October Edition

Page 1

EDITION: October, 2016

Experience Limitless Possibilities

FREE COPY TANZANIA | KENYA | RWANDA

www.kiliativegroup.com




Kutoka kwa Mhariri

THE MONTH COVER

Mpendwa

MSOMAJI Mbegu bora kwa ujumla huzalisha mazao bora yenye kukubalika zaidi sokoni. Kama mkulima,Je unatambua umuhimu wa kuchagua mbegu bora kutoka kampuni mbali mbali? Ni kipi hasa unazingatia katika uchaguzi wa mbegu? Je ni ubora wa mbegu? Asili ya mbegu? Chanzo cha mbegu n.k. Udongo wa eneo pia ni miongoni mwa vitu vya kuzingatia. Jarida lako pendwa la LIMA linakupa fursa wewe mkulima kuweza kufahamu na kutambua wadau mbali mbali wanahusika na maswala ya kilimo,iwe ni mbegu bora unataka,madawa kwa ajili ya mazao na mifugo,mbinu za kisasa za umwagiliaji na hata namna ya kuweza kuhifadhi mazao pindi tuu uvunapo bila kusahau mfumo wa soko. Tangaza nasi leo upate kujumuika na kutambulika kwa wadau wapya na wa zamani wenye kujikita katika kilimo. Vilevile unaweza kututembelea ili uweze kuunganishwa na wataalamu wa mambo ya KILIMO na pia kupatiwa ushauri nasaha, juu ya kilimo bora.

DISTRIBUTION CHANNELS Kibo Palace Hotel | Le patio | Kase Store | SIAN’GA INTERTRADE | MAMS | Meru Agro | Fifi’s Arusha | Africafe’ | Njiro Complex | Riverside Offices | Mchaki Agro & Pet care | Mohan’s Drinks Ltd | Kibo Seed | Roll Agrovet | TFA | Nakumatt Arusha | MOSHI | SINGIDA | BABATI | KILIAD SOLUTIONS - Nairobi | CAS - Monduli | MOROGORO | IRINGA Others: Agrovets, Restaurants, Hotels, Airports, Supermarkets, Airlines & Shops.

Tupo chini ya kampuni ya KILIATIVE SOLUTION (E.A) LTD ambayo kwa sasa tumeandaa bidhaa mbali mbali kwa ajili ya msimu wa sikukuu, pamoja na vitabu vya kutunza kumbukumbu (diaries), na kalenda za mwaka 2017. Tunashukuru kwa ushirikiano wako, kwani kuanzia toleo hili tunaanza kusambaza jarida hili katika nchi ya Rwanda, ni fursa kwako kujitangaza kimataifa zaidi!

Pauline Kimambo

To be appointed a distributor, or for a copy please call or email us. +255 764 515 222 limamagazine@kiliativegroup.com

MAKALA

ZA KUELIMISHA

Marketing Tips: 04 | Party survival strategies

2.

October, 2016

PUBLISHER & PRINTER Kiliative Solutions (EA) Ltd P.O. Box 16027 Arusha, Tanzania Meru View Business Park, Kaloleni near New NSSF Building, Tel: +255 784 712 303 +255 754 226 116 E-mail: marketing@kiliativegroup.com Web: www.kiliativegroup.com

A R T I C L E S AVA I L A B L E T H I S M O N T H

07 | Makala: Huduma za kulima, kupanda, kuvuna. Ni fursa ya soko la viwanda

12 | Mjasiriamali Anayejitambua

Mambo 20 niliyojifunza

14 | Makala: Soko la ajira ya

huduma za ugani kwenye mnyororo



Tips

Marketing

by: Jennifer Ayoti

Party Survival Strategies Wedding season is coming up…and yes those birthday parties we have to attend lest we are kicked out of family circles! My favorite part in all the celebrations is spending time with family and friends especially people I may not have seen in a long time. Catching up with the latest family gossip and events that happened in the past year makes me so happy. That’s the good part.

Eat before you go to the party. This one is my favorite, I use it for wedding occasions especially if I am attending with my kids. I eat a healthy meal that contains a good balance of carbs, fiber, protein, water and healthy fats as this keeps you full and satisfied for hours.

