Dkt (PhD) John P Magufuli Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
KARIBU MBEYA MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya
MV Njombe na MV Ruvuma
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
UTANGULIZI
Serikali ya Awamu ya tano ni mwendelezo wa Serikali zote tangu Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Historia ya Makuzi ya Demokrasia Tanzania inajipambanua kwa chaguzi za huru na haki kila baada ya miaka mitano. Utashi wa kiuongozi wa viongozi wetu ndio uliopelekea viongozi wengine kupokea kijiti cha uongozi wa taifa bila fujo au vurugu zozote. Hali ya Demokrasia nchini ni funzo kwa mataifa mengine mengi katika Afrika na duniani. Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassani Mwinyi alipokea kijiti cha Uongozi toka kwa Baba wa Taifa miaka ya 1985. Hata hivyo wakati wa uongozi wake, Taifa la Tanzania liliingia katika mfumo wa vyama vingi (1992) kama ishara ya kutanua zaidi mipaka ya Kidemokrasia nchini. Tangu Taifa limeingia katika mfumo wa vyama vyingi Chama Cha Mapinduzi (CCM) bado ni chama Tawala ambacho kimedumu kwa miongo takribani minne kikiwa madarakani. Ni kweli kwamba Chama Cha Mapinduzi kina mifumo ya kujisahihisha na kujikosoa mbele ya watu. Aidha kimejenga misingi bora ya urithishaji wa madaraka na uongozi pamoja na misingi mizuri ya kidemokrasia inayo ruhusu kuadabishana, kuheshimiana na kulinda utu na fikra za kila mmoja. Aidha Serikali ya Tanzania imepata vionjo vya Marais watano tangu nchi imepata uhuru. Rais Julius K. Nyerere 1960 – 1985, Rais Ali Hassan Mwinyi 1985 – 1995. Rais Benjamini William Mkapa 1995 – 2005, Rais Jakaya Mrisho Kikwete 2005 – 2015 na sasa Rais Dkt. John P. Magufuli 2015 hadi sasa.
3
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
UMOJA NA AMANI WA TAIFA
Taifa la Tanzania limejengwa katika misingi ya Umoja na Amani. Hali ya Amani na Umoja wa leo unatokana na misingi walioiweka waasisi wetu wa Taifa Hayati Mwalimu Julias K. Nyerere na Hayati Abeid A. Karume wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha Muungano wa leo wa Tanzania na Zanzibar ni moja ya jambo kubwa linalofaa kuenziwa wakati wote. Tuendelee kuwakumbuka na kuwaombea ili Mungu wetu aendelee kuzilinda na kuzihifadhi mahali patakatifu roho za marehemu waasisi wa Taifa letu.
UONGOZI WA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI
Uongozi wa Rais Mhe. Dkt . John Pombe Magufuli umeimarisha zaidi Uwajibikaji, Uzalendo, Uchapakazi na Nidhamu ya kila kitu katika maisha ya mtanzani. Pengine iwe ni muda muafaka kumshukuru Mhe. Dkt . John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa ya mfano katika kukuza na kuboresha Uchumi wa Taifa letu. Tumpongeze kwa yafuatayo:
• • •
•
Kukuza Uchumi wa Taifa. Kuhamasisha ujenzi wa viwanda vidogo vya kati na vikubwa. Kusimamia ipasavyo Elimu bora ya msingi na Sekondari kwa kupanua wigo wa wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu toka HESLB. Kuendelea kuimarisha na kupanua Miundombinu ya Barabara, Reli, Ndege, Meli n.k
4
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
• • •
Ujenzi wa Stigler’s gorge kwa ajili ya umeme Mkubwa, utakaokuwa mwafaka kwa uchumi wa viwanda. Ujenzi wa SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Dodoma. Uimarishaji wa Huduma za Afya ikiwa pamoja na ujenzi wa Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati nchini.
MKOA WA MBEYA
Mkoa wa Mbeya una Kilometa za mraba 35,960 na Wilaya tano. Kilimo kikuu ni Mpunga, Ndizi, Viazi, Mahindi, Alizeti, Tumbako na Pareto. Mkoa una watu wasiopungua 2,136,614 Hali ya amani ni kubwa na tunawakaribisha watu wote waweze kuwekeza.
