August (Nane nane Edition)

Page 1

NANE NANE SPECIAL EDITION

TANZANIA | KENYA | RWANDA

FREE COPY




Mpendwa

THE MONTH COVER

MSOMAJI

Kutoka kwa Mhariri

Sherehe za NANE NANE zipo usoni mwetu ambapo Kauli mbiu ya maonesho haya ni “ZALISHA KWA TIJA MAZAO NA BIDHAA ZA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI ILI KUFIKIA UCHUMI WA KATI” Ni dhahiri kuwa uchumi wetu unakuwa kwa kasi kubwa na utaendelea kuimarika kwa miaka ijayo kwa kuwa ipo miradi mikubwa ya viwanda na miundombinu inayoendelea na inayotarajiwa kuanza kazi siku za usoni ambayo itachangia katika kuimarika kwa uchumi. Kwa ajili ya kufikia matazamio ya Nchi yetu, wote kwa pamoja tunatakiwa kuhakikisha shuhuli zetu hasa za kilimo zina manufaa makubwa katika kuongezeka kwa Uchumi wa nchi kwa kuzalisha mazao kwa ajili ya biashara na sio kuzalisha mazao kwa ajili ya chakula peke yake. Ili kufanikisha hayo kuna uhitaji mkubwa wa mazao kuzalishwa kwa namna ya kisasa na pia swala la muhimu ni kuweka mawasiliano kati ya mzalishaji wa mazao, mnunuzi wa jumla wa mazao hayo na mnunuzi wa mwisho wa mazao hayo kwa njia ya matangazo kwenye jarida,mitandao ya kijamii n.k ili kusaidia ukuaji wa mzunguko wa sekta yetu ya kilimo hapa nchini. Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa kila mdau wa jarida la LiMA anayeshiriki kwa namna moja au nyingine maana kupitia ninyi jarida letu linatimiza miaka mitatu (3) sasa, ni bayana kua bila ninyi tusingefika hapa tulipo, tunaomba ushirikiano wenu zaidi ili kutimiza malengo kwenye sekta ya kilimo na maendeleo kwa ujumla. DISTRIBUTION CHANNELS Kibo Palace Hotel | Le patio | Kase Store | SIAN’GA INTERTRADE | MAMS | Meru Agro | Fifi’s Arusha | Africafe’ | Njiro Complex | Riverside Offices | Mchaki Agro & Pet care | Mohan’s Drinks Ltd | Kibo Seed | Roll Agrovet | TFA | Nakumatt Arusha | MOSHI | SINGIDA | BABATI | KILIAD SOLUTIONS - Nairobi | CAS - Monduli | MOROGORO | IRINGA Others: Agrovets, Restaurants, Hotels, Airports, Supermarkets, Airlines & Shops. NAIROBI: Utungi TV offices | Local Agrovets Nuclear Saccos | Mololine | Easy Coach

Gladness Joseph .................................................

PUBLISHER & PRINTER Kiliative Solutions (EA) Ltd P.O. Box 16027 Arusha, Tanzania Meru View Business Park, Kaloleni near New NSSF Building, Tel: +255 784 712 303 +255 783 857 777 E-mail: marketing@kiliativegroup.com Web: www.kiliativegroup.com

Kiliads Solutions (EA) Ltd - KENYA Softa Plant, Off Enterprise rd next to General Motors, P.O. Box 16745 - 00100 Nairobi. Mob: +254 780 712 303 Kiliative Solutions (EA) Ltd - RWANDA North Airport Rd, Mathias House - Remera P.O. Box 1863, Kigali - Rwanda Tel: +250 781 467 752

To be appointed a distributor, or for a copy please call or email us.

+255 764 515 222

limamagazine@kiliativegroup.com

MAKALA

ZA KUELIMISHA

DISCOVER MORE... Check out our issues online at www.kiliativegroup.com

A R T I C L E S AVA I L A B L E T H I S M O N T H

Wellness Tips: 04 | Health Spreads, an alternative to butter and margarine

2.

August, 2017

Makala 12 | Maadhimisho ya nane nane

15 | Makala Kilimo cha mzunguko na faida zake kwa mkulima



WELLNESS TIPS

Healthy spreads

an alternative to butter and margarine by: Jennifer Ayoti - Wellness Coach, Nutritionist I have found these amazing healthy spreads to be easy to make and they taste so good! I am one person who believes in simplicity. I also strongly believe in eating good food; if it tastes good then it will make you feel good! Because of the kids, we do bread once a week. We found a store that stocks sprouted grain bread and buns in one of the malls. Sprouted grain bread is a healthy alternative to white flour or whole grain flour bread. The preparation process involves soaking the grains in water until they begin to grow a sprout. Sprouted grain bread is better not only because it uses the whole grain, but the process sprouted grains go through actually breaks down the proteins and carbohydrates in the grain, increasing vitamin content to the consumer. Yes, it still contains a moderate amount of gluten but it is a healthier choice compared to white or whole grain bread.