What I am not so happy with, is the kind of food that is served sometimes. And yes, we get to experience those “friends” who push us to eat the junk food by taking us on a guilty trip “"Oh, just have a coke. It's a party, for goodness' sake and auntie really went out of her way to buy all these stuff and to make this food” I am sure you can relate. Here is what I feel- we should all treat ourselves to whatever tasty food we like as long as we are conscious about it. Going on an all-out spree in the name of “it’s a party” is just going to end up with having you feel awful in the long run.

This strategy is so effective in that when you are ushered to the long buffet, you end up keeping it light and enjoying the conversations and interactions more.

So since this party invites will keep coming and we have no choice but to attend, how can we get through them effectively and keep off the "junk-food pushers" and all those who are too quick to judge us? Here are my 3 party survival strategies you could use;

Drink enough water. Ensure you take enough water before heading to the party and during the party. This also works when you have planned to eat out at a restaurant, visiting a relative or when you're not the one preparing the food, you might be overindulging without even knowing it. Drinking water before meals not only hydrates your body, but also fills your stomach and keeps off unnecessary calories. Be mentally prepared to work it out the next day It’s never that serious and yes sometimes we overindulge especially when the company is too good! You ate too much cake or poured too much cream on your tea…its ok, it is not the end of the world- this shouldn’t dictate the rest of your week. The next important step is to get right back on your plan and start healthy the next day. Your healthy journey should be an enjoyable one- clean and healthy and not a do or die plan. The ability to “get back on your healthy eating plan is what’s important

4.

October, 2016

To your health!




Makala

Huduma za

Kulima, Kupanda, Kuvuna ni fursa ya soko la viwanda

Imeandaliwa na: Herment A. Mrema, Barua pepe: arudesiafrica@yahoo.co.uk | Simu: 0715-301494 / 0752-110290

Kilimo cha Watanzania wengi bado ni cha jembe la mkono ambalo mkulima wa kawaida hawezi kulima eneo kubwa licha ya kuwa tuna ardhi kubwa ambayo inafaa kwa kilimo lakini bado haijalimwa. Kutokana na kutumia jembe la mkono wakulima hasa wadogo wameendelea kuwa kwenye lindi la umaskini kwa kuzalisha ili kujikimu. Wakulima wengi hawaweki akiba ya chakula kwa kuwa hata kile kidogo wanachozalisha inabidi wakiuze kupata fedha za kununua mahitaji ya muhimu kama chumvi, sukari, kibiriti, mavazi, elimu, matibabu na mengineyo. Kwa hiyo wakulima wanalanguliwa kwa kuuziwa chakula kwa bei ya juu kwa mkopo wakati wanalima na wanatakiwa walipe mikopo hiyo kwa kutumia mazao hayo machache waliyopata. Hivyo kwa ujumla umaskini unaongezeka nchini Tanzania badala ya kupungua. Ili wakulima watoke kwenye huu mfumo wa kuporwa jasho lao lazima wabadilike wakumbatie kilimo cha kibiashara ambacho kitawapa fursa ya kuzalisha, kusindika na kuuza bidhaa zitokanazo na mazao kwa bei ya ushindani. Wakulima wakishirikiana na wadau wengine kwenye mnyororo wa ongezeko la thamani wanaweza kushiriki kupanga bei badala ya kupangiwa bei. Kwa kutumia mnyororo wa ongezeko la thamani kipato cha wakulima kitaongezeka sana na kutakuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya mashini na matrekta ya kulimia, kupandia, kuvuna na kusaďŹ risha. Badala ya wakulima kumiliki mashini zao mfumo huu wa ongezeko la thamani unajenga uwezo wa wakulima wafanyabiashara walio kwenye vikundi kuwa na mpango wa biashara ya kilimo na utekelezaji. Kwa kutumia mipango hii wanaweza kuingia mikataba na wasambazaji wa mwisho wa kiasi cha mazao watakayouza. Mpango biashara utaonyesha ni ukubwa gani wa mashamba ambayo yatazalisha mazao, jinsi yatakavyovunwa, kusindikikwa na kusambazwa. Kwa vile wakulima watahitaji kutumia mashini ili waweze kuwa na kilimo cha kibiashara wanajenga hoja ya uhitaji wa huduma za kulima mashamba yao, kupanda, kuvuna na kusaďŹ risha kwenda ghalani. Katika mfumo huu wa mnyororo kuna mkakati wa kuwahamasisha wafanyabiashara kuwekeza kwenye mashine ambazo tayari zitakuwa na kazi za kufanya.