ELIMU a) Shule za msingi zipo 738 za Serikali 706 wanafunzi 403022 wanaonufaika na elimu bure. b) Shule za Sekondari zipo 226. 158 za Serikali na 68 za binafsi(private) shule hizi za Serikali zina jumla ya wanafunzi 88,616 wanaonufaika na Elimu bure. Tunashukuru sana mwaka 2017/2018 tumepokea jumla ya sh. Bilioni 18,444,861.036. 6.9 Bilion Elimu ya msingi tu 11.4 Bilioni Elimu ya Sekondari. 3.4 Bilioni posho ya madaraka c) Tumepokeaa jumla ya shilingi 2.137 bilioni kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya vyumba vya madarasa katika shule 45 na madarasa 171. d) Mkoa wetu pia umepokea jumla ya fedha 5.4 Bilioni fedha za mradi lipa kulingana na matokeo (EP4R).
5
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
e) Mheshimiwa Rais asante kwa fedha ulizotupatia jumla ya shilingi 1.03 Bilioni kwa ajili ya ukarabati wa shule Kongwe za Loleza na Iyunga. f) Upanuzi na Ukarabati wa vyuo vya kati na Vyuo vikuu. (1) Chuo cha Ualimu Mpuguso umetupatia shilingi 9.6 Bilioni (2) Msasani 700,000 milioni. (3) Mzumbe – ujenzi wa madarasa na kumbi za mihadhara (4) MUST – Ujenzi wa maktaba ya kisasa. (5) Chuo kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi shirikishi Bewa la Mbeya(University of Dar es Saalam, College of health and allied Science, Mbeya branch. • Upanuzi wa majengo ya mihadhara. • Vifaa tiba n.k
(A) AFYA: Mheshimiwa Rais tunashukuru sana fedha Taslimu 6.7 Bilions kwa ajili ya vituo vya Afya (i) Iyunga (Mbeya Jiji) 400 Milioni (ii) Nzovwe (Mbeya Jiji) 500 Milioni (iii) Ntaba (|Busokelo) 400 Milioni (iv) Isanga (Busokelo) 500 Milioni (v) Mpata (Busokelo) 400 Milioni (vi) Mtande (Chunya) 400 Milioni (vii) Chalangwa (Chunya) 400 Milioni (viii) Masukuru (Rungwe) 500 Milioni (ix) Ikuti (Rungwe) 500 Milioni (x) Santilya (Mbeya DC) 500 Milioni (xi) Ilembo (Mbeya DC) 400 Milioni (xii) Ikukwe (mbeya DC) 800 Milioni (xiii) Ipinda (Kyela) 500 Millioni (xiv) Utengule – Usangu 500 Milioni
6
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
(B) HOSPITALI Jumla ya tumepokea bilioni 4.5 kwa ajili ya Hospitali za wilaya Mbarali 1.5 Bilioni, Mbeya DC 1.5 Bilioni na Busokelo 1.5 Bilion. Pia tunashukuru kwa fedha zaidi ya million 500 kukarabati na kupanua kitua cha Afya cha Igawilo kuwa Hospitali ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya. (C) BARABARA TANROAD inahudumia barabara zenye jumla ya urefu wa km 1270.3 kilometa 577.8 Barabara kuu na 692 Barabara za mikoani km 389.7 ni lami. • Barabara kuu Igawa Mbeya km 116 • Barabara Mbeya hadi Songwe km 38 • Barabara Iyayi hadi Igawa Km. 12 zimekamilika • Barabara Njombe hadi Isyonje Km 205 • Barabara Isyonje hadi Kikondo Km 22 • Barabara zote hizi zimefanyikwa upembuzi yakinifu • Barabara ya mchepuko kutoka Inyala km 40 hadi mbalizi • Barabara Mbeya hadi Chunya Km 72 shilingi 95 bilioni • Barabara Chunya hadi Makongorosi Km 39.5 shilingi bilioni 56 • Barabara Kikusya hadi Ipinda Km 59.9 • Barabara Tenende hadi Matema Km 6.6 Juml KUU 65.5 bilioni. • Barabara Igawa Ubaruku 6.1 Bilion Km. 6 • Jiji la Mbeya linatekeza mradi wa uboreshaji miundombinu ya kimkakati katika Manispaa za majiji. Tunashukuru tumepokea jumla ya shilingi 14.04 Bilioni. (D) UCHUKUZI (1) Upanuzi wa bandari ya Itungi (2) Ujenzi wa Meli 3 = 20.1 Bilioni (3) Ukarabati Uwanja wa ndege wa Songwe. (4) Kuongeza idadi ya ndege uwanja wa Songwe kufikia ndege 2.
