari yako, yapo humu kwenye hii bahasha,” akasema ACP Kelvin Kayanda akimkabidhi


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.