Kazi ya meneja wa mnyororo wa ongezeko la thamani ni kuhakikisha mashini hizi zinapatikana, kazi ya kufanya ipo, na zinasimamiwa kuhakikisha kuwa zinatumika vyema na wenye mashine hizi wanalipwa kwa huduma walizotoa. Kwa sasa hivi kila mwenye trekta lake anakimbizana kutafuta kazi, na kumsimamia dereva na meneja wake jambo linalofanya kazi ya kulima kwa trekta kuwa ngumu na kutokuwa na faida. Madereva wa trekta na wasimamizi wa trekta hizo wanakula njama kumdhulumu mwenye trekta hivyo biashara inakuwa haina faida kwa mwenye mali. Kwa mfumo huu wa mnyororo wenye mashine watakuwa na kazi za uhakika, mashine zao zitasimamiwa kwa gharama nafuu na wenye mashine watalipwa vizuri na kufanya biashara hiyo iwe ya faida. Kwa kutumia utaratibu huo kutakuwa na wawekezaji wengi sana kwenye shughuli za kulima, kupanda, kuvuna na kusaďŹ risha na matokeo yake ni kuwa na soko kubwa la mahitaji ya mashini kama matrekta, planters, combine harvesters, na mashine nyingine nyingi. Kuongezeka kwa mahitaji hayo kutahamasisha wawekezaji wa nje na wa ndani kujenga viwanda vya kutengeneza mashine hizo hapa nchini. Kwa kufanya hivyo Serikali ya awamo ya tano itakuwa imetimiza sehemu ya ndoto zake za kufanya Tanzania nchi ya viwanda. Kama ilivyo kawaida viwanda vitahitaji nguvu kazi hivyo viwanda hivi vitaweza kuajiri vijana wengi ambao watakuwa wanafanya kazi viwandani na wengine kutoa huduma kwa wafanyakazi wa viwandani. Viwanda hivi vitakuwa na faida kubwa kwa sababu ya kutumia mfumo wa mnyororo wa ongezeko la thamani hivyo kuwa na uwezo wa kulipa kodi za serikali.

October, 2016

7.



October, 2016

9.




“Mambo 20 Niliyojifunza

Kwenye Kitabu cha YOU CAN WIN (UNAWEZA KUSHINDA)”