7
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
(E) MAPATO Makusanyo ya maduhuli ya Serikali (Uhamiaji). 500,035,000 (2018) - 1,052,310,000 (2019) $159,920 (2018) - 237,630 (2019) (F) VITAMBULISHO VYA NIDA Jumla ya vitambulisho 940. (G) KILIMO Kilimo kimechangia 45% ya uzalishaji mazao ya chakula tani 3,352,623 mahitaji yalikuwa 569.705 ziada ilikuwa 83%. Mahitaji ya Mbolea ni tani 97.862. hadi sasa tumeshatumia tani 64,273 (H) MIFUGO Jumla ya mifugo 3,399,805 Ng’ombe 703.726, Mbwa 195.569, Kondoo 79,850. (I) VIWANDA Kuna jumla ya viwanda 3,660 vikubwa 10 vidogo 3630 vya kati 60. (J) UWEKEZAJI Tunakaribisha ana wawekezaji. (K) TAASISI ZA FEDHA • Vyama vya Ushirika jumla vipo 488 SACCOS 210 • Mfuko wa Wanawake na vijana jumla ya milioni 845.00 • Wanawake vikundi 95 – 427.7 milioni • Vijana 56 – 402.3 milioni • Tarafu – Walengwa 41.889 kutoka vijiji 520 – 36,259,620,150 • Tarafa 15 vijiji 533 (L) VIVUTIO VYA UTALII Mkoa wa Mbeya una unavivutio vingi sana vya utalii kama vile Ziwa ngosi. (M) TANESCO: Vijiji vipo 533 kati ya 380 vina Umeme. Taarifa hii Imeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila 8
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
TIMU YA VIONGOZI WA SERIKALI YA MKOA WA MBEYA
Mh. Albert Chalamila Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mh. Marryprisca Mahundi Mkuu wa Wilaya ya Chunya
Mh. Mariam A. Mtunguja Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya
Mh. Paul Ntimika
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya
Mh. Reuben Mfune
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali
Mh. Claudia Kitta
Mkuu wa Wilaya ya Kyela
Mh. Julius Chayla
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe
9
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
VIVUTIO VYA KITALII
Mkoa wa Mbeya Una vivutio vingi sana vya kitalii, ambavyo vinaweza kuwa vutia wageni wengi kuutembelea mkoa huu na hivyo kuwa chanzo kikubwa sana cha mapato. Vivutio hivyo ni 1. Nyumba ya Maficho ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. 2. Ukumbi wa mkapa na jukwaa Ndani yake. 3. Shule na Nyumba ya Samora Machel. 4. Shule ya sekondari ya wasichana ya Loleza. 5. Shule ya Iyunga. 6. Barabara iliyojuu zaidi nchini Tanzania. 7. Sehemu ya kuangalizia Bonde la Ufa. 8. Ziwa Nyasa. 9. Ziwa Ngosi. 10. Ziwa Kiungululu. 11. Ziwa kisiba. 12. Ziwa Itende. 13. Ziwa Kingili. 14. Ziwa ilamba. 15. Mlima Rungwe. 16. Mlima Loleza. 17. Mlima Mbeya. 18. Lusiba Lukafu. 19. Lusiba lwa Misi. 20. Maporomoko ya Maji Malasusa.
21. Maporomoko ya Maji Kapiki. 22. Maporomoko ya Maji Malamba. 23. Maporomoko ya Maji Kapologwe. 24. Maporomoko ya maji Mwalalo. 25. Kipunji. 26. Maji Moto Mbambo. 27. Maji Moto Kyela. 28. Pango la kuabudia Likyala 29. Msitu wa Katago. 30. Ikato lya Nyerere. 31. Daraja la Mungu. 32. Kijungu jiko. 33. Majengo ya wakoma 34. Majengo ya wajerumani Masoko. 35. Makanisa ya zamani, Mwakaleli, Roma, Anglikana. 36. Mti Mkubwa wa Masoko. 37. Mahakama ya chifu lyoto. 38. Kilimo cha mazao mbalimbali Mpunga, Ndiiz, Chai Nk. 39. Utamadani wa watu wa Mbeya. 40. Samaki wa Rangi.
