MWELEKEZO WA WAZAZI
O 3 0
3 0 F
TUZUNGUMZE ZAIDI KUHUSU HIV !
Tumempa mtoto wako kitabu hiki cha ‘Kuwa Shujaa’ ili aweze kujifunza kuhusu HIV na Ukimwi; na pia, kuhakikisha kwamba atajifunza njia za kujikinga.
Tunahitaji usaidizi ili kuhakikisha kwamba kuna mazingira mema shuleni kwa wanafunzi wasio na virusi vya HIV, na pia wale walio na virusi vya HIV. Waweza kutusaidia kusoma mwelekezo huu na kuzungumza juu ya vitabu vya ‘KUWA SHUJAA’ na watoto wako.
Ndani ya mwelekezo kuna maswali ambayo utaweza kumuuliza mtoto wako kuhusu HIV. Haya maswali yatakusaidia kuzungumza na mtoto wako kuhusu HIV. Kando ya hayo, maswali haya yatamsaidia mtoto wako kuangalia swala la HIV katika mwangaza mpya..
Watoto wengi huchokozwa shuleni na watoto wenzao ambao hawajui ukweli kuhusu HIV na Ukimwi. Nia ya kitabu hiki ‘Kuwa Shujaa’ ni kubadilisha tabia hizo
This publication has been made possible with the generous support of the American people through USAID/Kenya, under the APHIA II Operations Research Project, a cooperative agreement (No. 623-A-00-09-00001-00) between the Kenya Mission and the Population Council.
3
PAGE 04
DEBATE!
PAgE 9
Umuhimu wakujadili swala hili ni kuwahimiza kuzungumza juu ya HIV.
Jadili na familia yako.
MJADALA: Wanafunzi walio kwenye uhusiano wa kimapenzi ndio wanastahili kupimwa virusi vya HIV. MJADALA: Je, shule zinafaa kuwapa wanafunzi walio na virusi vya HIV huduma ya binafsi? MJADALA: Hakuna faida ya kupimwa virusi HIV.
Katika hadithi hii, Benson anachokozwa na wanafunzi wengine kwasababu wanadhani kwamba ana HIV
MTOTO WAKO ANACHOKOZWA KWA SABABU ANA VIRUSI VYA HIV? UNGEFANYA NINI KUBADILISHA TABIA HII?
MUULIZE MTOTO WAKO ANGECHOKOZWA KWA SABABU YA HALI YAKE YA HIV, ATAHISI VIPI?
i: ukwel tu HIV ya m a hali ya . Njia ya u j u k i lia tu Huwez a muanga HIV ni kupimw kwa ku ya ! o e k w ya im i p l u ha cha VCT kujua a kituo tu. End
TRUST ME!
PAgE 10
Kupimwa virusi vya HIV ni rahisi kama una marafiki unaowaamini, na ambao watakusaidia hata majibu matokeo yawe vipi. JE, WATOTO WAKO WANAKUAMBIA SHIDA ZAO ZA KIBINAFSI? UNAWEZA KUFANYA NINI KUJENGA UAMINIFU KATI YAKO NA MTOTO WAKO? UNAFIKIRI MTOTO WAKO ATAKUAMBIA AKITAKA KUPIMWA VIRUSI VYA HIV?
PAgE 18
ULIZA DAKTARI Baadhi ya wanafunzi waliuliza maswali...yafuatayo ni maswali waliouliza na majibu waliopata... Q. Kuna hatari ukilala kwa kitanda kimoja na mtu ambaye ana virusi vya HIV? A. Hakuna hatari. Ni hatari tu ukiwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu aliye na virusi vya HIV bila kutumia kinga.
Katika hadithi hii, shule inaulizwa kama wanajua hali yao ya HIV…wengi wao hawajui kwa sababu hawajapimwa. MTOTO WAKO ANAJUA HALI YAKE YA HIV?
WEWE UNAJUA HALI YAKO YA HIV?
Msikize mtoto wako. [Kumbuka ulipokuwa umri wao. Wasaidie na uwape fursa ya kukueleza hisia zao.] Kama mzazi, utamsaidia mtoto wako vipi kuwapenda na kuwaheshimu wanafunzi ambao wameambukizwa virusi vya HIV?
4
Q. Ndugu yangu ana HIV. Atapona akila vizuri? A. Nasikitika kwamba HIV haina tiba. Hata hivyo, ndugu yako anaweza kuishi maisha marefu na yenye afya akila vizuri na kunywa dawa zake. Q. Niligusa sehemu za siri za mpenzi wangu na nashuku kwamba ana virusi vya HIV. Je, nimeambukizwa virusi vya HIV? A. Hapana! Huwezi kuambukizwa virusi vya HIV kwa kumgusa mtu. Sana sana, HIV hupita kutoka mtu mmoja kuenda kwa wengine wasipotumia kinga wakati wa ngono. Wakati huo maji ya kimwili au damu kutoka aliye na virusi yanapita kumwabukiza mwenzake. Q. Nataka kupimwa, lakini wazazi wangu wanasema kwamba watu watanisengenya. Huu ni ukweli? A. Kama watu wanataka kukusengenya basi huo ni uamuzi wao. Ni ujinga kumhukumu mtu kwasababu ameamua kufanya jambo la busara. Usitie maanani watu wanvyosema, wewe fikiri tu uzuri wa kujua hali yako.
Zungumza na watoto wako kuhusu virusi vya HIV ili uwakinge.
5
PAGE 14
Katika hadithi hii Jipendo anaogopa kupimwa lakini Malkia anamshawishi mpaka anaenda kupimwa!