Mjasiriamali Anayejitambua

imeandaliwa na Daudi Mwakalinga

Inaendelea.... 9. Hatua ya Tano: Tengeneza heshima binafsi (self-esteem). Heshima binafsi ni jinsi unavyojihisi mwenyewe au jinsi unavyojiona ndani yako. Kama ukijihisi vizuri ndani mwako hata utendaji wako unakwenda juu, mahusiano yako yanakua bora kuanzia nyumbani hadi kazini, hata dunia unaiona nzuri zaidi. Sababu ni kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya jinsi tunavyojihisi wenyewe na tabia au mwenendo wetu. Kama unataka kutengeneza heshima binafsi chanya, njia ya haraka ni kufanya kitu kizuri kwa wale wasiokua na uwezo wa kukulipa. Unaweza kutoa msaada wa fedha au wa kujitolea kwa wengine ambao ni wahitaji. Unapowasaidia wengine bila kulipwa unajihisi vizuri, heshima binafsi inaongezeka. Givers have high self-esteem, positive attitude and they serve society. 10. Hatua ya Sita: Epukana au kaa mbali na Vishawishi hasi (negative influences). Vishawishi hasi vinaweza kua watu au marafiki wenye mtazamo hasi, ama vyombo vya habari vyenye habari hasi. Mfano unakuta watu wanaokuzunguka kila siku ni kuongea umbea tu kuhusu wengine, au kukuelezea habari mbaya mbaya tu mara za uchawi, kufumaniwa, ajali au habari za mapenzi tu. Yaani hakuna siku mnajadili mawazo (ideas) zenye kuwapeleka mbele. Kwenye vyombo vya habari, unakuta kila mara unasikiliza ajali, mara siasa chafu, mara vita, tena habari hizi unazisikia au kuziona asubuhi mchana na hata jioni. Hivi akilini mwako unadhani ni nini kinajengeka? Ni mtazamo hasi kuhusu dunia, watu au hali fulani. Stay Away from negative influences. 11. Hatua ya Saba: Jifunze kupenda vitu ambavyo vinahitajika kufanywa. Baadhi ya vitu vinahitaji kufanywa bila kujali tunavipenda au hatuvipendi. Mfano mama kulea mtoto wake haijalishi anapenda au hapendi anahitajika kumlea. Vipo vitu ambavyo kila mmoja wetu anapaswa kuvifanya bila kujali anavipenda au hapendi, lakini ni muhimu kuvifanya. Kutokuvipenda ndio hupelekea kuviahirisha au kuacha kabisa kuvifanya. Sasa chakufanya, angalia vile vitu vyote unavyodhani vimekua ni vya muhimu sana kwako lakini kila ukitaka kuvifanya unavipiga kalenda. Orodhesha vitu hivyo anza na kimoja kimoja, jifunze kukipenda, angalia uzuri wa shughuli hiyo, pata picha jinsi utakavyonufaika pale utakapokua umekifanya tayari. This may not always be fun, and may even be painful. But learn to like the task, the impossible becomes possible. 12. Hatua ya Nane: Ianze siku yako na kitu chanya. Soma au sikiliza kitu chanya wakati wa asubuhi. Baada ya kulala akili inakua imepumzika na kutulia vizuri. Tunapoamka akili yetu ya ndani (subconscious mind) inakua ipo tayari kupokea kitu cha kwanza asubuhi, kitu hicho ndicho kitakachoitawala siku yako nzima. Kwa bahati mbaya akili yetu hii (subconscious mind) hua haichagui, inaingiza kinachokuja. Unapoanza asubuhi yako na habari hasi, uwezekano ni mkubwa wa kukutana na mambo hasi siku nzima. Hivyo ni muhimu sana unapoamka kabla ya kukutana na watu anza kuipatia akili yako kifungua kinywa kizuri. Unaweza kusoma, kusikiliza au kuangalia vitu chanya vyenye kukuhamasisha. Start your day with something positive. 13. Mwanadamu amepewa Zawadi Kuu. Ukiangalia mwanadamu hawezi kupeperuka kama ndege, hawezi kukimbia kumzidi chui au duma, hawezi kupanda miti kwa haraka kama tumbili au ngedere. Mwanadamu hana jicho lenye uwezo mkubwa kama tai, wala hana meno na makucha makali kama Simba. Ukicheki mwili wa mwanadamu ulivyo hauna kinga au vitu vya kujilinda kama walivyo viumbe wengine. Hata mdudu mdogo tu anaweza kumuua mwanadamu. Lakini Mungu ni wa ajabu sana, akampatia mwanadamu zawadi kubwa sana. Zawadi kuu hiyo tuliyonayo wanadamu inayotutenganisha na viumbe vingine ni UWEZO WA KUFIKIRI. Kwa kutumia uwezo huo, mwanadamu anaweza kutengeneza mazingira yake ya kuishi wakati wanyama wao huchukuliana na mazingira (adapt) kama yalivyo. Uwezo wa kufikiri ndio unamsaidia mwanadamu kuumba au kutengeneza vitu ambavyo vinaweza kurahisi shughuli na kuboresha maisha yake. Cha kuhuzunisha ni kwamba wachache sana ndio wanaoweza kutumia zawadi hii hadimu kwa kiwango chake cha mwisho.

12.