10
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
ASILI YA NENO MBEYA
Historia ya mkoa wa Mbeya imegawanyika katika vipindi tofauti tofauti kabla ya uhuru na baada ya uhuru, Mji wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni waingereza mnamo mwaka 1927, Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana sana katika milima iliyopo karibu na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa. Katika kipindi cha ukoloni ulifahamika kama “Southern highland provience” kwa kujumuisha baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa na Rukwa na baadaye Mbeya. Asili ya neno Mbeya imekuwa na nadharia kadha wa kadha ambazo zinaelezwa na wataalam na wazee mbalimbali. Baadhi ya nadharia hizo ni pamoja na:1. Ibheya - Chumvi Nadharia hii inaeleza kuwa asili ya Neno Mbeya ni neno la kisafwa “Ibheya” lenye maana ya chumvi, Hii inatokana na wafanya biashara kufika katika mji huu na kubadirishana mazao yao kwa chumvii liyokuwa ikipatikana kwa wingi kipindi hicho. Ikapelekea wenyeji kuita eneo hili Ibheya kama sehemu ya kubadilishia chumvi na mazao, kutokana na sababu zakimatamshi ikapelekea wageni kuzoea kutamka na kuandika Ibheya. 2. Agamba mbeye – Kamlima Mbeye Nadharia hii inaeleza kuwa jina Mbeya limetokana na Mlima uliopo nyuma ya Chuo cha Kilimo Uyole (Agricultural Research Institute -ARI- Uyole) uliojulikana kwa jina la kisafwa kama Agamba Mbeye (kamlima Mbeye kwa kiswahili) Ambao hivi sasa ni maarufu sana kwa jina la Mlima ugari, ni mlima ambao una muonekano wa mviringo, sehemu za chini umeota nyasi japo si nyingi sana kama ilivyo sehemu ya juu ambayo haioti nyasi kabisa, hivyo ikawa sehemu nzuri ya kupumzikia wageni ilikupata hewa nzuri na muonekano mzuri wa mji, kutokana na changamoto za kimatamshi ikapelekea wageni kuliendeleza sana jina la eneo kama Mbeya kimaandishi na kimatamshi.
11
ZIWA NGOSI (NGOSI CRATER LAKE) Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini na 33.553°Mashariki, ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika katika crater lake baada ya lile lililoko nchini Ethiopia.Ziwa hili lina kina cha mita sabini na nne (74) Urefu wa kilomita 2.5, upana wa kilomita 1.5. Hata hivyo, wataalamu wanasema kwamba Ziwa Ngosi lina sifa za kipekee linazo litofautisha na lile lililoko Ethiopia. Moja ya tofauti hizo ni kwamba Ziwa Ngosi lime zungukwa na milima na misitu minene tofauti na lile la Ethiopia ambalo liko eneo lililo wazi na hufikika kwa urahisi kabisa kwagari kitu ambacho hakiwezekani kwa Ziwa Ngosi. Wataalamu wanasema kwamba kuwepo kwa ziwa hilo sehemu hiyo kunasaidia kuzuia milipuko ya mara kwa mara ya volcano kwakuwa linasaidia kupunguza misukumo ya gesi inayojijenga chini na kuanza kutafuta upenyo wa kutokea chini ya ziwa. Kitu cha kushangaza ni muonekano wa ziwa hili linakaribia kuwa na muonekano kama ramani ya bara la Afrika pamoja na visiwa vyake kama ilivyo kule Njombe ambapo kuna mwamba wenye ramani ya bara la Afrika unaitwa Lwivala, uliopo katika pori la hifadhi ya msitu Lwivala kijiji cha Igodivaha. Wilayaya Njombe ziwa 12
hili pia linaingiza tu maji na halitoi maji kwasababu liko katikati ya milima hivyo kuonekana kama liko shimoni na pia halina ufukwe. Ziwa hili linalopatikana katika Hifadhi ya msitu Uporoto (Poroto Ridge) yenye eneo la hekta 9,332 ipatikanayo karibu na vijiji vya Kisanga 4.3km Uyole (24.4km) na mji mdogo wa Tukuyu upatikanayo wilaya ya Rugwe. Yapo masimulizi mengi sana juu ya ziwa hilo la maajabu watu husema ziwa hili lilichomwa moto na wakazi wa kijiji cha Mwakaleli kwasababu lilikuwa likileta mikosi mingi kijijini hapo ikiwemo vifo vya mara kwa mara kwa watu na wanyama, Zipo imani miongoni mwa watu kuwa ziwa Ngosi watu wanapotea kimazingara, Kuwapo kwa sauti za watu wasiooneka na ndani ya misitu, wengine huamini huruhusiwi kuzungumza kinyakyusa, huruhusiwi kunywa maji, ziwa hilo limekuwa likigeuka rangi mara kwa mara nakuwa na rangi za kijani, bluu, nyeusi na nyeupe kitu ambacho kina wafanya waamini kuwa ziwa hilo sio la kawaida.