Spreads just like toppings in food can make the dish unhealthy. Most of us are limited to butter and margarine, yet there are so many other simple, healthy and delicious choices. We can opt to use Nut butters; almond, macadamia, almond or avocado which is natural and tastes so good. My favorite is hummus which is so easy to make.

Here is my simple recipe Make Tahini first (sesame paste) You will need 1 cup of sesame seeds; toast them on a pan until they are golden brown then after they have cooled down, blend as you add 3-4 tablespoons of olive oil. Blend to your desired consistency. There you go! Simple. Pour the paste in an air- tight jar and put in the fridge. For your hummus (chickpeas plus sesame paste) Tahini paste 1/2 cup I cup of chickpeas that have been soaked for 24-48 hours 1/4 cup olive oil 4 tablespoons of lemon juice 2 cloves garlic 1/4 teaspoon sea salt Method: Boil the chickpeas with some baking soda until they are soft. Drain the water and put them in a blender. Add olive oil, tahini paste, garlic, lemon juice and sea salt. blend until smooth. Add some water until you reach your desired consistency. Chickpeas which is one of the foods that contain Phytoestrogens is highly encouraged for women going through menopause. Phytoestrogens are thought to block the body’s uptake of unhealthy estrogen and where there is a deficiency of estrogen, provide an alternative source. Sesame seeds are a nutritional powerhouse containing vitamins, minerals, natural oils, and organic compounds which consist of calcium, iron, magnesium, phosphorous, manganese, copper, zinc, fiber, thiamin, vitamin B6, folate and protein. The combination of these two ingredients plus olive oil, garlic and lemon juice, will leave your organs smiling! Happy cooking!

4.

August, 2017









Makala

MAADHIMISHO YA NANENANE MWAKA 2017 Nane Nane ni maonyesho ya wakulima yanayoadhimishwa mara moja kwa mwaka ambapo shughuli hii hufanyika wiki ya kwanza ya mwezi wa nane (8). Maadhimisho ya NANENANE yalianza mnamo mwaka 1993 ambapo kwa sasa ni miaka 24.

ambapo imeleta manufaa makubwa kwa watu wengi na jamii nzima hasa wale wanaojihusishaa na nyanja mbalimbali za sekta nzima ya kilimo.

Maonyesho ya nane nane husherekea kazi ya wakulima na umuhimu wao katika Nchi yetu. Kwa hali ya juu uchumi wa Tanzania unategemea Kilimo. Aina kuu ya mazao inayozalishwa Tanzania ni Mahindi, Mhogo, Viazi vitamu, Maharage, Ndizi, Mchele, Mtama, Sukari, Pamba, Korosho, Kahawa, Katani na Chai. Maadhimisho ya sherehe hizo hupangwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Kwa kushirikiana na Chama cha Wakulima Tanzania (TASO) Ili kushirikisha taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali , Makampuni pamoja na watu binafsi kushiriki katika maonesho hayo ya kilimo ili kuonyesha mazao ama bidhaa mbalimbali zinazohusu kilimo inayoandaliwa kwa muda wa wiki moja katika Miji na Mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Kila mwaka maadhimisho haya huambatana na kauli mbiu tofauti ili kuweka mkazo kwenye nyanja mbalimbali katika sekta hii ya kilimo ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni “ZALISHA KWA TIJA MAZAO NA BIDHAA ZA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI ILI KUFIKIA UCHUMI WA KATI� Ni dhahiri kua kwa sasa Serikali yetu iko kwenye michakato mbalimbali ya kuhakikisha kwamba Uchumi wa Nchi yetu unafikia Uchumi wa Kati hivyo kupitia kilimo chenye tija na manufaa tutaweza kuchangia / kukuza pato la Taifa letu kwa kiasi kikubwa ukizingatia kua kilimo ndio chanzo kikuu cha mapato ya Nchi yetu. Maadhimisho ya nanenane yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakutanisha wakulima, wasambazaji na watumiaji wa bidhaa na mazao mbalimbali ya kilimo na pia kuwakutanisha sekta ya kilimo na sekta zingine 12.

August, 2017

Nane Nane ni maonyesho ya muhimu sana katika taasisi ya kilimo kwani ni njia rahisi ya kuwakutanisha wahusika wote katika sekta ya kilimo na nyanja zake zote hivyo ni vyema wananchi na wahusika wengine wote kushiriki maadhimisho haya kwa moyo ili kwa pamoja kuweza kufanikisha malengo ya maadhimizo ya nanenane na kuleta manufaa kwa Taifa zima kwa ujumla.