October, 2016

14. Maisha yamejaa machaguo (choices). Kila chaguo lina madhara yake chanya au hasi. Mfano unapochagua kula kupita kiasi ni kwamba unachagua kua na kiriba tumbo (obesity) au uzito uliozidi ambao hupelekea kupatwa na magonjwa mengi kama kisukari, shinikizo la damu, matatizo ya moyo n.k. Tuna uhuru wa kufanya uchaguzi, ila tukishachagua, uchaguzi tuliofanya ndio unaotudhibiti. Fanya uchaguzi sahihi. 15. Mafanikio hayapimwi kwa nafasi uliyofikia katika maisha, wala hayapimwi kwa vitu ulivyonavyo kama fedha, magari, nyumba n.k. Mafanikio ya kweli yanapimwa kwa vikwazo ulivyoweza kuvishinda. Nelson Mandela aliwahi kusema kwamba watu wasiyapime mafanikio yake kwa kutizama alikofika, bali kwa kutizama ni mara ngapi alijaribu akashindwa na kuinuka tena. Vile vile mafanikio hayapimwi kwa kujilinganisha na wengine bali unapaswa kujipima kwa kuangalia jinsi unavyofanya ukilinganisha na uwezo wako (potential) ulionao wa kufanya mambo. Kila mtu ana uwezo wake binafsi ambao ni mkubwa sana kutegemeana na kusudi mtu alilopewa, hivyo ukitumia wengine kama kipimo utakua hujitendei haki, maana yawezekana uwezo ulionao (Potential) ni mkubwa kuliko hao unaojilinganisha nao. Watu waliofanikiwa wengi wao walishindwa mara kadhaa, walianguka mara nyingi lakini wakapanda juu tena. 16. Mafanikio sio kitu kinachotokea kama ajali au kama bahati. Kuna hitajika maandalizi ya kutosha pamoja na tabia. Maandalizi ni kwa ajili ya kupata hayo mafanikio, tabia ndiyo itakayokufanya uendelee kuwepo kwenye mafanikio. Kila mtu anapenda kushinda, lakini watu wengi hawako tayari kutia juhudi na muda wa kujiandaa kushinda. Kwenye mafanikio bahati hutokea pale maandalizi yanapokutana na fursa, yaani fursa ikitokea unakua ulishajiandaa tayari, wewe ni kuitumia vizuri. Mafanikio yanahitaji kujidhabihu/kujitoa sana pamoja na kuweka nidhamu binafsi. Everything that we enjoy today is a result of someone’s hard work. There is no substitute for hard work. 17. Katika biashara matatizo mengi ni matatizo yanayohusu watu. Tukiweza kutatua matatizo ya watu wetu (wafanya kazi) basi matatizo ya biashara nayo yanatatulika.


Mfano kuna hoteli moja hapa Mwanza hua ninapenda kwenda hasa mwisho wa wiki, hua napenda kwenda hapo Kujisomea kwa sababu pametulia na ni jirani kabisa na ziwa Victoria. Ila sasa wahudumu hua wanagombana na wateja mara kwa mara, wengine wanawajibu wateja jinsi wanavyotaka, yaani huduma kwa wateja ni mbovu. Kuna wakati wahudumu wao kwa wao wanajibizana hata mbele ya wateja. Sasa wateja wakipungua na mauzo yakishuka hapa unaweza kusema biashara ndio tatizo? Kwa bahati nzuri wiki hii nilifanikiwa kwenda tena hotelini hapo, na kulikua na kikao cha wafanyakazi wa hoteli hiyo. Walipata ugeni wa viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Mahotelini, Majumbani, Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWU). Viongozi hao walikua wamekuja kuwaelimisha wafanyakazi hao kuhusiana na wajibu wa chama hicho lakini pia kusikiliza kero zao. Kwa vile nilikua siko mbali sana nilisikia kila kilichokua kinaongelewa. Mfanyakazi mmoja akasema, kwamba mwajiri wao hawajali, akatolea mfano hata chakula kila siku wanapewa ugali kabichi, kitu kinachowafanya hata wakati mwingine kushinda bila kula kuliko kufululiza tu kula kabichi. Mwingine akadakia kabla mwenzake hajamaliza, akasema “yaani wakati mwingine unamhudumia mteja huku wewe hujala, unatamani hata chakula cha mteja”, Hapo unaweza kuona uhusiano kati ya huduma wanayotoa na jinsi wanavyojaliwa na mwajiri. Hii ni wazi kwamba wafanyakazi hawafurahii kazi yao na ndio maana hawawajali wateja. Jali wafanyakazi wako, na wao watawajali wateja wako. 18. Katika kuweka malengo, ni muhimu sana kuzingatia uwiano (balance). Watu wengi wanapoweka malengo hutizama fedha na vitu kama magari nyumba viwanja n.k Hebu jiulize ukipata fedha nyingi halafu afya yako ikawa ya mgogoro kisha ukatumia fedha hizo kwenda kujitibu utakua umefanya nini? Au ikitokea umefanikiwa kupata fedha nyingi lakini ndoa yako au familia imesambaratika kwa sababu ya kukosa muda wa kuilea kwa kuwa uko bize kutafuta fedha, hapo utafurahia maisha? Katika kuweka malengo hebu tanua mawazo yako yasitazame fedha peke yake.