Kwanini utembelee ziwa Ngosi? • • • • •
Lipo ndani ya safu ya poroto ambayo ni sehemu ya hifadhi ya mlima Rungwe Ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika kwama ziwa yatokanayo na mlipuko wa volkeno. Ziwa lina muonekano wa ramani ya Afrika na visiwa vyake Maji yake yanabadirika rangi kutoka Bluu kijani, na Bluu Bahari Halina mto unaoingiza maji wala kutoa maji 13
MAPOKEZI YA MH. RAIS KATIKA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA
HIFADHI YA MSITU WA MLIMA RUNGWE (MOUNT RUNGWE NATURE RESERVE) Hifadhi ya Msitu wa Mlima Rungwe inapatikana katika Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya Nchini Tanzania, ilinzishwa kisheria na Serikali ya kikoloni mnamo mwaka 1949, kwa lengo la kuhifadhi vyanzo vya maji na Baionuai (Biodiversity). Hifadhi hii inaukubwa wa Hekta 13,652.1 ipo umbali wa Kilomita 25 kusini Mashariki Mwa mji wa Mbeya na Umbali wa Kilomita 7 Kaskazini mwa Mji wa Tukuyu. Baada ya Kuona Umuhimu mkubwa wa Hifadhi ya mlima Rungwe, Mchakato wa kuipandisha hadhi ulianzishwa Mwaka 2008 na hatimaye mwaka 2009 msitu huu ulipandishwa hadhi ya uhifadhi wake na kuwa Hifadhi ya mazingira Asilia ya Mlima Rungwe Uhifadhi asilia una maana ya kupunguza muingiliano wote wa shughuli za kibinadamu katika Hifadhi na kuacha uasilia wa mahali utegemee mabadiliko ya kiasili tu (non-consumptive type of conservation). Shughuli kuu zinazoweza kufanyika katika hifadhi ni pamoja na Elimu, utafiti na Utalii. Hifadhi asilia ya Mlima Rungwe inamilikiwa na Serikali kuu chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Usimamizi wake uko chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ulianzishwa mwaka 2010 kwa ajili ya kusimamia Rasilimali za Misitu na Nyuki kwa Tangazo la Serikali na. 269 la tarehe 30/07/2010. Kwa Tanzania kuna Hifadhi 12 tu zenye hadhi ya Mazingira asilia ambazo ni Mlima Rungwe (Mbeya), Kilombero (Iringa & Morogoro), Uzungwa (Iringa & Morogoro), Uluguru (Morogoro), Mkingu (Tanga), Rondo (Lindi), Amani (Tanga), Chome (Kilimanjaro), Nilo (Tanga), Minziro (Kagera), Magamba (Tanga) na Mlima Hanang (Manyara). Vivutio vya kitalii ndani ya hifadhi ya msitu wa mlima Rungwe. Hifadhi hii ina vivutio vingi sana na vyenye upekee, • Uwepo wa Viumbe Mbalimbali ambao baadhi yao hawapatikani sehemu nyingine yoyote isipokuwa katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Mlima Rungwe tu. mfano wa viumbe hao ni nyani aina ya Kipunji (Rungwecebuskipunji) aliyegunduliwa kwa mara ya kwanza katika Hifadhi hii na Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori (WCS) mwaka 2003.
14
•
Mlima wa tatu kwa urefu Nchini Tanzania Mlima Rungwe wenye Urefu wa mita elfu mbili mia tisa themanini na moja (2981) maalum kwa wana mazoezi, na wapanda milima (Mountain Hikers).
•
Mashimo ya volkano Kama vile Paluvalalutali, Lusiba Lwamisi, Lusiba Lukafu na Ng’ombe ambayo mashimo hayo kwa sasa yamekufa (Dead volcanic craters).
•
Wanyama wadogo wadogo zaidi ya aina miatano (500) kama vile Minde (Abbot duiker), chura wekundu, mijusi, nyoka wa chi baridi, panya nkpiaAinazaidiyamianne (400).
•
Ushoroba wa Bujingijila, Ni miongoni mwa eneo muhimu sana kiutalii linalo unganisha Hifadhi ya Taifa ya Kitulo pamoja na Hifadhi ya Mazingira asilia ya Mlima Rungwe, ni eneo ambalo wanyama hupita kutoka hifadhi moja kwenda hifadhi nyingine.
MUONEKANO WA MKOA WA MBEYA NA MANDHARI NZURI IVUTIAYO
Nakala hii imeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila
Kwa ushirikiano na Mbeya Advertise with Macrine Uyole Cultural Tourism Enterprise OSE Creative Agency