KILIMO CHA MZUNGUKO

Makala

NA FAIDA ZAKE KWA MKULIMA

Hichi ni kilimo kinachozingatia kulima mazao tofauti katika shamba moja kwa muda ambao umepangiliwa kwa kuyapa muda wa kupanda zao moja na lingine. Kupanda mazao kwa mzunguko humaanisha kua na aina mbalimbali ya mazao katika eneo moja kwa kipindi (msimu) tofauti. Kwa mfano kama shamba lako umepanda mahindi na maharage kwa kipindi cha mwaka mmoja, mkulima anashauriwa kubadili aina ya mazao atakayopanda katika eneo hilo kwa msimu mwingine unaofuata. Sio kila mmea unashauriwa kupanda katika mzunguko, moja ya mmea unaoshauriwa kupandwa katika mzunguko ni kunde maana ni moja ya zao linalosaidia kuongeza rutuba kwenye udongo. Endapo mkulima atakua na kawaida ya kupanda zao aina moja katika shamba lile zaidi ya misimu miwili wadudu na magonjwa hushambulia zaidi zao hilo kwani wadudu hao na magonjwa mbalimbali hua sugu katika shamba hilo na ndio maana kilimo cha mzunguko hushariwa kwa wakulima kwani mazao tofauti huchukua virutubusho tofauti katika ardhi na hivyo kuiruhusu ardhi kutokua na uwiano sawa wa rutuba. Moja ya umuhimu mkubwa wa kuzungusha mazao ni kusaidia kuongeza rutuba na kuzuia wadudu na magonjwa shambani. Kwa mkulima kufanya kilimo cha mzunguko ardhi itarutubishwa kwa kiwango kikubwa hasa kwa kupanda mazao ya jamii ya mikunde, inapunguza wadudu na magonjwa katika mazao, huwezesha viumbe hai (bacteria) waliopo kwenye udongo kufanya kazi yao ipasavyo, huongeza rutuba shambani, hupunguza gharama za kuzuia magonjwa na wadudu shambani na pia huwezesha afya/uhai wa ardhi ambapo matokeo hayo hua na manufaa makubwa sana kwa mazao yanayozalishwa.

Kanuni ambazo ni muhimu kuzingatia wakati wa kufanya kilimo cha mzunguko ni kama ifuatavyo: kuna aina mbili ya mazao ya kwanza ni mazao ambayo huchukua rutuba nyingi katika udongo (heavy feeders) na ya pili ni mazao yanayochukua rutuba kidogo katika udongo (light feeders) hivyo katika upangiliaji wa mzunguko, mazao yanayochukua rutuba nyingi kwenye udongo yanatakiwa yabadilishane na mazao yanayochukua rutuba kidogo kwenye udongo au kinyume chake ni sahihi. Mazao yenye mizizi mifupi yabadilishane na mazao yenye mizizi mirefu na hii ni kwa sababu mazao yenye mizizi mirefu huchua kiasi kikubwa cha unyevu katika ardhi hivyo ni muhimu kubadilisha ili udongo uweze kustahimili matumizi ya maji yanayopatikana katika eneo husika. Zifuatazo ni faida ambazo zinapatikana katika kilimo cha mzunguko ni pamoja na: i) rotuba ya udongo kutumika vyema na mazao yatakayobadilishana, ii) kilimo cha mzunguko pia husaidia katika kudhibiti wadudu na magonjwa iii) pia husaidia kuongeza rotuba katika udongo. Ili mkulima ufanikiwe katika kilimo cha mzungusho kuna mambo ya muhimu ya kuzingatia nayo ni: i) Kuhakikisha unabadilisha mazao kulingana na kanuni, kwa msaada zaidi unaweza kumshirikisha mtaalamu wa kilimo aliye karibu nawe. ii) Pia kuweka mpango mzuri wa kuachanisha mazao katika shamba lako kwa kuandaa kalenda nzuri za uzalishaji.

August, 2017

15.












MANAGING DIRECTOR

As we celebrate our 3rd birthday as the LIMA family, I take this opportunity to sincerely thank our super team for keeping the fire burning. Being almost the first agricultural magazine in the Tanzanian market, I can attest that it has not been a walk in the park. At first the idea seemed very unpopular and I would say that it has been a journey fueled by passion, dedication and relentless efforts to ensure the culmination of our dream. During the last three years, we have continued to achieve several milestones and this has been made possible by very supportive stakeholders from different sectors who have bestowed their trust and confidence on us and our magazine. As at now, we have over 50 companies across East Africa that have signed up with us in our monthly publication and the list is still growing.

MESSAGE

Our continued interaction with different players especially in the agricultural sector has been a great eye opener and as advertising and marketing experts, our resolve is to continue investing in powerful; future oriented and unparalleled strategies to ensure increased value for money for all players. In order to ease communication and speed of doing business, one of our winning strategies will be though our highly interactive app that will be released soon. This is to ensure that different players and industry experts are brought together in a highly interactive platform to have their FAQs answered on a real-time basis. Finally; as we celebrate the farmers’ exhibition for the next 10 days, I wish you good health and God’s blessings as you enjoy reading our highly distributed publication. Also plan to visit our stand No. 28, NANE NANE Grounds.

“Zalisha kwa tija Mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia Uchumi wa kati” Kauli mbiu (2017), TASO

Patrick K. Waithaka

Managing Director; Kiliative Group Kenya I Tanzania I Rwanda

26.

August, 2017






Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.