Weka uwiano, angalia swala la afya yako, weka malengo ya kuhakikisha unakua na afya njema. Weka malengo yanayohusu mahusiano yako na Mungu wako, mahusiano yako ya kifamilia (ndoa na watoto) na mahusiano yako na watu wengine. Weka malengo yanahusu kazi au biashara yako, Weka malengo yanahusu fedha. Pia waweza kuweka malengo binafsi. Hayo ni baadhi ya makundi muhimu katika kuweka malenga. Goals must be balanced. 19. Ukarimu ni lugha ambayo kiziwi anaweza kuisikia, na kipofu anaweza kuiona. Bora zaidi kumjali rafiki yako kwa ukarimu wakati yuko hai, kuliko kupeleka maua mazuri kwenye kaburi lake wakati ameshafariki. Kind words never hurt the tongue. 20. Washindi wanaacha kumbukumbu zinazoishi (legacy) hata baada ya wao kuondoka. Hebu pata picha watu kama kina Abraham Lincoln, Mother Theresa, Patrice Lumumba, Bob Marley, Martin Luther King Jr., Alfred Nobel, Nelson Mandela, J.K Nyerere. Mahatma Gandhi, Isaac Newton n.k hadi leo watu hawa wanaishi japo hawapo nasi kimwili, dunia bado inawakumbuka na inatumia falsafa zao kwenye mambo mbalimbali. Je wewe baada ya kuondoka hapa duniani, utaiachia dunia kitu gani ambacho kitabakia kama historia yako? Kama tu watu wengi wanakufa wakati bado wanaishi, sasa wakishakufa kimwili si ndio wanasahaulika baada tu ya matanga? Bila kujali umri wako unaweza kuamua leo, kutengeneza historia yako unayotaka ikumbukwe baada ya wewe kuondoka hapa duniani. Ukishajua unataka dunia ikukumbuke kwa lipi, nenda mbele zaidi kwa kujua ni vitu gani unapaswa kufanya ili uweze kufikia hiyo hatua ya kukumbukwa kisha anza kuvifanyia kazi. Our greatest responsibility is to pass on a legacy that the coming generation can be proud of. Asante sana, Tukutane toleo lijalo. Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe: daudimwakalinga@yahoo.com dd.mwakalinga@gmail.com

October, 2016

13.


Soko la ajira

Article:

ya huduma za ugani kwenye mnyororo

Imeandaliwa na: Herment A. Mrema

Huduma za ugani ni pamoja na maelekezo ya kitalaamu na usimamizi wa shughuli zote zinazohusiana na kilimo kuanzia kutayarisha mashamba, kuchagua mbegu, kutayarisha mbegu ambazo ni pamoja na vitalu, kupanda, kuhudumia mashamba, kuvuna, kuhifadhi na kuuza. Huduma hizi kwa kawaida zinatolewa kwa wakulima wadogo na watalaamu ambao ni waajiriwa wa serikali. Kwa muda mrefu sana mpaka sasa hivi Serikali haijaweza kuajiri maafisa ugani kufuatana na mahitaji licha ya jitihada kubwa kwa serikali kuipa kipaumbele shughuli za ugani. Miaka kama ishirini iliyopita Serikali ilikuja na wazo la kubiashara huduma za ugani ambazo wakulima wangetakiwa wagharamia huduma hizi. Kuna wafanyakazi wachache waliacha kazi serikalini na kuwezeshwa kwa muda fulani kujijenga ili waweze kutoa huduma za ugani kibiashara. Bahati mbaya bidii hizi zilishindikana na wafanyakazi waliojaribu kutoa huduma za ugani kibiashara walirudi serikalini kama waajiriwa wa kawaida. Katika kufanya utafiti mdogo kushindwa kwa madhumuni ya kutoa huduma za ugani kibiashara kumetokana na sababu nyingi lakini sababu kubwa kuu ni pamoja na wakulima wenyewe kutokuwa tayari kufanya kilimo cha kibiashara, watalaamu wa ugani kutokuwa na maono au utashi wa kutoa huduma kibiashara na ile imani kuwa ni vigumu kuwa na kilimo cha kibiashara. Ukweli usiopingika ni kuwa hakuna biashara yenye faida kama kilimo ali mradi vihatarishi vyote vinafanyiwa kazi na kuwa na mpango wa kuepuka na vihatarishi hivyo.