PAGE 14 Baadaye, Jipendo na Malkia wanakutana na msanii stadi Wyre anayepimwa ili ajulie maisha yake ya usoni‌
Hebu tuangalie tena orodha hii inayotupa maelezo zaidi kuhusu HIV/AIDS. Itumie orodha hii kama mwelekezo ukiwa unataka kuzungumza zaidi na watoto wako. Ukifanya hivi, unahakikisha kwamba wanajua na kuelewa ukweli. Kumbukaujuzi wa kutosha utawaokoa!
Ukimwi husababishwa na virusi vya HIV. Virusi hivi vinasababisha ukosefu wa kinga mwilini. Watu walioambukizwa virusi vya HIV huishi hata miaka na miaka kabla waanze kuonyesha dalili zozote za ugonjwa. Wanaonekana wenye afya na hata kujihisi wagonjwa, lakini bado wanaweza kuwaambukiza wengine. Ukimwi ni kituo cha mwisho mtu akiwa na virusi vya HIV. Watu walio na virusi hukosa nguvu kwasababu miili yao haina kinga. Katika watu waliokomaa, Ukimwi hujitokeza kama miaka saba, nane, tisa au kumi baada ya kuambukizwa. Kwa watoto wadogo, muda ni mfupi zaidi. Ukimwi hauna tiba lakini madawa mapya yanaweza kusaidia watu walio na ugonjwa huu, kuishi maisha marefu ya afya..
UNAJUA KAMA MTOTO WAKO AMEENDA VCT? KAMA AMEENDA, ALIFUNDSHWA NINI? RAFIKI ZAO WALISEMA NINI BAADA YA HAYO?
wyre
celeb speak!!! Kevin Wyre [anayejulikana kama Wyre] anawashawishi wanafunzi kupimwa na kujua hali yao ili waweze kupanga maisha yao ya usoni. Wyre (ambaye pia ni mzazi) alituambia jinsi anapanga kuzungumza na mtoto wake kuhusu HIV: KS: Kama mzazi, ni mawaidha gani ungeweza kuwapa wazazi wengine kuhusu kuzungumza na watoto wao kuhusu a.) Ushauri wa HIV b.) Kupimwa na c.) Ugonjwa wa HIV/AIDS? WYRE: Anza kuzungumza nao wakiwa wachanga, Zungumza nao kama marafiki. Wape mifano ya maisha yako ya kitambo, ili waelewe kwamba hata wewe ni binadamu.
Sana sana, HIV hupita kutoka kwa mtu mmoja na kumuendea mwingine watu wakiwa na uhusiano wa kimapenzi bila ya kutumia kinga. HIV pia yaweza kuenea watu wanapotumia sindano ambazo hazijasfishwa (hutumiwa sana kutumia madawa ya kulevya) wembe, visu ama vifaa vingine vinavyokata mwili. Pia kuwekwa damu iliyo na virusi. Damu yote inayotolewa yafaa ipimwe. Ukishika mtu aliye na virusi, huwezi kuambukizwa. Kukumbatiana, kushikana mikono, kukohoa au kupiga chafya, hakutaeneza ugonjwa. HIV na AIDS haziwezi kuenea kupitia viti vya choo, vifaa vya kula, vikombe, au mahala pa kuogelea. HIV na AIDS hazienei kutokana na mbu au wadudu wengine. (Taken from Facts for Life, UNICEF)
KS: Kama mtoto wako angekuwa shule ya upili, ungetaka apimwe? WYRE: Ndio. Ni muhimu sana. Nawashawishi wasomaji wapimwe. Ukishajua, roho itatulia. Ikiwa una virusi, waweza kusaidiwa. Kama huna virusi, ujuzi huu utakusaidia kupanga maisha yako.
6
Zungumza juu ya Celeb Speak na watoto wako. waulize fikra zao kuhusu Wyre na mashujaa wao wengine...wanafanya nini kupambana na HIV?
Kumbuka, kinga inayofaa dhidi ya stigma ni ujuzi wa sawa sawa.
7
Haya ni marudio kuhusu utaratibu wa kuenda VCT. Ni muhimu ujue utaratibu huu, ili uwasaidie watoto wako, kisha wewe nawe ujisaidie.
VCT inamaanisha Voluntary Counselling and Testing.Katika VCT mtu atatambua kama ana virusi au hana. Ukienda kupimwa, unazungumza kwanza na anayetoa ile huduma. Kumbuka, kwamba kupimwa au kuangalia majibu ni chaguo lako. Matokeo yakiwa kwamba hujaambukizwa, basi anayehudumu atazungumza na wewe juu ya umuhimu was kujikinga dhidi ya HIV na magonjwa mengine ya zinaa. Mazungumzo haya hayatakuwa kuhusu kinga peke yake, watajaribu sana kukufikiria wewe binafsi na kuona kama mbinu hizi zitakusaidia. Kumbuka: Kupimwa hakuhakikishi kwamba hutaweza kupata HIV. Sana sana lazima tabia zibadilike. Ikiwa kwamba kweli una virusi, anayekuhudumia atazungumza na wewe na kueleza jinsi ya kujikinga. Jambo hili ni muhimu ili usiende ukaambukiza watoto wako. Isitoshe , Counsellor yuko hapo ili kuwa rafiki na kukusaidia. Tutaendelea kufuatana na watoto ili kuhakisha kwamba wamepata ujuzi wa kutosha.
Courtesy of ‘Tuko Pamoja: Adolescent Reproductive Health and Life Skills Curriculum’
kuwa shujaa production charles j ouda | bridget deacon | fatima aly jaffer design salim busuru art salim busuru | eric muthoga | noah mukono | kevin mmbasu stories grace irungu | daniel muli | peter kades published by well told story: www.wts.co.ke