Vihatarishi vikubwa ni pamoja na ukame, wadudu, na magonjwa ya mazao ambavyo vinaweza kujengewa uzio kwa kuwa na kilimo cha umuagiliaji, kutumia madawa yenye ubora ya uhakika ambayo yapo sokoni, kutumia mbegu mbazo zinaweza kuhimili ukame na magonjwa na pia kilimo cha umwagiliaji. Kwa kutumia mfumo wa mnyororo wa ongezeko la thamani ambao unamjengea uwezo mkulima kwa kushirikiana na wadau wengine, kulima, kusindika na kuuza bidhaa zilizoongezewa thamani zenye nembo ya mkulima, anakuwa na haki ya kupanga bei ambayo inalipa gharama zote na kupata faida kubwa. Wakulima wakishirikiana na Meneja wa Mnyororo wa ongezeko la thamani wanaweza kuajiri na kutumia huduma za maafisa ugani kibiashara na kulipa ujira mzuri zaidi kuliko ujira unaolipwa na serikali. Kwa vile maafisa hawa wanalipwa kutokana na huduma ambazo zinachangia kuboresha kilimo maafisa hawa wanaweza wakawa na hadhi sawa na maafisa mifugo. Maafisa mifugo huwa wanapewa heshima zaidi kwa sababu wafugaji huwa wanathamini mifugo yao kuliko wakulima wanavyothamani mazao yao. Wakulima watathamini mazao yao ikiwa itawalipa zaidi kuliko mifugo na hii tataokea wakati kilimo kitakuwa cha kibiashara na wakulima kuuza bidhaa badala ya kuuza mali ghafi. Hatua zozote za kulima kilimo cha kibiashara na kutumia maafisa ugani kibiashara, kitaongeza kipato cha wakulima ambao watahitaji huduma nyingi zaidi za maafisa ugani. Hivyo maafisa ugani walioajiriwa na serikali watakuwa wanatoa huduma zao kibiashara na kulipwa na wakulima. Kazi ya Serikali na sekta binafsi ni kuzalisha maafisa ugani ambao watahitajiwa na wakulima kila shughuli za kilimo zinavyoongezeka na wakulima wengi kukumbatia kilimo biashara na kuongezeka kwa kipato. Kwa sasa hivi Tanzania ina tatizo la ajira na wanafunzi wengi hawapendi kusomea kilimo kwa sababu shughuli za kutoa huduma za ugani hazilipi. Hivyo ni muda muafaka kwa Serikali kuweka nguvu nyingi katika minyororo ya ongezeko la thamani ya mazao ambayo inasimamiwa na wakulima mdogo wakishirikiana na wadau wengine. Mkakati huu wa serikali utapunguza gharama za kuhudumia kilimo, utaongeza ajira, utaongeza kipato kwa wakulima, kupanua soko la ajira na kujenga mfumo mzuri wa ukusanyaji wa kodi. Jinsi Serikali inapopanua wigo wa vyanzo vya kodi na walipaji kodi kuongezeka inakuwa rahisi kupunguza kiasi cha kodi kwa kila mlipaji.

14.

October, 2016




EVENTS BY PICTURES

A SEMINAR ON ENSURING EFFICIENCY IN COMMERCIAL EGG PRODUCTION

Organizers: PREMIUM INGRIDENTS LTD & EVONIK VENUE: MOUNT MERU HOTEL, ARUSHA -TANZANIA | DATE: 28th September 2016

A technical seminar organized by Premium Ingredients Ltd in partners with Evonik at the Mount Meru Hotel. The aim was to educate farmers on the importance of egg production and the advantages that lead to a great source of income and a better reliable market in the end. LIMA Magazine was on location together with other participants in the agricultural industry including Kijenge Animal Poultry, Mchaki Agrovet ,Harsho Group, Bontera, Sianga Intertrade Ltd just to mention a few.







Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.